Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

UN TANZANIA YAZINDUA RIPOTI YA MAENDELEO DUNIANI 2013 IKIONYESHA NCHI ZINAZOENDELEA 40 ZIMEPIGA HATUA KUBWA SANA YA MAENDELEO YA BINADAMU

$
0
0

Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akitoa hotuba ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 - Kuchomoza kwa Nchi za Kusini: Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai akisema kwa mujibu wa ripoti hii mwaka huu iaonekana kuwa Tanzania tumefanya vizuri na kiwango chetu kimeongezeka kama ngazi mbili ikilinganishwa na ripoti iliyopita.
Hata hivyo amesema kwa bado kuna mikoa mingi ambayo unapopima maendeleo kwa ujumla wake mikoa mingi ipo asilimia 20 hadi 30 ambapo hii inapima ujumla wa maendeleo katika Jamii.
Bw. Lyimo amesema kwa sasa serikali ina mipangp mizuri ya kuisaidia mikoa hiyo, akitolea mfano kilimo kuwa kuanzia miaka ya 80 hatukuiangalia vizuri tulikuwa na taasisi za kilimo, mashirika ya maendeleo ya viwanda lakini katika kipindi hiki cha mageuzi tumepata matokeo mazuri.
Mratibu Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 ikiainisha Kuchomoza kwa Nchi za Kusini:Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai ambapo amesema sera kabambe, zilizotengenezwa vizuri zinaweza kufanya mafanikio ya kimaendeleo ya binadamu kuwa endelevu katika miongo ijayo na kupanuka kufikia nchi nyingi zaidi zinazoendela.
Lakini pia Dkt. Kacou ameonya hatua za kubana matumizi zisizo na mtazamo wa mbali, zaweza kushindwa kushughulikia hali ya kukosekana usawa, na kukosekana kwa ushiriki wa maana wa jamii na kutishia maendeleo haya kama viongozi hawatachukua hatua za kurekebisha.
Aidha amesema baadhi ya mataifa yanayoongoza kwenye nchi za Kusini yanajenga mwelekeo mpya wa kukuza maendeleo ya binadamu na kupunguza tofauti za kimaisha kwa kuweka sera bunifu ambazo zinasomwa na kuigwa sehemu nyingine duniani.
Baadhi ya Wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini wakimsikiliza Dkt. Alberic Kacou (hayupo pichani) alipokuwa akisoma hotuba yake kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013 iliyofanyika jijini Dar leo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>