Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

Tawi la Simba la Mpira Pesa la magomeni lafunguliwa

$
0
0
SIKU moja baada ya kung'atuka madarakani kwa viongozi wawili wa Simba, Zacharia Hans Poppe na Godfrey Nyange Kaburu, Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, imetangaza kulifungulia Tawi la Mpira Pesa la Magomeni.

Poppe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Kaburu, Makamu Mwenyekiti walitangaza kujiachia ngazi katika klabu hiyo kwa sababu mbalimbali ikiwemo timu kufanya vibaya katika mechi zake za kitaifa na kimataifa.

 Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage alitangaza kulifungia Novemba 26, mwaka jana. Mwenyekiti wa Muda wa Kikao hicho kilichofikia uamuzi huo, Joseph Itangare 'Kinesi' alisema kuwa sababu kubwa ni kuleta umoja ndani ya klabu.

"Hatuhitaji tena mpasuko katika Simba,ni wakati wa kushirikiana na kuleta hamasa kwa wachezaji, tunataka kuleta umoja kwa kuwa bado tuko katika mapambano ya kuinusuru timu," alisema Itangare.

Hata hivyo, Rage ambaye ndiye aliyekomalia kufungwa tawi hilo, hakupatikana kwa kuwa yuko nje ya nchi  kwa matibabu.

Kiongozi wa tawi hilo, Masoud Awadh alipotafutwa kuzungumzia hali hii alisema kikubwa wao wanataka mkutano mkuu ufanyike March 17 ili waweze kutoa madukuduku yao na kama tawi lao limefunguliwa inabidi pia wanachama wao watatu nao wafunguliwe.

"Sasa ivi timu imeyumba lazima waone umuhimu wetu,sisi hatuna kinyongo kwa sababu tunafanya kazi kwa maslahi ya timu na si wachezaji wachache,kwanza tunataka mzee kilomoni atambue kesi ipo mahakamani na yeye anatakiwa kuhudhuria Machi18 kama anavyotakiwa kwani kila anapoitwa anakaidi tunamtaka afanye ivyo mara moja,"alisema Kundi la mpira pesa lilimfungulia kesi Hamis Kilomoni baada ya kuwakashifu wanatumiwa na matajiri wa klabu katika kuihujumu timu na kwa sasa kesi hiyo ipo mahakamani na itasomwa tena Machi18.

Katika hatua nyingine Kinesi alisema kwa kuwa ligi bado inaendelea na Simba ina mechi ngumu mbele yao Kamati ya utendaji ya wekundu hao wa Msimbazi imeunda kamati ndogo ya ushindi ambayo itaongozwa na Rahma Al Kharoos maarufu kama 'Malkia wa Nyuki, lengo likiwa ni kuhakikisha Simba inashinda katika mechi zilizosalia.

Kwa upande wa Kocha msaidizi wa wekundu hao Jamhuri Kihwelo 'Julio' amewaonya wachezaji wake kuacha kujihusisha na mgogoro unaoendelea ndani ya klabu hiyo iliyopo mtaa wa Msimbazi na badala yake waelekeze nguvu na akili zao katika Ligi inayoendelea na kesho Simba itashuka dimbani kumenyana na Coast Union ya Tanga kwenye uwanja wa taifa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>