Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

TAARIFA KWA UMMA


UVCCM ZANZIBAR WAOMBA KUPATIWA MRITHI WA MZEE KINGUNGE KUNOGESHA USHINDI WAO

$
0
0
 Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini-Unguja ndugu Mbarouk Mrakib katikati akizungumza na Waandishi wa habari huko ofisini kwake Bububu kuhusu mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuomba kupatikana kwa Kamanda Mpya wa UVCC Taifa baada ya Mzee Kingunge kuvuliwa Ukamanda huo. Kulia kwake ni Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini Canal Msaafu Masoud Ali Khamis na kushoto ni Mjumbe wa Kamati tendaji UVCCM Wilaya Khadija Ramadhan Abdu. Picha na Faki Mjaka- Maelezo Zanzibar.
 Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini-Unguja ndugu Mbarouk Mrakib akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake Bububu kulia Mjumbe wa Kamati tendaji UVCCM Wilaya Khadija Ramadhan Abdu.
Baadhi ya wanachama wa UVCCM wakimpongeza Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini-Unguja ndugu Mbarouk Mrakib (hayupo pichani) mara baada ya kuzungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake Bububu.

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar  21/08/2015
Baraza kuu Taifa la Umoja wa Vijana CCM limeombwa kumtamfuta Mtu wa kuchukua Nafasi iliyoachwa wazi ya Ukamanda Mkuu wa UVCCM Taifa ili kuongeza kasi ya kuutafuta ushindi wa CCM katika uchaguzi unaokuja.
Kupatikana kwa Kamanda huyo Mkuu kutachochea zaidi Kasi na ari ya mchakato wa Kampeni kuelekea ushindi wa CCM katika uchaguzi huo.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini-Zanzibar ndugu Mbarouk Mrakib alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari huko ofisini kwake Mfenesini.

Amesema UVCCM Wilaya inapongeza kwa kuvuliwa wadhifa wa Ukamanda Mkuu Taifa Mzee Kingunge Ngumbale Mwilu kutokana na Kauli zake zinazokinzana na Chama na hivyo kushauri hatua za haraka zichukuliwe kupatikana Mrithi wake.

Aidha ameongeza kuwa hatua iliyochukuliwa na CCM ya kumuenguwa Edward Lowasa katika nafasi ya Urais kupitia CCM inafaa kupongezwa kutokana na kasoro alizokuwa nazo mgombea huyo.

“Sisi wenyewe Tulimuunga Mkono Lowasa kipindi kile lakini baada ya kuelezwa Mapungufu yake na Viongozi wetu tumegundua hafai kabisa na Chaguo sahihi ni Magufuli pekee”Alifahamisha Mrakib.

Amefahamisha kuwa Siasa za Tanzania zinahitaji Viongozi Wasafi, Waadilifu na Wasiopenda Dhulma wala Ufisadi na kwamba kiongozi aliyepitishwa na CCM Dkt, John Pombe Magufuli ndio chaguo sahihi.

Aidha amedai kuwa Chama cha Mapinduzi tayari kimeshajipatia ushindi kutokana na kutekeleza vyema Ilani yake na kwamba Wanachama na Wananchi kwa ujumla watakipigia kura za ndio bila hata chembe ya Shaka.
Hata hivyo Mrakib ambaye aligombea nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo la Mtoni na kushindwa alisema Mipango yake kwa sasa nikuhakikisha anatoa kila aina ya Ushirikiano ili Wagombea wote kutoka Chama hicho washinde katika Uchaguzi unaokuja.

Mrakib aliwapongoza Vijana waliojitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali kupitia chama hicho ambapo anaamini walioshinda wataweza kukipeperusha Vyema chama hicho ili kupata ushindi wa kishindo.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.

ZAIDI YA WATOTO MILIONI 3.1 WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO HUFARIKI DUNIA KILA MWAKA HUKU WENGINE MILIONI 161 KUPATA MATATIZO YA KUDUMAA MWILI

$
0
0
 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John akizungumza juu ya Upungufu wa vitamini na Baadhi ya Madini muhimu kama Vitamini A, folate, Madini chuma Zinki na madini joto ni chazo cha vifo kwa Watoto chini ya miaka Mitano na chanzo kikubwa cha maradhi mbalimbali kote Duniani, kulia ni Mkurungenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Alliance for Iproved Nutrition (GAIN) ,Marc van Amerngen katika mkutano uliofanyika  leo Jijini Dar es Salaam.
 Kulia ni Mkurungenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Alliance for Iproved Nutrition (GAIN), Marc van Amerngen akizungumza na waaandishi wa habari hawapo pichani juu ya Kongamano la kimataifa litakalofanyika jiji Arusha Septemba 9-10 mwaka huu  katika mkutano uliofanyika leo Jiji Dar es Salaam kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Michael John.
Mkurungenzi Msaidizi huduma za lishe Dr.Vincent Asey kuliani Dr. Generose Mulokozi akizungumza juu ya  Matatizo ya lishe yanamgusa kila mmoja wetu kote Duniani katika mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandish wa habari walio hudhulia mkutano huo jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Emmanue Massaka.

TAKWIMU zinaonyesha zaidi ya watoto milioni 3.1 wenye umri chini ya miaka mitano hufariki Dunia kila Mwaka huku wengine Milioni 161 kupata matatizo ya kudumaa mwili kutokana na kukosekana kwa virutubisho vya chakula.

Madhara hayo yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuongeza virutubisho kwenye vyakula ikiwemo Unga,Mafuta ya kula pamoja na Chumvi.


Hayo yalisemwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Michael Jonh wakati wa mkutano na waandishi wa habari ikiwa lengo ni kutoa tamko kuhusu Kongamano la kimataifa la Urutubishaji Chakula litakalo septemba 9 hadi 11 mwaka huu jijini Arusha.


Aidha amesema kuwa Chanzo cha Vifo hivyo ni upungufu wa vitamini pamoja na dbaadhi ya madini muhimu kama vile vitamin A,Folate,Madini Chuma,Zinki na Madini Joto hali inayosababisha maradhi mbalimbali katika maeneo mengi duniani.


Kwa upande wake Mkurugezi Msaidizi wa huduma za lishe kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Vicent Assey alisesema kuwa utafiti wa mwaka 2010 umebainisha asilimia 42 ya watoto ni walemavu kutokana na Lishe Duni.


Alisema kuwa nchi ambazo zimeathirika na  tatizo la vifo kwa watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano kutokana na ukosefu wa virutubisho kwenye chakula ni zile ambazo zipo kusini mwa jangwa la sahara Barani Afrika.


Alizitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na Tanzania ambayo ipo nafasi ya tatu kulingana na takwimu za vifo kwa watoto ,huku  DRC Kongo ikishika nafasi ya pili, na Ethiopia ikiwa ni ya  kwanza kutokana na sababu kubwa  ya kukumbwa na migogoro ya kivita katika nchi hizo.


Kutokana na changamoto hizo Serikali ya Tanzania kwa Kushirikiana na Shirika la masuala ya urutubishi wa chakula duniani la Global Alliance For Improved Nutrition (GAIN) inatarajiwa kuwa mwenyeji wa kongamano hilo la kwanza la kimataifa ambalo shabaha yake kubwa ni kuzungumzia masuala ya urutubishaji chakula.                              

KAMATI YA UCHAGUZI DRFA YAPANGUA AGIZO LA KAMATI YA UCHAGUZI TFF KUSIMAMISHA UCHAGUZI WA TEFA

$
0
0
Kamati ya uchaguzi ya chama cha soka mkoa wa Dar e salaam DRFA,imeshindwa kutekeleza agizo la lililotolewa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF la kusimamisha mchakato wa uchaguzi wa chama cha soka wilaya ya temeke TEFA uliopangwa kufanyika jumapili agosti 23/2015.

Baada ya kupitia kwa umakini kanuni za uchaguzi za TFF za mwaka 2013 ibara ya 6, na kujiridhisha kuwa hakuna kipengele chochote kinachoruhusu kamati ya uchaguzi ya TFF kuingilia kati mchakato wa uchaguzi wa TEFA,Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya DRFA,Rashid Saadallah,(mwanasheria ),amemuandikia barua mwenyekiti wa uchaguzi wa TFF,Aloyce Komba kumjulisha hilo na kumueleza kuwa mchakato huo sasa utaendelea kama ulivyopangwa kufanyika jumapili agosti 23/2015.

Mwenyekiti huyo wa uchaguzi DRFA,amesema mpaka sasa taratibu na maandalizi yote kuelekea uchaguzi huo wa jumapili yamekamilika ikiwemo usikilizwaji wa rufaa mbalimbali na kuzitolea uamuzi,hivyo  kitendo cha kuingilia kati mchakato huo ni kinyume cha utaratibu,kwa kuwa TEFA ni mwanachama wa DRFA na siyo wa TFF.

SIMU TV: HABARI TOKA VITUO VYA TELEVISHENI

BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZIMBABWE AKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Zimbabwe Lt.Gen.Mstaafu Charles Makakala alipofika Ikulu Mjini Zanzibarkujitambulisha leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatana  na Balozi  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Zimbabwe Lt.Gen.Mstaafu Charles Makakala baada ya mazungumzo yao leo alipofika  Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Zimbabwe Lt.Gen.Mstaafu Charles Makakala alipofika kujitambulishaIkulu Mjini Zanzibar.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MPANGO WA KAZI WA KIMATAIFA NA KANUNI ZA SHERIA YA KUZUIA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua Mpangokazi wa Kimataifa na Kanuni za Sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa Binadamu, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika leo Agosti 21, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Kinemo Kihonamo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mpangokazi wa Kimataifa na Kanuni za Sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa Binadamu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, baada ya kuzindua rasmi Mpango kazi huo, kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Agosti 21, 2015. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpangokazi wa Kimataifa na Kanuni za Sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa Binadamu, uliyofanyika leo Agosti 21, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua mpango kazi huo, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Agosti 21, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 

JK APOKEA HATI YA UTAMBULISHO WA BALOZI WA DENMARK NCHINI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akipokea hati ya utambulisho ya Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kulia) leo Ikulu jijini Dar es salaam wakati alipokwenda kujitambulisha.
Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen akisaini kitabu cha wageni wakati alipokuwa anaenda kukabidhi hati ya utambulisho na kujitambulisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kulia) wakati alipokwenda kujitambulisha na kukabidhi hati ya utambulisho leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akisalimiana na Balozi wa Denmark (kushoto) nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen mara baada ya kukabidhi hati ya utambulisho leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akibadilishana mawazo na Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kushoto) wakati alipokwenda kujitambulisha na kukabidhi hati ya utambulisho leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Maadhi Juma Maalimu (wa pili kushoto) leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (katikati mstari wa mbele) akiwa amesimama wakati nyimbo za taifa za Tanzania na Denmark zikiimbwa leo Ikulu jijini Dar es salaam alipokwenda kujitambulisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
 Bendi ya Jeshi la Polisi nchini ikipiga nyimbo za taifa za Tanzania na Denmark wakati Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (katikati mstari wa mbele) alipokuwa anakwenda kujitambulisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

MARAFIKI WA WAFANYE WATABASAMU WATOA MSAADA KWA WATOTO WA AMANI ORPHANAGE CENTRE, BAGAMOYO

$
0
0

Marafiki wa Wafanye Watabasamu, hivi karibuni, walitembelea kituo cha watoto yatima (Amani Orphanage Centre) kilicho katika Kijiji cha Zinga, Bagamoyo kwa ajili ya kutoa misaada mbali mbali kisha kuchora nao. Mbali na marafiki waishio nchini, pia kulikuwa na walimu sita toka Shule ya Msingi ya Catton Grove ya Uingereza na wawakilishi wa taasisi ya The Tanzania Norwich Association pia ya Uingereza. (Picha: Nicolas Calvin).
Msafara wa Wafanye Watabasamu ukiwasili kituoni hapo. Zaidi kuhusu programu hii tembelea: https://www.facebook.com/wafanyewatabasamu.
Mkurugenzi wa kituo cha Amani Orphanage Centre, Bi. Margareth Mwegalawa wa pili toka kulia aliyesimama, akitoa taarifa fupi kuhusu kituo hiko.
Mratibu wa Wafanye Watabasamu ambaye pia ni mchora vibonzo ITV, Nathan Mpangala akiwashukuru marafiki mbalimbali waliochangia misaada na kufanikisha ziara hiyo.
Sanaa ya uchoraji nayo ikachukua nafasi yake.
Baadhi ya watoto na marafiki wa Wafanye Watabasamu wakionesha kazi zao.
Naam, raha ya shughuli mlo bwana.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA AGOSTI 21, 2015

WAGOMBEA WA URAIS WA VYAMA MBALIMBALI VYA SIASA NCHINI WARUDISHA FOMU ZA UTEUZI WA NEC

In Loving Memory of Generosa Hilary Ngonyani

$
0
0
Sunrise 01/12/1937  - Sunset 22/08/2012

Three years have passed since you left us to be with the Lord. The pain of your death is as fresh as the day you left us. 

Your anniversary is a painful reminder of our loss. We miss you so dearly mum.  We miss you every day and much more during the family gatherings. We miss your love, guidance, support, friendship and care.  You were our joy, our pillar, our light and our strength.  .

We are comforted by the great moments you shared with us which have become our treasure.  Your heart brought great great joy not only to us but to many.  Our hearts can never truly forget you. 

You are greatly missed by your mother Agatha Ntamanyali; your children David Ngonyani, Joyce Kafanabo, Fortunata Ngonyani, Chille Ngonyani and Angela Ngonyani; your in-laws Joyce Kuoko Ngonyani, Rose Namundi Ngonyani,  Jerome Msefya and Gosbert Kafanabo; grandchildren Kemilembe, Josephine, Lipyana, Rose, Fortunatus, Alfred, Generosa, Mary, Grace, Shangwe, Chile Junior, Lugano,   Joseph and Maximillian; the Ngonyani and Ngatunga families and the rest of the family and friends.

In God's hands you rest but in our hearts you live forever.


Rest in Peace Our dearest mother.

GLOBAL EDUCATION LINK (GEL) YASAFILISHA WANAFUNZI KWENDA KUSOMA NCHINI INDIA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, Abdulmalik Mollel akiwa ameambatana na wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwasindikiza wanafunzi 30 wanaokwenda kusoma nchini India jana Agosti 21, 2015 katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, Abdulmalik Mollel akiwaita majina wanafunzi waliokuwa wanaondoka kwenda kusoma vyuo vikuu nchini India mapema jana Agosti 21, 2015 katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, wakikagua wanafunzi vyaraka muhimu walizopaswa kusafiri nazo ikiwemo viza, vyeti, na passport. Picha zaidi BOFYA HAPA

WAHE. MAJAJI WAPYA WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA WAPEWA MAFUNZO ELEKEZI JUU YA UTENDAJI KAZI MAHAKAMANI

$
0
0
 Mhe. Shaban Ali Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (katikati) akitoa neno la utangulizi katika Semina ya Mafunzo elekezi kwa Wahe. Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania walioapishwa hivi karibuni, aliyeketi kushoto ni Mhe. Anold Nsekela, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani (T) kulia ni Mhe. Salvatory Bongole, Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

             Mhe. Jaji Ferdinand Wambali (aliyesimama), Mkuu wa Chuo cha Mahakama  Lushoto (IJA),akitoa mada juu ya utendaji kazi katika Mahakama katika mafunzo yaliyoanza kufanyika mapema leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Mhe. Shaban Ali Lila, Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (katikati) Mhe. Anold Nsekela, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Salvatory Bongole, Kaimu Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania walioapishwa hivi karibuni, Majaji hao wapo katika mafunzo elekezi yenye lengo la kuwawezesha sheria mbalimbali na taratibu za Kimahakama. Mafunzo haya yataendelea kufanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA) kuanzia tarehe 24.08.2015 ambapo mada mbalimbali zitatolewa ili kuwawezesha Wahe. Majaji hao kuifahamu Mahakama, ikiwa ni pamoja na misingi  na taratibu za utoaji huduma ya haki nchini. (Picha na Mahakama).

Wasichana walio katika mazingira magumu wahitimu Chuo Kukuu Huria cha Tanzania

$
0
0
Na erasto Ching’oro
 Wasichana 22 kutoka mazingira hatarishi wamehitimu mafunzo ya ujasiriamali, mawasiliano, ususi wa nywele na urembo katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania jijini Dar es salaam na kutunukiwa vyeti vya umahiri na Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto Mhe. Dkt. Pindi H. Chana ambaye alikuwa mgeni rasimi kwenye mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo (OUT) tarehe 20 Agosti, 2015. 
Mapema mwezi Januri, 2015 Chuo Kikuu Huria kwa ushirikiano na asasi ya ‘Nafasi Opportunity Society (NOS)’ ya nchini Canada walibaini wasichana 22 wanaoishi katika mazingira hatarishi kutoka mikoa mbalimbali na kuwapa fursa ya kujiunga na mafunzo ya ujasiriamali, ususi na ulembo kwa lengo la kuwawezesha kupata stadi na weledi ili kuboresha kazi zao. 
Katika kufanikisha lengo hilo asasi ya NOS ilikubali kugharimia mafunzo ya wasichana hao kuanzia Januri 2015 hadi Agosti, 2015 na wote kuweza kuhitimu na kutunukiwa vyeti na Mhe. Pindi Chana. Mgeni Rasimi Mhe. Pindi aliwapongeza waliohitimu maana mafunzo waliyopata yamewaongezea mbinu katika ajira. 
Pili, wameweza kupata maarifa na stadi za ujasiriamali hivyo kuwawezesha kujiajiri na kuajiri wengine. Fursa ya mafunzo waliyopata wasichana itaongeza thamani ya utumishi wao katika soko la ajira maana wamepata mafunzo kutoka katika Chuo makini (OUT) na huduma ya wahitimu hao itawawezesha kupata kazi zenye staha katika soko na watatangazia vizuri nafasi ya Chuo Kikuu Huria Tanzania katika kumwendeleza mwanamke. Mhe. Pinda alisisitiza kuwa elimu ya urembo ni fani ambayo inahitajika kwa wanaume na wanawake wa vijijini na mijini. Kama fani hii ya urembo itaendelezwa itaongeza nafasi za ajira kwa wasichana na wavulana kwa kiasi kikubwa maana mahitaji yake ni ya hakika katika soko. 
Awali Kaimu Mkuu wa Chuo Huria cha Tanzania Prof. matern Victor, alieleza kuwa mafunzo hayo maalum kwa wasichana wanaoishi katika mazingira magumu yalilenga kujenga uwezo wa familia na jamii katika mikoa na kwamba kama rasilimali fedha ikipatikana na jamii ikaendeleza juhudi za kutoa haki sawa ya elimu kwa wote wasichana wengi wenaweza kufikiwa kupitia Ofisi za mikoa. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto  Mhe. Dkt. Pindi H. Chana (Mb)akimpongeza Bi. Jane Malyi kiongozi wa wahitimu wa mafunzo ya ujasiriamali na urembo mara baada ya kutoa neno fupi kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo katika chuo Kikuu Huria cha Tanzania, jijini Dar es salaam 

MKURUGENZI MKUU WA AGPAHI AAGANA RASMI NA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Laurean Bwanakunu aliyekwenda kumuaaga ofisini kwake baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD). (Picha na Francis Dande)

 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (katikati) akizungumza na uongozi wa Shirika lisilo la Kiserikali la AGPAHI uliokwenda ofisini kwake wakati Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo alipokwenda kumuaga. 

SIMU TV: MATUMIZI MABAYA YA MTANDAO - SHEIKH NURDIN KISHKI AZUSHIWA AKAUNTI YA FACEBOOK

WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDRECK SUMAYE AONDOKA CCM NA KUJIUNGA NA UKAWA

$
0
0
 Waziri Mkuu mstaafu, Fredreck Sumaye (kushoto), akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo mchana.
 Waziri Mkuu mstaafu, Fredreck Sumaye (kulia), akipeana mkono na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe Dar es Salaam leo mchana, baada ya kujiunga na chama hicho. Anayeshuhudia katikati ni Mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
 Sumaye akisisitiza jambo
Sumaye (wa tatu kulia), akiwa na viongozi wanaunda Umoja wa Katiba (UKAWA) baada ya kuondoka CCM na kujiunga na Chadema. PICHA NA HABARI ZA JAMII BLOG

Rais Kikwete amuapisha Balozi Mpya wa Tanzania nchini Zimbabwe

$
0
0
Balozi mpya wa Tanzania nchini Zimbabwe Luteni Jenerali Charles Lawrence Makakala akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam jana.Hafla hiyo ilihudhuriwa (picha na Freddy Maro)

CAROLINA CHILELE AIBUKA MSHINDI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015

$
0
0
Hatimaye Shindano la Mama Shujaa wa Chakula  linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitia Programu yake ya Grow ambapo kauli mbiu ni Wekeza kwa wakulima wanawake wadogo wadogo inalipa lafika tamati ambapo kulikuwa na mchuano mkali kati ya washiriki 15 ambao walikuwa katika Kijiji cha Kisanga Wilayani Kisalawe Mkoani Pwani wakiwa na shughuli mbalimbali za Kilimo ambazo zililenga hasa katika kuwakomboa wakulima wadogo wadogo wanawake.  Washiriki hao walikaa kijijini kwa muda wa siku 21  hatimaye kufikia kumpata mshiriki mmoja ambaye amejishindia kiasi cha Tsh 20,000,000 fedha ambazo zitanunua pembejeo za Kilimo. Fainali hizo zilifanyika katika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam 
 Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne akitoa neno la Shukurani kwa ushindi alioupata , Ameshukuru shirika la Oxfam kwa kuendesha shindano hilo na kuahidi kuwa atakwenda kuwa Balozi mzuri na kusema kuwa washiriki wote ni washindi na yeye amepata zawadi hiyo kuwawakilisha wote.
 Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa Nne 2015 Bi. Carolina Chilele(Kulia) akikabidhiwa Ngao yake ya Ushindi na Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam

Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images