Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 119527 articles
Browse latest View live

SEKRETARIET YA AfCFTA YAENDESHA WARSHA KWA WABUNGE NA WAWAKILISHI KUHUSU MKATABA WA AfCFTA

$
0
0






Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Omar Said Shabaan akifungua Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi ili kuwa na uelewa wa pamoja na kutekeleza kwa ufanisi Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.



Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Exaud Kigahe akizungumza katika Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi ili kuwa na uelewa wa pamoja na kuutekeleza kwa ufanisi Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofayika Zanzibar.



Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Omar Said Shabaan (katikati) katka meza kuu wakati wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.



Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Yussuf Hassan Iddi (katikati) akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Hashir Abdallah (kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Dkt. Aboud S. Jumbe (kushoto) wakifuatilia ufunguzi wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.


Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.


Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.


Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.


Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.


Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi katika icha ya pamoja na meza kuu baada ya ufunguzi wa warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.


Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi katika icha ya pamoja na meza kuu baada ya ufunguzi wa warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.




Wajumbe wa Sekretarieti ya AfCFTA kutoka Accra, Ghana katika picha ya pamoja na meza kuu baada ya ufunguzi wa warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.



Sekretarieti ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) limeendesha Warsha ya kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Mkataba huo kwa Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi ili kuwa na uelewa wa pamoja na kuutekeleza kwa ufanisi.

Akifungua warsha hiyo mjini Zanzibar, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Omar Said Shabaan amesema uelewa wa pamoja kuhusu mkataba huo ni muhimu kwakuwa utaiwezesha nchi kuutekeleza kwa vitendo na hivyo kunufaika na malengo ya kuanzishwa kwake.

"Kutekeleza mkataba huu lazima kuwe na uelewa wa pamoja, hii itawezesha nchi kujipanga na kwenda pamoja kuutekeleza na hivyo kunufaisha nchi kwa ujumla wake," alisema mhe. Omar

Amesema uelewa wa pamoja wa Mkataba huo wa AfCFTA kutawezesha nchi kupata tija iliyokusudiwa wakati nchi ilipoamua kuuridhia na kusaini na hivyo kuwa miongoni mwa watekelezaji wake.

Amesema Serikali zote mbilii za Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar zimeufanyia tathmini Mkataba huo na kuja na mkakati maalum wa kusaidia utekelezaji wake

Amezitaka taasisi za uratibu wa mkataba huo kuendeleza juhudi za kuwezesha utekelezaji wa Mkataba huo ili kufahamu na kuzikamata fursa zinazopatikana katika soko la Mkataba huo ili kuutekeleza kwa ufanisi na hivyo kunufaika nao.

Amesema kama nchi haina budi kuangalia fursa za soko la AfCFTA ambalo litakuwa mbadala wa masoko mengine ambayo yana ukomo kutegemeana na nchi inavyokua kiuchumi.

Amesema kwa ukubwa wa soko la AfCFTA unaweza kuleta changamoto lna kueleza kuwa Serikali zimejipanga kukabiliana na changamoto za biashara kwa kuboresha mazingira ya kufanya biashara, kuvutia wawekezaji na kuwafaanya wazalishaji wake wawe na uwezo wa kuzalisha bidhaa zenye viwango ili kufikia mahitaji ya bidhaa katika soko hilo la AfCFTA.

Amesisitiza kuwa utekelezaji wa Mkataba wa AfCFTA utapelekea ukuaji wa biashara, uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa bora kwa nchi na hivyo kama nchi lazima itilie mkazo ili kunufaika na soko hilo.

Warsha hiyo inayoendeshwa na Sekretariati ya AfCFTA yenye makao yake makuu mjini Accra ,Ghana ililenga kutoa elimu na mahitaji ya Mkataba wa AfCFTA ambao Tanzania kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliuridhia na kuusaini mwezi Septemba 2021.

Tanzania iliwasilisha Hati ya kuuridhia Mkataba huo kwa Kamisheni ya Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia mwezi Februari ,2022 na hivyo kuwa miongoni mwa mataifa yanayotekeleza mkataba huo.

Mkataba wa AfCFTA ulianzishwa na Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika walipokutana katika kikao kilichofanyika jijiini Kigali, Rwanda mwaka 2018.


GEITA GOLD FC WAKOSA TSH. MIL 30/- ZA MKURUGENZI

$
0
0


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

KIKOSI cha Geita Gold FC kimekosa kiasi cha fedha Shilingi Milioni 30/- baada ya kupata sare ya bao 1-1 na Kikosi cha Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa Mji wa Geita, Mhe. Zahara Michuzi aliahidi kiasi hicho cha fedha endapo Kikosi cha Matajiri wa Dhahabu kikipata ushindi mbele ya Wekundu wa Msimbazi, Simba SC.

Geita Gold FC walianza kupata bao katika dakika ya 19 kupitia kwa Mshambuliaji wake kinara, George Enock Mpole baada ya Walinzi wa Simba SC kushindwa kuondoa mpira uliokuwa una zagaazagaa katika lango lao.

Dakika ya 25, Simba SC walisawazisha bao hilo kupitia kwa Mshambuliaji wao, Kibu Dennis Prosper baada kupiga Kichwa safi kilichowashinda Golikipa na Walinzi wa Geita FC na kujaa wavumi.

Baada ya mchezo huo, Geita Gold FC wanafika alama 35 na michezo yao 25 watabaki kwenye nafasi ya 5 ya msimamo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, wakati Simba SC wakibaki kwenye nafasi ya pili na alama zao 51 na michezo 25.



 

MAKATA, NAFTALI WAOMBA RADHI

$
0
0


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

KOCHA Mkuu wa Mbeya Kwanza FC, Mbwana Makata na Meneja wa timu hiyo, David Naftali wameomba radhi kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Bodi ya Ligi (TPLB), Wadhamini wa Ligi hiyo na Wadau wengine wa Soka baada ya kupewa adhabu ya kufungiwa miaka mitano.

Kocha Makata na Meneja Naftali walipewa adhabu hiyo ya kufungiwa miaka mitano wakituhumiwa kuamuru Wachezaji wa timu hiyo kugomea mchezo wao wa Ligi ya Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC kwenye uwanja wa Ilulu mkoani Lindi, Mei 13, 2022.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kocha Makata ameomba radhi kwa TFF, Bodi ya Ligi na Wadau wengine wa Soka kutokana kuonyesha dosari kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo kwa sasa ni miongoni mwa Ligi bora katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

“Sisi tusiwe miongoni mwa watu ambao wanaitia doa Ligi yetu ya Tanzania Bara, tunasema Ligi yetu ni Ligi Bora, ubora ambao unachagizwa na Uongozi wa TFF, chini ya Wallace Karia, na Uongozi wa Bodi ya Ligi chini ya Mwenyekiti Steven Mguto na Wadhamini wote,” Makata amesema.

“Toka nimeanza kucheza Soka hadi sasa nimekuwa Kocha, sijawahi kupewa adhabu kama hii, tunaahidi kutakuwa mfano mzuri kwa faida ya Soka letu la Tanzania endapo tutasamehewa adhabu hii”, ameeleza.

Hata hivyo, baada ya kuomba radhi Kocha Makata ameomba Kamati hiyo iliyotoa adhabu kurudia upya hukumu hiyo, amesema kipindi cha nyuma hawakuwa na rekodi mbaya.

Naye, Meneja wa timu hiyo, David Naftali ameomba radhi kwa TFF, Bodi ya Ligi, Wadhamini wa Ligi hiyo sanjari na Wadau wengine wa Soka la Tanzania kwa kitendo hicho kilichopelekea kufungiwa miaka mitano.

Kocha Mbwana Makata na Meneja David Naftali walifungiwa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) kwa kuzingatia Kanuni ya 32:7 ya Ligi Kuu kuhusu kuvuruga mchezo, baada ya Kamati hiyo kukaa Mei 16, 2022 kupitia masuala mbalimbali ya Ligi hiyo.


CCM SIMANJIRO WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UZINDUZI WA FILAMU YA THE ROYAL TOUR

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Simanjiro

WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuandaa filamu ya Royal Tour ambayo itasaidia kuchochea utalii nchini.

Wajumbe hao wa Halmashauri ya Wilaya hiyo wametoa azimio hilo walipokutana kwenye kikao hicho kilichofanyika mji mdogo wa Orkesumet ambayo ni makao makuu ya Wilaya ya Simanjiro.

Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Amos Shimba amesema kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya hiyo kwa kauli moja wanampongeza Rais Samia kwa kufanikisha Royal Tour ambayo itaongeza watalii nchini.

Shimba amesema Royal Tour imezidi kuitangaza nchi kimataifa hivyo kufaidika na idadi kubwa ya watalii ambao watafika wengi zaidi na fedha za kigeni kuongezeka.

Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka amesema Rais Samia wanampongeza na kumshukuru Rais Samia kwa kuzidi kuitangaza Tanzania katika ngazi ya kimataifa.

"Kupitia mapato yatakayopatikana kupitia wageni watakaokuja nchini baada ya kuiona Royal Tour tunatarajia kupata madarasa ya shule za msingi na sekondari, zahanati, vituo afya na huduma za maji," amesema Ole Sendeka.

Katibu wa UWT Wilaya ya Simanjiro, Leokadia Fisso amesema kupitia filamu ya Royal Tour vivutio vingi nchini vitapata watalii wengi hivyo kuongeza pato la Taifa nchini.

"Hifadhi zetu za Taifa za Tarangire na Manyara nazo kwa kiasi kikubwa zitafaidika kupitia filamu hii ambayo muhusika mkuu ni mama yetu Rais Samia kwani watalii wataongezeka," amesema Fisoo.

Diwani wa Kata ya Loiborsiret Ezekiel Lesenga Mardad amesema Rais Samia ameionyesha dunia kuwa Tanzania ina vivutio vingi vya utalii.

Mjumbe wa kikao hicho kutoka Kata ya Mirerani, Jack Momo amesema wanamshukuru Rais Samia kwa kutoa kazi nzuri ya filamu ya Royal Tour itakayoongeza idadi ya watalii nchini.





JUST IN: TAARIFA KWA UMMA KUHUSU PUNGUZO LA TOZO (GHARAMA) ZA KUVUKA DARAJA LA NYERERE (KIGAMBONI)

Wanahisa wa Benki ya CRDB Waidhinisha Malipo ya Gawio la Shilingi Bilioni 94 kwa Mwaka wa Fedha wa 2021

$
0
0
Wanahisa wa Benki ya CRDB wamepitisha kwa kauli moja mapendekezo ya Bodi ya Wakurugenzi kuhusu malipo ya gawio la Shilingi 36 kwa kila hisa ambayo yanaleta jumla ya thamani ya gawio la mwaka wa fedha 2021 kufikia Sh 94 bilioni.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 27 wa Benki hiyo uliofanyika jana katika mazingira ya mseto, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Dkt. Ally Laay alisema gawio lililoidhinishwa kwa kila hisa ni ongezeko la asilimia 64 ikilinganishwa na Shilingi 22 kwa kila hisa iliyotolewa mwaka jana. Alisema hiyo inaashiria ukuaji wa mapato kwa kila hisa ambapo katika kipindi cha mwaka 2021 yalikuwa Shilingi 102.7.
"Kwa mara nyingine tena, tunafuraha kuwasilisha thamani endelevu kwa Wanahisa wetu. Utendaji wa Benki katika mwaka wa 2021 ulitoa matokeo mazuri sana, ambayo unadhihirisha mafanikio ya mikakati yetu ya biashara. Mwaka 2021 Benki ilipata faida baada ya kodi ya Shilingi bilioni 268.2 bilioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 62.3,” alisema Dkt. Laay.

Aidha alibainisha kuwa kampuni tanzu za Benki hiyo ziliendelea kuchangia vyema katika biashara ya kundi huku kampuni tanzu ya Burundi pekee ikichangia faida ya jumla ya Shilingi bilioni 12.8 huku kampuni tanzu ya bima ikichangia faida ya TZS 859.0 milioni. Jumla ya mchango wa kampuni tanzu kwenye faida ya kundi ilikuwa 5%.
" Nafurahi kuripoti kwenu kwamba tumepata maendeleo makubwa katika kupata leseni na vibali vinavyohitajika kutoka kwa mamlaka za nyumbani pamoja na DRC. Tunatarajia kuanza uendeshaji ndani ya nusu ya pili ya mwaka wa fedha wa 2022.,” alibainisha alipokuwa akiwasasisha wanahisa kuhusu upanuzi wa kimkakati wa Benki hadi DRC.

Akizungumzia utendaji wa mwaka uliopita, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema mapato ya uendeshaji ya Kampuni yaliongezeka kwa asilimia 14.3% hadi Shilingi bilioni 924.0 kutoka Shilingi bilioni 808.7 mwaka 2020. Ukuaji huo ulitokana na ongezeko la 11.3% ya mapato ya jumla ya riba, yaliyotokana na ukuaji mzuri wa mikopo kwa wateja wadogo na wakati. Pamoja na ukuaji wa mikopo Benki hiyo lilifunga mwaka na uwiano wa mikopo chechefu wa 3.3% kulinganisha na kiwango cha udhibti cha soko cha 5%.
Nsekela alisema Benki ya CRDB pia ilirekodi ukuaji mkubwa wa mizania wa mwaka hadi mwaka wa 23% kutoka Shilingi trilioni 7.2 i mwaka 2020 hadi Shilingi trilioni 8.8. Ukuaji huo ulisababishwa na ukuaji wa asilimia 19.4 wa amana za wateja hadi Shilingi trilioni 6.5 kutoka Shilingi trilioni 5.4 zilizoripotiwa mwaka 2020, na ukuaji wa 20.6% wa fedha za wanahisa.

"Kutokana na mtazamo wetu makini katika mwaka huo, Benki yetu iliendelea kukamata masoko kwa bidhaa na huduma bunifu, hivyo kupelekea ukuaji endelevu katika mapato na faida yetu. Tuliendelea kufanyia kazi changamoto za wateja ili kuboresha utoaji wetu wa huduma na kuhakikisha tunawapa uzoefu uliobora zaidi pindi watumiapo huduma zetu,” aliongeza.
Akizungumzia kuhusu mipango ya mbeleni, Nsekela alisema kipaumbele cha Benki hiyo ni kuimarisha vichocheo vya ukuaji, na kujenga misingi imara ya uendelevu. Alitaja mwaka wa fedha wa 2022 kuwa mwaka wa mwisho wa mkakati wa muda wa kati wa Benki ya CRDB ambao ulikuwa na jukumu muhimu katika kuimarisha utendaji, na umeipa msingi mzuri benki hiyo kukabiliana na siku zijazo.

Aliwashukuru wanahisa kwa imani yao na kuendelea kuunga mkono uongozi na wafanyakazi wa benki hiyo, ambako kumeiwezesha benki hiyo kupata mafanikio makubwa katika sekta ya huduma za kifedha Tanzania, na kuwahakikishia dhamira ya Benki hiyo ya kuendelea kutoa thamani endelevu zaidi kwao.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Dkt. Ally Laay aliwaeleza wanahisa kwamba katika kipindi cha mwaka huo, Benki ya CRDB ilipokea Wajumbe wapya wa Bodi Bw. Gerald Kasato, aliyechukua nafasi ya Bi. Rose Metta, akiwakilisha wanahisa wanaomiliki kati ya 1% -10% ya hisa na Bw. Roya Lyanga aliyechukua nafasi ya Bi. Ellen Gervas Rwijage kama mwakilishi wa Mfuko wa Uwekezaji wa DANIDA (DIF).

Bodi pia ilimteua Bi. Jessica Nyachiro kuongoza kampuni tanzu ya Benki ya CRDB katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Hadi kuteuliwa kwake, Bi. Nyachiro alikuwa Mkuu wa Mikakati na Mahusiano ya Wawekezaji. Pia alifahamisha wanahisa Afisa Mkuu wa Biashara wa muda mrefu wa Benki hiyo Dkt. Joseph Witts alitimiza umri wake wa kustaafu Desemba 2021. Hata hivyo, Bodi ilimuongezea mkataba wa miezi sita ili kuruhusu kukamilika kwa zoezi la kuajiri.

Kwa upande mwingine, Wanahisa waliidhinisha Ernst & Young kama Wakaguzi wa Nje wa Benki kwa mwaka wa fedha wa 2022, kuashiria imani yao katika sheria ya kiakili ya kampuni na kuendelea kwa Benki kuzingatia itifaki za utawala bora.

Wanahisa wa Benki pia walimchagua tena Wajumbe watatu wa Bodi Bw. Abdul Ally Mohamed kuwakilisha wanahisa wenye umiliki chini ya 1%, Dk. Fred Msemwa kuwakilisha wanahisa wenye hisa kati ya 1% na 10%, Bw. Martin Warioba kama Mkurugenzi Huru. 
Akizungumzia malipo ya gawio hilo, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki hiyo na Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei, alieleza kufurahishwa kwake na kuendelea kuongezeka kwa gawio huku akibainisha kuwa ukuaji huo ni mkubwa kupata kutokea. Dkt. Kimei  alisema kuwa hisa za benki hiyo zimebakia kuwa chachu ya wawekezaji kwasababu benki hiyo haijawahi kushindwa kutoa gawio kwa Wanahisa wake.



T-MARC Tanzania’s efforts in increasing access to priority health products in Tanzania mainland and Zanzibar

$
0
0
T-MARC Tanzania delivered 76,000 cycles of oral contraceptives to the Ministry of Health, Zanzibar. The consignment was received by Hon. Hassan Khamis Hafidh Deputy Minister of Health Zanzibar. During the ceremony the Deputy Minister Hassan expressed his sincere appreciations to T-MARC Tanzania for their support and effort in supporting health sector in Zanzibar.

" More efforts now should be based on educating people on advantages and disadvantages on the use of contraceptives, and its significance in improving community lives" Deputy Minister said. 

He also went through to insist T-MARC Tanzania and other players to support the government in its efforts to reduce maternal and child mortality rate in the country. 

'This is one of the things which pains me a lot witnessing death of pregnant women or children during the delivery, our societies need to be educated about reproductive health to avert these deaths". Says the Deputy Minister Hassan. 
On their part The Managing Director of T- MARC Tanzania Tumaini Kimasa said this initiative is part of T-MARC Tanzania’s efforts in increasing access to priority health products in Tanzania mainland and Zanzibar. He also asked the Government to strengthen Partnership with the health sector Implementing Partners and other stakeholders including non-state actors as they support and complement the Government’s role to improve health and social development to people and communities. "Private Public Partnership” must be increased in order to complement health efforts going forward and positively impact our society ".

Since 2004 T-MARC Tanzania has been operating in Tanzania Mainland and Zanzibar and as one of Tanzania’s largest NGOs governed and managed solely by Tanzanians, employs bold and dynamic approaches to expanding access to health products and improving lives. 

And among its services marketed products and behaviour change communication initiatives address pertinent health issues in reproductive health, family planning, child survival, water and sanitation, nutrition and communicable/non-communicable infections like malaria, HIV/AIDS, tuberculosis, and cervical cancer.

 T-MARC Tanzania has also promoted other product categories - branded and non-branded including anti malaria drugs, Zinc, ORS, Water disinfectants in collaboration with other partners.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO MEI 23,2022

$
0
0

 


         

       

       


Hotuba Ya Bajeti Ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Mwaka 2022-23

$
0
0

 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.

TIA SINGIDA WAHITIMISHA TAMASHA LA WIKI YA MICHEZO, WAHIMIZWA KUHAMASISHA SENSA

$
0
0

Mgeni Rasmi Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani (mwenye skafu) akimkabidhi kombe kepteni wa timu ya mpira wa miguu ya Diploma mwaka wa kwanza, Anuary Amimu (kushoto) baada ya kuibuka washindi dhidi ya Timu ya Bachelor mwaka wa pili katika Tamasha la Michezo la wiki moja la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida lililofikia tamati leo Mei 23, 2022 katika viwanja vya kampasi hiyo mjini Singida. Kulia ni Mratibu wa Tamasha hilo, Mwalimu Ambwene Kajula na Muhadhiri Flora Lemnge. 
Furaha baada ya ushindi.
Mshindi wa MISS TIA, Haika Amiry (katikati) akiwa na mshindi wa pili Sumaiya Adam (kushoto) na Mshindi wa Tatu, Tumaini Donald (kula) wakati wakiangalia fainali ya mpira wa miguu kati ya wanafunzi wa Diploma mwaka wa kwanza na Bachelor mwaka wa pili.
Furaha ya ushindi baada ya kukabidhiwa kombe kwa Timu ya Diploma mwaka wa kwanza.
Majaji wa tamasha hilo wakijitambulisha kwa staili ya kusakata Rhumba.
Wanafunzi wakiwa kwenye tamasha hilo.
Tamasha likiendelea.
Bidhaa za Mjasiriamali Eddy  Ice Cream ambaye ni mwanafunzi wa TIA zikioneshwa kwenye tamasha hilo.
Mjasiriamali Eddy, akielezea jinsi alivyopata wazo la kuanzisha ujasiriamali huo akiwa shuleni ambapo alitoa wito kwa wanafunzi wenzake kuwa wabunifu na kuanzisha biashara yoyote au kufungua kampuni wakiwa masomoni kama alivyofanya.
Meneja wa TIA Kampasi ya Singida Dk.James Mrema akikabidhiwa bidhaa zinazotengenezwa na wanafunzi wajasiriamali wa taasisi hiyo.
Bidhaa zikikabidhiwa kwa wanafunzi.
Dk. Mrema akipokea bidhaa za wajasiriamali wanafunzi.
Viongozi wa taasisi hiyo wakipata viburudisho kwenye tamasha hilo.
Mmoja wa wagombea nafasi ya MISS TIA akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
Taswira ya tamasha hilo.
Washiriki wa MISS TIA wakiwa jukwaani na vazi la ubunifu.
Madansa wakionesha umahiri wa kusaka dansi.
Warembo wakipita jukwaani.
Warembo wakiwa jukwaani na vazi la utamaduni.
Warembo wakiwa na vazi la ufukweni.
Mrembo akipita jukwaani na vazi la ofisini.
Warembo wakiwa na vazi la ofisini
Madansa wakionesha umahiri wakulitawala jukwaa huku mmoja wapo akiwa ameruka juu
Vazi la ufukweni hilo
Vazi la ufukweni hilo.
Mrembo akipita jukwaani.
Vazi la utanashati likioneshwa.
Vazi la ofisini likioneshwa.
Vazi la ofisini hilo.
Vazi la ufukweni hilo likioneshwa.
Tamasha likiendelea..
Mashindano yakiendelea. Mtanashati huyo akipita jukwaani.
Mshereheshaji (MC) akifanya yake jukwaani.
SIR.event Mwenzegule akifanya yake jukwaani.
Mrembo akipipita jukwaani na vazi la ubunifu.
Mrembo akipita jukwaani
Picha zikipigwa kwenye tamasha hilo.
Tamasha likiendelea.
Tamasha likiendelea.
Majaji wakiwa kazini.
Vipaji vya mziki vikitafutwa.
Ngoma za Pwani zikipigwa nafikiri ni mdumange au Sengeli hilo.
Diana Happe akiwatoka wapinzani wake katika mchezo wa Netball.
Agnes Msigwa akionesha umahiri wa kudaka mpira katika mchezo huo.
Heka heka uwanjani zikiendelea.
Wanafunzi wakiwa uwanjani kuangalia kabumbu kati ya Timu ya Diploma mwaka wa kwanza dhidi ya Bachelor mwaka wa pili.
Tamasha likiendelea.
Wanafunzi wakiwa uwanjani. Ni bonge la Nyomi.
Joseph Dida wa Timu ya Bachelor mwaka wa pili akimtoka mchezaji wa Timu ya Diploma mwaka wa kwanza Gadafi Omari.
Joseph Dida wa Timu ya Bachelor mwaka wa pili akimpigisha kwata mchezaji wa Timu ya Diploma mwaka wa kwanza Gadafi Omari.
Kepteni wa Timu ya Diploma mwaka wa kwanza Omega Mwamkinga akichomoka na mpira dhidi ya mchezaji wa timu ya Bachelor mwaka wa kwanza. 
Tamasha likiendelea.
Washindi wakishangiliwa.
Mchezo dhidi ya Diploma mwaka wa kwanza na Bachelor mwaka wa pili  ukiendelea
Watizamaji wakiendelea kuangalia mchezo huo.
Ushangiliaji ukiendelea.
Mchezo ukiendelea.
Mchezo ukiendelea.
Mratibu wa Tamasha hilo, Mwalimu Ambwene Kajula akitoa neno la shukurani.
Zawadi ya mbuzi ikitolewa na mgeni rasmi.
Zawadi ya mbuzi ikitolewa.

Medani zikifikwa kwa washiriki wa tamasha hilo.

Watu na kombe lao nifuraa tupu kwa Timu ya Diploma.
Nifura tupu.
Mgeni rasmi akikabidhi ng'ombe kwa kepteni wa Timu ya Diploma.
Wachezaji wa timu ya Diploma wakiwa na ng'ombe wao.
Zawadi zikitolewa.
Zawadi zikitolewa kwa Ma Miss.
Mgeni rasmi akimvika Medani mratibu wa Tamasha hilo, Mwalimu Ambwene Kajula.Kulia ni WARDEN wa TIA, Asia Hansy.
Mgeni rasmi akitoa pongezi kwa washiriki wa tamasha hilo.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Bachelor mwaka wa pili na viongozi mbalimbali wa TIA.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Diploma mwaka wa kwanza na viongozi mbalimbali wa Taasisi hiyo..
Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani akimpongeza mjasiriamali mwenye kampuni ya Eddy Ice Cream ambaye ni mwanafunzi wa TIA alipotembelea duka lake. 


Na Dotto Mwaibale, Singida



TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida imemaliza  rasmi wiki ya Tamasha la Michezo huku wakimihizwa kutumia michezo kuhamasha jamii kushiriki sensa ya watu na makazi itakayofanyika hapa nchini Agosti 23,2022.

Akifunga michezo hiyo Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema mwaka huu tamasha hilo la michezo lilikuwa na mwamko mkubwa na kueleza michezo ni furaha, amani na ni ajira.

Alisema kijana yeyote ambaye hathamini kipaji chake atakuwa ni kijana ambaye hajitambui kwa kuwa kila kijana Mungu amempa kipaji chake kuna wachoraji, wacheza mpira, waimbaji hao wote ni karama kutoka kwa Mwenyezi Mungu hivyo aliwaambia vijana hao waendelee kuvithamini vipaji vyao walivyonavyo.

Ndahani alisema matajiri wengi duniani sio kwamba wamesoma sana bali ni watu wenye vipaji hasa wasanii na wachezaji wa mpira ambao hata hapa nchini wapo.
"Mnapokuwa vyuoni endelee kuona namna gani mnaweza kuendeleza vipaji vyenu ili mfikie mafanikio" alisema Ndahani.

Ndahani alitumia nafasi hiyo kuwaomba vijana hao na wanamichezo wote kwa ujumla kutumia michezo kuhamasisha jamii kushiriki zoezi la senza ya watu na makazi ambalo litafanyika Agosti 23 mwaka huu.

Mratibu wa tamasha hilo  Mwalimu Ambwene Kajula alisema michezo iliyofanywa katika tamasha hilo ni mpira wa pete, mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa kikapu, mchezo wa bao na kuinua vipaji kwa kutafuta MISS na MR tia, waimbaji, wachekeshaji, waigizaji, wacheza muziki na ngoma, watanashati, wabunifu, wasiriamali.  

Pia alisema washiriki wa shindano la MISS TIA waliweza kupita jukwaani wakiwa wamevaa vazi la ufukweni, ubunifu, utamaduni na ofisini huku MR TIA wakivaa vazi la ufukweni, utamaduni na ofisini.

Alisema kuwa vilevile kulikuwa na maonyesho ya wajasiriamali mbalimbali wa ndani na nje ya Taasisi na kuwa kwao  ilikuwa ni fursa kubwa kwa wanafunzi wao na jamii nzima inayowauzunguka ambapo zawadi leo Mei 22,2022 ndio siku ya kilele ambapo wametoa zawadi  kwa washindi mbalimbali akiwepo ng'ombe kwa mshindi namba moja , mbuzi,fedha taslimu na kufikwa medani kwa baadhi  ya washiriki.

Alitaja zawadi zilizotolewa kwa mshindi wa kwanza kwa mpira wa miguu ambao walikuwa ni wanafunzi wa diploma mwaka wa kwanza kuwa ni kombe na ng'ombe mmoja, mshindi wa pili wanafunzi wa Bachelor mwaka wa pili wao walipata mbuzi watatu, na wanafunzi wa Bachelor mwaka wa tatu ambao walikuwa washindi wa tatu wakiambulia zawadi ya mbuzi wawili.

Alisema kwa upande wa Netball wanafunzi wa diploma mwaka wa pili waliopata nafasi ya kwanza walipatiwa mbuzi watatu huku diploma mwaka wa kwanza waliokuwa washindi wa pili wakiambulia mbuzi wawili na mshindi wa tatu akipata cheti.

Alisema katika mchezo wa Basketball mshindi wa kwanza alipata mbuzi wawili na mshindi wa pili akiambulia mbuzi mmoja na halikadharika katika mchezo wa Volleyball zawadi zilikuwa hivyo hivyo.

Kajula alitumia nafasi hiyo kuipongeza TIA kwa kuweka wiki hiyo ya Tamasha la Michezo na hasa wanafunzi walioshiriki na wadau mbalimbali waliofanikisha kwa namna moja hama nyingine kufanyika kama Hoteli ya Jalmini na Cocacola kwani limewaongezea wanafunzi wao uelewa wa maisha na kwamba si elimu tu inayoweza kukufanikisha katika maisha ni wazi kazi na dawa ndio njia pekee ya mafanikio. 

Alisema kusoma kunahitaji uweze kucheza ili uweze kuelewa na si kucheza pekee ila kujishughulisha na shughuli zingine ili kutanua ubongo, kulinda na afya ya kiakili ili kutia chachu katika kupambana mawazo hasi na kuruhusu kuwaza katika mlengo chanya. 

Pia alisema michezo ni kukuza ushirikiano na urafiki kwani michezo hunoga pale mnapokuwa wengi na kujumuika kwa pamoja, Hii inamaana kwamba kidole kimoja hakivunji Chawa. 

Alisema michezo huwalinda wao na wengine waliokaribu nao kiafya, kiakili, kimwili na kuwa michezo inaweza kutumika kama njia bora sana katika kujikinga na maradhi mbalimbali na kuokoa kipato kinachoweza kutumika katika ununuzi wa madawa ya kujitibu na zaidi ya yote ni lazima wajikite katika kukuza vipaji vya wanafunzi.

"Tunapenda kuishukuru nchi yetu kwani toka enzi za mababu imekuwa ikijitahidi kuhakikisha wananchi wanajihusisha na michezo kwani hii husaidia katika ulinzi na usalama, kuzuia kutenda uhalifu, kuongeza ajira, kupunguza matumizi ya changamoto za kiafya nakadhalika hakika uhuru huu tulionao ndio pekee unaoturuhusu kupata nafasi ya kuweza kujikita katika shughuli hizi za maendeleo na tunaipongeza Serikali hii kwa dhati kwani Amani, Utulivu, iliyopo ni fahari kubwa sana kwetu na vizazi vyetu' alisema Mrema. 

Aidha Kajula alisema katika wiki hii ya michezo TIA kwa mwaka 2022 wanajivunia furaha waliyonayo japo kuwa kuna mambo kadhaa ambayo wanayatamani kama kuweka viwanja vya michezo vya kisasa ambavyo vitaamsha hari za wengi kujihusisha na michezo,kuweka uzio kuzunguka Taasisi hiyo ili kulinda maeneo yao na wanafunzi kwa ujumla katika changamoto mbalimbali wanazozipitia, kuongeza mabweni ya kisasa katika iddi kubwa ambayo itaweza kuwasaidia wanafunzi kujiingiza katika changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa wanakaa mtaani, kuwakinga wanafunzi katika maambukizi mapya ya magonjwa ya zinaa na VVU na UKIMWI.

Alitaja mambo mengine wanayoyatamani kuwa ni kuwakinga wanafunzi katika kujiingiza katika madawa ya kulevya na tabia hatarishi, kutumia mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s na wadau wengine kuhakikisha wanawasaidia wanafunzi ambao hawana uwezo kuweza kusomeshwa na kujikwamua katika janga la umaskini, kuwasaidia wanafunzi kupata ajira mbalimbali za muda mfupi na mrefu ili kuweza kupata fursa wakipambana na maisha.

Akizungumzia namna ya kujiunga na masomo katika chuo hicho kwa Mwanafunzi mwenye ufaulu kuanzia alama D4 anaweza kutuma maombi yake kwani atakuwa amekidhi sifa za kujiunga na dirisha liko wazi tangu Mei 14 hadi 15 Agost 2022. 

Alisema wanawakaribisha kujiunga na programu za fani ya Uhasibu na Fedha, Uhasibu wa Umma, Ugavi na manunuzi, usimamizi rasilimali watu, masoko na uhusiano wa umma, usimamizi wa biashara. Fomu za maombi zinapatikana katika tovuti  ya tassisi yaani www.tai.ac.tz au wanaweza kufika chuoni na kujaza fomu hizo. Pia wanaweza kupata fomu hizo katika shuile za sekondari walikohitimu kidato cha nne na kuwa wanawahakikishia kuwa Taasisi ya Uhasibu Tanzania inatoa elimu bora yenye ujuzi wa maarifa na vitendo hivyo kumjengea mhitimu weledi na uwezo mkubwa wa kujiajiri na kuajiriwa.

TICTS yaendelea kuboresha huduma kwa kuleta mashine tatu za ziada

$
0
0



Na Mwandishi wetu

Kampuni ya Kimataifa ya huduma ya Kontena Tanzania (TICTS) imendelea kuleta ufanisi katika shughuli zake baada ya kuleta mashine tatu za kutoa huduma ya ushushaji na kupandishaji wa makontena zijulikazo kwa jina la Rubber-Tyred Gantry Cranes (RTGCs).

Mashine hizo za kisasa zinatumia na matairi zimenunuliwa naTICTS kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora zaidi za kontena ikiwa pamojana mpango unaoendelea wa uwekezaji ambapo kampuni hiyo imewekeza Sh12.5 billioni katika kununua vifaa hivi vya ziada.

Hivi karibuni, TICTS ilivunja rekodi ya kuhudumia jumla mizigo 61, 000 ya makontena yenye ujazo wa futi 20 (TEU) kwa mwezi Machi na jumla ya TEU 2,841 mnamo mwezi huu (Mei).

Mkurugenzi Mkuu wa Hutchison Ports Andy Tsoi, alisema kuwa wanaendelea kunufaika katika shughuli zao na kuendelea kutoa huduma bora kwawateja wao.

“Kama mwanachama wa Bandari za Hutchison, TICTS inaendelea kunufaika kutokana na kupata usaidizi mbalimbali kutoka makao makuu ya kampuni yetu. Tuna historia kubwa ya ushirikiano nchini Tanzania na tunatamani sana kuendelea kusaidia ukuaji wa Tanzania na ukanda huu,” alisemaTsoi.

Akizungumzia ujio wa vifaa hivyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TICTS Matt Clifftn alisema kuwa, “Kulingana na kuendelea kukua kwa uchumi, tunayofuraha kupokea vifaa hivi vya ziada kwani vitatusaidia kukidhi mahitaji katika kutoa huduma bora. Lengo letu ni kupunguza muda wa meli kusubiri na kuongeza tija.”

TICTS ipo katika sehemu ya gati Nane(8)8 hadi 11, eneo lenye urefu wa mita 725 bandarini ikiwa na ‘crane’ sita kila moja ikiwa na uwezo wa kubeba tani 45.

Pamoja na kuwasili kwa vifaa, TICTS kwa sasa kina idadi ya mashine za RTGC 23 ambazo zinafanya kazi katika eneo la hekta 18.75.


Mashine tatu za kutoa huduma ya ushushaji na kupandishaji wa makontena zijulikazo kwa jina la Rubber-Tyred Gantry Cranes (RTGCs) baada ya kuwasili nchini kupitia kampuni ya Kimataifa ya huduma ya Kontena Tanzania (TICTS)


Mashine tatu za kutoa huduma ya ushushaji na kupandishaji wa makontena zijulikazo kwa jina la Rubber-Tyred Gantry Cranes (RTGCs) katika muonekano tofauti baada ya kuwasili nchini kupitia kampuni ya Kimataifa ya huduma ya Kontena Tanzania (TICTS)


Mashine tatu za kutoa huduma ya ushushaji na kupandishaji wa makontena zijulikazo kwa jina la Rubber-Tyred Gantry Cranes (RTGCs) katika muonekano tofauti baada ya kuwasili nchini kupitia kampuni ya Kimataifa ya huduma ya Kontena Tanzania (TICTS)



PUNGUZO LA TOZO (GHARAMA) ZA KUVUKA DARAJA LA NYERERE (KIGAMBONI)

Rais Samia akutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya AngloGold Ashanti

$
0
0

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika Picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Dkt. Alberto Calderon mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 23 Mei, 2022.

-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Dkt. Alberto Calderon mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 23 Mei, 2022.

RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI GHANA

DK .MAHENGE ASISITIZA UMUHIMU WA KUFIKIWA MALENGO YA CHANJO

$
0
0



Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge akiwa amempaka mtoto wakati akisubiri apatiwe chanjo Kata ya Iguguno wilayani Mkalama wakati alipoongoza uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya polio uliofanyika Mei 18,2022. Kutoka kulia ni Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) Cuthbert Kong'ola, Dk.Ritha Willilo kutoaka Shirika la Afya Duniani (WHO) Mganga Mkuu Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick, Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Honest Nyaki, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Ibrahim Pazia na Mkuu wa wilaya hiyo, Sophia Kizigo.


Dk.Ritha Willilo kutoaka Shirika la Afya Duniani (WHO) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya chanjo.


Dk.Ritha Willilo kutoaka Shirika la Afya Duniani (WHO) akiwa amempakata mtoto wakati akipatiwa chanjo hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo.


Wananchi wa Iguguno wakiwa kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa kampeni hiyo.


Na Abby Nkungu, Singida


MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge amewaagiza Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na Manispaa mkoani humo kuhakikisha wanafikia malengo waliojiwekea kwa kuwapatia chanjo ya polio watoto wote walio chini ya umri wa miaka mitano.

Akiongoza Uzinduzi wa kampeni ya siku nne ya chanjo ya matone ya polio uliofanyika kimkoa katika Kata ya Iguguno wilayani Mkalama, Dk Mahenge alisema iwapo malengo yatafikiwa, mkoa utakuwa na uhakika kuwa unalea Taifa ambalo litaingia kwenye shughuli za uzalishaji likiwa na afya njema.

Aidha, aliezea kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutenga bajeti kubwa kwa Sekta ya afya ambapo Mkoa wa Singida ulipokea zaidi ya Sh bilioni 30 kwa mwaka huu huku hospitali za wilaya zikijengwa Ikungi, Manyoni, Mkalama na Halmashauri ya wilaya Singida pamoja na vituo vya afya 15 katika wilaya zote.

"Nimeyasema haya ili kuonesha jinsi Rais wetu anavyotujali Watanzania na ndio maana leo tupo hapa tunazindua kampeni hii ya polio baada ya Serikali kutuwezesha" alisema Dk.Mahenge.

Awali, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Victorina Ludovick alisema kuwa mkoa unatarajia kufikia jumla ya watoto 286,736 walio chini ya miaka mitano kwa kipindi cha siku tatu na kwamba lengo ni kufika kwenye maeneo yote ambapo itafanyika nyumba kwa nyumba .

Alitaja madhara ya ugonjwa wa Polio kuwa ni ulemavu wa ghafla wa viungo na usiotibika kwa hiyo ni muhimu kwa kila mzazi na mlezi kuwatoa watoto wao wenye umri tajwa ili wapate chanjo hiyo salama.

Dk.Ritha Willilo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) alitoa mwito kwa wazazi kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa watoa huduma ya chanjo hiyo ili malengo ya Serikali yaweze kutimia.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa waliahidi kujitokeza kwa wingi kuwapeleka watoto wao kwenye chanjo kwa kuwa sasa wameelimika vya kutosha na kwamba wameachana na imani potofu zilizokuwa zikiwazuia kukubali chanjo mbalimbali.

Kwa mujibu wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) 2021/22 - 2025/26, Serikali ya Tanzania kupitia Sera ya Afya 2007 imewekeza sana katika kuboresha uhai wa mtoto kupitia utoaji wa huduma bure za afya kwa akinamama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.


Tunzaa yawakarabisha wafanyabishara kuuza bidhaa zao

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni Tunzaa, Ng'winula Kingamkono akizungumza na waandishi habari kuhusiana na biashara ya kuuza bidhaa kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam.

Picha mbalimbali zikionyesha namna wanavyopata wateja kwa njia ya Mtandao


*Ni kwa njia mtandao wateja kulipa kidogo kidogo

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
KAMPUNI ya Tunzaa ya kununua bidhaa kupitia program Nununu (APP) imesema kuwa tangu kuanza kwake imeanza kuwa na wateja mtandao wengi ambapo bidhaa zilizopo sokoni ni chache ambapo amewata wafanyabiashara wateja  kuingia makubalino na kampuni hiyo ili kuweza kuuza bidhaa zao kukidhi mahitaji ya wateja hao.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Kampuni Ngw'inula Kingamkono amesema kuwa wanaonunua bidhaa kwa njia ya mtandao wamekuwa wengi ambapo bidhaa zingine wanazikosa ambayo ni fursa ya wafanyabiasha kuingia na Tunzaa na kufanya biashara kutokana na uhakika wa soko.

Amesema kuwa ununuzi wa bidhaa katika maduka mbalimbali ni kuweka kidogo kidogo katika mfumo wa malipo ndani ya Tunzaa na mara kukamilika malipo ndipo mteja atapata bidhaa mahali popote alipo kama alivyotoa pendekezo lake.

Kingamkono amesema hadi sasa wateja hadi sasa wamefikia 12000 ambapo mwitikio mkubwa ambao haundani na bidhaa hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kujiunga ili kwenda kuwafikia wateja kwa wingi.

Amesema mfanyabiashara anayetakiwa ni wale walio katika mifumo ya biashara wanamaduka yaliyosajiliwa ili kuendelea kuweka imani kwa wateja.

Aidha amesema lengo ya kampuni ni kuona wafanyabishara wanafikia matarajio yao kwani kufanya biashara na kampuni ya Tunzaa kutawafanya bidhaa zao kutoka kwa haraka na kuagiza bidhaa zingine na kufanya kumudu ulipaji wa kodi pamoja na huduma zingine katika biashara.

"Tunzaa ipo katika kufanya biashara zikuwe kwani wateja wa kulipa kidogo kidogo ni wengi kuliko wa kulipa kwa pamoja lakini hivyo suluhu imepatikana kuanzisha Tunzaa ambapo wafanyabiashara ndio watatoa huduma ya mahitaji ya jamii" amesema Kingamkono

Hata hivyo amesema wateja wengi wamekuwa wakiuliza vifaa vya ujenzi na magari ambapo hakuna wafanyabiashara walioko katika mfumo wa Tunzaa.

Amesema licha ya kuanzisha hiyo wamekuwa wakitoa huduma nyingine ya kutengeneza teknolojia ikiwa ni pamoja ya kuwainua vijana waliosomea masuala ya tekonolojia.

WATEJA KUOKOA HADI TSH 1,000,000 KAMPENI MPYA YA 'LGs SOMETHING BETTER'

$
0
0

 KAMPUNI mashuhuri kwa uuzaji wa  bidhaa zinazotumia  umeme ya  LG Electronics East Africa imetangaza kuzindua Kampeni ya " LGs Something Better "  kote nchini inayolenga kuboresha uzoefu wa ununuzi kwa wateja.

Kampeni hiyo, inatarajia kuendelea hadi tarehe 12 Juni 2022 kwa lengo la kuwapa wateja punguzo la hadi 20% kwa bidhaa zilizochaguliwa pamoja na thamani na manufaa zaidi kwa wateja wanaonunua bidhaa kutoka kwa maduka ya chapa ya LG.

Kwa punguzo la ofa, wateja wanatarajiwa kuokoa kuanzia shilingi 50,000/= hadi kufikia Tsh 1,000,000/= katika kipindi cha wiki tano zijazo katika bidhaa zote katika kategoria ya Burudani , Vifaa vya Nyumbani na Viyoyozi vya Makazi.

Akitoa maoni yake kuhusu kampeni hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa LG Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim alisema, 

“Kupitia ubunifu na bidhaa zetu za hivi punde, lengo letu ni kuwasaidia wateja wetu kuishi maisha bora na rahisi zaidi. Huu ukiwa ni mwezi wa Eid al-Fitr, tunatoa nafasi kubwa kwa kila mtu kuchagua maisha haya bora sio tu ya leo bali ya kesho pia”. 

"Hii pia ni fursa kwa Watanzania kubadilisha na kuboresha burudani zao za nyumbani au vifaa ambavyo wamekuwa navyo kwa muda mrefu hadi kufikia teknolojia mpya, ya kisasa na vifaa vya ufanisi zaidi".

 Hii si tu katika maduka yenye chapa ya LG bali pia katika maduka makubwa ya washirika kama vile Shoppers na Game Super Market.

Wanunuzi wamehakikishiwa kupata punguzo kubwa la hadi Tsh 539,200/=kwenye jokofu za LG Instaview 668(L), na Tsh 225,000/= kwenye jokofu la LG Instaview 544(L). Kwenye mashine za kufulia zinazotolewa, punguzo linaanzia Tsh 100,000/= hadi Tsh. 300,000 kwa mashine za kufulia ya 8Kg hadi ya 15Kg / dryer. LG microwaves, Neo Chef 20L, 23LNeoChef na 42L Neo Chef zote zina punguzo la kati ya Tsh 81,600/= na TZsh 122,800/=

Kufahamu zaidi kuhusu kampeni hii kabambe tafadhari tembelea mitandao ya kijamii ya LGs East Africa.

Kanisa la House of Prayers Shield of Faith Christian Fellowship waiomba Serikali kufanya uchunguzi sehemu alipo 'Mzee wa Yesu'

$
0
0
Mama Mteule wa Kanisa la House of Prayers Shield of Faith Christian Fellowship,  Greener Mkombo  akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuhusu kutojulikana alipo Askofu wa Kanisa hilo Mulilege Kameka maarufu kama 'Mzee wa Yesu'.
Kuhani wa Kristo wa Kanisa la House of Prayers Shield of Faith Christian Fellowship Nazar Nicholaus  akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuhusu kutojulikana alipo Askofu wa Kanisa hilo Mulilege Kameka maarufu kama 'Mzee wa Yesu'.
Baadhi ya waumini na viongozi wa kanisa wakifatilia tamko la kanisa kuhusiana na kutoweka kwa Askofu wa Kanisa hilo Mulilege Kameka maarufu kama 'Mzee wa Yesu'.

*Wadai Serikali ina Mkono mrefu wa kujua aliko Mzee wa Yesu

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
KANISA la House of Prayers Shield of Faith Christian Fellowship limeiomba Serikali kusaidia kujulikana alipo Askofu wa Kanisa hilo Mulilege Kameka maarufu kama Mzee wa Yesu.

Ombi hilo limetolewa Mei 22, 2022 jijini Dar es Salaam na Kuhani wa Kristo Nazar Nicholaus akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni Siku saba zimepita tangu kutoweka kwake licha juhudi kufanyika.

“Rai kwa Serikali, tunachotaka kujua ni Askofu Mulilege yupo wapi ili aweze kuhudumiwa kwani hadi sasa tumeshazunguka kila mahali ikiwemo kwenye vituo vya Polisi lakini hatujamuona,” amesema Nicholas na kuongeza kwamba.

“Tumemua kuongea na vyombo vya habari Rais asikie pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwani Rais ameshaiweka nchi kwenye Sheria."

Nicholaus amesema tangu wamezungumza juu ya hilo Jumatano iliyopita bado hakuna jipya hadi leo juu ya taarifa za aliko 'Mzee wa Yesu'.

“Tunaamini Serikali ina mkono mrefu hakuna kitu kinaweza kufanyika wahusika wasijulikane, amesema Nicholaus.

Hata hivyo Nicholaus amesema wataendelea kumtafuta na kufanya maombi bila kuchoka ili kuhakikisha Askofu anapatikana.

Kwa upande wake Mama Mteule wa Kanisa hilo ambaye pia ni Mke wa Mzee wa Yesu Greener Mkombo amefichua kwamba tangu mwaka 2011 amekuwa akisumbuliwa kwa madai kwamba sio Raia wa Tanzania.

Kwamba tatizo hilo lilianza mara tu walipohamia jijini Dar es Salaam wakitokea mkoani Mbeya.

Hata hivyo amesema pamoja na hayo 'Mzee wa Yesu' amekwisha shinda kesi na Mahakama Kuu kuthibitisha kwamba ni Mtanzania.

Hivyo amesisitiza Serikali kusaidia kupatikana kwa 'Mzee wa Yesu' ili kama anashikiliwa kwa makosa yoyote aweze kufikishwa Mahakamani ili mkondo wa Sheria uchukuliwe.

TIBA yasisitiza Bima kwa wanamichezo wote

$
0
0
Chama cha Washauri wa huduma za bima nchini (TIBA) kimetoa rai kwa wasimamizi wa michezo nchini kuweka takwa la kisheria kwa wachezaji kuwa na bima ya ajali na afya ili kuchangia kutoa hamasa na maendeleo ya michezo nchini.

Rais wa TIBA, Amir Kiwanda alisema kuwa kwa sasa msisitizo zaidi umewekwa katika timu za mpira wa miguu za Ligi Kuu na kusahau kuwa Tanzania ina michezo mingi ambao inashirikisha wachezaji ambao wap katika hatari kupata ajili michezoni.

Kiwanda alisema kuwa mchezaji mwenye bima anakuwa na  moyo wa kujituma zaidi uwanjani kwani  endepo anapata tatizo  la kuumia, hatokuwa na wasiwasi katika kupata matibabu.

“Hii ni tofauti na mchezaji ambaye hana bima na hasa ukizingatia kuwa kuna matukio kadhaa ya kusikitisha yanayowahusu wachezaji ambao ilifikia kipindi wadau wanachezesha mechi ili kupata fedha za kusaidia matibabu,”alisema Kiwanda.

Alisema kuwa kazi ya TIBA ni kutoa ushauri kwa watoaji huduma ya bima na wamefanikiwa kwani mpaka sasa kuna huduma nyingi za bima zinazotolewa na makampuni hayo.

Alifafanua kuwa huduma hizo ni muhimu kusaidia kuepuka gharama kubwa za matibabu wanapopatwa na matatizo ya kiafya na janga la kuumia kwenye shughuli za michezo.

Alisema kuwa Tanzania ina michezo mingi na wachezaji wamekuwa wakikumbana na ajali mbalimbali katika michezo na kujikuta kuanza kuangaika katika gharama za matibabu.

Alifafanua kuwa ili kuweza kuwa na mshikamano, wameamua kufanya bonanza la michezo na kushirikisha wadau mbalimbali na kuendelea kutoa ushauri  wa shughuli za bima nchini.

“Bonanza hili ni jukwaa la kuwakutanisha wadau wa bima na kucheza huku tukikumbushana umuhimu  wa utoaji  huduma za bima hapa nchini,” alisema.

Bonanza hilo la tatu lilifanyika kwenye viwanja vya  Don Bosco Namanga na kushirikisha timu ambazo ni TIBA, TAN-RE, IFM, Magnet, Assemble, ATI, TIRA, Sanlam, Alliance, bancassurance na Mawakala.

Wachezaji wa netiboli wakishindana


Hotuba Ya Bajeti Ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Mwaka 2022-23

$
0
0

 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.
Viewing all 119527 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>