Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MSAJILI WA MAHAKAMA YA RUFANI APONGEZWA BAADA YA KUAPISHWA LEO

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akimkabidhi shada la ua Mhe. Katarina Revocatti, Msajili Mteule wa Mahakama ya Rufani mara baada ya kuapishwa na Mhe. Rais mapema leo tar. 08.01.2015.
Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania, Mhe. Ignas P. Kitusi akimpongeza Mhe. Katarina Revocatti kwa kuteuliwa kwake kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani (T).
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, (kulia), Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Ignas P. Kitusi (Kushoto), Mhe. Katarina Revocatti, Msajili Mteule wa Mahakama ya Rufani ( katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Mahakama katika hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika katika Ofisi za Mahakama ya Rufani (T) baada ya kuapishwa kwake na Mhe. Rais. (Picha na Mahakama).

Rais Kikwete amwapisha Msajili wa Mahakama ya Rufaa

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Msajili wa Mahakama ya Rufaa Bibi Katarina Tengia Revocati ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi muongozo wa kazi Msajili wa Mahakama ya Rufaa Bibi Katarina Tengia Revocati ikulu jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Freddy Maro).

MAKALA YA SHERIA: JIFUNZE NAMNA YA KUANDIKA MKATABA KISHERIA UNAPOUZA AU KUNUNUA

$
0
0

Na  Bashir   Yakub

Katika shughuli zetu za kuuza na kununua  ambazo tunazifanya kila siku mikataba ya maandishi  ni jambo ambalo wengi tunakutana nalo. Mikataba hii iwe rasmi au isiwe rasmi suala la msingi ni kuwa  huwa tunaifanya. Aidha wakati mwingine si  wote wenye kuhusisha suala la mikataba ya maandishi  katika makubaliano yaombalimbali  na hii hutokana na  sababu mbalimbali ikiwemo ya kuaminiana. 
Kuhusu kuaminiana niseme jambo moja tu kuwa suala la mikataba ni muhimusana  hata kana  mwenzako unamuamini kwa kiwango cha juu kabisa( highest degree of trust). Nathubutu kusema kuwa hata awe mzazi wako kama kuna jambo la msingi mmelifanya  ni vema kukawapo mkataba wa maandishi.  
Nasema hivi kwakuwa kwa uzoefu wangu wa mambo haya  mara nyingi mgogoro hautokani na waliouziana  au kukubaliana isipokuwa mgogoro unakuja kuanzishwa na walio nyuma ya hao.  Kwa mfano baba anaweza kumpa mwanae kiwanja   na wasifanye  mkataba wowote wa maandishi kwa kuwa wanaaminiana. 
 Hiyo ikaenda kwa miaka kadhaa ambapo baba akawa amefariki. Baaada ya hapo anaibuka mtu anasema mimi  ni mtoto wa  marehemu kwa hiyo nahitaji  kiasi kadhaa kutokamali hii. Hapa mgogoro si kati ya baba na mwana tena   isipokuwa ni kati ya mwana na mtu mwingine. Kama huna mkataba wowote wa maandishi  mpaka kesi hii kuisha waweza kuwa umepoteza kila kitu. 
Huu ni mfano tu katika kusisitiza kuwa mtu asiseme mi na  fulani tunaaminiana. Mgogoro sio lazima utokane na nyie wawili  isipokuwa walio nyuma yenu waweza kuanzisha mgogoro.

MADHARA   YA   KUTOFANYA  MKATABA  WA  KISHERIA .

Ni vema sana kujihadhari kwakuwa ukisikia neno  mgogoro ujue kuna mambo makubwa mawili. 
Kwanza gharama kubwa ni uwezekano wa kupoteza kabisa ilemali na haijalishi iwe uliinunua au ulipewa isipokuwa tu ukishakuwa na mgogoro upo katika hatari hiyo. Pia gharama ya pesa  kama kuwalipa wanasheria, gharama za uendeshaji kesi,  nauli  na matumizi mengineyo ambayo hujitokeza bila hata kutarajia. 
Pili kuna  gharama ya muda . Hii  huhusisha  kushinda mahakamani kila siku  na wote mwajua  mahakama zetu  zilivyo, kushinda vituo vya polisi huku shughuli zako za msingi za kila siku zikisimama. Pia hapa  kuna muda wa  kusubiri hukumu ambapo kesi yaweza kukaa mahakamani hata miaka  sita . Hakika unakuwa umesurubika(suffer) na  umepoteza mambo mengi katika kushughulikia jambo hili.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE KUANZA TAREHE 13 – 23 JANUARI 2015

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA




BUNGE LA TANZANIA


TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO HABARI KUHUSU VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE KUANZA TAREHE 13 – 23 JANUARI 2015


Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawatangazia Waheshimiwa Wabunge wote, wadau na umma kwa ujumla kuwa Kamati za Kudumu za Bunge zitaanza vikao vyake tarehe 13 hadi 23 Januari 2015. Vikao hivyo vitakavyoutangulia mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge la Kumi vitajadili na kuchambua pamoja na mambo mengine Miswada mbalimbali ya sheria.


Miswada  itakayopitiwa na chambuliwa (pamoja na kamati husuka kwenye mabano) ni hii ifuatayo:

        i.            Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji wa Mwaka 2014 [The Immigration (Amendment) Bill, 2014], [Kamati ya Mambo ya Nje]


     ii.            Muswada wa Sheria ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI wa Mwaka 2014 [The Tanzania Commision for AIDS (Amendment) Bill, 2014, [Kamati ya Masuala ya UKIMWI]


   iii.            Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Silaha wa Mwaka 2014 [The Firearms and Ammunition Control Bill, 2014], [Kamati ya Ulinzi na Usalama]


   iv.            Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wa Mwaka 2014 [The Disaster Management Bill, 2014], [Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala]


       v.            Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Ajira za Wageni wa Mwaka 2014 [The Non-Citizen Employment Regulation Bill, 2014], [Kamati ya Maendeleo ya Jamii]

   vi.            Muswada wa Sheria ya Wataalam wa Kemia wa Mwaka 2014 [The Chemist Professionals Bill, 2014], [Kamati ya Huduma za Jamii]


 vii.            Muswada wa Sheria ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2014 [The Government Chemistry Laboratory Bill, 2014], [Kamati ya Huduma za Jamii]


 viii.            Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Stakabadhi Ghalani wa Mwaka 2014 [The Warehouse Receipts (Amendment) Bill, 2014, [Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara]. Angalizo: Wakati wa uchambuzi Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara itashirikiana na  Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji.


    ix.            Muswada wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya wa Mwaka 2014 [The Drug Control and Enforcement Bill, 2014], [Kamati ya Masuala ya UKIMWI]


       x.            Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2014 [The Written Laws (Miscelaneous Amendments) Bill, 2014, [Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala]. Angalizo: Aidha inashauriwa wakati wa kuchambua Muswada huu Kamati za kisekta zishirikishwe kwenye  kutoa maoni kwenye marekebisho ya sheria ya sekta husika.


    xi.            Muswada wa Sheria ya Bajeti wa Mwaka 2014 [The Budget Bill, 2014], [Kamati ya Bajeti]


Aidha, kwa taarifa hili Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaombwa kuwasili Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Januari 2015 tayari kwa kuanza kazi tarehe 13 Januari 2015.


Imetolewa na Ofisi ya Bunge,

Idara ya Habri, Elimu kwa Umma na

Uhusiano wa Kimataifa


07 Januari,  2015

Vijana Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara wajiajiri kupitia mfuko wa mendeleo ya Vijana

$
0
0
Kikosi kazimaalum kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo wa kiongea na Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ,Bw. Rashid Mohamed walimpotembelea leo ofisini kwake kwa ajili ya kufuatilia na kufanya tathmini ya mikopo iliyokwishatolewa katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-mikindani.
Wajumbe wa kikundi cha AMKENI kutoka Halmashauri ya manispaa ya Mtwara mikindani wakiwa katika majadiliano na wajumbe wa kikosi kazi maalum kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo walipowatembea leo ili kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mikopo iliyokwishatolewa kwa kikundi hicho ilikujua nichangamoto gani wamekutana nazo ilikuboresha zaidi Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Afisa Uchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo ,Bw.Yohana Ngao akiwa katika majadiliano na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara Vijijini Bw.Oscar Ng’itu ilikujua maoni na changamoto wanazopata wana vikundi waliopata mkopo kupitia mfuko wamaendeleo yaVijana katika eneo lake.
4875:Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mtwara Vijijini Bw. Musa Said akimkaribisha ofisini kwake kiongozi wa kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Afisa uchumi mwandamizi Bw.Ngao Yohana walipotembelea wilaya iyo ilikufanya tathmini na ufuatiliaji wa mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

SEAN TIZZLE EXCLUSIVE ON THE SPORAH SHOW

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue akutana na Mabalozi ikulu

$
0
0
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akikutana na mabalozi wa nchi za nje na wakuu wa mashirika ya kimataifa yaliyo chini ya Umoja wa Mataifa Ikulu jijini Dar es Salaam leo
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea  na mabalozi wa nchi za nje na wakuu wa mashirika ya kimataifa yaliyochini ya Umoja wa Mataifa ikulu jijini Dar es Salaam leo
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisikiliza hoja za mabalozi wa nchi za nje na wakuu wa mashirika ya kimataifa yaliyochini ya Umoja wa Mataifa ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Freddy Maro

TAARIFA YA MHE LAZARO NYALANDU

$
0
0
Waziri Nyalandu
SIKU ya Mkesha wa Mwaka Mpya, Desemba 31, 2014, nilikaribishwa kushiriki ibada ya Mkesha na Baba Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ephata, Josephat Mwingira, iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Mkesha huo ulitangazwa moja kwa moja kwenye kituo cha luninga cha Star TV na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.
Katika Mkesha huo, nilipewa fursa ya kuwasalimia waumini na kushirikiana nao katika neno la Mungu, ambapo huku nilieleza matumaini yangu kwa Taifa letu na ushiriki wa vijana katika uongozi wa nchi, kama yanenanvyo maandiko 'vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataona ndoto'. 
Hata hivyo, jana nimesikitishwa sana na kuumizwa na habari ambazo hazina mashiko, za uzushi na za kutunga zenye lengo la kunipaka matope kwa kunihusisha na maneno ambayo kinywa changu hakikuyatamka wala kuyafanyia rejea. Nimeshangazwa sana.
Katika maisha yangu kama mtanzania, kiongozi na mkristo, kamwe sijawahi na sitarajii kutoa kauli hasi dhidi ya imani za dini ningine, ikiwepo dini ya Kiislamu. Nisisitize kuwa ninawapenda watu wa dini zote na makabila yote na kamwe sina ubaguzi kama inavyojaribu kuwekwa ili kunipaka matope katika jamii. Naamini taarifa hizo potofu zina malengo binafsi na watu wasionitakia mema.
Katika jimbo langu la Singida Kaskazini, nimeshiriki kusaidia ujenzi wa nyumba za ibada ikiwemo makanisa na misikiti kwa uwazi kwa kuboresha miundombinu na kuziwezesha taasisi hizi kutoa mchango katika elimu.
Sio hivyo tu, kuonyesha ninachojaribu kuzungumzwa kuwa ni uongo na uzushi mtupu, katika Jimbo la Singida Kaskazini, nimepeleka masheikh wa vijijini mbalimbali kwa ajili ya kuhiji Mecca, mpango ambao ni endelevu kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Ni muhimu demokrasia ikaendelezwa kwa kuhimiza mijadala ya kuwaletea wananchi maendeleo na sio kwa kueneza chuki za kidini, kijinsia au kikabila.
Mungu ameliweka Taifa letu kuwa heri katikati ya mataifa na ni muhimu sote kudumisha amani na mshikamano badala ya kusingiziana uongo. Imeandikwa katika vitabu, usimsingizie jirani yako uongo'.

Imetolewa na
Lazaro Nyalandu,
MNEC, CCM


mambo ya nathan mpangala

MAELEZO BADILISHENI MFUMO WA UTOAJI PRESS CARD

$
0
0

WASOMAJI na wadau wangu nawasalimu na naimani kuwa Mwenyezi Mungu ametujalia tumeuona mwaka mpya wa 2015 salama salmini. Nawatakia heri na fanaka katika mwaka huu pia na karibuni tena katika porojo zangu za ukweli.

IDARA ya Habari –MAELEZO ndiyo idara ya serikali inayoshughulika na kufanya kazi zake kama chombo cha usimamizi wa vyombo vya habari na waandishi wake.

Idara hiyo pia ndio msemaji wa masuala mbalimbali ya serikali lakini pia ndiyo idara yenye jukumu la kusajili au hata kuyafutia usajili magazeti hapa nchini na vyombo mbali mbali vya hjabari.

Waandishi wa habari waajiriwa na wale wa kujitegemea wameanza mchakato wa kujaza fomu kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vipya vya kazi (PRESS CARD) kwa mwaka 2015.

Jambo hili ni zuri kwa waandishi wa habari maana kitambulisho hicho cha serikali hutolewa kwa waandishi walio na sifa za uandishi tu na sio wale waparamia fani za watu maarufu kama kanjanja.

Ndio! Uandishi wa habari ni taaluma kama taaluma nyingine, kwa hiyo kila mwanahabari anatakiwa kuwa na Press Card ambacho ndicho kitambulisho cha serikali, kama huna basi wewe sio muandishi au laa hujakomaa kuwa muandishi. 

MWANASHERIA MKUU AMTEMBELEA SPIKA MAKINDA OFISI NDOGO ZA BUNGE JIJINI DAR

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anne Makinda akimkaribisha ofisini kwake Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Masaju wakati alipofanya ziara fupi ya kubadilishana mawazo hii leo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju akitia saini kwenye kitabu cha wageni wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kuanza kubadilshana mawazo. Ziara hiyo fupi imefanyika ofisi ndogo za bunge Dar-es-salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Masaju akiwa kwenye mazungumzo ya kubadilishana mawazo na Spika wa Bunge Mheshimiwa Anne Semamba Makinda kwenye ofisi ndogo za bunge Dar-es-salaam.

Mada ya mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia na athari zake kwa nchi yawasilishwa kwa maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje

$
0
0
Bw. Allan William mtaalamu wa sekta za kibenki nchini, akizungumza katika mhadhara na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa juu ya Mwenendo wa bei za mafuta duniani  na athari zake kwa nchi yetu, mhadhara huo umefanyika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa JNICC uliopo jijini Dar es Salaam mapema leo Asubuhi.
Balozi Simba Yahaya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati (wa kwanza kulia), Balozi Mbelwa Kairuki (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Austrasia na Bw. Togolani Mavura kwa pamoja wakimsikiliza kwa makini Bw. Allan William.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA MJINI ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, wakiwa katika Sala na Dua ya kumuombea aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bibi Fatma Othman Ali kabla ya mazishi yake iliyofanyika Januari 08,2015 katika msikiti wa Mohammed Ali Jang’ombe Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, wakisaidia kutoa nje ya msikiti Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bibi Fatma Othman Ali baada ya Sala na Dua maalum iliyofanyika Januari 08,2015 katika msikiti wa Mohammed Ali Jang’ombe Zanzibar.

TWAWEZA YAMUAGA RAKESH RAJAN JIJINI DAR LEO

$
0
0
Balozi wa Sweden nchini Tanzania,Mh. Lennarth Hjelmaker akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga aliekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza, Rakesh Rajani iliyofanyika jana jioni kwenye viwanja vya Karimjee,Jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga aliekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza, Rakesh Rajani iliyofanyika jana jioni kwenye viwanja vya Karimjee,Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza (aliemaliza muda wake), Rakesh Rajani (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe (katikati) pamoja na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (Mstaafu),Ludovick Utouh wakati wa hafla fupi iliyofanyika jana jioni kwenye viwanja vya Karimjee,Jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

JK kuzindua nyumba mpya za makazi ya Wanajeshi eneo la Gongolamboto kesho

$
0
0
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), linatoa taarifa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete atazindua nyumba mpya za makazi ya Wanajeshi eneo la Gongolamboto mnamo tarehe 10 Januari, 2015,    Saa 3:00 Asubuhi.
 
Aidha, uzinduzi wa nyumba hizo ni sehemu ya nyumba elfu kumi za  mwanzo za makazi ya Maafisa na Askari wa JWTZ zilizojengwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuondoa tatizo la nyumba za makazi kwa Wanajeshi.
 
Ujenzi wa nyumba hizo za kisasa umefanywa na Kampuni iitwayo ‘Shanghai Construction Group’ ya Jamhuri ya watu wa China.
 
Waandishi wa Habari wanaombwa kuhudhuria na kufanya ‘Coverage’ katika tukio hili muhimu.
   
 
Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

KUMBUKUMBU

$
0
0
CASSIAN KIGESO MALIMA


Ni kama jana tu lakini tayari leo imetimia miaka 6 tangu Mpendwa wetu Cassian Kigeso Malima ulipotutoka ghafla jioni ya tarehe 9 Januari 2009 katika hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaamna kupumzishwa katika makao ya milele kwenye makaburi ya Mwisenge, Musoma mjini tarehe 14 Januari 2009.

 Daima tutakukumbuka kwa upole, ucheshi na uchapakazi wakati wa uhai wako. Tunamuomba Mungu wa Rehema aendelee kukupumzisha kwake katika amani ya milele. Amina.


1 Wathesalonike 4:13-14 (Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti). 

TASWIRA YA MWAKA YA WADAU WA KUCHEKESHA NA KUHABARISHA

$
0
0
Si mara nyingi wadau hawa hukutana namna hii. Ila wakati wa mnuso wa kumuaga bosi wa taasisi ya Twaweza Rakesh Rajani jana jioni pale viwanja vya Karimjee ilikuwa tofauti. hapo mpiga picha aliambiwa apige full yaani viatu vionekane. Wao kwa pamoja tena bila kuambiwa na mtu wakainua miguu kumuonesha hivyo viatu. Kutoka kushoto ni Othman Michuzi, Masoud Kipanya, Nathan Mpangala "Kijasti", Evans Bukuku "Mnyambala", David Kyungu, Robert Mwampembwa "Bi Mkora", David Chikoko (Cartoonist wa the Guardian) na Ankal

Article 9

CCM YALAANI VIKALI VURUGU ZILIZOFANYWA NA WAFUASI WA CHADEMA NA CUF KWA VIONGOZI WAO WA SERIKALI ZA MITAA.

$
0
0
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itakutana Zanzibar Januari 13, kwa kikao cha kawaida cha siku moja chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete. 

Kikao hicho cha Kamati Kuu kitatanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu kitakachofanyika Januari 10, jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo CCM inalaani vikali vurugu zilizofanywa na wafuasi wa Chadema na CUF kwa viongozi wetu wa serikali za mitaa katika maeneo kadhaa nchini ikiwemo mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam na Mbeya.

Vurugu hizo zilizosababisha baadhi ya viongozi wetu kujeruhiwa zimetokea katika mkoa wa Mwanza ambapo Ndugu Christopher Mgeta kutoka Mtaa wa Ibungilo na Ndugu Pascal Charles wa Mtaa wa Kitangiri A katika wilaya ya Ilemela walivamiwa na kupigwa wakati wa kuwaapisha.

Katika mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Sultan Jeta wa mtaa wa Ukwamani katika jimbo la Kawe alifanyiwa fujo na wafuasi hao na Katika Mtaa wa Msisiri A kata ya Mwananyamala katika jimbo la Kinondoni Ndugu Juma Mbena alipigwa na kuvunjwa mkono.

Katika Manispaa ya Ilala, wafuasi hao wa vyama vya upinzani walifanya vurugu wakati wa kuwaapisha viongozi hao wa serikali za mitaa wilayani humo na kusababisha zoezi hilo kuahirishwa.

Mkoani Mbeya vurugu za aina hiyo zimetokea katika wilaya za Kyela na Rungwe ambapo wilayani Kyela zoezi la kuapisha viongozi wa serikali za mitaa lilishindika na kuahirishwa kutokana na vurugu za kurushiwa mawe zilizofanywa na wafuasi wa Chadema walioletwa kutoka katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Katika kijiji cha Ilundo wilayani Rungwe wafuasi hao wa Chadema waliwapiga mawe viongozi na wanachama wa CCM na baadae kufyeka mashamba yao ya migomba na kusababisha vijana sita kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Rungwe kwa sababu ya hasira za kushindwa uchaguzi.

Vurugu hizi ni mwendelezo wa tabia na mazoea ya vyama vya upinzani nchini kutoheshimu na kufuata sheria na taratibu za nchi.  Tabia hizi si za kiungwana na ni uthibitisho wa kuharibikiwa na kufa kwa vyama vya upinzani nchini.  Mara zote wamekuwa wakikataliwa na wananchi kwa kura, wao hukataa uamuzi huo wa wananchi kwa kufanya fujo na vitimbi.  Asiye kubali kushindwa si mshindani.  Vurugu hizi sasa inatosha.

 Imetolewa na:-
  
Nape Moses Nnauye,    
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,

ITIKADI NA UENEZI
09/01/2015

ARUSHA KUPATA MIJI MIWILI YA KISASA-NHC

$
0
0
Wawasilishaji, James Kisarika, Yusufalli Murad, Meneja Mradi Wa USA River Satellite City na Ms. Meena Pandit, Mkurugenzi , PHILS International  ambao ni Washiriki wa NHC katika katika uendelezaji wa Mradi huo.
 Pichani.
James Kisarika akisalimiana na  Katibu Tawala Mkoa, Ndugu Ado Mapunda, muda mfupi Kabla kuanza mawasilisho ya Mradi Wa Safari City.
 Yusufalli Murad, Meneja Mradi Wa USA River Satellite City akitoa mada kuhusu mradi huo .
 Baadhi ya Washiriki wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) wakifutilia mawasilisho ya miradi ya Miji Midogo ya Safari Satellite City na USA River Satellite City.
Baadhi ya Washiriki wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) wakifutilia mawasilisho ya miradi ya Miji Midogo ya Safari Satellite City na USA River Satellite City.
 Mkuu Wa Mkoa mpya wa Arusha akifungua kikao cha RCC kabla ya Mawasilisho.

Arusha to get 2 new towns: NHC

The National Housing Corporation (NHC) plans to construct two satellite towns on the outskirts of Arusha, the Regional Consultative Committee (RCC) meeting was told here on Wednesday. The NHC regional manager for Arusha, Mr James Kisarika, named the sites as Usa River Satellite City to be put up on the southern fringes of the city and Safari Satellite City to be built at Mateves.
Mr Kisarika said the ambitious projects were in line with the vision of the oldest state-owned real estate corporation to address market needs for world class settlements.
“Arusha does not benefit much from tourism, as much of the receipts accrued from the hospitality industry go to hotels in Karatu township and national parks,” he observed.
Mr Kisarika said while the Usa River Satellite City targeted the tourism industry, the Safari one was meant for de-congesting the Arusha Central Business District (CBD).
Phils International, a firm manned by Tanzanians living in Dubai, which built Dubai Sports City, will construct the Usa River Satellite City at a 1.17-million-square-metre block situated a stone’s throw from Dolly Estate near Kilimanjaro International Airport. “One can reside at the Usa River Satellite City and work in Moshi Municipality or Arusha City,” Phils International director of Projects Murad Yusufali told the RCC.
He said the design of the city would enable each of the 19,000 dwellers in four petals of the residential segment to view both mounts Meru and Kilimanjaro from their living rooms.
“The city will tap underground water and use solar for street lights,” said Mr Yusfali, adding that a US firm would construct a sewerage system which would recycle sewage for irrigation usage.
He said the Lands, Housing, and Human Settlement Development ministry had approved a master plan for the project ready for the construction work to begin. CHANZO THE CITIZEN TANZANIA
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images