MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Solomon Mukubwa ameibuka kidedea kwa wasanii wa nje watakaoshiriki Tamasha la Pasaka mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa mashabiki wengi wamempigia kura Mukubwa kuomba ashiriki kwenye tamasha la mwaka huu kama ilivyokuwa matamasha yaliyopita.
“Kwa hiyo leo naomba kumtangaza Mukubwa, ambaye ni raia wa DRC lakini anayeishi Kenya kwamba ni mwanamuziki wa kwanza nje ya Tanzania ambaye tayari kamati imeafiki ashiriki tamasha letu,” alisema Msama. Alisema maandalizi yanaenda vizuri na idadi ya wasanii kutoka nje ya Tanzania waliopendekezwa ni kubwa, lakini wanachokiangalia si kupendekezwa tu lakini pia nafasi ya msanii husika kuja kwenye tamasha hilo.

“Msanii akishapendekezwa vya kutosha kwa njia ya kura za maoni ambazo ni kupiga simu au kutuma ujumbe wa simu ya mkononi kwa kamati, kinachofuata ni mazungumzo kati ya sisi waandaaji na msanii na tukifikia makubaliano ndiyo tunamtangaza,” alisema Msama.
Mwimbaji huyo wa nyimbo za kumsifu Mungu mwenye ulemavu wa mkono mmoja, anatamba na albamu mbalimbali ikiwemo Usikate Tamaa, Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu.
Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Wasanii ambao mpaka sasa wameshatangazwa kushiriki ni Rose Muhando, John Lissu na Upendo Nkone ambao wote ni Watanzania.
Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.
Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.