Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 120391 articles
Browse latest View live

BENKI YA DUNIA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA

$
0
0

Na Benny Mwaipaja, Dodoma


KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba, amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano wake na Benki ya Dunia ili kuharakisha maendeleo ya nchi kiuchumi na kijamii.

Dkt. Mwamba amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia, Kundi Namba Moja Afrika, Dkt. Zarau Kibwe, aliyefika Ofisi za Hazina, Jijini Dodoma, kujitambulisha.

Alisema kuwa mazungumzo yao yalilenga kuchambua fursa zinazopatikana kwenye Benki ya Dunia ambazo Tanzania kama Mwanahisa inaweza kuzifikia na kuzitumia kwa ajili ya maendeleo ya nchi na watu wake.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, anayesimamia maslahi ya nchi 22 za Kanda Namba Moja Afrika kwenye Taasisi hiyo kubwa ya Fedha Duniani, Dkt. Zarau Kibwe, alisema kuwa majadiliano yao yamekuwa na mafanikio makubwa.

Hii ni mara ya kwanza kwa Viongozi hao kukutana kikazi baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba kuteuliwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushika wadhifa wa Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, hivi karibuni.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba (kulia) akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi 22 za Kundi Namba Moja Afrika, Dkt. Zarau Kibwe, aliyefika Ofisi za Hazina, Jijini Dodoma, kwa ajili ya kukutana na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa Benki hiyo na Tanzania.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba, akiongoza mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi 22 za Kundi Namba Moja Afrika, Dkt. Zarau Kibwe (wa tatu kushoto), aliyefika Ofisi za Hazina, Jijini Dodoma, kwa ajili ya kufahamiana na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania. Kulia ni Naibu Kamishna Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Robert Mtengule, kushoto ni Maafisa wa Wizara Idara ya Fedha za NJe Bw. Peter Masolwa na Bw. Charles Longo.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba (kulia) akisisitiza Jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi 22 za Kundi Namba Moja Afrika, Dkt. Zarau Kibwe, aliyefika Ofisi za Hazina, Jijini Dodoma, kwa ajili ya kufahamiana na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa Benki ya Dunia na Tanzania.


Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi 22 za Kundi Namba Moja Afrika, Dkt. Zarau Kibwe, akizungumza jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba (kulia), Ofisi za Hazina, Jijini Dodoma, kwa ajili ya kufahamiana na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa Benki ya Dunia na Tanzania.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)


SERIKALI KUENDELEA KUZISAIDIA KAMPUNI KUKABILIANA NA ATHARI ZA UVIKO – 19

$
0
0

 Na. Peter Haule, WFM, Dodoma.

Serikali imeeleza kuwa inaendelea kutekeleza hatua za kiutawala na kibajeti kusaidia Kampuni za Wazawa zenye Mikopo katika Taasisi za fedha kukabiliana na athari za shughuli zao zilizosababishwa na UVIKO-19.

 

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mpendae Mhe. Taofiq Salim Turky, aliyetaka kujua mpango wa Serikali kusaidia Kampuni za Wazawa zenye Mikopo katika Taasisi za fedha kutokana na athari walizozipata kutokana na UVIKO-19.

 

Mhe. Chande alisema Serikali imeendelea kutekeleza hatua hizo kwa kuwa athari za UVIKO - 19 zilizojitokeza zilitokana na kuvurugika kwa mnyororo wa uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma katika Nchi washirika wa kibiashara ikilinganishwa na soko la ndani ambapo shughuli zote za kibiashara ziliendelea kama kawaida.

 

Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuziagiza benki na taasisi za fedha kutoa unafuu katika urejeshwaji wa mikopo kwa kuongeza muda wa urejeshaji wa mikopo (loan rescheduling)”, alisema Mhe. Chande.

 

Alitaja hatua nyingine zilizochukuliwa kuwa ni pamoja na kuishirikisha Sekta Binafsi katika zabuni za watoa huduma na wakandarasi wakati wa utekelezaji wa Mpango wa Kukabiliana na Athari za UVIKO 19 (TCRP) kwa lengo la kuiwezesha kutengeneza faida na kurejesha mikopo katika benki na taasisi za fedha.

 

Mhe. Chande alisema pia Serikali ilitoa kipaumbele kwa malipo ya malimbikizo ya madeni, madai na marejesho ya kodi yaliyohakikiwa ili kuongeza mzunguko wa fedha katika uchumi na kutoa unafuu wa kikodi, ikiwemo kodi ya kuendeleza ufundi stadi (SDL) kutoka asilimia 4.5 hadi asilimia 4.

 

Aidha, aliongeza kuwa Serikali ilipandisha kiwango cha chini cha idadi ya waajiriwa wanaotakiwa kulipiwa kodi na Kampuni kutoka wafanyakazi 4 hadi 10 ili kupunguza gharama za uendeshaji kwa waajiri ili kuwawezesha kurejesha mikopo kwenye benki na taasisi nyingine za fedha.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb)

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUBALI OMBI LA KUMEGWA ENEO LA HIFADHI KWA AJILI YA UJENZI WA ZAHANATI

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kumegwa eneo la ekari 100 lililokuwa linamilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS ) kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Mninga iliyopo wilayani Mufindi mkoani Iringa

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mninga wilayani Mufindi, Iringa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana ameeleza kuwa uamuzi huo wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan umetokana na yeye kuguswa na kujali afya na maendeleo ya maisha ya wananchi wake.

Amesema eneo hilo lililomegwa ni moja ya sehemu ya Shamba la Miti la Sao Hill ambalo lina miti ya kupandwa aina ya misindano yenye zaidi ya miaka mitano lakini hata hivyo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekubali eneo hilo ijengwe zahanati ili wananchi wasisafiri umbali mrefu.

Amesisitiza kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anathamini sana uhifadhi na yeye ndiye Mhifadhi namba moja lakini kutokana na adha ya wananchi wanayopata kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 16 ameona ni vyema Zahanati ijengwe ili wananchi wahudumiwe kwa urahisi

Katika hatua nyingine, Waziri Balozi Dkt.Pindi Chana amewataka wananchi hao kuacha kusafisha mashamba kwa kutumia moto hali ambayo imekua chanzo cha moto pale unaposhindwa kudhibitiwa na kusababisha hasara .

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi ambaye ni Diwani wa Kata ya Mninga, Mhe.Festo Mgina amesema anamshukuru sana Rais Samia Hassan kwa kukubali ombi la wananchi wa Mninga lililowasilishwa kupitia Halmashauri ya Mufindi na kusisitiza kuwa Zahanati hiyo itawapa ahueni wananchi wake waliosumbuka kwa muda mrefu.

" Tangu nchi hii ipate uhuru wananchi wangu wamekuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu ili kupata huduma za afya lakini kwa kitendo hiki cha Mhe.Rais kutupa eneo la ujenzi wa Zahanati, tunamuahidi tutaendelea kumpa ushirikiano zaidi, amesisitiza Mhe. Mgina
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana akikata utepe katika eneo la Hifadhi la Shamba la Miti.Sao Hili ambapo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 10 limegwe ili Zahanati ya Kata ya Mninga ijengwe

.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi ambaye ni Diwani wa Kata ya Mninga, Mhe.Festo Mgina akizungumza na wananchi wa Mninga amvapo amesema anamshukuru sana Rais Samia Hassan kwa kukubali ombi la wananchi wa Mninga  kumegewa eneo la Hiifadhi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana ( katikati ) akielekea  kukagua eneo la ekari 10 ambalo ni sehemu ya shamba la miti  la Miti Sao Hili ambalo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia eneo hilo  limegwe ili Zahanati ya Kata ya Mninga iweze  kujengwa, Wengine aliombatana nao ni baadhi ya madiwani ww Halmashauri ya wilaya ya Mufindi.


Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Dkt.Pindi Chana akizungumza na wananchi wa Kata ya Mninga kufuatia ombi lao kumegewa sehemu ya eneo la Hifadhi  kwa ajili ya ujenzi wa zahanati kukubaliwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan umetokana na yeye Rais  kuguswa na kujali  afya na maendeleo ya maisha ya wananchi wake.

RAIS MWINYI AZUNGUMZA NA MWAKILISHI NA MKURUGENZI WA OFISI KAMISHNA MKUU WA HAKI ZA BINADAMU KANDA YA AFRIKA MASHARIKI NA UMOJA WA AFRIKA

$
0
0





RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mwakilishi na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Kanda ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika.Bw.Marcel Akpovo, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-2-2023.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mwakilishi na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Kanda ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika Bw.Marcel Akpovo akiwa na ujumbe wake,mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-2-2023.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mwakilishi na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Kanda ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika Bw. Marcel Akpovo, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar na ujumbe wake,mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 10-2-2023.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Kanda ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika.Bw. Marcel Akpovo, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-2-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mwakilishi na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Kanda ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika.Bw. Marcel Akpovo, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-2-2023.(Picha na Ikulu)


RAIS SAMIA AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Gerald Mbonimpa Ndika kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bahame Tom Mukirya Nyanduga kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dosca Kemilembe Mutabuzi kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Rashid Kassim Mchatta kuwa Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Viongozi mbalimbali mara baada ya hafla ya Uapisho wa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Skauti Mkuu Rashid Kassim Mchatta katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Mawaziri, Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Skauti Mkuu Rashid Kassim Mchatta wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Februari, 2023.

MAKINDA: REDIO ZINA UMUHIMU MKUBWA WA KUTOA TAARIFA SAHIHI ZA MATOKEO YA SENSA

$
0
0

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Tanzania Bara, Anne Makinda, ambaye alikuwa mgeni rasmi akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wahariri wa habari wa redio jamii yanyayohusu matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yanayofanyika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali mkoani hapa ambayo  yameanza leo Februari 10, 2023 na yatafikia tamati kesho.

Na Dotto MwaibaleSingida

KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Tanzania Bara, Anne Makinda amesema redio zinategemewa sana na wananchi kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali zinazotolewa na Serikali na taasisi zingine zikiwemo za idara ya takwimu.

Makinda ambaye alikuwa mgeni rasmi ameyasema hayo leo Februari 10, 2023 wakati akifungua mafunzo ya wahariri wa habari wa redio jamii yanyayohusu matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yanayofanyika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali mkoani hapa ambayo yatafikia tamati kesho..

Alisema redio jamii pamoja na zile za mikoa zimekuwa redio pendwa kwa wananchi wa mikoa husika kwa kuwa zinatangaza habari nyingi zinazohusu na kugusa maendeleo ya kiuchumi, kijamii.mazingira na utamaduni wa watu na kwa kufanya hivyo zimejiweka karibu na wananchi wa maeneo yao.

“Redio jamii zinaelezwa ni chombo muhimu katika kujenga jamii zenye mwamko, kuwajengea uwezowananchi kuwasilisha mahitaji yao kwa mamlaka husika kwa urahisi na zaidi zinaaminika na jamii” alisema Makinda.

Aidha Makinda alisema wameanza kutoa mafunzo hayo kwa wahariri wa redio  na wala sio magazeti na televisheni kwasababu redio ni chombo kinachowafikia wananchi kwa urahisi na katika njia rafiki wakati wote tofauti na njia nyingine za upashanaji habari kama vile magazeti na televisheni, hivi sasa Tanzania Bara kila mkoa una vituo vya redio kati ya viwili hadi vitano ukiachia mikoa kama Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Morogoro na Mwanza ambayo ina utitiri wa vituo hivyo.

Alisema sababu kuu ya kuanza mafunzo haya kwa redio ni kutokana na uwezo wa redio kuwafikia wananchi katika maeneo yote ya nchi kama ilivyo katika nchi nyingi zinazoendelea kama Tanzania, redio ndio chombo kikuu kinachotegemewa na wananchi wengi kupata habari na kuwa hapa nchini hivi sasa, redio zimejipambanua kwa kuwa na vituo vya redio zaidi ya 200.

Aidha, Makinda alisema kutokana na maendeleo ya teknolojia, siku hizi huhitaji tena kuwa na redio ili uweze kupata matangazo ya redio bali yamerahisishwa hadi mwananchi anaweza kupata matangazo ya redio kiganjani yaani kupitia simu ya mkononi ikiwemo simu za bei nafuu maarufu humu nchini kama Vitochi au kiswaswadu.

“ Matangazo ya redio yanapatikana pia kwa njia ya mtandao yaani intaneti. Katika hali hiyo, nidhahiri kuwa redio ndio chombo pekee ambacho watanzania wengi wanakitegemea kupata taarifa. Mathalan, hata tafiti ambazo tulizifanya wakati wa kupima uwelewa wa wananchi kuhusu Sensa, asilimia 49.0 walisema wamepata taarifa za Sensa kupitia redio ikifuatiwa na asilimia 47kupitia ujumbe mfupi kupitia simu za kiganjani. Hivyo, mafunzo haya kwetu ni muhimu sana kwa kuwa tuna uhakika kuwa yakifanikiwa wananchi wetu wataweza kupata matokeo ya Sensa kwa urahisi zaidi na kusaidia utekelezaji wa mpango kazi wa usambazaji wa mafunzo ya matokeo ya Sensa” alisema Makinda. 

Akizungumza kwa niaba ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa, Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Mkoa wa Singida,  Naing'oya Kipuyo, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuviwezesha vyombo vya habari kuwa na uelewa mpana wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ili viweze kutimiza wajibu wao wa kusambaza, kuelimisha na kuhamasisha wananchi kutumia matokeo ya Sensa na vikifanya hivyo, vitakuwa vimetimiza wajibu wao kwa taifa hususan kufanikisha malengo ya sensa.

“ NBS imekuwa ikiandaa mafunzo ya aina hii kwa vyombo vya habari mara kwa mara kwa kuwa jukumu letu la uzalishaji na usambazaji takwimu linakuwa rahisi kama tutakuwa na ushirikiano mzuri na wa karibu na vyombo hivi” alisema Kipuyo.

 Aidha, Kipuyo alisema kwa kawaida kabla ofisi yao haijafanya mazoezi makubwa ya ukusanyaji takwimu ikiwemo Sensa ya Watu na Makazi wana utaratibu wa kuvifanyia mafunzo maalum vyombo vya habarikuwawezesha kuwa na ufahamu mpana wa tafiti ili viweze kuielewesha jamii kuhusu mazoezi hayo na inafanya hivyo hivyo, hata baada ya matokeo kutolewa  ili kuwaelewesha nini kimejiri katika tafiti hizo kwa kuwafundisha na kuwafafanulia matokeo hayo kwa kina iliviweze kuyasambaza kwa wadau wote ipaswavyo.

Alisema katika mnasaba huo, NBS imejenga uhusiano na ushirikiano wa karibu na vyombo vya habari nchini na kama ilivyo kuwa wakati wa Sensa kwani havikuwaangusha kabisavilifanya kazi nzuri na matokeo yake yameonekana.

“Vyombo vya habari ni sehemu ya mafanikio tuliyoyapata katika utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ambayo ilikuwa ya kihistoria. Hivyo, sina shaka yoyote kuwa vyombo vya habari vitaendelea na mwenendo ule ule wa kuzipa umuhimu habari za Sensa ambapo kwa sasa ni matokeo ambayo yanapaswa kuwafikia wananchi popote walipo hivyo naomba nichukue fursa hii kuvishukuru kwa dhati” alisema Kipuyo.

Mratibu wa Mtandao wa Redio za Kijamii nchini (TADIO)  Cosmas Lupoja alisema mtandao huo umekuwa ukifanya kazi kwa karibu na Serikali na taasisi mbalimbali na kuwa unajumuisha redio wanachama 42 Zanzibar zikiwa tano 5na Tanzania Bara 37.

“Wanachama wetu wengine ni Chama cha Waandishi wa Habari Pemba (Pemba Press Club) Dodoma TV na Dodoma FM ambapo kwa ujumla tuna kuwa 44” alisema Lupoja.

Lupoja alitumia nafasi hiyo kuwashukuru sana Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa ushirikiano mkubwa wanao wapa kwa kuwashirikisha kuanzia mwanzo wa mchakato wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 hadi mwisho wake na kueleza kuwa redio za kijamii zimekuwa na mchango mkubwa kutokana na kuwafikia watu wengi zaidi ambapo aliomba ushirikiano huo uendelee kudumu.

Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Mkoa wa Singida,  Naing'oya Kipuyo (kushoto) akitoataarifa kwa niaba ya  Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa.
Mratibu wa Mtandao wa Redio za Kijamii nchini (TADIO)  Cosmas Lupoja akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mratibu wa Mafunzo hayo, Said Ameir akifanya utambulisho kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Tanzania Bara, Anne Makinda, akisalimiana na washiriki wa mafunzo hayo.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Tanzania Bara, Anne Makinda, akisalimiana na washiriki wa mafunzo hayo muda mfupi baada ya kupiga nao picha.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Tanzania Bara, Anne Makinda, akisalimiana na mshiriki wa mafunzo hayo Mhariri wa RedioMwangaza, Godfrey Lutego.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.
Ufunguzi wa mafunzo hayo ukiendelea.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo, Godfrey Lutego kutoka Dar es Salaam na Meneja Redio Unyanja FM Patrick Kosima (kulia) kutoka Nyasa mkoani Ruvuma wakiteta jambo wakati wa mafunzo hayo.



Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa busy.
Taswiraya washiriki wa mafunzo hayo.
 Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Tanzania Bara, Anne Makinda (katikati waliosimamam mbele) , ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.

Wataalamu JKCI Waadhimisha siku ya wapendanao kwa kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto 28

$
0
0


Na Salome Majaliwa – JKCI

10/02/2023 Watoto 28 wenye magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo katika kambi maalumu ya siku tano ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wazawa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

Kambi hiyo maalum ya upasuaji wa moyo ilifanyika kwa lengo la kusherehekea siku ya wapendanao itakayofanyika duniani kote tarehe 14 Februari mwaka huu ambapo wataalamu hao wameiadhimisha kwa kuonesha upendo wao kwa watoto wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo kutokukaa katika mpangilio wake.

Akizungumza wakati wa kambi hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya alisema kambi hiyo imefanyika mahususi kwa watoto wenye magonjwa ya moyo ili kuwapa upendo na kurejesha tabasamu kwao kwani watoto hao hupitia maumivu makali kutokana na maradhi waliyonayo.

Dkt. Angela ambaye pia ni daktari wa usingizi alisema Idadi ya watoto wenye magonjwa ya moyo inaongezeka kila siku kwani watoto huendelea kuzaliwa, hivyo Idara ya upasuaji ikaona ni vizuri kufanya kambi hiyo huku lengo likiwa kupunguza idadi ya watoto hao wanaosubiria huduma ya upasuaji.

“Sisi kama madaktari pia ni wazazi na tumebarikiwa kuwa na watoto, tunaelewa mtoto anapokuwa mgonjwa wazazi wanakuwa kwenye wakati mgumu na kupelekea baadhi ya mambo kwenye familia kusimama ndio maana tumeona ni vizuri kufanya kambi hii ili kupunguza idadi ya watoto wanaosubiri matibabu pamoja na kuwapa furaha”, alisema Dkt. Anjela .

Naye Daktari wa bingwa wa upasuajiwa moyo na mishipa ya damu kwa watoto wa JKCI Godwin Sharau alisema katika kambi hiyo walifanya upasuaji wa kuziba matundu kwenye moyo, kuachanisha mishipa iliyokaribiana pamoja na kuzibua mishipa iliyoziba.

“Tumewafanyia upasuaji mkubwa wa moyo watoto ambao mioyo yao ina matundu pamoja na wale ambao mishipa yao ya damu imeziba haipeleki damu vizuri kwenye moyo”,.

“Upasuaji tulioufanya katika kambi hii tumekuwa tukiufanya sisi kama wataalamu wazawa lakini kwa kufanya kambi maalumu tumewafikia watoto wengi zaidi kwa kipindi cha muda mfupi”, alisema Dkt. Sharau.

Daktari huyo bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto alisema uzoefu wa madaktari wazawa wa upasuaji wa moyo kwa watoto umeongezeka kwani hapo awali kuna baadhi ya upasuaji kama wazawa walikuwa hawawezi kufanya lakini sasa wamebobea katika matibabu hayo bila hata ya kuwa na uangalizi kutoka kwa wenzao wa nchi mbalimbali ambao wamekuwa wakifanya nao upasuaji huo.

Dkt. Sharau alisema kutokana na ufinyu wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo idadi ya watoto waliohudumiwa imekuwa chache lakini kama wodi hiyo ingekuwa kubwa watoto wengi zaidi wangefanyiwa upasuji huo.


“Watoto tuliowafanyia upasuaji wanaendelea vizuri na wengine wameshatoka katika wodi ya uangalizi maalum (ICU) na kupelekwa wodini kwa ajili ya kuendelea na matibabu ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi”, alisema Dkt. Sharau.

Kwa upande wa wazazi ambao watoto wao wamefanyiwa upasuaji katika kambi hiyo waliishukuru JKCI kwa matibabu waliyayatoa kwa watoto wao na kuomba kambi kama hizo ziwe zinafanyika mara kwa mara ili watoto wengi zaidi waweze kutibiwa kwa muda mfupi.

Rehema Yacob ambaye mtoto wake alizaliwa na tundu kwenye moyo pamoja na mshipa mmoja wa damu kutokupeleka damu vizuri kwenye moyo alisema kama JKCI isingekuwepo hapa nchini asingeweza kumpeleka mtoto huyo nje ya nchi kutokana na kipato chake kuwa kidogo hivyo kushindwa kumudu gharama za matibabu.

“Kutokana na ugonjwa huu wa moyo mtoto wangu alichelewa kutembea, lakini pia baada ya kutembea alikuwa akichoka mapema hivyo kushindwa kujumuika na wenzake kufanya michezo mbalimbali. Baada ya kufanyiwa upasuaji naona mabadiliko kwani sasa amechangamka na anafanya mazoezi”,.

“Kupitia changamoto za mwanangu niliona umuhimu wa kuwa na bima ya afya hivyo kutafuta bima hiyo ambayo imenisaidia kupata matibabu kiurahisi, nawashauri wazazi wenzangu kuwakatia watoto wao bima ya afya kwani matatizo huja ghafla”, alisema Rehema.




Wataalam wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifanya upasuaji wa kuziba tundu la moyo katika kambi maalum ya matibabu ya siku tano inayofanywa na wataalamu wazawa wa Taasisi hiyo ambapo watoto 28 walifanyiwa upasuaji.


Wataalam wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifanya upasuaji wa kuzibua mshipa wa damu wa moyo uliokuwa umeziba wakati wa kambi maalum ya siku tano iliyofanywa na madaktari hao ambapo watoto 28 walifanyiwa upasuaji.

Picha na JKCI

ATAKAYEMZUIA MWANAFUNZI KUPATA ELIMU KUCHUKULIWA HATUA-MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitosita kumchukulia hatua mzazi au mtu yeyote atakayemzuia mwanafunzi kupata haki yake ya elimu, hivyo amewataka wazazi wote wenye wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza kuhakikisha kuwa watoto hao wanaripoti kwenye shule walizopangiwa mara moja.

 

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Februari 10, 2023) wakati akiahirisha Mkutano wa 10 wa Bunge la 12, Bungeni Jijini Dodoma. Waziri Mkuu ametumia fursa hio kuziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo bado hazijakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa kuhakikisha vyumba hivyo vinakamilika.

 

Mheshimiwa Majaliwa amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali ilitoa shilingi bilioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 8,000 vya madarasa katika shule za sekondari ikiwa ni maandalizi ya kupokea wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023.

 

Waziri Mkuu amesema hadi kufikia tarehe 03 Februari 2023 vyumba vya madarasa 7,874 sawa na asilimia 98.43 vimekamilika na vyumba vya madarasa 126 sawa na asilimia 1.57 vipo katika hatua mbalimbali za umaliziaji.

 

“Ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya sekondari umewezesha wanafunzi wote 1,076,037 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2022 kupata fursa ya kupangiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwezi Januari 2023 kwenye shule za Serikali kwa awamu moja pekee.”

 

“Mafanikio haya ni kielelezo tosha cha umakini, uzalendo, maono na kazi iliyotukuka inayotekelezwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kulinda maslahi na kujenga mustakabali mzuri wa Taifa letu.”

 

Akizungumzia kuhusu uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza na awali,Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kufanya vizuri ambapo hadi kufikia tarehe 03 Februari, 2023 wanafunzi 1,363,320 wa darasa la awali wameandikishwa wakiwemo wenye mahitaji maalum 2,944 sawa na asilimia 100.18 ya lengo la kuandikisha wanafunzi 1,360,737.

 

Waziri Mkuu amesema katika kipindi hicho wanafunzi 1,657,533 wakiwemo wenye mahitaji maalum 3,825 waliandikishwa kwa ajili ya darasa la kwanza sawa na asilimia 101.29 ya wanafunzi 1,633,659 waliotarajiwa kuandikishwa.

 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kudhibiti matumizi ili kuendana na mpango na bajeti ya 2022/2023, ambapo ametumia fursa hiyo kuielekeza Wizara na taasisi zote za Serikali kuzingatia vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/2024 katika maandalizi ya bajeti za mafungu husika.

 

Waziri Mkuu amezielekeza Halmashauri zote nchini zenye mapato yasiyolindwa chini ya shilingi bilioni mbili (Kundi C), zihakikishe zinatenga kiasi kisichopungua asilimia 20 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikijumuisha asilimia 10 ya mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu;

 

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka Wakuu wote wa Mikoa wahakikishe wanasimamia kwa karibu miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao ili miradi hiyo iweze kuakisi thamani ya matumizi ya fedha za umma.

 

Pia, Mheshimiwa Majaliwa amewaelekeza  Maafisa Masuuli wote wazingatie kikamilifu maelekezo yote yaliyopo kwenye Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2023/2024 ikiwa ni pamoja na kuzingatia kikamilifu Sheria ya Bajeti (SURA 439) na Kanuni zake.

 



MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AIPONGEZA BODI YA WAKALA WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

$
0
0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza Bodi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na uongozi wake kwa kutekeleza kajukumu yao kwa mafanikio makubwa.

Mhe. Hemed ametoa Pongezi hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na Bodi hiyo Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.

Amesema ni muda mchache tokea kuanzishwa kwa Wakala huo ambapo wameanza kutekeleza dhamira ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ya kuwawezesha wanchi kupata mitaji na kutoa fursa za kukuza uchumi na kupunguza changamaoto zinazoikabili jamii.

Amesema ni vyema kwa wakala huo kuanzisha mifumo ya kieletroniki katika shughuli za uendeshaji ili kuweza kutoa huduma bora Zaidi na gharama nafuu kwa wananchi.

Aidha Mhe. Hemed ameridhishwa na utendaji kazi wa wakala kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na Sekta binafsi na washirika wa maendeleo ndani na nje ya nchi katika utafutaji na upatikanaji wa rasilimali fedha.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Ndg. Juma Amour Mohammed amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa baada ya kuchaguliwa kwa Bodi hiyo wameweza kutayarisha muundo wa taasisi pamoja na kuandaa mpango mkakati na kuratibu upatikanaji wa rasilimali fedha.

Aidha ameeleza kuwa Bodi inaendelea na mazungumzo na wadau mbali mbali wa Maendeleo kwa lengo la kukuza sekta ya Uwezeshaji nchini.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa wakala wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi Ndg. Juma Burhan amesema kuwa jumla ya wananchi 17,665 wamenufaika na fedha za uwezeshaji kati ya hao 8686 kutoka unguja wakiwemo wanaume 3311 na wanawake 5375 aidha kwa upande wa Pemba jumla ya wananchi 8979 wamenufaika wakiwemo wanaume 3425 na wanawake 5554.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Bodi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na uongozi wake waliofika kijitambulisha Ofisini kwake Vuga.

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA 18 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA UCHUKUZI, MAWASILIANO NA HALI YA HEWA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshiriki Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) unaofanyika jijini Bujumbura, Burundi

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajabu

Mkutano huo ulianza tarehe 6 - 8 February 2023 kwa ngazi ya wataalamu waandamizi, ulifuatiwa na kikao cha ngazi ya makatibu wakuu uliofanyika tarehe 9 Februari 2023 na utakamilishwa kwa kuwakutanisha Mawaziri katika kikao kitakachofanyika tarehe 10 Februari 2023 jijini humo.

Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu umepokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa Programu na Miradi; Maamuzi; na Maagizo ya Mikutano ya awali katika sekta za Mawasiliano; Hali ya Hewa na Miundombinu ya Uchukuzi inayojumuisha sekta za Barabara, Vituo vya Huduma kwa pamoja Mipakani (OSBP), Reli, Usafiri wa anga na Bandari kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkutano huo pia ulipokea taarifa ya utekelezaji wa Maagizo 12 kati 34 ya mikutano ya awali ya Baraza la Mawaziri wa sekta husika yaliyokamilika na maagizo mengine yaliyosalia utekelezaji wake upo katika hatua mbalimbali.

Mkutano huo unahudhuriwa na washiriki kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia sekta za ujenzi, uchukuzi, mawasiliano na fedha.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajabu (kushoto) akifuatilia Mkutano wa 8 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) unaoendelea jijini Bujumbura, Burundi
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajabu (kushoto) akifuatilia Mkutano wa 8 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) unaoendelea jijini Bujumbura, Burundi. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe. Balozi Jilly Maleko
Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) ukiendelea jijini Bujumbura, Burundi 

RC NAWANDA AKABIDHI PIKIPIKI ZILIZOTOLEWA NA RAIS SAMIA KWA MAAFISA UGANI MKOA WA SHINYANGA

$
0
0



Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda amekabidhi pikipiki 224 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maafisa ugani kilimo mkoa wa Shinyanga.

Hafla fupi ya ugawaji wa pikipiki kwa maafisa ugani imefanyika leo Ijumaa Februari 10,2023 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi na maafisa ugani kutoka wilaya za Kishapu, Shinyanga na Kahama.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yahaya Nawanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema jumla ya pikipiki zilizotolewa mkoa wa Shinyanga ni 224 ambapo Wilaya ya Kahama inapata pikipiki 100, Shinyanga 82 na Kishapu 39.

“Pikipiki hizi ni kutoka kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan. Nendeni mkazitunze zidumu ili kufikia malengo ya 10/30 ambapo tunataka kilimo kichangie asilimia 10 ya mapato ya nchi ifikapo mwaka 2030. Msizigeuze za kufanyia anasa wala kufanyia biashara ya bodaboda bali kazitumieni kuleta tija kwa wananchi/wakulima. Tunataka mzitumie kusaidia wananchi na si vinginevyo”,amesema Dkt. Nawanda.

“Pikipiki hizi ni mali ya Serikali, hizi ni fedha za umma na Mhe. Rais Samia ameleta pikipiki hizi ili tuongeze tija katika kilimo, tufanye kilimo biashara. Tunataka tuone tija ya pikipiki hizi, hatuwezi kufikia ajenda ya 10/30 kwa kupiga maneno tu hivyo tunataka vitendo zaidi ili kuwasaidia wakulima”,ameongeza Dkt. Nawanda.


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira kubwa inayoonesha katika kuleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya kilimo ikiwemo kuongeza bajeti katika sekta ya Kilimo huku akieleza kuwa Serikali itakeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo.

Kwa upande, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi wameahidi kusimamia matumizi yaliyokusudiwa ya pikipiki hizo huku wakiwasisitiza maafisa ugani kuepuka kubadilisha matumizi ya pikipiki hizo.

Nao baadhi ya maafisa ugani wameishukuru serikali kwa kuwapatia vitendea kazi hivyo wakisema vitawasaidia kuwafikia wakulima wengi zaidi ili kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Februari 10,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga

Muonekano wa sehemu ya pikipiki 224 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga.

Muonekano wa sehemu ya pikipiki 224 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga.

Muonekano wa sehemu ya pikipiki 224 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga.

Muonekano wa sehemu ya pikipiki 224 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga.

Muonekano wa sehemu ya pikipiki 224 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude (kushoto) pikipiki kwa maafisa ugani wilayani Kishapu

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi pikipiki kwa maafisa ugani wilayani Shinyanga.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude (katikati) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko wakijaribishia pikipiki zilizotolewa kwa maafisa ugani

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda (katikati) , Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude (wa pili kushoto) ,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko (kushoto), Mwenyekiti wa CCM Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi wakiwa wamepanda kwenye pikipiki zilizotolewa kwa maafisa ugani

Maafisa ugani na wadau wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi pikipiki kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga

RAIS WA HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA MWAKILISHI NA MKURUGENZI WA OFISI YA KAMISHNA MKUU WA HAKI ZA BINADAMU KATIKA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI NA UMOJA WA AFRIKA

$
0
0

AIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mwakilishi na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Kanda ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika.Bw.Marcel Akpovo, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-2-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Kanda ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika.Bw. Marcel Akpovo, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-2-2023.(Picha na Ikulu)   
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mwakilishi na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Kanda ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika.Bw. Marcel Akpovo, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-2-2023.(Picha na Ikulu)   

DKT. TAX ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA UTURUKI

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa Uturuki Jijini Dar es Salaam, kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Uturuki tarehe 6 Februari, 2023.

Baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, Dkt. Tax ametoa salamu za pole kwa Serikali ya Uturuki na kuwasihi kuendelea kuwa wavumilivu wakati huu wa msiba mkubwa kwa Taifa hilo uliosabaisha vifo vya watu zaidi ya 18,000.

“Serikali ya Tanzania na Watanzania kwa ujumla tunaungana na Serikali ya Uturuki katika kuombeleza msiba huo mzito,” alisema Dkt. Tax.

Mwaka 1999 Uturuki ilikumbwa na tetemeko la ardhi ambapo watu wapatao 17,000 walipoteza maisha kutokana na tetemeko hilo. Kadhalika, mwaka 2011 ilikumbwa na tetemeko la ardhi katika mji wa Van lilipelekea vifo vya watu 500.



 

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA UNAENDELEA KUTEKELEZWA-BYABATO

$
0
0

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato amesema kuwa, utekelezaji wa mradi Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania (EACOP) unaendelea kutekelezwa na kwamba shughuli mbalimbali zinaendelea kufanyika nchini Tanzania na Uganda.


Naibu Waziri amesema hayo tarehe 10 Februari, 2023 wakati Wajumbe wapya wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe.Dunstan Kitandula walipopewa semina na Wizara ya Nishati kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta (EACOP) , Nishati Safi ya Kupikia na ushiriki wa watanzania katika mradi wa EACOP. 

Semina hiyo ilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Byabato ametaja baadhi ya shughuli hizo kuwa ni pamoja na utwaaji wa ardhi ya mkuza wa bomba ambapo hadi tarehe 31 Januari 2023 jumla ya wananchi 8,781 wamesaini mikataba na asilimia 95.2 ya wananchi hao tayari wamelipwa fidia, na kwamba wananchi waliobaki wanaendelea kupatiwa elimu na kusainishwa mikataba ya fidia.

Aidha, amesema kuwa, ujenzi wa karakana ya kuhudumia vipande 86,000 vya mabomba yatakayotumika kwenye mradi huo, inayojengwa katika eneo la Sojo-Nzega umefikia asilimia 58.

Wajumbe hao pia walielezwa jitihada zinazofanywa na Serikali katika usambazaji wa nishati safi na salama ya kupikia vijijini ambapo moja ya juhudi hizo ni  usambazaji nishati ya gesi asilia kwa ajili ya kupikia katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani ambapo kazi hiyo inafanywa na TPDC kwa kushirikiana na REA.
Jitihada nyingine ni pamoja na kusambaza majiko banifu ambayo, hayatumii mkaa mwingi pamoja na kuni nyingi ambayo pia hayatoi moshi mwingi, pia, Serikali kuendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kuongeza kasi ya upatikanaji nishati safi vijijini ikiwemo kujenga mitambo ya bayogesi katika taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 300.

Katika Semina hiyo Wajumbe wa Kamati pia walipata uelewa kuhusu EWURA inavyosimamia ushiriki wa watanzania katika mradi wa EACOP na jitihada zinazofanywa na Serikali ili kutatua changamoto mbalimbali zinazotokea kwa baadhi ya kampuni za kitanzania zinapopata changamoto ya utekelezaji wa kazi walizopata katika mradi huo.

Kamati hiyo ya Bunge pamoja na  kupongeza  Wizara ya Nishati kwa ubunifu wa mradi wa nishati safi ya kupikia, walitoa maoni mbalimbali yatakayoboresha utekelezaji wa mradi huo pamoja na miradi mingine ya nishati inayoendelea kutekelezwa nchini.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dunstan Kitandula  akizungumza wakati Wizara ya Nishati ilipotoa semina kuhusu  Mradi wa Bomba la Mafuta (EACOP), Nishati Safi ya Kupikia na ushiriki wa watanzania katika mradi wa EACOP   kwa Wajumbe wapya wa Kamati hiyo jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato na kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali.Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akizungumza wakati Wizara ya Nishati ilipotoa semina kuhusu  Mradi wa Bomba la Mafuta (EACOP), Nishati Safi ya Kupikia na ushiriki wa watanzania katika mradi wa EACOP   kwa Wajumbe wapya wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma.



 

MKUU WA WILAYA YA TUNDURU WAKILI JULIUS MTATIRO ATANGAZA KUWAFUKUZA WAFUGAJI WASIOTAKA KWENDA KWENYE VITALU,AFUNGUA NYUMBA YA KULALA WAGENI YA MFUGAJI IKIWA NI UTEKELEZA WA AGIZO LA SERIKALI LINALOWATAKA WAFUGAJI KUPUNGUZA SEHEMU YA MIFUGO YAO NA KUWEKEZA KWENYE MIRADI MINGINE YA KIUCHUMI

$
0
0

Na Muhidin Amri, Tunduru

SERIKALI ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma imesema,itawakamata na kuwatoza faini  kubwa wafugaji  wote wanaoishi kiholela na kuchunga mifugo nje ya maeneo yaliyotengwa(vitalu).

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro,wakati akizungumza na wafugaji wakati wa ufunguzi wa nyumba ya kulala wageni ya Kajima Guest House iliyojengwa na mfugaji wa jamii ya Kisukuma Mahembo Shamba.

Mfugaji huyo amelazimika kuuza sehemu ya mifugo yake na kujenga nyumba ya kulala wageni, ikiwa ni utekelezaji wa agiza la serikali linalowataka wafugaji kupunguza mifugo na kuwekeza kwenye miradi mingine ya maendeleo.

Aidha Mtatiro alisema,wafugaji watakaochelewa kwenda kwa hiari kwenye vitalu vilivyotengwa kwa ajili ya shughuli za ufugaji na kukuta vimejaa wataondolewa kwa nguvu na kupelekwa nje ya mipaka ya wilaya hiyo.

Alisema,hatua hiyo ni maamuzi halali ya serikali katika kumaliza migogoro ya mara kwa mara kati ya wafugaji na wakulima iliyoanza kutokea wilayani humo huku chanzo kikitajwa ni kuwepo kwa baadhi ya wafugaji wasiotaka kufuata sheria na taratibu.

Alisema,katika utekelezaji wa operesheni hiyo,serikali itatumia vikosi vya ulinzi na usalama,ikiwa ni juhudi za kuwaondoa kabisa wafugaji na ufugaji holela unaofanywa na wafugaji wauni katika maeneo mbalimbali wilayani humo.


“serikali inawapenda wananchi wote wakiwamo wafugaji na ndiyo maana imeandaa utaratibu wa kutenga jumla ya vitalu 279 vyenye ukubwa wa ekari 500 kila kimoja  kwa ajili ya shughuli ya ufugaji”alisema Mtatiro.


Kwa mujibu wa Mtatiro,licha ya mapenzi makubwa ya serikali kwa jamii ya wafugaji wilayani humo,lakini bado kuna  wafugaji  wanakahidi na kufanya ufugaji kiujanja ujanja kwenye makazi ya wakulima na kusababisha migogoro mingi kati ya makundi hayo mawili.

Alisema,wilaya ya Tunduru ni ya kilimo licha ya kukaribisha wafugaji,hata hivyo suruhisho la migogoro inayojitokeza kati ya wakulima na wafugaji ni lazima wafugaji wakapelekwa katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli zao.

Mtatiro,amempongeza mfugaji huyo kwa kuitikia wito wa serikali kwa kupunguza idadi ya mifugo yake na kufanya uwekezaji wa nyumba ya wageni na kuwataka wafugaji wengine kuiga mfano huo.

Kwa upande wake mfugaji huyo alisema,amelazimika kujenga nyumba ya wageni baada ya kupoteza sehemu kubwa ya mifugo yake mkoani Mbeya na Morogoro na amelazimika kuja wilayani Tunduru baada ya kusikia kuna mazingira mazuri  kwa ajili ya kuchungia.

Alisema,hadi kukamilika kwa nyumba hiyo  yenye vyumba 10 vya kulala wageni ametumia fedha nyingi baada ya kuuza Ng’ombe 220 na kuwataka wafugaji wengine kupunguza mifugo yao na kuwekeza katika miradi mingine ya kiuchumi.


ZABUNI YA KUUZA MRADI WA DEGE BADO IPO KATIKA MCHAKATO

$
0
0

-Mkurugenzi Mkuu asema thamani ya Mfuko imeongezeka na fedha za wanachama zipo salama

Zabuni iliyotangazwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya kuuza mradi wa Dege Eco Village uliopo Kigamboni, Dar es Salaam, bado ipo katika mchakato.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Mfuko kwa mwaka wa fedha 2022/23 katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.

Alisema mradi huo uliamuliwa uuzwe baada ya kufanyika tathimini mwaka 2020 na kwamba kuuzwa kwa mradi huo kutarudisha gharama  zilizotumika.

"Hivi sasa tulitangaza Zabuni ambayo bado ipo katika mchakato na endapo ikatokea kwamba hatujapata mtu ambaye amefika bei ya kurudisha ile gharama maana yake ni kuwa tutatangaza tena kwa mara nyingine," alifafanua.

Alisema kwa jinsi ambavyo wawekezaji wanavyoongezeka nchini wataweza kununua mradi huo katika kiwango ambacho kitakuwa na manufaa kwa Mfuko.

Mshomba alisema kuuzwa kwa mradi huo kutakuwa na faida kwa wanachama na Taifa kwa ujumla kwa maana kutaepusha hasara ambazo Mfuko ungepata kutokana na kuendelea nao.

Masha aliwahakikishia wanachama kuwa Mfuko upo salama na kwamba thamani ya Mfuko imeongezeka na kufikia shilingi trilioni 6.6 mwezi Desemba 2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 36 kutoka shilingi trilioni 4.7 iliyokuwa mwezi Machi, 2021.

“Ongezeko hili linatokana na kuongeza michango ya wanachama pamoja na mapato yatokanayo na uwekezaji, hivyo ukuaji huu wa Mfuko unathibitisha kuwa NSSF ipo imara na endelevu kwa ajili ya utoaji huduma za hifadhi ya jamii nchini,” amesema Mshomba.

Alisema katika mwaka wa fedha unaoishia mwezi Juni 2023, Mfuko unatarajia kukusanya michango ya shilingi trilioni 1.6 ambayo ni ongezeko la asilimia 14 ukilinganisha na michango ya shilingi trilioni 1.4 kwa mwaka 2021/22.

Mshomba amesema mapato yatokanayo na uwekezaji kwa mwaka 2022/23 yanatarajiwa kuendelea kuwa shilingi bilioni 700 kiasi ambacho ni ongezeko kubwa ukilinganisha na miaka ya hivi karibuni ambapo mapato hayo yalikuwa chini ya shilingi bilioni 500.



TANZANIA, IRAN KUSHIRIKIANA SEKTA ZA KIMKAKATI

$
0
0

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimeahidi kushirikiana katika sekta za kimkakati hususani kilimo, pamoja na biashara na uwekezaji kwa lengo la kukuza na kuimarisha diplomasia ya uchumi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) katika sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya siku ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Tanzania zilizofanyika tarehe 10 Februari 2023 Jijini Dar es Salaam.

“Tanzania na Iran tumekuwa tukishirikiana katika maeneo mbalimbali, hadi sasa tumekuwa tukishirikiana katika sekta za elimu, afya, utalii, nishati, madini. Pia kwa sasa Irani imeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya kilimo hasa ukizingatia kilimo ni kipaumbele cha Serikali,” alisema Dkt. Tax

Waziri Tax ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na Iran katika maeneo mapya ya kimkakati ikiwemo sekta ya kilimo ili kupata uzoefu katika maendeleo na uwekezaji wa kuifanya nchi kuwa na uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha pamoja na kuongeza viwanda.

Akielezea kuhusu biashara na uwekezaji, Dkt. Tax alisema kuwa kupitia kongamano la wafanyabiashara na wawekezaji lililofanyika Mwezi Agosti, 2022 limefungua fursa za biashara na uwekezaji. “Tanzania inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuwavutia wafanyabiashara na wawekezaji wengi zaidi kuwekeza nchini,” alisema Dkt. Tax

Naye Balozi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh alisema kuwa Iran imekuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Tanzania kwa miaka 40 hadi sasa na mataifa hayo yamekuwa yakishirikiana kijamii, kisiasa, kiuchumi na utamaduni kwa maslahi ya pande zote mbili.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Tanzania zimekuwa marafiki wa muda mrefu na itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza na kuimarisha sekta za kilimo, elimu, afya pamoja na biashara na uwekezaji kwa maslahi ya mataifa yote mawili.

Balozi Alvandi aliongeza kuwa mazingira ya biashara kati ya Iran na Tanzania yanaridhisha kwani hadi mwaka jana 2022 biashara kati ya Iran na Tanzania iliongezeka kutoka dola milioni 20 hadi dola milioni 70.

“Biashara kati ya Iran na Tanzania imeongezeka kutoka dola milioni 20 hadi dola milioni 70 mwaka jana, hii ni ishara kuwa uchumi wa mataifa yetu mawili unazidi kuimarika,” alisema Balozi Alvandi

Tanzania na Iran zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1983 na zimekuwa zikishirikiana katika sekta za biashara, kilimo, masoko, utalii, uwekezaji, afya, madini, nishati na utaalamu.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akikata keki pamoja na Balozi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh wakati wa maadhimisho ya miaka 44 ya siku ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Tanzania zilizofanyika tarehe 10 Februari 2023 Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwasiliha hotuba yake katika sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya siku ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Tanzania zilizofanyika tarehe 10 Februari 2023 Jijini Dar es Salaam




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa amesimama na Balozi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh katika sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya siku ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Tanzania zilizofanyika tarehe 10 Februari 2023 Jijini Dar es Salaam




Balozi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh akizungumza katika maadhimisho ya miaka 44 ya siku ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Tanzania tarehe 10 Februari 2023 Jijini Dar es Salaam



Sehemu ya washiriki wakifuatilia maadhimisho ya miaka 44 ya siku ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Tanzania tarehe 10 Februari 2023 Jijini Dar es Salaam



BARRICK NORTH MARA YAWA MWENYEJI KIKAO CHA TAIFA CHA SHIMMUTA

$
0
0


Mwenyekiti wa SHIMMUTA Taifa,Roselyne Massam akizungumza wakati wa kikao hicho

Mgodi wa Barrick wa North Mara, umekuwa mwenyeji wa kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma, Kampuni na Taasisi Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) ngazi ya Taifa kilichofanyika kwa mara ya kwanza mkoani Mara.


Kikao kilifunguliwa na Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi huo, Jan Jacobs, ambaye alieleza kuwa kampuni inayo program ya kuhakikisha wafanyakazi wake wanaimarisha afya zao kupitia michezo na mazoezi.


Mwenyekiti wa SHIMMUTA Taifa, Roselyne Massam ambaye aliongoza kikao hicho alisema kuwa lengo la kukutana ni kuweka mikakati, kufanya tathmini ya mashindano ya michezo mbalimbali yatakayoendeshwa na shirikisho hilo, lakini pia kuamua yafanyike lini na wapi mwaka huu.

“Tunaishukuru Barrick kama mwanachama na mdau wetu wa SHIMMUTA kukubali ombi letu la kuja kufanya kikao hiki hapa, hakika kikao kimekuwa cha mafanikio,” alisema Roselyne Massam.

Katibu wa SHIMMUTA Taifa, Dkt. Maswet Crescent Masinda, alisema kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Taifa, na maagizo ya Mlezi wa SHIMMUTA ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Philip Mpango, yanayolitaka shirikisho hilo kuhakikisha kuwa linawafikia wadau wake kuhamasisha ushiriki wa watumishi katika michezo.

Meneja Rasilimali Watu wa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara, Emmanuel Msaki, alisema kuwa kampuni imejipanga kushiriki mashindano ya mwaka huu“Hatukuweza kushiriki mashindano ya SHIMMUTA kwa miaka mitatu iliyopita kutokana na mlipuko wa corona uliokuwepo, ila niwahakikishie kuwa tutakuwa pamoja kwani kwenye bajeti zetu mwaka huu tumeweka na ya kutuwezesha kushiriki,” Msaki ameiambia Kamati hiyo.

Naye Meneja Usalama na Afya Mahali pa Kazi wa mgodi wa North Mara, Dkt Nicholas Mboya - katika kukazia kauli ya Msaki, amesema “Mwaka huu tunarudi kuwa sehemu ya familia ya SHIMMUTA kwa maana ya kushiriki kwenye michezo

Wajumbe Kamati hiyo ya SHIMMUTA pia walipata fursa ya kutembelea mgodi huo ikiwemo miradi ya kijamii inayotekelezwa na kampuni katika vijiji vinavyopakana na Mgodi huo.

Wajumbe wakifuatilia kikao na kubadilishana mawazo na wafanyakazi wa Barrick North Mara

Wajumbe wakifuatilia kikao na kubadilishana mawazo na wafanyakazi wa Barrick North Mara


Wajumbe wakifuatilia kikao na kubadilishana mawazo na wafanyakazi wa Barrick North Mara

Picha ya pamoja ya wajumbe wa kikao cha Kamati ya Utendaji ya SHIMMUTA Taifa na wafanyakazi wa Barrick North Mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara uliopo Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani Mara.

WAZIRI TAX APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WA MISRI, MAREKANI

$
0
0

Dar es Salaam, 10 Februari 2023

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amepokea nakala za Hati za Utambulisho za mabalozi wateule wa nchi za Misri na Marekani.

Mhe. Waziri Tax amepokea nakala za hati za utambulisho za Balozi wa Misri nchini, Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail na Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Michael Battle jana jioni katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mabalozi hao kwa nyakati tofauti mara baada ya kupokea nakala zao za hati za utambulisho, Dkt. Tax amewahakikishia ushirikiano kutoka Serikalini wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao hapa nchini na kuwasihi kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na nchi zao.

Balozi mteule wa Misri nchini, Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail ameahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Misri na Tanzania katika sekta za nishati hususani mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere, kilimo, biashara na uwekezaji.

“Misri na Tanzania tunayo mengi ya kushirikiana, tunaahidi kuendeleza ushirikiano wetu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili, wakati wa utumishi wangu hapa Tanzania nitaendeleza kwa maslahi mapana ya wananchi wetu wote,” alisema Balozi Ismail.
     
Kwa upande wake Balozi Mteule wa Marekani, Mhe. Michael Battle amesema Marekani na Tanzania zimekuwa marafiki wa muda mrefu, na itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta za Utalii, Kilimo, afya, biashara na uwekezaji pamoja na sekta nyingine za kimkakati.

“Ni furaha kwangu kuwepo hapa leo na kukabidhi nakala ya hati ya utambulisho wangu hapa nchini Tanzania, napenda kuahidi kwa kipindi nitakachokuwa hapa nitahakikisha kuwa uhusiano wetu wa kidiplomasia unakuwa na kuimarika kwa maslahi ya mataifa yetu,” alisema Balozi Battle.


 

DKT.DIMWA- ATUA PEMBA, MAELFU YA WANANCHI NA WANA CCM WAJITOKEZA KUMPOKEA.

$
0
0


NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Mohammed Said Mohammed 'Dimwa',amesema hakuna mtu yeyote mwenye hati miliki ya Chama hicho bali ni Chama cha watu wote.

Alisema wakati umefika wa Chama hicho kurudi kwa wanachama wenyewe ili waamue masuala mbalimbali yenye tija ya kisiasa na kiuchumi.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na maelfu ya Wanachama wa Chama hicho huko katika Afisi ya CCM ya Kitengo cha uratibu Chachani Chake Chake kisiwani Pemba.

Alisema CCM itashuka kwa wananchi kuhakikisha wanajengewa uwezo kupitia madarasa ya itikadi kwa lengo la kujiimarisha kisiasa kuanzia ngazi hizo zenye wanachama wengi.

Dkt. Dimwa, alitumia nafasi hiyo kuwaonya baadhi ya wanasiasa na wanachama wa vyama vya upinzania nchini kuacha kauli za uchochezi wa vurugu na badala yake wajielekeze katika kudumisha amani na mshikamano.

Alisema, kumeanza kujitokeza maneno ya choko choko na kwamba CCM msimamo wake ni kujibu maneno hayo kupitia usimamizi wa utekelezaji wa Ilani yake ya mwaka 2020/2025 inayotekelezwa kwa kasi kubwa na Serikali zote mbili ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kazi yetu kubwa ni kuwahudumia wananchi waliotupa kura za kuongoza dola, hatuwezi kukatishwa tamaa na kauli za baadhi ya wasioitakia mema CCM.

Alisema, serikali ya Umoja wa Kitaifa SUK inatambuliwa ndani ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984,hivyo wasioridhika wana nafasi ya kufuata taratibu ili kama kuna changamoto zitatuliwe.”,alisema Dimwa.

Aidha aliwatataka viongozi na wanachama wa CCM kuwa na mipango kazi inayoendana na mikakati ya kuimarisha Chama hicho.

"Naamini kuwa Chama cha Mapinduzi 2025 kitashinda kwa kishindo tena saa nne asubuhi kwani tuliyoahidi tunaendelea kuyatekeleza kwa vitendo”.alifafanua Dkt.Dimwa.

Katika maelezo yake Dkt.Dimwa, alisema CCM itafanya siasa za kisayansi kwa kuhakikisha kila mwanachama ananufaika na fursa zinakazopatikana kupitia taasisi hiyo kubwa ya kisiasa.

Aliwatoa hofu baadhi ya wananchi wanaokosoa maamuzi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuruhusu mikutano ya hadhara kwani Viongozi wa Chama na Jumuiya zake wana uwezo wa kujibu hoja hizo kwa ufasaha.

"Sisi hatuwezi kujibu maneno ya khanga bali tutawajibu kwa hoja, ndani ya miaka miwili CCM imefanya mambo makubwa sana haija wahi kutokea hivyo tuna mengi ya kuwajibu wapinzani kwa maendeleo yaliyofanyika kwa kipindi kifupi," alisema.

Alisema, Dkt.Dimwa kuwa ana kazi mbili kubwa kwanza ni kumtetea Mwenyeti wa CCM, kumsemea lakini na kumlinda, na kazi yake ya pili ni kumlinda na kumsemea Makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Mwinyi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba, Yussuf Ali Juma aliahidi kutoa ushirikiano na kutekeleza maelezo yote yaliyotolewa.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Inocent Nyanzaba, alisema hali ya kisiasa ndani ya Mkoa huo ipo vizuri.

Aidha alisema, kuna mahusiano mazuri ya Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake na kwamba pale panapotokea changamoto basi mamlaka husika kwenye ngazi hizo huzitatua.

Mapema Mkuu wa Mkoa huo Mantar Zahor Masoud, alisema kwamba ndani ya Mkoa huo wametekeleza kwa ufanisi Ilani ya CCM kwa kuimarisha huduma za afya,maji,elimu,uvuvi,kilimo,biashara na mindombinu ya usarifi wa anga nan chi kavu.

Alieleza kwamba katika juhudi za kuwawezesha wananchi kiuchumi serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni nne kwa ajili ya mikopo ya kuviwezesha vikundi 45.

Zahor, alisema pamoja na mafanikio hayo wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa huduma za maji safi na salama kwa baadhi ya maeneo, changamoto hiyo ina sababishwa na umeme kuwa na nguvu ndogo za kuendesha mitambo ya maji.

Akijibu hoja hiyo, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis, alisema CCM tayari imeanza kuchukua juhuzi za kuzungumza na viongozi wa TANESCO ili wakutane na viongozi wa ZECO kwa ajili ya kumaliza changamoto hiyo kisiwani Pemba.

Viongozi wanaounda Sekretarieti hiyo ya NEC Taifa Zanzibar waliofanya ziara hiyo ya kujitambulisha Pemba ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed,Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Organazesheni Omar Ibrahim Kilupi na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis.

Wengine ni Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Khadija Salum Ali na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya uchumi na fedha CCM Zanzibar Afadhali Taibu Afadhali.


NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohamed (Dimwa), akizungumza na Wananchi wa kisiwa cha Pemba mara baada ya kuwasili katika Afisi ya uratibu Pemba.



NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohamed (Dimwa),akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba mara baada ya kuwasili katika ziara ya kuitambulisha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar huko katika Uwanja wa Ndege Pemba.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohamed (Dimwa),akiongoza matembezi ya msafara wa Sekretarieti ya NEC Taifa Zanzibar kuelekea katika Afisi ya CCM kitengo cha uratibu Chachani Chake Chake Pemba.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohamed (Dimwa),akivishwa skafu mara baada ya kuwasili katika Afisi ya uratibu Pemba.


Viewing all 120391 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>