Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

yale yaleeee:kinyesi changanyika na maji masafi Regent Estate

$
0
0
Wakazi wa mikocheni, eneo la Regent Estate jijini Dar es salaam wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu katika kipindi hiki cha kuelekea mvua za masika kutokana na maji ya taka ikiwemo kinyesi, yanayotoka kwenye nyumba zote zilizoko mtaa wa Mgombani, kutiririka juu ya mtaro uliokuwa ukitumika kupeleka takataka hizo baharini kama inavyoonekana katika picha. 

Wakazi hao hasa waliopo katika makutano ya mtaa wa Mgombani na njia ya kuelekea mtaa wa Chwaku (nyuma ya Shoppers Plaza) wameieleza Globu ya Jamii kwamba wamepitia njia zote za uongozi kuanzia kwa serikali ya mtaa, diwani hadi uongozi wa juu wa manispaa ya Kinondoni bila mafanikio. 

Uongozi wa DAWASCO ambao ndio wanahusika na suala hili walipoambiwa na wakazi wa maeneo hayo walidai kwamba pump ya kunyonya maji hayo kuyapeleka baharini imeharibika na hawana namna nyingine ya kufanya ingawa Ankara zao za kila mwezi zinalipiwa huduma hiyo. Hali hii imekuwa hivyo toka mwezi wa nane 2012 hadi leo. 

Na jambo la hatari zaidi ni kwamba maungio ya mabomba ya maji masafi yapo katikati au yamefunikwa na kinyesi hicho. 

Wadau mnaombwa ushauri. Kama vipi tumepanga kuandamana...
 Mkazi wa mtaa wa mgombani.
Mtaa huo pia ni makao makuu ya taasisi za utafiti maarufu nchini, ikiwemo REPOA na 
IPSOS SYNOVATE ambazo bila shaka zitatoa tafiti kuhusu madhara ya mitaro hiyo iliyojaa kinyesi....
Mtaro mchafu
Maji yaliyojaa kinyesi kutoka katika vyoo vya mitaa yote ya hapo
Hatari kwa wakaazi na hata wapita njia


Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>