Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

DIAMOND & WCB DANCERS KUWEKA HISTORIA NDANI YA AVYA CENTER MAY 25 - USKOSE


Ibada Maalum ya Miaka Mitano ya Ibada ya Kiswahili na Kusimikwa Mchungaji Ipyana Mwakabonga - Juni 1, 2014 Kuanzia 3:30pm

$
0
0
 Anza Siku njema na NENO la MUNGU kila siku kwa kutembelea Ibada ya Kiswahili website na Ukurasa wa Ibada ya Kiswahili kwenye Facebook.

BISHOP MABOYA KUHUBIRI NENO KATIKA JIJI LA DALLAS,TEXAS USA

$
0
0
Kwa niaba ya uongozi wa Kanisa la Umoja International Outreach lenye makao yake ktk jiji hili la Dallas, ninapenda kumkaribisha kila mtu ktk semina ya neno la Mungu. 
Semina hii ya aina yake itaongozwa na mtumishi Bishop Dunstan Maboya (pichani juu) kutoka Tanzania.
Mungu amekuwa  akimtumia huyu mtumishi kwa ishara na miujiza mingi.Ninapenda kumkaribisha kila mtu ktk semina hii.Leteni wagonjwa mbali mbali kwa ajili ya maombezi.

Siku: Tarehe 16-18 (Friday-Sunday)
Time:Friday ni 6:00pm
          Saturday & Sunday ni 5:00 pm.
Mahali:Umoja Church; 6411LBJ FREEWAY DALLAS TEXAS,75240
Mawasiliano: 214 554 7381,
                       682 552 6402
Karibuni sana.

President Obama Speaks at 9/11 Museum Dedication

$
0
0
President Obama delivers remarks at the dedication of the National September 11 Memorial & Museum at Ground Zero, May 15, 2014.
Courtesy of the White House

WAFANYAKAZI WA BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR WAPATA MAFUNZO YA SIKU TATU JUU UTOAJI HUDUMA BORA.

$
0
0
 Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakimskiliza kwa makini Mkufunzi wa Peter Ssali (hayupo pichani) katika mafunzo yasiku tatu juu ya utoaji huduma bora kwa Bodi hiyo ili kuwa sambamba na Bodi za vyakula za Afrika Mashari.  
 Mkufunzi wa mafunzo ya utoaji uduma bora kwa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Bwa. Peter Ssali kutoka Uganda akifundisha katika mafunzo hayo.
 Waziri wa Afya Zanzibar Juma Duni Haji akitoa tarifa kwa wandishi wa Habari juu ya kupatika kwa wagojwa watatu wa Homa mbaya ya (DENGUE) Visiwani hapa, na kuwataka wananchi kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuangamiza mazalio ya Mbu, kufyeka vichaka vilivyo karibu na makazi namengineyo ili kujinginga na kutafunwa na Mbu huyo.
 Mkuu wa kitengo cha kuzuiana kudhibiti maradhi Zanzibar Dkt. Salma Masauni akitoa ufafanuzi kuhusiana na ugonjwa huo (kulia) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Juma Duni Haji..
Picha ya pamoja ya wakufunzi na washiriki wa mafunzo yasiku tatu juu ya utoaji huduma bora kwa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar.Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar

Miss Uni College Temeke Jumamosi Dar Live, Snura kuliteka jukwaa

$
0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Snura Mushi “Mamaa Majanga” atapamba mashindano ya Miss Uni-College Temeke 2014 yaliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Dar Live Mbagala Jumamosi. 
Mbali ya Snura ambaye atafanya shoo kwa kutumbuiza nyimbo zake zote kwa mara ya kwanza, pia bingwa wa masindano ya Tikisa dance 2012 Hassan Jigoro naye atapamba mashindano hayo yatakayoshirikisha juma ya warembo 12 kutoka vyuo mbali mbali vya elimu ya juu vilivyomo manispaa ya Temeke. 
Warembo hao ni Martha Mashaka, Sarah Joseph, Diana Joachim Kato, Theola Benedict, Eliana Lucumay, Nyangeta Kuboja, Naila Haroun Yusuph, Martha Manzawa, Susan Joseph, Karen Swai, Sarah Jacob na Flora Kimaro. Warembo hao wanatoka vyuo vya Kumbukumbu ya ya Mwalimu Mwalimu Nyerere, Chuo Cha Utalii, TIA na Magogoni. 
Mshindi wa kwanza atazawadiwa Sh 300,000 na vocha ya manunuzi yenye thamani ya Sh250,000 kwenye dula la Robby One fashion,wakati mshindi wa pili atapata Sh250,000 na vocha ya manunuzi ya Sh250,000 na wa tatu Sh 200,000 na wanne na wa tano watapata sh100,000 kila mmoja. 
Pia kutakuwa na zwadi ya kifuta jasho ya Sh50,000 kwa warembo waliobaki na zawadi ya simu tatu za Huwawei kwa warembo watakaoonyesha nidhamu ya hali ya juu, kujiamini na mrembo bora katika muonekano pichani. 
Mashindano hayo yamedhaminiwa na Continental outdoor, Global Publishers, Robby One fashion, Clouds Media group, Leluu Saloon, New Habari Corporation,Mesho decoration, Millard Ayo, salut5, Huwawei , Lamada Hotel, Shamoo Hotel.
Mratibu wa mashindano ya Miss Uni-College Temeke, Silas Michael (katikati) akiwatambulisha baadhi ya warembo ambao Jumamosi watapanda jukwaani kwenye ukumbi wa Dar Live kuwania nafasi ya mshindi wa kwanza. Mashindano hayo yatapambwa na burudani kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Snura Mushi “Mamaa Majanga” .

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA SHULE YA MSINGI YA MSIMBAZI MSETO KWENYE KITUO CHA WATOTO WENYE USONJI (AUTISM).

$
0
0
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha na watoto Abdallah Athuman (kulia) na Nasma Jumanne (kushoto) wenye matatizo ya usonji  (autism) wakati alipotembelea kwenye Shule ya Msingi Msimbazi Mseto
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki katika kuimba na kucheza na watoto wenye matatizo ya usonji (autism),wazazi na walimu wakati alipotembelea  Shule ya Msingi Msimbazi Mseto 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki katika kuimba na kucheza na watoto wenye matatizo ya usonji (autism),wazazi na walimu wakati alipotembelea  Shule ya Msingi Msimbazi Mseto 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na walimu na wazazi (hawapo pichani) wa watoto wenye matatizo ya usonji (autism) wanasoma katika Shule ya Msingi Msimbazi Mseto mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo cha kuwaelimisha watoto hao 

CALL FOR APPLICATIONS FOR TRAINING OF JOURNALISTS IN LAND DEGRADATION AND DESERTIFICATION IN SUB SAHARAN AFRICA


KINANA AMALIZA ZIARA SIKONGE KWA KUHUZUNISHWA NA VILIO VYA DHULMA WANAZOFANYIWA WAKULIMA WA TUMBAKU

$
0
0
Kinana akisoma vijiji vitavyopata umeme wilayani Sikonge mwaka huu wa fedha.
 Katibu Mkuu  wa CCM, Kinana akihutubia katika mkutano huo leo Mei 15, 2014, ambapo akijibu Malalamiko ya Wananchi wa Kata ya Kitunda, alielezea kusikishwa kwake na kitendo cha vyama vya ushirika kudaiwa kuwadhulumu bila huruma wakulima wa tumbaku wa Kata hiyo, huku akionyesha kushangazwa kwake na hatua ya  waziri mwenye dhamana na kilimo, Chakula na Ushirika kutotembelea wakulima kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi. Mapema baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kuuliza maswali au kutoa maoni kuhusu kero  walidaikuwa zaidi y  asilimia 64 ya wakulima hawajapewa malipo yao ya mauzo ya tumbaku ya mwaka jana na vyama vya ushirika katika Kata ya Kitunda, wilayani Sikonge, mkoani Tabora. Pia wakulima hao walisema kuwa wanadaiwa zaidi ya sh. bilioni 112 za mauzo hewa ya  pembembejeo.
 Mkulima wa tumbaku katika Kata ya Kitunda, wilayani Sikonge, akielezea mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana jinsi viongozi wa vyama vya ushirika walivyosaini mkataba hewa wa pembejeo zenye thamani ya s dola za kimarekani 150.
 Mwakilishi wa wakulima wa tumbaku katika Chama cha Ushirika  cha Tumbaku Mkoa wa Tabora ( WETCO), Lameck Mnyama, akielezea  jinsi viongozi wa ushirika huo wanavyowanyonya wakulima wa zao hilo, wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kitunda uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM ambapo alidai hadi sasa wanaudai ushirika dola za kimarekani 76. Picha zaidi BOFYA HAPA

Wanaharakati Waandamana jijini Dar es salaam Kupinga Utekaji wa Wasichana Nigeria

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi (aliyeshika kipaza sauti) akisoma barua maalumu iliyotumwa kwa ubalozi wa Nigeria nchini Tanzania kuonesha wanaharakati hao kupinga utekaji wa wasichana uliofanyika Nigeria. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi (aliyeshika kipaza sauti) akisoma barua maalumu iliyotumwa kwa ubalozi wa Nigeria nchini Tanzania kuonesha wanaharakati hao kupinga utekaji wa wasichana uliofanyika Nigeria.Mkurugenzi wa WiLDAF, Dk. Judith Odunga, akizungumza kupinga ukatili uliofanywa kwa wanafunzi wa kike kutekwa na kitendo cha Jeshi la Polisi nchini Tanzania kuzuia maandamano hayo ya wanaharakati.  
Mkurugenzi wa WiLDAF, Dk. Judith Odunga, akizungumza kupinga ukatili uliofanywa kwa wanafunzi wa kike kutekwa na kitendo cha Jeshi la Polisi nchini Tanzania kuzuia maandamano hayo ya wanaharakati.Viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) wakipokea mabango yenye jumbe anuai za kupinga vitendo vya kikatili vilivyofanywa  na wanamgambo wa Boko Haram. Viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) wakipokea mabango yenye jumbe anuai za kupinga vitendo vya kikatili vilivyofanywa na wanamgambo wa Boko Haram.Baadhi ya wanafunzi wa kike na wanaharakati wakiandamana kupinga vitendo vya kikatili vinavyofanywa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram. Baadhi ya wanafunzi wa kike na wanaharakati wakiandamana kupinga vitendo vya kikatili vinavyofanywa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram. Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

PROIN PROMOTIONS YATANGAZA RASMI KUDHAMINI LIGI YA MPIRA WA MIGUU KWA WANAWAKE LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Katibu wa Michezo kutoka Kampuni ya Proin, Godlisten Anderson akitambulisha viongozi wa kampuni ya Proin Promotions kwa waandishi wa habari wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika leo katika Hoteli ya Southern Sun. Kampuni ya Proin imetangaza kudhamini ligi ya mpira wa miguu kwa Wanawake inayotarajiwa kuanza Mwezi wa Nane.
Rais TFF, Mh Jamal Malinzi na Mwenyekiti wa makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza wakitia saini katika mkataba wa makubaliano ya udhamini wa ligi ya mpira wa miguu kwa wanawake itakayoanza mwezi wa Nane.
Raisi wa TFF, Mh Jamal Malinzi (kushoto) akibadilishana mkataba wa udhamini na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza (katikati) mara baada ya kumaliza kutiliana saini katika mikataba hiyo mbele ya waandishi wa habari leo katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Southern Sun.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Cha Wanawake, Bi Lina Muhando akiongea na Waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Sourthen Sun wakati Kampuni ya Proin ilitangaza kudhamini ligi ya wanawake inayotarajiwa kuanza Mwezi wa Nane
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza akijibu maswali ya waandishi wa habari leo katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hotel ya Southern Sun.
 
Rais wa TFF, Mh Jamal Malinzi akiteta jambo na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Mh Johnson Lukaza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
 Mwandishi wa Habari kutoka gazeti la Jambo leo, Bi Asha Kigundula akiulizwa swali katika mkutano huo.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Na Josephat Lukaza - Dar Es Salaam
Kampuni ya Proin Promotions leo imetangaza rasmi kudhamini ligi ya mpira wa miguu kwa wanawake inayotarajiwa kuchezwa mnamo mwezi wa nane mwaka huu Jijini Dar Es Salaam ambapo itahusisha timu za wanawake washindi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Proin Promotions imeingia mkataba wa miaka miwili kwaajili ya kudhamini ligi hiyo. Proin Promotions inaendelea na lengo lake la kusaka vipaji katika Mpira wa miguu kwa wanawake ambapo sasa Proin imeanza kusaka vipaji katika Tasnia ya Filamu nchini kwa kuanzisha shindano liitwalo Tanzania Movie Talents.
Akiongea na Waandishi wa Habari leo Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza amesema Kuwa Sasa imefika wakati Kuanza kuibua vipaji vya mpira wa miguu kwa wanawake ambapo ndio lengo kubwa la Kampuni yake hiyo ya Proin Promotions. Vilevile aliongezea Kampuni yake tayari imeshaanza mchakato wa kuibua vipaji vya Kuigiza kwa Kuanzisha Shindano lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambapo kuanzia tarehe 17 Mwezi huu kipindi cha kwanza kitaanza kurushwa hewani katika kituo cha Runinga cha ITV kuanzia Mida ya Saa Nne Usiku na sasa ni zamu ya Watoto wa kike kung'ara katika Mpira wa Miguu.
Vilevile Kampuni ya Proin Promotions Imesema inawakaribisha makampuni mengine pia kujitokeza kudhamini ligi hii ya mpira wa miguu kwa wanawake ambapo itasaidia kuibu vipaji na kuifanya timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars kupata wachezaji wenye viwango vya juu ambao wataliletea Taifa la Tanzania sifa na wao pia kuweza kuuzika kimataifa.

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MISRI WASHEREHEKEA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Introducing "Think about it" by Witnesz Feat. Ochu Sheggy

$
0
0
10376459_10203551940270317_716031196_o
Kuwa wa kwanza kusikiliza Single mpya ya Msanii Witnesz aliyemshirikisha Ochu Sheggy "THINK ABOUT IT" hapa chini.

TAARIFA YA MSIBA WA PRIVATE BRIAN SALVA RWEYEMAMU

$
0
0
Private Brian Salvatory Rweyemamu

Bwana Salvatory Rweyemamu wa Kinondoni Dar es Salaam, anasikitika kutangaza kifo cha mtoto wake mpendwa Private Brian Salvatory Rweyemamu aliyefariki alfajiri ya kuamkia  tarehe 15 Mei,2014 katika hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alipokuwa akitibiwa.

Mipango ya mazishi ambayo yanatarajiwa kufanyika Jumamosi inafanyika. Msiba uko  nyumbani kwa Bwana Salvatory Rweyemamu Kinondoni jirani na Vijana Social Hall ama Mango Garden, jijini Dar es salaam. Ratiba ya mazishi itatolewa punde.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki walioko Dar es Salaam, Kagera, Malawi, Afrika Kusini, Uingereza na Canada.

Sisi tulimpenda, lakini Bwana kampenda zaidi.
Jina la Bwana na lihimidiwe.
Amin

AUTHORIZED RESELLER AND DISTRIBUTOR OF THE QUICKBOOKS ACCOUNTING AND PAYROLL SOFTWARE RANGE OF PRODUCTS NETWORK AFRICA NOW IN DAR ES SALAAM, TANZANIA. CYBER CONSULT (T) LTD.


ONESHO LA KITALII LA S!TE LATAMBULISHWA RASMI INDABA

$
0
0
Na Geofrey Tengeneza Onesho la Kimataifa la Utalii la Tanzania lijulikanalo kama Swahili International Tourism Expo (S!TE) linaroratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB na litakalokuwa likifanyika kila mwaka mwezi Oktoba katika eneo la Mlimani City jijini Dar es salaam limetambulishwa rasmi kwa wadau mbalimbali waliohudhuria maonesho ya Kimatatifa ya Utalii ya INDABA huko Durban Afrika Kusini. 
Akizungumza wakati wa kutambulisha onesho hilo, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mh. Radhia Msuya amewaambia washiriki wa INDABA kuwa onesho hilo litakuwa likifanyika kila mwaka na kwa kuanzia mwaka huu litafanyika tarehe 1 -4 Oktoba. 
Amesema kuwa S!TE linatarajiwa kuwa onesho la pilii kwa ukubwa barani Afrika baada ya lile la INDABA na amewakaribisha wadau na makampuni yote yaliyoshiriki maonesho ya INDABA kushiriki pia onesho hilo la S!TE. 
 Maonesho ya INDABA hufanyika Durban Afrika Kusini kila mwaka mwezi Mei ambapo mwaka huu yalifanyika kuanzia tarehe 10-12 Mei na waoneshaji kutoka Tanzania  uliongozwa na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB Profesa Isaya Jairo. Jumla ya makampuni 41 kutoka Tanzania yalishiriki katika maonesho hayo.
 Baadhi ya washiriki wa taasisi za Serikali katika Banda la Tanzania wakati wa maonesho ya INDABA Afrka Kusini.

Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji na Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bibi Devota Mdachi akitoa maelezo kuhusu vivutio vya utalii vya Tanzania kwa mmoja wa watu waliotembelea banda la Tanzania katika maonesho ya INDABA huko Durban Afrika Kusini.

EXIM BANK’S FIRST QUARTER PRETAX PROFIT UP BY 42%

$
0
0
Exim Bank Tanzania Chief Finance Officer, Mr. Selemani Ponda (Centre) briefs journalists at a news conference to announce the bank’s financial results for the first quarter of 2014 in Dar es Salaam Looking on is Head of Treasury, Mr. George Shumbusho (first left) and Seniour Finance Manager, Mr Issa Hamisi (first right). The EXIM Bank Group 1st quarter (Q1) 2014 pretax profit rose by 42% to TZS 6.4 billion from the same period last year as per recently published results.

“We are pleased to report good results to start the year,” said Selemani Ponda, Exim Bank Chief Finance Officer. “Strong top-line revenue growth reflects the success of the Bank’s highly diversified income streams. We continue to improve upon operational efficiency to optimize our customers’ satisfaction. “Our Bank is continuing to move in the right direction. We are making progress towards fulfilling our ambitions. Our Q1 results show that we have had an encouraging start to the year,” he added. 

MADIWANI WA CUF WILAYANI URAMBO WASHIRIKI MAPOKEZI YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE

$
0
0
 Madiwani wa Chama cha CUF,wilayani Urambo wakimpokea kwa bashasha kubwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwasili katika wilaya ya Urambo,mapema leo akitokea wilayani Sikonge.Shoto ni Diwani wa CUF,Mh.Kandola Nyanda wa kata ya Nsenda na kati ni Diwani wa CUF,Kata ya Usoke,Mh.Kadada Mohamed,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya elimu,afya na maji katika halmashauri ya Urambo mkoani Tabora.Pichani nyuma ya Kinana ni Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye akifurahia jambo.
Diwani wa CUF,Mh.Kandola Nyanda wa kata ya Nsenda akimpokea kwa bashasha kubwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwasili katika wilaya ya Urambo,mapema leo akitokea wilayani Sikonge.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh Fatma Mwasa akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Urambo,Mh.Samwel Sitta mara baada ya kuwasili kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana Wilayani Urambo mapema leo.
 Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta akimkaribisha katika jimbo lake Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake mapema leo.
 Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta,Pichani kati ni Mkuu wa Mkoa,Mh.Fatma Mwasa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.
  Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Kinana pamoja na Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta wakishiriki ujenzi wa jengo la maabara katika shule ya sekondari Uyumbu,katika kata ya Uyumbu wilayani Urambo mkoani Tabora.

Picha na Michuzijr-Urambo Tabora

Maonesho ya Biashara ya Bidhaa za Uturuki na Tanzania Yafunguliwa Diamond Jubilee Dar

$
0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dk. Reginald Mengi (wa tatu kulia) akikata utepe kuzinduwa maonesho ya biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania leo jijini Dar es Salaam yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia leo tarehe 15 hadi tarehe 17, 2014. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dk. Reginald Mengi (wa tatu kulia) akikata utepe kuzinduwa maonesho ya biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania leo jijini Dar es Salaam yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia leo tarehe 15 hadi tarehe 17, 2014.Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dk. Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, akizungumza na wafanyabiashara wanaoshiriki maonesho ya biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania kabla ya kuyafungua rasmi maonesho hayo leo jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yameanza leo tarehe 15 hadi tarehe 17, 2014. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dk. Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, akizungumza na wafanyabiashara wanaoshiriki maonesho ya biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania kabla ya kuyafungua rasmi maonesho hayo leo jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yameanza leo tarehe 15 hadi tarehe 17, 2014.Bidhaa ya wananchi wakiangalia bidhaa mbalimbali kutoka zinazooneshwa katika Maonesho ya Biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania yanayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Bidhaa ya wananchi wakiangalia bidhaa mbalimbali kutoka zinazooneshwa katika Maonesho ya Biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania yanayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania zikioneshwa katika Maonesho ya Biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania. Bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania zikioneshwa katika Maonesho ya Biashara ya bidhaa kutoka nchi za Uturuki na Tanzania.

Airtel yadhamini Mafunzo ya waandishi wa habari

$
0
0

Mwenzeshaji wa Mafunzo ya waandishi wa habari bwana Ndimata Tegambwage akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imedhamini mafunzo ya wapigapicha yatakayofanyika kuanzia kesho katika kituo cha Msimbazi jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na MP5 2011 Entertainment. Pichani katikati ni Afisa mawasiliano na Matukio bi Dangio Kaniki akifatiwa na mratibu wa semina Mpochi Selemani.
 KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imesema itaendelea kuwajengea uwezo wapiga picha za habari kwa kuendela kuwapatia mafunzo ili wapate ujuzi zaidi kwa kuwa wao ni balozi katika kuipasha jamii habari.

Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam jana na Afisa Uhusiano na Matukio wa Kampuni ya Airtel Dangio Kaniki alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa wapiga picha wa habari kuwajengea uwezo kufanya kazi katika mazingira hatarishi.

"Tutaendela kuwapatia mafunzo wapiga picha ili wapate ujuzi zaidi katika utendaji wao wa kazi kwa kuwa mabalozi wetu,na tutawatafutia vifaa vya kisasa kwa ajili ya kufanyia kazi katika mazingira hatarishi"alisema Dangio

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Baraza la Habari (MCT),na kudhaminiwa na kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya MP5 2011 yanashirikisha wapiga picha kutoka magazeti na TV.

Akizungumza katika mafunzo hayo mshiriki Suleiman Mpochi ambae pia ni mratibu wa mafunzo hayo alisema watanufaika nayo kwa kuwa watajifunza mbinu mpya za kufanya kazi katika mazingira hatarishi pamoja na kufuata maadili ya taaluma ya waandishi wa habari.

Kampuni hiyo ni mara ya tatu inadhamini mafunzo hayo kwa wapiga picha za habari ambamo Mwezeshaji katika mafunzo hayo Mkongwe wa Habari katika fani ya habari Ndimara Tegambwage aliiomba kampuni kuendela kudhamini mafunzo hayo na kuwapatia zana za kisasa za kazi wapiga picha.
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live


Latest Images