Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 328 | 329 | (Page 330) | 331 | 332 | .... | 3348 | newer

  0 0


  Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawatangazia Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa wafike Jijini Dar es Salaam Jumapili tarehe 26 Januari 2014 kwa ajili ya shughuli za Kamati za Bunge zitakazoanza tarehe 27 Januari 2014 hadi tarehe 8 Februari 2014. Moja ya shughuli hizo ni pamoja na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.


  Imetolewa na

  Ofisi ya Bunge,

  Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na

  Uhusiano wa Kimataifa

  Dar es Salaam


  17 Januari 2014.


  0 0

  JE UNGEPENDA KUFAHAMU MAJINA YA WATU/KAMPUNI ZILIZOPATA MGAO WA UVUNAJI KATIKA MASHAMBA YA MITI YA SERIKALI 2014?

   KAMA NDIVYO BASI USISITE KUTEMBELEA UKURASA WA FACEBOOK WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII:
  Ministry of Natural Resources and Tourism - Tanzania
  UKITEMBELEA USISAHAU 'KU-LIKE' PAGE HII:

  0 0

  Bendi za Muziki wa Dansi za African Stars "Twanga Pepeta" na Msondo Ngoma Music, Jumapili tarehe 19 Januari zimepanga kufanya onyesho moja kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014.

  Onyesho hilo limepangwa kufanyika katika ukumbi wa C.C.M kata ya 14 wilayani Temeke na maandalizi yote yamekwishamalizika.

  Bendi hizo ambazo zipo kwenye mahusiano mazuri ya muda mrefu, zimeamua kufanya onyesho hilo ili kuwapa burudani mashabiki wao kwa kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014.
  Kwa Upande wa Twanga Pepeta ambao kwa sasa wanatamba na albamu yao ya "Nyumbani ni Nyumbani" watatumia onyesho hilo ili kuwaonjesha mashabiki ladha mpya za 2014 wakiwa na wakali wao wote wakiongozwa na Kiongozi wao Luizer Mbutu.
  Kwa Upande wa Msondo wao wanataraji kumualika aliyekuwa Kiongozi wao Mkuu Mzee Ngurumo ili aje kutoa sapoti ya kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014.
  Onyesho litaanza mapema saa 12 kwa Msondo kuanza kutoa burudani Kabla ya kuwaachia vijana wao kuendeleza kutoa burudani.

  0 0

  Tunasikitika kutangaza kifo cha Ndg. Deus Mtambalike kilichotokea tarehe 15/01/2014 katika hospitali ya Milpark nchini Afrika ya Kusini.
  Katika uhai wake marehemu aliwahi kuwa Mkuu was wilaya katika sehemu mbali mbali nchini zikiwamo Ngara, Igunga, Tunduru, Ludewa na Muleba. 

  Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya jumapili 19/01/2014 Nyumbani kwa marehemu  Kimara Bonyokwa jijini Dar es salaam  majira ya saa sita mchana Bwana alitoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe 
  Amina.

  0 0
 • 01/17/14--22:37: SHUKURANI ZA DHATI
 • Shukurani kwa Watanzania waishio DMV na State nyingine hapa Marekani kwa kufanikisha kumsafirisha kwa mazishi ya mpendwa wetu Zaynab Haroun Buzohera ( Zay B, Zay Dulllah).
  Mimi  Ngalu Mariam Buzohera, Yusuf Buzohera wadogo wa marehemu, mumewe Dullah, kamati ya mazishi Rais wa jumuiya ya watanzania DMV,IddI Sandaly, Said Mwamende ,Jabir Jongo ,Hidaya Mahita, Catherine Mukami, Irene Milembe na Latifa Mzese. tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru watanzania wote mnaoishi hapa DMV,  Texas, New York, New Jersey, Massachusetts, Ohio, California,North Calorina, Illinois na state nyingine zote kwa kujitoa kwa hali na mali kusaidiana nasi kufanikisha shughuli nzima ya matayarisho na hatimaye kuwezesha kumsafirisha mpendwa wetu kwenda kupumzishwa nyumbani Tanzania na mliweza kuwa nasi kuanzia hospitalini, msibani na kutufariji nyumbani kwa marehemu na hadi sasa.
  Tunapenda  kuwashukuru sana watu wa media zikiwemo blogu ambazo zilitusaidia kutangaza habari za msiba, zikiwemo vijimambo, Swahili villa, Swahili blog, Michuzi, Sunday Shomary, Je huu ni uungwana Blog, Changamoto yetu, Jestina George Blog, Lukaza Blog, Sufiani Mafoto Blog,Mtaa kwa mtaa Blog na nyinginezo na watu mbalimbali waliosambaza habari hizi za msiba kwa njia ya text za aina zote, simu, facebook, instagram na vihabarishi mbalimbali bila kumsahau Dada yetu wa DMV Tuma Katule kwa jinsi alivyoendesha harambee.
  Tunapenda kutoa shukurani za pekee wa Watanzania wenzatu waliowahiishi DMV na wanaoendelea kuishi ambao walituwakilisha wenzao wa Marekani kwa kujumika na familia ya mpendwa wetu nyumbani Tanzania tangia siku ya kwanza ulipotokea msiba huu mpaka siku ya mazishi.
  Shukurani zetu za dhati kwa aliyekuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Maajar na mumewe Shariff Maajar wakiwemo aliyekuwa Mwambata wa Jeshi kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Emmanuel Maganga na mkewe Love Maganga kwa ushiriki wao wa kuwafariji wafiwa nyumbani Tanzania tangia siku waliposikia msiba huu.
  Shukurani za pekee kwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula kwa kujumuika na wafiwa nyumbani kwao Ukonga Banana pia tunapenda kuwashukuru maafisa wa ubalozi wa Tanzania hapa Marekani kwa ushirikiano wao wa hali na mali waliouonyesha.
  Tunapenda kutoa shukurani kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara na Mbunge wa Iramba Mhe. Mwigulu Nchemba kwa kutafuta muda wake na kuweza kufika nyumbani kwa wafiwa Ukonga na kujumuika nao.
  Kama kuna yeyote tutakuwa tumemsahau kwa njia moja au nyingine tunaomba utuelewe sio kusudio letu kufanya hivyo tunathamini mchango wako wa hali na mali uliosaidia na hatimaye kuwezesha na kufanikisha mazishi ya mapendwa wetu.
  Hatuna tutakacho walipa kitakacholingana na yote mliotufanyia zaidi ya kumuomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awalipe.
  Tunamuomba Mwenyezi Mungu ampumzishe mpendwa wetu Zainab Buzohera mahali pema peponi na sisi wote tuzidi kuombeana Kheri.
  Innah Lillah wa Inaillah Rajiun 
  ( Sisi ni wa Mola na kwake tutarejea).

  0 0

  Waumini wa Dini ya Kiislamu popote walipo katika kipindi hichi cha kusherehekea uzawa wa Kiongozi wa Dini hiyo Ulimwenguni Mtume Muhammad { SAW } wana wajibu wa kupitisha maazimio ndani ya nafsi zao ya kuachana na maovu na kukumbatia mema yote kama alivyokuwa akiyahubiri Kiongozi huyo wakati wa uhalifa wake. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo katika kisomo cha mazazi ya Mtume Muhammad { SAW } kilichofanyika katika ukumbi wa wapenzi wa Mtume Muhammad { SAW } wa Chaurembo waliopo katika Mtaa wa Msimbazi Kariakoo Mjini Dar es salaam. 
  Balozi Seif alisema mkusanyiko wa waumini wa Kiislamu katika kutukuza uzawa wa Kiongozi wao utakuwa na manufaa makubwa endapo kila muumini atadhamiria kusoma kwa kina maisha ya kiongozi huyo kwa lengo la kufuata mwenendo wake. 
  Alitoa wito kwa wapenzi wa Mtume Muhammad { SAW } kufanya utafiti mbali mbali zitakazotoa fursa kwa waumini wa dini ya Kiislamu popote pale kusoma na hatimae kuelewa vyema maisha na mfumo aliokuja nao Kiongozi huyo wa umma wa Kiislamu. 
  “ Ikiwezekana tafiti hizo ni vyema zikaandikwa kwa lugha ya Kiswahili ili watu wengi zaidi wapate kuzisoma. Kuelewa maisha ya Mtume Muhammad { SAW } ni hatua muhimu kwa muumini wa Kiislamu kuielewa Dini yake “. Alisisitiza Balozi Seif. 
  Akinukuu baadhi ya maandiko yaliyotolewa na wanafalsafa wa Dini ya Kiislamu Balozi Seif alisema kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad { SAW } ni sawa na kusherehekea kuzaliwa kwa Uislamu “. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwasisitiza waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuwa na utiifu, subra wakati wa matatizo sambamba na kujijengea maisha bora ya milele ambayo kila muumini anayaelewa. Balozi Seif alielezea faraja yake kutokana na uwepo wa Umoja wa wapenzi wa Mtume Muhammad { SAW } hapa Tanzania ambao unastahiki kupongezwa pamoja na kuungwa mkono . Alisema jamii katika kipindi kirefu ilikuwa ikishuhudia kuwepo kwa umoja wa wapenzi wa vilabu vya mchezo wa mpira wa miguu au wanamuziki badala ya kuwa na umoja kama huo unaoleta faida pande zote mbili Duniani na Makazi ya milele. 
  “ Maandalizi ya sherehe hiziyameonyesha wazi kwamba nyinyi kweli ni wapenzi wa Mtume Muihammad { SAW }. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuzidishie mapenzi yetu kwa kiongozi wetu huyo “, alifafanua Balozi Seif. 
  Akitoa salamu kwenye hafla hiyo ya kisomo cha mazazi ya Mtume Muhammad { SAW } Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi alisema waumini wa Dini ya Kiislamu wana wajibu wa Kumshukuru Mola kwa kuupatia umma huu wa mwisho Kiongozi aliyekamilika kwa tabia, nasabu pamoja na Umbo. 
  Mzee Mwinyi aliwataka waislamu hao kuendelea kuheshimu nema walizopewa na Mwenyezi Mungu za kupatia Kitabu kitukufu na bora chenye mfumo kamili wa kufuatwa na wanaadamu katika maisha yao ya kila siku. Mapema Mkurugenzi wa Kituo cha Kiislamu kilichopo Tandika Mjini Dar es salaam akiwa miongoni mwa matunda ya chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu cha Al – Akhzal nchini Misri Sheikh Usama Ismail alisema dalili za utukufu wa Mtume Muhammad { SAW } zilianza kujichomoza tokea zama za Mitume waliomtangulia. 
  Sheikh Usama alifahamisha kwamba Kiongozi huyo wa Umma wa Kiislamu alibashiriwa utukufu wa kuja kwake duniani ambao baadhi ya maulamaa wa enzi zilizopita waliushuhudia ndani ya vitabu vitukufu. Katika hafla hiyo ya kisomo cha mazazi ya Mtume Muhammad { SAW } Muasisi wa Umoja wa wapenzi wa Mtume Muhammad { SAW } wa Chaurembo waliopo katika Mtaa wa Msimbazi Kariakoo Sheikh Majid aliwapongeza Viongozi hao kwa ukaribu wao na waumini pamoja na wananchi kwenye masuala mbali mbali ya kijamii. 
  Katika kuunga mkono harakati za kijamii zinazofanywa na viongozi hao Sheikh Majid kwa niaba ya Umoja huo alikabidhi zawadi za Juzuu, Mashafu pamoja na hati maalum kama ukumbusho kwa wageni hao waalikwa akiwemo pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al Hajj Daktari Ali Mohamed Shein.
   Wanamadrasat Nurul Huda wa Tandika Jijini Dar es salaam wakifanya vitu vyao wakati wa hafla ya kisomo cha Maulid ya Mtume Muhammad (SAW) kilichofanyika katika ukumbi wa wapenzi wa Mtume Muhammad { SAW } wa Chaurembo wa Mtaa wa Msimbazi Kariakoo Jijini Dar es salaam.
    Mwana Umoja wa wapenzi wa Mtume Muhammad { SAW } wa Chaurembo wa Mtaa wa Msimbazi Rais Mstaafu wa Tanzania Al- Hajj Mzee Ali Hassan Mwinyi akitoa salamu zake wakati wa kisomo cha mazazi ya Mtume Muhammad (SAW) hapo Mtaa wa Msimbazi Mjini Dar es salaam.Kulia ya Mzee Mwinyi ni Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kushoto ya Mzee Mwinyi ni Mkurugenzi wa Kituo cha Kiislamu Tandika Dar ves salaam Sheikh Usama Ismail.
  Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Mwinyi akimkabidhi Zawadi za Juzuu, Mashafu , vyeti pamoja na tuzo Maalum Mgeni Rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye hafla ya mazazi ya Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika Mtaa wa Msimazi Kariakoo Jijini Dar es salaam. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0
 • 01/18/14--00:31: KIWANJA KINAUZWA BAGAMOYO


 • Kiwanja kinauzwa, kiko Bagamoyo Ukuni jirani na standi kuu ya mabasi yaendayo mikoani, kina square meter 2,400, kinafaa kwa ujenzi wa shule, hoteli na aina nyingine ya uwekezaji. Kina hati, bei ni maelewano.
  Kwa maelezo zaidi piga simu: +255 657 803139  0 0
 • 01/18/14--00:48: Nissan hard body inauzwa
 •                                                            Engine Capacity CC 2400
  Model ya mwaka 2009
  Imetembea KM 64902
    Bei Milioni 26 Tshs.
  Gari ipo kwenye hali nzuri kabisa haina matatizooo,Gari ipo Dar
  Serious buyers piga namba zifuatazo 0713 966552 na 0717 585602


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua kazi ya uwekaji viti vipya katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Januari 18,2014 ikiwa ni maandalizi ya Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa ameketi kitini wakati akikagua marekebisho yanayofanyika katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Januari 18, 2013 ikiwa ni maandalizi ya Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA UKARABATI JENGO LA BUNGE
  *Ni maandalizi ya Bunge la Katiba
   WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema ameridhishwa na kazi ya ukarabati inayoendelea kwenye maeneo mbalimbali ya jengo la Bunge ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya Bunge la Katiba. 
  “Maendeleo ni mazuri na kazi inayofanywa ni nzuri, kikubwa ni kuhakikisha mnaikamilisha hii kazi katika muda uliopangwa,” alisisitiza. 
  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumamosi, Januari 18, 2014), wakati akipokea maelezo ya ukarabati kutoka kwa Mhandisi Mkuu wa Ofisi Bunge, Eng. Dk. Philemon Mzee ambaye alikuwa akimtembeza kwenye maeneo mbalimbali yanayofanyiwa ukarabati. Kwa mujibu wa Dk. Mzee, kazi hiyo inatarajiwa kukamilika Januari 30, mwaka huu. 
  Ndani ya ukumbi wa Bunge, Waziri Mkuu alikuta viti vyote vya zamani vimekwishaondolewa na akaonyeshwa sehemu moja ya mfano iliyopangwa viti vinane kuashiria muonekano utakavyokuwa mara baada ya kazi hiyo kukamilika. 
  Dk. Mzee alimweleza Waziri Mkuu kwamba wanatarajia kuweka viti 670 vya wajumbe wa kawaida pamoja na viti 24 kwa ajili ya wajumbe wenye mahitaji maalum. “Kule nyuma tutaweka viti vya kuzunguka ili hata kama mjumbe mmoja ana ulemavu wa miguu na amekuja na baiskeli yake aweze kutoka na kukaa kwenye kiti chake kwa urahisi,” alisema. 
  Alimweleza Waziri Mkuu kwamba viti vya Spika na Makatibu wa Bunge vipo tayari, mfumo wa vipaza sauti uko sawa na kwamba kila kipaza sauti kimoja kitakuwa kinatumiwa na watu wawili kulingana na mpangilio wa ukaaji ulivyo. 
  Alipoulizwa na Waziri Mkuu kuhusu sehemu ya kukaa waandishi wa habari, Eng. Mzee alisema sehemu zao zitaendelea kubaki zilivyo. Alipohoji endapo kutakuwa na kazi za Kamati, zitafanyikia wapi, Waziri Mkuu alijibiwa kwamba kuna kumbi tisa za kutosha watu 25-30 zinaandaliwa katika jengo la utawala Annex. 
  Waziri Mkuu pia alikagua sehemu ya mgawaha kwa ajili ya wajumbe wa bunge hilo na kuonyeshwa sehemu ya basement ambayo alikuta inafanyiwa matengenezo ili iweze kuchukua watu 500 kwa wakati mmoja. Pia alikagua mgahawa wa zamani wa bungeni na kuelezwa kwamba utatumiwa na watumishi tu na hivi sasa unafanyiwa ukarabati ili uweze kutosha watu 120 kwa wakati mmoja. 
  Waziri Mkuu alikagua pia chumba cha Hansard ambako alielezwa kuwa kimeongezwa ili kiweze kutosha watumishi 80 ikilinganishwa na watumishi 25 waliokuwepo zamani. Pia alikagua server room ambayo imehamishiwa eneo yalipokuwa matawi ya benki na zahanati. 
  Alipouliza kuhusu eneo la kuegeshea magari, Waziri Mkuu alielezwa kwamba limetengwa eneo la kutosha magari 400 ambalo hivi sasa linafanyiwa maandalizi. 
  Katika jengo la Utawala Annex, Waziri Mkuu alielezwa jengo hilo litakuwa na ofisi, vyumba vya mazoezi (gym), zahanati na ofisi za kutolea huduma za kibenki. 
  Akitoa maelezo kuhusu kazi ya ukarabati inayoendelea, Kamishna Msaidizi wa Magereza ambaye ni msimamizi wa ujenzi wa jengo la Utawala Annex, Eng. Salum Omari alisema walianza kazi hiyo Januari 2, mwaka huu na wanatarajia kuikamilisha ifikapo Februari 2, mwaka huu.
   Alipoulizwa kama watamudu kuikamilisha kazi hiyo katika tarehe iliyopangwa, Eng. Omari alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba wataikamilisha katika muda huo.
   Waziri Mkuu amerejea jijini Dar es Salaam mchana huu.
    
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  DODOMA.
  JUMAMOSI, JANUARI 18, 2014


  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwahutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar waliomaliza masomo yao ya shahada ya kwanza kwenye mahafali ya 13 ya chuo hicho.Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Ali Juma Sahamuhuna na kulia yake ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Dr. Abdulrahman El- Muhailan.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akikabidhi zawadi kwa baadhi ya wanafunzi bora wa masomo mbali mbali waliofanya vizuri kwenye masomo yao ya shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani. Kulia yake wanaofurahia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Dr. Abdulrahman El – Muhailan na Mkuu wa Chuo Kikuu chukwani Profesa Hamed Rashid Hikman.
  Baadhi ya wanafunzi wa chuo Kikuu Shirikishi cha Elimu chukwani wakiwa katika madaha kwenye mahfali yao ya 13 ya kumalizia masomo yao ya shahada ya kwanza.
  Wanafunzi wa Chuo Kikuu shirikishi cha elimu chukwani wa fani ya Geagraph wakiwa katika vitendo vya kuashiria kukamilisha masomo yao ya shahada ya kwanza chuoni hapo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0


  0 0

  Kiongozi wa msafara wa Kifimbo cha Malkia kwa Ukanda wa Afrika Mashariki Kipchoge Keino (kulia) akimkabidhi Kifimbo cha Malkia kwa Mkuu wa msafara kwa Tanzania Gullam Rashid mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Dar es Salaam leo mchana.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo ambaye pia aliwakilisha Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo katika mapokezi ya Kifimbo cha Malkia Bi. Juliana Yassoda (katikati) akipokea Kifimbo hicho kutoka kwa Mke wa Rais wa Kamati ya Olympic Tanzania Bi. Anna Bayi leo jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Dianna Patricia Melrose akiwa na Rais wa Kamati ya Olympic Tanzania (TOC) Filbert Bayi (mwenye miwani) wakiwa na watoto waliofika uwanja wa ndege kupokea Kifimbo cha Malkia leo jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Kamati ya Olympic Tanzania (TOC) Filbert Bayi akiwa katika picha na vikundi vya ngoma vilivyotumbuiza wakati wa mapokezi ya Kifimbo cha Malkia leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Frank Shija - Wizara ya Habari.

  0 0


  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


  Telephone: 255-22-2114512, 2116898
                press@ikulu.go.tz             

  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,
        THE STATE HOUSE,
                P.O. BOX 9120,  
  DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   
  TAARIFA KWA UMMA
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumamosi, Januari 18, 2014,  amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wapya wa mikoa mitano na kuhamisha makatibu tawala wengine na Wakurugenzi wa Majiji nchini.

  Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue iliyotolewa jioni ya leo, Ikulu, Dar Es Salaam inasema kuwa uteuzi na uhamisho huo unaanza leo hii.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo,  Makatibu Tawala wapya ni Ndugu Wamoja A. Dickolangwa ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa ambako alikuwa Kaimu Katibu Tawala; Ndugu Abdallah D. Chikota ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi. Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Newala na Ndugu Symthies E. Pangisa ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Pangisa alikuwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara.

  Wengine ni Ndugu Alfred C. Luanda ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara. Kabla ya uteuzi wake,  alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na Ndugu Jackson L. Saitabau ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Kabla ya hapo, alikuwa Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Arusha.

  Taarifa hiyo iliwataja waliohamishwa kuwa ni Ndugu Beatha Swai aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani na sasa anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI; Ndugu Sipora J. Liana ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI; Ndugu Benedict Ole Kuyan ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga anahamishiwa Mkoa wa Mara na Ndugu Salum M.Chima ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa anahamishiwa Mkoa wa Tanga.

  Wengine waliohamishwa ni Ndugu Mgeni Baruani ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe anahamishiwa Mkoa wa Pwani; Ndugu Juma R. Iddi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya anahamishiwa Jiji la Arusha kama Mkurugenzi; Eng. Omari Chambo ambaye alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi anahamishiwa Mkoa wa Manyara kama Katibu Tawala wa Mkoa huo na Dkt. John Ndunguru aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi anahamishiwa Mkoa wa Kigoma kama Katibu Tawala wa Mkoa huo.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  18 Januari, 2014

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mheshimiwa Damian Zefrin Lubuva kufuatia kifo cha Mke wake, Mama Martha Peter Lubuva kilichotokea tarehe 17 Januari, 2014 katika Hospitali ya Apollo iliyoko New Delhi nchini India alikopelekwa kwa matibabu akisumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.

  “Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha Mke wako, Mama Martha Peter Lubuva aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Apollo nchini India akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Kisukari ambao umesumbua kwa muda mrefu”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake za Rambirambi.

  Rais Kikwete amesema anatambua fika machungu ambayo hivi sasa wanapitia watoto na Familia nzima ya Mheshimiwa Damian Zefrin Lubuva kutokana na kuondokewa na Mama yao Mzazi na Kiongozi muhimu wa Familia, lakini amewaomba wawe watulivu na wavumilivu, lakini muhimu zaidi wawe na moyo wa ujasiri katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya mpendwa wao.

  “Ninawahakikishia kuwa niko pamoja nayi katika kuomboleza msiba huu mkubwa na namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu, Mama Martha Peter Lubuva kwa kutambua kuwa yote ni Mapenzi yake Mola”.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  DAR ES SALAAM.
  18 Januari, 2014

  0 0

  Naitwa Cyril August Chami (PhD) Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini na Mjumbe wa NEC-CCM kupitia Wilaya ya Moshi Vijijini.

  Nimesikitishwa na kufadhaishwa sana na mtu au watu waliotengeneza akaunti kwa jina langu kwenye  Mtandao wa Kijamii wa Facebook na kujifanya yeye au wao ndio mimi.

  Wamepachika hata picha zangu zinazopatikana kirahisi kwa sababu ya majukumu ambayo nimeshawahi kuwa nayo kama Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, na Waziri wa Viwanda na Biashara.

  Hilo lenyewe, yaani kutengeneza akaunti kwenye Facebook kwa jina la mtu na kuweka picha zake bila ridhaa yake, ni kosa la jinai.

  Lakini ubaya zaidi ni kwamba mtu huyo au watu hao wanawasiliana na wapiga kura wangu kule Moshi Vijijini na walio nje ya jimbo na kuwauliza kero zinazowakabili. Wanawajibu hao wananchi kana kwamba wao ndio mimi. Kwa vile wao sio mimi, majibu yao siyo sahihi. Lakini kwao hilo halina tatizo maana nia yao ni kunichafua.

  Wanaenda mbali zaidi na kukitukana Chama changu cha Mapinduzi wakionyesha kuwa mimi ni shabiki na/au sympathiser wa CHADEMA.  Wanatukana wanachama wenzangu wa CCM na kwa maana hiyo, viongozi wangu wa CCM.

  Naamini wanajua kuwa nia yao hii ni ovu lakini nawaomba watambue kuwa hawatafanikiwa katika malengo yao kwa sababu mtetezi wangu ni mkubwa kuliko nia hiyo yao.

  Siyo siri kuwa asilimia kubwa ya mawasiliano kwenye mitandao yanafanyika kwa anwani feki, hivyo wajue kuwa hata wasomaji wangenishangaa sana kama ningejiundia akaunti ya Facebook,  niweke picha zangu, halafu NIANZE KUWATUKANA VIONGOZI, WANACHAMA NA CHAMA CHANGU CHA MAPINDUZI.

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Bagamoyo alipowasili kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za udiwani kata ya Magomeni.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa shina la wakereketwa la stendi ya Kangowe mara baada ya kulifungua shina hilo.


  0 0

  Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Msanga, Wilaya ya Kisarawe.
  Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Msanga, Wilaya ya Kisarawe.


  0 0
 • 01/18/14--13:24: Article 1
 • SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD 
  WAZEE WA KAZI

  NEW YEAR OFFERS!
  SAVE OVER £600 ON CONTAINERS!
  20' CONTAINER TO DAR /MOMBASA NOW £1,250 
  40' CONTAINER TO DAR MOMBASA NOW £1,750 

  SALOON CARS TO DAR/MOMBASA NOW £700
  4 X 4 CARS TO DAR MOMBASA NOW £780
  AIR CARGO TO DAR £3.80 INCLUSIVE CLEARANCE
  FREE COLLECTION FROM EASE LONDON 
  COLLECTION POINT IS
  ILALA MTAA WA BUKOBA
  CONTACT; TORNADO +255713607116
  SIMPLY THE BEST IN BUSINESS
  JUST DROP YOUR CAR AT OUR OFFICES AND WE WILL TAKE CARE OF IT
  WE WILL GET IT INSPECTED AND DELIVERED TO PORT FOR YOU!

  BEI ZETU HAZINA WASHINDANI
  WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
  Tupigie kwa namba hizo hapo chini au  tutumie email tafadhali

  SIMON  LOUIS +44 (0) 79 506 89 243

  HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
  Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477

  0 0

  Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Oman (Tanzania Club in Oman-TANCO) ilifanya mkutano wake mkuu hapo Ijumaa tarehe 17.01.2014 mkutano uliohudhuriwa na watanzania jumla ya 150 wanaoishi na kufanya kazi nchini Oman.

   Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa TANCO ndugu Hassan Wazeer Mtonga alitumia mkusanyiko huo kutafuta usahihi wa habari zilizoenea pamoja na picha zikionyesha wanawake wawili wakiwa wameungua na kudai kuwa ni wadada wakitanzania na kuwa wamefanyiwa ukatili huu na mabosi wao wa kioman.

  Ndugu mtonga alieleza kuwa alizipata taarifa hizo nayeye kwa nafasi yake ya Uenyekiti aliziwasilisha Ubalozi wa Tanzania nchini Oman ambao nao walizifanyia kazi kushirikiana na Serikali ya Oman kupitia polisi, hospital na viwanja vya ndege, lakini taarifa hazikuonesha kuwepo kwa tukio hilo na kuthibitisha kuwa ni uzushi na uongo kwani hawakuweza kupata majina ya watanzania hao, waajiri wao na mazingira ya mashambulio hayo.

  Ndugu Mtonga aliwaomba watanzania wote waliohudhuria Mkutano huo ambaye anataarifa sahihi kuhusu matukio hayo aziwasilishe , lakini hakuna hata mmoja aliekiri kuwa na taarifa kamili zaidi ya kupokea picha hizo kupitia mtandao wa Whatsapp.

  Mwenyekiti alisisitiza kuwa habari ile si ya kweli na kwamba ni uzushi usio na misingi yeyote ambao unaweza kuwa na athari kubwa katika mahusiano ya nchi.

  Mwenyekiti alieleza kuwa habari hii ya uvumi wa kuunguzwa na kumwagiwa tindikali kwa watanzania haikupokelewa vizuri na wenyeji wetu waoman na kuwa inatishia kuharibu uhusiano wa kundugu na kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Oman na pia watanzania na waoman kwa kupelekea kuzuiwa kwa watanzania kuja Oman kufanya kazi na hivyo kushindwa kutumia fursa za ajira zinazopatikana Oman
  Mwenyekiti aliwaasa watanzania kuwa makini na matumizi ya mtandao na kuepusha kutumia mitandao kusambaza habari ambazo si za kweli. Aliwaomba kuwa habari yeyote inayomuhusu mtanzania mahala pa kuanzia ni ubalozini au kwenye Jumuiya ya Watanzania nchini Oman.

  Mwenyekiti pia aliwasihi wa Tanzania kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na nidhamu ili kuijengea sifa nzuri Tanzania. Aliwakumbusha Usia wa Rais Jakaya Kikwete alipokutana na watanzania wanaoishi Oman wakati alipotembelea Oman mwaa 2012 alipowausia watanzania kuwa raia wema na kujiepusha na vetendo vya uvunjaji sheria za nchi wanamoishi.

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya watanzania Oman Ndugu Hassan Mtonga( Aliesimama) akiongea na watanzania katika mkutano mkuu wa Jumuiya watanzania nchini Oman uliofanyika Muscat, Oman Ijumaa tarehe 17 Januari 2014.
  Sehemu ya Watanzania wanaoishi nchini Oman wakiwa kwenye mkutano huo.

  0 0

  DSC_0029

  Marehemu Mzee Arnold Wilfred Nkhoma Kambonapany (kulia) enzi za uhai wake akiwa na mmoja wa watoto wake kwenye ibada maalum ya kutoa shukrani alipotimiza miaka 100 iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Andrea Magomeni jijini Dar hivi karibuni.

  Familia nzima ya Nkhoma Kambonapany wanasikitika kutangaza kifo cha baba na babu yao mpendwa Mzee Arnold Wilfred Nkhoma Kambonapany, kilichotokea kwenye hospitali ya Mount Ukombozi tarehe 17/01/2014.

  Taarifa za msiba ziwafikie Doctors Colin na Nicholas Darch wa Cape Town Afrika Kusini , Bi Laura Amrei wa Hamburg Ujerumani , Bi Ajira Darch wa San Fransisco , California , Marekani , Bwana Monday Wamunza akiwa Maryland , Marekani , ndugu na jamaa popote walipo.

  Alijaliwa kupata watoto 11, wajukuu 36 , na vitukuu 25. Msiba unafanyika kwa mtoto wake Professor Alice Wamunza Nkhoma , Nyumba na. 07 , Mtaa wa Koroshoni , Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.

  Maziko yatafanyika tarehe leo 19/01/2014 kwenye makaburi ya Kinondoni.
  Msafara wa mazishi utaanzia saa tano za asubuhi chuo kikuu baada ya chakula na kutoa heshima za mwisho. 

  Baada ya hapo utaelekea Kanisa la Mtakatifu Andrea Magomeni kwa ajili ya Misa.

  Baada ya hapo utaelekea Kinondoni makaburini kwa kumpumzisha Mzee Kambonapany.

older | 1 | .... | 328 | 329 | (Page 330) | 331 | 332 | .... | 3348 | newer