Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

John Lissu aula Tamasha la Pasaka

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

MWIMBAJI anayekuja juu kwenye muziki wa kiroho nchini, John Lissu ni miongoni mwa wasanii wapya watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema jana kuwa mwimbaji huyo anakuwa msanii wa pili wa hapa nchini kutangazwa baada ya kung’ara katika upigwaji wa kura za maoni kwa mashabiki zilizoendeshwa na kamati hiyo, ambapo wa kwanza alikuwa Rose Muhando.

“Tulimtangaza Rose Muhando na sasa tuna John Lissu, kadri mambo yatakavyokuwa tutazidi kuwatambulisha. Hawa tayari tumekubaliana nao kuwatangaza washiriki kwenye tamasha letu,” alisema.

Kwa upande wake, msanii huyo alisema atatumia tamasha hilo kutambulisha nyimbo zake mbalimbali zilizopo kwenye albamu zake mbili ambazo ni Yehova Yu Hai na Upo Hapa alizozieleza kuwa ni moto wa kuotea mbali.

“Hivi sasa nina albamu yangu inaitwa Uko Hapa ambayo ni moto wa kuotea mbali, nataka mashabiki wote wafurahie na waitambue siku hiyo. Hii ni mara yangu ya kwanza kupata nafasi ya kushiriki kwenye tamasha hilo, hivyo lazima niwape furaha kubwa mashabiki,” alisema msanii huyo.

Alizitaja baadhi ya nyimbo zake zilizopo katika albamu ya Uko Hapa kuwa ni Wa Kusifiwa, Yu Hai Yehova, Fungua Macho, Uko Hapa, Hakikisha, Uko Juu, Nitakushukuru na Nijaze.

Kabla ya albamu hiyo aliwahi kutamba na albamu ya Yehova Yu Hai iliyokuwa na nyimbo kama vile Nisimamishe, Wastahili, Tunakuabudu Bwana na Tunakushukuru.

Tamasha la Pasaka litafanyika Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam, kasha Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>