Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

moshi mweusi wafuka vatican; papa bado hajapatikana

$
0
0

Moshi mweusi umefuka leo katika Chapel ya Sistine huko Vatican, kuashiria kwamba Papa mpya bado hajachaguliwa katika siku ya kwanza ya upigaji kura za siri.
Papa Benedict XVI aliustua ulimwengu kwa kuwa Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani wa kwanza kujiuzuru katika miaka 600,  na hali hii ya leo inaonesha Makardinali 115 wanaochagua wanataka kuhakikisha mrithi wa Joseph Ratzinger (jina la Papa aliyepita) ni mtu sahihi.
Habari toka Vatican zinasema kwa kawaida Makardinali hao watapiga kura mara nne kwa kila siku hadi atapopatikana mteule wao. Wanatarajiwa kurejea tena kupiga kura kesho katika uchaguzi huo ambao hauna kikomo cha siku za kufikia uamuzi.
Katika uchaguzi uliopita mwaka 2005, uchaguzi ulichukua siku mbili, lakini kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopot, mnamo mwaka 1268 iliwachukua miezi 33 kumpata Papa Gregory wa Tano.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles