Mkuu wa Vodacom kanda ya kaskazini Bw. Philemon Chacha akigawa vifaa vya shule kwa baadhi ya watoto wenye ulemavu wa akili wa kituo cha KKKT usharika wa Longuo Mjini Moshi ikiwa ni sehemu ya zawadi mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa Vodacom Kanda ya Kaskazini vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.5 ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Pamoja na Vodacom.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili cha KKKT usharika wa Longuo Mjini Moshi walipotembela kituoni hapo na kukabidhi msaada wa vyakula, vifaa vya shule na vitu vingine mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 1.5 katika kituo hicho ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Pamoja na Vodacom.
Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Philemon Chacha akifuatilia kwa karibu mtoto mwenye ulemavu wa akili Arnold Justine anavyoandika jina lake kwa ufasaha huku mtoto mwenzie Gloria Isaack nae akishuhudia. Wafanyakazi wa Vodacom kanda ya Kaskazini walitembelea kituo hicho na kukabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi Milioni Moja na Nusu ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Pamoja na Vodacom inayosaidia makundi yenye mahitaji maalum.