Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

HOME GYM MWENGE YASHEREHEKEA MIAKA 17 TANGU KUANZISHWA

$
0
0
 Washiriki wa Jogging iliyoandaliwa na kituo cha mazoezi ya viungo cha Home Gym Mwenge jijini Dar es Salaam kilichopo chini ya Andrew Mangomango (kulia) kwa lengo la kuhamasisha umuhimu wa mazoezi kwa ajili ya afya ya mwili na akili ambapo kituo hicho kimetimiza miaka 17 tangu kuanzishwa, mbio hizo zilianzia Mlimani City na kuishia ufukwe wa Escape One. (Picha na Francis Dande) 
 Washiriki wakiwa katika Jogging.

 Washiriki wakiwa katika Jogging.
Wanachama wa kituo cha mazoezi ya viungo cha Home Gym Mwenge wakikata keki wakati wa kusherehekea mika 17 tangu kunzishwa kwa kituo hicho, hafla hiyo ilifanyika katika Ufukwe wa Escape One jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mazoezi ya Viungo cha Home Gym Mwenge cha jijini Dar es Salaam (kulia) akilishwa keki na mke wake wakati wa hafla ya kutimiza miaka 17 tangu kuanzishwa kwa kituo hicho.

NYUMBANI NA DIASPORA TBC1- EPISODE TEN

MAKAMU WA RAIS MOHAMED GHARIB BILAL AHUDHURIA KUWEKWA WAKFU ASKOFU KENEN PANJA MJINI TUKUYU LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Songwe mkoani humo leo Sept 20,2015 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu mteule  wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim  Pannja zilizofanyika katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu  Mkoani Mbeya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia waumini wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini kwenye sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu mteule wa Kanisa hilo Mchungaji Kenan Salim  Panja iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo wa Tandale mkoani Tukuyu Mkoani Mbeya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na kumpongeza Askofu mteule wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim  Panja wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu  Mkoani Mbeya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Askofu wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Kenen Salim Panja baada ya kumalizika kwa Misa na Ibada maalum ya kuwekwa wakfu Askofu huyo iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu Mkoani Mbeya.
Wasanii wa kwaya ya Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo kuu la kusini wakitoa burudani wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu Kenen Salim Panja iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu  Mkoani Mbeya. Picha na OMR.

MSUMAJI WA SIMBA HAJI SUNDAY MANARA AWAPONGEZA WAPENZI WAO

$
0
0
Wapendwa wana-Simba wenzangu,
Ninawaandikia ujumbe huu makhsus kuwashukuru kwa mara nyingine kwa kazi nzuri mliyoifanya uwanjani Leo kwa kuishangilia timu yenu mwanzo mwisho kwenye mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Taita.
Mimi  naamini bila ya support yenu Simba haiwezi kufanya vizuri hata siku moja.


Pia kwa niaba ya uongozi wenu tunawashkuru sana wapenzi wetu ambao  hawakujaaliwa kufika uwanjani hii leo. Sisi tunaamini dua na sala zao zmesaidia kutupa nguvu hii leo na kupata points tatu muhimu.
Na kwa umuhimu wa pekee tuwapongeze sana wachezaji wetu na bench la ufundi kwa kazi kubwa wanayofanya ya kutupa furaha.hakika hiki ndio wanasimba wanachotaka
Mwisho niwaombe sana.sote wiki hii tuwekeze akili yetu tarehe 26 yaan wiki ijayo.mnajua tuna mechi ngumu dhidi ya watani zetu. Kwa upande wa uongozi umejipanga kwa kila hali kuhakikisha tunashinda game hyo.iwe jua.iwe mvua yanga hawatoki Taifa Jumamosi ijayo.
Wapenzi wetu, tunawaomba sana umoja na mshikamano wenu kuelekea game ya Jumamosi.
Kila mmoja ruksa kufanya awezacho kuhakikisha tunawalaza tena mapema vibonde wetu.Narudia RUKSA.
Mwisho ingawa si  kwa umuhimu niwashukuru wanahabari wote kwa kazi nzuri waifanyayo ya kutuhabarisha habari za mnyama.

Reclaiming our glory
Simba nguvu moja

Imeandikwa na mtumishi wenu
Haji S.Manara

Msemaji wa SSC

MABASI 138 YA MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (DART) YAWASILI BANDARINI DAR ES SALAAM

$
0
0
TATIZO la usafiri katika jiji la Dar es Salaam linatarajia kupungua kufuatia kuanza kupindi cha mpito cha mabasi Yaendayo Haraka (BRT) mwezi ujao kufuatia kuwasili kwa mabasi 138 katika Bandari ya Dar es Salaam kutoa China tayari kwa huduma ya usafiri. 

 Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki aliwaambia waandishi wa habari jana wakati alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kujionea kuwasili kwa mabasi hayo, kuwa wakazi wa Dar es Salaama kwa sasa wataanza kutumia usafiri wa mabasi hayo. 

 “Tumefikia hatua nzuri na naipongeza Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT) kwa kuleta mabasi hayo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hii ya usafiri katika kipindi cha mpito," hii itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji hili", alisema na kuongezeas kuwa kampuni hiyo imepewa jukumu la kuendesha kipindi cha mpito ili waweze kupata uzoefu na zabuni ya mwendesha mradi kipindi cha kudumu itakapo tangazwa itasaidia wao kushindana. 

 Alisema serikali ilifanya kazi kubwa kuwainganisha Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wamiliki wa daladala na baadaye kuanzisha kampuni ya UDA-RT. 
 Aidha alikanusha kuwa nauli za mabasi hayo imepangwa kuwa Tsh. 900 zilizotolewa katika mitandao ya jamii, na kusema huo ni uzushi na upotoshaji na aliyefanya hivyo anatafutwa ili sheria ichukue mkondo. 
 Alisema suala la nauli linahusisha ushiriki wa taasisi mbalimbali chini ya Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) hivyo uzushi huo umewaletea usumbufu mkubwa wakazi wa Dar es Salaam hivyo wanatakiwa kuwapuuzia. 

Msemaji wa Kampuni ya UDA Rapid Transit(UDA-RT),Bw,Subri Maburuki alisema mabasi yote yameingia yakiwemo ya mita 12 yapo 101 na mita 18 yapo 39 na huduma ya usafiri kipindi cha mipito itanza baada ya kukamlisha taratibu za bandari. 

 “Tuliahidi kuwa mwezi huu wa tisa mabasi yatakuwa yamewasili na ni keli yamemekuja,” na kwa pamoja na yale ya kufundishi yatakuwa jumla mabasi 140", alisema Bw. Maburuki na kufafanua kwamba mabasi hayo yametokea kiwandani China na yanakidhi miundombinu ya barabara ya mradi wa BRT kama walivyokubaliana. 

 Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw.Hebel Mhanga alisema meli iliyobeba mabasi hayo ilipitia Kenya na kimsingi ilitokea China ilikuwa imebeba magari 1700 yakiwemo mabasi ya UDA-RT. 

 “Hatua hii ni ya msingi kwa nchi yetu, itasaidia wakazi kusafiri kwa urahisi na haraka,”alisema Bw. Mhanga. UDA-RT ni kampuni iliyoundwa na wazalendo kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri katika barabara ya DART jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki (kulia) akiwa katika bandari ya Dar es Salaam alipofanya ziara ya  kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) tayari kuanza kwa kuanza huduma ya kipindi cha mpito mwezi ujao. Kushoto ni Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw.Hebel Mhanga, wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni UDA Rapid Transit (UDA-RT),Bw. Robert Kisena ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wa pili kushoto ni Msemaji wa Kampuni hiyo,Bw, Sabri Maburuki.
 Sehemu ya  mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) yaliyowasili katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya usafiri katika kipindi cha mpito kwenye miundombino ya mfumo wa mabasi yaendayo haraka (BRT)kuanzaia mwezi ujao
 Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akijaribu basi la Mradi wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam  kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika Kipindi cha mpito
Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akishuka katika basi la Mradi wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam  kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika kipindi cha mpito.

CHATO YAZIZIMA WAKATI MAELFU WAKIHUDHURIA MKUTANO WA KAMPENI WA DKT. MAGUFULI LEO

$
0
0
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akifafanua jambo kwa msisitizo mkubwa wakati akiwahutubia wakazi wa Chato na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika uwanja wa shule ya sekondari Chato mkoani Geita.
  Wakazi wa Chato na Vitongoji vyake wakifuatilia na kusikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba ridhaa mbele yao jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari chato mkoani Geita.
 Wakazi wa Chato wakishangilia kuonesha kuwa watampa kura za ushindi Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Chato na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato mkoani Geita.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Chato,Dkt Meedad Kalemani mbele ya wakazi wa Chato waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita.
  Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
 Wakazi wa Chato ilikuwa ni shangwe tu kila kona ya uwanja.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita ,Joseph Kasheku almaarufu King Msukuma akiwaomba ridhaa wananchi wa Chato ya kumchagua Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli ili aweze kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano.
 Wakazi wa Chato wakishangilia kwa shangwe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Chato na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika katika shule ya sekondari Chato mkoani Geita.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Chato mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita.

President Kikwete at UN High level panel on Global Response to Health Crises briefing to member states

$
0
0
The Chairman of the UN High level panel on Global Response to Health Crises President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete briefs delegates of member states during a consultative session in New York over the weekend with Other panel members including  Celso Amorim from Brazil, Micheline Calmy Rey from Switzerland, Marty Natalegawa from Indonesia, Joy Pumaphi from Botswana and Rajiv Shah from the US
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete briefs delegates of member states during a consultative session in New York over the weekend 
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete briefs delegates of member states during a consultative session in New York over the weekend. Photos by Freddy Maro

Mama janeth magufuli akonga nyoyo za watanzania ndani na nje ya nchi

$
0
0
 Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua mumewe Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kwenye  uchaguzi mkuu unaotarajiwa wa Oktoba 25 mwaka huu. 
Mara bada ya kuhutubia chumba chetu cha habari kilihemewa na simu za wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kuelezea furaha yao sio tu kwa kumuona jukwaani bali pia kwa kuongea kwa kujiamini. Mama Magufuli amekuwa haonekani sana kwa sababu ya kuuguza mgonjwa nyumbani kwao Chato. Wamesema wametiwa moyo sana na haiba ya Mama Magufuli na wameshangazwa kwa uwezo wake mkubwa wa kuongea mbele za watu bila woga na bila kumung'unya maneno. 
Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu.
 Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akipeana mkono na Mgombea Ubunge wa jimbo la Chato,Dkt Meedad Kalemani mara baada ya kuwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano 
Wananchi wa Chato wakimshangilia Mama Magufuli kwa shangwe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato  mkoani Geita.

Moto mkubwa wazuka mlima meru mkoani arusha

$
0
0
Moshi mkubwa umetanda katika anga ambapo Kuna taarifa kuwa Eneo la hifadhi ya Mlima Meru Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha linawaka moto. Chanzo cha moto huo, ambao unasemekana ulianza jana, bado hakijafahamika. Tunaendelea kufuatilia taarifa hii na tutawajuza zaidi mara tupatapo habari za uhakika kutoka eneo la tukio.
Usiku huu

SHINE A LIGHT - HUC BOOK DONATION TO MSAMARIA CENTER FOR STREET CHILDREN MOSHI

$
0
0
Shine A Light :This is a group founded by KCMC (Kilimanjaro Christian Medical College)students in June 2010 aimed at helping children who are less fortunate achieve their dreams, have a chance at life and a bright future .
 If you feel you can participate or support us in any way or means (currently based in Moshi, Tanzania), Contact us: email-sal.kcmc@gmail.com Shine a Light under the sponsorship of Help For Undeserved comminities (HUC) based in the USA delivered 85 primary school textbooks to the msamaria center for street children in moshi . Shine A Light would like thank HUC and look forward to working with them again in the near future to support our local communities .



CHAMA CHA AFYA YA JAMII (TPHA) CHATOA ELIMU DHIDI YA KUPAMBANA NA TUMBAKU KWA VIJANA WADOGO DAR

$
0
0
Mratibu wa Mradi wa Madhara ya Tumbaku (TPHA) Dk. Bertha T.A. Maegga akizungumza wakati akifungua kongamano hilo lililo washirikisha wadau mbalimbali kwa kutoa muhutasari wa Madhara ya Tumbaku. (Picha na Geofrey Adroph).
Na Andrew Chale, modewjiblog [Dar es Salaam] 
CHAMA cha Afya ya Jamii nchini (TPHA), kimeendesha kongamano maalum kwa wanafunzi wa shule msingi zaidi ya Saba ndani ya Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kutoa elimu ya madhara yatokanayo na utumiaji wa bidhaa za Tumbaku pamoja na kujikinga na athari zake mbaya baadae.

 Akielezea katika kongamano hilo, Afisa wa TPHA ambaye pia ni msimamizi na mtaafiti wa masuala ya kupambana na madhara ya Tumbaku, Dk. Bertha Maegga amebainisha kuwa, kwa sasa Chama hicho kinaendesha mradi uliopewa jina la “80 CHILDREN STRONG” ukitoa elimu kwa vijana wadogo wenye umri wa miaka 10-14, hasa wa shule za msingi.

 Dk. Maegga akihutubia umati wa wanafunzi wa shule hizo saba katika kongamano hilo lililofanyika shule ya Msingi Kijitonyama Visiwani, aliwataka wazazi, walimu, walezi na jamii kuwalinda na kukemea watoto wao kuachana na vitendo vya matumizi ya bidhaa za Tumbaku ikiwemo sigara, ugoro, shisha na Tumbaku yenyewe.

 Aidha, amebainisha kuwa, wameweza kulenga kundi hilo kutokana na kuwa na changamoto za kiukuaji wa kiakili na kisaikolojia. “Umri huu kuna utundu na utukutu mwingi na akili nazo bado hazijakomaa kuepuka ushawishi wa namna mbalimbali ukiwemo na wa matendo yasiyofaa katika maisha yao ya baadaye. Tukiweza kuwalinda katika umri huo. watabaki salama hadi watakapojitambjua nafsi zao na kuamua mambo ya busara na salama katika maisha yao ya baadae” alibainisha Dk. Maegga.
Mshauri wa masuala ya Afya na Familia, mgeni rasmi Dk. Ali Mzige akizungumza kwa kutoa elimu kwa miongoni mwa watu walio weza kuhudhuria kongamano hilo la uelimishaji kuhusu Tumbaku na matumizi ya yanayotokana na bidhaa za Tumbaku.Kwa upande wake, Dk. Ali Mzige mganga wa hospitali ya kimataifa ya Afya ya uzazi ametoa elimu kwa vijana hao na kubainisha kuwa sigara, tumbaku, shisha, ugoro na kuberi ni hatari kwa afya za mwili huku ikisababisha magonjwa mbalimbali.


Miongoni mwa magonjwa hayo yatokanayo na matumizi ya sigara ambapo wanaoathirika zaidi ni vijana kwa sababu ya kufuata mkumbo pamoja na kuhisi kwamba uvutaji wa sigara unaongeza sifa ya kuwa mwanaume kamili kitu ambacho si kweli.

Changamoto kubwa ni kwamba serikali imeshindwa kudhibiti watengenezaji wa Sigara kwa sababu wanapata kodi kutoka katika viwanda vya sigara japokuwa mapato ni madogo kuliko madhara.“Sigara ina kemikali 4000 ambazo zina uwezo wa kusababisha magonjwa zaidi ya 40, ambayo ni pamoja na ugonjwa wa moyo, kisukari, na saratani ya mapafu, saratani ya kinywa na mengine mengi.Tumbaku na Sigara zote zimekuwa na madhara yanayofanana.

 Tumbaku imekuwa ikitumika hasa maeneo ya vijijini na sigara watumiaji wengi wanatoka mjini” alieleza Dk. Ali Mzige.Kwa upande wao wanaharakati wa kupambana na matumizi ya sigara kutoka chuo cha Tiba Muhimbili, kupitia taasisi yao ya African Fight Cancer, Bernard Temba amewaelezea wannafunzi hao kuwa, ni wakati wa kuepuka vishawishi dhidi ya watu wanaotumia sigara kwani wasipofanya hivyo wataweza kupata madhara makubwa ya kiafya.
Mwalimu Margareth William mshereheshaji katika siku hiyo ya kongamano la uelimishaji vijana kuhusu Tumbaku na madhara yatokanayo na bidhaa zake. 

Naye Mratibu wa Elimu Kata ya Makumbusho ambaye pia alikuwa mgeni katika kongamano hilo, alitoa wito kwa walimu na wazazi kuwa waangalifu kwa watoto wao ikiwemo kufuatilia nyendo zao mara kwa mara ili kuwakinga na vishawishi hivyo vya matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku kwani zina madhara makubwa hasa kwa afya za watoto wadogo.

Mradi huo wa ’80 Children Strong’, unaosimamiwa na Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) unafadhiliwa na Shirika dogo la Conquer Cancer Foundation ambalo linahusiana na American Society for Clinical Oncology (ASCO) ya nchini Marekani (Chama cha kitabibu cha masuala ya uchunguzi wa tiba ya saratani. 

Hata hivyo, TPHA imedhamiria kuwa kila mtoto anapata haki ya kuelimishwa kujikinga na matumizi hayo mabaya ya tumbaku, ambapo kwa darasa la watoto 80, asiwepo hata mmoja atakayeingia kwenye viashiria vibaya vya matumizi ya tumbaku hivyo wataendelea kutoa elimu hiyo sehemu mbalimbali nchini.Kwa upande wa shule hizo zilizohudhuria kongamano hilo ni pamoja Shule ya Msingi Mapambano, Kijitonyama Visiwani, Victoria, Mwananyamala B, Mwananyamala Kisiwani, Mashujaa, Shekilango na Mapambano.Kwa upande wa watoto hao walipata pia wasaha wa kuuliza maswali na kupatiwa majibu huku pia kukifanyika na masuala ya maigizo, ngoma, shahiri na ngonjera zilizokuwa na jumbe mbalimbali za kupambana na matumizi ya tumbaku.
Wanafunzi wakisoma na kuelekezana jarida lililochapishwa mahususi kwa ajili ya kuelimisha matumizi mabaya ya Tumbaku. DSC_0019
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka mashirika na vyuo mbalimbali.
Kikundi cha majigambo ya jukwaani (ngonjera) kikitoa ujumbe kwa wageni waalikwa pamoja na wanafunzi wenzao kuhusiana na kupambana na kudhibiti matumizi hatari ya Tumbaku.
Wanafunzi wakionesha vipaji vyao vya kuigiza kwa kuelimisha kuhusiana na na madhara ya Tumbaku na ni namna gani ya kuweza kujikinga.
Bernard Temba kutoka Chuo cha Afya cha Muhimbili akitoa somo kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizohudhuria kongamano hilo lililofanyiaka katika shule ya Msingi ya Kijitonyama Kisiwani
Shairi mahususi likiimbwa na wanafunzi hao likiwa limebeba ujumbe wa kijana jiepushe na matumizi ya Tumbaku na bidhaa zitokanazo na Tumbaku.
Mwanafunzi wa darasa la tano, Tadei Ladislausi kutoka shule ya msingi Shekilango (kulia)akisoma madhara yanayo wakumba watumiaji wa Tumbaku.
Wawili kulia ni wanafunzi kutoka Chuo cha Afya Muhimbili, kushoto ni wanafunzi wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani wakiwa wanasikiliza kwa makini maada zilizo kuwa zikiendelea katika kongamano hilo.
Wanafunzi wakiuliza maswali kwa watoa mada inayo husiana na afya kwa kijana na kuepuka matumizi mabaya ya Tumbaku
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani, Bw. Charles Nombo akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali walioweza kuhudhuria katika kongamano hilo.
Mjumbe wa Chama cha Afya ya Jamii Bi. Elizabeth Nchimbi akitoa nasaa kwa vijana walioweza kuhudhuria na wale walioko nje wasiweze kutumia Tumbaku kwani ni hatari kwa afya za binadamu
Waandhishi wa habari wakiwa kazini.
Afisa Elimu kata ya Kijitonyama, Mwalimu Shangwe Temba akifunga kwa kutoa neno kwa vijana kuacha kujiingiza katika makundi mbalimbali kwani ndio yanayo pelekea vijana wengi kuhamasika na kuanza kutumia Tumbaku ambayo huwaletea vijana wengi matatizo hususani kwa wanafunzi kuacha shule kwa kuugua vifua vikuu na magonjwa mengine mengi
Picha ya umoja wa kikundi cha wanafunzi kinacho elimisha matumizi mabaya ya bidhaa zinazotokana na Tumbaku.

MTANDAO WA KWANZA WA MAGARI TANZANIA cheki.co.tz WATIMIZA MWAKA MMOJA

$
0
0
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara katika maonyesho ya magari akisaini kwenye kitabu cha wageni katika banda la Cheki.co.tz mara baada ya kuwasili katika kiwanja cha Biafra jijini Dar wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya magari na bidhaa shirikishi ya Auto Fest.

Tarehe 19 Mwezi wa septemba 2015 Mtandao wa magari unaoongoza nchini Tanzania Cheki.co.tz umetimiza mwaka mmoja wa utoaji huduma ya kipekee na iliyo salama ya biashara ya kuuza na kununua kwa njia ya mtandao pande zote za Tanzania. 

 Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa utendaji wetu, maelfu ya watu wamekuwa wakitembelea tovuti yetu kila siku na maelfu ya magari yamenunuliwa.

 Msingi wetu wa wateja umeongezeka mara 21% tangu uzinduzi . 90% ya wafanyabiashara wa magari nchini utumia mtandao cheki.co.tz kuuza magari yao na zaidi ya 50 ya majengo ya kuuzia magari nchini yana nembo ya Cheki.co.tz katika sehemu zao “Nayaweka mafanikio yetu katika mambo mawili: Kwanza, unatokana na urahisi wa kununua, kwani tumewezesha wateja kununua gari wakati wowote, na mahali popote wanapohitaji. 

Sababu ya pili, ni mahusiano mazuri na wauzaji wa magari uliotokana na ubora wa biashara” alisema Bwana Mori Bencus, Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania.

Naye Juliana Ntemo, Msaidizi wa Masoko wa Cheki.co.tz alisema, “ tuna shauku ya kuboresha zaidi huduma yetu kwa miaka ijayo kwa kuendelea kutoa huduma ya uuzaji na ununuzi kwa njia ya mtandao iliyo salama na ya kipekee kabisa”.

Ushuhuda wa kipekee kutoka kwa wateja kwa mwaka 2015 Cheki wameturahisishia biashara, tunapata wateja kutoka nchi nzima.Wateja wanaingia moja kwa moja cheki.co.tz na kuona magari yakiwa na maelezo muhimu,na kama mtu anahitaji anawasiliana nasi- Ramadhani Makame, Planet Motors Cheki.co.tz ni duka la kimtandao, ambapo wanunuzi wa magari na wauzaji wa Kitanzania hukutana.

 Ndani ya tovuti hii magari ya kila aina yanapatikana kwa wanunuzi Tanzania nzima huku wauzaji wakipata fursa ya kuuza zaidi. Tembelea www.Cheki.co.tz
Mfanyakazi wa kampuni ya Cheki.co.tz akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kulia) kuhusu ununuaji na hata kuuza gari kupitia mtandao.
Msaidizi wa Masoko wa Cheki.co.tz, Juliana Ntemo (kushoto) akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kulia) wakati wa ufunguzi wa maonyesho.
DSC_0390
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akikata keki ya kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni ya kuuza na kununua magari ya Cheki.co.tz. Kushoto ni Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania Mori Bencus akiwa na Msaidizi wa Masoko wa Cheki.co.tz, Juliana Ntemo (katikati).
DSC_0406
Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania Mori Bencus (kushoto) akimlisha keski mgeni rasmi wa maonesho hayo ambaye ni Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kulia).
DSC_0404
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo(kulia) akimlisha keki Meneja wa Cheki.co.tz nchini Tanzania Mori Bencus baada ya kampuni ya Cheki.co.tz kutimiza mwaka mmoja.
DSC_0405
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akimlisha keki Bw. Ally Nchahaga kwa niaba ya watu wote waliofika kwenye ufunguzi huo.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara katika maonyesho ya magari akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo.
Bw. Ally Nchahaga ambao ni waandaaji wa tamasha la magari Tanzania (Autofest) akizungumza jambo wakati wa ufunguzi huo uliofanyika katika viwanja vya Biafra Jijini Dar.
Mkurugenzi wa CW Net Tanzania, Desmond Andrew(kushoto) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo kuhusu matumizi ya modem za CW Net wakati alipitembelea banda hilo.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kushoto) akitizama modem ya CW Net zinazotengenezwa na watanzania na kutumia laini ya mtandao wowote ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akipata maelezo kutoka kwa Bw. Zohail Hassanali (kushoto) kuhusu uzibaji wa pancha kwenye magari na vifaa gani mtu anabidi kuvitumia.
Bw. Athman Hamis ambaye ni mwakilishi wa Auto Mobile akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo alipokuwa anatembelea mabanda hayo
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maonesho hayo akipata ufafanuzi kuhusu uoshaji wa magari kutoka kwa Afisa Mauzo wa KARCHER, Josephine Scarion.
Mfanyakazi wa Kampuni ya TFL Motor Group, Maria C. Sangiwa (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo kuhusu uuzaji wa magari na hata kufanya service ya magari yote. Katikati ni Khalid Abdallah.
Maonesho ya uendeshaji wa magari yakiendelea katika viwanja vya Biafra jijini Dar. (Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)

SERIKALI YAKIRI CHANGAMOTO LICHA YA MAFANIKIO AJIRA KWA VIJANA

$
0
0
IMG_9847
Meza kuu katika warsha ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF. Kutoka kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Kazi na Ajira kitengo cha Ajira, Joseph Nganga, Mkurugenzi wa Kazi katika Wizara ya Kazi na Ajira, Ally M. Ahmed, Mkuu wa utafiti na machapisho Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga.
(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Na Mwandishi wetu
PAMOJA na kuwepo na maendeleo ya kuridhisha katika suala la ajira kwa vijana, serikali imekiri kwamba ukosefu wa ajira bado ni tatizo kubwa duniani na kwa taifa kwa ujumla.

Kutokana na hali hiyo suala la ajira kwa vijana limebaki kuwa ajenda kuu nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kazi katika Wizara ya kazi Ally M. Ahmed wakati akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofanyika hoteli ya Double Tree by Hilton.

Alifanya ufunguzi huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wiza
ra hiyo Eric Shitindi.

Alisema Tanzania inaendelea kukabiliana na tatizo la ajira kutokana na wigo mdogo wa fursa za ajira, tatizo la utaalamu na ukosefu wa uzoefu .

Alisema hata hivyo vijana wanaoamua kujiajiri wenyewe wamekuwa wakikabiliana na tatizo kubwa la mtaji, maeneo ya kufanyia kazi na utaalamu katika ujasiriamali utakaowawezesha kuendesha miradi wanayoibuni.

Alisema kutokana na uwapo wa sera, mipango na miradi ya maendeleo kuhusu ajira kwa vijana inayoendeshwa kitaifa na kimataifa kumekuwepo na dalili njema za kupungua kwa ukosefu wa ajira.

Alisema utafiti wa mwaka 2014 (ILFS) umeonesha kwamba ukosefu wa ajira umepungua kutoka asilimia 11.7 kwa mwaka 2006 hadi kufikia asilimia 10.3 ka mwaka 2014 huku kwa vijana (wenye umri wa miaka 15 hadi 35) ukipungua kutoka asilimia 13.2 kwa mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 kwa mwaka 2014.
IMG_9768
Mkuu wa Utafiti na mchapishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa hotuba ya utangulizi katika warsha ya vijana na ajira iliyofanyika hoteli ya Double Tree by Hilton. 

Katika hotuba yake ya ufunguzi alitoa wito wa washiriki kuangalia kwa undani tatizo la ajira kwa vijana na kutoa mwelekeo utakaosaidia watunga sera kuwa na sera madhubuti kuhusu ajira kwa vijana.

Alisema mafanikio yaliyopatikana hayaondoi ukweli kuwa kuna tatizo kubwa la ajira miongoni mwa vijana na kutokana na mazingira ya sasa ni vyema wadau wa ajira kuangalia kwa undani tatizo la ajira la sasa ili kutoa ushauri wa kukabiliana nalo kwa kipindi kifupi na kirefu.


Shitindi alisema kwamba serikali inafurahishwa na juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali kutafuta majibu ya tatizo la ajira, majibu ambayo alisema yakifanywa vyema yatasaidia sana wataalamu wa serikali kutengeneza sera na kanuni zitakazo kidhi haja.

Alisema ipo haja kwa wachambuzi (watafiti) kuelekeza nguvu zao katika kutafiti soko la ajira ili kusaidia watengeneza sera kuona mahitaji ya soko katika miaka kadhaa ijayo.

Alisema wakati uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia 7 kwa mwaka kwa miaka kumi iliyopita ajira zimekuwa haziendi sambamba na ukuaji wa uchumi na hivyo kuleta maswali mengi ya sintofahamu.

Alisema serikali kwa sasa inataka kuhakikisha kwamba inaboresha upatikanaji wa ajira lakini hilo linawezekana kama taasisi zake zinazotengeneza sera na kuweka mipango zinatambua tatizo na kuona namna ya kuliangalia.

Alisema watafiti wana wajibu mkubwa wa kusaidia serikali kuwezesha vijana kuwa na kazi zenye staha kama sera ya ajira ya taifa inavyotaka.
IMG_9895
Mkurugenzi wa kazi wizara ya kazi na ajira, Ally Msaki Ahmed, akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Eric Shitindi katika warsha ya kitaifa ya ajira kwa vijana iliyofanyika hoteli ya Duble Tree by Hilton. Katika hotuba yake aliwataka washiriki kujadili kwa makini matatizo ya vijana na kutoa suluhu itakayosaidia watendaji kutunga sera na kutoa mwelekeo mpya wa kukabiliana na tatizo hilo.

Alisema kwa kuangalia ukuaji wa kisekta, sekta ambayo sasa hivi inahitaji watu ndio ambayo haina wataalamu wa kutosha na hivyo ukuaji wa sekta hizo kama za mawasiliano hauendi sanjari na utaalamu uliopo katika soko.

Katibu Mkuu huyo alitoa wito kwa watu binafsi na serikali kuhakikisha kwamba wanakabiliana na vikwazo vya ajira kwa kutoa elimu na taaluma ili fursa zionekane na kutumika ipasavyo.

Alisema tija inaweza kuonekana katika ukubwa wa utaalamu, ubunifu na namna mafunzo yanavyowawezesha wanafunzi kuwa na uhakika na kazi wanazotaka.

Alisema ipo haja kwa wadau mbalimbali kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kwamba vijana wanaingizwa katika soko la ajira na tatizo la ajira linapunguzwa.
  IMG_9829
Kiongozi Mpango wa ukuaji na ajira wa taasisi hiyo, Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC), Dk. Arjan de Haan akielezea sababu za taasisi hiyo kuunga mkono tafiti kwa ajili ya kusaidia kupatikana ufumbuzi wa tatizo la ajira katika warsha ya ajira na vijana iliyofanyika Double Tree by Hilton hotel.

Katika moja ya maazimio yaliyotolewa na washiriki vijana, walitaka kuwepo na mabadiliko makubwa katika utoaji elimu, ambapo walisema elimu itolewe kwa Kiswahili lakini pia wanafunzi waandaliwe kuwa wabunifu na kujiajiri.

Aidha wametaka kurejeshwa kwa shule za ufundi na shule maalumu kama ilivyokuwa zamani.

Walisema vijana Wanatakiwa kushiriki katika utengenezaji wa sera na kanuni na si kushirikishwa na kutaka matakwa yao yanastahili kuangaliwa na kuzingatiwa ili mtu ajifunze kila anachoona anaweza kukifanya vyema.
Warsha hiyo ya ajira kwa vijana imewezeshwa na IDRC na kuratibiwa na ESRF na mada mbalimbali ziliwasilishwa ambazo zilichambua masuala ya elimu, elimu ya ufundi, changamoto na fursa za vijana katika ajira.
Aidha kulikuwa na mada za majukumu ya serikali na sera katika kuboresha mchakato wa ajira kwa vijana.
IMG_0011
Mchumi na Mshauri huru Bi. Mahjabeen Haji akiwasilisha mada kuhusu hali ya ajira kwa vijana nchini katika warsha ya vijana na ajira ilyofanyika hoteli ya Double Tree by Hilton, katika mada yake alielezea mazingira ya ajira ambapo elimu katika sekta zinazokua kwa kasi kama Tehama ni kikwazo kikubwa katika kuwezesha ajira kwa vijana.
  IMG_9932
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akijadiliana jambo na Mkuu wa Utafiti na mchapishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene wakati warsha hiyo ikiendelea.
IMG_0154
Mkurugenzi wa Salama Foundation, Shadrack John Msuya akiwasilisha mapendekezo ya vijana juu ya namna ambavyo vipaji, elimu na ubunifu vinavyoweza kutengeneza ajira kwenye maeneo ya Sayansi, Teknolojia, Kilimo na Ufugaji.Moja ya azimio ni kuwa na sera mpya ya vijana yenye mpango mkakati na tafiti zinazotekelezeka katika warsha ya vijana na ajira.
IMG_0180
Mshauri mwelekezi katika uanzishwaji na uendelevu wa biashara na maendeleo ya jamii, Gidufana Gafufen akiwasilisha mapendekezo yaliyowasilishwa katika vikundi nini kifanyike ili vijana wapende kilimo katika warsha ya vijana na ajira iliyofanyika katika hoteli ya Double Tree by Hilton.
IMG_9875
Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau pamoja na makundi ya vijana waliohudhuria warsha ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
IMG_9704
IMG_9952
IMG_9944
IMG_0110
Mmoja wa washiriki akitoa maoni kwenyewarsha ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
   
IMG_0348
 
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
IMG_0354
IMG_0150
Pichani juu na chini ni wadau kutoka Taasisi mbalimbali walioshiriki warsha hiyo wakibadilishana mawazo.
IMG_0130
Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga (kulia) akiteta jambo na baadhi ya washiriki.
IMG_0134
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akifurahi jambo na Mtafiti Mwandamizi ESRF, Dk. Georgina Ole Saibul mara baada ya kumalizika kwa warsha hiyo.

KIDS PLANET PRE SCHOOL - MBWENI JKT IN DAR ES SALAAM

$
0
0
 Introducing Kids Planet pre school at Mbweni JKT. We have experienced and qualified staff who provide our students with a solid early learning foundation supported by state of the art learning facilities in a friendly and safe environment. School is now open and enrolling. Transport is also available. For more information call 0785 570857.
 The school
 Friendly kids play ground and facilities

WENGI WAMZIKA MTOTO WA KIONGOZI WA WAFUGAJI LUGOBARAIS ATUMA SALAMU

$
0
0
Na John Gagarini, Lugoba 
 Wagombea wa nafasi za uongozi hapa nchini wametakiwa kukubali matokeo mara uchaguzi utakapofanyika Oktoba 25 mwaka huu kwani kuna maisha mengine baada ya uchaguzi, na   kuendelea kufanya kampeni zao huku wakiendelea kuhubiri na kulinda amani iliyopo kwani wana nafasi kubwa ya kuwashawishi wafuasi wao wasifanye vurugu au kufanya vitendo vinavyosababisha uvunjifu wa amani. 
 Pia wagombea watakaoshindwa kwenye uchaguzi mkuu wameombwa wakubali matokeo kwani kwenye washindani lazima kuwe na washindwa ili kuondoa hali ya mafarakano kwani kwa wale watakaoshindwa wasipokubali matokeo wanaweza kuleta uvunjifu wa amani. 
 Hayo yalisemwa katika  Kijiji cha Maviayangombe kata ya Lugoba wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na Askofu mkuu wa Dayosisi ya Morogoro ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jacob Mameo Ole Paulo wa Dayosisi ya Morogoro wakati wa mazishi ya mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa wafugaji Laban Moreto, Karokya Moreto (33) ambaye alikuwa mwanajeshi wa kikosi cha 04/691 cha Mtwara. 
 Askofu Ole Paulo alisema kuwa wagombea hao wanauwezo wa kudumisha amani kwa kuhubiri au kuingiza nchi kwenye machafuko endapo watayatumia vibaya majukwaa wakati wa kipindi hichi cha kampeni za uchaguzi. 
 “Wanapaswa kuhubiri amani na kuacha kutumia maneno yatakayo haribu amani ya nchi iliyopo ambayo imedumu kwa kipindi kirefu tangu nchi ilipopata uhuru miaka zaidi ya 50 hivyo itakuwa ajabu ivunjwe kisa kuwania uongozi tu,” alisema Askofu Ole Paulo. 
Alisisitiza kuwa vyama vya siasa vinapaswa kupingana kwa hoja na kwa malumbano ambayo hayana maana bali yanaweza kuleta mitafaruku isiyokuwa ya lazima hasa kwa wale wanaoshindwa kwani wanapaswa kukubali matokeo. 
 Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alisema kuwa amesikitishwa na kifo cha marehemu ambaye alikuwa ni ndugu kwani wamekuwa wakiishi kama familia moja na walikuwa na ushirikiano mkubwa baina ya familia zao. 
 Ridhiwani alisema kuwa kifo hicho ni pigo kwa familia hiyo pia kwa Taifa kwani alikuwa ni mtumishi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na alikuwa mtaalamu wa rada hivyo pengo lake haliwezi kuzibika kikubwa ni kumwombea marehemu. 
Rais Dk Jakaya Kikwete alituma salamu za pole kwa familia hiyo kupitia kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na kusema kuwa anatoa pole na Mungu awape nguvu katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo na yuko pamoja nao. 
 Alisema kuwa Rais alishindwa kuhudhuria msiba huo kwani kwa sasa yuko nje ya nchi lakini pindi atakaporudi ataitembelea familia hiyo kwa ajili ya kuifariji kufuatia kifo cha mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa kabila wafugaji 
 Naye mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mathayo Torongei alisema ili amani iendelee kuwepo ni vema dola ikatenda haki badala ya kupendelea upande mmoja. 
 Marehemu alifariki kwa ajali baada ya gari alilokuwa akiendesha kupasuka tairi la mbele na kusababisha ajali iliyopelekea kifo chake siku ya Septemba 16 mwaka huu huko Mtwara. Ameacha mke na watoto watatu.
 Baadhi ya akinamama ambao ni ndugu wakaribu wakilia
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa limebebwa na wanajeshi ukiwasili makaburini

 Baadhi ya Wazee wakiwa wamekaa kwenye msiba huo huko kijiji cha Maviyangombe Lugoba wilayani Bagamoyo.
 Kulia ni Ridhiwani Kikwete mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga, mkuu wa wilaya ya Nachingwea Pololet Mgema na mgombea ubunge Jimbo hilo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Matayo Torongei wakiwa kwenye msiba huo.
 Askofu Jacob Mameo Ole Paulo akizungumza wakati wa msiba huo.


FREDDY MACHA KUTUMBUIZA ONESHO LA PICHA ZA WATOTO WA KITANZANIA LONDON

$
0
0
Flyer by Evelina Moceviciute 2015 
Mwanamuziki mkazi London, Freddy Macha, anatazamiwa kutumbuiza kwa ngoma na muziki wa gitaa, kwenye tafrija ndogo kutangaza na kuuza picha za watoto wa Kitanzania. Tafrija na maonesho yametayarishwa na wapiga picha watatu wa Kizungu, Amy Read, Evelina Moceviciute na Saraya Cortaville waliofanya kazi za kujitolea Mbeya vijijini mapema mwaka huu. 
Mauzo ya taswira hizo yatatumika kusaidia maisha na elimu ya watoto hao hao waliopigwa picha. Mradi mzima unaitwa "Ahsante Children"...kutukuza na kutangaza lugha ya Kiswahili, Tanzania na wananchi Afrika Mashariki. 

Onesho litafanywa katika mkahawa wa:

The Chapel St Margaret's House, 
21 Old Ford House, 
Bethnal Green, 
Hackney, London E2 9PL. 
Jumapili 4 Oktoba 2015. Saa 11 na nusu jioni hadi 3 usiku. 
HABARI ZAIDI www.freddymacha.com/ Freddy Drums - Germany May 2012- pic by Luis Tome Passarello 
Freddy Macha na ngoma. Picha ya Luis Tome Passarello

CHAMA CHA AFYA YA JAMII (TPHA) CHATOA ELIMU DHIDI YA KUPAMBANA NA TUMBAKU KWA VIJANA WADOGO DAR

$
0
0
Mratibu wa Mradi wa Madhara ya Tumbaku (TPHA) Dk. Bertha T.A. Maegga akizungumza wakati akifungua kongamano hilo lililo washirikisha wadau mbalimbali kwa kutoa muhutasari wa Madhara ya Tumbaku. (Picha na Geofrey Adroph). 

Chama cha Afya ya Jamii nchini (TPHA), kimeendesha kongamano maalum kwa wanafunzi wa shule msingi zaidi ya Saba ndani ya Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kutoa elimu ya madhara yatokanayo na utumiaji wa bidhaa za Tumbaku pamoja na kujikinga na athari zake mbaya baadae. 
Akielezea katika kongamano hilo, Afisa wa TPHA ambaye pia ni msimamizi na mtaafiti wa masuala ya kupambana na madhara ya Tumbaku, Dk. Bertha Maegga amebainisha kuwa, kwa sasa Chama hicho kinaendesha mradi uliopewa jina la “80 CHILDREN STRONG” ukitoa elimu kwa vijana wadogo wenye umri wa miaka 10-14, hasa wa shule za msingi. 
Dk. Maegga akihutubia umati wa wanafunzi wa shule hizo saba katika kongamano hilo lililofanyika shule ya Msingi Kijitonyama Visiwani, aliwataka wazazi, walimu, walezi na jamii kuwalinda na kukemea watoto wao kuachana na vitendo vya matumizi ya bidhaa za Tumbaku ikiwemo sigara, ugoro, shisha na Tumbaku yenyewe. 
Aidha, amebainisha kuwa, wameweza kulenga kundi hilo kutokana na kuwa na changamoto za kiukuaji wa kiakili na kisaikolojia.
“Umri huu kuna utundu na utukutu mwingi na akili nazo bado hazijakomaa kuepuka ushawishi wa namna mbalimbali ukiwemo na wa matendo yasiyofaa katika maisha yao ya baadaye. 
"Tukiweza kuwalinda katika umri huo. watabaki salama hadi watakapojitambjua nafsi zao na kuamua mambo ya busara na salama katika maisha yao ya baadae” alibainisha Dk. Maegga.

TANGAZO LA MIGOGORO YA ARDHI DAR ES SALAAM

$
0
0
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI INAPENDA KUWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA MHE. WAZIRI WA ARDHI ATAPOKEA MALALAMIKO YA WANANCHI WENYE MIGOGORO INAYOHUSU ARDHI KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM TAREHE 22 – 23, SEPTEMBA, 2015 KUANZIA SAA 4.00 ASUBUHI MAKAO MAKUU YA WIZARA. KATIKA TUKIO HILO, MNATAKIWA KUZINGATIA YAFUATAYO;-

1)    TAREHE 22 SEPTEMBA 2015 ATAPOKEA MALALAMIKO YA WANANCHI KWA MANISPAA YA KINONDONI;

2)    TAREHE 23 SEPTEMBA 2015 ATAPOKEA MALALAMIKO YA WANANCHI KWA MANISPAA YA TEMEKE NA ILALA;

3)    MALALAMIKO HAYO YAWASILISHWE NA MUHUSIKA MWENYEWE NA SIYO MWAKILISHI;

4)    MALALAMIKO AMBAYO YAMEKWISHA WASILISHWA MAHAKAMNI HAYATAPOKELEWA. 
KATIBU MKUU


WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA SABA WA KIMATAFA KUHUSU NAMNA YA KUZUWIA MAGONJWA YA ASILI NA ULEMAVU KATIKA NCH ZINAZOLEA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye mkutano wa saba wa kimataifa kuhusu namna ya kuzuwia Magonjwa Asili na Ulemavu katika Nchi zinazoendelea (ICBD) uliofanyika leo Septe 21,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Washiriki wa mkutano wa saba wa kimataifa kuhusu namna ya kuzuwia Magonjwa Asili na Ulemavu katika Nchi zinazoendelea (ICBD) wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akifungua mkutano huo leo Septe 21,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

 Wasanii wa kikundi cha Ngoma Troup wakiburudisha kwenye mkutano wa saba wa kimataifa kuhusu namna ya kuzuwia Magonjwa Asili na Ulemavu katika Nchi zinazoendelea (ICBD) uliofanyika leo Septe 21,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa  mkutano wa saba wa kimataifa kuhusu namna ya kuzuwia Magonjwa Asili na Ulemavu katika Nchi zinazoendelea (ICBD) uliofanyika leo Septe 21,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa saba wa kimataifa kuhusu namna ya kuzuwia Magonjwa Asili na Ulemavu katika Nchi zinazoendelea (ICBD) uliofanyika leo Septe 21,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Picha na OMR

UONGOZI MPYA WA KAMATI YA MISS TANZANIA YAANZA KUSAKA UPYA MAWAKALA WA MIKOA

$
0
0
Kutoka maktaba: Shindano la Miss Tanzania la kwanza mwaka 1967 ambapo mshindi aliibuka Theresa Shayo (No. 5) na ambalo lilikuwa la mwisho baada ya serikali kulipiga marufuku kwa kile kilichoitwa kukiuka maadili ya Mtanzania. Mwaka 2004 Miss Tanzania ikaibuka na mshindi alikuwa Ainda Maeda. Mwaka jana shindano hilo lilifungiwa kwa muda kabla ya Baraza la Sana la Taifa kuruhusu liendelee tena hivi karibuni.
--------------------------------------------------------------
Kamati ya Miss Tanzania inapenda kuwatangazia wadau wote wanaotaka kuandaa Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 kutuma maombi yao ya uwakala kuanzia sasa hadi tarehe 30 Novemba 2015 ndio mwisho wa kupokea maombi hayo. 
Mashindano yatakayo fanyika ni ya mikoa tu, hakutakuwa na mashindano katika ngazi ya wilaya wala Kanda. 
 Sifa za kuwa Wakala wa Miss Tanzania ni pamoja na:

 1) Uwe na Kampuni iliyosajiliwa na Mamlaka husika ya Serikali. 
2) Uwe na mtaji wa kutosha. 
 3) Uwe na uwezo wa kuandaa shindano katika ufanisi mkubwa. 
 4) Uwe mstari wa mbele katika kukuza sanaa za utamaduni nchini. 

 Wakala atakaye pitishwa na Kamati ya Miss Tanzania atapaswa kujisajili Baraza la Sanaa la Taifa.(BASATA) kabla hajapewa kibali cha kuandaa shindano. Wilaya za Mkoa wa D’salaam, Ilala, Kinodoni na Temeke zitapewa hadhi ya Kimkoa, ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Elimu ya Juu. 
 Ada ya Uwakala ni shilingi milioni moja. 
 Ada ya Uwakala italipwa kwa Kamati ya Miss Tanzania baada ya maombi kukubaliwa na kupitishwa. Maombi yatumwe kwa barue pepe misstanzania2015@yahoo.com
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images