Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

WWF hands over Infrastructure to support Local Communities efforts in WMAs’ management

$
0
0
Mr. Lucason Maiga, representing the WWF TZ Country Director signing transfer documents of the cash for work infrastructure handover ceremony at Ipole WMA in April 2014.
Mr. Lucason Maiga handing over the signed Ipole WMA infrastacture documents to JUHIWAI Chairperson, Mr. Reuben Kasanda, witnessed by the Sikonge DC, Mrs. Hanifa Selengu.
Sikonge DC, Mrs. Hanifa Selengu tasting water pumped from water borehole at Ipole WMA, Tabora. The water pump installation was part of the facilities handed over to Ipole WMAs.

KATIBU MKUU WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA USAFIRI WA ANGA (ICAO) BW,RAYMOND BENJAMIN AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin baada ya kuwasilia katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,kwa ziara ya kikazi nchini kuanzia leo tarehe 14n hadi 18 Mei 2014. Tanzania ni moja ya nchi mbili ikiwemo Ethiopia atakazotembelea katika Kanda ya ICAO .
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe watatu kutoka (kushoto) akiwa na wakurugenzi wa Wakuu wa Mamlaka ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCCA) wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin wakati walipokuwa wakibadilishana mawazo baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi kuanzia leo tarehe 14n hadi 18 Mei 2014.
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin( Kulia) baada ya kuwasilia katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ziara ya Kiakazi hapa nchini.
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe wapili kutoka kushoto akiongea wakati alipokuwa akimkalibisha Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin watatu kutoka (kushoto)baada ya kuwasilia katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,kwa ziara ya kikazi nchini kuanzia leo tarehe 14n hadi 18 Mei 2014. Tanzania ni moja ya nchi mbili ikiwemo Ethiopia atakazotembelea katika Kanda ya ICAO .
Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) Raymond Benjamin wa tatu kutoka (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe na Viongozi mbalimbali wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania.

SAUTI SOL, RADIO &WEASEL, DJ TIRA KUPAMBA ZIARA YA KUHAMASISHA UTOAJI WA TUZO ZA MUZIKI ZA MTV JIJINI DAR KESHO

$
0
0
Ikiwa imebaki siku moja kufika ziara ya uhamasishaji wa tuzo za MTV wasanii kutoka sehemu mbalimbali nje ya Tanzania wanatarajiwa wasili jijini Dar es Salaam siku ya kesho kwa ajili ya maandalizi ya sherehe hiyo itakayo fanyika Club Bilicanas.

Wasanii watakao wasili siku ya kesho ni pamoja na Diamond aliyekua Uingereza, Proffesor (Afrika Kusini), Sauti Sol na Amani kutoka Kenya na Radio na weasel wa Uganda ambao wanatarajiwa kupanda jukwaani siku ya Ijumaa ya tarehe 16 Mei ndani ya ukumbi wa club Bilicanas.

Mbali na wasanii hao pia DJ Tira kutoka Afrika Kusini ambae pia ni DJ wa kituo cha Televisheni cha MTV Base nae anatarajiwa kuwasili siku ya kesho kwa ajili ya shughuli hiyo, ataungana na ma DJ wengine wakali kutoka hapa hapa Tanzania ambao watatoa burudani katika sherehe hiyo ya uhamasishaji wa tuzo za MAMA, nao ni pamoja na DJ Zero, DJ Steve B, na DJ Mafuvu.

Sherehe hizo zinalenga kuhamasisha wananchi katika kushiriki kikamilifu katika tuzo hizo na hapa nchini, zitafanyika Club Bilicanas , katika jiji la Dar es Salaam naTiketi zitauzwa mlangoni kwa bei ya shilingi 15,000 kwa mtu moja, mwezi ujao wasanii wataelekea jiji Lagos Nigeria kwa ajili ya uhamasishaji pia.
Vilevile  wasanii  kutoka Afrika Kusini akina mafikizolo na Davido wa Nigeria wamependekezwa kwenye vipengele vingi Zaidi ya moja, wamependekezwa katika vipengele vinne muhimu, hivyo wameumana katika kuwania tuzo za msani bora wa mwaka pamoja na wimbo bora wa kushirikishwa pia.

Pia kutakua na washiriki wawili  ambao ni Radio na weasel wa Uganda , na Kenya msanii Amini kupitia wimbo wake wa kiboko changu alioshirikiana na Radio and Weasel nao utashindanishwa.

MTV leadership ward, ni tuzo inayo lenga vijana wa Afrika wanaume na wanawake wenye umri mdogo mpaka miaka 40 ambao wanafanya vizuri kwenye mambo mbalimbali ikiwemo muziki biashara na science. MTV pia inatambua mafanikio ya muzkik na wana muziki ambao wana wakilisha Afrika nchini na inje ya Afrika.

MAMA 2014 itausisha wasanii  wa Afrika na wa Kimataifa pamoja ikiwa pamoja na tuzo 'sahihi kwa kushirikiana kati ya wasanii wa muziki na tamaduni mbalimbali.

 Upigaji kura MTV Africa Awards uko wazi kwenya  www.mtvbase.com kuanzia 16 April 2014 mpaka usiku wa manene  4 Juni 2014.

 Kwa maelezo Zaidi juu ya MTV Afrika Muziki Awards kwaZulu –Natal, tembelea tovuti www.mtvbase.com, like us on Facebook at www.Facebook.com/MTVBaseVerified, or follow us on Twitter @MTVBaseAfrica. To join the conversation about the awards please use the hashtag #MTVMAMA.

MACHIFU 120, MRISHO MPOTO NA WEMA SEPETU KUNOGESHA TAMASHA LA MTU KWAO ARUSHA

$
0
0
Na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii, Arusha
Zaidi ya machifu 100 kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini wanatarajia kushiriki  katika tamasha la "Mtu Kwao" linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi May 15 hadi 20 mwaka huu katika kiwanja cha kumbu ya sheikh Amri Abeid jijini hapa. 
Akiongea na waandishi wa habari jijini hapa Mratibu wa tamasha hilo ambaye ni mkurenzi wa kampuni ya Utamaduni Traning L.T.D Janeth Jonas alisema kuwa tamasha hilo litashirikisha machifu 120 kutoka katika mikoa mbalimbali na makabila mbalimbali ya hapa nchini. 
Alibainisha kuwa nia na dhumuni la kuandaa tamasha hili la mtamaduni wetu ni kuweza kuuenzi utamaduni wa mtanzani ambapo ni kuanzia mavazi ya makabila mbalimbali,vyakula pamoja na ngoma kutoka katika makabila yote hapa nchini.
“Pia katika tamasha hili tumeamua kuwaita machifu mbalimbali l kutoka katika makabila mbalimbali hapa nchini na baadhi ya mchifu ambao watauthuria ni pamoja na chifu kutoka oldmoshi ambaye yeye ameshawasili hapa Arusha kwaajili ya tamasha hili Gerald Mandera ,chifu Gilbert Rugal Isambe kutok a kasulu na wengine wengi wote watakuwepo”alisema Janeth
 Aidha alisema kuwa katika tamasha hili kila mtu atapata fursa ya kuona ngoma kutoka katika makabila mbalimbali pamoja na kuonja chakula cha kila aina cha makabila ya hapa nchini pamoja na nje ya nchi 
Alisema kuwa pia katika tamasha hili zaidi ya vikundi vya ngoma 100 vitatumbuiza pamoja na wasanii mbalimbali akiwepo msanii wa ngoma za utamaduni Mrisho mpoto, Wema Sepetu, kundi la Weusi kutoka Arusha, Jambo Squard, Dogo Janja pamoja na msanii kutoka nchini Kenya Daniel ole Sekuo. 
 Naye mmoja wa machifu ambaye atahudhuria tamasha hilo Chiefu Gerald Mandera kutoka Old Moshi alisema kuwa waandaaji wamefanya jambo jema sana kuanda tamasha hili kwani wao ndio wametambua uwepo wa machifu na wameona umuhimu wao mpaka wameamua kuwakusanya pamoja katika tamasha kama hili. 
 Alisema kuwa sasa hivi serikali nayo inawajibu wa kujipanga vilivyo na kutenga siku maalumu kwa ajili ya kufanya tamasha hili kama jinsi wenzetu kutoka katika nchi zingine wanavyo azimisha siku hii katika tarehe hizi na mwezi huu kila mwaka. 
Aidha alibainisha kuwa kuwakusanya watu mbalimbali kutoka katika tamaduni mbalimbali pamoja na makabila mbalimbali itasaidia kwani inaweza kuwezesha hata nchi kupata vazi la taifa kwani makabila haya yate yanakuja yakiwa yamevaa vazi la ukabila wao na hii itakuwa fursa pekee ya kuweza kuchagua vazi hasili la mtanzanzia.
 “Ni aibu kubwa sana unakuta sisi kama Watanzania hadi leo hii hatuna vazi linaloweza kutuwakilisha sisi kama Watanzania na ukiangalia wenzetu wa n je ya nchi wanamav azi yao ya kiutamaduni ambao ukimuona tu mtu amevaa unajua katoka katika kabila Fulani ,naitanishangaza sana kuona mtu anauzarau utamaduni wake na anauweka mbele utamaduni wa kigeni “alisema chifu Gilbert Isambe akibainisha kuwa hii ni fursa ya watu kuja kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo

 Chifu  Gilbert Isambe akiwa na vazi la kichifu
Chifu  Gilbert Isambe akiongea na vyombo vya habari. Pembeni yake ni mratibu wa tamasha la Mtu kwao Bi. Janeth Jonas










DAWASCO ISIYO RASMI YABAMBWA HUKO KIMARA

$
0
0
Hujuma ya Miundombinu ya Majisafi, wizi wa Maji ni vitendo vinavyoendelea kufanywa na wananchi licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali kuhakikisha huduma ya Majisafi ni muhimu kwa kila kaya. 

Hayo yameelezwa na Afisa Uhusiano wa DAWASCO Bi, Everlasting Lyaro wakati wa operesheni maalumu inayoendelea ya kuwabaini na kuwakamata wananchi wanaojihusisha na vitendo vya uhujumu wa shirika hilo. Alisema katika zoezi hilo maalum jumla ya watu na vifaa mbalimbali vilivyokuwa vinatumika kinyume na taratibu zilikamatwa.

 “Zoezi hili limeanza kwa maeneo yote ya Jiji na jana tulikuwa Kimara Michungwani ambapo tumekamata watu kadhaa na kuchukua matanki manne yenye ukubwa wa lita za ujazo 10,000, pampu 2 na mipira yenye ubora pungufu ya mipira inayotumiwa na inayoshauriwa kutumiwa na DAWASCO” Alisema Lyaro. 

 “Sisi tunaita huu ni ujangili maana ujangili sio tu kwa wanyama hata kwa maisha ya kawaida binadamu tunafanyiana ujangili mkubwa tu, leo hii mtu anaenda kukata mipira ya Maji ya kaya nzima ambayo wameungiwa kihalali na DAWASCO ili atengeneze mazingira ya yeye kuweza kufanya biashara ya Maji kirahisi hii haikubaliki hata kidogo, biashara ya Maji watuachie DAWASCO wenyewe” alifafanua Lyaro.

 Aliongeza kwa kutoa wito kwa wanachi kutoa ushirikiano kwa serikali yao yenye mipango mingi mizuri ya kuwapatia wananchi wake uhakika wa Maji kwa kutoa taarifa za wizi wa Maji na uharibifu wa miundombinu kwa mamlaka husika ili kuleta usawa kwa wananchi katika upatikanaji wa huduma hiyo.

 “Changamoto zipo bado katika upatikanaji wa Maji kwa wananchi hasa suala la Migao ya Maji, ila bado juhudi binafsi za wananchi zinahitajika katika kuelewa na kupunguza kero nyingine ambazo si za lazima katika kuipa DAWASCO nguvu ya kufikia malengo yake” alisema Lyaro Upatikanaji wa Majisafi na Salama kwa mkoa wa Dar umekuwa na changamoto mbalimbali, huku suala kubwa ikiwa ni Wizi wa Maji na uhujumu miundombinu ya Maji kwa maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam.
Nyumba iliyokamatwa kwa uhujumu wa miundombinu ya Maji pamoja na wizi wa Maji eneo la Kimara Michungwani ambapo ilikutwa na tanki 4 zenye ujazo wa lita 10,000 kila mmoja huku wananchi wa eneo hilo wakikosa huduma hiyo kwa takribani miezi 3 kutokana na uhujumu huo.
Sehemu iliyojengwa na wezi wa maji kama kituo cha kusambaza Maji (Pumping Statiion) kwa wateja waliofanya maungio kinyume na taratibu. Ilibainika zaidi ya wananchi wanne katika eneo la Kimara Michungwani.
Afisa uhusiano wa Dawasco, Bi Everlasting Lyaro akionyeshwa sehemu ya maungio ya wezi wa Maji ambapo mipira na pampu zilizotumika kufanya uhujumu uchumi zilikamatwa kwa ushirikiano wa wananchi na kikosi maalum cha DAWASCO.

WAZIRI WA FEDHA ZANZIBAR ASOMA HUTUBA YA BAJETI YA SERIKALI LEO

$
0
0
 Waziri wa Fedha Mhe. Omar Yussuf Mzee akionyesha begi lenye Hutuba ya Bajeti ya Serikali ya Zanzibar ya mwaka 2014-15.
  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifutilia Hutuba yamapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2014-15.
Baadhi ya wakuu wa sekta mbali mbali pamoja na wananchi wakisikiliza Hotuba ya Waziri wa Fedha Mhe. Omar Yussuf Mzee (hayupo pichani) kuhusu mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2014-15 katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Bweni Zanzibar. Picha na Makame wa Maelezo Zanzibar.

Diamond achaguliwa (nominated) kugombea BET Awards 2014

$
0
0

Msanii maarufu na mtumbuizaji Hapa nchini Nassib Abdul, maarufu kama DIAMOND PLATNUMZ,  ni miongoni mwa wasanii waliochaguliwa kwenda katika Tuzo za B.E.T zinazoandaliwa na kituo cha Television cha watu weusi nchini Marekani 'Black Entertainment Television' (BET) Tuzo ambazo zinatambulika sana kimataifa.


Msanii huyu ambae amekuwa nominated kwenye category ya 'Best African Acts' akichuana na wasanii kama Davido (Nigeria), Mafikizolo (Afrika Kusini), Sarkodie (Ghana), na Tiwa Savage (Nigeria). Diamond ambae amekuwa nominated ndio msanii pekee kutoka Africa Mashariki ambae ametangazwa rasmi siku ya Jana katika mtandao wa BET.com.

JK azindua Humuma ya M-PAWA ya benki ya CBA na Vodacom jijini Dar leo

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa VODACOM Tanzania Bwana Rene Meza akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo alizindua Huduma ya M-PAWA leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Huduma ya kampuni ya simu ya VODACOM iitwayo M-PAWA itakayowawezesha watumiaji kutuma na kupokea pesa kwa urahisi zaidi na pia kupata mikopo ya pesa kwa matumizi mbalimbali.Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo.
 Rais Jakaya Kikwete (wa tatu kushoto)akiwa pamoja na kutoka kushoto  Mwenyekiti wa CBA Tanzania Ndewirwa Kitomari, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania Balozi Mwanaidi Maajar, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa Bodi ya CBA Group Desterio Oyatsi na Naibu Mwenyekiti wa CBA Group Muhoho Kenyatta mara baada ya Rais kuzindua huduma mpya ya M-pawa ya kuweka pesa, kutoa na kukopa kupitia simu ya mkononi kwa njia M-pesa kwa ushirikiano na Benki ya CBA jijini Dar es salaam

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza  wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya M PAWA ambayo inamwezesha mteja kupata huduma za kibenki kwenye simu ya mkononi kwa njia ya M-pesa iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa Vodacom Tanzania na Benki ya CBA. Kupitia huduma hiyo mteja wa M-pesa anaweza kuweka, kutoa na kukopa pesa.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Huma ya-M-PAWA ya kampuni ya simu ya VODACOM wakisikiliza kwa makini hotuba ya uzinduzi iliyotolewa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
Wasanii waionesha mabango wakati wa uzinduzi wa huduma ya M-PAWA.(picha na Freddy Maro)

DMV na New York watambiana kuwa kila timu wako gado

$
0
0
Timu kabambe ya DMV

Mazoezi yanaendelea kesho Alhamisi  May 15, 2014 kwa maandalizi ya mechi na New York itakayofanyika Jumamosi May 24, 2014 kwenye Memorial Weekend ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio.
Kikosi cha kwanza  cha  New York Team

Hiki ndicho kikosi  kitakachoanza tarehe 24 jumamosi Memorial weekend.  DC hawachomoki siku hiyo team itaingia DC mapema na kuwa mafichoni hili kupata fursa ya kupata massage maalum kwa kutumia mafuta ya karafuu mambo ya nakish nakish za kipwani hayo. Wachezaji wa New York tumeni majina yenu haraka kwa captain wa team hii kujua vyumba vingapi vya hotel vinaitajika  team ikiwa DC.

FA CUP FINALS

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy Mohamed, bungeni mjini Dodoma Mai 15, 2014.
Mbunge wa Viti Maalum, Mchungaji Dr. Getrude Rwakatare (kulia) akizungumza na Mbunge wa Ileje, Aliko Kibona, bungeni mjini Dodoma Mei 15, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia bungeni mjini Dodoma Mei 15, 2014.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dr.Asha-Rose Migiro akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara yake bungeni mjini Dodoma Mei 15, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, bungeni mjini Dodoma Mei 15, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TANGAZO LA KAZI HOTEL VICTORIA MTWARA (KWA CHEF ISSA)

$
0
0
HOTEL VICTORIA MTWARA INATAFUTA MTAALAMU WA MASOKO MWENYE UZOEFU WA KUTOSHA NA ANAEJIAMINI  KISHA TUMA MAOMBI KWA EMAIL HII issa@hotelvictoria.me AMBATANISHA CV YAKO NA PASSPORT SIZE. MSHAHARA MZURI SANA NA MNONO PAMOJA NA MAZINGIRA HURU YA KAZI. MWAMBIE RAFIKI NA NDUGU WACHANGAMKIE FURSA. CHEERS
 
PIA UKIWA HOTEL VICTORIA MTWARA UNAWEZA KUENJOY HAYA....
 

Butter chicken na garlic naan

 
Paneer masala na butter naan


Tandoor chicken
 

 
Naan bread ya kila ladha mfano chili naan, garlic naan, butter naan, cheese naan na plain naan

SOUTHERN AFRICAN DEVELOPMENT COMMUNITY VACANCY ANNOUNCEMENT

$
0
0

Background
The Southern African Development Community (SADC) currently has fifteen Member States with a population of approximately 250 million people and a combined GDP of USD 467.3 billion (2006). The overall objective of SADC is to achieve development and economic growth, which is to be attained through increased regional integration, built on democratic principles and equitable and sustainable development.

The Southern African Development Community (SADC) is made up of Angola, Botswana, Democratic Republic of the Congo, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Seychelles, South Africa, Swaziland, Tanzania, Zambia, Zimbabwe

It is following this background that SADC Secretariat wishes to invite suitably qualified, experienced citizens of SADC to apply for the following positions tenable at its Headquarters in Gaborone, Botswana:

Position Job Grade
1. Programme Officer –Cereal Production 6
2. Programme Officer-Competition Policy 7

Remuneration

The SADC Secretariat offers a competitive package for all the positions listed below.

Job Grade Average Package Per Annum:
Job Grade 6 US$ 91,717
Job Grade 7 US$ 87,148

Submission of Applications
Applications must be submitted to the:

Permanent Secretary,
Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation
Attn: SADC National Contact Point,
P. O. Box 9000,
DAR ES SALAAM.
Fax: + 255 222 116600 or
+ 255 222 120529
Email:nje@foreign.go.tz

Closing Date: Not later than 16th May 2014:

Your application should accompany the following: REF: SADC/2/3/3/3
a) a short covering letter stating the position that you want to be considered for and describe how your qualifications, experience and competencies are relevant to the position;
b) a detailed and updated curriculum vitae;
c) certified copies of your degree(s), Diploma(s) and Certificate(s); and
d) duly completed SADC Application Form.

Should you be shortlisted, you will be required to produce evidence of any educational and professional qualifications supporting your application, on the day of your interview.

Gender Mainstreaming
SADC is an equal opportunity employer and particularly encourages applications from female candidates.

If you are results oriented, you have a passion for the transformation and development of Southern Africa, and possess the required competencies, please submit your application.

Only applicants, who meet the requirements of the SADC Secretariat and being considered for interview, will be contacted. Should you not hear from the SADC Secretariat within four weeks after the closing date, kindly consider your application as unsuccessful.

For further details on the position that you want to apply for, job profiles and SADC Application Form, refer to the SADC Website:www.sadc.int

Details can also be obtained from the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation.

ISSUED BY THE MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, DAR ES SALAAM.
15TH MAY 2014

WAZIRI MEMBE AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANAYAKAZI WA MAMBO YA NJE

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)-katikati) kwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (wa tatu kutoka kushoto) na viongozi wengine wakiimba wimbo wa "Solidarity" wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Mei, 2014.
Mhe. Membe akitoa hotuba ya ufunguzi wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambapo alitoa rai kwa Wafanyakazi hao kujituma na kuongeza bidii katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Waziri Membe alipofungua kikao cha Baraza hilo.
Katibu Mkuu, Bw. Haule nae akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

oldies & old scul kila ijumaa na jumamosi ndani ya isumba lounge

$
0
0
Je wewe ni mpenzi wa oldies/old scul na unazitambua vizuri? Kama jibu ni YES basi ungana na The legends DJ JD na DJ Fast Eddie kila ijumaa na jumamosi ndani ya isumba lounge kuanzia saa 3 usiku; kiingilio 10000/- tu .Zawadi zitatolewa kwa atakaetambua jina na muimbaji wa song of the night. ungana na DJ JD kupitia facebook.johndilinga.com pls like page


Article 19

$
0
0
Kiongozi wa Wanafunzi 46 wa Skuli mbali mbali za Sekondari kutoka Nchini marekani waliopo Kiwengwa Zanzibar Bwana Criss Backam akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi uwepo wao wa kujitolewa katika ujenzi wa skuli kupitia mradi wa Give Kutoka nchini humo.Kati kati yao ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwashukuru na kuwapongeza Wanafunzi wa skuli mbali mbali za Sekondari Nchini Marekani ambao wapo Zanzibar wakijitolea katika mradi wa ujenzi wa skuli mpya ya Kiwengwa.
Balozi Seif, Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na Waziri wa Elimu Mh. Ali Juma Shamhuna wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa kujitolea kutoka skuli mbali mbali za Sekondari Nchini Marekani hapo Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Baadhi ya msaada wa Kompyuta zilizokabidhiwa Wizara ya Elimu kwa ajili ya Skuli za Zanzibar zikitoka Rotary Klabu ya Kimataifa ya Mji wa Seattle Nchini Marekani.

MPAMBANO WA MASUMBWI: SULEIMAN TALL, DULA MBABE ULINGONI MAY 24

$
0
0
Bondia mzoefu wa ngumi za kulipwa nchini Suleiman said Galile ”tall” (pichani) anategemea kupanda tena ulingoni may 24 katika ukumbi wa Friends Corner Manzese jijini Dar es salaam kuzipiga na Abdalah Pazi “dula mbabe/kiroba” katika pambano lisilo la ubingwa. 
Akithibitisha kuwepo kwa pambano hilo katibu wa ngumi za kulipwa nchini na ndie anayesimamia mapambano yote ya utangulizi bw Ibrahim Abbas kamwe amesema, “Galile na Dula wamekubaliana kusheza siku hiyo ya jumamosi ya terehe 24 na watazipiga katika uzito wa kg76 wakiwasindikiza Karama Nyilawila na Said Mbelwa watakaogombania ubingwa wa UBO.
Amesema hapo awali ilipangwa Karama kuzipiga na Thomas Mashali ambae amepatwa na majeraha kutokana na ajali ya gari. Pia siku hiyo kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi yenye ushindani.
Wakati Adam Ngange akimkabili Alan Kamote wa Tanga, Zumba Kukwe atazipiga na kamanda wa makamanda, Ramadhan Kumbele ataoneshana umwamba na hasan kiwale “Moro best”, Bakari Dunda na Mbena Rajabu, huku madogo wanaokuja juu kwa kasi katika ngumi Idd Athuman atacheza na Julias Thomas Kisarawe, Mwaite juma na Daud Giligili. 
Kamwe alimaliza kwa kusema mpaka sasa hakuna bondia mwenye matatizo wote wapo katika hali ya ushindani wanaisubiria kwa hamu hiyo siku ifikie wabanjuane kiukweliukweli na watu wategemee mashindano mazuri yenye uwezo mkubwa wa kusukuma masumbwi

Tamasha la kitamaduni la "Mtu kwao" laanza leo jijini Arusha

$
0
0
 Chifu wa  kinadi  ambayo ipo katika wilaya ya Itilima  mkoani Simuyu  Wenceslaus Clement  akiwa anabadilishana mawazo na malagwanani wa kimasai katika siku ya kwanza ya tamasha la "Mtu kwao" laanza katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abein jijini Arusha leo
Mkufunzi wa kabila la Wabarabaigi akiwaonyesha malegwanani wa Kimasai mishale ya sumu ambapo alisema kuwa mishale hiyo ina sumu kali ambayo imetengenezwa kutoka dawa za miti aina saba tofauti, na kwamba  ikikupiga tu hauwezi kukimbia hata hatua ishirini kabla hujaanguka na dawa yake haipatikani hospitalini zaidi ya wao wenyewe wanaotengeneza mishale hiyo kukupa dawa
 Maandamano ya washiriki wa tamasha hilo
 Mwanadada wa libeneke la kaskazini Woinde Shizza akiwa amejumuika na waimbaji wa ngoma ya kichaga wakiwa wanacheza pamoja hii yote ni kuuenzi utamaduni wetu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA WATAFITI KUTOKA TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO UYOLE MBEYA KUJADILI KUINUA KILIMO CHA NGANO MKOANI RUKWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na watafiti kutoka taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole iliyopo Mkoani Mbeya walipomtembelea ofisini kwake leo kutambulisha mpango wa SARD (Strategic Agriculture Reseach Development) unaodhaminiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika ADB (Africa Development Bank). Mpango huo una lengo la kupunguza utegemezi wa chakula nchini kwa kuongeza uzalishaji wa vyakula mbalimbali ikiwemo zao la ngano ambalo ni sehemu ya mradi huo Mkoani Rukwa.
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alisisitiza juu upatikanaji wa masoko ya kudumu kwa mazao yatakayozalishwa katika mpango huo badala ya kuwekeza nguvu katika uzalishaji pekee.
Ndugu Anthony Elanga mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole Jijini Mbeya ambae pia ni Mratibu wa Utafiti wa Zao la Ngano Tanzania akizungumza katika kikao hicho. Amesema mpango huo utahusisha wakulima na vikundi vya wakulima ambao watapatiwa elimu na kuwezeshwa mikopo mbalimbali ya kuendeleza kilimo cha ngano Mkoani Rukwa.
Mkutano ukiwa unaendelea.
Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

MISS DAR CITY CENTRE 2014 TALENT SHOW KUTIKISA MAISHA CLUB

$
0
0


 Warembo wanaowania taji la Miss Dar City Center 2014 wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano na waandishi wa Habari hii leo.
Mratibu wa shindano hilo, Judith Michael akizungumza na wanahabari, pamoja nae ni Mkufunzi wa warembo hao. 
 *********
Na Father Kidevu Blog 
WANYANGE 20 wanao wania taji la Miss Dar City Center kesho Mei 16 mwaka huu watawasha moto vikali katika ukumbi wa Maisha Clab wakati wa shindano lao la Vipaji.

Shindano hilo litaongozwa na wasanii, Rich Mavoko, Bonge la Nyau na TID ‘Mnyama’ wanataraji kuwaongoza warembo hao kuwania taji la Vipaji 'Miss Talent Dar City Center 2014."

Akizunguumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo mratibu wa Shindano hilo, Judith Michael Amesema warembo wote 20 wapo katika hali nzuri na wamejifua vya kutosha kwaajili ya shindano hilo la vipaji.

“Tunaamini shindano la mwaka huu litakuwa zuri sana warembo wamejiandaa vya kutosha, tunapenda kwaalika wadau mbalimbali wa masuala ya urembo waje kwa wingi Club Maisha siku hiyo ya Ijumaa ili waweze kushuhudia wenyewe jinsi warembo wa jiji letu walivyojaliwa vijapaji hakika miss Tanzania yupo Dar City Centre,” alisema Judith.

Aidha Judith amesema shindano la Miss Dar City Centre litafanyika Mei 24 mwaka huu katika ukumbi wa Escape One Mikocheni ambapo pia ameahidi shindano hilo kuwa la aina yake.

Judith amewataja warembo wanao wania taji hilo kuwa ni pamoja na Naomy Kisaka,  Nasreen Abdul, Gladys Matson, Habiba Israel, Jenny Zahn,
Doreen Elias, Winniefrida   Msusa, Grace Mella na Rehema Athumani.

Wanyange wengine ni Francisca Simon, Salha Suleiman, Dorica Daud, Agriphina Yelezwa, Sabina Thomas, Jihan Dimachk, Aziza Thabiti, Hatma Rshidi Nyembo na Neema Sisamo.

Huku wadhamini wa Shindano hilo la Miss Dar City Centre ni Prima Total Hair Collection,Gumbo Investment Diamond Bureau Dechange, Father Kidevu Blog, Maisha Club,Q Plus, Zanzi Cream, Clouds Fm, Machapta, Flamour Cosmetics, Valley Spring, Best Point Hotel, Atik Aluminium, Jambo Leo, Blog Ya Wananchi na Skylight Band.
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images