Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza akitoa maelekezo ya kazi kwa (kutoka kushoto) Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa, Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazji Hassan Saleh, Mkuu wa Idara ya Uhandisi - Ubora wa Huduma Nguvu Kamando na Meneja wa Vodacom Pwani Asajile Mwakisunga alipotembelea Kongowe Pwani
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza (wa pili kulia) akiwaelekeza jambo Ofisa MKuu wa Masoko wa Vodacom Charity Safford(wa kwanza kulia) na Mkuu wa Idara ya Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa mjini Kongowe, Mkoani Pwani. Meza jana alifanya ziara ya kukagua mwenendo wa kibiashara wa Vodacom katika meneo kadhaa Mkoani Pwani baada ya Vodacom kufanya maboresho makubwa katika miundombinu ya utoaji wa huduma zake za simu za mkononi mkoani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza (wa pili kulia) akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Uhandisi wa kampuni hiyo Nguvu Kamando wakati Meza alipotembelea eneo la Kibaha kujionea hali ya soko kibiashara kwa Vodacom. Kushoto mwenye fulana nyekundu ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Hassan Saleh
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza(mwenye fulana nyeusi) akiongea na vijana wa Mjini Kongowe namna wanavyopata huduma za Vodacom. Meza jana alitembelea maeneno mbalimbali ya mkoa wa Pwani kujionea upatakinajai wa huduma za Vodacom baada ya kampuni hiyo kufanya maboresho makubwa katika utoaji wa huduma zake mkoani humo
Vijana wa Kongowe mkoani Pwani wakifurahia kasi na ubora wa huduma za Vodacom baada ya kampuni hiyo kufanya maboresho makubwa ya kuongezea nguvu minara yake ili kuboresha huduma zake za simu z amkononi ikiwemo kiupiga simu,intaneti na M-pesa