Ngoma bado mbichi katika lala salama za uchaguzi mkuu wa Kenya, japo mgombea wa Jubilee Mhe. Uhuru Kenyatta (shoto) anaongoza kwa kura 6,035,582 dhidi ya Mhe Raila Odinga ambaye kapata kura 5,285,771 hadi kufikia wakati huu ambapo ni saa saba na robo za usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Wagombea wote wawili wameshatimiza asilimia 25 zinazohitajika kutoka kwa angalau majimbo 24. Uhuru Kenyatta anahitaji kura za asilimia 0.1 tu kujinyakulia ushindi, ingawa kura toka za majimbo yaliyosalia yanaweza kumpaisha Mhe Odinga pia. Matokeo rasmi ya mwisho yanategemewa kutangazwa saa tano asubuhi leo.
Globu ya Jamii inaendelea kufuatilia mambo.....
Globu ya Jamii inaendelea kufuatilia mambo.....