Timu ya Malindi ya Zanzibar huku ikiwa pungufu kutokana na mchezaji wa ke mmoja kulimwa kadi nyekundu mapema dakika za mwanzo wa mchezo, jana iliibuka mshindi kwa kuinyuka Mundu mabao 2-1 ligi kuu ya Grand Malt ya Zanzibar kwenye uwanja wa Mao Tse Tung mjini Zanzibar.
Mshambuliaji wa timu ya Mundu, Ulrasa Juma akimtoka mlinzi wa Malindi, Nadir Rashid (kushoto) wakati wa mchezo wa wa ligi kuu ya Grand Malt,Zanzibar uliochezwa jana jioni kwenye uwanja wa Mao Tse Tung.
Abdalla said wa Malindi (kushoto) na Thabit Khamis wa mundu wakiwania mpira.