Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 982 | 983 | (Page 984) | 985 | 986 | .... | 3285 | newer

  0 0


  Shirika la Viwango Tanzania linapenda kuwatangazia waombaji wa nafasi za kazi zilizotangazwa 25.5.2015 katika kada zifuatazo, kuwa usaili wa mahojiano utafanyika tarehe 28 na 29 Septemba 2015 katika ofisi za TBS, Ubungo Dar es Salaam:-
  1. Standards Officer II (Pharmacy),
  2. Standards Officer II (Microbiology and Chemistry)
  3. Standards Officer II (Animal Science) 
  4. Quality Assurance Officer II (Microbiology with Chemistry)
  5. Quality Assurance Officer II (Laboratory Science and Technology)
  6. Inspector II (Food & Biochemical Engineering)
  7. Quality Assurance Officer II (Food & Biochemical Engineering) 
  8. Quality Assurance Officer II (Petroleum and Gas)
  9. Metrologist II (Legal and Industrial Metrology)
  10. Metrologist II (Physics)
  11. Chief Procurement Officer
  Tafadhali bofya hapa kupakua nakala ya orodha 
  ya walioitwa na taarifa zaidi za mambo ya kuzingatia.

  0 0

  Na Mwene Said wa
  Blogu ya Jamii

  Kulia ni msanii wa Nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha (32) aliyekuwa anakabiliwa na mashitaka ya ubakaji leo  aliachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, baada ya ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo. 
   Mbasha ambaye pia ni mume wa msanii wa nyimbo za injili nchini, Flora Mbasha, alipiga magoti na kuangua kilio nje ya mahakama baada ya kusomwa hukumu hiyo iliyomwachia huru dhidi ya tuhuma za ubakaji. 
  Hukumu hiyo ilisomwa jana saa 4:45 hadi saa 5:15 asubuhi na Hakimu Mkazi Flora Mgaya wa mahakama hiyo. 
   Hakimu alisema baada ya ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa Jamhuri na ushahidi wa mshtakiwa, mahakama imeona bila kuacha shaka hautoshelezi kumtia hatiani. 
   Alisema mahakama yake inamwachia huru mshtakiwa Mbasha. Mbasha alitoka kasi kwenye chumba cha mahakama na kupiga magoti huku akili kwa sauti na kusema ‘Mungu amenitetea katika maisha yangu… Mungu amenilinda, ameniepusha na kwenda kuozea jela … namshukuru sana sina cha kumlipa’ alisisitiza wakati akilia mahakamani hapo.
   “Mniache sina kitu cha kuongea Mungu wangu yu hai amenitetea na kuniepusha na kuozea jela mimi…” alisema Mbasha huku akilia na kuzungukwa na watu pamoja na wanahabari. 
   Katika kesi ya msingi, ilidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa). 
  Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa). Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo na alikuwa nje kwa dhamana.

  0 0

  Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Nordic na Baltiki, Mhe. Dora Msechu amewasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa Iceland, Mhe. Ólaf Ragnar Grimsson 
   Mhe. Balozi Dora Msechu sasa amekamilisha kazi ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwenye nchi zote nane za Eneo lake la Uwakilishi; Sweden, Denmark, Estonia, Finland, Iceland, Latvia, Lithuania na Norway. 
   Mhe. Balozi Dora Msechu amepata pia fursa ya kutembelea Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa, tawi la Iceland na kukutana na Mkuu wa Chuo Bw. Ludvik Georgsson kwa madhumuni ya kuwatafutia Watanzania fursa za masomo chuoni hapo kwenye fani ya joto ardhi (Geothermal).
  Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Nordic na Baltiki, Mhe. Dora Msechu akiwa na na Rais wa Iceland (HOM Iceland) pamoja na Bw. Yusuph Mndolwa, Afisa Ubalozi, baada ya kuwasilisha hati za utambulisho leo

  Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Nordic na Baltiki, Mhe. Dora Msechu akiwa na na Rais wa Iceland (HOM Iceland) baada ya kuwasilisha hati za utambulisho.
  Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Nordic na Baltiki, Mhe. Dora Msechu akiwa katika mazungumzo  na Rais wa Iceland (HOM Iceland)  baada ya kuwasilisha hati za utambulisho.
  Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Nordic na Baltiki, Mhe. Dora Msechu akilakiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa, tawi la Iceland Bw. Ludvik Georgsson. Katikati  ni Bw. Ngereja Mgejwa, Mwanafunzi wa Kitanzania anayesoma Chuoni hapo.
  Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Nordic na Baltiki, Mhe. Dora Msechu katika mazungumzo ya kuombea watanzania nafasi za masomo na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa, tawi la Iceland Bw. Ludvik Georgsson. Katikati  ni Bw. Ngereja Mgejwa, Mwanafunzi wa Kitanzania anayesoma Chuoni hapo.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimtambulisha mgombea Uwakilishi Jimbo jipya la Tunguu Simai Mohammed Said  wakati wa  Mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM uliofanyika leo katika uwanja wa mpira Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimtambulisha mgombea Uwakilishi Jimbo la Uzini Mohammed Raza Dharamsi wakati wa  Mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM uliofanyika leo katika uwanja wa mpira Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimtambulisha mgombea Ubunge Jimbo jipya la Tunguu Khalifa Salum Suleiman wakati wa  Mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM uliofanyika leo katika uwanja wa mpira Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimtambulisha mgombea Ubunge Jimbo la  Chwaka Bangwanji Suria Mshamba  wakati wa  Mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM uliofanyika leo katika uwanja wa mpira Bungi Wilaya ya kati, Mkoa wa Kusini Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimtambulisha mgombea Ubunge Jimbo la Uzini Salum Mwinyi Rehani wakati wa  Mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM uliofanyika leo katika uwanja wa mpira Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwatambulisha Wagombea Udiwani CCM wakati wa  Mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM Wilaya ya Kati uwanja wa mpira Bungi  Mkoa wa Kusini Unguja.

  0 0  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donnan Mmbando akizungumza  na waandishi wa habari juu ya matumizi ya dawa  katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yawe na uwiano sawa na kuwa na kiwango kinachokubalika Kimataifa. Amesema  mamlaka husika inapaswa kusimamia na wataalam wa dawa ili kuendana na soko  la Jumuiya ya  Afrika Mashariki, leo Jijini Dar es Salaam
   Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jinsi namna  wananchi watapata dawa zilizo bora na salama zaidi kwa kutumia vigezo vya kikamataifa kwa kuwa kuzingatia masharti yanayotolewa na Shirika la Afya Duniani. Amesema Tanzania ni nchi ya kwanza kutoa uhamasishaji huu kwa wadau  wazalishaji na wasambazaji wa  dawa na wote wanaojihusisha na biashara ya dawa na kwamba  hii ni jumuiya  ya kwanza  katika bara la Afrika kutekeleza mpango wa kuwa na mifumo ya aina moja ya uthibiti wa dawa kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
   Sehemu ya wadau wa dawa walio hudhulia kikao hicho leo Jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donnan Mmbando na  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donnan Mmbando na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo wakifurahia jambo baada ya kikao hicho (Picha na Emmanuel Mssaka)

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi leo amefunga fainali za michuano ya kombe la Airtel Rising Stars katika uwanja Karume jijini Dar es salaam.
  Akiongea kwakati wa ufungaji michuano ya airtel mbele ya halaiki ya vijana walioshirki michuano hiyo, Malinzi ameishukuru kampuni ya simu ya Airtel kwa kuendelea kudhamini michuano hiyo ambayo inawapa nafasi vijana ya kucheza mpira na kuonekana na baadae kujipatia ajira.
  “Lengo la TFF ni kushirki fainali za Olimpiki za Dunia mwaka 2020 Tokyo –Japan hivyo wachezaji wenye vipaji kutoka kwenye michuano hii ya Airtel na vijana wengine wataendelea kutunzwa kwa ajili ya timu ya Taifa ya baadae” Alisema Malinzi.
  Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ambao ndio wadhamini wakuu wa michuano hiyo, amesema airtel wataendelea na program hiyo ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 kwa wanawake na wanaume, na kuahidi kuendelea koboresha michuano hiyo kila mwaka.
  Michuano ya Airtel Rising Stars iliyomalizika leo, ilizisihirkisha timu za wanaume na wanawake kutoka mikoa saba nchini, huku mashindano hayo yakiwa yanafanyika kwa msimu wa tano sasa tangu kuanzishwa mwaka 2011.
  Kwa upande wa wanaume, timu ya Ilala imeibuka mabingwa baada ya kuifunga Mbeya kwa mabao 4-0 katika mchezo wa fainali ulochezewa jioni ya leo, huku timu ya wanawake ya Temeke wakiibuka washindi baaada ya kuibwaga Kinondoni mwa mikwaju ya penati 5-4.


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0


  Aisha, mke wa mtu, msichana mfamasia mkaazi wa jijini anakwenda kijijini kumtembelea dada yake ambaye anatarajia kuolewa na mtoto wa mwenyekiti wa kijiji. Anakutana na wengi anaowajua na kukumbuka mengi aliyopitia. Ingawa, tamu inageuka kuwa chungu pale mpenzi wake wa zamani anapopanga kulipiza kisasi, Aisha anajikuta matatizoni na juhudi zake za kutafuta haki hazizai matunda pale jamii inapojitia upofu.


  Aisha, a young married pharmacist living in the city visits her younger sister in the village who is about to be wedded to the son of a local village leader. She meets with familiar faces and attempts at rekindling the past. However, when an old flame turns cold and an ex-boyfriend seeks revenge, she is faced with dire consequences. Her struggle for justice becomes a tough one when everyone would rather turn a blind eye.
  CLICK HERE TO READ ARTICLE

  0 0

  Nafasi Art Space present a new public art exhibition in partnership with DARCH and the National Museum and House of Culture, Tanzania
  Exhibition opening includes public tours of artworks across the city centre, drop-in art activity, contemporary dance performances and live music!
  Be part of something new for downtown Dar!
  Events starts at 14.00 until 18.30.
  Karibuni!

  0 0

  Mikataba ya madini, gesi, mafuta kupitiwa na timu ya wataalam kabla ya kusainiwa. Na Greyson Mwase, Morogoro Ili kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wananufaika na rasilimali za madini mbalimbali pamoja na gesi iliyogunduliwa kwa wingi hivi karibuni, Serikali imeanza kutoa mafunzo kwa wataalam kutoka taasisi za serikali watakaohusika na upitiaji wa mikataba yote ya shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini, gesi na mafuta kabla ya kusainiwa. 
  Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene katika uzinduzi wa warsha kuhusu dira mpya ya madini Afrika iliyofanyika mjini Morogoro. 
  Warsha hiyo ya siku tatu iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini ilikutanisha wataalam kutoka taasisi za serikali ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais- Tume ya Mipango, Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) 
  Pia ilikutanisha wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na taasisi zake kama vile Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Nchini (TEITI), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Chuo cha Madini Dodoma (MRI). 
  Simbachawene alisema uundaji wa timu ya wataalam mbalimbali kwa ajili ya kupitia mikataba ya madini, gesi na mafuta ni moja ya makubaliano katika utekelezaji wa Dira ya Madini ya Africa (Mining Vision for Africa) iliyoasisiwa na wakuu wa nchi zenye madini katika mkutano wake uliofanyika mwaka 2009. 
   Alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa sekta ya madini inachangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika zinazozalisha madini wakuu wa nchi walikubaliana kuanzishwa kwa Dira ya Madini itakayowezesha sekta ya madini katika nchi wanachama kuboreshwa na kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi 
  Alisema kuwa katika utekelezaji wa Dira ya Madini ya Afrika, nchi ya Tanzania imeanza kutoa mafunzo kwa wataalam mbalimbali katika taasisi za Serikali katika upitiaji wa mikataba hususan ya utafiti na uchimbaji wa rasilimali za madini, gesi na mafuta. Alisisitiza kuwa mara baada ya wataalam hao kupata mafunzo wataweza kupitia mikataba mbalimbali kabla ya kusainiwa. 
  “Ieleweke kwamba suala la mikataba litakuwa si kati ya watu wawili bali wataalam watashirikishwa kwa kupitia mikataba hiyo na kutoa mapendekezo yao kabla ya mikataba kusainiwa na Waziri ambaye ni msimamizi wa sekta husika,” alisisitiza Simbachawene. Akielezea ushirikishwaji wa wananchi katika usimamizi wa sekta za madini, gesi na mafuta, Simbachawene alisema kuwa Serikali imehakikisha kuwa mikataba yote inalenga kuwanufaisha wananchi kwa kushirikishwa katika utoaji wa huduma katika sekta husika. 
  Akitolea mfano wa sekta ya gesi nchini, alisema fursa za utoaji wa huduma zipo nyingi na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hizo Hata hiyo alieleza kuwa Serikali ina mkakati wa kutoa mafunzo kwa wanachi kuhusu uzalishaji wa bidhaa bora ili ziendane na soko la kimataifa. 
  “ Tunataka ifike mahali makampuni yanayofanya shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini, gesi na mafuta yanunue huduma na bidhaa kwa wananchi wa Tanzania badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi,” alisisitza Simbachawene. 
  Naye mtaalam kutoka Kitengo cha Nishati na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Abbas Kitogo alisema kuwa shirika la UNDP limekuwa likishirikiana na Serikali katika utoaji wa mafunzo kuhusu sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na usimamizi wa mikataba 
  Alisema sekta nyeti kama za madini, gesi na mafuta zisiposimamiwa kikamilifu zinaweza kuibua migogoro badala ya kuleta maendeleo. 
   
  Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akifungua  warsha kuhusu Dira ya Madini Afrika  iliyokutanisha wataalam kutoka   taasisi za serikali nchini lengo likiwa ni kuwapa uelewa juu  ya sekta ya madini na usimamizi wa mikataba. Katikati ni Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu na Mbadala Mhandisi Edward Ishengoma. Kushoto ni mtaalam kutoka  Kitengo cha  Nishati na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Abbas Kitogo.
   Washiriki  wa warsha kuhusu Dira ya Madini Afrika wakifuatilia kwa makini  hotuba ya ufunguzi iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, George  Simbachawene (hayupo pichani)
  Picha ya pamoja baada ya ufunguzi

  0 0


  Baadhi ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alifanya mkutano wa kampeni leo. 
  Baadhi ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alifanya mkutano wa kampeni leo. 
  Mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Usagara Tanga Mjini leo. Idadi kubwa ya wananchi walihudhuria mkutano huo hadi wengine kuzimia kutokana na msongamano.

  Baadhi ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alifanya mkutano wa kampeni leo. 
  Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM Kitaifa, Bi. Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi kwenye moja ya mikutano ya kampeni za CCM timu ya mgombea mweza iliyofanyika mkoani Tanga leo.
  Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   WAZIRI wa Maliasili na Utalii na mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu,  akiingia kuzindua rasmi kampeni zake katika Uwanja wa Mtinko huku akisindikizwa na msafara mkubwa wa bodaboda.
   WAZIRI wa Maliasili na Utalii na mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu,  akisoma bango lenye ujumbe wa kumpongeza lililoandaliwa na wananchi wa Kata ya Mntiko, wakati wa uzinduzi wa kampeni zake za ubunge.
   WAZIRI wa Maliasili na Utalii na mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakicheza kwa furaha wakati wakiwasili kuzindua kampeni zake za ubunge katika Kata ya Mtinko.
    MKE wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Faraja, akicheza na wanachama na wapenzi wa CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni katika Jimbo la Singida Kaskazini, juzi.
   WAZIRI wa Maliasili na Utalii na mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, akihutubia umati wa wanachama na wakazi wa Kata ya Mtinko wakati uzinduzi wa kampeni zake, juzi.
   MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, mkewe Faraja na Mbunge mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, wakicheza muziki wa hamasa wa CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika Kata ya Mtinko, juzi
  WAZIRI wa Maliasili na Utalii na mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, akisalimia na mamia ya wanachama na wakazi wa Mtinko wakati alipozindua kampeni zake juzi, ambapo maelefu ya watu walijitokeza kumsikiliza

  0 0


  Tanzanians: Edha Nahdi (AMSONS GROUP/CAMELOIL), Reginal Mengi (IPP), Mohammed Dewji (MeTL)
  Big Up for Tanzanians. For whole report click the links below:http://www.aablawards.com/east-africa.php
  http://venturesafrica.com/meet-the-east-african-winners-of-aabla-2015/
  Mohammed-Dewji

  0 0


  Moto unaoendelea kuwaka Mlima Meru katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Martin Loibooki akiongea na wanakijiji wa Olosinoni wanaoshiriki zoezi la kuzima moto unaonendelea kuwaka Mlima Meru katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha jana.
  --- 
  HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA

  Moto mkubwa umezuka mwishoni mwa wiki hii na kuunguza sehemu ya Mlima Meru katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa chanzo cha moto huo ni vitendo haramu vya urinaji wa asali ndani ya msitu wa hifadhi hiyo.
  Wananchi wapatao 200 kutoka vijiji jirani vya Olosinoni na Kisimiri Juu wakishirikiana na TANAPA wamefanikiwa kuudhibiti moto huo ili usiweze kuleta madhara makubwa kwa binadamu hususan wageni wanaotembelea hifadhi kwa lengo la kupanda Mlima Meru.
  Hadi sasa hakuna wageni waliodhurika na moto huo na tahadhari zote zimechukuliwa ili kudhibiti madhara zaidi kwa binadamu na shughuli za utalii ndani ya hifadhi.
  Shirika la Hifadhi za Taifa linaendelea kuwatahadharisha wananchi juu ya vitendo vya kuingia ndani ya hifadhi bila kibali kwa shughuli ambazo zinaweza kuwa chanzo cha kuzuka kwa mioto hii ambayo husababisha uharibifu wa mazingira pamoja na kuharibu vyanzo vya maji.
  Aidha, katika kuhakikisha kuwa moto huo unadhibitiwa kwa haraka, TANAPA imeongeza nguvu kazi ya wananchi wakishirikiana na vyombo vingine vya dola ili kuweza kuudhibiti moto huo.
  Mwisho, taarifa kamili juu madhara yaliyosababishwa na moto huo itatolewa mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuzima moto na umma utaendelea kupewa taarifa ya maendeleo ya zoezi la uzimaji wa moto kila wakati.
  Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
  HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
  dg@tanzaniaparks.com
  www.tanzaniaparks.com

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mheshimiwa Wilson Masilingi akimkabidhi Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Tuzo ya Utawala Bora ya Baraza la Biashara la Wana-Afrika Mashariki Waishio Marekani na nchi nyingine (East African Diaspora Business Council Award)  Jumatatu, Septemba 21, 2015 mjini Washington, D.C. Balozi Masilingi ndiye alimwakilisha Dkt. Kikwete katika sherehe ya kukabidhi tuzo hiyo usiku wa Jumapili, Septemba 20 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Dallas, Jimbo la Texas. Picha na Freddy Maro.  

  0 0

    
  DAR ES SALAAM, Tanzania. Tarehe 21 Septemba 2015 -- Symbion Power yenye tawi lake maeneo ya Ubungo leo imetangaza kuwa imefanikiwa katika majaribio ya kutumia gesi asilia katika mitambo yake . Gesi inapatikana  Ghuba ya  Mnazi iliyo karibu na Mtwara Kusini mwa Tanzania. 

  Kwa zaidi ya Mwaka mmoja sasa ; Mitambo hii yenye uwezo wa kuzalisha kiasi cha Megawati 120 haikuweza kufanya uzalishaji wowote kutokana na ukosefu wa gesi asilia kama chanzo cha nishati Tanzania


  “Kwa mara nyingine Symbion ina uwezo wa kufanya kazi kwa kutumia gesi asilia badala ya kutumia nishati ya mafuta ambayo pamoja kuwa ni aghali Symbion ililizamika kuitumia kati ya mwaka 2012 na 2014” alinena Mtendaji Mkuu Bwana Paul Hinks. 
  Kwa hivi sasa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) nalo litaweza kuendesha mitambo yake kadhaa ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi kutoka Mtwara. 
  Aidha Bwana Hinks aliongeza na kusema “ Hii ni habari njema kwa TANESCO ambayo imekuwa na wakati mgumu kifedha kutokana na gharama kubwa inayotumia kununulia mafuta ambayo huingizwa kutoka nchi za nje. Matokeo ya utumiaji gesi asilia katika kuzalisha umeme yatapelekea kuwepo kwa matokeo chanya kifedha kama matokeo mtambuka ya gharama nafuu za uzalishaji umeme”. 
  Mitambo ya Symbion Power iliyoko maeneo ya Ubungo ilikuwa ni eneo kuu ambalo Rais Barack Obama alilitumia kuhutubia mnamo Julai mwaka 2013 ambapo pamoja na mambo mengine aliainisha dhana yake ya “Power Africa” ambayo yaweza kutafsiriwa kama Afrika yenye Umeme.Hii dhana ililenga kwenye kuongeza upatikanaji wa umeme mara mbili katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara. Kama sehemu ya “Afrika yenye Umeme” Symbion imedhamiria kuwekeza kiasi cha dola za kimarekani billion 1.8 katika sekta ya Umeme kwenye nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara kati ya Julai 2013 mpaka Julai 2018. 
   Kampuni ya Symbion kwa kushirikiana na TANESCO; ziko katika harakati ya kutengeneza mitambo mingine yenye uwezo wa kuzalisha kiwango cha Megawati 600 huko Mtwara. Pamoja na hilo kutakuwepo nguzo za kusambaza umeme mpaka Songea Magharibi huko Kusini mwa Tanzania na kusini mwa Msumbiji. Mara hii miradi itakapokamilika; itaifanya Mtwara kuwa kitivo kikuu cha nishati; kwa maana hiyo itasaidia kuleta umeme ambao unahitajika sana kwenye eneo hilo na hivi kusaidia katika kutengeneza maelfu ya ajira nchini Tanzania.

  0 0

   Mgombea Urais wa wa Jamhuri ya Muunganano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe magufuli akiwahutubia wakazi wa Bukoba mjini kwenye kutano wa hadhara wa kampeni uliofamyika katika uwanja wa Gymkhana Bukoba mkoani Kagera kumsikiliza Dkt -John Pombe Magufuli.
  Mgombea Urais wa wa Jamhuri ya Muunganano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe magufuli akiwahutubia wakazi wa Bukoba mjini kwenye kutano wa hadhara wa kampeni uliofamyika katika uwanja wa Gymkhana Bukoba mkoani Kagera kumsikiliza Dkt -John Pombe Magufuli.
   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Balozi Hamis Kagasheki akiwahutubia wananchi wa Bukoba na vitongoji vyake waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni wa Urais,ambapo Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia jioni ya leo mkoani Kagera.
    Wakazi wa kijiji cha Nshamba wilayani Muleba wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kufunga barabara wakitaka kusikilizwa shida zao, alipokuwa akiwasili eneo hilo na kuwasalimia Magufuli alipokuwa . 
   Sehemu ya wafuasi wa chama CCM wakifuatilia mkutano wa kampeni.
    Sehemu ya wananchi wa mji wa Bukoba waliohudhuria leo katika viwanja vya Gymkhana Bukoba mkoani Kagera wakimsikiliza Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.older | 1 | .... | 982 | 983 | (Page 984) | 985 | 986 | .... | 3285 | newer