Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa akiongea katika hafla hiyo
Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa akitoa shahada ya heshima kwa waandaaji
Queense Community Collage ambacho ni sehemu ya mtandao wa Vyuo vikuu vya Jiji la New York ( City University of New York ) mwishoni wa wiki kiliandaa maonesho sanaa za kitanzania.
Maonesho hayo yaliyofanyika katika Chuo hicho yanaelezwa na waandaji ni ya kwanza kufanyika nje ya Tanzania na Ujerumani, yalipewa jina la SHANGAA-Art of Tanzania likihusisha mkusanyiko sanaa zaidi ya 112 lakini kila moja ikibeba maudhui yake. Kwa kweli kama lilivyo jina la maonesho hayo, ziliwashagaza wageni mbalimbali waliohudhuria maonesho hayo.
Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ndiye aliyepamba maonesho hayo kama mgeni wa heshima, akiambatana na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania Nchi Marekani, Bi. Lily Munanka.
Sanaa zilizopamba maonyesho hayo zilikuwa ni za kuchonga nyingi kati yake zikitoka katika Mikoa ya Usukumani na Umakondeni. Laini pia kulikuwa na video zilizokuwa zikionyesha aina mbalimbali za ngoma zikionyesha mila na utamaduni wa mtanzania katika uhalisia wake.
Jumla ya sanaa 121 zilikusanywa kutoka wa wadau mbalimbali lakini ni 112 tu zilizoweza kuoneshwa kutokana na uhaba wa nafasi.
Kwa kutambua umuhimu wa maonyesho hayo Halmashauri ya Jiji la New York ilitoa Hati kwa waandaaji wa maonesho hayo.