Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115101

MAADHIMISHO YA VITA VYA MAJIMAJI KUFANYIKA RUVUMA TAREHE 25-27 FEBRUARI 2013

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki atakuwa mgeni rasmi katika siku ya kilele cha maadhimisho ya Kumbukizi ya vita vya Maji Maji na Utalii wa Utamaduni yatakayofanyika Songea mkoani Ruvuma Februari 27 mwaka huu.
Maadhimisho hayo ya siku tatu ambayo kitaifa yameandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Mkoa wa Ruvuma yatafunguliwatarehe 25 Februari katika Makumbusho ya Vita vya Majimaji mjini Songea.
Madhumni ya maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka ni kuwakumbuka mashujaa 67 walionyongwa tarehe 27 Februari 1906 walipokuwa katika harakati za kupinga ukoloni wa Mjerumani.  Baadhi ya mashujaa hao ambao wote walizikwa katika kaburi moja ni Ndugu Mputa Gama, Songea Mbano, Mpambalyoto Soko na MajiyaKuhanga Komba.
Katika siku tatu za maadhimisho wananchi na wadau mbalimbali wa utalii watapata fursa ya kutembelea na kujionea utajiri wa vivutio vya utalii ulioko Kusini mwa Tanzania hususan  Mkoa wa Ruvuma  ili waweze kuongeza uelewa na kushiriki kuvitangaza vivutio hivyo.
Aidha, Wizara itaendesha mdahalo Februari 25 katika Club ya Songea ili kutoa nafasi kwa wadau wa malikale na utalii kujadili namna bora ya kutumia fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii Kusini mwa Tanzania.
Wananchi wote wa mkoa wa Ruvuma, na nchini kote kwa ujumla, wanakaribishwa kuhudhuria maadhimisho hayo ya Kumbukizi ya vita vya Maji Maji na Utalii wa Utamaduni.
G. Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115101

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>