Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

ASIA IDAROUS,GYMKHANA HILALL NA MARTIN KADINDA WATEULIWA KUTOA UAMUZI UNIQUE MODEL 2012

$
0
0

Baraza la sanaa la taifa limeteua majina matatu ya wabunifu wa mavazi nchini Tanzania kuwa waamuzi wa shindano la wanamitindo bora wa mwaka wenye sifa za kipekee nchini Tanzania (Unique Model 2012).

Uteuzi wa majaji hawa umezingatia sifa za cv za majaji sita zilizowakilishwa baraza la sanaa la taifa na hatima yake yakarudi majina matatu ambayo ni Asia Idarous,Gymkhana Hilall (paka wear) na Martin Kadinda.

Fainali za unique model 2012 zinafanyika ijumaa ya wiki hii tarehe 28 Desemba katika kumbi la maraha ulioko kule Oysterbay yaani naongelea New Maisha club ambapo wanamitindo 12 watapanda jukwaani kuwania taji hilo.

Burudani ya bendi mahili katika muziki dansi,Mashujaa band ikiongozwa na Chalz Baba watatoa burudani kali kwa mashabiki watakaohudhulia fainali hizo siku ya Ijumaa hii.

pia msanii B-shop kwa mara ya kwanza ataonekana jukwaani. Ikiambatana na mashamushamu ya Costa siboka na burudani ya wanamuziki mbalimbali kwa kiingilio cha Tsh 15,000 tu.

Shindano hili limedhaminiwa na Giraffe ocean view hotel,Kitwe general Traders,sophanaa investment ltd,dtv,88.4 clouds fm,Gazeti la Tanzania Daima,Gazeti la Kiu,mashujaa investment ltd,Michuzi blog,jiachie blog,Lmada Apartments & Hotel,mtaa kwa mtaa blog,Fabak fashins,Genessis health center na Yung don Records,Paka wear,Mtoko Design,Dina ismail blog na Unique Entertainment Blog. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles