Siku ya Jumanne, tarehe 19 machi, majira ya saa tatu na nusu asubuhi, Baba Mtakatifu Francis, amezindua rasmi utume na utawala wake kwa Ibada ya Misa, katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican. kwenye Ibada hii ya uzinduzi Baba Mtakatifu ameongoza Ibada pamoja na Makardinali na Maaskofu wapatao 180 na kuhudhuriwa na Wakuu wa nchi 31, Viongozi wa Kifalme 6, Wana Wafalme 3, Mawaziri Wakuu 11. Ibada hii iliudhuliwa na umati wa watu, sio tu waumini wa Kikatoriki bali hata waumini wa madhehebu mbalimbali na zaidi watu tokea dini mbalimbali. Umati wa watu unakadiriwa kutokupungua 200.000.
Katika Ibada hii, Baba Mtakatifu alivalishwa Pete ya Petro na Kardinali Angelo Sodano , ikiwa kama ishara ya wadhifa wake.
Bendera ya Tanzania ilipeperushwa vizuri sana na umati mkubwa wa Watanzania walioudhulia Tukio ili la Kihistoria.
Kwa picha na video ya Tukio ili la Kihistoria mnakaribishwa kutembelea blog ya Jumuiya ya Watanzania Rome:www.watanzania-roma.blogspot. com
Picha zote zimeletwa kwenu na ndugu: Andrew Chole Mhella.
Baba Mtakatifu akipita kubariki watu
Bendera ya Tanzania ikipeperushwa mbele ya Baba Mtakatifu.
Kulia ni katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma Ndugu
Andrew Chole Mhella pamoja na Ndugu Safari Mwacha wakiipeperusha bendera ya Tanzania.
Masista na ma Padri wa Kitanzania wakiifurahia bendera yetu.
Kwa pembeni ni baadhi ya Watalii wa kiargentina.
Furaha ziliwajaa baadhi ya Watanzania waliokuwepo mbele ya Kanisa
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma ndugu Andrew Mhella Pamoja na Ndugu Safari Silvanus Mwacha na ndugu Dusten wakipata picha ya Pamoja na askali waliokuwepo kwenye kuhakikisha shughuli nzima inaenda salama.