Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 120208 articles
Browse latest View live

MTENDAJI MKUU TEMESA AKAGUA VIVUKO NGARA KAGERA

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle aliyevaa suti akizungumza na wakazi wa kata ya Kibimba Ngara vijijini wakati alipotembelea eneo hilo kuangalia uwezekano wa kupeleka kivuko, kushoto kwake ni Mbunge wa jimbo la Ngara mkoani
Kagera Mhe. Alex Gashaza aliyevaa miwani.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akikagua kivuko cha MV. Kyanyabasa kinachotoa huduma katika mto Kyanyabsa mkoani Kagera kushoto ni Meneja wa TEMESA Mkoa wa Kagera Mhandisi Zephrine Bahyona.



Mbunge wa jimbo la Ngara mkoani Kagera Mhe. Alex Gashaza kulia akijadiliana jambo na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Japhet Maselle wakati wakisubiri kuvuka katika kivuko cha MV. Ruvuvu kinachotoa huduma katika mto Ruvubu Wilaya ya Ngara mkoani Kagera. Kushoto ni meneja wa TEMESA Kagera Mhandisi Zephrine Bahyona.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wa pili kushoto, meneja wa TEMESA kagera Mhandisi Zephrine Bahyona mbele na Mbunge wa jimbo la Ngara mkoani Kagera Mhe. Alex Gashaza wa tatu kutoka kushoto wakikagua kivuko cha Rusumo.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)

SERIKALI YAHAMISHA MNARA WA MAWASILIANO KUMALIZA MGOGORO

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akiielekeza kampuni ya Vodacom kuhamisha mnara na ujengwe eneo la shule ili kuepusha mgogoro na mmiliki wa eneo ulipojengwa mnara huo wakati wa ziara yake kwenye mnara huo, kijiji cha Bukuku, kata ya Rufita wilayani Nyang’hwale, Geita.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akipata maelezo ya mgogoro wa mnara kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji cha Bukuku kilichopo kata ya Kafita, Nyang’hwale mkoani Geita, Eunice Gombanila wakati wa ziara yake kwenye eneo ulipojengwa mnara huo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Hamimu Guyama akitoa taarifa ya mgogoro wamnara wa Kata ya Kafita kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) wakati wa ziara yake wilayani humo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano. Wa kwanza kushoto ni mbunge wa jimbo hilo, Houssein Amir.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto)akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Hamimu Guyama kitabu cha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote chenye orodha ya minara iliyojengwa na Serikali wilayani humo wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano.
Mhandisi wa Kampuni ya Vodacom, Benedict Marwa, akimshukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) kwa niaba ya Serikali kwa kuielekeza kuhamisha mnara wa kata ya Kafita ili kuepusha mgogoro na mmiliki wa eneo wakati wa ziaa yake wilayani Nyang’hwale, Geita.



******************************



Na Prisca Ulomi, Nyang’hwale, Geita

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ameielekeza kampuni ya simu ya Vodacom kuhamisha mnara wake uliopo kijijii cha Bukuku, Kata ya Kafita wilayani Nyang’hwale mkoani Geita ili kumaliza mgororo uliopo baina ya Serikali na mwananhi anayemiliki eneo ulipojengwa mnara huo na kuujenga kwenye eneo la shule ya Msingi kulumbai iliyopo karibu na mnara huo ili wananchi wa kata hiyo waendelee kupata za mawasiliano.

Nditiye amtoa maelekezo hayo alipofika kwenye eneo la kijiji cha Bukuku ulipojengwa mnara huo wakati wa ziara yake wilayani Nyang’hwale ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwa wananchi na kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Hamim Guyama kuwa mmiliki wa eneo hilo Bi. Rukia Kashokelo na mme wake Clement Fungameza amekataa kusaini mkataba wa Vodacom na ameridhia mnara huo ung’olewe.

“Mnara huu kwa huyu mama uhame tu kwa kuwa upo kwenye jiwe na anataka alipwe shilingi mioni kumi kwa mwaka na anakosesha mawasiliano, amegoma kupokea shilingi milioni mbili na laki nne kwa mwaka na eneo hili kuna migodi mitatu na mapato ya takribani bilioni 20 kwa mwaka na ni eneo linalohitaji mawasiliano kwa uchumi na ulinzi na usalama wa kata ya Kafita,” amesema Guyama.

Guyama amefafanua kuwa mmiliki wa eneo amefanya jitihada za kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ili kuhakikisha kuwa wanapata malipo hayo kwa kukodisha eneo lao ulipojengwa mnara na kukataa kusaini mkataba na Vodacom wa malipo ya awali waliyokubaliana.

Nditiye ameipata kampuni ya simu ya Vodacom kuhakikisha kuwa inahamisha mnara huo ndani ya mwezi mmoja na amepiga marufuku kwa kampuni za simu zinazojenga minara kwa kutumia ruzuku ya Serikali wanayopewa kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kujenga mnara kwenye eneo la mtu binafsi ili kuepusha migogoro kwa kuwa Serikali haiko tayari kuingia migogoro na wananhi wake bali minara ijenge kwenye maeneo yanayomilikiwa na Serikali ya kijiji, shule au maeneo ya kanisa au misikiti ili wananchi wanufaike na fedha zinazolipwa na kampuni za simu.

Naye Mtendaji wa Kijiji cha Bukuku kilichopo kata ya Rufita wilayani Nyag’hwale mkoani Geita, Eunice Gombanila ulipojengwa mnara huo amemweleza Nditiye kuwa mama huyo amekataa kupokea na kusaini mkataba baina yake na Vodacom ambapo alilazimika kukaa na mkataba huo ofisini kwake kwa muda wa wiki nne bila ya mafanikio na alipomfuata mmmiliki wa eneo hilo alikataa kusaini mkataba huo na maeridhia ung’olewe.

Mkuu wa Uedeshaji wa UCSAF, Mhandisi Albert Richard amesema kuwa ujenzi wa mnara huo umegharimu dola za marekani 180,000 ambazo ni zaidi ya shiingi milioni 200 za kitanzania na kuongeza kuwa mnara huo umehujumiwa kwa kung’olewa paneli tatu za sola ambazo zinazalisha umeme wa jua kwa ajili ya kuwasha mnara huo ili uweze kuwaka na kusambaza mawasiliano kwa wananchi.

Mhandisi wa Vodacom, Benedict Mara ameishukuru Serikali kwa kutoa maelekezo ya kuhamisha mnara huo na watatekeleza maelekezo hayo ili waweze kuendelea kutoa huduma za mawasiliano kwa wananchi na wakazi wa kata ya Kafita.

Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kulumbai iliyopo Kata ya Kafita wilayani Nyang’hwale, James Jacob amefurahia uamuzi wa Serikali wa kujenga mnara huo kwenye eneo la shule baada ya mmiliki wa eneo ulipojengwa mnara huo hapo awali kuridhia ung’olewe kwa kutaa malipo ya Vodacom na amesema kuwa malipo hayo yataiwezesha shule kujiendesha.

Mbunge wa Nyang’hwale, Houssein Nassoro Amir amemweleza Nditiye kuwa
anaiomba Serikali kuboresha mawasiliano ya kata ya Nyamtukuza, Nundu, Nyijundu, Kafita, Kaboha na Shabaka kwa kuwa kuna shida ya mawasiliano na ukitaka kupata taarifa saa tano asubuhi unapata saa kumi jioni hivyo inaleta changamoto ya ulinzi na usalama.

“Serikali inatumia mtandao kukusanya mapato yake ila mtu analazimika kukaa na fedha kwa muda mrefu kwa sababu usikivu wa mawasiliano sio mzuri hivyo tunashindwa kukusanya mapato ya Serikali kwa wakati,” amesisitiza Amir.

Katika hatua nyingine, Nditiye amemwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika laMawasiliano Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba na Posta Masta Mkuu waShirika la Posta kufika wilayani Nyang’hwale ndani ya mwezi huu wa Oktoba, 2019 na kufungua ofisi zao ili kuweza kuwahudumia wananchi na kusogeza karibu huduma zao

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA VIJANA WA KWAYA YA RIGHT ANGELS MORAVIAN CHURCH IKULU NDOGO YA TUNDUMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Mafuguli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela, Mkuu wa Wilaya ya Tunduma Mhe. Juma Irando akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Mhe. David Kafulila na wanaKwaya ya Vijana wa Right Angels Moravian Church ya Tunduma walipokuwa Ikulu ndogo ya Tunduma kuonana na Rais Dkt John. Pombe Magufuli ambaye alikaribisha na kuonana nao baada ya kufurahishwa na wimbo wao mzuri wa kulaani rushwa waliomwimbia wakati wa zira yeke mkoani humo. 
 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Mafuguli katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela, Mkuu wa Wilaya ya Tunduma Mhe. Juma Irando, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe
Mhe. David Kafulila na wanaKwaya ya Vijana wa Right Angels Moravian Church ya Tunduma katika Ikulu ndogo ya Tunduma kuonana na Rais Dkt John. Pombe Magufuli ambaye aliwaita na kuonana nao baada ya kufurahishwa na wimbo wao mzuri wa kulaani rushwa waliomwimbia wakatiwa zira yeke mkoani humo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pompe Magufuli na mkewe Mama Janeth Mafuguli  pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela, Mkuu wa Wilaya ya Tunduma Mhe. Juma Irando, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Mhe. David Kafulila wakiimba na wanaKwaya ya Vijana wa Right Angels Moravian Church ya Tunduma katika Ikulu ndogo ya Tunduma  walipokwenda kuonana na Rais Dkt  John. Pombe Magufuli ambaye aliwaita na kuonana nao baada ya kufurahishwa na wimbo wao mzuri wa kulaani rushwa waliomwimbia wakati wa zira yeke mkoani humo. Aliyesimama muelle ni kiongozi wa kwaya hiyo Joana Schinga.PICHA NA IKULU
 Wana Kwaya ya Vijana wa Right Angels Moravian Church ya Tunduma wakipata chaikatika Ikulu ndogo ya Tunduma walipokaribishwa kuonana na Rais Dkt. John. Pombe Magufuliambaye aliwaita na kuonana nao baada ya kufurahishwa na wimbo waomzuri wa kulaani rushwa waliomwimbia wakati wa zira yake mkoani humo.
 Mkuu wa Wilaya ya Tunduma Mhe. Juma Irando akiwa na Katibu Tawala wa  Mkoa wa Songwe Mhe. David Kafulila wakiwa wameongozana na wanaKwaya ya Vijana wa Right Angels Moravian Church ya Tunduma wakiwasili Ikulu ndogo ya Tunduma kuonana na Rais Dkt  John. Pombe Magufuliambaye alikaribisha na kuonana nao baada ya kufurahishwa na wimbo waomzuri wakulaani rushwa waliomwimbia wakati wa zira yeke mkoani humo.

RAIS DKT MAGUFULI AKIMUAGIZA KWA SIMU IGP SIRRO KUMSIMAMISHA KAZI MKUU WA POLISI SUMBAWANGA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John  Pombe Magufuli akiongea kwa simu na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na kumuagiza kumsimamisha kazi mara moja Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Sumbawanga ACP Polycarp Urio kwa kutowasilisha taarifa kwa Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa  maelekezo ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Kangi  Lugola ambaye hivi karibuni aliagiza kuhamishwa kituo cha kazi askari polisi Tisa waliokuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa na kuwabambikizia kesi wananchi. Mhe. Rais alitoa maagizo hayo alipotembelea Kituo cha Polisi cha Laela mara baada ya kuzindua rasmi Barabara ya Tunduma-Laela-Sumbawanga yenye urefu wa kilometa 223.2 ambayo ni sehemu ya barabara kuu katika ushoroba wa Magharibi unaoanzia Tunduma-Mpanda-Kigoma-Nyakanazi wenye urefu wa kilometa 1,286.

TRC YAENDELEA NA ZOEZI LA ULIPAJI FIDIA ILI KUPISHA MRADI WA UJENZI WA RELI YA KISASA MOROGORO - MAKUTUPORA

$
0
0
Shirika la Reli Tanzania - TRC laendelea na zoezi la ulipaji wa fidia na kifuta machozi ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa - SGR kwa awamu ya pili Morogoro - Makutupora hivi karibuni Oktoba 2019.

Zoezi hilo linaendelea katika Halmashauri ya jiji la Dodoma katika mtaa wa Ihumwa ambapo zaidi ya wananchi elfu mbili watapatiwa fidia ya majengo, mashamba na viwanja pamoja na vifuta machozi kwa ndugu wa marehemu ambao makaburi yao yamehamishwa .

Katika zoezi hilo lililofunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Patrobas Katambi, Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi wanaopatiwa fidia kuzitumia katika mambo yenye maslahi ikiwemo kujenga nyumba nzuri na za kisasa kwa kufuata taratibu kwa kuwa eneo la Ihumwa ni la kimkakati.

Aidha maeneo mengine yatakayo patiwa fidia hizo ni pamoja na Chilwana, Kikombo na  Chololo,  Chamwino, Igandu, msamalo na Mnase.

Mhe. Katambi amesema kuwa wananchi wanapaswa kuwekeza na kuangalia mipango mizuri ya kifedha ili kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kupata maelekezo na ushauri wa kitaalamu wa ujenzi kutoka kwa wataalam kuanzia ngazi za vijiji kuendana na mipango miji.

“Mnalipwa fedha hizi nyingi hivyo msizitumie vibaya, mjiwekee misingi na mikakati ya utumiaji wa fedha hizi", alisema Mhe. Katambi 

Vilevile Mhe. Katambi ameongeza kuwa Jiji la Dodoma litanufaika sana kutokana na mradi wa SGR kwa kurahisisha usafirishaji ambao utakuza biashara na mzunguko wa bidhaa kwa ujumla pia amewaasa wananchi kulipa kodi ipasavyo hasa kutoa na kupokea risiti pindi wanapouza au kununua bidhaa au huduma ili kuzidi kuingiza mapato serikalini. 

Naye Meneja msaidizi Mradi wa SGR Morogoro - Makutupora Mhandisi Christopher Mang’wela amesema kuwa Shirika  limezingatia fidia ambayo ni ya haki kamilifu inayozingatia wakati hivyo wananchi wanatakiwa kufanya mambo ya maendeleo kama kujenga nyumba za kisasa pamoja na kuwekeza katika kilimo kwa manufaa ukuzaji uchumi wa Taifa.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Patrobas Katambi, akizindua zoezi la ulipaji wa fidia na kifuta machozi ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa - SGR kwa awamu ya pili Morogoro - Makutupora hivi karibuni Oktoba 2019.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Patrobas Katambi, akizungumza na Wananchi  wa Halmashauri ya jiji la Dodoma katika mtaa wa Ihumwa,kabla ya kuanza kuzindua zoezi la ulipaji wa fidia na kifuta machozi ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa - SGR kwa awamu ya pili Morogoro - Makutupora hivi karibuni Oktoba 2019.
    Wananchi wa mtaa wa Ihumwa ,Halmashauri ya jiji la Dodoma wakimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Patrobas Katambi alipokuwa akizungumza nao kabla ya zaoezi  la ulipaji wa fidia na kifuta machozi kuanza ,ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa - SGR kwa awamu ya pili Morogoro - Makutupora hivi karibuni Oktoba 2019.
 Mkutano ukiendelea
 Wananchi wakifurahia jambo 
 Kazi ya uhakiki ikiendelea

Ole Nasha atoa onyo kwa watakaovujisha mitihani, awapa neno Wanafunzi

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imewaonya walimu na maafisa elimu kuacha tabia ya kuvujisha mitihani na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote wakataojaribu kuvujisha mitihani.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe William Ole Nasha wakati akizungumza na wanafunzi, walimu na wazazi kwenye mahafali ya kidato cha nne kwenye Shule ya Sekondari ya Kwamtoro iliyopo Wilayani Chemba mkoani Dodoma.

Ole Nasha amesema kumekuepo na tabia ya baadhi ya walimu na viongozi wanaohusika na elimu kuvujisha mitihani hasa ile ya ngazi ya Taifa jambo ambalo linaharibu taswira ya elimu nchini.

Amewataka wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne kutodanganyika kununua mitihani kutoka kwa watu wanaowalaghai kutaka kuwauzia na badala yake watoe taarifa kwenye vyombo vya sheria.

" Niwapongeze wanafunzi wote ambao leo mnaagwa, hatua hii ni kubwa sana kwenye maisha yenu. Tunajivunia nyinyi kwa kuwa ndio zao la kwanza la Elimu bure toka Mhe Rais alivyotangaza kufuta ada mashuleni mwaka 2016 ambapo nyie ndio mlikua mnaanza kidato cha kwanza.

Niwasihi msidanganyike eti mkauziwa mitihani. Hasara zake ni kubwa na zitawaponza. Tumieni elimu na maarifa ambayo walimu wenu wamewafundisha kuweza kufanya vizuri mitihani yenu, lengo ni kuona nyinyi nyote mnaogwa leo mnafaulu na kuendelea na kidato cha tano," Amesema Ole Nasha.

Amesema Wilaya ya Chemba mwaka jana ilikutwa na kashfa ya kuvujisha mitihani hivyo kuwataka kuacha tabia hiyo na watakaobainika sheria kali itachukuliwa dhidi yao.

Ole Nasha ameahidi pia kumaliza changamoto ya nyumba za walimu katika shule hiyo ambapo amesema atatoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara yake ili Shule ya Kwamtoro iweze kupatiwa fedha za ujenzi wa nyumba hizo.

Aidha ameitaka Bodi ya Shule kuhakikisha inaharakisha ujenzi wa bweni la wasichana ili likamilike haraka ili waweze kupatiwa fedha zingine kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bweni lingine la wavulana.

" Nimefika hapa na nimekagua maendeleo ya ujenzi wa bweni la wasichana, sijaridhishwa nalo ndio maana mlivyoomba niwapatie fedha za ujenzi wa bweni la wavulana nimekataa. Hakikisheni mnamaliza hilo la kwanza ndio mje tuwapatie fedha za ujenzi wa bweni la pili.

Mhe Rais amefanya Mapinduzi makubwa kwenye sekta ya elimu zaidi ya Bilioni 945 zimetumika kwenye sera hii ya elimu bure. Ni jukumu lenu sasa wanafunzi kusoma kwa bidii ili kumpa moyo Rais wetu kwa kazi kubwa anayofanya ya kutuletea maendeleo wananchi tulio wanyonge," Amesema Mhe Ole Nasha.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amemshukuru Mhe Naibu Waziri kwa kukubalj kuhudhuria mwaliko huo na kumuahidi kuongeza usimamizi katika sekta hiyo muhimu kwenye maendeleo ya Nchi na hasa katika kudhibiti vitendo vya uvujishaji mitihani.

Nae Mbunge wa Jimbo la Chemba, Juma Nkamia amishukuru Wizara ya Elimu kwa namna ambavyo imekua ikitoa fedha katika kuhakikisha miradi ya elimu ndani ya Jimbo lake inatekelezwa.

" Mhe Naibu Waziri nakushukuru sana kwa kukubali mwaliko wetu wa kuwa mgeni rasmi. Tunakupongeza wewe na wizara unayoiongoza kwa jinsi ambavyo mmekua mstari wa mbele kutuletea maendeleo wananchi wa Chemba," Amesema Nkamia.

Awali Mhe Ole Nasha aliendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa matundu ya vyoo kwenye Shule hiyo ambapo kiasi cha Shilingi Milioni mbili zilipatikana na kuzikabidhi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ili kukamilisha ujenzi huo na kumaliza changamoto hiyo.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe William Ole Nasha akikagua ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari ya Kwamtoro wakati alipofika kwenye mahafali ya kidato cha nne.
 Mbunge wa Jimbo la Chemba, Juma Nkamia akizungumza wakati wa mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kwamtoro ambapo yeye ndie mlezi wa Shule hiyo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe William Ole Nasha akizungumza wakati wa mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kwamtoro wilayani Chemba, Dodoma.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Chemba, walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kwamtoro wilayani humo wakati wa mahafali ya kidato cha nne ambapo Mhe Ole Nasha alikua mgeni rasmi.

WAZIRI MKUU LEO KUZINDUWA MAONESHO YA PILI VIWANDA VIDOGO (SIDO) KITAIFA 2019 MKOANI SINGIDA

$
0
0

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Promised Eden Environmental Care (PEEC) iliyopo Karagwe, Kagera, Tanzania, East Africa, Ascarlyon Lufurano akionesha mapapai yanayolimwa na Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Pili ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa 2019 Mkoa wa Singida.
 Ascarlyon Lufurano akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lao katika maonyesho hayo.
 Ascarlyon Lufurano akiwa na Mratibu wa Miradi wa Taasisi hiyo, Leonard Bandio.
 Mhandisi Mohamed Kimia wa Shirika la Sema (kushoto) akielekeza namna ya kutumia pampu ya maji ya  kamba jinsi inavyofanya kazi.
 Mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Sabasaba chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Mkoa wa Singida, Janifa Olais (kushoto) akimuonesha Gelard Kilomo mfuko wa kitambaa ulioshonwa na 
chuo hicho.
 Wanafunzi wa chuo hicho wakiwa kwenye banda lao na walimu wao.Katikati waliosimama ni mkuu wa chuo hicho, Fatuma Malenga na kushoto ni Mwalimu, Maria Joram.
 Mwanafunzi wa fani ya umeme wa majumbani wa chuo hicho, Stephen Lucas (katikati) akimuekeza namna ya kuwasha taa, Ester Mvati alipotembelea banda hilo. Kulia ni Mwanafunzi, Omari Salum.
 Mjasiriamali wa kuuza dawa za asili kutoka Aspera 4 Women, Sophia David (kulia) akitoa maelezo ya matumizi ya dawa kwa wananchi waliotembelea banda lake.
 Muonekano wa banda la wajasiriamali wa dawa za asili zitokanazo na mimea.
 Muonekano wa mabanda ya maonyesho hayo.
 Mzee Hassan Magomba kutoka Urambo Tabora akiwaelekeza wanafunzi wa Veta namna mashine ya kuangulia vifaranga vya kuku inavyofanya kazi.
 Soud Bakari (wa pili kushoto) akiwaelekeza wanafunzi wa Veta jinsi mashine ya kuangulia vifaranga vya kuku inavyofanya kazi.
 Afisa Masoko wa Kampuni ya Poly Machinery Com.LTD, Amos Leng'oko (katikati) akiwaelekeza wananchi waliotembelea banda lao jinsi ya mashine ya kusaga mahindi inavyofanya kazi.
 Meneja Masoko wa  Deve General Supplies Company, Gisela Denis akiwaelekeza wakina mama waliotembelea banda la kampuni hiyo jinsi ya kutumia vitanda vya kujifungulia na kulalia wagonjwa.
 Gisela Denis akielekeza namna ya kutumia kitanda cha kujifungulia.
 Mtaalamu wa kutengeneza majiko ya kisasa ambayo yanatumia mkaa na kuni kidogo na kutunza joto, Omari Komba (wa pili kulia) akitoa maelezo jinsi ya kutumia majiko hayo.
 Mjasiriamali wa kutengeneza vyungu kutoka Kondoa Dodoma, Sophia Mumba (kushoto) akielekeza jinsi ya kutengeneza bidhaa hizo.
 Mjasiriamali wa kusindika vyakula vya kimiminika kama pilipili, jamu ya asali, karanga na vinginevyo kutoka Madima Enterprises ya Manyara, Lilian Joseph (kulia) akielezea ubora wa 
bidhaa zake.
 Mjasiriamali  Hyasinta Wanchelele (kulia) kutoka Mwanza, akimuonesha dagaa Fanuel Dissa wanao tengenezwa na kampuni yake.
 Wajasiriamali Anna John na Boniface John kutoka Chonde Group mkoani Manyara wakiwa mbele ya bidhaa zao.
 Mjasiriamali kutoka Kamshuu Food Industry, Shufaa Mubago Arusha akiwa na bidhaa zake katika maonesho hayo.
 Mjasiriamali Esther Songoi kutoka Wisdom Food Products jijini Mwanza akiwa na bidhaa zake.
 Mjariamali Theresia Mbili kutoka 2 Super Unga wa Ubuyu mkoani Mara akiwa mbele ya bidhaa zake.
 Mjasiriamali wa kutengeneza Mvinyo kutoka Kampuni ya Epac Products Centre ya Jijini Dodoma akiwa mbele ya bidhaa zake.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Panako Products ya Nansio Ukerewe inayotengeneza Mvinyo Rosela, Paschal Mahotola  (kushoto) akizungumza na wananchi waliotembelea banda lake katika maonesho hayo.
 Mjasiriamali Pasikazia Sebastian (kushoto) kutoka Kagera Organic Farmers Community (Kaofaco Food Processing) akiwaelezea wananchi ubora wa bidhaa wanazo zitengeneza. 
 Wajasiriamali Soud Rajab (kulia) na Daniel Crown  kutoka Misuna Oil Mill wakiwa mbele ya bidhaa zao kwenye maonesho hayo.




 Afisa wa Kampuni ya Faida Mali, Lazaro Mnkumbu (katikati) akitoa maelekezo jinsi ya kutumia mashine ya kupandia mbegu zinazosambazwa na kampuni hiyo.
 Watoto wakipata burudani ya kubembea katika maonesho hayo. Bembea hiyo imetengenezwa na Mjasiriamali Kapalata wa mjini Singida.
Mjasiriamali ambaye ni mwandishi wa vitabu Mwalimu Jilu Muna Mpanda wa mkoani Singida, akionesha kitabu alichokiandika cha Chimbuko la koo mbalimbali za Arimi (Wanyaturu $ Wanyiramba)

KIGWANGALA ATOA SIKU 14 KWA MANAIBU KATIBU WAKUU NA KATIBU MKUU KUWASILISHA MCHAKATO WA MSWAADA WA SHERIA UUNDWAJI JESHI USSU

$
0
0
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya jeshi ussu wakionyesha uwezo wao wa kupanga risasi ndani ya dakika mbili kwenye maonesho yaliyofanyika mbele ya Mhe.Waziri wa utalii na maliasili.
Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya jeshi ussu wakipita mbele ya Waziri wa utalii na maliasili katika sherehe hizo.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya awali ya jeshi ussu akipita juu ya kamba katika moja ya maonesho yaliyofanyika mbele ya waziri wa utalii na maliasili Mhe.Khamis Kigwangaka katika sherehe ya kuhitimisha mafunzo hayo

Na Jusline Marco-Arusha

Waziri wa maliasili na utalii Dkt.Khamis Kigwangala ametoa siku 14 kwa manaibu katibu wakuu na katibu mkuu wa wizara hiyo kuwasilisha mchakato wa mswada wa sheria ya uundwaji Jeshi Ussu ofisini kwake ili iweze kuwasilisha bungeni.

Ametoa agizo hilo katika sherehe za kuhitimisha mafunzo ya Awali ya Jeshi Ussu katika kituo cha mafunzo cha Mbulu-mbulu kilichopo katika kata ya Kambi ya simba,Wilayani Karatu Mkoani Arusha.

Dkt.Kigwangala amesema kuwa kutokukamilika kwa mswada huo ni mapungufu ya wizara kwani amekuwa akielekeza mara kadhaa mswada huo ukamilike na umekuwa haukamilishwi.

"Katika maagizo niliyopewa na Mhe.Rais sikusudii kujiona nikitumbuliwa kwasababu ya kuchelewa kutimiza wajibu wangu,"Alisema Dkt.Kigwangala huku akiongeza kuwa kama ni madokezo ameandika mara kadhaa lakini wamekuwa wakijivuta.

Ameongeza kuwa kwa  zaidi ya miaka kumi tangu ilipoelekezwa na sheria ya uhifadhi ya wanyamapori haijawahi kuanza ila kwasasa taasisi mbalimbali za uhifadhi wa wanyamapori zimeanza kuonyesha bidii katika kuwapatia mafunzo wafanyakazi wao kwenye eneo la Jeshi Ussu.

Vilevile ametoa jukumu kwa bodi ya mamlaka ya uhifadhi wa wanyamapori Ngorongoro kupeleka ushauri wa mapendekezo yaliyotolewa ya kufanya kiwtuo hicho kuwa kamili kwa kuangalia vigezo vyote vitakavyowezesha kufanya kituo hicho kuwa kituo cha kudumu.

Awali akitoa risala yake kwa mgeni rasmi  mkuu wa kutuo hicho Kanali Martin kilugha  amesema kuwa jumla ya wahitimu wa mafunzo hayo ni 112 ambapo katika mafunzo hayo wakufunzi wa ndani wametumika,wakufunzi wa hifadhi pamoja na wakufunzi wa muda kutoka katika jeshi la JWTZ kwa ajili ya kuimarisha Jeshi Ussu.

Amesema kuwa wahitimu hao wamefundishwa mafunzo mbalimbali ya uhifadhi ikiwemo utimamu wa mwili,na ulinzi wa nadharia na vitendo na kufaulu kwa madaraja mbalimbali.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo amesema kuwa kumekuwa na matukio mengi ya ujangili ya kuuawa kwa wanyama hivyo wahitimu wa mafunzo hayo wanapaswa kufahamu kuwa wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanalinda rasilimali za nchi.

"Niwaomba wahitimu walio chini ya uongozi wako Mhe.Waziri wakapambane na ujangili ili kukomesha mchezo huo na rasilimali za nchi ziweze kuwa salama kwa faida ya wananchi kwani huo ndio msimamo wa Rais wetu ndiyo maana ameridhia tuende kwenye mfumo wa kijeshi kama sehemu yake ya kuonyesha dhamira ya kupambana na ujangili na kulinda rasilimali zetu".Amesema  Mkuu huyo.

Waandikishaji wapiga kura serikali za mitaa watakiwa kuzingatia weledi, nidhamu na uzalendo

$
0
0
ZIKIWA zimesalia wiki chache kudika Uchaguzi wa serikali za mitaa, Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel amewataka waandikishaji wote wa wapiga kura katika Tarafa hiyo kuzingatia nidhamu,Weledi na Uzalendo kwa kipindi chote cha zoezi hilo linalotarajia kuanza rasmi tarehe Oktoba 8  hadi 14 Oktoba 2019.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Semina maalumu iliyolenga kutoa Elimu kwa waandikishaji wa wapiga kura tarafani Itiso  na kufanyika  makao makuu ya tarafa hiyo ikiwa ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa mwaka 2019.

Katika Ujumbe wake kwa waandikishaji hao Remidius amewataka kutambua dhamana kubwa waliyopewa katika kufanikisha zoezi hilo muhimu la kitaifa kupitia Tarafa ya Itiso.

"Ninasisitiza sana mzingatie yale yote mtakayoelekezwa katika jukumu hili zito, nina hakika hamtaniangusha, nina imani na uwezo wenu mkubwa,lakini haya yote yatawezekana  ikiwa mtamtanguliza mungu  pamoja na kufanya kazi hii kwa weledi,nidhamu na uaminifu mkubwa,"amesema Emmanuel

Hata hivyo, kiongozi huyo amewashukuru na kuwapongeza wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo ngazi ya vijiji,Kata na Wilaya kwa namna walivyojipanga vyema katika kufanikisha zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2019. 

"Kazi hii inahitaji sana uzalendo, ninatoa onyo kwa wale wote watakaojaribu kukwamisha zoezi hili, tunazo kanuni, miongozo muhimu pamoja na ratiba ya matukio yote ya uchaguzi, sisi tuhakikishe tunazingatia haya na sio kuwa sehemu ya kufifisha ufanisi wa shughuli za uchaguzi katika maeneo yetu,"

"Lazima mkumbuke kwamba kazi hii mnayoifanya ndio itakayowawezesha kutoa haki ya msingi kwa wananchi wetu kuwachagua viongozi wao katika ngazi za Vitongoji, Mitaa na Vijiji, kwa hiyo kazi mliyonayo ni muhimu katika maslahi mapana  ya Taifa letu," ameongezea Emmanuel.

Kwa upande wake Afisa  wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Wilaya ya Chamwino Idda Siriwa  ametoa elimu ya kuzuia,kupambana na kutokomeza  rushwa kwa waandikishaji hao pamoja na Wasimamizi wasaidizi ngazi ya vijiji na Kata  na kuwasisitiza kutojihusisha kabisa na vitendo vya kutoa au kupokea rushwa.

Idda amesema ikiwa watabaini uwepo wa matukio hayo watoe taarifa kwa kupiga namba 113 kwa mitandao yote ya simu au kutuma Ujumbe mfupi au kubonyeza *113#  kisha kubonyeza OK na kufuata maelekezo  ambapo watapata maelezo na kutoa tuhuma au malalamiko husika.

Aidha Afisa huyo ametoa namba ya simu ya mkononi ya Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Chamwino  kama njia ya ziada ya kufikisha malalamiko yoyote ya Rushwa kutoka Tarafa ya Itiso na Wilaya hiyo kwa ujumla.

Zoezi hilo la Elimu kwa Waandikishaji wa wapiga kura  lilifanyika kwa mujibu wa ratiba ya matukio ya  uchaguzi wa Serikali za Mitaa iliyoelekeza Elimu hiyo kutolewa kwa wahusika  kati ya tarehe  4-6 Oktoba,2019 na Msimamizi wa uchaguzi pamoja na wasaidizi wake ngazi ya Wilaya.

Baadhi ya Waandikishaji walioshiriki Semina hiyo wameahidi kuzingatia yote waliyojifunza  na kwamba wanatambua uzito wa kazi hiyo waliyonayo kwa kipindi chote watakachoshiriki katika zoezi hilo na kuwa sehemu ya kufanikisha zoezi hilo la  uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2019 kupitia Tarafa ya Itiso.
 Afisa Tarafa ya Itiso Remidius Emmanuel  akizungumza wakati anafungua Semina Maalum kwa  waandikishaji wa Wapiga kura katika Tarafa ya Itiso, Semina hiyo imefanyika Makao Makuu ya Tarafa hiyo.
 Afisa TAKUKURU Wilaya ya Chamwino Bi.Idda Siriwa akitoa Elimu ya kupambana na Rushwa katika Semina maalum kwa waandikishaji wa wapiga kura katika Tarafa ya Itiso
  Mmoja wa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Wilaya, Raymond Mwachango akiwasilisha mada katika Semina maalum kwa waandikishaji wa wapiga kura  katika Tarafa ya Itiso.


 Baadhi ya waandikishaji wa wapiga kura  katika Tarafa ya Itiso wakifuatilia semina hiyo iliyoandaliwa ili kuwaongezea ujuzi kwenye kazi yao

WAZIRI MHAGAMA: JAMBO JEMA VIJANA KUENZI FALSAFA ZA MWL. JULIUS KAMBARAGE NYERERE

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amepongeza vijana kwa kuonesha niya njema ya kuendelea kumuenzi Baba wa Taifa sambamba na kuendeleza mambo mema yote aliyoyafanya enzi za uhai wake.

Ameyasema hayo Oktoba 6, 2019 wakati wa hafla ya kuwaaga vijana 60 waliopanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuadhimisha kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika Marangu, Mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mhagama alisema kuwa, Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere alikuwa kiongozi mzalendo kwa nchi yake na aliyejali utu na usawa, hivyo ni jambo zuri kuona vijana wakiendelea kuenzi falsafa za mhasisi wa Taifa hili Mwl. J. K. Nyerere pamoja na Hayati Mzee Abeid Aman Karume ambao kwa kiasi kikubwa wamechangia katika suala zima la kudumisha umoja na msikamano wa Taifa.

“Kitendo hiki wanachofanya vijana kwa kupanda mlima Kilimanjaro ni jambo la kishujaa na uzalendo wa hali ya juu kwa Taifa ni matumaini yangu vijana wengi wataiga mfano huu mzuri,” alisema Mhagama

Alieleza kuwa, Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere alifanya kazi kubwa ya kujenga misingi imara ya nchi kuwa na amani, umoja, mshikamano pamoja na misingi ya kuwa na uchumi wa kujitegemea.

“Vijana mnatakiwa kuendeleza na kuiga utendaji kazi wa Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere alijitolea kwa mambo mengi ili kujenga Taifa, alikuwa mstari wa mbele katika kupambana na mambo mengi ikiwemo  ujinga, maradhi na umaskini ili kila mtanzania awe na maisha bora. Hiyo ilikuwa ni ishara tosha kwa vijana kutambua namna Baba wa Taifa alivyolipigania nchi yetu,” alisema Mhagama

Aliongeza kuwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Dkt. Alli Mohammed Shein ni mfano tosha wa kuigwa na vijana, wanaonesha namna wanavyojitoa kwa ajili ya Taifa na kuhudumia wananchi pamoja na kukuza uchumi wa nchi.  

Waziri Mhagama alifafanua kuwa, kuelekea kilele cha mbio za mwenge mwaka huu vijana hao waliopanda mlima Kilimanjaro watapata fursa ya kujumuika na vijana kutoka kwenye nchi jirani ikiwemo Angola, Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini, Uganda, Rwanda na Kenya katika kongamano la kujadili mchango wa Baba wa Taifa barani Afrika.

Aidha Waziri Mhagama alitoa wito kwa watanzania wote hususan vijana kuendelea kuenzi falsafa za waasisi wa taifa hili Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Abeid Aman Karume kwa kutambua kuwa waasisi hao ni urithi tosha. Pia aliwasihii vijana kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuyaenzi yaliyofanywa na waasisi hao.

Sambamba na hayo alipongeza vijana ambao walijitolea kupanda mlima huo toka zoezi hilo lilipoanzishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa ni sehemu ya kuendelea kukumbuka falsafa za Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Pamoja na hayo alitoa shukrani kwa Wizara ya Maliasili na Utali, Uongozi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Taasisi na Wadau kwa kushirikiana na Ofisi yake katika kufanikisha suala hilo muhimu kwa vijana.

Kwa Upande wake, Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu alieleza kuwa suala la vijana hao kujitolea kupanda mlima Kilimanjaro ni kitendo cha kijasiri na kizalendo, itawajengea uwezo wa kuwa mabalozi wazuri wa vijana wenzao na pia wataweza kutangaza Mlima huo na vituo mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini.

“Tumefanikiwa kuweka majina kwenye vituo 5 vilivyopo kwenye mlima huo ili kuwapa hamasa wanaopanda kutambua kuwa wanao uwezo wa kupanda hadi kileleni, kinachotakiwa ni kufuata ushauri utakao kuwa ukitolewa na waongozaji,” alisema Kanyasu

Naye Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba aliwataka vijana kuendelea kutambua kuwa tunu za amani na umoja zilikuwa miongoni mwa falsafa kuu ya Mwalimu Nyerere ambapo matokeo yake ni umoja na mshikamano wa Taifa uliopo hadi sasa.

Pia Mkurugenzi wa Vijana katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Mwanaidi Mohamed Ali alisema kuwa vijana wanapaswa kuendeleza yale yote yaliyofanywa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja na Hayati Mzee Abed Aman Karume ili waendelee kudumisha muungano.

Katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019, Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana inaratibu shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa Vijana. Jumla ya vijana 88 tayari wameshapanda mlima huo ikiwa ni kumbukizi ya miaka 20 ya kifo ca Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na vijana pamoja na wakazi wa Marangu wakati wa hafla ya kuwaaga vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
 Sehemu ya Vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuwaaga iliyofanyika Mkoani Kilimanjaro.
 Baadhi ya Vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuwaaga iliyofanyika Mkoani Kilimanjaro.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu akieleza jambo wakati wa hafla hiyo ya kuwaanga vijana waliopanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuadhimisha kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika Marangu, Mkoani Kilimanjaro. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Bwai Biseko na Kaimu Kamishna wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Angela Nyaki.
 Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba akielezea jambo wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. James Kajugusi na Mkurugenzi wa Vijana katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Mwanaidi Mohamed Ali.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. James Kajugusi akifafanua jambo kuhusu ushiriki wa vijana hao kabla ya kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro Oktoba 6, 2019 Mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni Mkurugenzi wa Vijana katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Mwanaidi Mohamed Ali.
 Kiongozi wa Vijana waliopanda Mlima Kilimanjaro Dkt. Ally Matunzia akielezea jambo wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipowatembelea kwa lengo la kuwaaga kabla hawajapanda Mlima huo.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu (Kushoto) akiteta jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kuwasili katika Hifadhi hiyo ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa ajili ya kuwaaga vijana 60 waliopanda mlima huo. Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kippi Warioba.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Kamishina Msaidizi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Angela Nyaki (aliyesimama) alipokuwa akiwasilisha taarifa fupi kuhusu Mlima huo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikabidhi Bendera ya Taifa kwa Kiongozi wa Vijana Dkt. Ally Matunzia kabla ya kuanza kupanda Mlima huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali na Vijana waliopanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

WANAFUNZI WAKEMEWA KUFANYA VISASI KWA WALIMU PAMOJA NA KUCHOMA MOTO SHULE-ALHAJ LASENGA

$
0
0
 Na Mwamvua Mwinyi
WANAFUNZI hususan wa shule za sekondari, wamekemewa kujiepusha kuweka visasi na walimu wao kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha madhara ikiwemo kuchoma moto shule husika na kurudisha nyuma maendeleo ya shule.

Pamoja na hilo ,wazazi na walezi wametakiwa ,kushirikiana na wawekezaji wa masuala ya elimu na kuacha kuwakwamisha katika juhudi hizo.

Akizungumza katika mahafali ya tano ya shule ya kiislamu ya sekondari ya Vuchama,iliyopo Ugweno Kilimanjaro, mlezi wa walimu BAKWATA Mkoa wa Kilimanjaro, Alhaj Sheikh Yusufu Lasenga 
 Alisema ,baadhi ya shule nchini zimekuwa zikichomwa moto na wanafunzi ambapo kwa upande mwingine inatokana na visasi visivyokuwa na tija kwa maendeleo ya kielimu.

"Jiepusheni migongano na walimu wenu, usiweke tofauti kisa mmechapwa viboko ama mmeonywa na walimu kwakuwa nao ni sehemu ya wazazi wenu"alisisitiza Lasenga.

Lasenga aliwasihi, wanafunzi kuwa na nidhamu na maadili yaliyo mema ndani ya jamii ili kuinua taaluma zao.

Nae mkurugenzi  wa wakurugenzi wa shule zinazomilikiwa na Njuweni Institute, Yusuph Mfinanga hakusita kukemea baadhi ya wazazi na walezi wanaobagua kutoa elimu kwa watoto wakiume na wakike.
Mfinanga, aliomba ushirikiano na jamii katika jitihada zake za kuunga mkono juhudi za serikali kuinua sekta ya uwekezaji kwenye masuala ya elimu.

Kwa upande wake, mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Vuchama, Jumanne Mkoga alisema shule hiyo inafanya vizuri kitaaluma kwa miaka mitatu mfululizo ambapo mwaka 2016 ilikuwa ya tatu kimkoa kati ya shule 33 na kitaifa 58 kati ya shule 1,439.

"Mwaka 2017 tulikuwa wa pili kimkoa kati ya shule 55 na kitaifa 32 kati ya shule 1,738 na mwaka 2018 tulikuwa wa kwanza kimkoa huku kitaifa tukiwa wa 22 kati ya shule 1,371.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Azungumza na Ujumbe wa Taasisi ya China National Research Institute of Food &Fermentation Industries

$
0
0
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Ndg. Salum Maulid Salum akizungumza na Ujumbe wa Taasisi ya China National Research Institute of Food &Fermentation Industries ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Dong Jianhui kulia akiwa na ujumbe wake wakati wa mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais leo 7-10-2019.(Picha na Ikulu)

AFISA MANUNUZI, MZABUNI, KINAMPANDA WAKAMATWA KWA KUGHUSHI NYARAKA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Singida, Bw. Adili Elinipenda amkamate Afisa Manunuzi wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, Bw. Francis Muyombo kwa kukiuka taratibu za manunuzi ya Serikali na kughushi nyaraka.

Pia alimwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Sweetbert Njewike amkamate na kumhoji Bw. Joseph Kisaka ambaye alikuwa mzabuni wa chuo hicho kwa kuwapatia (kusupply) vifaa ambavyo ni chini ya kiwango.

Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Oktoba 6, 2019), wakati akikagua ukarabati wa majengo ya chuo hicho kilichopo wilayani Iramba, mkoani Singida ambako alibaini delivery note ikionesha kitasa kimoja kimenunuliwa kwa sh. 70,000 badala ya sh. 25,000.

Waziri Mkuu alisema quotation ya manunuzi inaonesha kwamba walipaswa kununua vitasa ambavyo vinafunga mara tatu (vya 3-level) lakini alipokwenda kukagua milango kwenye mabweni, ukumbi, na bwalo alikuta ni vitasa vya kufunga mara moja (vya 1-leavel).

“Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 kwa kila chuo ili kufanya ukarabati wa vyuo vya elimu kikiwemo hiki cha kwenu. Ninyi mnanunua vifaa kinyume na utaratibu wa Serikali, hamvikagui, mnaweka tu vitu hafifu ambavyo havidumu. Haiwezekani!”

“Quotation yenu hapa inanionesha mlinunua vitasa 368 vya 3-level kwa gharama ya shilingi 70,000 kila kimoja. Lakini vitasa vilivyoko mlangoni ni vya 1-level ambavyo vinauzwa shilingi 25,000. Haya ni mabweni ya wanafunzi, wanaingi na kutoka kila wakati, ni kwa nini mnaweka vitu cheap wakati mnajua vitaharibika mapema? Maelekezo ya ununuzi wa Serikali yakoje?”

Alipoulizwa wametumia utaratibu gani kununua vifaa hivyo, Mkuu wa Chuo hicho, Bw. Hamisi Njau alisema walikuwa wakitumia kamati ya manunuzi ambayo mwenyekiti wake alikuwa ni Makamu Mkuu wa Chuo na Katibu wake ni Afisa Manunuzi, Bw. Muyombo.

Bw. Muyombo alipoulizwa kama walikuwa wanayo BOQ ambayo ilikua ikiwaongozwa kufanya manunuzi, alijibu kwamba hawakuwa nayo bali alikuwa wakiorodhesha mahitaji yao na kuyapeleka kwa mhandisi.

Alipoambiwa aeleze tofauti ya vitasa vya 3-level na vya 1-level, Bw. Muyombo alijibu kwamba waliambiwa na mhandisi kwamba ndani ya kitasa kuna kibati ambacho kinatofautisha vitasa hivyo.

Waziri Mkuu alisema alisema Serikali inakataa udanganyifu kwenye manunuzi na haitavumilia watumishi wasiokuwa waaminifu. “Tena hili duka la huyo Kisaka ni la nguo wala siyo la hardware (vifaa vya ujenzi).”

Alimwambia Mkuu wa Chuo hicho alipaswa kusimamia ikiwa ni pamoja na ujenzi na ukarabati unaofanyika chuoni hapo.

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilitoa sh. 1,439.235,746 ili kukarabati chuo hicho kwenye maeneo ya utawala, maeneo ya kujifunzia, kumbi na mabweni ya wanachuo. Awamu ya kwanza ya fedha hizo iliingia Novemba, 2017 na awamu ya pili ikaingia Juni 2018.

Akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho baada ya kufanya ukaguzi huo, Waziri Mkuu alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini. “Mheshimiwa Rais alitoa sh. bilioni 1.4 kwa vyuo vyote ili kukarabati na kuboresha hadhi ya vyuo hivyo vikiwemo vya Monduli, Patandi, Kinampanda, Mtwara, Songea, Nachingwea, Korogwe, Kasulu na Butimba.”

“Nimeingia kwenye maktaba yenu nimeona bado vitabu vilivyopo ni vya muda mrefu, lakini kwa upande wa ajira bado tunaendelea kuajiri kwa awamu. Julai mwaka huu tuliajiri walimu 4670 na sasa hivi tumepata kibali cha kuajiri walimu 16,000,” alisema.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimhoji Afisa Manunuzi wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, Bw. Francis Muyombo (kushoto), kwa kukiuka taratibu za manunuzi ya Serikali na kughushi nyaraka, Oktoba 6.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua maktaba ya Chuo cha Ualimu Kinampanda, mkoani Singida, wakati akikagua ukarabati wa Chuo hicho Oktoba 6.2019.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua ukarabati wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, mkoani Singida, Oktoba 6.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua mlango, kwenye ukarabati wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, mkoani Singida, na kutoridhishwa na vitasa hafifu vilivyotumika katika milango hiyo, Oktoba 6.2019.

Benki ya CRDB Tawi la Holland waanza wiki ya Huduma kwa Wateja

$
0
0
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Holland, jijini Dar es salaam wakingozwa na Meneja wao, John Almas (walioketi katikati) wakiwa katika picha ya pamoja ikiwa ni siku ya kwanza ya wiki ya huduma kwa wateja, inayoendelea sasa Duniani kote. 
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Holland, John Almas akisaidia kuwahudumia chakula baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo, ikiwa ni sehemu ya wiki ya huduma kwa wateja, inayoendelea sasa Duniani kote. 

Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Holland, John Almas akiwapatia keki baadhi ya wateja wa Benki hiyo waliofika kupata kuduma mapema leo asubuhi.

Picha: Rais Dkt. Magufuli akiwasili katika uwanja wa Nelson Mandela

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Sumbawanga mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa mpira wa Nelson Mandela kwa ajili ya kuwahutubia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB agawa chai kwa wateja

$
0
0
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amewaongoza baadhi ya watendaji wa benki hiyo kugawa chai kwa wateja wao.

Akizungumza akiwa kwenye tawi la Kariakoo Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, Nsekela alisema ni wiki muhimu kwa wateja wa CRDB.

Alisema ni wiki ya viongozi wa benki hiyo kutoka matawi yote kuwafuata na kuwahudumia wateja kwa upendo chini ya kaulimbiu ya 'Ulipo tupo kukupa Magic'.

"Hii ni wiki ya huduma kwa wateja duniani kaulimbiu ya dunia ni 'The magic of service' na sisi benki yetu tunashiriki kwa kuwahudumia wateja wetu.

"Tunawaambia ulipo tupo kukupa Magic. Tumeandaa vitu vingi vizuri naamini wateja wetu watafurahia," alisema Nsekela.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akifungua Shampeni kuashiria kuanza kwa wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa sehemu mbalimbali duniani, katika hafla iliyofanyika kwenye tawi ya Benki ya CRDB, Karikoo jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akimiminia Shampeni  mmoja wa wateja wa Benki hiyo, waliofika kupata huduma kwenye tawi ya Benki ya CRDB, Karikoo jijini Dar es salaam.











WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAJIPANGA KUCHANGIA PATO LA TAIFA KWA ASILIMIA 10-PROFESA OLE GABRIEL

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KATIBU  Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel, amesema sekta ya mifugo na uvuvi inachangia takribani asilimia 7.9 ya pato la Taifa.

Wazara hiyo imejipanga  huku kuboresha sekta hiyo na kutarajia kufikia asilimia 10  hadi 25  ifikapo 2025 pamoja  na uzalishaji wa malighafi katika sekta ya viwanda .

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa wadau wa Sekta ya Mifugo wakiwemo wastaafu, Ole Gabriel amesema uboreshwaj kwa sekta hiyo kutafanya Tanzania kuwa ya viwanda na  kuwafanya wafugaji kuwa na uchumi wa kati ikiwa ni kuchana na ufugaji wa mazoea.

Amesema ili kufikia lengo la kuongeza pato la taifa watanzania wanapaswa kupenda vitu vya ndani na kuhakikisha wananunua bidhaa za  ngozi zinazotokana na mifugo hali ambayo italeta tija kwa nchi.

“Tatizo kubwa la Watanzania bado wanaumwa ugonjwa wa kununua vitu vya nje na sio ndani ya nchi wakiamini ndio bora wakati bidhaa zilizopo ni bora sana kwani uzalishaji madawa ya mifugo na vyakula vyake vinazalishwa hapa hapa nchini ”alisema Prof. Ole Gabriel

Aidha alisema Wastaafu waliofanya kazi katika sekta hiyo wanawajibu wa kuendelea kuisaidia serikali ya awamu ya tano  katika kutoa mafunzo mbalimbali katika vyuo vya mifugo ili mchango wao uendelee kuonekana katika jamii.

Prof. Ole Gabriel alisema katika mkutano huo watapata fursa ya kujadili mambo saba ikiwemo namna ya kuondoa vikwazo vya biashara ya mifugo ndani na nje ya nchi,kushauriana namna ya uboreshaji wa viwanda vya Mifugo,Namna  ya kupata pembejeo za Mifugo kwa bei nafuu,Kudhibiti uingizaji wa mazao ya mifugo na mifugo ambayo zipo chini ya viwango na kujadili Mkakati wa uboreshaji wa Sekta ya mifugo.

Nae Mdau wa Uzalishaji wa Dawa za Mifugo wa Kampuni ya Farm Base Salim Mselemu amesema kuwa wanashirikiana na serikali vizuri kwa kuwaamini katika dawa.

Amesema kuwa Farm Base ni kampuni ya wazawa hivyo nia yao ni kuona wafugaji wanapata bidhaa bora katika kuendeleza sekta ya mifugo nchin.

“Wafugaji wengi wanafuga kwa mazoea wanaangalia bei ya kuuza na sio kuangalia bei ya gharama alizotumia katika utunzaji wa mifugo yake nah ii inawaangusha wafugaji wengi,”alisema  Prof. Ole Gabriel

Kwa Upande wake Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dkt Mary Mashingo alisema wanaishukuru wizara hiyo  kwa kuwakutanisha pamoja katika mkutano huo na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya mifugo.

“Mataifa mengi wazee waliostaafu katika sekta mbalimbali  wamekuwa wanafanya kazi na kujitoa katika kutoa utaalamu wao huku wakijipangia muda wa kufanya kazi hizo,”alisema
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na Wastaafu wa Wizara hiyo pamoja na wadau sekta  Uvuvi katika Mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Mstaafu  wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Dkt Mary Mashingo akitoa namna sekta ya mifugo inavyoweza kuwa na mchango kwa wafugaji kupata mikopo Benki ya TIB Wastaafu wa Wizara hiyo pamoja na wadau sekta  Uvuvi katika Mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wastaafu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wadau wa Mifugo wa Uvuvi katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
 Mdau wa Uzalishaji wa Dawa za Mifugo wa Kampuni ya Farm Base Salim Mselemu akizungumza namna wanavyoshirikiana serikali katika uzalishaji wa dawa za mifugo katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha  ya pamoja Wastaafu wa Wizara hiyo pamoja na wadau sekta  Uvuvi uliofanyika jijini Dar es Salaam
Bidhaa za Dawa zinazozalishwa na Farm Base wakionesha katika Mkutano Wastaafu wa Wizara hiyo pamoja na wadau sekta  Uvuvi uliofanyika jijini Dar es Salaam.

UAGIZAJI BIDHAA ZA NJE UTAENDELEA KUPUNGUA-MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kupunguza uagizaji wa baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nje na kuongeza ununuzi wa bidhaa zinazozalishwa ndani ili kukuza viwanda vya ndani mfano ni bidhaa za mbao na mafuta ya kula.

 “Napenda kuwahakikishia kuwa, bidhaa zetu ni nzuri na zinapendwa na watu wengi hata wa nje ya nchi. Mnachotakiwa kukifanya ni kuzalisha bidhaa kwa wingi na kwa kutumia malighafi zinazopatikana kwenye maeneo yenu, hii itawezesha kuwa na uzalishaji wenye gharama ndogo na kuwa na bei shindani katika soko."

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 7, 2019) wakati akifungua Maonesho ya Sido Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya BomberdiaManispaa ya Singida. Amesema Serikali itaendelea kujenga mazingira mazuri ya kuwa na viwanda vya kuongeza thamani ya madini nchini.

“Niwasihi Watanzania wote hasa wale wanaofikiria kuwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi ndizo zenye ubora kuliko za hapa nchini, kuachana na dhana hiyo potofu, kwani bidhaa zetu ni bora na zina viwango vinavyostahili.”

Amesema wakizalisha bidhaa kwa kutumia malighafi za ndaniitawezesha ajira endelevu kuwepo kwa vijana, itasaidia malighafi kutoharibika lakini pia bidhaa zitakazozalishwa zitakuwa na thamani kubwa badala ya kuuza malighafi kwa bei ya chini.

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda ili kuifikisha nchi kwenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Amesema uanzishwaji wa viwanda umejikita zaidi katika uongezaji wa thamani wa mazao ya kilimo na maliasili yanayopatikana nchini, kama, kilimo, mifugo, misitu, uvuvi na madini kwani wananchi wengi wanategemea mazao na rasilimali hizo kwa maisha yao.

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuhimiza uongezaji thamani wa mazao husika kwa kuwa ndiyo njia sahihi. “Kwa misingi hiyo, usindikaji, uchakataji na uchenjuaji, vitachangia kupunguza upotevu unaotokea msimu wa mavuno, kuongeza ajira na thamani ya mazao kwa lengo la kuwapatia wazalishaji kipato.”

Amesema uongezaji thamani utahitaji teknolojia (mashine na ujuzi), ambapo baadhi ya teknolojia hizo zimeoneshwa kwenye maonesho hayo. “Vilevile, maonesho hayo yametoa fursa ya kuonesha teknolojia zinazoweza kurahisisha uzalishaji na kuleta ufanisi zaidi ili kuongeza tija na kuhimili ushindani katika soko la ndani na nje.”

Mapema, akitoa taarifa kuhusu maonesho hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SIDO, Prof. Elifas Bisanda alisema wamekuwa wakiandaa maonesho hayo ili kuwahamasisha wajasiriamali wadogo na wa kati wapate mbinu mpya juu ya viwanda vidogo.

"Pia tumekuwa tukifanya maonesho haya ili kuwapa wananchi uelewa kuhusu bidhaa zinazozalishwa nchini. Tangu mwaka 2006, yalikuwa yakifanyika kikanda, lakini kwa sasa yanafanyika kitaifa," alisema.

Alisema kupitia maonesho hayo, wajasiriamali hupata mafunzo ya ufungashaji wa bidhaa lakini pia hupata fursa ya kubadilishana uzoefu miongoni mwao na kupata taarifa kutoka kwenye taasisi zinazojihusisha na viwanda vidogo na vya kati.

Alisema anaiomba Serikali iwapatie fedha zaidi ili waweze kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa ikizingatiwa kuwa Serikali imepeleka umeme hadi vijijini lakini wananchi wengi hawanufaiki na uwepo wa umeme huo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi alisema hii ni mara ya pili maonesho hayo yanafanyika mkoani humo.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe , kufungua maadhimisho ya Wiki ya Viwanda Kitaifa, kwenye uwanja wa Bombadia mjini Singinda, Oktoba 7. 2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na Mkewe, Marry Majaliwa (kulia) akifafanuliwa jambo na Afisa Masoko Mwandamizi wa TBS, Gladness Kaseka, wakati alipotembelea mabanda, katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Viwanda Kitaifa, yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bombadia mjini Singinda, Oktoba 7. 2019. Kushoto ni Afisa Mkaguzi TBS, Domisiano Rutahala. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mbegu ya kisasa ya alizeti, kwenye banda la Chama cha Wasindikaji Mafuta wa Mkoa wa Singida (SISUPA), wakati alipotembelea mabanda, katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Viwanda Kitaifa, yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bombadia mjini Singinda, Oktoba 7. 2019. Anayetoa ufafanuzi (katikati) ni Mwenyekiti wa Wasindikaji hao, Juma Mene. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia viatu, vinavotengenezwa SIDO, wakati akitembelea mabanda katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Viwanda Kitaifa, yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bombadia mjini Singinda, Oktoba 7. 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Meneja wa Kituo cha Kuendeleza Teknolojia (SIDO), Arthur Ndedya, wakati akitembelea banda la SIDO, katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Viwanda Kitaifa, yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bombadia mjini Singinda, Oktoba 7. 2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na Mkewe, Marry Majaliwa (wapili kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stela Manyanya, wakati akiwasili kwenye uwanja wa Bombadia Singinda, kufungua maadhimisho ya Wiki ya Viwanda Kitaifa, Oktoba 7.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Wiki hii ya huduma kwa mteja Airtel yatangaza punguzo la simu za Smartphone la hadi elfu 35 katika maduka yake yote

$
0
0
Airtel wiki ya huduma kwa mteja yaja na punguzo kabambe la simu katika maduka yake
Airtel yaja kauli mbiu 'Thamani ya Mteja ni huduma' kwa kushusha bei ya Simu za Smartphone 

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel katika wiki hii ya huduma kwawateja imetangaza kuwa wataendelea na dhamira yake kuu ya kutoa huduma bora za kidigital huku wakisimamia kauli mbiu yao ya ‘Thamani ya mteja ni huduma’ kwa kushusha bei ya simu za Smartphone katika maduka yao yote nchini ndani ya wiki hii.

Mkuu wa kitengo cha huduma kwa Mteja Adrina Lyamba alisema “Airtel katika wiki hii ya huduma kwa wateja kama kawaida yetu tunaungana na watoa huduma wote katika shamra shamra za wiki yetu inayoanza tarehe 7 hadi tarehe 11 mwezi Oktoba na kuadhimishwa duniani kote,

“Mwaka huu kauli mbiu ni ‘The Magic of Services’ kwetu inamaana kuwa ‘Thamani ya Mteja ni huduma bora’

“Wiki hii tunawatangazia wateja wetu punguzo la simu za mkononi la hadi elfu thethini na tano (35,000)  ili waendelee kufurahia kuwa ndani ya familia ya Airtel Mtandao bora wa Smartphone ‘The Smartphone Network’ alisema Bi, Lyamba

“Yaani, Tunalenga kuendelea kuwapa wateja wote huduma bora zaidi na zinazotoa suluhisho la haraka kwa kila hitaji la mteja” Sisi Ni Mtandao Bora wa huduma za Smartphone’ alifafanua Lyamba

Bi Lyamba aliendelea kusema “Katika kuadhimisha wiki hii, Airtel Tanzania tunatoa shukrani zetu kwa  wateja wote wanaotumia huduma zetu, Pia tunawakaribisha katika maduka yetu ya huduma kwa wateja zikiwemo Airtel Money Branch zetu zote zaidi ya 1000 nchini  ili kuendelea kujipatia huduma bora ikiwa ni pamoja na kusajili laini kwa mfumo wa alama za vidole (Biometria) au kupata huduma mbali mbali”

Katika wiki hii ili kujipatia huduma bora kama vile kusajili laini mpya, kujipatia simu na vifaaa vya mawasiliano original kwa bei nafuu na kutakuwa na ofa kabambe maalum kwa ajili yako Bi Lyamba alisema “watoa huduma wote wataeleza jinsi yakutumia huduma zote ikiwemo tuma pesa BURE na Airtel Money, Airtel Yatosha bando, huduma ya kukopa kwa Airtel Money yaani Timiza na nyinginezo nyingi.

 Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba akimlisha keki mmoja kati ya wateja wa Airtel aliyetembelea duka la Airtel morocco jijini Dae salaam bi, Pili Mgunda kwa niaba ya wateja ikiwa ni ahadi ya Airtel kuendelea kutoa huduma bora na zakibunifu. Airtel wiki hii ya huduma kwa wateja wamejipanga kuendelea kutoa huduma kwa ubunifu zaidi ili kuonesha thamani ya Mteja kupitia huduma zake zote.
 Mmoja kati ya wateja wa Airtel aliyetembelea duka la Airtel morocco jijini Dae salaam bi, Pili Mgunda akimlisha keki Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba ili kumshukuru kwa niaba ya wateja wengine kwa hudumia nzuri. Airtel wiki hii ya huduma kwa wateja wamejipanga kuendelea kutoa huduma kwa ubunifu zaidi ili kuonesha thamani ya Mteja kupitia huduma zake zote.
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba akishirikiana na baadhi ya wateja wa Airtel kukata keki leo ikiwa ni ishara ya kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja inayoanza tarehe 7 hadi tarehe 11 mwezi Oktoba na kuadhimishwa duniani kote, “Mwaka huu kauli mbiu ya dunia ni ‘The Magic of Services’ ambapo kwa Airtel inamaana kuwa ‘Thamani ya Mteja ni huduma bora’

LUKUVI AAHIRISHA SHEREHE ZA SIKU YA MAKAZI NA KUAGIZA FEDHA ILIYOTENGWA KUBORESHA MAPATO YA SEKTA YA ARDHI

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameahirisha sherehe za maadhimisho siku ya Makazi Dunia na kuagiza fedha iliyopangwa kwa ajili ya sherehe hiyo shilingi milioni 23 kutumika kuboresha mfumo wa mapato na utoaji huduma za ardhi.

Katika salamu zake za siku ya Makazi Duniani yenye kauli mbiu ‘Matumizi ya Teknolojia Bunifu Kubadili Taka kuwa chanzo cha Mapato’ Lukuvi ametaka maadhimisho ya mwaka huu kutofanyika sherehe na badala yake yatumike kutafakari kauli mbiu ya na kujipanga upya kutekeleza agizo la rais alilolitoa muda mrefu la kuwataka wananchi kujitolea kufanya kazi za usafi katika maeneo ya miji na wanayoishi.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inaelekeza kutafakari kwa kina namna changamoto ya uwepo wa taka mijini kuwa fursa ya kujiongezea kipato kwa kutumia teknolojia rahisi.

Alisema, mwaka huu inaelekezwa kuingia kwa undani zaidi kutumia ubunifu kubadili taka kuwa mtaji na kuongeza kipato kwa wananchi bila kuathiri afya za wakazi wa mijini na mazingira na hatimaye kupunguza gharama za udhibiti taka.

 ‘’Mamlaka za miji zina wajibu wa kukusanya taka kama mojawapo ya huduma wanazotakiwa kuzitoa kwa wananchi na kwa upande mwingine wananchi wanao wajibu wa kulipia huduma hiyo kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha mamlaka za mitaa’’ alisema Lukuvi.

Aliwaasa wananchi kuepuka kutupa taka kando ya mito , maeneo ya wazi , barabarani na katika mitaro ya maji ya mvua kwa kuwa kufanya hivyo kunasababisha uharibifu wa mazingira , kuziba kwa mitaro ya maji ya mvua  na kutengeneza mafuriko.

Aidha, ameaalika wadau wote wenye teknolojia rahisi ya kuchakata taka ngumu kushirikiana na mamlaka za miji nchini ili kutumia ujuzi huo kupambana na changamoto ya wingi wa taka ngumu na kwa njia hiyo wataweza kutengeneza ajira kwa jamii huku miji ikiendelea kuwa safi na afya za wananchi kuimarika.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Makazi Duniani (UN Habitat) kupitia azimio Namba 40/202 la Baraza la Umoja wa Mataifa la mwezi Desemba mwaka 1985 limetenga jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba ya kila mwaka kuwa siku ya Makazi Duniani. Kwa mara ya kwanza maadhimisho hayo yalifanyika jijini Nairobi, Kenya mwaka 1986. Mwaka huu Maadhimisho hayo yanafanyika kimataifa katika jiji la younde Cameroun.
Viewing all 120208 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>