Basi la Kubeba wanafunzi la Shule ya Sekondari ya St. Anthony ya Mbagala jijini Dar es Salaam lenye nambari za usajili T 631 AZY (pichani kulia) leo majira ya saa kumi jioni,limenusurika kupiga mweleka kama si kuparamia magari ya watu wengine mara baada ya kufeli breki likiwa kwenye mteremko wa eneo la Mtongani kuelekea Africana,Mbezi Beach.
Basi hilo ambalo lilionekana kuwa kwenye mwendo kasi kiasi,lilishindwa kusimama wakati wa foleni iliyokuwepo kwenye barabara hiyo,hali iliyompelekea dereva wa Basi hilo kuchukua uamuzi wa kuikwepa foleni hiyo na kupita upande wa kushoto wa barabara kwa mwendo ambao hauzungumziki huku wanafunzi waliokuwemo ndani ya basi hilo wakisikika wakipiga mayoe ya kuhitaji msaada,hali iliyowafanya watu wengi waliokuwepo katika eneo hilo kulifuata basi hilo kwa kukimbia huku wazee wa boda boda wakiwasha vyombo vyao na kulifukuzia basi hilo huku wakiwa tayari tayari kwa kutoa msaada wowote utakao hitajika.
Ila kwa kuwa Mungu ni muweza wa kila jambo,Basi hilo lililweza kusimama baada ya kuligonga basi lingine (daladala lenye nambari za usajili T 254 BCR) kwa nyuma ambalo nalo inaonekana lilikuwa limesikaka barabarani hapo (haikufahamika mara moja sababu ya kusimama kwa basi hilo) na hapo ndipo walionekana wanafunzi hao wakishuka kwenye basi hilo huku wakiwa hawaamini kile kilichotokea.
Hakuna aliejeruhiwa kwenye tukio hilo.
Wanafunzi hao wakiwa nje ya Basi hilo huku wakihadithiana jinsi hali ilivyokuwa wakati basi lao limefeli breki.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa.
Wengine walipoona mambo yameharibika kule mbele wakaona wachukue uamuzi mbadala wa kuvuka ng'ambo ya pili ya barabara.
Jamaa wakilikimbilia basi hilo ili kwenda kuona litakapoishia.
Wengine wakaona isiwe shinda,ngoja wapite pembeni kule ili wawahi waendako.
Bodaboda zikiwa tayari tayari stand by...