KATIBU Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kuhusu shughuli za kilimo alipotembelea mji wa Dantong, Nanchong kwenye miradi ya kilimo kwa ajili ya kupambana na umasikini, Machi 16, 2013. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, akiwasalimia wazee katika kijiji cha mradi wa wakulima wa kupunguza umasikini cha Nanchong, jimbo la Sichuan, China, alipotembelea kijiji hicho, Machi 16, 2013. Anayemsalimia ni Ning Xiu (78). Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China, jimbo la Sichuan, Zhang Ning, wakitazama kazi za watoto, katika shule ya awali katika kijiji cha Dantong, wilaya ya Nanchong, Kinana na ujumbe wake walipotembelea miradi ya kilimo kwa ajili ya kupunguza umasikini, katika kijiji hicho, Machi 16, 2013.Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndugu Amina Makilagi, akitazama vifaa vya michezo ya watoto katika shule ya awali ya Kijiji cha Dantong, jimbo la Sichuan, Msafara wa Kinana ambao Amina yumo, ulipotembelea kijiji hicho kuona shughuli za mradi wa kilimo wa kupunguza umasikini, Machi 16, 2013. Kinana yupo China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, na Watatu kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM , Khadija Aboud.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman na akipata maelezo katika duka la kisasa na mazao ya chakula, katika kijiji cha Dantong, wilaya ya Nanchong, jimbo la Chengdu China, Machi 16, 2013. Duka hilo ni la mazao ya wakulima katika kijiji hicho kupitia mradi wa kupunguza umasikini Nanchong. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC.
Katibu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akitazama moja ya mashamba makubwa ya wakulima walipo kwenye mradi wa kupunguza umasikini, katika Kijiji cha Dantong, Jimbo la Sichuan, China, Machi 16, 2013. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. Picha zote na Bashir Nkoromo.