Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115299

patakuwa hapatoshi tamasha la pasaka

$
0
0

KWAYA ya Kinondoni Revival  (pichani juu) na kundi la Glorious Celebration ni miongoni mwa burudani zitakazokuwepo kwenye Tamasha la Pasaka Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama jana ilieleza kuwa makundi hayo ya jijini Dar es Salaam tayari yamethibitisha ushiriki wao pamoja na mwimbaji mahiri Upendo Kilahiro ambaye pia atashiriki.



"Niseme mambo yanaenda vizuri na leo (jana) kuna msanii tunamalizana naye kutoka Afrika Kusini, nina imani wakati wowote kuanzia Jumanne (leo) tutamtangaza kwa mashabiki wetu, nia ni kulifanya tamasha liwe zuri zaidi," ilisema taarifa hiyo.

Wasanii wengine wa Tanzania ambao watashiriki tamasha hilo mwaka huu ni Rose Muhando, John Lissu na Upendo Nkone, wakati wa nje ya Tanzania ni Ephraim Sekeleti wa Zambia anayetamba na albamu zake za Acha Kulia na Mungu Mwenyewe. 

Wasani wengine wa nje watakaokuja ni Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya, ambapo pia mwaka huu kuna ingizo jipya ambalo ni kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kigali Rwanda inayotamba na albamu ya Mtegemee Yesu.
Kundi la Glorious Celebration likiwa kwenye moja ya kazi zake jukwaani.

Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na  litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti, kundi la Glorious Celebration, kwaya ya Kinondoni Revival na Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115299

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>