Na Abdulaziz,Lindi
Hospital ya mkoa wa Lindi(Sokoine hospital) imenusurika kuungua usiku wa kuamkia leo kutokana na kilichotajwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Muuguzi wa Zamu ,Bi Rehema Mbinga alieleza kuwa Moto huo ulioanzia katika swichi ya Umeme uliweza kudhibitiwa vyema kufuatia huduma ya haraka ya kuzima moto iliyokuwepo hospitalini hapo.
Hata hivyo alieleza masikitiko yake kufuatia simu walizopiga katika kikosi cha kuzima moto cha Manispaa ya Lindi na mpokeaji kujibu majibu rahisi ya Acheni kutania nyie na kukata simu kila ikipigwa.
"Mwandishi tunashukuru kwa msaada wa wauguzi wenzangu tumefanikiwa kuzima moto huo ulioanzia katika dirisha la kutolea dawa
"Ila fikisha ujumbe Kikosi cha zimamoto waache dharau na majibu rahisi wanapopigiwa simu vinginevyo watasababisha maafa. leo sijui ingekuwaje kama tusingewahi kuuzima huo moto"limalizia Bi Rehema