Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

KUMBUKUMBU

$
0
0
Marehemu Bwana Ali Shariff Mussa Al Shirazi,baba yetu mpendwa alifariki siku ya kama leo tarehe 5/03/1988 ameshatimiza miaka 25 tokea kufariki. Baba yetu tunakukumbuka sana kwa upendo wako na Imani na uchangiaji wako wa kuondosha utumwa na ubaguzi wa makabila Zanzibar .

Na kuwapa uongozo mwema watoto wako na watoto wa wenzako ambao leo wengi wao ndio Viongozi Wakuu wa Tanzania na Zanzibar. {Hivyo washirazi walianza kujikusanya na kuunda jumuiya yao iliyojulikana Jumuiya ya Washirazi, au Shirazi Association. Jumuiya hii ilianzishwa mnamo mwaka 1940 na washirazi huko Pemba. Muasisi wa Jumuiya hii alikuwa Bwana Ali Sharif Mussa Al Shirazi wa Pandani.

Wakati akitoa hoja ya kuanzisha jumuiya hii, Bwana Ali Sharif alimuandikia barua mkuu wa wilaya wa serikali ya kikoloni huko Pemba kwamba kati ya wenyeji 73,000 wa Pemba asilimia kubwa yao walikuwa washirazi.

Hivyo basi alifafanua kwamba jumuiya yao ina malengo ya kujaribu kupata uwakilishi wa kitaifa kwa kuwa jumuiya ya waafrika inayotetea maslahi ya watu wenye asili ya kibantu ilikuwa haiwawakilishi watu wa Pemba kwa kuwa watu wa asili hiyo walikuwa wachache huko Pemba’’ (http://mzalendo.net/habari/dr-shein-enzi-za-wizara-ndogo-ya-kisonge-zimekwisha-chonde-chonde.html)

Mpaka sasa unakumbukwa sana,Wewe ndio mtu wa mwanzo aliyemuandikia barua Mkoloni na kuwaendea mpaka Mahakama za nyumbani kwao (Lancaster House) kutetea haki za wazanzibari na kuondosha utumwa na ubaguzi wa aina zote. Baada ya kuchaguliwa kuwa Mtunga Sheria 1948.

Muasisi wa mwanzo( ASP) huko Pemba na (ZPPP).Baba yetu mpendwa tunakuombea dua wewe na wote waliotangulia mbele ya haki Mola azilaze roho zenu mahala pema peponi.(Amin) Watoto wako ( HASANAT,KHALILA,THAMRA,RIDHWANA,AHMED,HABIB,ZAHID,SHARIFF,SALIM, MOHD)

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>