Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

MSAMA PROMOSHENI KUANDAA TAMASHA LA KUOMBEA AMANI HAPA NCHINI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

0
0
 Muandaaji wa matamasha ya injili hapa nchini, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari katika ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kuhusiana na tamasha la kuombea Amani ya nchi juu ya uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu hapa nchiini na kushoto ni Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya tamasha la kuombea amani ya nchi yetu kuelekea uchaguzi, Hamis Pembe. Msama pia aliipongeza serikali kwa kukataza uwanja wa taifa kutumika kufanyia matukio ya kisiasa. Pia amesema kuwa katika tamasha hilo litahudhuriwa na wananchi mbalimbali pamoja na wasanii wa nyimbo za injili hapa nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Alex Msama jijini Dar es Salaam leo. pia amengeza kuwa kwa waimbaji waliopo tayari kwa tamasha hilo ni pamoja na Boniface Mwaitege pamoja na Christopher Mwahangira.


Picha na Avila Kakingo Globu ya Jamii.


VIJANA WAHAMASISHANA JUU YA FURSA ZILIZOPO NDANI NA NJE YA NCHI

0
0
Mwenyekiti na mwanzilishi wa kikundi cha vijana cha Tanzania Youth Network (TYN), Agnes Mgongo akizungumza na vijana mara baada ya kukutana  katika ukumbi wa Don Bosco  jijini Dar es Salaam leo.
Afisa vijana  wa wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo, Racheal Kasanda akizungumza na vijana mbalimbali waliounda kikundi kiitwacho Tanzania Youth Network (TYN), wakijadili changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana pamoja na vijana kuunda vikundi mbalimbali ili kutumia fursa zilizopo hapa nchini na Nje ya nchi ameyasema hayo katika mkutano uliowakutanisha vijana hao katika ukumbi wa Don bosco jijini Dar es Salaam leo.
Afisa vijana  wa wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo, Racheal Kasanda  akipokea kitabu cha ujasiliamali  kutoka kwa Balozi wa vijana wa jumuia ya Afrika Mashariki, Eric Ngilangwa katika mkutano wa vijana uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.





Baadhi ya vijana wakiwa katika mkutano uliowakutanisha vijana mbalimbali leo jijini Dar es Salaam.
Afisa vijana  wa wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo, Racheal Kasanda akiwa katika picha ya pamoja na kikundi kilichowakusanya vijana mbalimbali kutoka Bagamoyo,Morogoro pamoja na Dar es Salaam.

Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.  Picha zaidi BOFYA HAPA

GLOBAL EDUCATION LINK (GEL) YASAFILISHA WANAFUNZI KWENDA KUSOMA NCHINI INDIA

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, Abdulmalik Mollel akiwa ameambatana na wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwasindikiza wanafunzi 30 wanaokwenda kusoma nchini India jana Agosti 21, 2015 katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, Abdulmalik Mollel akiwaita majina wanafunzi waliokuwa wanaondoka kwenda kusoma vyuo vikuu nchini India mapema jana Agosti 21, 2015 katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, wakikagua wanafunzi vyaraka muhimu walizopaswa kusafiri nazo ikiwemo viza, vyeti, na passport.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, Abdulmalik Mollel akiwaonyesha wanafunzi sehemu ya kwenda kukaguliwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

SHERIA MTANDAO: YASIYOTAJWA ITAKAPO ANZA KUTUMIKA SEPTEMBA MOSI

0
0

Na Yusuph Kileo
Zikiwa zimebaki siku chache kuanza kutumika kwa sheria mtandao Nchini Tanzania, Mengi yame endelea kuzungumzwa ikiwa ni pamoja na kurudia mapungufu yaliyopatikana katika sheria ya awali iliyo wasilishwa bungeni na kusambazwa kwa maneno kua sharia hii mtandao ipo kuziba watanzania midomo huku wengine wakizungumzia itakiuka faragha za watanzania. Sheria hii inakuja kusaidia mambo mengi na ni wazi mengi hayo yamekua hayazungumzwi kabisa.
Hivi karibuni kupitia mkutano mkuu wa mwaka wa maswala ya usalama mitandao ambapo moja ya mijadala iliangazia sharia hii na kutolea ufafanuzi yale yaliyokua hayajaeleweka vizuri. Binafsi Nilikua mmoja wa washiriki ambapo kwa ujumla wetu tulianisha mambo kadhaa na kuzidi kutoa hofu kwa yale ambay yameendelea kupotoshwa kuelekea matumizi ya sharia hii mtandao. Makala hii itajikita kwenye hayo yasiyo zungumzwa kwa wingi hivi sasa.
Upotevu wa fedha, hivi karibuni akizungumza na Jeshi la polisi waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alitahadharisha kua shilingi trilioni 54.4 zitakuwepo kwenye hatari ya kuingia katika mikono ya wahalifu wa mitandao, endapo Sheria za Mitandao na Miamala ya fedha haitatumika.
Alianisha kua fedha hizo ni sawa na trioni 4.4 kila mwezi. Profesa Mbarawa amesema fedha hizo lazima zilindwe  kwa kuwekewa sheria zenye kuzuia na kutoa adhabu kwa watu watakaoingilia mihamala ya fedha. Kuzilinda fedha hizo Sheria mtandao haina budi kuwepo ili kuwapa uwezo wahusika kufanya kazi yao ipasavyo.

YANGA YATWAA NGAO YA JAMII KWA KUICHAPA AZAM KWA MIKWAJU YA PENATI 8-7 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO

0
0
 Kikosi cha Timu ya Yanga, kikishangilia kwa pamoja ushindi wao mara baada ya Ngao ya Jamii yenye kuashiria kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, katika mtanange uliopigwa jioni hii dhidi ya Timu ya Azam, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Yanga imepata ushindi huo kwa mikwaju ya penati 8-7, baada ya dakika tisini za mchezo kumalizika bila kufungana.
Wachezaji wa Timu ya Yanga, wakishandilia ushindi wao huo pamoja na mashabiki wao wakuojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kushabikia timu yao iliyokuwa ikikipiga na Timu ya Azam. Yanga imepata ushindi huo kwa mikwaju ya penati 8-7, baada ya dakika tisini za mchezo kumalizika bila kufungana.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amis Tambwe akiondoka na mpira mara baada ya kumpiga chenga ya mwili Beki wa Timu ya Azam, Pascal Wawa (aliekaa chini) wakati wa mtangange wa kuwania Ngao ya Jamii ya Ufungunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, hakuna timu iliyoona lango la mwenzie mpaka dakika hii.
Kiungo machachari wa Azam, Farid Mussa akiangalia namna ya kumtoka, Geofrey Mwashiuya wa Yanga, wakati wa mtangange wa kuwania Ngao ya Jamii ya Ufungunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, hakuna timu iliyoona lango la mwenzie mpaka dakika hii.
Beki wa Azam, Pascal Wawa akionyesha umahiri wake wa kuondosha hatari langoni kwake mbele ya Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Mshumaa wa wiki.....Barry White

0
0
 Mshumaa wa wiki ni kipengele kinachozungumzia kuhusu msanii ama kundi la muziki wa zamani katika kipindi cha Mishumaa ya Kale. Kipindi hiki hukujia kila Ijumaa kuanzia saa 11 jioni mpaka 1 usiku kwa saa za Marekani ya Mashariki Kinatayarishwa na kurushwa na Vijimambo Radio na Kwanza Production, kwa ushirikiano na NesiWangu Media

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU CCM YAKAMILIKA, MAGUFULI, SAMIA KUUNGURUMA JANGWANI KESHO

0
0
 Katibu Muenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Juma 'Gadafi' akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisi kwake leo asubuhi, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya uzinduzi wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa chama hicho utaofanyika kesho viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

SIMU TV: HABARI KUTOKA KATIKA VITUO VYA LUNINGA

0
0

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

INTRODUCING FAU - KIDEGE (OFFICIAL MUSIC VIDEO)

HAPPY BIRTHDAY BLOGGER MC BARAKA WA BUKOBA WADAU BLOG

0
0
Leo Aug 23 ni siku ya kuzaliwa kwangu Mwanalibeneke Mc Baraka,Namshukru sana mwenyezi mungu kwa kunilinda mpaka kufika hapa nilipo. Namshukuru Mola kwa kunipa nguvu na ujasili wa kupambana na misukosuko ya hapa na pale,hakika yeye ndiye muweza wa kila jambo .
Natoa shukrani kubwa kwa timu nzima ya BUKOBAWADAU Media na member wa TBN na wote waliweza kuwa nami katika safari yangu ya maisha mpaka hii leo Inshaalah namuomba Mwenyezi mungu (Omkama Katonda) aniongezee uhai na uzima HAPPY BIRTHDAY TO ME!

JEMBE FM MWANZA YAFUNGUA MILANGO KWA VYAMA VYA SIASA KUTANGAZA MIKUTANO LIVE.

0
0
 Mbio za kampeni ya uchaguzi mkuu 2015 tayari zimeanza. Ni wasaa sasa kwa wagombea wa vyama mbalimbali kupishana huku na kule vijiji kwa vijiji, kata kwa kata, wilaya kwa wilaya, mkoa kwa mkoa wakifanya mkutano ya kampeni za siasa kutambulisha wagombea wao na kuzinadi sera zao al-muradi wapate ridhaa ya wananchi. 


Zoezi hilo ni gumu ila sisi kama jEMBe fM tunalirahisisha!! Sasa ili upate kuwafikia wananchi wengi ndani ya muda mfupi jEMBe fM imefungua milango kwa kutoa huduma ya matangazo ya moja kwa moja yaani LIVE toka viwanja vya mikutano tena full kiwango (HATUBAHATISHI) kwa maelezo zaidi piga simu kitengo cha masoko katika namba ±255282506068 au fika katika ofisi zetu zilizopo jengo la PPF ghorofa ya 6.



@jembenijembe

SIMU TV: MPAMBANO WA KOMBE LA HISANI AZAM VS YANGA

0
0
SIMUtv: Mpambano wa kinyanganyiro cha kombe la ngao ya hisani kati ya Azam FC na Yanga umepamba moto huku bao bado ni bila. https://youtu.be/MbaSDAaq3XM
SIMUtv: Mambo ya Msuva dimbani ni hatari sana, hebu cheki  akionyesha jitihada na maujuzi yake dhidi ya goli  la Azam; http://simu.tv/OvKYhrO
SIMUtv: Ule wasaa uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu hatimaye umewasilili, dimbani ni Yanga FC na Azam FC  wakilisakata . Endela kuwa na Simu.Tvhttps://youtu.be/cjSAxyHE5kA
SIMUtv:  Ni dakika ya 15 si yanga wala azam imeweza kuona lango la mwenzake lakini yanga wanapata kadi ya manjano; https://youtu.be/yg-go2m8Jds
SIMUtv: Azam walazimika kubadilisha mchezaji kabla hata ya dakika 30, ni baada ya beki Shomari Kapombe kupata jeraha na kutolewa nje ya uwanja; https://youtu.be/yg-go2m8Jds
SIMUtv: Mambo ya Msuva dimbani ni hatari sana, hebu cheki  akionyesha jitihada na maujuzi yake dhidi ya goli  la Azam;  https://youtu.be/hoIsRcCcWGM

MAFUNZO YA HUDUMA ZA LESENI KWA NJIA YA MTANDAO MKOANI KATAVI

0
0
Hatimaye mafunzo ya matumizi ya mfumo wa huduma ya leseni kwa njia ya mtandao yaani Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP) kwa wachimbaji madini mkoani Katavi yamemalizika. 
 Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya Maji, mjini Mpanda na kuhudhuriwa na wachimbaji wadogo wa madini kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo yakiwa yamelenga kuwapatia uwezo wachimbaji madini wa kuutumia mfumo huo. 
Akizungumza kwa niaba ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda Magharibi-Mpanda, Mhandisi Gilliard Luyoka aliwakumbusha wachimbaji hao kuhakikisha wanafika kwenye Ofisi ya madini ili kusajiliwa kwa ajili ya kutumia mfumo huo. 
 Pamoja na malengo mengine, inaelezwa kwamba Mfumo huo umeanzishwa ili kutekeleza agizo la Serikali la kutaka Wizara na taasisi za Serikali ziwe zinapokea malipo ya Serikali kwa njia za kielektroniki. Mfumo wa Huduma za Leseni kwa njia ya mtandao ulizinduliwa rasmi mnamo tarehe 8 Juni, 2015.
 Mhandisi Gilliard Luyoka akizungumza kwa niaba ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda Magharibi-Mpanda wakati wa mafunzo hayo


 Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Kitengo cha Leseni, Idd Mganga akiwasilisha mada wakati wa mafunzo hayo.

 Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini wakifuatilia mafunzo hayo


Mwenyekiti wa KATAREMA, William Mbogo (kulia) akiuliza swali kwa Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idd Mganga (kushoto)

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AMDUNDA ALLY MUHURO KWA T.K.O YA RAUNDI YA TATU

0
0

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' (kulia) akimshambulia kwa makonde mazito Ally Muhuro wakati wa mpambano wao ulifanyika siku ya jumamosi Class alishinda kwa T.K.O ya raund ya tatu Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' (kushoto) akimtupia konde mpinzani wake Ally Muhuro wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamos Class alishinda kwa T.K.O raundi ya tatu Picha zaidi BOFYA HAPA

AFRICAN IN NEW YORK: What Do We Learn from the People of Benin?

0
0
Chams Linkpon is the founder of Chegoun Production, an organization that helps African Artists to get performances and shows in the United States.
With the Beninese origin, Chams understands the challenges facing African artists and wants to help them promote themselves here in the United States where he believes that the market is open to everybody.
This is a good opportunity for artists from Africa to connect with Chegoun Production, and, perhaps who knows what Chams and his colleagues could do to help them get some gigs here in the US apart from realizing their dreams of promoting the African Artists?

In this interview Chams explains in details what his plans are. Stay tuned.

You are welcome to watch this show on Friday August 28th from 4:00 pm to 5:00 pm (New York Time) on the following channels depending on who your service provider is. Total Duration: 60 Minutes. The above video has only 36 minutes of the 60 minutes. To watch the entire 60 minutes of the show please see the details below.

Provider Channel
Times Warner Cable (TWC) 67 and 1998
FiOS 36
RCN 85
To stream online tune to channel 4 @ www.mnn.org/4-culture-channel%20 every friday from 4:00 pm to 5:00 pm (New York Time).
Thank You and Stay Tuned.

KAMPENI ZA URAIS ZAANZA RASMI, TUME YATOA RATIBA ZA MAENEO NA MUDA WA KAMPENI

0
0

Tume ya Taifa ya uchaguzi inakutana na Kamati Maalumu inayo undwa na wajumbe kutoka vyama nane vilivyo na wagombea wa urais na makamo kuandaa Ratiba ya mikutano ya hadhara kurahisisha kubaini vyama vilivyopanga mkutano mmoja katika mkoa mmoja, wilaya moja, na Eneo moja kwa Tarehe moja
Mkurugenzi wa NEC Kailima Ramadhani amesema anafarijika sana na ushirikiano wanaouonyesha Wawakilishi Wa vyama katika kuhakikisha mchakato kuwa wa Amani na utulivu bila kujali itikadi za vyama vyao kikao kitaendelea  hadi kufikia makubaliano ya Ratiba kwa vyama vyote.

+255(0)772 55 55 53
LISTEN LIVE
http://myradiostream.com/focusradiotz
Tume ya Taifa Ya Uchaguzi Tanzania
FACEBOOK
http://bitly.com/1zIiIkq 
TWITTER
http://bit.ly/1678Vq2

SIMU TV: CHAMBUZI NA MIJADALA KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI ASUBUHI YA LEO

0
0
SIMUTV: Nape azungumzia ufunguzi rasmi wa kampeni za CCM hii leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam.
SIMUTV: Nape Nauye asema kwa mara ya kwanza uongozi wa CCM umezingatia demokrasia kwa Kumteua Mgombea mwenza Mwanamke, huku akitanabaisha mfumo wa CCM.
SIMUTV: Nape Nauye azungumzia wanao kihama chama chao huku akisema ni jambo jema kwani wanakipa ahueni chama cha Mapinduzi
SIMUTV: Mchambuzi mahili wa Siasa Hamphrey Polepole, azungumzia kasumba ya baadhi ya Mkada wa CCM kukatwa huku akisema dhahiri kwamba vigezo na mashariti vilizingatiwa kikamilifu
SIMUTV: Mchambuzi Hamphrey Polepole Akinzana na hoja pamoja na kuhama kwa Fredrick Sumaye huku akisema yeye ndiye aliyekuwa akimponda Lowassa akimwita Fisadi na aliapa kujitoa CCM endapo akichaguliwa, iweje leo anaungana naye ili hali alimwita Fisadi; https://youtu.be/J-5ljUokNog
SIMUTV: Hamprey Polepole atanabaisha dhahiri kwa hoja tunduizi ya kwamba, Dr.Magufuli alikidhi vigezo na Masharti yote yaliyowekwa na CCM hivyo ni Chaguo Sahihi
SIMUTV: Hamphrey Polepole, asema si vibaya mtu kuwa tajiri ila jinsi unavyotumia utajiri wako kama kiongozi ndio tatizo kubwa huku akelezea mienendo na mashaka ya baadhi ya Viongozi wa juu katika kusaka madaraka kwa utajiri wao; http://youtu.be/xZ6E5Cyykuo

KILOMETA 6,276 ZA BARABARA ZAJENGWA NCHINI KWA MIAKA 10

0
0
Ujenzi wa barabara ya Iringa-Dodoma umekamilika kwa asilimia 95, bado maeneo machache tu likiwemo hili la Mlima Nyang'oro ambapo Wachina wameuchonga ili kupunguza kona katika umbali wa kilometa 15. 
Wakati wakandarasi walipokuwa wanajenga daraja hili katika eneo la Miangalua kwenye barabara ya Tunduma-Sumbawanga mwaka 2011. Barabara hiyo sasa imekamilika.
Barabara ya Mwanza-Musoma iko katika hali nzuri. 
Ujenzi wa barabara ukiendelea katika baadhi ya miradi nchini.

MAMIA WAJITOKEZA KATIKA UFUNGUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU ZA CHAMA CHA CCM LEO

0
0
Mzee akiwa amevaa Picha ya Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,John Magufuli leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.




Wiliam ngereja ajitokeza katika kumunga mkono Magufuli katika ufunguzi wa Kampeni leo jijini Dar es Salaam.
Vijana wakiwa wamebebana ili waweze kuona mbele katika ufunguzi wa kampeni za chama cha mapinduzi leo katika viwanja vya Jangwani  jijini Dar es Salaam.
 Furaha imetawala kwenye mioyo ya wanaCCM kama inavyoonekana kwenye taswira yetu hapo katika ufunguzi wa kampeni za chama cha Mapinduzi CCM kwenye viwanja vya jangwani leo jijini Dar es Salaam.
 Vijana wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam leo. 
Picha na Avila Kakingo na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.


Mambo yoote Jangwani leo

0
0
Kwa wale ambao wako mikoani na wale waliopo nje ya nchi, mnaweza kutazama Uhuru Tv kwenye kinga'amuzi cha Digitek na Azam chanel number 2017 au online www.uhurutv.co au www.ccmtv.co 
Itakuwa live kutoka Jangwani.
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images