Sherehe katika mji wa Kharkiv, Ukraine, hivi karibuni ambapo kituo hicho kimeanzsihwa kuimarisha uhusiano wa Elimu, Utamaduni na Maendeleo kwa ujumla kati ya Ukraine na Afrika.
Mhe. Balozi Jaka Mwambi aliweza kuzungumza na wataalamu wa mambo ya Elimu kuhusu kusaini mkataba wa Elimu kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Ukraine ambapo wamekubaliana kuhuisha mkataba huo katika vipingele kadhaa kwa upande wa Ukraine.
Mkataba huo utaruhusu Watanzania wengi kusoma vyuo vya Ukraine, wanafunzi wa Ukraine kusoma Tanzania pia, maprofessa kwenda kufundisha Tanzania, kubadilishana uzoefu wa tafiti (research) mbalimbali na hata kubadilishana mambo ya kiutamaduni.
Wanazuoni wa kiTanzania waishio Ukraine katika picha na Balozi wa Tanzania nchini Urussi, Mhe. Jaka Mwambi na Msaidizi wake - Mhe. Mbarouk N. Mbarouk.
Mhe. Vil Bakirov - Rector wa Kharkiv National University named after V.N. Karazin, Mhe. Irina Gagarina - Director of Ukrainian State Centre of International Education of Ukraine, Balozi wa Angola nchini Urussi, Mhe. Jaka Mwambi - Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Urussi wakipongezana kwa uzinduzi wa kituo cha UKRAINIAN - AFRICAN EDUCATION CENTRE.
Wanazuoni kutoka Nigeria, Tanzania, Tunisia na Kenya.