Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 120152 articles
Browse latest View live

MADIWANI LINDI WAWASHA MOTO KWA MKUU WA MKOA WA LINDI KUHUSIANA NA KUFUNGA OFISI YA MIPANGOMIJI BILA MADIWANI KUFAHAMISHWA

$
0
0
Madiwani 14 kati ya 25 wa Manispaa ya Lindi wamejiorodhesha na kuandika barua kwa Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo kumtaka kuitisha kikao maalum cha Baraza la madiwani ili kupata taarifa mbalimbali ikiwemo hatua ya Mkuu wa Mkoa kufunga Ofisi ya Mipango Miji kwa zaidi ya mwezi mmojapamoja na kuanza kwa mauzo ya Viwanja huku madiwani wakiwa hawana taarifa.

Hatua hiyo ya madiwani hao akiwemo Mbunge wa jimbo la Lindi Mjini Bw Salum Barwany imekuja kufuatia kutoshirikishwa kwa madiwani kuhusiana mambo mbalimbali yanayotekelezwa hususan Ulipaji wa Fidia na mauzo ya viwanja chini ya mpango wa UTT pamoja na hatma ya mgogoro wa wananchi wenye maeneo hayo yaliyoanza kuuzwa.

Akiongea na waandishi wa Habari,Diwani wa kata ya Nachingwea ,Omary Chitanda alieleza kushangazwa na hatua ya mkuu wa mkoa kufunga ofisi ya Idara ya Mipango Miji kwa zaidi ya mwezi mmoja kinyume na taratibu za ofisi za serikali.

“Sisi ndio Halmashauri ila imetushangaza sana Kitendo cha mkuu wa mkoa kufunga ofisi ya mipango miji na kuunda tume ambayo ilimaliza kazi ila sisi madiwani tumeomba taarifa ya Tume hiyo atupewi akaunda tume tena kuhusiana na mgogoro wa wananchi na manispaa kuhusiana na ardhi iliyochukuliwa katika mpango wa UTT Pia madiwani atupewi taarifa Je sisi kweli ni wawakilishi wa wananchi tunafichwa hivi?alielezaChitanda Pamoja na hilo Madiwani hao walieleza kusikitishwa na kutofahamishwa na hatma ya Vibanda 8 vilivyojengwa katika eneo la kituo cha mabasi na baadhi ya madiwani kinyume na utaratibu na kuzuiwa na manispaa hiyo kwa muda mrefu.

Jitihada za kumpata mkuu wa mkoa Lindi,Ludovick Mwananzila ana kwa ana hazikuzaa matunda na kufanikiwa kumpata kwa njia ya Simu ambapo alikiri na kueleza kuwa tayari ameshatoa maelekezo kwa Meya na Mkurugenzi wa manispaa kwa utekelezaji na pia Taarifa ya Tume zake amewasilisha Tamisemi na kwa kwa Waziri Mkuu.

Hivi karibuni Ofisi ya Manispaa ya Lindi imeanza kutangaza kupitia vyombo vya habari kuhusiana na Uuzaji wa Viwanja katika maeneo ya mmongo,Mabano na Mitwero chini ya mpango uliofadhiliwa na UTT Madiwani waliojiorodhesha na barua yao Ni kama inavyosomeka na sahihi zao
Baadhi ya madiwani waliokutana na waandishi wa Habari kutoa tamko la kumtaka Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Lindi kuitisha kikao maalum ndani ya siku 14 ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya madai ya madiwani.
Meya wa Manispaa ya Lindi
Barua iliyoandikwa na Madiwani hao kwenda kwa Meya.

Bereavement of Late Mama Martha Lubuva

$
0
0
The Chairman of National Electoral Commission (NEC), the Retired Judge Damian Z. Lubuva announces the death of her beloved wife Mrs. Martha Peter Lubuva who passed away on 18th January 2014 at New Delhi Apollo Hospital in India.

Relatives and friends are meeting at his Residence, Oysterbay, Bongoyo Street, House No.6.

There will be a Holy Mass at St. Peters Catholic Church on Tuesday, 21st Jan 2013 from 2pm and she will be laid at rest at Kinondoni Cemetery.

May her Soul Rest in Eternal Peace.

MWENGE WA JUMUIYA YA MADOLA WATEMBELEA MUHIMBILI

$
0
0
Mwenge wa Jumuiya ya Madola (Queens Baton Relay) leo umetembelea
Hospitali ya Taifa Muhimbili jumapili ukiongozwa na Mheshimiwa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Dianna Melrose pamoja na mshindi wa mbio za kilomita 1500 za jumuiya ya madola Bw. Filbert Bayi.

Mwenge huu umetembelea Hospitalini hapa kwa nia kubwa ya
Kukutana na watoto wanaougua saratani mbalimbali ili kuwapa
matumaini ya kuishi na kwamba jamii inawanathamini. Watoto hawa
wamepata fursa ya kuushika mwenge huu na kupiga picha kama
kumbukumbu muhimu katika maisha yao fuatulia katika picha jinsi
watoto walivyofurahia mwenge huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela akipokea mwenge kutoka kwa kiongozi  wa michezo ya Olimpiki kutoka Kenya Bw. Kipchoge Keino
 Dkt. Njelekela akimkabidhi mwenge mtoto anayeugua ugonjwa wa saratani.

Mwandishi na Mtangazaji wa BBC,Komla Dumor afariki dunia

$
0
0
Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa BBC,Komla Dumor amefariki dunia ghafla nyumbani kwake kutokana na mshtuko wa moyo. Alikuwa na miaka 41 alipopata mauti yake.Komla Dumor ameelezewa kuwa miongoni mwa waandishi shupavu barani Afrika. 

Rais wa Ghana, John Dramani Mahama amemtaja marehemu kama zawadi ya Ghana ulimwenguni na kuongezea kuwa Ghana imempoteza mmoja wa wajumbe wake. 

Komla hivi karibuni alikuwa anaongoza kipindi cha Runinga kinachozungumzia maswala ya Afrika baada ya kufanya kazi katika radio mmoja nchini Ghana na vilevile radio ya BBC. Muhariri wa habari za ulimwengu Andrew Whitehead amemtaja kuwa mwadishi shupavu aliyekuwa na uhusiano mzuri na wasikilizaji.

CHANZO: BBC SWAHILI

SHIWATA yakabidhi vyeti 1,000 kwa wasanii

$
0
0
Na Mwandishi wetu

 MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umetoa vyeti kwa wasanii 1,000 waliofanya kazi zao vizuri katika kipindi cha mwaka 2013-2014 katika kongamano lililofanyika ukumbi wa Lamada, Ilala Dar es Salaam.

Katika kongamano hilo lililohudhuriwa na wasanii,wanamichezo,wanahabari na vijana zaidi ya 1,500 mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete aliyewakilishwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana utamaduni na Michezo, Amos Makala aliwaasa wasanii watumie kipato chao kujiandaa kwa maisha ya baadaye baadaye.

Makala aliwataka wasanii kujiunga na Shiwata na kujenga nyumba zao za pamoja kwa gharama nafuu katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga ambako mpaka sasa zimejenga nyumba 55 kati ya hizo 38 zimekabidhiwa wenyewe na nyingine zinaendelea kujengwa ambazo zitakabidhiwa wenyewe Machi mwaka huu.

Katika risala ya Shiwata kwa mgeni rasmi iliyosomwa na Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Juma Ikangaa ambaye pia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Tanzania (TAA),SHIWATA imetoa ekari 5 kwa ajili ya Rais Kikwete ajenge  nyumba katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga na ekari 5 nyinguine kwaq ajili ya kilimo katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga.

Pia risala hiyo imemuomba Rais Kikwete asaidie kurudisha vituo vya burudani, viwanja vya michezo, na wapewe sehemu ya bustani ya mnazi Mmoja kwa ajili ya maonesho ya wazi, ujenzi wa makao makuu ya Mtandao na ununuzi wa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kazi zao.

Pia SHIWATA iliomba kuwepo mwakilishi wa wasanii katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na taasisi zote za Umma kama Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Sheria yHaki Miliki iangaliwe upya kwani ina upungufu.

Katika kongamano hilo SHIWATA imezindua Mpango wake wa umoja ambao utawasaidia wasanii kujitegemea wenyewe katika kazi mbalimbali badala ya kusubiri misaada kutoka kwa wafadhili kwa kutoa misaada kwa wasanii wachanga kurekoodi miziki yao,kurekodi filamu, na kupata michezo.

Taarifa ya SHIWATA iliyotolewa na Mwenyekiti wake, Cassim Taalib alisema mpango huo utawafaidisha wasanii  kupata fedha za matibabu, mazishi pamoja na kununua na kusambaza kazi za wasanii.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga mstaafu, Henry Clemence aliyetoa mada kuhusu maadili mema na juzalendo, aliwataka wasanii kuwa na tabia nzuri wanapokuwa ndani na nje ya nchi kwa mavazi ya heshima na mwenendo bora.

Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alisema athari za matumizi ya dawa za kulevya zinaiaibisha Tanzania inayofahamika kuwa kisima cha wananchi waadilifu kwa wanavyotumiwa wasanii na wanamichezo kusaifirisha na kutumia dawa za kulevya.

Mgeni rasmi Naibu Waziri Makala aliyemwakilisha Rais Kikwete aliwaasa wanamichezo kutumia fedha wanazozipata katika kazi zao vizuri ili ziwasaidie wanapostaafu na wanapozeeka na kuwataka wajiunge  na SHIWATA ili wapate nyumba za gharama nafuu katika kijiji chao cha Mwanzega, Mkuranga.

COMMUNIQUE OF THE 12th MEETING OF SECTORAL COUNCIL ON FOREIGN POLICY COORDINATION OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY

Praise Power Radio interview with Vincent Mughwai's on the importance of solar energy use

wanawake nchini watakiwa kujiamini sambamba na kuwalea watoto wao katika maadili mema

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya sherehe za Maulid kwa
wanawake wa mkoa wa Dar es salaam, kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume
Muhammad (S.W.A), Aisha Sururu (wa pili kushoto), akifuatilia jambo
katika sherehe hizo, zilizoshirikisha na wanawake kutoka mkoa wa Pwani.



Kikundi cha kaswida kutoka madrasa ya Al Itiswam, Sokota  
Temeke Dar es Salaam, ikisherehesha katika sherehe hizo.

 Mtoa mada ihusuyo elimu ya kiislam na mwanamke, Atwiya Adam Ahmad,  akieleza ujumbe muhimu kuhusu kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), na  umuhimu wa kuadhimisha siku hiyo.

Kikundi cha kaswida kutoka madrasa ya Al Itiswam, Sokota  
Temeke Dar es Salaam, ikisherehesha katika sherehe hizo.
========   =======  =======
WANAWAKE nchini wametakiwa kujiamini sambamba na kuwalea watoto katika  maadili mema ili kuzuia mmomonyoko wa maadili ambao ni chanzo cha  uhalifu nchini.


Mwanaharakati wa Kiislam na diwani wa viti maalum kwa tiketi ya Chama
cha Mapinduzi Ilala,Aisha Sururu aliyasema hayo jijini Dar es salaam
wakati wa maadhimisho ya Maulid ya kuzalima Mtume, Muhammad(S.A.W),  yaliyoandaliwa na wanawake wa mkoa huo.



"Kinamama na jamii nzima ya Kiislam sote tunapaswa tuwe wakuzi wazuri
wa watoto wetu ilu kuzuia mmomonyoko wa maadili" alisema.


Alisema wao kama wanawake wameamua kusherehekea mazazi ya Mtume kwa  kuwa kabla ya kuzaliwa mtume wanawake walidhalilishwa sana, lakini kwa  kipindi chake wanawake walipewa nafasi kubwa.


"Zamani wanawake tulinyanyaswa na kudhalilishwa sana ila enzi ya Mtume
Mohamad ndo tukapewa nafasi. Hivyo wanawanke tuko mbele toka enzi ya
mtume" alisema.



Aliwataka wanawake kujiamini kwamba wanaweza katika mikakati yoyote ya  maendeleo kwa kuwa wanatambulika tangu enzi za mtume.



Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa baraza hilo, Mayasa Sadala
aliitaka jamii kufuata taratibu za mtume alizoziacha ikiwemo stara ili
kuendelea kuidumisha amani na utulivu.

MAHAFALI YA TANO YA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA YAFANA SANA

$
0
0
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Elimu, Mh. Philipo Mulugo akihutubia wahitimu na wageni waalikwa kwenye Mahafali ya Tano ya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ufundi Arusha, Bw. Abraham Nyanda akitoa Hotuba wakati wa Mahafali.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi, Eng. Dkt. Richard Masika akitoa Hotuba wakati wa Mahafali ya Tano ya Chuo.
Wafunzi bora Kumi (10) wakiwa wameshikilia Mfano wa Hundi ya Sh. Mil 10 wakiwa katika picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mh. Philipo Mulugo pamoja na baadhi ya Wageni Waalikwa. Fedha hizi ni Ahadi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Peter Pinda (MB) kwenye mahali ya Nne na Tano.

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAKAMILISHA ZOEZI LA KUWANOA WAKUFUNZI WA UTAFITI WA WATU WENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI

$
0
0
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa sekta ya Elimu, Wariambora Nkya, (wapili kutoka kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi mwaka 2014, mara baada ya kufunga mafunzi hayo, jana kwenye ukumbi wa Edema, Mjini Morogoro ( wapili kutoka kushoto) ni Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo.
Wakufunzi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa sekta ya Elimu Wariambora Nkya (hayupo kwenye picha) aliyefunga mafunzo ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi mwaka 2014 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendela.( Picha zote na John Nditi).

Na Veronica kazimoto – Morogoro

 Viongozi wote wa Serikali katika ngazi zote kwa ujumla wameombwa kutoa ushirikiano katika kuhamasisha na kuelimisha umma umuhimu wa kushirikiana na Wadadisi pamoja na Wasimamizi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi unaotarajia kuanza rasmi mwezi Februari na kumalizika Disemba mwaka 2014.

Hayo yamesemwa jana na Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Morogoro Wariambora Nkya wakati akifunga Mafunzo ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Edema mkoani Morogoro.

Nkya amefafanua kuwa ni muhimu viongozi wote wa Serikali kutoa ushirikiano kwa wadadisi na wasimamizi kwani utafiti huo ni muhimu katika kuboresha sera na program mbalimbali za kukuza ajira, kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama vile Malengo ya Milenia, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2015 na Malengo ya MKUKUTA na MKUZA.

"Nitoe wito kwa viongozi wote wa Serikali kutoa ushirikiano kwa Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 ili waweze kutekeleza majukumu yao kama ilivyopangwa", amesema Nkya.

Wakati huo huo Katibu Tawala Nkya amewaomba Wananchi kutoa ushirikiano wa kujibu maswali na kutoa taarifa sahihi wakati watafiti watakapopita katika makazi yao kukusanya taarifa za soko la ajira katika ngazi ya Kaya.

"Napenda kuwahakikishia Wananchi kwamba shughuli zao za kiuchumi na kijamii hazitasimamishwa na zoezi la Utafiti huu kwa kuwa Wadadisi watakusanya takwimu za Utafiti huu wakati shughuli zingine zikiedelea kama kawaida", amesisitiza Nkya.

Wariambora Nkya ameyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera na mafunzo hayo ya wiki mbili yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu yamemalizika ambapo jumla ya Wakufunzi 60 kutoka mikoa mbalimbali nchini walihudhulia mafunzo hayo.

JAHAZI YATIKISA KWA MUZIKI MKALI WA TAARAB DAR LIVE

$
0
0
WAPENZI wa muziki usiku wa kuamkia leo waliburudika kwa mapigo ya bendi ya taarab ya Jahazi katika onyesho la nguvu la kwanza kwa mwaka 2014 ndani ya uwanja wa Taifa wa Burudani Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
 Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki waliofurika Dar Live.
 Mzee Yusuf na wanenguaji wake kazini.

shamra shamra za kuwakaribisha Wanafunzi wapya wa Vyuo vya Uandishi wa Habari DACICOSTUA

$
0
0
Mchezaji wa Timu za Dacico Pooltable, Yohana Mathius, akijaribu kulenga shimo wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlimani Profesional Pooltable katika hafla ya Sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Dar es Salaam City College na Mlimani Profesional(School Bush) iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Dar es Salaam City College Kibamba jijini Dar es Salaam Jana.
Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala Dar es Salaam City College, wakati wa wakati wa kutafuta washindi wa Urembo Miss & Mr. Dacico kwenye Hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Vyuo vya DACICO na Mlimani Profesional, iliyofanyika Makao makuu ya Chuo cha DACICO kibamba Chama jana na kushirikisha michezo mbali mbali ikiwamo Soka, Pooltable, kuimba, kucheza muziki, kuogelea, Urembo Mr. & Miss New Intake DACICO na mashindano ya kujibu Mada(Debate).
Wachezaji wa Timu za Dacico Fc, kiungo Machejo Dula (nyekundu) na mlinzi wa timu ya Mlimani Profesional Fc. Masanga Mkama wakiwania mpira wakati wa mchezo wa kirafiki katika hafla ya Sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Dar es Salaam City College na Mlimani Profesional(School Bush) iliyofanyika kwenye Viwanja vya Kibamba Chama, jijini Dar es Salaam Jana. hadi mwisho wa mchezo Dacico iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

TANZANIA YAOMBOLEZA KIFO CHA MWANDISHI WA BBC KOMLA DUMOR

MGOGORO WA SUDAN YA KUSINI UNATISHA - BAN KI MOON

$
0
0
Wawakilishi wa Kudumu kutoka nchi 193 wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon wakati alipolizungumza Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa. Alitumia fursa hiyo, kuainisha vipaumbele vyake vya mwaka 2014, mafanikio na changamoto zinazoukabili Umoja wa Mataifa ikiwamo migogoro inayoendelea huko Sudan ya Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati na kwingineko Duniani. Akatahadharisha kwamba kama Jumuiya ya Kimataifa haitakuwa makini kuna hatari kubwa ya kutokea mauaji makubwa ya raia kama ambavyo imeshawahi kutokea huko nyuma.

MERCEDES BENZ ML 320, MODEL FOR SALE

$
0
0
 MERCEDES BENZ ML 320, MODEL 1999
 IMPORTED FROM UK, HAS BEEN IN TANZANIA SINCE 2008. Duty paid.
Automatic Gear, Petrol Engine, Colour- Blue-Black, meticulous running Condition, great value for money, 6 CD Changer, Leather seats, 4x4,,  Air condition, Mileage -93,384 miles,
PRICE NEGOTIABLE,  20,000,000.  (Or nearest offer)


MAMIA YA WAMZIKA DEUSDEDIT MTAMBALIKE

$
0
0
Jaji Mstaafu Mark Bomani,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Mh.Stephen Wassira ni miongoni mwa viongozi mbali mbali walioshiriki mazishi ya kada maarufu ambaye pia alishawahi kuwa Mkuu wa Wilaya katika Wilaya mbalimbali nchini.
Mama Anna Mkapa,Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini Elizabeth Minde wakiwa miongoni mwa mamia ya Watanzania waliojitokeza kumzika kada wa siku nyingi Deusdedit Mtambalike.
Mke wa Marehemu Deusdedit Mtambalike akiweka shada la maua juu ya kaburi .
Watoto wa marehemu wakiweka shada la Maua kwenye kaburi la baba ya mpendwa Marehemu Deusdedit Mtambalike aliyefariki dunia tarehe 15 Januari 2014 nchini Afrika ya Kusini.

hepi besdei ya kuzaliwa mbunifu wa mitindo ally remtullah

$
0
0
Keki ya besdei ya kuzaliwa  mbunifu wa mitindo maarufu wa Tanzania Ally Rhemtullah amnbayo  ni spesho kwa ajili yake
Hapa Ally akipata ukodak na marafiki zake kwenye besdei  hiyo, kivutio kikubwa katika birthday hii ni cake ambayo ilikuwa ya aina yake yenye mfano wa mwili wa binadamu. Hii ni kuonyesha kuwa yeye ni mwanamitindo wa nguo eeeh!! mambo mengine mwachie baba na mama.

TEACH ME BY REN AND ITIKA Feat J'COB.RECORDED AT FLEXIBLE MUSIC

NEWS ALERT: Katibu Mkuu Kiongozi aongelea mapendekezo ya wajumbe wa bunge la katiba, mabadiliko katika Baraza la Mawaziri 2014

BARAZA LA MAWAZIRI LATANGAZWA WAKATI DR.MAGUFULI AKIKAGUA DARAJA LA KIGAMBONI

$
0
0
Nimeshangaa hata kutoamini macho yangu kipindi tupo twasikiliza redio kutangazwa baraza la Mawaziri , Dkt John Pombe Magufuli alikuwa hapa kwenye Ujenzi wa daraja la Kigamboni na tena akiwa peke yake kavaa casual alikuwa ana-drive Gari lake mwenyewe. Watu wamecheka na kufurahi kwa vile kaondoka pale kwenda kukagua eneo lenye utata wa kupisha Ujenzi. inaonekana  alikuewa hata hajui kinachoendelea Ikulu!
Mdau
Viewing all 120152 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>