Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) Bw. Peter Noni (wapili Kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO), Bw Michael Laizer, ambayo yanalenga ujenzi wa maeneo ya viwanda kwa wajasiliamali wadogo na wakati. Hafla iliyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni Mwanasheria na Katibu wa Bodi wa TIB Bi. Martha Maeda, na kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bulilo Mafwimbo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) Bw. Peter Noni (Kushoto) wakibalishana mawazo na Mkurugenzi wa Shirila la Maendeleo ya Viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO), Bw Michael Laizer kabla ya kusaini hati ya makubaliano. Makubaliano hayo yanalengaujenzi wa maeneo ya viwanda kwa wajasiliamali wadogo na wakati. Hafla iliyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) Bw. Peter Noni (wapili Kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano na Mkurugenzi wa Shirila la Maendeleo ya Viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO), Bw Michael Laizer, ambayo yanalenga ujenzi wa maeneo ya viwanda kwa wajasiliamali wadogo na wakati. Hafla iliyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
======
Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) imesaini makubaliano na shirila la maendeleo ya viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO) yenye lengo la kushirikiana kuweka miundombinu ya viwanda kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo. Mpango huu wa ushirikiano utawezesha ujenzi wa maeneo ya viwanda (industrial areas), ambao utaanza na mkoa wa Dar es Salaam, kabla ya kutanuka katika miji mingine.
Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo jana katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Peter Noni, alisema kuwa lengo ni kuwasaidia wajasiriamali kuweza kuzalisha bidhaa za viwandani.
“Hapa benki tumebaini kwamba kunamatatizo makubwa sana kwa mjasiriamali Mtanzania anapojaribu kuwekeza kwa ajili ya uzalishaji. Vita vya kuondoa umasikini nchini vinategemea uzalishaji. Uzalishaji pia unategemea uwezo wa kupata mikopo kutoka benki.
“Benki yetu ya Rasilimali Tanzania imekuwa ikiwafikia wajasiriamali ili kuwapa mikopo kwa ajili ya kuendeleza biashara zao, lakini wengi wao wanashindwa kufikia vigezo, vinayotokana na gharama kubwa inayohitajika ili kuwekeza katika kiwanda.
“Kwa hiyo, benki yetu kwa kushirikiana na SIDO tumeweza kupanga mkakati wa kuwawezesha wajasiriamali kuondokana na tatizo hilo. Tumekubaliana kuanza kushirikiana kutafuta maeneo ambayo tutayawekea miundombinu ya viwanda ambayo itawasaidia hawa wazalishaji wadogo wadogo kuja kukodi, hatua ambayo itawapunguzia gharama za uendeshaji.
“Huu utaratibu pia utamwezesha mjasiriamali huyu aweze kukopesheka na taasisi za kibenki, kwa sabau atakuwa na mahala maalum pa kuzalishia kwa gharama ndogo,” alisema Noni.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Michael Laizer alisema riba ya mikopo inayotolewa na mabenki hapa nchini bado ni changamoto kwa wajasiriamali wadogo kwa sababu ni kubwa mno.
“Riba ya mikopo kutoka katika benki za kibiashara hapa nchini bado ni changamoto kwa wajasiriamali wadogo. Riba hizo zinawakwamisha wajasiriamali, zinawaruduisha nyuma na pia wanashindwa kupanua biashara zao,” alisema Bw Laizer.
Alisema ushirikiano wa SIDO na TIB utawasaidia wajasiriamali watakaoingia katika mpango huu kupata maeneo ya kuanza uzalishaji kwa gharama nafuu, alisema kuwa utakuwa ni mkombozi kwa wazalishaji wadogo wadogo nchini. “Tunashukuru uongozi wa TIB kukubali kushirikiana na SIDO katika kusaidia kuwapa maeneo ya kuzalishia bidhaa kwa wingi zaidi ambayo yatasaidia kuwaondolea umasikini na kusaidia kuondoa janga la ukosefu wa ajira nchini,” alisema Bw. Laizer.