SERIKALI YAZIHAKIKISHIA KAMPUNI ZA USWISI MAZINGIRA SALAMA YA BIASHARA, UWEKEZAJI
WAZIRI SIMBACHAWENE AZINDUA MCHORO WA BARABARANI UNAOONESHA ENEO MAALUM LA KUSIMAMA PIKIPIKI JIJINI ARUSHA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo na kulia kwake ni Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mkadam Mkadam ambae ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakiwa katika picha ya pamoja na Wadau mbalimbali katika uzinduzi (MOTORCYCLE BUFFER ZONE) katika eneo la Sanawari mkoani Arusha.(Picha na Jeshi la Polisi).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe, George Simbachawene, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mkadam Mkadam, ambae ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani na Wadau mbalimbali wakikata utepe katika uzinduzi wa mchoro wa Barabarani unaoonesha eneo maalum la kusimama Pikipiki (MOTORCYCLE BUFFER ZONE) katika eneo la Sanawari mkoani Arusha.(Picha na Jeshi la Polisi).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Simbachawene akisalimiana na moja wa madereva Bodaboda kabla ya uzinduzi wa kivuko cha mchoro wa Barabarani unaoonesha eneo Maalum la Kusimama Pikipiki (MOTORCYCLE BUFFER ZONE) katika eneo la Sanawari mkoani Arusha. (Picha na Jeshi la Polisi).
WAJASIRIAMALI WADOGO NA WA KATI WAHAMASISHWA KUSHIRIKI MAONESHO YA 21 YA NGUVU KAZI/JUA KALI JIJINI

Serikali ya awamu ya Sita imeweka mikakati ya kupambana na ukatili wa kijinsia -Mratibu Kulaya
ZIARA YA KUTEMBELEA VISIMA VYA MAJI SAFI NA SALAMABBUMBWISUDI MAGHARIBI “A”



MANISPAA KAHAMA YATAKIWA KUONGEZA KASI YA UKUSANYAJI KODI YA ARDHI
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Clemence Nkusa wakati wa ziara yake katika manispaa hiyo tarehe 25 Novemba 2021.
POLISI WATAKIWA KUONGEZA KASI YA UKUSANYAJI MAPATO



KILI MARATHON YAWATAKA WASHIRIKI WA KANDA YA KASKAZINI KUJISAJILI MAPEMA
Na Mwandishi Wetu.
MAANDALIZI ya mbio maarufu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon ambazo zinatimiza miaka 20 tangu kanzishwa kwake, yamefikia hatua nzuri huku waandaaji wakitoa wito kwa washiriki kutoka Kanda ya Kaskazini wajisajili mapema kuepuka usumbufu dakika za mwisho.
Wito huo umetolewa kutokana na uzoefu wa miaka ya mnyuma ambapo washiriki kutoka kanda hiyo ya kaslkazini ambayo ndio mwenyeji wa mbio hizo, wamekuwa wakisubiri hadi dakika za mwisho ili wajisajili jambo ambalo huwaacha baadhi na masikitiko baada ya kukuta namba zote zimeshauzwa.
“Tunatoa wito kwa washiriki kutoka Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara kujisajili kwa njia ya mtandao kupitia Tovuti yetu Au kwa njia ya Tigopesa kwa kupiga *149*20#,” alisema Aggrey Marealle ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Executive Solutions, waratibu wa mbio hizo kitaifa.
Alisema mbio hizo za mwakani zinategemewa kuwa kubwa zaidi kwa sababu itakuwa ni mwaka wa 20 tangu kuanzishwa kwake kwa hivyo washiriki wana kila sababu ya kujisajili na kuhakikisha wanathibitisha ushiriki wao kwa kujisajili.
“Huwa inasikitisha sana kuona washiriki kutoka Moshi au Arusha wanakosa namba wakati wanatokea katika kanda mwenyeji wa mbio hizi. Namba zikishaisha usajili huwa unafungwa. Kwa kawaida hakuna namba zinazouzwa katika vituo vya kutolea namba isipokuwa tu kwa mbio za KM 5 kama zitakuwa zimebakia,” alisema.
Alisema kujisajili ni rahisi mno na kwa sasa kuna punguzo la bei la asilimia 20 lakini ifikapo Januari 7, 2022 bei zitapanda kwani hakutakuwa na punguzo tena.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa mbio hizo, Bw. John Bayo alisema washiriki wote wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager 42km , Tigo 21km na Grand Malt 5km waanze mazoezi mapema ili wajiandae na mbio hizi za 20 za Kilimanjaro Marathon ambazo ni za kihistoria.
“Tunataka mbio hizi ziwe za ushindani zaidi na ziache kumbukumbu ya aina yake miongoni mwa washiriki kwa hivyo maandalizi ni muhimu sana. Ni matumaini yetu kuwa zawadi nyingi zitabaki hapa nyumbani safari hii. Kama waandaaji tutafanya sehemu yetu na tunatoa wito kwa washiriki wafuate maelekezo ili kufanya mbio za mwakani ziwe za kufana zaidi kwani tunatarajia washiriki kutoka nchi zaidi ya 55 na umati unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi kuliko miaka ya nyuma,” alisema.
Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania Bw. Jackson Ndaweka alisema wameridhishwa na maandalizi hadi sasa kwani wamekuwa wakipokea taarifa kutoka kwa waandaaji wa Kilimanjaro Marathon.
“Hili ndio tukio kubwa kabisa la riadha nchini ambalo huwaleta pamoja zaidi ya washiriki 12,000 kutoka ndani na nje ya Tanzania kwa maana hiyo tunashirikiana na waandaaji kwa karibu kuhakikisha mbio hizi zinafanikiwa na zinaweka riadha ya Tanzania katika kiwango cha kimataifa. Wanariadha wa hapa nchini hujipatia kipato kwa kushiriki mbio hizi lakini pia huwandaa vizuri katika mashindano ya nje ya nchi.Mbio hizi pia zinachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la nchi kwa sababu ya watalii ambao hutembelea vivutio mbalimbali,” alisema.
Alisema RT pia imefarajika kusikia kuhusu maonesho yaliyoandaliwa na wandaaji wa Kilimanjaro Marathon kama sehemu ya madhimisho ya miaka 20 ya mbio hizo. “Maonesho hayo yatatoa fursa nzuri kwa wadhamini kujitangaza vizuri na pia wananchi watapata maelezo mengi kuhusu Kili Marathon na riadha kwa ujumla. Tutakuwepo kutoa mchango wetu katika suala hili,” alisema.
Wadhamini wa Kilimanjaro Marathon 2022 ni Kilimanjaro Premium Lager- 42km, Tigo- 21km, Grand Malt -5km wadhamini wa meza za maji ni Absa, Unilever, TPC Sugar, Simba Cement, Kilimanjaro Water, na wasambazaji maalumu Kilimanjaro Leather Industries Company Limited, GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel na CMC Automobiles.
Mbio za mwakani zitafanyika katika Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi Februari 27, 2022.
Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon huandaliwa na kampuni ya Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive Solutions Limited.
ZIMAMOTO YAPATA UGENI KUTOKA HAMBURG, UJERUMANI



WATANZANIA WAUSHUKURU UBALOZI WA TANZANIA UBELGIJI
MILIONI 950 KUJENGA VITUO VIWILI VYA AFYA MANISPAA YA SONGEA
DC TANDAHIMBA AIPONGEZA REA


UCHUMI WA TANZANIA UNATARAJIWA KUKUA KWA KASI...
SHIRIKA LA POSTA, MRISHO MPOTO WAINGIA MAKUBALIANO YA KUTANGAZA BIDHAA NA HUDUMA
BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA YAIPATIA TANZANIA MKOPO WA DOLA MILIONI 116.34 KUJENGA BARABARA MKOANI MTWARA
UTT AMIS YADHAMINI WIKI YA NENDA KWA BARABARANI JIJINI ARUSHA
Inawakumbusha wawekezaji wake na watanazania wote kwa ujumla kujali usalama wao wawapo barabarani na kujali usalama wa wengine.
Sambamba na udhamini huo UTT AMIS inashiriki maonyesho yanayoambatana na maadhimisho hayo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
UTT AMIS inawakaribisha wakazi wa Arusha kutembelea banda lao ili kujifunza juu ya uwekezaji wenye tija kwenye mifuko inayosimamiwa na UTT AMIS. Maadhimisho hayo yameanza rasmi Novemba 23 na yatafikia kilele chake Novemba 28.
Benki ya Exim Yatangaza washindi wa droo ya kwanza ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’
Benki ya Exim imetangaza washindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’inayoendeshwa na benki hiyo ikilenga kuhamasisha watanzania kujiwekea amana huku wakipata fursa za kunyakua zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu pamoja na gari aina Toyota Vanguard.
Akitangaza washindi wa droo ya kwanza ya kampeni hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano Msaidizi wa Benki hiyo Bi Mariam Mwapinga alisema jumla ya washindi 6 walipatikana kupitia droo hiyo na kujishindia zawadi ya shillingi million sita fedha taslimu.
“Katika droo ya leo jumla ya washindi sita (6) wamepatikana na wameweza kujishindia zawadi za fedha taslimu kiasi cha sh mil 6. Washindi hawa sita watakabidhiwa zawadi zao katika maeneo yao waliopo na tutaendelea na droo kama hizi kila mwezi na washindi wataendelea kuingia kwenye droo itakayowawezesha kushinda zawadi kubwa ya gari aina ya Toyota Vanguard.’’
“Wateja wetu wa sasa na wale wapya watakuwa kwenye nafasi ya kujishindia zawadi hizi kila wakapojiwekea akiba ya kuanzi Tsh. 500,000 na kuendelea. Kadili wanavyojiwekea amana kubwa zaidi ndivyo wanavyojiweka kwenye nafasi ya kushinda zawadi kubwa zaidi,’’ alisema Bi Mariam wakati wa droo hiyo iliyohudhuriwa pia na muwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini.
Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo Bi Mariam alisema inalenga kuleta mabadiliko kwenye mtazamo wa uhifadhi wa amana miongoni mwa watanzania kutoka kuhifadhi pesa majumbani na badala yake wazihifadhi kupitia benki hiyo kwa usalama wa fedha zao sambamba na faida nyingine nyingi ikiwemo riba.
“Lengo si tu kuhamasisha watanzania kujenga utamaduni wa kujiwekea amana, tunachohitaji ni kuona kwamba Watanzania wengi wanajiwekea amana zao sehemu salama ili kujiendeleza kukua kiuchumi ndio maana tumejipanga kuwahamasisha watumie akaunti zetu mbalimbali ikiwemo akaunti ya mshahara inayotumika kwa matumizi mbalimbali ya kila siku,’’ alitaja.
Alitaja akaunti nyingine kuwa ni pamoja na akaunti ya mzalendo inayoendeshwa bila makato ya kila mwezi, akaunti ya haba na haba, akaunti ya faida ambayo inakuruhusu kuweka akiba na kupata riba pamoja na akaunti ya Nyota ambayo ni akaunti maalum kwa ajili ya Watoto pamoja na akaunti ya wajasiriamali inayowahudumia wafanyabiashara na mahitaji yao tofauti tofauti ya kibiashara.
Kwa upande wake Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bi Bi Neema Tatock alitoa pongezi kwa washindi wa promosheni hiyo huku akiwahamasisha walengwa kushiriki kwa wingi na kwamba wana nafasi kubwa ya kujishindia zawadi lukuki katika droo zinazofuata huku akiwahakikishia kuwa Bodi hiyo imejipanga kuhakikisha zoezi la kupata washindi linafanyika kwa kwa uwazi na kwa kufuata misingi halali ya kubahatisha.
Meneja Masoko na Mawasiliano Msaidizi wa Benki ya Exim Bi Mariamu Mwapinga (wa kwanza kushoto) akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani ) zawadi kubwa ya gari aina ya Toyota Vanguard itakayotolewa kwa mshindi wa kampeni ya benki hiyo inayofahamika ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’inayolenga kuhamasisha watanzania kujiwekea amana kupitia benki hiyo. Wengine ni pamoja na Wengine ni ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bi Neema Tatock (wa pili kushoto) na maofisa wa benki hiyo.
Meneja Masoko na Mawasiliano Msaidizi wa Benki ya Exim Bi Mariamu Mwapinga (Katikati) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’ inayolenga kuhamasisha watanzania kujiwekea amana kupitia benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bi Neema Tatock (Kulia) na Ofisa Bidhaa za Rejareja, Callist Butinga (Kushoto)
VIONGOZI UBUNGO WANOLEWA JINSI YA KUTUMIA MFUMO WA KIDIGITALI KULIPIA FEDHA ZA MAEGESHO YA MAGARI
Semina hiyo ilijikita katika kufafanua kwa kina kuhusu mfumo mpya wa Kielektroniki wa malipo ya Ushuru wa maegesho ya magari ambao unatarajia kuanza Desemba 1,2021.
Akifungua semina Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James ameipongeza TARURA kwa kuandaa semina hiyo na amehaidi kutoa ushirikiano.Ofisi ya Rais ya Rais TAMISEMI, TARURA kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango wameboresha mfumo, sasa kumbukumbu namba (Control number) itapatikana ndani ya dakika moja kwa kutumia njia ya kutolewa ankara kupitia kwa Mkusanya Ushuru
Kwa kutumia TeRMIS App (inayopatikana PlayStore), Kwa kutumia GePG App (inayopatikana PlayStore & AppStore), Kwa kutumia simu ya mkononi Piga *152*00# kisha fuata maelekezo na Kwa kutumia Wavuti ya mfumo inayopatikana kwa www.termis.tarura.go.tz.
Pia, TARURA imeboresha eneo la utoaji wa Elimu kwa kuanzisha Dawati la Malalamiko na kuweka namba za simu ambazo ni 0733-149658, 0733–149659 au 0733-149660 na kupitia namba hizi mteja atapiga simu na kutatuliwa changamoto yake. Pia anaweza kuwasilisha lalamiko lake katika Ofisi za TARURA zilizopo karibu yake.
Katika semina hiyo washiriki wa semina hiyo wameelezwa jinsi ambavyo unatakiwa kulipa maegesho kidigitali ambapo mhusika atatakiwa kutumia simu ya mkononi
Piga *152*00#
1. Chagua 4 (Nishati, Madini na Usafiri)
2. Chagua 2 (TARURA)
3. Chagua 1 - Lipia Maegesho
4. Ingiza namba ya chombo cha Moto
5. Utapokea ujumbe mfupi
6. Bonyeza 1 Kuendelea
7. Ingiza namba ya Siri
8. Bonyeza 1 Kuthibitisha malipo ya Serikali.
MADAKTARI WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI YA TAALUMA
WAMJW-Dodoma
Wanataaluma ya Udaktari wametakiwa kuzingatia Sheria, Kanuni Na Maadili ya taaluma hiyo katika utendaji kazi wao kama inavyoainishwa katika kifungu cha Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno na Wataalamu wa Afya Shirikishi.
Hayo yamesemwa leo na Msajili wa Baraza la Madaktari Tanganyika Dkt. David Mnzava alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari jijini Dodoma.
Dkt. Mnzava amesema kumekuwa na uvunjifu wa Sheria kwa baadhi ya wanataaluma kwa kukiuka Kanuni za Madaktari, Madaktari wa Meno na wanataaluma wa Afya Shirikishi, hivyo amewataka kuzingatia sheria hizo.
Sheria ya mwaka 2017 inasimamia utendaji Kazi wa kada ya Udaktari, Udaktari wa Meno, Wataalamu wa mazoezi ya tiba, Wataalamu wa viungo bandia, Wataalamu wa Magonjwa ya Akili na utengemao, Matabibu, Matabibu Wasaidizi na Wataalamu wa Meno wasaidizi.
Aidha Dkt. Mnzava amesema Uvunjwaji wa Kanuni hizi utasababisha kosa la Kimaadili kama inavyonukuliwa katika kifungu cha 41 (2).
"Kifungu hicho kinasema Mtaalamu wa Udaktari, Udaktari wa Meno au Afya Shirikishi ataonekana kukosa sifa ya kutoa huduma, chini ya Sheria hii atakuwa amekiuka Sheria za Maadili." Amesema Dkt. Mnzava.
Hata hivyo Baraza limetoa wito kwa wasimamizi wa Mikoa na Wilaya kuweka mipango thabiti ya kusimamia utendaji wa wanataaluma katika maeneo yao