SIKU MOJA baada ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kuwatembezea wadau na wanachama wake katika nyumba za mradi wa nyumba za makazi ambazo zimejengwa na Shirika hilo eneo la Buyuni kata ya Majohe Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene nae ametembelea na kujionea nyumba hizo na kuumwagia sifa Mfuko huo kwa ubunifu na kuwajali wananchama wake.
Mbene pia alitembelea Ujenzi wa jingo la Kitegauchumi la Ghorofa 35 linalojengwa na Mfuko huo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu akimpa maelezo Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene juu ya muundo kamili wa Jengo hilo la ghorofa 35 ambalo linajengwa na PSPF jijini Dar es Salaam na litakuwa na maduka, makazi na Ofisi.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Jengo hilo la PSPF Tower, Ghazi Al Shamali (kushoto) akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu juu ya hatua zilizofikiwa hadi sasa katika ujenzi huo.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI