Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 120255 articles
Browse latest View live

MILIONI 700 ZAMALIZA KERO YA MAJI KIPAPA NA MHILO

$
0
0

Na Muhidin Amri, Mbinga
MAMLAKA ya maji safi na usafi wa mazingira Manispaa ya Songea(Souwasa),imekamilisha ujenzi wa miradi miwili ya maji kwa mafanikio makubwa katika vijiji vya Mhilo na Kipapa katika Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Kukamilika kwa miradi hiyo kumemaliza kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa vijiji hivyo ambao kabla ya ujenzi wa miradi hiyo, walilazimika kutumia maji ya visima vya asili vilivyochimbwa kienyeji na wengine kwenda mtoni kuchota maji ambayo hayakuwa safi na salama.

Meneja ufundi wa Souwasa Jafari Yahaya alisema, Serikali imetoa jumla ya shilingi milioni 772 ili kujenga miradi yote mwili iliyohusisha ujenzi wa matenki, miundombinu mbalimbali na vituo vya kuchotea maji vilivyojengwa katika makazi ya watu na kwenye taasisi za umma.

Akizungumzia mradi wa Kipapa Jafari alisema, serikali kupitia wizara ya maji imetoa shilingi milioni 569 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na kuboresha huduma ya maji ambapo kati ya hizo, tayari imetoa milioni 444 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.

Alisema, kazi zilizopangwa na zilizofanyika ni ujenzi wa chanzo,ujenzi wa tenki la kusambazaji maji,usambazaji wa bomba za kusafirishia na kusambaza maji na kujenga vituo 23 vya kuchotea maji.

Kwa mujibu wake,kazi zimekamilika kwa asilimia 98 na wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama, isipokuwa ujenzi wa uzio ambao hajakamilika na unaendelea kujengwa.

Aidha katika mradi wa Muhilo Jafari alisema, Serikali imetoa shilingi milioni 203 na kazi zilizofanyika ni ujenzi wa tenki wa lita 50,000 na shughuli nyingine ambapo wakazi 1,247 wamenufaika na mradi huo.

Aliongeza kuwa, serikali imetoa fedha hizo kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji kwa wananchi wa maeneo hayo ili watumie muda mwingi kufanya shughuli za maendeleo, badala ya kupoteza muda wao kwenda kutafuta maji mbali na makazi yao.

Alisema, miradi yote ipo chini ya wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) mkoa wa Ruvuma na Souwasa ilipewa kazi ya kujenga kama fundi.

Jafari alisema, miradi yote imekamilika kwa asilimia 98 na sasa wananchi wanapata huduma ya maji katika maeneo yao pamoja na taasisi za serikali kama shule na zahanati na kuishukuru Ruwasa kwa kwa kuwaamini na kuwapa kazi ya Ujenzi wa miradi hiyo.

Manfred Nchimbi(56) mkazi wa Kipapa alisema, awali walilazimika kuamka saa 9 usiku na kutembea umbali wa km 3 kwenda kutafuta maji, lakini sasa kero hiyo imemalizika na kuishukuru serikali kupitia wizara ya maji kutekeleza mradi huo ambao umemaliza kabisa mateso ya muda mrefu.

Alisema, kabla ya kujengwa kwa mradi huo na wakala wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) chini ya fundi Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Songea(Souwasa) walitumia maji kutoka katika vyanzo visivyo rasmi lakini havikutosheleza mahitaji yao.

Kanisia Komba mkazi wa kijiji cha Mhilo,mbali na kuishukuru serikali kwa kupeleka huduma ya maji katika kijiji hicho alisema, maji hayo yamerudisha na kuboresha mahusiano na kuimarika ndoa zao.

Alisema, baadhi ya ndoa zimevunjika kwa sababu ya akina mama kuchelewa kurudi nyumbani kutoka kutafuta maji, hivyo wanaume kudhani walikuwa kwenye michepuko(nyumba ndogo) jambo ambalo lilichangia ndoa nyingi kuvunjika na kusambaratika kwa familia.

UBALOZI WA USWISI, FSDT KUZINDUA UTAFITI WA HUDUMA JUMUISHI ZA FEDHA KWA VIJANA VIJIJINI

$
0
0

 


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

 KATIKA kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani leo Machi 8, Ubalozi wa Uswisi (Switzerland)  kwa kushirikiana na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), watazindua utafiti wa Huduma jumuishi za fedha kwa Vijana wa Vijijini katika hafla itakayofanyika kwa njia ya mtandao itakayofanyika saa 8;00 mchana. Utafiti huo unalenga kusambaza maarifa ya kina kuhusu tabia na changamoto za vijana wa vijijini nchini Tanzania hususani wasichana,wenye umri wa miaka kati ya 16 na 24 katika masuala ya fedha.

Taarifa ya FinScope Tanzania ya mwaka 2017 ilibainisha kuwa wanawake na wanaume wa vijijini wenye umri kuazia miaka 16 hadi 24 waliokadiliwa kufikia  takriban watu milioni 4.4 walikuwa sehemu ya idadi ya watu waliotengwa katika huduma za fedha, huku asilimia 45 wakiwa hawajachukua huduma yoyote ya fedha  rasmi au isiyo rasmi.

Utafiti wa Fedha jumuishi kwa Vijana wa Vijijini unaonyesha wasifu halisi wa vijana wa vijijini ili kuwezesha ufumbuzi/ubunifu wa bidhaa/huduma zinazolenga kundi hili la soko linalojitokeza. Inachunguza zaidi mahitaji, mtamanio na hali ya sasa ya kiuchumi ya vijana wa vijijini, na jinsi mawasiliano ya sasa na mikakati ya watoa huduma za fedha kuingia sokoni, mipango ya uwezeshaji vijana na sera mbalimbali zinavyowaakisi.

“Mfuko wa Kuendeleza sekta ya Fedha Tanzania (FSDT) walibainisha kuwa Vijana wa Vijijini ni kundi muhimu sana katika kuleta mabadiliko kupitia huduma jumuishi za fedha, hivyo ushirikiano baina yake na Ubalozi wa Uswisi umewasilisha fursa nzuri kuimarisha uelewa wa ndani wa kundi hili”, alisema Bwana Sosthenes Kewe, Mkurugenzi Mtendaji wa FSDT

Utafiti huu unataka kutarifu mikakati ya maendeleo ya uchumi kwa vijana wa vijijini, huduma za fedha na mikakati inayolenga kuongeza ajira kwa vijana wa vijijini kwa kujiajiri kupitia huduma za fedha jumuishi zilizoboreshwa. Utafiti wa Vijana ulitumia jicho la jinsia katika  taarifa nzima kubainisha changamoto na fursa mahususi zilizopo kwa ajili ya mwanamke wa vijijini.   

“Kuongeza huduma jumuishi za fedha kwa vijana  vijijini ni changamoto kubwa – na kuongeza huduma jumuishi za fedha kwa vijana wadogo wa kike vijijini ina umuhimu wa kipekee kwani hawajanufaika kiusawa. Utafiti huu unachunguza kiini cha tofautiza usawa  wa kijinsia unaozuia kuwajengea uwezo wanawake”, alisema Balozi wa Uswisi Didier Chassot. “Upatikanaji na matumizi ya  bidhaa na huduma bora za fedha ni muhimu kwa ukuaji wa  uchumi jumuishi na katika kupunguza umasikini”.   

Tukio hili litasambaza ufahamu unaoweza kufanyiwa kazi kutokana na utafiti uliolenga kutatua changamoto mbalimbali zinazolikumba  kundi lengwa la vijana. Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, tukio hilo litazingatia hasa wasichana. Utafiti wa Fedha jumuishi kwa Vijana Vijijini ulifanywa na taasisi ya  IPSOS kwa kushirikiana na Fundacion Capital.

Uswisi imekuwa ikiunga mkono miradi ya pande mbili na ile ya kikanda nchini Tanzania tangu mwanzoni mwa miaka ya 1960. Mwaka 1981, Tanzania ikawa nchi ya kipaumbele kwa misaada rasmi ya maendeleo kutoka nchi ya Uswisi na inaendelea kupokea takriban dola za Marekani milioni 22 kila mwaka. Mpango wa Ushirikiano wa Uswisi nchini Tanzania 2021 - 24 unalenga kuwawezesha vijana, hasa wasichana masikini, kuendelea kijamii na kiuchumi kupitia matokeo matatu mtambuka ya kisekta: (i) Kuimarisha taasisi za serikali, (ii) Kukuza nafasi za uraia na (iii) Kuboresha maisha ya vijana. Mwaka 2021 inatimia miaka 40 ya ushirikiano wa maendeleo baina ya Uswisi na Tanzania.

Mfuko wa Kuendeleza sekta ya Fedha Tanzania (FSDT) ni taasisi inayo jihusisha na ujenzi wa masoko wezeshi kwa kusaidia kutatua vikwazo na changamoto zilizoko sokoni na kuchagiza ukuaji wa sekta ya fedha inayolenga  kupunguza hali ya umaskini wa watu na kipato. FSDT imejikita katika tasnia kuu nne (4), yaani Wanawake, Vijana waishio Vijijini,biashara na ujasiriamali na wakulima wadogo na wakati waliopo vijijini.

FSDT inatumia wigo mpana wa nyenzo, miundombinu na utaalamu wa kifedha kama mikopo nafuu, udhamini na misaada ya kifedha au ruzuku katika kuchochea ubunifu miongoni mwa Watoa Huduma za Fedha kwa ajili ya kuendeleza sekta ya fedha na mifumo yake. Kwa kutumia nafasi yake ya ushawishi na kitovu cha mawazo mapya/mbadala katika huduma jumuishi za fedha, FSDT inasimama kama muwezeshaji katika sekta ya fedha kwa kutumia muunganiko wa mbinu na utaalamu wa kuitisha mijadala, uzengezi na kufadhili majadiliano yanayogusa wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti mbalimbali na kuchochea shughuli za ubunifu katika sekta ya fedha.

Kutoa matokeo ya tafiti na kuzalisha machapisho juu ya sekta ya fedha ni moja ya nguzo muhimu katika kazi za FSDT zinazoiwezesha taasisi kuelewa kwa kina hali ya Huduma za Kifedha Jumuishi katika nchi yetu na kusaidia utoaji wa maamuzi unaozingatia Ushahidi wa kitafiti kwa wasimamizi wa sekta,na watunga sera na mwisho wahusika wenyewe, yaani  watoa huduma za kifedha. Ushahidi huu wa kitafiti pia ndio chachu na hutumika katika kubuni na kutengeneza miradi au shughuli zinazokidhi mahitaji halisi ya sekta ya fedha.

 

 

NCHI ZA AFRIKA KULETA SAMPULI ZAO KUCHUNGUZWA TANZANIA

$
0
0

MAMLAKA  ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema kuwa kutokana na umahiri wa maabara zilizopo kwenye Mamlaka hiyo zimeweza kutoa huduma ya upimaji wa sampuli mbalimbali kutoka Katika nchi tofauti za Afrika.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA ,Adam Fimbo katika mkutano maalum na waandishi wa habari kuhitimisha ziara ya siku tatu ya mafunzo kwenye maabara za kisasa zilizopo Dar es salaam kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo .

Amesema kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuwa na utaratibu wa kukagua na kuthibisha umahili wa maabara mbalimbali Duniani ambapo kwa nchi za Afrika Tanzania ni moja kati ya nchi chache iliyothibitishwa kuwa na maabara zenye ubora hivyo kupelekea baadhi ya nchi za Afrika kuleta Sampuli zao kwaajili ya kuchunguzwa.

"Kuna viwango vilivowekwa na WHO ukifika hicho kiwango wanakutangaza na kukupa cheti hivyo kupelekea nchi nyingine kutaka kujifunza na kuleta Sampuli zao" amesema Fimbo.

Ameongeza kuwa  Nchi hizo ni pamoja na Zambia, Lesotho, Malawi, Uganga na Kenya na kwamba hilo limewezekana kutokana na tangazwa na WHO. 

Ziara hiyo ya siku tatu imehitimishwa rasmi Machi 5,2021 kwa waandishi wa habari kutembelea maabara ya Dawa na Vifaa Tiba nyongeza kwa kuangalia maabara maalumu ya MICROBIOLOGY inayotumika kupima vifaa tiba mbalimbali ikiwemo Barakoa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano maalum wa kuhitimisha ziara ya siku tatu ya mafunzo kwenye maabara za kisasa zilizopo kwenye Ofisi zao  leo Dar es Salaam. kushoto Meneja wa Elimu ya Umma na Mawasiliano wa TMDA, Gaudensia Semwanza.
Meneja wa Elimu ya Umma na Mawasiliano wa TMDA, Gaudensia Semwanza (kushoto) akizungumza na waandishi wakati wa kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu kuzungumza na waandishi hao leo Dar es Salaam.
Mchunguzi wa Maabara  TMDA,Gerald Sambu  akufafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa ziara ya kutembea Maabara hiyo leo Dar es Salaam.
Mchunguzi wa Maabara wa TMDA Olson Mkeya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika Maabara Maalum ya MICROBIOLOGY inayotumika kupima vifaa tiba mbalimbali ikiwemo Barakoa leo Dar es Salaam.Waandishi wa habari wakimsiliza Mchunguzi wa Maabara  TMDA,Gerald Sambu wa (kulia)  leo Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
kazi ikiendelea 
Muonekano wa Maabara hiyo.

WANANCHI WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA KATIKA SUALA LA KUDHIBITI UVUVI HARAMU

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza na Viongozi wa Serikali wa Kanda ya Ziwa Victoria kuhusu ulinzi na usimamizi shirikishi wa rasilimali za uvuvi katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Na Elibariki Mafole, MWANZA
WANANCHI wametakiwa kushirikiana katika suala la kudhibiti uvuvi haramu Ziwa Victoria ili kuendelea kunufaika na rasilimali za uvuvi.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki, katika kikao cha wadau wa Uvuvi kanda ya Ziwa kilichojadili kuhusu ulinzi na usimamizi wa rasilimali za Uvuvi na kusema suala la udhibiti wa uvuvi haramu katika mwambao huo ni la kila mmoja.

Mashimba alisema suala la ulinzi wa rasilimali zilizopo ziwani ni jukumu la kila mmoja katika ngazi zote kuanzia kitongoji mpaka wilaya hadi wizarani na si jukumu la askari kudhibiti uvuvi haramu.

“Ikiwa uvuvi haramu tutaukumbatia wenyewe mtajiangamiza wenyewe, ninyi mnaofaidika na ziwa mpo, na athari mnaiona kwanini waje maaskari kutoka Dodoma au sehemu nyingine kuja kufanya msako kwenu, ndugu zangu naomba tushirikiane wote, ngazi ya Kitongoji, Kijiji, Kata wote hili ni jukumu letu suala la uvuvi haramu halikubaliki” alisema Ndaki

Mashimba alisema ipo dhana inazungumzwa kuwa uvuvi haramu ni dhana tu inayojengwa na wataalamu na serikali na kuna dhana nyingine kuwa samaki wapo tu ziwani na kuongeza kuwa ikiwa uvuvi haramu tutaukumbatia tutajiangamiza wenyewe

“Kuna dhana kuwa uvuvi haramu ni dhana tu inayojengwa nawataalam na serikali , kwamba uvuvi haramu hamna, na dhana hiyo inasema kuwa samaki wapo ziwa litaenda wapi, lakini ninyi wenyewe ni mashahidi, kuna wakati mmeanza kulia ninyi wenyewe kwamba samaki hawapo, mpaka sasa upungufu upo sasa kwanini isiwaume ninyi imuume zaidi waziri au Katibu Mkuu wa Uvuvi ambaye nyumbani kwao ni Mtwara bahari pana kuliko ziwa letu, kwanini lisituume sisi,” alisema Ndaki.

Mwenyekiti wa kikundi cha usimamizi shirikishi wa rasilimali za uvuvi (BMU) Wilaya ya Rorya Stephano Mchoye alisema halmashauri ishirikiane na vikundi hivyo ili kudhibiti uvuvi haramu kwa manufaa ya vizazi vilivyopo na vizazi vijavyo.

Ulinzi shirikishi katika ziwa letu haujaanza leo, ninaomba Wizara iangalie zana hizi zinazotumika tika uvuvi haramu zinatoka wapi dawa ya hiyo ikishapatikana naamini uvuvi haramu Tanzania hautapatikana.

Kwa upande wake Nadhil Sadick msambazaji wa mazao ya samaki nje ya nchi aliomba serikali kuangalia tozo mbalimbali wanazotozwa pasipokuangalia madhara yake kwa wanaotoza pamoja na wale wanaotozwa.

Mashimba amewaagiza halmashauri pamoja na mabaraza ya madiwani kuangalia upya tozo wanazotoza katika mialo na katika rasilimali mbalimbali za uvuvi ili kuwapunguzia mzigo wavuvi.

“Niombe halmashauri pamoja na mabaraza yenu ya madiwani hebu kaangalieni upya tozo mnazowatoza kwenye mialo na mazao mbalimbali ya uvuvi, mkaangalie upya tuone tutakapowapunguzia, tuwapunguzie mzigo kwenye hayo maeneo tunayotoka,” alisema Mhe. Ndaki.

“Mimi ni shahidi nimeenda kule Geita tozo za kwetu ngazi ya wizara kwa upande wa dagaa ni mbili tu royality na leseni, lakini zipo tozo 8 ambazo halmashauri inatoza, jumla tozo 10 anatozwa mtu mmoja halmashauri tuangalie pia ustawi wa watu wetu, anaondoka na nini kwenye hicho tunachotaka kumtoza vinginevyo mtapunguza mapato yeye ninyi wenyewe,” alisema Mhe. Ndaki.

BARBARA AMKINGIA KIFUA MORRISON

$
0
0

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa sababu za kiufundi ndio zimefanya Mchezaji Bernard Morrison kuachwa kwenye kikosi cha timu hiyo iliyoenda Sudan kwa mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji El Merreikh.

Katika mazungumzo yake na Waandishi wa Habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam baada ya kutua nchini Tanzania, Barbara amesema Morrison ni Mchezaji mzuri, mwenye nidhamu katika Kikosi cha Simba SC

Kuhusu taarifa za Mchezaji huyo kugomabana na Kocha Didier Gomes Da Rosa, CEO Barbara amesema ni uzushi taarifa hizo si za kweli, ameshauri Waandishi wa Habari kutoa taarifa zenye ukweli na uhakika kwa kuzifanyia upembuzi yakinifu kabla ya kuzitoa kwa jamii.

“Hili taarifa zinazoenea mitandaoni si za kweli ni uzushi na uongo, Waandishi wa Habari lazima watumie Uandishi wa Habari wa Kiuchunguzi (Investigative Journalim) ili kupata uhakika wa stori ambayo unataka kuitoa kwa jamii”, amesema Barbara.

Pia Barbara amesema taarifa hizo zinamkumbusha taarifa za nyuma kati ya Mshambuliaji wa timu hiyo, Medie Kagere na Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kikosi hicho, Sven Vandenbroeck.

“Mimi naona haisaidii, naona haijengi Mpira wetu, leo tungekuwa tunazumgumzia Simba SC imerejea baada ya kutoa sare na El Merreikh nyumbani kwao Sudan, labda Simba SC sasa infanye nini katika michezo yake ijayo”, ameeleza Barbara.

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii, kulienea tetesi za Mchezaji huyo wa Simba SC, Bernard Morrison kuachwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo kutokana na kutoelewana na baina yao.


 

VIONGOZI WA DINI ZANZIBAR WAMKUMBUKA MAALIM SEIF

$
0
0

 

VIONGOZI wa kidini na wale wa vyama vya siasa Zanzibar wamesema kuwa malim Seif sharif Hamad ni mtu aliyemaliza muda wake wa kuishi katika ulimwengu akiwa amewacha mafanikio  makubwa.

Hayo wameyasema katika kanisa la PEFA church of Zanzibar nje kidogo ya mji wa Zanzibar  huko Kisauni wakati wakitoa historia ya marehemu maalim Seif Sharif Hamad  katika hafla ya kumbukumbu ya kusherekea maisha ya kiongozi huyo aliyekuwa  Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo.

Viongozi hao wamelezea kuwa wanakila aina ya sababu ya kumkumbuka na kumuenzi kiongozi huyo kutokana na kile walichokisema wema mkubwa aliowatendea wazanzibar.

“Maalim alikuwa kiongozi wa aina ya kipekee na mwenye kuipenda Zanzibar na watu kutoka ndani ya moyo wake kwa nini tusimkumbuke.” walisema viongozi hao.

Naibu Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Zanzibar  Katherin Pitanao   alisema kuwa kiongozi huyo  amemaliza muda wake   akiwa na kila alama ya wema.

Alisema  Malim seif amekwenda kwa baba akiwa ameiacha Zanzibar salama na wala hawana  mashaka na  mtu aliyetangazwa kushika nafasi ya malim Seif wana imani Zanzibar itatengamaa. 

Katherina ameleza ana imani kuona Zanzibar inakwenda mbele zaidi na hana mashaka na Dk husein Mwinyi kwani ameonesha wazi kutaka umoja , maendeleo na kuinua uchumi imara wa Zanzibar.

Alisema hana mashaka na viongozi waliopo sasa anajua wanayo dhamira ya kweli ya kuitumika nchi hii sambamba na kuendelea  kuwa na mshikamano wa pamoja. 

 “Sisi tuliamini maalim Seif ameacha mali kwa muda aliotumikia nchi hii  tuliamini ameacha  majumba Dubai ana majumba Dar es Salaam ana majumba Zanzibar lakini hapana amekwenda akiwa maskini amekwenda kama alivyokuja hakuacha mali yeyote”Alisema Katherina .

Muwakilishi kutoka katika dini ya kikristo Joshua Goma amesema malim amekuwa mfano mzuri kwa kuwaunganisha na kuwaeka pamoja  watu ambao walikuwa wametofautiana kutokana na vyama vyao .

Amesema ni wajibu wa vyama vya siasa kuchukua nafasi ya kunganisha watu bila ya kujali itikadi zao za kisiasa kwani kufanya hivyo ni kuwa na uono wa mbali . 

Naibu Katibu mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo  Nassor Ahmed Mazrui amesema Marehemu maalim Seif Sharif  Hamad ameacha urathi ambao unataka  kuendelezwa ili Zanzibar ifike pale inapotaka kwenye uchumi wa bluu.

Mazrui amesema bila ya kuendelezwa yale aliyoyacha umoja maelewano na mshikamano  Zanzibar haiwezi kufika pale inapotakiwa kufika.

Kwa upande wake afisa  kutoka ofisi ya Makamo wa kwanza wa rais Makame Khatib Makame amezitaka tasisi zote nchini kuiga wigo wa kumkumbuka Maalim Seif kwa kwa kuyaenzi yale mazuri aliyoyawacha.

“Tumkumbuke Maalim Seif kwa azma yake ya kuleta umoja na mshikamano nchini Sote tusimame kwa msingi wa kuepuka rushwa na ubadhirifu na kuweka upendo miongoni mwetu.”alisema Makame.

Amesema kuwepo kwake kumeleta mashirikiano ya msingi wa kuwaleta watu pamoja na Zanzibar imepata mafanikio ya kutosha.

 “Tunamkumbuka Maalim Seif kwa kutuachia ushirikiano hatuna budi kila mmoja kuendeleza kwa nguvu zote”alisema Makame.

 

SERIKALI ITAENDELEA KUTOA FURSA KWA WANAWAKE NA WATOTO WA KIKE-DKT ABBASI

$
0
0

 

Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa fursa na kuwaamini zaidi wanawake na watoto wa kike katika nafasi za uongozi, siasa, masomo na katika taasisi za umma kwa kuwa siku zote wameonesha upendo, uchapakazi, uzalendo, umakini na utekelezaji uliotukuka.
 
 Ikumbukwe Serikali imetekeleza kivitendo na itaendelea kufanya hivyo kwani leo wanawake wameendelea kuvunja rekodi ya kushika nafasi kubwa za kiuongozi hapa nchini akiwemo Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhandisi Zena Ahmed Said ambaye kwa sasa ni mwanamke wa kwanza kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar. Tunawapenda sana wanawake na hakika mnaweza.

Kwa kuwa leo ni Machi 8, Siku ya Wanawake Duniani, kwa niaba ya Serikali tunawatakia wanawake wote wa Tanzania heri ya siku hii na waendelee kufanya  tafakuri juu ya mchango wao zaidi kwa Taifa na dunia. Tunawapenda sana

Dkt. Hassan Abbasi
Msemaji Mkuu wa Serikali.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII AAGIZA FARU WALIOTOWEKA HIFADHI YA MIKUMI KUREJESHWA

$
0
0

 



Na Lusungu Helela-Morogoro

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameiagiza Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kuhakikisha inawarejesha Faru ambao walitoweka  miaka ya 80 kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ujangili katika Hifadhi hiyo.

Akizungumza leo mkoani Morogoro  na Menejimenti ya Hifadhi hiyo, Dkt.Ndumbaro amesema kwa kuwa Faru hao walikuwepo kipindi cha nyuma lakini tatizo la ujangili lilipelekea faru hao kutoweka kabisa.

Amesema Hifadhi hiyo kwa sasa ina Wanyamapori wakubwa wa nne na sio watano ambao ni Simba, Tembo, Nyati na Chui. "Kwanini Faru hawapo katika Hifadhi hii, Je mazingira sio rafiki kwao" alihoji Dkt.Ndumbaro

" Katika uongozi wangu lazima nihakikishe Hifadhi ya Taifa ya Mikumi inakuwa "Big Five na sio Big Four " , Menejimenti nataka kuwaona faru katika Hifadhi hii kwani naamini wanaweza kuishi" alisisitiza Dkt.Ndumbaro.

Amesema ikolojia ya Hifadhi yaTaifa ya Mikumi inaruhusu Faru kuweza kuishi katika eneo hilo ikizingatiwa kuwa kipindi cha nyuma waliishi, Hivyo kurejeshwa kwao kutasaidia Hifadhi ya Mikumi kuwa Hifadhi bora zaidi kwa vile itakuwa imesheheni kiu ya Watalii wenye matamanio ya kuona Wanyamapori wakubwa wote katika Hifadhi hiyo

Ameagiza kuwa mara baada ya faru hao  kurejeshwa katika Hifadhi hiyo ni lazima ulinzi uimarishwe maradufu ili kosa lililotokea kipindi cha nyuma liisijirudie.

" Hakikisheni mnawafunga vifaa maalum vitavyowasaidia kuangalia mienendo yao ili kuwahakikishia usalama wao" alisisitiza Ndumbaro   

Amesema kurejeshwa kwa faru hao ni ishara tosha kuwa tatizo la ujangili nchi  nzima umepungua kwa asilimia 90 hivyo kuna usalama wa Wanyamapori wote wakiwemo faru watakaoletwa.

Kwa upande wake, Mtafiti wa kutoka Taasisi ya Utafi wa Wanyamapori  Tanzania( TAWIRI) Dkt. Gabriel Ottawa  amesema inawezekana faru watakaorejeshwa wataweza kuishi vizuri kwa vile kipindi cha nyuma faru hao walikuwepo katika Hifadhi hiyo

Ameahidi mbele ya  Waziri kuwa watafanya kila liwezekanalo kwa kufanya  tafiti mbalimbali kabla  ya kuwaleta faru hao ili kujua changamoto pamoja na kuzitafuta ufumbuzi wa namna faru hao wakishaletwa waweze kuishi kwa usalama ili waweze kuendeleza kizazi katika Hifadhi hiyo.

Naye Kamishna Mwandamizi wa Kand ya Mashariki, Asteria Ndaga alikiri kuwepo kwa faru katika kipindi cha nyuma na hivyo kuahidi kuwa maelekezo aliyoyatoa Mhe.Waziri yatatelelezwa haraka na kwa umakini wa hali ya juu.



Wakulima wa chai Njombe waliotaka kugoma kuchuma majani wapigwa 'stop'

$
0
0
Na Amiri Kilagalila,Njombe
MKUU wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya ameagiza wamiliki wa viwanda vya chai vya Lupembe estate na kampuni ya DL kufika ofisini kwake jumatatu wakiwa na taarifa za utekelezaji wa maelekezo waliyopewa kuhusiana na malipo ya wakulima na wasafirishaji wa chai.

Agizo hilo amelitoa leo katika kikao na waandishi wa habari ambacho kimefanyika ofisini kwake hapa mkoani Njombe.

Amesema kwa kipindi kirefu kumekuwa na mgogoro wa wakulima wa chai kutolipwa fedha zao na wamiliki wa viwanda vya kuchakata chai.

Amesema wakulima na wasafirishaji walikuwa wanadai fedha zao kuanzia mwezi wa kumi mwaka jana hadi januari mwaka huu ambapo fedha wanazodai ni shilingi milioni 996.

"Jana nilifanya kikao na viongozi na wakulima wa chai kule Lupembe katika kikao hicho ilibainika kuwa wamiliki hawa bado hawajalipa fedha za wakulima na fedha za wasafirishaji kama nilivyoelekeza kwenye barua yangu" amesema Rubirya.

Aidha amesisitiza kuwa zoezi la kusitisha uchumaji wa chai halikubaliki kwasababu viwanda vinahitaji malighafi licha ya kuwa wakulima nao wanahitaji fedha zao kwa ajili ya kuendesha maisha yao na familia zao.

Amesema pia siku hiyo atakutana na mbunge wa jimbo la Lupembe na madiwani ambapo atatoa maelekezo na msimamo wa serikali.juu ya suala hilo.

"Ni lazima kuvuna chai kwasababu inahitajika viwandani kitendo chochote cha kuendelea kusitisha uvunaji wa chai kinatafsiriwa kama ni uhujumu uchumi" amesema Rubirya.

NIC, TPB WAKUBALIANO KUTOA HUDUMA ZA BIMA KWA PAMOJA KWA WATEJA WAO

$
0
0

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC,) na Benki ya TPB wameingia makubaliano ya kutoa huduma za Bima kwa pamoja kwa wateja wao ili kufikia lengo la sekta ya bima na kuhakikisha asilimia 50 ya watanzania wanafikiwa na huduma za bima ifikapo mwaka 2028.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mkoani Dar es Salaam ,Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Sabasaba Moshingi amesema, huduma za bima bado zipo chini lakini kupitia ushirikiano huo na watapiga hatua katika kutoa huduma za bima zinazohitajika kwa kiasi kikubwa na Watanzania.

"Kwa taarifa nilizozipata lengo la sekta ya bima ni kuhakikisha asilimia 50 ya watanzania wanafikiwa na huduma za bima ifikapo mwaka 2028 na kwetu tumedhamiria kuhakikisha watanzania wanapata huduma za kifedha ikiwemo kutoa fedha na kufungua akaunti na kupata huduma za mikopo...

*Lakini suala la bima ni muhimu zaidi niwapongeze NIC kwa kutuamini na kutupa nafasi, niwahakikishie kuwa sisi tupo kibiashara na tumefarijika sana na tutadumisha mahusiano haya katika kuendeleza soko la bima nchini,"amesema.

Aidha amesema benki hiyo italipa ada ya awali  kwa wateja wa NIC kupitia mkopo wenye riba wenye pamoja na kuendelea kubuni bidhaa za bima za maisha pamoja na huduma nyingine za bima kwa malengo ya kuwasaidia watanzania katika kupata huduma za bima na fedha.

"Tunategemea kuunganisha mifumo ya usajili wa bima yaani wa TPB na NIC na kuendelea na harakati za pamoja za kukuza uelewa wa bima kwa wananchi kote nchini na niwaombe wananchi na wateja wote wa TBP kutembelea  matawi yetu yaliyopo kote  nchini ili waweze kupata huduma za bima bora zaidi kutoka NIC,"amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC,) Dkt. Elirehema Doriye amesema, NIC inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 hivyo watanzania hawana budi kufurahia makubaliano hayo na TPB ambayo pia inamilikiwa na Serikali na wanahisa wachache.

"Tunawafikishia huduma kwa ukaribu zaidi kupitia matawi ya NIC na TPB kote nchini, tumezogeza huduma karibu ili tuweze kuwahudumia na kuwasilikiza wananchi kwa ukaribu zaidi." Amesema.

Pia amesema, benki ya TPB ina wataalamu wa bima kwenye kila tawi nchini na hiyo ni katika kutengeneza bidhaa za bima zinazojibu maswali ya kibima yenye uhitaji zaidi kwa Watanzania.

Amesema kupitia TBP, wanawawezesha Watanzania kupata huduma za kibima bila kuwa na fedha mkononi bali kwa  kukopa kupitia TBP kupitia makubaliao yao kwa bei nafuu na kupata huduma zote muhimu za kibima.

"Makubaliano haya yana mtazamo chanya kwa watanzania na ndoto za Rais Magufuli kwa watanzania tunaamini zitafikiwa kupitia hili na nimuhakikishie Sabasaba tutakuwa pamoja katika hili na kufanikisha kutimiza ndoto za watanzania wengi,"amesema.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC,) Dkt. Elirehema Doriye kwa pamoja wakitia saini makubaliano ya kutoa huduma za Bima kwa pamoja kwa wateja wao ili kufikia lengo la sekta ya bima na kuhakikisha asilimia 50 ya watanzania wanafikiwa na huduma za bima ifikapo mwaka 2028,hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC,) Dkt. Elirehema Doriye wakikabidhiana nyaraka za makubaliano ya kutoa huduma za Bima kwa pamoja kwa wateja wao ili kufikia lengo la sekta ya bima na kuhakikisha asilimia 50 ya watanzania wanafikiwa na huduma za bima ifikapo mwaka 2028,hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dar es Salaam.

WAZIRI CHAMURIHO AKAGUA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA KASULU HADI NYAKANAZI

$
0
0

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Kibondo hadi Kabingo (km 62.5), inayojengwa kwa kiwango cha lami na Kampuni ya China Henan International Cooperation kwa gharama ya Shilingi Bilioni 80.9. Kushoto kwa Waziri ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma, anae elekeza ni Mhandisi Mshauri Hamis Khatibu.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho akiangalia ramani ya eneo la mradi wa  barabara ya Kanyani hadi Mvugwe (km 70.50), inayojengwa kwa kiwango cha lami na Kampuni ya M/s Synohydro Corporation kutoka Korea kwa gharama ya Shilingi Bilioni 98.8. Alieshika ramani hiyo ni Mhandisi Mshauri Hilary Rugarabamu pembeni yake ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Kigoma Mhandisi Narcis K. Choma.

 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho akiangalia mpango kazi wa ujenzi wa barabara ya Kibondo hadi Nyakanazi (km50), inayojengwa kwa kiwango cha lami na Kampuni ya Nyanza Road Works Limited kwa gharama ya Shilingi Bilioni 45.9, bila VAT. Anae elezea mpango kazi huo ni Mhandisi Mshauri Sharma, alieushika ni Meneja wa Wakala wa Barabara mkoa wa Kigoma Mhandisi Narcis Choma.

Ujenzi wa Daraja la Mwiyovozi katika barabara ya Nyakanazi Kibondo (km 50), inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi Bilioni 45.9 bila VAT. Mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi mahiri wa Rais, Dkt. John Magufuli.

Bi. Christina Richard mtaalamu wa kupima udongo katika maabara ya kampuni ya China Henan International Cooperation (CHICO), inayojenga barabara ya Nduta-Kibondo-Kabingo (km 62.5), mkoa wa Kigoma kwa gharama ya shilingi Bilioni 89.9.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho akishuka kutoka kwenye kivuko cha MV. Mwanza upande wa Kigongo (Wilaya ya Misungwi), baada ya kukamilisha ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi wa barabara kutoka Kasulu (kigoma) hadi Nyakanazi (Kagera).

WANAWAKE NBAA WASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0

 

Tarehe 8 Machi ya kila mwaka ni Siku ya wanawake duniani, ambapo siku hii inataka kukumbushia na kutafakari juu ya matokeo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi waliyofikia wanawake na msimamo wao imara katika ngazi ya kijamii kwa ujumla.

Katika kuadhimisha siku hiyo Wanawake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na  Wakaguzi wa Hesabu Tanzania(NBAA) wameshiriki maadhimisho hayo yaliyofanyika leo Mkoani Dar es Salaam. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Wanawake katika Uongozi, chachu kufikia Dunia yenye usawa” Akizungumza  kwenye maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Wanawake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na  Wakaguzi wa Hesabu Tanzania(NBAA, Irene Mutagaywa amewataka wanafunzi walioko mashuleni  kujikita katika kutengeneza ndoto zao kwa kusoma kwa bidii ili kuwa sehemu ya wanawake waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali hapo baadaye.Pia amesema mafanikio yoyote yanayoonekana nchini na duniani kote kwa kiasi kikubwa pia yamechagizwa na uwepo wa wanawake huku pia akimpongeza Rais Dk John Magufuli kwa kuendelea kuwaamini wanawake katika nafasi mbalimbali za kiuongozi kwenye Serikali yake.

Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura. Kilikuwa ni chama cha kisoshalisti cha Amerika kilichotangaza kuwa ni siku ya kwanza ya kitaifa ya wanawake, mwaka mmoja baadaye. Wazo la kuwa siku ya kimataifa lilianzishwa na mwanamke kwa jina la Clara Zetkin. Yeye alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark.



Maadhimisho Siku Ya Wanawake Duniani: Konyagi Yatengeneza Nembo Maalum Kutambua Jitihada, Weledi Na Ujasiri Wa Mwanamke.

$
0
0

 Katika jitihada za kutambua weledi, ujasiri na taaluma za Wanawake walio na mchango chanya kwenye jamii, kampuni ya Tanzania Distilleries Limited  kupitia kinywaji chake cha Konyagi imebadili muonekano wa nembo ya kinywaji hicho ikiwa na picha ya mwanamke katika nembo yake iliyozoeleka kuwa na alama ya mwanaume  shupavu aliyenyanyua mikono juu.

Chupa hizi maalum zina nembo yenye mwanamke aliyenyanyua mikono juu na ujumbe wa kuwatakia waTanzania heri ya siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila Tarehe 8 ya mwaka, mwezi wa 3.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa bidhaa hiyo Pamela Kikuli alisema: “Konyagi ni kinywaji kinachotumiwa na watu wa jinsia zote, lakini kwa upekee, imeamua kuunga mkono wanawake wa nguvu wenye ujasiri, weledi na uwezo wa kufanya vitu vingi ambavyo vimekua vikionekana kufanyika Zaidi na wanaume kuanzia ufundi wa magari hadi uendeshaji wa kampuni kubwa” amesema Pamela.

Pamela ameongeza kwamba Konyagi imekua ikifahamika kama kinywaji kinachopendwa Zaidi na wanaume laki ni kinywaji kinachofurahiwa na jinsia zote hivyo kumekua na umuhimu wa kipekee kutengeneza nembo maalum katika kipindi hiki cha Kusherekea Siku ya Wanawake Duniani ili kutambua ujasiri wao, uwezo wao wa kusimama kama wao pamoja na utaalamu wanaotoa katika kuchangia kuendeleza jamii inayozizunguka.

“Zaidi pia tumeamua kutambua wanawake 100 wenye ujasiri, weledi na mchango kwenye jamii ya Kitanzania na kuwazawadia vitu mbali mbali ikiwemo chupa hiyo yenye nembo mpya” amesema Kikuli.

Miongoni mwa wanawake hao ni waliotambuliwa michango yao na kupewa zawadi ni pamoja na Esther Maongezi (Mtangazaji wa TV na Redio Kipindi cha Michezo), Hellen Kazimoto (Muandaaji wa Matamasha ya Muziki) na Angellah Karashani (Mshauri wa Habari na Burudani ambao walipata fursa ya kuhudhuria kipindi cha Friday Night Live cha East Africa TV & Radio siku ya ijumaa kuzungumzia harakati zao, utaalamu wao pamoja na mchango wao katika jamii ili kuwa hamasisha Wanawake wenzao wenye ndoto waweze kuzitimiza kwa ujasiri bila uoga.

Wengine ni Leah Mollel (Muanzilishi wa Starshine TV), Mwanaidi Msuya (DJ Sweet Lady) – DJ na Rachel Pallangyo ambaye ni Refa wa Mpira wa Miguu katika ligi kuu ya Tanzania Bara (VPL). Wote walizungumzia tansia walizopo ambazo zimekua na historia ya kua na wanaume Zaidi lakini wao wamewaeza kuvunja fikra hiyo kwa kuwa vinara katika tasnia zao bila uoga.

Katika kipindi hicho cha Friday Night Live kinachodhaminiwa na Konyagi, mmoja ya waalikwa hawa waliotambuliwa na Konyagi, Angellah amesema “wanaume wamekua wakiongoza vitu vingi lakini Wanawake wana uzingatiaji zaidi katika utendaji hivyo basi wakipewa kazi hua tunaitenda vizuri Kuliko wanaume. Kinachotakiwa kufanywa sio sisi kupewa fursa bali kupishwa ili tuoneshe maajabu…” alimaliza Angellah

Hii ni mara ya kwanza kwa chapa ya Konyagi kutambua mchango mkubwa wa Wawanawake katika shughuli tofauti za kimaendeleo lakini haitokua ya mwisho kwani Konyagi ina mpango wa kuendelea kuwasilisha chapa hiyo kama kinywaji kinachofurahiwa na jinsia zote.

Mtaalamu wa masuala kidigitali (Digital Specialist) Bi Lilian Flavian (Katikati) akipokea zawadi ya kinywaji cha Konyagi yenye muonekano wa nembo ya mwanamke badala ya nembo iliyoezoeleka ya mwanaume shupavu ikiwa ni ishara ya  kutambua weledi, ujasiri na taaluma za Wanawake walio na mchango chanya kwenye jamii. Chupa hizo maalum zina nembo yenye mwanamke aliyenyanyua mikono juu na ujumbe wa kuwatakia waTanzania heri ya siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8  kila mwaka. Wanaomkabidhi zawadi ni wawakilishi kutoka  kampuni ya Tanzania Distilleries Limited  watengenezaji wa  kinywaji hicho.

wanawake wajasiriamali wajichangisha kununua kitanda cha kujifungulia na kukabidhi zahanati ya Likokoma wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara

$
0
0

 Na Mwaanidishi Wetu Mtwara

WANAWAKE wajasiriamali wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara wamechanga na kununua kitanda cha kujifungulia wanawake kwa ajili ya kusaidia zahanati ya Likokona ambayo inapokea wanawake 4 mpaka 6 kwa siku huku ikiwa na kitanda kimoja cha kujifungulia,

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi kitanda hicho, Mganga Mfawidhi wa Zahana hiyo Rehema Akili amesema zahanati hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1974 inapokea wanawake zaidi ya 300 kwa mwaka huku wanawake wengine wakilazimika kujifungulia sakafuni.

Amesema kwa mwaka 2018 zahanati hiyo ilipokea wanawake 254 na kwa mwaka 2019 walipokea 229 na huku 2020 na wakipokea wanawake 330.

Amesema zahanati hiyo inahudumia vijiji 4 na kwamba ina watumishi 3 wakimo wauguzi wawili pekee. Ameiomba serikali na wadau wengine kusaidia hiyo zahanati katika kuchangia vitanda na vifaa vingine ikiwemo ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama ambayo kwa sasa inajengwa na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.

“Changamoto zetu kubwa ni idadi ndogo ya watumishi ambapo tuna watumishi watatu wakiwemo wauguzi wawili tu, uhaba wa majengo wa kutolea huduma,” alisema Akili.

Aliomba zahanati hiyo kusaidiwa katika kujenga jengo la wazazi kuboresha huduma za akina mama na kuongeza watumishi ili tuweze kutoa huduma bora kwa jamii yetu.

Pia aliomba serikali kuwajengea kituo cha afya kama walivyoahidi kwenye ilani ya CCM kuwa watawajengea kituo cha afya ili kuboresha huduma za afya. Pia aliwashukuru akina mama hao kwa kuguswa kuchangia kitanda ambacho kwa sasa kitasaidia zahanati kupokea wanawake wanaojifungua.

Kwa upande wake, Mratibu wa kikundi cha akina mama wajasiriamali Eloisi Malisa amesema wanawake hao waliamua kuchagishana na kununua hicho kitanda ili kuunga mkono juhudi za Raisi John Magufuli katika kuboresha huduma za afya nchini.

“Tumeamua kuchangishana kama akina mama ili kuunga juhudi za Raisi ambazo anafanya haswa katika kuboresha miundombinu ya afya hususan majengo na sisi tukaona tusaidie katika kuchangia vifaa tiba kama kitanda kusaidia akina mama wa Likokona,” amesema.

Baadhi ya akina mama wajasiriamali walioguswa wakikabidhi kitanda walichonunua Kwa kuchanga pesa ili waweze kusaidia zahanati ya Likokona ambayo ilikuwa na kitanda kimoja toka ianzishwe 1974.

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MARIAM MWINYI AZINDUA MRADI WA AMKA MWANANGU SOMA KWA BIDII

$
0
0

 

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii wa Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) na Mshika Fedha wa Taasisi hiyo Bi, Valeria Rashid Haroub, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar jana usiku 7-3-2021.(Picha na Ikulu)

BAADHI ya Wabunge na Viongozi wa mbalimba na Wananchi wakifuatilia Uzinduzi wa Mradi wa Amka  Mwanangu Soma kwa Bidii, wakati Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuuzindua Mradi huo jana usiku 7-3-2021, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Risala ya Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) na Katibu wa Jumuiya hiyo Bi. Tatu Hussein Abdalla, wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar jana usiku 7-3-2021.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akihutubia na kuzindua Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii Ili Kutengeneza Kesho Yako, mradi huo wa Jumuiya ya Rafiki wa Mwanamke na Watoto Zanzibar.(RAWWAZA) uzinduzi huo umafanyika jana usiki 7-3-2021 katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar na (kushoto kwake) Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” Unguja Bi. Suzan Kunambi na Mwenyekiti wa Jumuiya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) Mhe. Tauhida Cassian Gallos.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Jahazi iliotolewa na Jumuiya ya RAWWAZA kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, akikabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii Ili Kutengeneza Kesho Yako, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akionesha Tunzo aliyokabidhiwa na Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar ( RAWWAZA) ya  ‘Kumpongeza Mama Mariam Mwinyi Kwa Kuungana Nasi Zidi ya Kuwapigania Wanawake na Watoto Zanzibar’ baada ya kukabidhiwa na Walezi wa Jumuiya hiyo Mhe. Taufik Salim Turky na Mhe Faharia Khamis Shomar. Wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii Ili Kutengeneza Kesho Yako.(Picha na Ikulu)

KIJANA  Suleiman Said Humoud akitowa ushuhuda  yaliomkuta wakati akitumia dawa za kulevya na athari alizozipata wakati wa matumizi hayo na kupata msaada kupitia Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar( RAWWAZA) na sasa ameachana na matumizi ya Dawa za Kulevya, akitowa maelezo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimsikiliza mmoja wa shuhuda wa matumizi ya Dawa za Kulevya Ndg. Suleiman Said Humoud akitowa maelezo wakati wa uzinduzi wa Mradii wa Jumuiya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, uliozinduliwa katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar na (kushoto kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na (kulia kwake) Mwenyekiti wa Taasisi ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) Mhe. Tauhida Cassian Gallos.(Picha na Ikulu)

 


TSC YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0

 
 Na Veronica Simba - TSC
 
Wafanyakazi wanawake wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Makao Makuu Dodoma, wameadhimisha siku ya wanawake duniani kwa ufanisi.

Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika leo, Machi 8, 2021 jijini Dodoma, Wafanyakazi hao wameshiriki katika maandamano yaliyoshirikisha Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi, yaliyoanzia Uwanja wa Jamhuri hadi katika Uwanja wa ‘Nyerere Square.’

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wanawake wa TSC, Mwenyekiti wao, Catherine Kamili ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwathamini wanawake na kuwapatia nafasi za uongozi katika nyanja mbalimbali nchini.

Aidha, amewataka wanawake wote nchini, hususani watumishi wa TSC, kuendelea kuchapa kazi kwa weledi na kujituma katika kuhakikisha, wanakuwa sehemu ya waleta maendeleo ya jamii na Taifa.

Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kitaifa, mwaka huu ni “Wanawake katika Uongozi, Chachu kufikia Dunia yenye Usawa.”

Wafanyakazi wanawake wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Makao Makuu Dodoma, wakishiriki katika maandamano wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, 2021.
 Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), wakiungana na wenzao kutoka Taasisi mbalimbali kucheza, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa ‘Nyerere Square’ jijini Dodoma, Machi 8, 2021.

DK NDUMBARO : TUNAWAKARIBISHA WAWEKEZAJI ZAIDI KATIKA SEKTA YA HOTELI ZA KULALA WATALII .

$
0
0

Na John Nditi, Morogoro

SERIKALI inawakaribisha wawekezaji zaidi katika  ujenzi wa  hoteli za  kitalii  na kutakazilizopo kuboresha huduma zake  kwa gharama nafuu ili kila Mtanzania aweze kutalii katika   hifadhi mbalimbali za Taifa nchini. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro  alitoa kauli hiyo wakati akifunga na mkutano wa siku nne uliomalizika  mjini Morogoro wa  wadau wa Utalii  kwa ajili ya kujadili kuhusu kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na shughuli za utalii nchini.

Wadau waliioshiriki kwenye mkutano huo wa siku nne ni pamoja na wa Uwindaji wa Kitalii, Wasafirishaji  Watalii, Waongozaji Watalii na Wakala wa Safari za Ndege , Watoa huduma za Malazi, Wadau wa Usafirishaji wa Anga na Meli.

Katika hitumisho ya mkutano huo Dk Ndumbaro ,alisema bado kuna hoteli za kutosha katika hifadhi zetu mbalimbali nchini  na kwamba Serikali inaendelea kukaribisha uwekezaji zaidi katika sekta ya hoteli  kwa ajili ya kutoshereza malazi ya idadi yoyote ya watalii .

“ Ukitembelea mbuga za Taifa unaweza kulala hoteli ya dola 9,000 kwa siku moja na pia unaweza kulala hoteli kwa Sh 30,000  huo ni uwezo wa mtu mwenyewe  tu ul;ale wapi , kwa hiyo hoteli zipo nyingi  za viwango tofauti ili kuhakikisha kwamba kila mtu anapata stahiki yake na ahdi kwenye Tent Camps watu wanalala” alisema Dk Ndumbaro.

Waziri Dk Ndumbaro, alisema;  “ Na ndiyo maana  Machi 5 , 2021  tulikuwa  hapa nawadau wote wa mahoteli na tumeongea mambo mengi ikiwa na kuboresha hudunma zao kwa gharama nafuu ili kila  Mtanzania aweze kutalii” alisema Dk Ndumbaro.

Dk Ndumbaro alirejea hotuba ya Rais Dk  John  Magufuli katika hotuba yake ya ufunguzi  wa Bunge la 12  la  Novemba 13,  2020  alisisitiza umuhimu wa kuendeleza sekta ya utalii nchini ili iweze kuchangia zaidi katika pato la Taifa.

Kwa mujibu wa Waziri wa Malisili na Utalii , katika hotuba hiyo, Rais alitoa dira ya kufikia lengo la watalii millioni tano  sambamba na kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za utalii kufikia Dola za Marekani bilioni sita  ifikapo mwaka 2025.

Waziri Dk Ndumbaro , alisema masuala ambayo pia, yamesisitizwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025, hususan katika ibara ya 67.

Hivyo  alisema kuwa Utalii ni sekta muhimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu ambayo inachangia zaidi ya asilimia 25 ya mauzo yote ya nje na asilimia 60 ya mapato yote yatokanayo na biashara za huduma.

Kwa upande wake Mdau wa Utalii wa muda mrefu  na mwanzilishi wa huduma za ya utalii wa Puto   ( Balloon Safaris) kupitia Serengeti  Balloon Safari , Jimmy Mkwawa , alisema katika mkutano na waziri wadau wa utalii wamewasilisha kwa maandishi na uchanagiaji kuhusu changamoto kubwa ya utitiri wa kodi na pia mawasilisho yaliyofanyika kwenye vikao mbalimbali kwa nyakati tofauti kushindwa kufabnyiwa kazi na kuwa ni kikwazo cha uwezakano wa kuongezeka kwa idadi ya wataalii nchini.

Waziri  wa Maliasili na Utalii  Dk Damas Ndumbaro ( kati kati )  akijadiliana jambo na  Mdau wa Utalii wa muda mrefu  na mwanzilishi wa huduma za ya utalii wa Puto   ( Balloon Safaris) kupitia Serengeti  Balloon Safari , Jimmy Mkwawa , ( kulia) mara baada ya Waziri huyo kufunga  mkutano wa siku nne wa  wadau wa Utalii  kwa ajili ya kujadili kuhusu kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na shughuli za utalii nchini iliofanyika mjini Morogoro.


Kaimu Kamishna wa Uhifadhi  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) , Mabula  Misungwi Nyanda , ( kulia mtari wa mbele) akifuatilia hotuba ya Waziri  wa Maliasili na Utalii  Dk Damas Ndumbaro ( hayupo pichani) ya ufungaji  mkutano wa siku nne wa  wadau wa Utalii  kwa ajili ya kujadili kuhusu kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na shughuli za utalii nchini iliofanyika mjini Morogoro.


Baadhi ya  Maofisa wa Jeshi la Uhifadhi  wa TANAPA wakitoka uumbini mara baada  Waziri wa Malisaili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro ( hayupo pichani) kufunga  mkutano wa siku nne wa  wadau wa Utalii  kwa ajili ya kujadili kuhusu kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na shughuli za utalii nchini iliofanyika mjini Morogoro.( Picha na John Nditi).

 

Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. David Silinde Aridhishwa na Utekelezaji wa Ujenzi wa Miradi ya Elimu Busega

$
0
0
Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. David Silinde amefanya ziara ya siku moja wilayani Busega. Katika ziara hiyo ameweza kukagua na kuridhishwa na ujenzi wa miradi ya elimu inayotekelezwa. Ameyasema hayo alipotembelea Shule ya Sekondari Antony Mtaka kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu katika shule hiyo.

Akiwa katika Shule hiyo, Silinde amekagua mradi wa ujenzi wa bwalo, maabara, vyumba viwili vya madarasa na ujenzi wa vyoo, ambapo Serikali imetoa jumla ya TZS Milioni 196.6 kwaajili ya ujenzi wa miradi katika Shule hiyo.

Mhe. Silinde ametaka kuwepo kwa usimamizi bora wa fedha zinazotolewa na Serikali ili kukamilisha miradi kama azma ya kufanikisha lengo la Serikali. “Nimeridhishwa na hali ya ujenzi wa miundombinu iliyofanyika katika Shule hii, sababu nimeona thamani ya fedha, nimeona matumizi bora ya fedha za serikali na pia nimeona ubora wa majengo, hii ni kwasababu ya usimamizi bora uliopo hapa” aliongeza Silinde.

Awali, akisoma taarifa fupi ya Shule hiyo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Antony Mtaka Bw. Joseph Kazimoto amesema ukamilikaji wa ujenzi wa miradi hiyo kutasaidia kuongeza ufanisi katika ufundishaji, kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na kupunguza utoro kwa wanafunzi. Hata hivyo Bw. Kazimoto ametaja changamoto za miundombinu muhimu zinazoikabili Shule hiyo ikiwemo upungufu wa madarasa, jengo la utawala na maktaba.

Kwa upande mwingine, Mhe. Silinde ameongea na Wanafunzi wa Shule hiyo na kuwataka kuweka bidii katika masomo, kwani Taifa linawategemea pia amewaeleza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea kutatua changamoto zote zinazoikabili sekta ya elimu nchini, ili kuweka mazingira bora kwenye Shule na Taasisi za elimu nchini.

Ziara ya Mhe. Silinde wilayani Busega ilihitimishwa katika Shule mpya ya Venance Mabeyo, inayojengwa kijiji cha Nyamikoma, kata ya Kabita. Akiwa katika Shule hiyo, amekagua na kuridhishwa na ujenzi unaoendelea na kutoa maagizo ya taratibu za awali kufanyika kwa haraka ikiwemo kuisajili Shule hiyo ili ianze rasmi kutumika.


TANZANIA IMEPIGA HATUA KATIKA KUPUNGUZA MALARIA

$
0
0

Na. Catherine Sungura,Dar es Salaam.

Tanzania imepiga hatua katika kupunguza ugonjwa wa Malaria licha ya baadhi ya mikoa kuwa na maambukizi ya juu ya ugonjwa huo na mikoa ya Arusha,Manyara, Njombe, Kilimanjaro na Iringa kuwa na maambukizi chini ya asilimia moja na mikoa mingine kuwa na maambukizi ya kati.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi wakati akifungua kikao kazi cha kwanza cha wataalamu wabobezi wa kudhibiti wadudu wadhurifu waenezao magonjwa tangu kuanzishwa kwa kitengo cha kudhibiti wadudu wadhurifu hapa nchini.

Dkt. Subi amesema kikosi hicho cha wataalum kinaandaa muongozo wa jinsi ya kukabiliana na  wadudu wadhurifu waenezao magonjwa akiwemo mbu.Lengo ikiwa ni kuishauri Wizara njia bora za kukabiliana na wadudu hao.

Alitaja njia hizo ni pamoja na  udhibiti wa mazingira kwa kuhakikisha mbu na wadudu wengine  wadhurifu hawapati sehemu ya kuzaliana na kuweza kusambaza magonjwa na masuala ya usafi  wa mazingira ikiwemo uboreshaji wa nyumba ili kuzuia wadudu wadhurifu  pamoja kuhakikisha watu wanalala kwenye vyandarua vyenye dawa.

Kwa upande wa matumizi ya viuatilifu Dkt. Subi alisema katika kudhibiti mbu alitolea mfano vipo viuatilifu na viuadudu vya kuuwa viluilui kwenye mazalia ya mbu, na amesisitiza kutumia viwanda vya ndani kwa kuwa taasisi taasisi za ndani ambazo zinafanya tafiti na kuonesha mafanikio makubwa ya idadi ya mbu kupungua pamoja mnyororo wa  maambukizi.

“Matumizi sahihi ya vyandarua ni muhimu sana katika kudhibiti Malaria, tunataka angalau zaidi asilimia 80 ya watanzania walalie vyandarua vilivyoweka viuatilifu vya muda mrefu ili kumpunguzia mbu umri wa kuishi na hivyo kupunguza uwezekano wa kusambaza vinmelea vya Malaria ikiwa ni pamoja na upuliziaji wa viuatilifu ukoko ndani ya nyumba”.Alisisitiza Dkt. Subi.

Kwa upande wa ugonjwa wa kichocho Dkt. Subi amesema kikosi hicho kitaangalia pia ni namna gani watadhibiti ugonjwa huo kwenye maeneo yenye majaruba mengi kama mikoa ya kanda ya ziwa na mikoa mingine, “Mbu wanaeneza pia Matende na Mabusha, Dengue, Chikungunya, Homa ya Manjano na magonjwa mengine yanayokuja kwa vipindi vya mvua kwa hiyo tutapambana kwa kumuangalia mwananchi kudhibiti magonjwa hayo “.

Aliongeza pia wapo Inzi weusi (Simulium) ambao wanaeneza ugonjwa wa Usubi hususan kwenye mikoa ya Mbeya (Tukuyu), Morogoro (Mahenge) na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Iringa hivyo kikosi hicho kitaangalia pia jinsi ya kudhibiti Inzi hao ili kuzuia maambukizi kuliko kuendelea tu kuwamezesha wananchi dawa kila mwaka .

Hata hivyo Dkt. Subi aliwasisitiza wataalam hao kuangalia ni namna gani wanaweza kutumia dawa za asili katika kufukuza mbu  kwa kutumia mbinu za kisasa kwa kumia dawa hizo za asili  katika kufukuza na kua mbu na wadudu wengine wadhurifu waenezao magonjwa.

Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi

TAMKO LA TAKUKURU SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2021

$
0
0

 


SIKU YA KIMATAIFA YAWANAWAKE – 2021

 Siku ya Kimataifa ya Wanawake (International Women’s Day) huadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka. Siku hii ambayo imekuwa ikiadhimishwa na nchi za Urusi kuanzia mwaka 1917 ilitangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE kuanzia mwaka 1975.  Siku hii inalenga kutambua mafanikio ya mwanamke bila kuangalia rangi yake, dini, kabila au siasa ikiwa ni pamoja na kutafakari maendeleo ya mwanamke na namna ya kuendelea kujikwamua katika matatizo na changamoto zinazokuwa vikwazo vya yeye kujitegemea kifikra na kiuchumi.

 Kwa kutambua umuhimu wa siku hii pamoja na umuhimu wa mchango wa mwanamke katika mapambano dhidi ya rushwa, Machi 7, 2019, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ilitoa TAMKO kwamba inaunga mkono juhudi zinazoendelea duniani kote za kuhakikisha wanawake wanalindwa na inapinga unyanyasaji na udhalilishaji wa aina yoyote ile unaofanywa dhidi ya wanawake ikiwemo kulazimishwa kutoa RUSHWA YA NGONO. Hii ni hatua muhimu kwa TAKUKURU na JAMII katika harakati za KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA.

 RUSHWA YA NGONO ni kitendo cha mtu kutumia madaraka au dhamana aliyopewa kuomba au kulazimisha tendo au upendeleo wa kingono kutoka kwa mtu anayetaka kumhudumia kikazi. Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007 imetamka kosa hili chini ya kifungu cha 25 ambapo kwa tafsiri isiyo rasmi kifungu hiki kinasema:

 “Mtu yeyote ambaye kwa kutumia nafasi yake au mamlaka yake katika kutekeleza majukumu yake anadai au analazimisha upendeleo wa kingono au upendeleo mwingine wowote kama kigezo cha kutoa ajira, kupandisha cheo, kutoa haki au upendeleo wowote unaotambulika kisheria atakuwa ametenda kosa.”

 Tofauti na aina nyingine za rushwa zinazotumia ubadilishaji wa vitu yakinifu au ridhaa ya mtoa rushwa na mpokea rushwa, hii ni rushwa inayotokana na tabia ya mdai rushwa kutumia mamlaka yake kushawishi au kushinikiza ngono badala ya vitu yakinifu.

 Pamoja na TAMKO tulilolitoa, kwa mujibu wa kifungu cha 7 (a) na (c) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007, TAKUKURU inao wajibu wa kufanya uchambuzi na kupitia taratibu za mamlaka ya umma na binafsi kwa nia ya kuiwezesha kubaini mianya ya vitendo vya rushwa, na kushauri namna bora ya kuziba mianya iliyobainika, na kushirikiana na wadau kupambana na rushwa.

 Hivyo basi, kwa kutambua kuwa Vyuo Vikuu ni viwanda vya kuandaa wataalamu wanaotarajiwa kuingia kwenye fani mbalimbali za utoaji wa huduma, uzalishaji pamoja na kuwa walezi wa familia, TAKUKURU ilifanya utafiti wa kina katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwezi Februari 2020. Lengo kuu la utafiti wetu lilikuwa ni kupata taarifa za kisayansi zitakazosaidia kukabiliana na kero ya rushwa ya ngono katika Taasisi za Elimu ya juu nchini.

 

MATOKEO YA UTAFITI:

Matokeo ya utafiti yalibainisha mambo yafuatayo:

Mosi, tatizo la rushwa ya ngono kwenye vyuo tafitiwa lipo; wanafunzi asilimia 58 na watumishi asilimia 69 walieleza kuwepo kwa matukio ya vitendo vya rushwa ya ngono;

 Pili, utafiti ulibaini sababu za kuwepo kwa rushwa ya ngono katika taasisi tafitiwa ni kutokana na mifumo dhaifu ya kudhibiti matumizi mabaya ya mamlaka; mifumo dhaifu ya kusimamia uwajibikaji; mfumo dhaifu wa ajira hasa ajira za wahadhiri; kuwa na ufinyu wa huduma muhimu kama hostel na mikopo ya elimu; kuongezeka kwa wanafunzi pamoja na mmomonyoko wa maadili kwa ujumla;

 

Tatu, utafiti ulibaini mbinu zinazotumika kushawishi rushwa ya ngono ambazo ni kutoa alama za chini kwenye mitihani, vitisho vya kutofaulu kwa wanafunzi, kutoa ahadi kama kumpatia ajira, cheo, chumba chuoni, nafasi ya uongozi, kuongezea alama za ufaulu au kusaidia kupata ufadhili wa masomo, kuchelewesha utoaji wa huduma na wahadhiri kuwaita wanafunzi kwenye mazingira yasiyo rasmi kwa ajili ya kukagua kazi zao;

 

Baada ya kufanya utafiti huu TAKUKURU iliitisha kikao kazi cha wadau cha kujadili matokeo ya utafiti na kuweka mikakati ya kuidhibiti kero hii. Vilevile, tulitoa mapendekezo kwa Serikali pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu kuhusu namna ya kudhibiti kero hii katika eneo hili.

 

Pamoja na utafiti huu, kwa kutambua athari za rushwa ya ngono kwa wahanga, jamii na hata uchumi, TAKUKURU kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) Oktoba 2019 tulizindua kampeni iitwayo: VUNJA UKIMYA KATAA RUSHWA YA NGONO.

 

Kampeni hiiinafanyika katika mikoa yote 28 ya TAKUKURUna inalengakuelimisha na kuuhamasisha zaidi umma kuwa na ujasiri wa kutoa taarifa na kupinga vitendo vya rushwa ya ngono nchini. Tunashukuru kwamba mwitikio ni mkubwa na imekuwa ni ajenda inayozungumziwa kwa wingi katika jamii.

 WITO WANGU KWA JAMII ni kwamba TAKUKURU tuko imara na tumejipanga vizuri katika kushughulikia kero hii.

·        Tunaendelea kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa baada ya kufanya utafiti katika vyuo vikuu.

 ·        Tunaendelea kutoa elimu dhidi ya rushwa kupitia vipindi vya redio, kufanya semina na pia kupitia vipindi mbalimbali vya televisheni.

 ·        Tumeweka utaratibu maalum wa kushughulikia malalamiko ya kero ya Rushwa ya Ngono katika kila mkoa na kila Wilaya hapa nchini.

 ·        Tumepanua wigo wa mawasiliano yetu na wananchi ambapo sasa TAKUKURU imeanzisha TAKUKURU TV na pia imefungua kurasa za Tweeter: TAKUKURU.TZ; Instagram: takukuru.tz na Facebook: Takukuru Tz.

 Ninawasihi wananchi kutumia fursa hizi kuwafichua wadhalimu wanaodai RUSHWA YA NGONO na rushwa nyingine ili kwa ushirikiano huo tukomeshe vitendo hivyo.

 Kwa maelezo hayo na kwa kuadhimisha SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE kwa mwaka 2021, yenye Kauli Mbiu isemayo ‘WANAWAKE KATIKA UONGOZI: CHACHU KUFIKIA DUNIA YENYE USAWA’ Mkurugenzi Mkuu na watumishi wote wa TAKUKURU tunasema: ‘BADILI FIKRA, RUSHWA YA NGONO HAIKUBALIKI - TUWAUMBUE’.

 

 

(J.J. Mbungo, ndc)

Brigedia Jenerali

MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU

MACHI 8, 2021

Viewing all 120255 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>