Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

IDRIS SULTAN AMUOMBA RADHI MAGUFULI

$
0
0
Msanii wa vichekesho nchini Idris sultan katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salalam leo wakati akimwoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli. 

       Na Khadija seif, Michuzi TV
MSANII wa vichekesho nchini Idris sultan amemuomba  radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutumia picha yake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram Kama sehemu ya kumtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa.

Idris amesema lengo lake halikua baya kwani alitafuta njia ya kipekee katika kumtakia heri na kufafanua kuwa Rais kwake ni baba,rafiki na mtu ambae analeta Maendeleo kwa mustakabali wa Taifa kwa ujumla.

Idris ameeleza   baada ya hapo picha ilikua ikisambaa kwa kasi na alichukulia ni Jambo la Kawaida  na kupeleka Mkuu wa Mkoa kuiona na kumtaka afike kituo cha polisi.

" Nilitii maagizo nakufika kituo cha polisi na nashukuru niliweza kuelezwa  kosa langu na waliniamuru twende nyumbani kwangu nakufanya ukaguzi ili waweze kujiridhisha,"

Aidha, Sultan ameeleza lengo la kufika kwake lilikua ni kufanya upekuzi wa vifaa vilivotumika katika kutengeneza picha aliyorusha katika ukurasa wake wa Instagram na hawakufanikiwa kukuta chochote.

Hata hivyo Idris amewaomba wasanii hasa wachoraji wa katuni na vibonzo au hata waimbaji kupitia upya sheria ambazo zipo na zinaeleza mipaka ya kutumia kitu chochote cha kiongozi hasa  mkuu wa nchi ili isilete madhara yoyote kwani kwa sasa anakabiliwa na kesi hiyo .

"Nadhani sisi kama wasanii ni vema kupitia sheria na kuzisoma kwa ufasaha ili kuepuka makosa,"

Pia ameweka wazi kuwa kesi kwa sasa inaendelea na uchunguzi wake ili wajiridhishe na  novemba 18 mwaka huu itasomwa rasmi na kutolewa hukumu.

BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA KUSAIDIA UJENZI WA MIRADI YA NISHATI TANZANIA

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akiagana na Kaimu Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayehusika na miundombinu ya Nishati Bw. Wale Shonibare, baada ya kufanya mazungumzo kuhusu  ushirikiano wa Tanzania na Benki hiyo, Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Kaimu Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayehusika na miundombinu ya Nishati Bw. Wale Shonibare (kulia) akiwa na mmoja wa Mkurugenzi wa Benki hiyo Bw. Baldeh Batchi, wakiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) walipokutana Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akiwa na Kaimu Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayehusika na miundombinu ya Nishati Bw. Wale Shonibare, baada ya kufanya mazungumzo kuhusu  ushirikiano wa Tanzania na Benki hiyo, Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Kaimu Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayehusika na miundombinu ya Nishati Bw. Wale Shonibare akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) walipokutana Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango-Johannesburg)


Na Benny Mwaipaja, Johannesburg


BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi kuendelea kuisadia Tanzania kutekeleza miradi yake mikubwa ya kimkakati hususan miundombinu ya Nishati na Barabara kwa kuendelea kuipatia mikopo yenye masharti nafuu ili kuharakisha maendeleo ya nchi.

Ahadi hiyo imetolewa Mjini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini na Kaimu Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayesimamia Miundombinu ya nishati, Bw. Wale Shonibare alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, kando ya Kongamano la Pili la Jukwaa la Uwekezaji Afrika lililoandaliwa na Benki hiyo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao, Dkt. Mpango amesema kuwa ameiomba Benki hiyo kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kipaumbele inayojengwa na Serikali hususan katika Sekta za nishati, barabara, uongezaji thamani wa mazao ya kilimo, elimu na maji.

Dkt. Mpango ameitaja miradi iliyowasilishwa kwa kiongozi huyo kuwa ni mradi wa kuzalisha umeme wa Ruhudji (MW 358), mradi wa umeme wa Rumakali (MW 222) mradi wa umeme wa mto Malagarasi (MW 44.5), Mradi wa kuzalisha umeme wa Kakono (MW 87) na miradi mingine ambayo itajadiliwa na Bodi ya Benki hiyo itakayokutana mwishoni mwaka huu.

Amesema kuwa miradi hiyo mikubwa itakayoiwezesha nchi kuwa na umeme wa kutosha ni muhimu kwani itasaidia kufanikisha agenda ya Seikali ya kuwa na uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

“Tumewakaribisha waje Tanzania kwa ajili ya mazungumzo na kujionea namna miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vingine kama umeme jua na ule unaozalishwa kwa njia ya upepo kama ilivyo katika maeneo mengine ya Afrika hususan Kusini mwa Jangwa la Sahara” alisisitiza Dkt. Mpango

Amesema kuimarika kwa Sekta ya nishati nchini kutaleta manufaa makubwa ikiwemo kuziwezesha biadhaa za kilimo kama vile pamba kuongezewa thamani kutokana na kuwepo kwa umeme wa uhakika wa kuendesha viwanda.

Kwa upande wake Kaimu Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bw. Wale Shonibare, amesema kuwa Benki yake iko tayari kuisaidia Tanzania ili ifikie mapinduzi makubwa ya miundombinu ya nishati kutokana na umuhimu wake katika kuendesha uchumi.

Alisema nishati ni jambo muhimu ili nchi iweze kufikia mapinduzi ya viwanda na aliahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha Benki yake inachangia juhudi za serikali za kuongeza uwezo wa kuzalisha umeme, kujenga njia za kusafirishia umeme na usambazaji wake kwa kulijengea uwezo Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO)

WANAFUNZI WAJASIRIAMALI SHULE YA HOCET WASIITWE YATIMA- ASKOFU MWAMFUPE

$
0
0
Wanafunzi pamoja na baadhi ya wananchi wakicheza ngoma ya asili ya Maasai wakati wa sherehe za Mahafali ya kumaliza kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Hocet, iliyopo Kata ya Shungubweni,wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani hivi karibuni. Kulia ni Mkurugenzi wa na Mwasisi wa Hocet, Hezekiah Mwalugaja.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Good For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe ambaye alikuwa mgeni rasmi, akijumuika pamoja na wanafunzi Angel Kiphutu na Tibet Eliya kukata keki wakati wa mahafali hayo.
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondary Hocet, Hezekiah Mwalugaja akilishwa keki na mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne, Angel Kiphutu. 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Good For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe, akilishwa keki na mwanafunzi Tibeti Eliya.


Na Richard Mwaikenda, Mkuranga.

MKURUGENZI wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Edger Mwamfupe ameupongeza uongozi wa Shule ya Sekondari ya Hocet, kwa kuwanusuru Watoto Yatima kutoka kwenye hali ya mateso, kuwabadilisha tabia ya awali hadi kuwa na furaha ya maisha.

Kwa hatua nzuri waliyofikia, Mwamfupe aliutaka uongozi kuachana na mazoea ya wanafunzi hao kuwaita yatima au shule hiyo kuiita ya Yatima, bali iitwe ya shule maalumu kwa vile mambo mengi waliyofundishwa hapo yakiwemo ya ujasiriamali yameyatoa kwenye uyatima.

Mwamfupe ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akihutubia katika sherehe za mahafali ya Kidato cha Nne ya shule hiyo iliyopo wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

“Nawasihi kuanzia sasa muache kutumia jina Yatima, msiwarudishe watoto kwenye unyonge, kwani mmefanya kazi kubwa ya kuwafundisha mambo mbalimbali ya kujitegemea, hawa sasa si sawa na watu wanaotegemea kila kitu kutoka kwa watu wengine. Hawa ni tofauti wana uwezo wa kujitegemea, Hivyo nashauri shule hii iitwe ya wanafunzi maalumu si Yatima tena,” alisema Mwamfupe, huku akipigiwa makofi.

Alitoa ushauri kwa uongozi kushirikiana na Taasisi yake kuweka mpango maalumu wa kuwawezesha wahitimu kubaki shuleni hapo kwa kuendesha miradi ya ujasiriamali kwa kutumia elimu waliyopata badala ya kuwaachia kurudi mitaani walikotoka ambako ni rahisi kurudia tena katika hali waliyokuwa nayo awali ya maisha hatarishi..

Mkurugenzi wa shule hiyo, iliyoanzishwa mwaka 2007, Mchungaji Hezekiah Mwalugaja, alisema kuwa wanafunzi wanaojiunga na shule ni yatima pamoja na wanaoishi kwenye mazingira magumu ambapo huwabadilisha tabia na mwenendo na hatimaye kuwa na tabia nzuri.

Alisema hufundishwa masomo ya kawaida, stadi za kazi, ujasiriamali, kilimo cha mbogamboga, matunda na mazao mbalimbali ambayo baadhi hutumika shuleni hapo kwa mahitaji ya chakula.

Naye, Diwani wa Kata ya Shungubweni, Kamwiri Omari aliyekuwa mmoja wa wageni waalikwa katika mahafali hayo yaliyohudhuriwa pia na baadhi ya wananchi wa kata, alifurahia uwepo wa shule hiyo katika kata hiyo, ambapo aliahidi kutoa ushirikiano kutatua kero zinazoikabili. 

Alisema kuwa tayari amewasiliana na Wizara ya Nishati ili umeme wa Rea ufike shuleni hapo na kwamba nguzo zinaletwa na umeme unaweza kuwashwa kabla ya Januari mwakani. Hivi sasa shule inatumia umeme wa jua.

Pia, ameahidi kumpeleka shuleni hapo,Ofisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, akawapatie wahitimu 43 elimu ya mikopo kuunda vikundi ili wawezeshwe kupata mikopo kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali.Wahitimu Leila Mketo, Rahel Sarakikya na Fatuma Kalanje kila mmoja alikabidhiwa zawadi ya cherehani na kupata wasaa wa kuonesha kwa waalikwa nguo walizozishona.

Mahafali hayo yalihanikizwa kwa kwaya, ngoma za asili, shoo ya mitindo ya nguo na walioshinda michezo mbalimbali walizawadiwa ikiwemo mbuzi iliyotwaliwa na timu ya Shungubweni FC iliyoishinda timu ya Mamba FC. Zote kutoka kata hiyo ya Shungubweni.

Pia palifanyika michezo ya kuvuta kamba, kukimbia na yai likiwa kwenye kijiko mdomoni, kula apple zilizoning’inizwa kwenye kamba, Mr & Miss Hocet na mingineyo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Good For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe akihutubia katika mahafali hayo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
Wanafunzi wanaoagwa wakiwa na furaha wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu Mwamfupe akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi 43 waliomaliza kidato cha nne. Kushoto ni Mwalugaja. 
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu Mwamfupe akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi 43 waliomaliza kidato cha nne 
Mkurugenzi wa Hocet, Mwalugaja akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wahitimu
Wanafunzi wajasiriamali wakionesha mavazi waliyoyashona wakati wa mafunzo ya ushonaji shuleni hapo. Walikabidhiwa kila mmoja zawadi ya cherehani.Wanafunzi wajasiriamali Raila Mketo,Rahel Sarakikya na Fatuma Kalanje wakionesha 
Ni ngoma ya Kimasai 
Wanafunzi wakitoa burudani ya shoo ya muziki.
Wanafunzi wakiwa wamejipanga baada ya kuonesha mitindo ya mavazi.
Wahitimu wa Kidato cha Nne wakiwa katika picha ya pamoja.
Askofu Mwamfupe akifurahia jambo na Outrich wa Hocet, Richard Solomonpamoja na Mdau wa Hocet, Joyce Massawe kwenye viwanja vya shule hiyo.
Wanafunzi wakishiriki mchezo wa kukimbia na yai kwenye kijiko.
Selina Lihanda akimkabidhi zawadi ya mbuzi Nahodha wa timu ya Small Stone iliyoishinda Mamba FC katika mashindano yaliyoandaliwa na uongozi wa shule ya Hocet katika Kata ya Shungubweni.

TRA YAFAFANUA MABADILIKO YA SHERIA KWENYE VIWANGO VYA KODI

$
0
0
Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Emmanuel Msambwa (kulia) akimuelimisha Mfanyabiashara wa duka la nguo wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakati wa Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi Wilayani hapo.
Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Rahabu Kibona (kulia) akichukua maelezo ya Mlipakodi kwa ajili ya maandalizi ya kusajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) wakati wa Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi Wilayani hapo.
Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Ernesta Shirima (kushoto) akiwaelimisha Vijana wa Bodaboda wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kuhusu umuhimu wa kuhamisha kadi za vyombo vya moto wakati wa Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi Wilayani hapo.
*

Na Veronica Kazimoto,Mvomero


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa ufafanuzi wa mabadiliko ya
viwango vya kodi kama vilivyoainishwa na Sheria ya Fedha ya mwaka
2019 ambapo mabadiliko hayo yamegusa Sheria za Kodi ya Mapato,
Ongezeko la Thamani (VAT), Usajili wa Vyombo vya Moto pamoja na
Usalama Barabarani.

Akizungumza wakati wa Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani
Morogoro katika Wilaya ya Mvomero, Afisa Msimamizi wa Kodi Mkuu wa
TRA, Julius Mjenga amesema kuwa, mabadiliko katika sheria ya kodi ya
mapato, jedwali la viwango vya kodi kwa wafanyabiashara wadogo wakazi,
vimepunguzwa kutoka sh. 150,000 hadi kufikia sh. 100,000, kwa wale
wenye mzunguko wa mauzo yanayozidi sh. milioni nne hadi milioni 7 kwa
mwaka.

“Kwa wafanyabiashara wenye mauzo kati ya sh. milioni saba hadi sh.
milioni 11, viwango vya kodi vimepunguzwa hadi kufikia sh. 250,000 kutoka
sh. 318,000 iliyokuwepo hapo awali,” alisema Mjenga.

Pia, kwa wafanyabiashara wenye mauzo kati ya sh. milioni 11 hadi sh.
milioni 14, viwango vya kodi vimepunguzwa hadi kufikia sh. 450,000 kutoka
sh. 546,000.

“Lengo la kupunguza viwango hivi ni kukuza ridhaa ya kulipa kodi kwa hiari
na kuongeza Mapato ya Serikali,” alifafanua Mjenga.

Kwa upande wa sheria ya usajili na uhamishaji wa umiliki wa vyombo ya
moto, Mjenga ameeleza kuwa, ada ya kupata nakala ya kadi ya gari ni sh.
50,000, pikipiki ya magurudumu matatu (bajaji) sh.30,000 na pikipiki ni sh.
20,000 badala ya sh. 10,000 iliyokuwa ikitozwa kwa vyombo vya aina hiyo
kabla ya tarehe 1 Julai, 2019.

Aidha, akizungumzia juu ya mabadiliko ya viwango vya leseni za udereva
chini ya sheria ya usalama barabarani, Mjenga amesema kuwa, leseni ya
udereva inalipiwa sh. 70,000 kila baada ya miaka mitano ambapo kabla ya
mabadiliko ilikuwa inalipiwa sh. 40,000 kila baada ya miaka mitatu.

“Mabadiliko haya kwa ujumla wake yamelenga kuongeza fursa kwa
walipakodi na wananchi kwa ujumla kuongeza ufanisi katika biashara zao
na hatimaye kuongeza mapato ya Serikali. Hivyo, natoa rai kwa walipakodi
wote kutumia fursa hii adhimu kwa maendeleo ya taifa letu,” alieleza
Mjenga.

Wiki ya elimu kwa mlipakodi katika Mikoa ya Morogoro na Pwani
itamalizika tarehe 17 Novemba, 2019 ambapo shughuli zinazofanyika ni
pamoja na usajili wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), kupokea
mrejesho, kusikiliza kero na kujibu maswali yanayoulizwa na
wafanyabiashara pamoja na wananchi kwa ujumla.

TIC YASAJILI MIRADI 1174, SEKTA YA VIWANDA YAONGOZA UWEKEZAJI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekazaji nchini (TIC),
Bw.Geofrey Mwambe akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya TIC kwenye Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekazaji nchini (TIC),
Bw.Geofrey Mwambe akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)kuhusu mafanikio ya TIC kwenye Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO).


SERIKALI kupitia Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) katika kipindi cha miaka minne kuanzia Novemba 2015 hadi Novemba 2019, imesajili jumla ya miradi 1174 yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 15,756.9 huku sekta ya viwanda ikiongoza kwa kutoa asilimia 53 ya miradi yote nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) Geoffrey Mwambe wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Taasisi hiyo chini ya Utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.

Anaongeza kuwa kati yote iliyosajiliwa nchini, tasnia ya viwanda ina jumla ya miradi 626 huku miradi mahili yenye uwekezaji mkubwa ikiendelea kuwavutia wawekezaji na kuzidi kuajiri maelfu ya Watanzania pamoja na kusaidia kupunguza uagizaji wa bidhaa na malighafi kutoka nje ya nchi.

Aliongeza kuwa kupitia miradi hiyo, jumla ya ajira zipatazo 159,833 zimezalishwa katika ajira za moja huku ajira 60,465 zikizalishwa kutokana na ukuaji wa tasnia ya viwanda nchini na nyingine ikiwemo usafirishaji kutoa ajira (11482), utalii (7861) na huduma nyinginezo (5376).

‘’Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuongeza masoko ya bidhaa zetu za ndani, na tangu dhamira ya uchumi wa viwanda itangazwe na Serikali ya Awamu ya Tano tumeshuhudia ujenzi wa viwanda vingi ikiwemo viwanda vya maziwa katika maeneo mbalimbali ya nchi na sasa hatuagizi maziwa kutoka Uholanzi na jirani zetu nchi ya Kenya kama tulivyokuwa tukifanya huko nyuma’’ alisema Mwambe.

Mwambe alisema ili kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kufikia uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda, TIC ilifanya mageuzi na maboresho mbalimbali katika sera na sheria ya uwekezaji Na. 26 ya mwaka 1997 ili kuhakikisha kuwa wawekezaji wa ndani nanje ya nchi wanapata fursa ya kushiriki katika kujenga uchumi.

Kwa mujibu wa Mwambe alisema kuwa TIC imeendelea kuimarisha mifumo na taratibu mbalimbali za uwekezaji nchini ambazo awali zilikuwa zikileta usumbufu na vikwazo mbalimbali kwa wawekezaji, ambapo kwa sasa imeweza kuongeza idadi ya watumishi katika ofisi hiyo ili kurahisisha upatikanaji wa leseni na vibali mbalimbali.

Akitolea mfano alisema kabla ya kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, TIC ilikuwa na jumla ya watumishi 5 kutoka katika Idara mbalimbali za Serikali lakini kwa sasa kuna jumla ya Maafisa 25 kutoka Wizara, Idara, Wakala na Taasisi mbalimbali za Serikali.

‘TIC tumewaweka pamoja maafisa mbalimbali wa Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za Umma kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa leseni na vibali mbalimbali na sasa kuna huduma zote za msingi kwa mwekezaji zinazotolewa moja kwa moja katika dawati letu’’ alisema Mwambe.

Akifafanua zaidi Mwambe alisema ndani ya kipindi cha utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano Serikali imeweza kuanzia viwanda vikubwa kupitia miradi ya kimkakati yenye mtaji wa zaidi ya Dola 100- 500 za Marekani ambavyo vimetoa ajira lukuki kwa Watanzania.

Akitolea mfano wa kiwanda cha kutengeza vigae ‘tiles’ cha Twyford Ltd kilichopo Chalinze Mkoani Pwani, Mwambe alisema kiwanda hicho kina mtaji wa kiasi cha Tsh Bilioni 130 kimeweza kutoa ajira za moja kwa moja takribani 2000 ambapo takribani asilimia 90 ya malighafi zake zinazalishwa hapa nchini.

‘Vipo viwanda vikubwa kupitia wawekezaji mahiri ambao wameweza kuwekeza katika miradi mikubwa ya kimkakati nah ii imewezekana kutokana na kufanya mageuzi makubwa ya sera na sharia ya uwekezaji ya mwaka 1997 na sasa uwekezaji wake umeanza kuleta manufaa makubwa nchini’’ alisema Mwambe.

Aidha aliwataka wawekezaji pindi wanapopata changamoto mbalimbali wasisite kuwasiliana na ofisi yake kwa kuwa malengo ya ofisi yake ni kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwavutia wawekezaji nchini.

JAJI MKUU AWAAGIZA VIONGOZI WA MAHAKAMA KUSIMAMIA USAJILI WA KESI MTANDAONI

$
0
0
Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga likiwa katika ukarabati Mkubwa unaoendelea.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kushoto) akikagua ukarabati Mkubwa wa Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga Mhe. David Mrango (wa pili kushoto) akiongozana na Jaji Mkuu kukagua ukarabati mkubwa wa Jengo la Mahakama Kuu Sumbawanga. Kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Leonard Magacha akifuatiwa na Mtendaji wa Kanda ya Sumbawanga, Emmanuel Munda.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kushoto) akikagua shughuli za Mahakama katika Mahakama ya Mwanzo Sumbawanga mjini. kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga Mhe. David Mrango na katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Tehama wa Mahakama ya Tanzania, Machumu Essaba.
Jengo la Mahakama ya Mwanzo Laela lililopo Sumbawanga mkoani Rukwa.

***********************************

Lydia Churi-Mahakama, Sumbawanga

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Majaji, NaibuWasajili, Watendaji na Mahakimu wote nchini kutumia mamlaka yao ya usimamizi kuhakikisha wanakagua mfumo wa kusajili na kuratibu mashauri (JSDS II) ili kuona namna mashauri yanavyosajiliwa na kurekebisha endapo kuna makosa. Jaji Mkuu ametoa agizo hilo kufuatia hatua ya Mahakama ya Tanzania ya kuamu akufanya shughuli zake kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na kutaka kuacha kupokea takwimu zake kwa njia ya makaratasi na badala yake, itakuwa ikizisoma takwimu hizo kwa njia ya mtandao.

“Mwaka huu utakuwa ni mwaka wa mwisho kwa Mahakama kupokea takwimukwenye makaratasi, tutakuwa tukizisoma moja kwa moja kwenye mtandao”,alisema Jaji Mkuu alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari wakatiakifanya majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mikoa ya Songwe na Rukwa.

“Lengo ni kwenda katika Mahakama ya karne ya 21, Mahakama inayotegemeazaidi mtandao kuliko kutegemea makaratasi”, alisema.
Alisema mfumo wa kusajili na kuratibu mashauri utawawezesha viongozi wa
Mahakama kujua ni mashauri mangapi yamesajiliwa nchini, mangapi
hayajapangiwa Majaji na Mahakimu, na mangapi yamezidi muda wa kuwepoMahakamani na hivyo kufuatilia kwa urahisi.

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, mfumo wa JSDS II utasaidia kuzidisha uwazi katikashughuli za Mahakama na kuongeza imani zaidi ya wananchi kwa Mhimili huo.

Alisema Mahakama imedhamiria kuingia katika Tehama ambapo mwezi
Julai mwaka huu iliingia Mkataba wenye thamani ya Sh. bilioni 4.1 na
Shirika la Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) utakaowezesha
Mahakama kuingizwa kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambapo
majengo 157 ya Mahakama nchini yataunganishwa. 

Mkataba huo utawezesha kuunganishwa kwa majengo ya Mahakama
kuanzia Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu, Mahakama za Hakimu
Mkazi, Mahakama za Wilaya na baadhi ya Mahakama za Mwanzo zenye
majengo ya kisasa. Mahakama zitakazounganishwa kwenye mtandao huo ni Mahakama ya Rufani 1, Mahakama Kuu 16, Mahakama Kuu Maalumu
(Specialized Division 4, Mahakama za Mkoa 29, Mahakama za Wilaya 112
na Mahakama za Mwanzo 10.

Alizitaja faida za Mahakama kusajili mashauri kwa njia ya mtandao kuwa ni
pamoja na kuwasaidia mwananchi mwenye shauri Mahakama kufahamu
mwenendo mzima wa shauri kwa kujua kila hatua ya shauri lake kwa kufahamuhatua zinazofuata kwenye shauri lake kupitia mtandao.

Jaji Mkuu amehitimisha ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Songwe na Rukwaambapo alikagua shughuli mbalimbali za Mahakama ikiwemo miradi ya ujenzi wa majengo ya mahakama na hali ya utoaji haki kwa ujumla. Katika ziara hiyo, Jaji Mkuu alikagua ujenzi wa majengo ya Mahakama za Mwanzo za Mlowo mkoani Songwe na Mahakama za Mwanzo za Msanzi na Laela mkoani Rukwa.

SIMBACHAWENE AFUTA LESENI ZA KAMPUNI ZILIZOFANYA UDANGANYIFU

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene

Na Lulu Mussa

Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene ameagiza waliobainika kusafirisha vyuma chakavu ambavyo ni miundombinu ya majitaka na maji safi wachunguzwe kujua walikovitoa ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Pia ametahadharisha kuwa yeyote atakayekutwa amebeba, kuhifadhi, kuuza au kusafirisha vyuma chakavu bila kibali, atakuwa ametenda kosa la kisheria na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Simbachawene ametoa agizo hilo jana ofisini kwake jijini Dodoma ambapo ameagiza Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuichukulia hatua Kampuni ya Press Freight Tanzania Ltd (Wakala wa usafirishaji) kwa kusafirisha makontena ya chuma chakavu mali ya kampuni ya Eco Steel ambayo hayakuwa na kibali na ilisafirisha makontena hayo baada ya katazo alilotoa na kusisitiza hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Alisema kuwa katika makampuni nane yaliyokuwa yanamiliki makontena 147
yaliyokuwa Dar es Salaam yalipokaguliwa, makampuni manne 177 yalisema uongo kwani yaliweka vitu visivyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya kusafirishwa nje na havijulikani wamevitoa wapi.

“Kwa kampuni ya Eco steel Limited na Mahavir Implex Tanzania Limited ambazozilikiuka agizo langu la kusafirisha taka hatarishi nje ya nchi, naagiza taasisi zilizowapa leseni yaani Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira wazifutie leseni kwani wamekiuka sheria ya mazingira ya vibali vya kukusanya na kusafirisha taka hatarishi ndani ya nchi, vile vile kwa mamlaka niliyonayo sitatoa leseni kwa kampuni hizo kwa ajili ya kufanya biashara hiyo hata kile kinachoruhusiwa,” alisisitiza.

Hata hivyo alizitaka kampuni nne zilizodanganya ambazo zilikuwa na mapungufumadogo kwenda NEMC kwa ajili ya kufuata utaratibu kwa kulipa faini na kuanza upya mchakato wa kupata kibali cha Waziri cha kusafirisha nje ya nchi taka hatarishi.

Pia ameagiza kampuni manne yaliyokutwa na makosa kulipa faini ya sh. 460,000 kwa kila kontena lililokaguliwa na wataalamu pia mengine yenye makossa kulipa faini iliyopangwa kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004.

Aidha Waziri huyo alisisitiza kuwa biashara zote za ukusanyaji wa vyuma chakavu kwa mtu mmoja mmoja kwa ngazi za chini zitasimamiwa na Serikali za Mitaa huku akiagiza utekelezaji huo kuanza mara moja.

Itakumbukwa jumla ya makontena 142 yanayomilikiwa na makampuni tofautiyalifanyiwa ukaguzi na taarifa kuwasilishwa na Timu ya kitaifa ya ukaguzi Oktoba 16, 2019 na kuwa taarifa ilionesha uwepo wa ukiukwaji wa sheria na kanuni zinazosimamia na kudhibiti taka zenye madhara nchini na mkataba wa kimataifa wa Basel unaoruhusu udhibiti wa usafirishaji wa taka zenye madhara na taka nyingine baina ya nchi na nchi ambazo Tanzania ni mwanachama.

Katibu Mkuu Mlawi:Ongezeni juhudi za kutangaza umuhimu wa Sekta za Wizara

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi(kushoto) akimkabidhi taarifa mbalimbali za majukumu ya Wizara hiyo Naibu Katibu Mkuu Dkt.Ally Possi (kulia)ambaye atakaimu kuanzia kesho mpaka atakapoteuliwa mtu wa kushika nafasi hiyo, mara baada ya kuagana na Menejimenti ya wizara hiyo leo jijini Dodoma, kufuatia kufikia ukomo wa utumishi wa umma ambapo anastaafu rasmi kuanzia Novemba 15,2019.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi akizungumza uongozi wa Menejimenti ya Wizara hiyo leo Jijini Dodoma kwa ajili ya kuwaaga baada ya kufikia ukomo wa utumishi wa umma ambapo anastaafu rasmi kuanzia Novemba 15,2019 kwa mujibu wa sheria.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakiwakatika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi.Susan Mlawi (mwenye gauni nyekundu) ambaye amekabidhi rasmi ofisi yake leo kwa Naibu Katibu Mkuu Dkt.Ally Possi jijini Dodoma, baada ya kufikia ukomo wa utumishi wa umma ambapo anatarajia kustaafu rasmi kuanzia Novemba 15,2019.

Serikali Yaboresha Utoaji Huduma za Vivuko Nchini

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Maselle akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wakala huo kwa kipindi cha miaka minne toka Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani leo tarehe 14/11/2019 jijini Dodoma. Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano maalum ya Watendaji Wakuu wa Taasisi,Wakala na Idara za Serikali inayoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO kuzungumzia mafanikio ya taasisi zao kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma

Serikali imepiga hatua katika utoaji huduma za vivuko kwa asilimia 131 huku huduma za karakana zikizidi kuimarika nchini tangu Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) uanzishwe mwaka 2005.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Maselle wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma.

“Wakala umeendelea kuboresha na kusimamia uendeshaji wa vivuko vya Serikali nchini kwa kuongeza idadi ya vivuko kutoka 13 wakati Wakala unaanzisha mwaka 2005 hadi kufikia 30 katika vituo 19 Tanzania Bara,” alisema Mhandisi Maselle.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Maselle akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari leo tarehe 14/11/2019 jijini Dodoma. Mkutano huo ni mendelezo wa mikutano maalum ya Watendaji Wakuu wa taasisi,Wakala na Idara za Serikali inayoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO kuzungumzia mafanikio ya taasisi zao kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli. Kutoka kulia ni Afisa Habari toka Idara ya Habari – MAELEZO, Jonas Kamaleki na kushoto ni Afisa Habari wa TEMESA, Bi. Theresia Mwami.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Maselle akionyesha ramani ya maeneo ambapo TEMESA inaendesha vivuko wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo tarehe 14/11/2019 jijini Dodoma. Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano maalum ya Watendaji Wakuu wa taasisi,Wakala na Idara za Serikali inayoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO kuzungumzia mafanikio ya taasisi zao kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.

Akizungumzia mafanikio iliyopata ndani ya kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mhandisi Maselle amesema kuwa Wakala umefanikiwa kununua vivuko vipya vitatu ambavyo ni MV KAZI kinachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni mkoani Dar es Salaam,kilichogharimu sh bilioni 7.3, MV MWANZA kinachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi mkoani Mwanza kilichogharimu shilingi bilioni 8.9 na MV TANGA kinachotoa huduma kati ya Pangani na Bweni mkoani Tanga ambacho kimegharimu shilingi bilioni 4.02.

Ujenzi wa Vivuko vyote umegharimu jumla ya shilingi bilioni 20.22 ambazo ni fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Ameongeza kuwa pamoja na utoaji wa huduma za vivuko Serikali imenunua boti ndogo tano ambazo ni MV TANGAZO inayotoa huduma ya dharura kati ya Kilambo na Namoto mkoani Mtwara, MV KUCHELE kinachotoa huduma ya dharua kati ya Msangamkuu na Msemo mkoani Mtwara, MV MKONGO kinachotoa huduma kati ya Utete na Mkongo mkoani Pwani, MV BWENI inayotoa huduma dharura kati ya Pangani na Bweni mkoani Tanga pamoja na MV SAR III ambapo ujenzi wa boti zote umegharimu shilingi milioni 415.

Aidha amesema kuwa pamoja na uwepo wa vivuko hivyo TEMESA inaendelea na ujenzi wa vivuko vipya kwa ajili ya maeneo ya Mafia – Nyamisati uaogharimu shilingi bilioni 5.3, Bugorola – Ukara ambao unagharimu kiasi cha shilingi bilioni4.2, Chato – Nkome shilingi bilioni 3.1 na Kayenze – Bezi shilingi bilioni 2.7

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi, Japhet Maselle (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo tarehe 14/11/2019 jijini Dodoma. Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano maalum ya Watendaji Wakuu wa taasisi,Wakala na Idara za Serikali inayoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO kuzungumzia mafanikio ya taasisi zao kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.(Picha zote na: Idara ya Habari – MAELEZO.)

Akizungumzia huduma za karakana, Mhandisi Maselle amesema kuwa hadi sasa TEMESA ina karakana 26 katika mikoa yote ya Tanzania Bara na moja iliyopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ambayo imejengwa mahususi kusogeza huduma kwa wateja wa Wilaya za Mlimba, Malinyi na Ifakara ambazo ziko mbali na karakana ya mkoa wa Morogoro.

Amesema kuwa katika kuboresha huduma za karakana Wakala umeanzisha karakana inayotembea ambayo imegharimu shilingi milioni 95 na ambayo itakuwa ikitoa huduma katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Karakakana hii inayotembea pia itahudimia kwa makundi magari ya Bohari ya Dawa (MSD) yapatayo 100, pia itatoa huduma mkoani Pwani katia wilaya za Bagamoyo, Utete, Mkuranga, Kisarawe pamoja na kutoa huduma ya dharura kwa magari ya umma maeneo ya barabara ya Morogoro.

Wakala umefanikiwa kununua vitendea kazi vya karakana vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni 260 ambavyo tayari vimeanza kusambazwa katika karakana 12 zilizopo Katavi, Geita, Songwe, Pwani, Dodoma, Shinyanga, Mwanza, Rukwa, Morogoro, Kahama, Ifakara, Singida na Lindi.

Katika hatua nyingine Mhandisi Maselle amemshukuru Rais Dkt. Jon Pombe Magufuli kwa kutoa fedha zote bilioni 15 zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa vivuko na kusema kuwa hiyo ndiyo dhamira halisi ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

MKURUGENZI WA HUDUMA ZA TUME YA MADINI AFANYA ZIARA MTWARA

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma za Tume ya Madini, William Mtinya (kulia) akipokelewa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Ephrahim Mushi (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi hiyo iliyopo mjini Mtwara Mkoani Mtwara ikiwa ni sehemu ya ziara yake yenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili ofisi hiyo tarehe 14 Novemba, 2019.

Mkurugenzi wa Huduma za Tume ya Madini, William Mtinya (katikati) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara
Mkurugenzi wa Huduma za Tume ya Madini, William Mtinya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara

************************************

Na Greyson Mwase, Mtwara

Leo tarehe 14 Novemba, 2019 Mkurugenzi wa Huduma za Tume ya Madini, William Mtinya amefanya ziara katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Ephrahim Mushi ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara yenye lengo la kujifunza na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wanaofanya kazi katika Ofisi za Maafisa Madini Wakazi katika mikoa husika.

Katika ziara yake, Mtinya aliambatana na Afisa Utumishi wa Tume ya Madini, Jeremiah Chuma pamoja na Meneja Habari na Mawasiliano wa Tume ya Madini, Greyson Mwase.

Mara baada ya kuwasili na kupokelewa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Ephrahim Mushi pamoja na watumishi na kuelezwa changamoto mbalimbali zinazoikabili ofisi husika, Mtinya aliwataka maafisa madini wakazi wa mikoa nchini kufanya kazi kwa kujiamini huku wakifuata Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake.

“Napenda mtambue jukumu kubwa mlilopewa katika usimamizi wa Sekta ya Madini katika kuhakikisha inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa pato la Taifa; kwa mfano katika mwaka wa fedha 2019-2020 tumepangiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 470, ni vyema mkaweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha mnasimamia vizuri shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na ukusanyaji wa kodi mbalimbali,” alisema Mtinya.

Mtinya alishauri maafisa madini wakazi wa mikoa kujenga mtandao kwa ajili ya kubadilishana uzoefu pamoja na kushauriana mambo mbalimbali ya kikazi na kuendelea kusisitiza kuwa, Tume ya Madini Makao Makuu ipo tayari kupokea na kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zitakazowasilishwa.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtinya alielekeza maafisa madini wakazi wa mikoa kuchambua pamoja na kuainisha orodha ya leseni ambazo hazifanyiwi kazi ili uandaliwe utaratibu wa kuziandikia hati ya makosa kabla ya kufutwa rasmi.

Aliendelea kusema kuwa, ni vyema leseni husika wakapewa wachimbaji wenye nia ya kuendesha shughuli za madini badala ya kukaa nazo tu huku Serikali ikipoteza mapato yake.

Akielezea mikakati ya Tume ya Madini katika kuhakikisha inavuka lengo la ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wa fedha 2019-2020, Mtinya alieleza kuwa ni pamoja na kutoa ajira mpya 166 kwa kada mbalimbali ambapo wataalam watasambazwa kwenye ofisi za maafisa madini wakazi wa mikoa nchi nzima na kwenye masoko ya madini.

Aliendelea kufafanua kuwa, ofisi zenye upungufu wa watumishi zitapewa kipaumbele lengo likiwa ni kusogeza huduma karibu na wadau wa madini nchini.

Alieleza kuwa hatua nyingine zilizofanywa na Tume ya Madini ni pamoja na ununuzi wa magari 36 ambapo mpaka sasa magari 12 yemeshapokelewa na kusisitiza kuwa juhudi zinaendelea kufanywa ili kuhakikisha Desemba mwaka huu, magari yote yatakuwa yameshapokelewa.

Aliendelea kusema mbali na upatikanaji wa magari, pia Tume ya Madini imepata maderava wapya 20 ambao wametawanywa katika mikoa mbalimbali ya kimadini.

Aliongeza kuwa, Tume ya Madini imeshaagiza vifaa mbalimbali vya kupima madini vitakavyotumika kwenye masoko ya madini, lengo likiwa ni kuhakikisha Serikali inapata mapato stahiki.

Katika hatua nyingine, Mtinya aliwapongeza watumishi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara kwa kufanya kazi kwa weledi na uzalendo mkubwa na kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa bidii huku Ofisi ya Makao Makuu ya Tume ya Madini ikiangalia namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Wakati huohuo, wakizungumza katika nyakati tofauti watumishi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara waliupongeza Uongozi wa Tume ya Madini kwa kufanya ziara katika mkoa wa Mtwara na kuahidi kuongeza ubunifu kwenye ukusanyaji wa maduhuli na kufikia lengo lililokusudiwa.

Awali watumishi hao waliwasilisha changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kutosha kwenye shughuli za upimaji wa madini, magari ya ziada kwa ajili ya kufuatilia maeneo ya mbali yenye shughuli za madini, upungufu wa watumishi wa kada ya jemolojia n.k

VIWANDA VYA NGUO, GLASI KUJENGWA SIMIYU, WATU 2000 KUPATA AJIRA

$
0
0
Mwekezaji kutoka nchini Uturuki, Bw. Mustafa Albayram akizungumza na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea eneo la Isanga lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa Viwanda katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, wakati wa ziara yake ambayo amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akisalimiana na Mwekezaji kutoka nchini Uturuki Bw. Mustafa Albayram mara tu baada ya kuwasili Mjini Bariadi Novemba 13, 2019 kwa ziara ya siku mbili yenye lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika viwanda ambaye amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo(katikati).
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akionesha moja ya eneo linalofaa kwa uwekezaji katika Kata ya Nyakabindi Mjini Bariadi, wakati wa ziara ya Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo ambaye alifuatana na Mwekezaji kutoka nchini Uturuki Bw. Mustafa Albayram mara tu baada ya kuwasili Mjini Bariadi Novemba 13, 2019 kwa ziara ya siku mbili yenye lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika viwanda.
Mwekezaji kutoka nchini Uturuki Bw. Mustafa Albayram(kulia) akiwaonesha jambo Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kutoka katika simu yake mara baada ya kutembelea eneo la Isanga lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa Viwanda katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, wakati wa ziara yake ambayo ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini(kushoto) akisalimiana na Mwekezaji kutoka nchini Uturuki Bw. Mustafa Albayram mara tu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza Novemba 13, 2019 kwa ajili ya ziara ya siku mbili mkoani Simiyu yenye lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika viwanda ambaye amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo(katikati)

*************************************

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Mwekezaji kutoka nchini Uturuki, Bw. Mustafa Albayram ameahidi kujenga viwanda viwili; kiwanda cha nguo na kiwanda cha kutengeneza glasi katika eneo la Isanga Mjini Bariadi Mkoani Simiyu mwaka 2020, mara baada ya kuridhishwa na mazingira ya uwekezaji ambapo viwanda hivyo vinatarajia kuajiri wananchi takribani 2000.

Albayram ameyasema hayo Novemba 13, 2019 mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali kwa lengo la kuangalia mazingira wezeshi kwa uwekezaji wa viwanda, ambaye alifuatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo kwa ziara ya siku mbili mkoani Simiyu.

Amesema endapo miundombinu yote muhimu hususani umeme itawekwa kwa wakati katika eneo hilo uwekezaji huo utaanza mara tu baada ya kukamilisha taratibu zote muhimu zinazohitajika ikiwa ni pamoja na usajili wa kampuni na kutafuta hati miliki ya ardhi.

“Tumeamua kuwekeza Simiyu, kila kitu kikienda sawa kiwanda cha nguo kinaweza kujengwa na kufanya kazi ndani ya miezi tisa mpaka mwaka mmoja, kiwanda cha glasi ni mwaka mmoja; baada ya usajili wa kampuni nitarudi tena Simiyu kukamilisha masuala ya hati miliki ya ardhi, sitaki kumuangusha Mhe. Balozi maana amefanya mengi kwa ajili yetu,” alisema Albayram.

Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo amesema mwekezaji ameridhishwa na eneo hilo na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa kutoa ardhi bure huku akibainisha kuwa ombi kubwa la mwekezaji ni kuwa na nishati ya kutosha kwa kuwa viwanda hivyo hususani kiwanda cha nguo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemhakikishia mwekezaji huyo upatikanaji wa mahitaji yote muhimu na kuahidi kushirikiana na taasisi zote za Serikali zinazohusika kuhakikisha anapata huduma zote kwa wakati na bila urasimu wowote.

Kuhusu suala la Umeme Mtaka amesema katika Bajeti ya mwaka 2019/2020 Wizara ya Nishati kupitia Shirika la umeme TANESCO imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupozea umeme(substation) ambacho kitajengwa karibu na eneo la uwekezaji huo

Mtaka ameongeza kuwa mtazamo wa mkoa wa Simiyu ni kuwa na viwanda vichache vinavyoajiri watu wengi badala ya kuwa na viwanda vingi vinavyoajiri watu wachache, huku akitoa wito kwa wakulima wa pamba kulima pamba kwa wingi kwa kuwa kiwanda cha nguo kitakuwa mkombozi wa kuongeza thamani ya zao la pamba na itauzwa kwa bei ya uhakika.

Naye Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa pamba nchini, Bw. Boaz Ogola amesema kujengwa kwa kiwanda cha nguo mkoani Simiyu kutasaidia wakulima wa pamba kupata soko la uhakika kuondoa changamoto ya bei ya pamba kwa kuwa kitapanua wigo wa soko la pamba, ambapo pamba inayotumika hapa ni nchini ni asilimia 20-25 ya pamba yote inayozalishwa.

TAASISI ZA UMMA NCHINI ZATAKIWA KUWAPATIA HUDUMA YA USAFIRI WATUMISHI WA UMMA WENYE ULEMAVU

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Amina S. Mollel Bungeni leo jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu mpango wa Serikali wa kuwapatia huduma ya usafiri Watumishi wa Umma wenye Ulemavu.


Happiness Shayo-Dodoma


Tarehe 14 Novemba, 2019


Serikali imezitaka Taasisi za Umma nchini kuhakikisha zinatatua changamoto yahuduma ya usafiri kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu ili wawezekutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi waUmma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kwa niaba ya Waziriwa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika wakati akijibu swali la Mhe. Amina S. Mollel(Mb) (Viti Maalum) aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuwapatiahuduma ya usafiri Watumishi wa Umma wenye Ulemavu.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, ili kufanikisha azma hiyo ya Serikali,
Taasisi za Umma zinatakiwa kutekeleza miongozo inayotolewa ikiwa ni pamojana Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma Wenye Ulemavu wamwaka 2008 unaoelekeza Waajiri kuwapatia huduma ya usafiri au kulipiagharama za mafuta ya kwenda na kurudi kazini kwa Watumishi wa Umma wenyeUlemavu ambao wana vyombo binafsi vya usafiri, lengo likiwa ni kuwawezeshakutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, Waajiri ambao hawatekelezi Mwongozohuo, wanakiuka maelekezo ya Serikali kwa kuwanyima stahiki watumishi wenyeulemavu, hivyo wakibainika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu zakiutumishi zilizopo.

Serikali kupitia Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini imejipanga kufanya Ufuatiliaji wautekelezaji wa Mwongozo huo ili uweze kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa amewakumbusha Waajiri kutoa kipaumbele cha mikopoya vyombo vya usafiri kwa Watumishi wa Umma Wenye Ulemavu wanaokidhivigezo vya kukopesheka ikiwa ni utekelezaji wa Waraka wa Watumishi waSerikali Na.3 wenye Kumb.Na. C/AC.7/228/01/16 wa Juni 30, 2011 unaotoaUtaratibu wa Kukopesha Fedha Taslimu Watumishi wa Serikali kwa ajili yakununulia Magari au Pikipiki pamoja na Matengenezo ya Magari na Pikipiki hizo

VITAMIN U YAMPONZA ROSA REE, BASATA YAMFUNGIA MIEZI 6

$
0
0
     Na.Khadija seif, Michuzi TV

BARAZA Sanaa Taifa (BASATA) limemfungia miezi 6 msanii wa kike wa muziki wa kufoka foka (HIP HOP) hapa nchini, Rosa Ree kutojihusisha na shughuli zozote za kimuziki kwa makosa matatu likiwemo la kuachia video inayokiuka maadili ya kitanzania.

 Kaimu Katibu Mkuu Mtendaji Basata Onesmo Kayanda amesema kuwa msanii huyo pia amepigwa faini ya Tsh. milioni 2 kwa kosa la kufanya kazi za sanaa nje ya nchi bila kibali kutoka BASATA kama sheria inavyotaka.

Wimbo huo wa ‘Vitamin U’ uliomponza Rosa Ree, Ameshirikishwa na msanii mwenzie kutoka Kenya, Timmy Dat.
            
Hata hivyo siku chache Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya filamu dkt. Kilonzo Kiagho alisema bodi  ni  muhimili mkuu wa Sanaa kwani ina kazi ya kuhakikisha na kusimamia picha jongevu zote pamoja na video zote.

"Tulipitia video ya vitamin U ya Rosa ree na kujilidhisha kuwa inakiuka maadili ya Kitanzania.

Pia Rosa ree alikiri kosa hilo na kuomba msamaha kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kosa la kurusha video ya wimbo wake ambao upo nje ya maadili pamoja na kufanya kazi nje ya nchi bila kibali.


EBITOKE AVITAJA VITU VIWILI VILIVOMSUKUMA KUMFANYIA VURUGU MLELA NA BEYONCE

$
0
0

   Na.Khadija seif, Michuzi TV


CHAMA cha waigizaji wilaya ya Kinondoni (TFDAA) chaitisha kikao cha kimaadili kwa wasanii wa filamu Ebitoke,kitenge comedian,pamoja na Yusuf Mlela.

Akizungumza na waandishi wahabari wakati wa kumalizika kikao hicho Cha maadili Msemaji wa chama hicho Masoud Kafftan amekiri ni kweli waliwaita wasanii hao kufuatia ugomvi uliotokea katika utambulisho wa  kazi mpya ya Msanii wa filamu nchini Yusuf Mlela ya Tamthilia ya Kauli uliofanyika katika ukumbi wa protea hoteli jijini Dar es salaam na kuvamiwa na Msanii wa vichekesho nchini Ebitoke ambae alikua kwenye Mahusiano nae na kusababisha vurugu .

"Kupitia mitandao ya kijamii tuliona video iliyokua ikimuonesha Ebitoke pamoja na ana anaedaiwa kuwa kaka yake alietambulika kwa jina la Kitenge comedian wakimfanyia fujo  Mlela pamoja na mpenzi wake Beyonce,"

Kamati ilijiridhisha na kuona kuna haja ya kuwaita wasanii hao ili kuwaeleza maadili,sheria pamoja na taratibu zingine zinazotakiwa kuwepo kutokana na Ebitoke kutumia lugha yenye madhara (Matusi) katika purukushani hizo.

"Kwanza wamekiri makosa yao,ukizingatia wao ni wasanii ambao hawana rekodi mbaya katika chama  chetu (TFDAA) na ndio kosa lao la kwanza,"

Kafftan ameeleza kuwa kamati imeamua kuwasamehe kutokana na wasanii hao kuwa tegemezi na wanategemea kazi za Sanaa kuendesha maisha yao pamoja na wategemezi wao hivyo kuwafungia kutofanya kazi za Sanaa kunaweza kusababisha mtafaruku au kuyumba kwao.

Aidha,Amewasihi wasanii kuacha maisha ya Kiki na kuwa na maisha halisi ili kuboresha Sanaa zao."Wakati mwengine kiki hupoteza  mashabiki na kufanya uonekane muongo muongo mbele ya jamii,"

Kwa upande wake Annastazia a.k.a Ebitoke amewaomba radhi Mashabiki, wanahabari pamoja na Msanii mwenzie yusuf Mlela kutokana na kumfanyia fujo kwenye mkutano wake wa uzinduzi wa kazi yake mpya.

"Hisia na hasira viliniongoza na kupelekea kufanya fujo na kusababisha uharibu wa vifaa vya waandishi wahabari, vifaa vya hotelini pamoja na mpenzi wake Mlela,"Pia amewashukuru viongozi kwa kuwaita na kufanya kikao cha pamoja na kuelekezwa baadhi ya vitu na kuhaidi kujirekebisha.

"Kwa Sasa Sina tatizo na Mlela na tumeombana msamaha maisha yanaendelea ,"
Kamati ya Maadili kutoka chama Cha waigizaji wilaya ya Kinondoni (TFDAA) wakiongozwa na Msemaji wao Masoud Kafftan,Mama lolah,jaffary Makatu wakiwa pamoja na wasanii wa vichekesho Ebitoke,Kitenge comedian pamoja na Msanii wa filamu Yusuf Mlela baada ya Kumaliza kikao cha kimaadili kufatia vurugu alizozifanya Ebitoke Mwanzo mwa wiki hii.

Kwa kipindi cha miaka minne Serikali yaokoa zaidi ya shilingi bilioni 89 kwa wagonjwa 5954 waliofanyiwa upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. MohamedJanabi akimkabidhi zawadi ya ngao mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Taasisi hiyoProf. William Mahalu kama ishara ya kutambua na kuthamini kazi aliyoifanya kwa kipindicha miaka mitatu ya kuongoza bodi hiyo ambayo imemaliza muda wake tarehe13/11/2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. MohamedJanabi akielezea mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano kwa upande wamatibabu ya moyo katika kikao cha cha bodi ya wadhamani ya Taasisi hiyo kiichofanyikajana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)Prof. William Mahalu akizungumza na wajumbe wa bodi ya wadhanini pamoja namenejimenti ya Taasisi hiyo katika kikao cha mwisho cha bodi hiyo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.

*********************************

Na Mwandishi Maalum

14/11/2019 Kwa kipindi cha miaka minne Serikali imeweza kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 89 kwa wagonjwa 5954 wenye matatizo makubwa ya moyo ambao walifanyiwa upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Kama wagonjwa hawa 5954 waliofanyiwa upasuaji hapa nchini wangetibiwa nje ya nchi Serikali ingetumia zaidi ya shilingi bilioni 178 kulipia gharama za matibabu hayo.

Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akielezea mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano kwa upande wa matibabu ya moyo katika kikao cha bodi ya wadhamani ya Taasisi hiyo.

Prof. Janabi alisema kwa wagonjwa hao kutibiwa hapa nchini matibabu yao yamegharimu kiasi cha shilingi bilioni 89 fedha ambazo zimelipwa kupitia bima zao za matibu, misaada ya wafadhili mbalimbali wa nje, wagonjwa wenyewe kujilipia na Serikali kugharamia matibabu ya wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

“Gharama ya mgonjwa mmoja aliyefanyiwa upasuaji nje ya nchi ni zaidi ya shilingi milioni 30, lakini kwa mgonjwa mmoja kutibiwa hapa nchini gharama zake hazizidi shilingi milioni 15. Kwa kutibiwa hapa nchini fedha anazolipa mgonjwa zinatumika kununua vifaa tunavyomuwekea katika moyo wake kama vile pacemaker, high power device, stent, device closure na valvu vifaa hivi tunaviagiza nje ya nchi kwani hazipatikani hapa nchini”, alisema Prof. Janabi.

Mkurugenzi huyo Mtendaji aliendelea kusema kwa kipindi cha miaka minne wameweza kuona wagonjwa 300,836 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani pamoja na nchi jirani kama vile Demokrasia ya Congo, Malawi, Ethiopia, Zambia, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Visiwa vya Comoro.

“Jambo la kufurahia ni kuwa tumeweza kuokoa maisha ya watu ambao tumewatibu na hivi sasa wanaendelea na majukumu yao ya kazi za kila siku. Kwa kipindi cha miaka minne tulilaza wagonjwa 14,960 tumefanya upasuaji wa bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa wagonjwa 4,207 na upasuaji wa kufungua kifua na kusimamisha moyo kwa wagonjwa 1,747”,alisema Prof. Janabi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo ambayo inamaliza muda wake Prof. William Mahalu aliupongeza uongozi wa Taasisi hiyo pamoja na wafanyakazi kutokana na huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa kwa wagonjwa wanaowatibu.

Prof. Mahalu ambaye ni mmoja wa madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa kwanza hapa nchini alisema anamaliza muda wake kama Mwenyekiti wa bodi hiyo huku ndoto yake ya kuona Tanzania inakuwa na Hospitali ya matibabu ya moyo ikiwa imetimia.

“Ninamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuniteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi hii kwa kipindi cha miaka mitatu. Kama mtakumbuka tangu nchi yetu ipate Uhuru mwaka 1961 wananchi wengi wenye matatizo ya moyo yaliyohitaji kufanyiwa matibabu ya kibingwa iliwalazimu kwenda kutibiwa nje ya nchi.

“Kwa kuwa kutibiwa nje ya nchi ni gharama na pia mlolongo kuwa mrefu baadhi ya wagonjwa walipoteza maisha wakati wakisubiri fedha za kwenda kupata matibabu. Hivi sasa wananchi hawapati tabu tena wanatibiwa hapa nchini kwa wakati. Ukiangalia idadi ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi yetu imeongezeka kutoka wagonjwa 150 kwa mwaka 2016 hadi kufikia wagonjwa 300 kwa siku kwa mwaka 2019”, alisema Prof. Mahalu.

Prof. Mahalu alisema wakati anasomea upasuaji wa moyo nje ya nchi kuna daktari alimkatisha tamaa na kumwambia kuwa hawataweza lakini hakukata tamaa alihakikisha anasoma kwa bidii na baada ya kuhitimu masomo yake aliweza kufanya upasuaji na alimualika yule daktari aliyemkatisha tamaa kwenda kushuhudia jinsi wanavyofanya upasuaji.

Aidha Prof. Mahali aliwashukuru wajumbe wa Bodi ya wadhamini kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuhakikisha Taasisi ya Moyo inafanya kazi zake za kutoa huduma kwa wananchi kwa weledi na wakati.

Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo ambayo imemaliza muda wake jana tarehe 13/11/2019 kwa kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu ilizinduliwa na Mhe. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu tarehe 21 Machi 2017.

WAFANYABIASHARA ARUSHA WAPEWA SIKU MOJA KUHAMISHIA SHUGHULI ZAO NDANI YA SOKO

$
0
0


*********************************

Na Tito Mselem Arusha,

Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa siku moja kwa Wafanyabiashara
wote wa Madini Mkoani Arusha kuhamishia shughuli zao ndani ya Soko
na watakao bainika kununua madini nje ya Soko watachukuliwa hatua
za kisheria ikiwemo kufutiwa leseni zao na kufikishwa Mahakamani.

Hatua hiyo inafuatia ziara ya kushtukiza ya Waziri Biteko aliyoifanya
Sokoni hapo Novemba 13, 2019 na kubaini changamoto za wanunuzi
Wakubwa wa Madini kutolitumia Soko hilo na badala yake wameendelea
kununua Madini nje ya Soko.

Katika zira yake hiyo, Waziri Biteko ameambatana na viongozi
mbalimbaliwa Serikali pamoja na Wizara ya Madini akiwemo Katibu
Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, Mwenyekiti wa Tume
ya Madini Prof. Idris Kikula, Mkuu wa Jeshi la Polisi la Mkoa wa Arusha
Jonathan Shanna na wengine.

Pia, Waziri Biteko amemtaka Mkandarasi anayeendelea na ujenzi katika
Soko hilo ahakikishe anamalizia haraka ujenzi huo huku
wafanyabiashara wakiwa wanaendelea na shughuli zao katika Soko hilo.
Aidha, Waziri Biteko amemuagiza Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof.
Idris Kikula kumuondoa Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Arusha, Robert
Erick kwa kushindwa kusimamia ipasavyo shughuli za Madini Mkoani
humo.

Afisa Madini huyo anadaiwa kuwaachia wafanyabiashara wakubwa wa
Madini Mkoani Arusha kufanya biashara ya Madini maofisini mwao
tofauti na maelekezo ya Serikali iliyowataka wafanye biashara hiyo
kwenye Masoko ya Madini ambapo ofisi nne tu ndizo zilikuwa wazi
wakati Soko hilo lina ofisi za wafanyabiashara wakubwa 40 lakini kwa
zaidi ya miezi minne hawajahamia katika ofisi hizo.

Alisema jukumu hilo la kusimamia kufanya biashara ndani ya Soko hilo
na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wenye madini majumbani
mwao ni jukumu la Afisa Madini, lakini kazi hiyo kwa sasa inafanywa na
Waziri hatua ambayo haikubaliki kabisa, wakati wa kulindana umepitwa
na wakati sio kwa Serikali hii iliyopo madarakani.

Waziri Biteko alisema kuwa, biashara ya Madini ya Tanzanite Mkoani
Arusha imeshuka kwa asilimia kubwa na wanaofanya biashara hiyo
wanajulikana lakini hawachukuliwi hatua na kwamba ofisi yake haiko
tayari kuona ubadhilifu wa aina hiyo.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Biteko amesema kuwa haoni
sababu za msingi za wafanyabiashara wakubwa wa Madini Mkoani
Arusha kushindwa kufanya biashara katika Soko la Madini lililoandaliwa
na Serikali na badala yake wafanyabiashara hao wanafanya biashara
katika ofisi zao.

Amewaeleza wafanyabiashara Wakubwa na Wadogo wa Madini Mkoani
Arusha kuwa haitaji kupigiwa makofi kwani yeye anasimamia kanuni na
sheria namba 20 ya Madini inayosema kuwa kila mfanyabiashara wa
Madini awe Mdogo ama Mkubwa anapaswa kufanya biashara ndani ya
Soko la Madini na sio vinginevyo.

Ameongeza kuwa, Wafanyabiashara wakubwa waliomba muda wa
mwezi mmoja katika kufanya biashara ndani ya Soko hilo na Wizara
iliongeza muda huo waliohitaji lakini hadi sasa ni zaidi ya miezi minne
hakuna mfanyabiashara mkubwa aliyekuwa akifanya bishara katika
Soko hilo na badala yake wanafanya biashara katika ofisi zao na
wanamiliki kilo nyingi za madini kinyume cha utaratibu.

Waziri amesema anazo taarifa za uhakika baadhi ya wafanyabiashara
wakubwa 97 wana ofisi za madini Arusha na Nairobi na wanafanya
ujanja ujanja ili wafanye biashara hiyo kwa njia haramu na kuikosesha
Serikali mapato hilo halikubaliki watachukuliwa hatua kali ikiwemo
kufilisiwa mali zao na kufikishwa Mahakamani.

Akizungumzia suala la wafanyabishara Wadogo wa Madini amesema
ofisi yake ina idadi ya wafanyabishara wenye leseni 263 lakini
wanaofanya biashara hiyo mtaani ni zaidi ya watu 1,300 hali inaonesha
wazi kuwa zaidi ya wafanyabiashara 1037 wanafanya biashara bila ya
kuwa na leseni na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Arusha analijuwa hilo
lakini ameshindwa kusimamia majukumu yake ya kazi.

Pamoja na mambo mengine Waziri Biteko amesisitiza uaminifu katika
sekta ya madini.

Airtel yazindua Airtel 4G kuboresha mawasiliano nchini

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughuliki Uwekezaji Mheshimiwa Angellah Kairuki na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw, George Mathen wakiwa wameshika nembo ya Airtel 4G baada ya uzinduzi wa Airtel 4G Dodoma. kulia ni Mwakilishiwa wa katibu mkuu wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiano Munamu Mulemwa, kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Airtel Bw Lekini Moleli . Airtel imezindua 4G ikiwa ni utekelezaji wa mipango ya uwekezaji iliyowekeana na serikali ili kutoa huduma bora kwa watanzania wote na kendendelea kuijenga Airtel mpya, hafla ya uzinduzi wa Airtel 4G ilifanyika jana jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughuliki Uwekezaji Mheshimiwa Angellah Kairuki akizindua mtandao wa Airtel 4G mkoani Dodoma, Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw, George Mathen na wengine katika picha wapili kutoka kulia ni mjumbe wa bodi ya Airtel Lekini Molel, Mwakilishiwa wa katibu mkuu wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiano Munamu Mulemwa, Mbunge wa viti maalum Mariam Ditopile . Airtel imezindua 4G ikiwa ni utekelezaji wa mipango ya uwekezaji iliyowekeana na serikali ili kutoa huduma bora kwa watanzania wote na kendendelea kuijenga Airtel mpya itakayoendelea kutoa gawio kwa wanahisa ikiwemo Serikali, hafla ya uzinduzi wa Airtel 4G ilifanyika jana jijini Dodoma.


  • Airtel yawekeza katika teknolojia ya mawasiliano ya 4G-LTE ili kutoa mawasiliano bora ya huduma za kimtandao
  • Uwekezaji wa Airtel katika teknolojia ya Mawasilaino kutachangia kufikia malengo ya serikali kwa kuchangia ukuaji wa uchumi kidigitali
    Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza kuzindua huduma ya Airtel 4G ikiwa ni muendelezo wa kupanua wigo wa mtandao wake    nchini ili kutimiza dhamira yake ya kutoa huduma bora za kimtandao kwa wateja wake.

    Akizindua huduma hiyo ya Airtel 4G leo jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughuliki Uwekezaji Mheshimiwa Angellah Kairuki alisema kuwa ni furaha kuona Airtel inatekeleza mipango ya uwekezaji na kuja na  huduma za mtandao wa Airtel 4G  kwa lengo la kukidhi mahitaji ya watanzania wote, hii ni ishara tosha inayoonesha mikakati ya kuijenga Airtel mpya itakayoendelea kutoa gawio kwa wanahisaikiwemo Serikali yetu.

    “Nimefarijika kusikia taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Airtel kwamba Airtel inatekeleza mikakati yao ya uwekezaji wa kuboresha huduma kwa kuanzisha huduma hii ya 4G/LTE ikiwa na wigo mkubwa wa kutoa huduma za mawasiliano, mimi kama Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji inanipa ishara nzuri ya matokeo ya mazingira mazuri tuliyoyaweka ili wawekezaji wetu nchini waweze kutekeleza majukumu yao na kulifaidisha taifa, haya yote yanafanikiwa  chini ya uongozi wa Serikali yetu ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dokta John Joseph Pombe  Magufuli.

    “Wote tunatambua, Airtel Tanzania na Serikali yetu waliingia makubaliano mazuri hivi karibuni kwamba serikali yetu iwe na umiliki wa asilimia 49 wa hisa ndani ya Airtel Tanzania, kutokana na makubaliano hayo pia hadi leo Airtel Tanzania imeshailipa serikali jumla ya bilioni 8 kama sehemu ya makubaliano hayo na leo hii Airtel wanatekeleza upanuzi wa mtandao, hii ndio mikakati ya kuijenga Airtel mpya ili kuendelea kuleta tija kwa shughuli za kijamii na uchumi, alisema kairuki

    Mheshimiwa Waziri Kairuki pia alitoa pongezi kwa Airtel kutokana na taarifa yao inayoonesha  kasi ya kusambaza huduma hiyo ya Airtel 4G  katika miji mikubwa takribani 25 ambapo leo wamewasha mtandao wa Airtel 4G mkoani Dodoma. “ Naamini ya kwamba kwa uzinduzi huu wa mtandao wa Airtel 4G, Airtel itazidi kuwa imara sana na sisi serikali tuko tayari kuwaunga mkono kwa hili”. Kairuki aliongeza.

    Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Bw, George Mathen alisema kuwa uzinduzi huu wa huduma ya Airtel 4G ni moja ya malengo ya muda mrefu ya kuifanya kampuni ya Airtel kuwa na uwezo wa kutoa huduma bora ukizingatia sasa ni ulimwengu wa kidigitali.
    “ili mteja aweze kutumia huduma ya Airtel 4G anatakiwa kuwa na Simu ya Smatifoni yenye uwezo wakupokea mawimbi ya 4G na awe amewezesha laini yake ya simu kuwa ya Airtel 4G. Kupata uhakika kwamba simu yake inauwezo wa kutumia 4G piga *149*95#”
    Mathen alisema Uwekezaji na upanuzi wa mtandao kwa kuzindua huduma za Airtel 4G ni kutelekeza makubaliano baina wa wabia wetu ambao ni serikali ya kuhakikisha ya kwamba Airtel inaendeleza uwekezaji kwenye upanuzi wa mtandao kwa lengo la kuzidi kuwa na mtandao imara,

    Aliongeza kuwa huduma ya 4G itatoa nafasi kukuza teknolojia ya kidigitali hapa nchini kwa kuwa na huduma nafuu na zenye kasi za intaneti na hivyo kubadilisha maisha ya Watanzania. “Airtel tutaendelea kuzindua huduma na bidhaa nafuu kwa ajili ya Watanzania wa kila rika” Mathen aliongeza.

Wahadhiri watakiwa kujiongeza katika ufundishaji -Hasunga

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema kuwa dunia imebadilika katika mifumo ya kuandaa wataalam hivyo wahadhiri vyuo wabadilike na kuachana na mfumo wa mazoea ya kuandaa wataalam kuajiriwa.

Waziri wa Hasuga ameyasema ameyasema hayo wakati wa Kongamano la Kitaaluma katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) jijini Dar es Salaam,amesema kuwa wanataaluma wanazalishwa wawe wanaweza kujitegemea kuliko kuwa wataalam wanaosubiri ajira.

Amesema kuwa vijana wanaohitimu lazima wafikirie kwenda sekta ya kilimo sio kwa kubeba jembe ila kwa kwenda kutoa elimu kwa wakulima katika mazao ya biashara ikiwa ni kutafuta masoko.

Hasunga amesema kuwa Chuo cha IFM kuzalisha wataalam wa ushauri na kuwa mahiri katika eneo hilo ili kila mtu akitaka suala la ushauri katika biashara ajue anamtoa kutoa chuo hicho.

Amesema katika kwenda uchumi wa Kati wa viwanda wataalam wana nafasi kubwa ya kuishauri serikali namna bora ya kufika kwani mazingira ya teknolojia yanabadilika kila siku.

Amesema Tanzania ina vitu vingi vya kufanya hivyo kwa wataalam kwenda mbali zaidi katika kutumia taaluma hizo kuanzisha kampuni au biashara ambapo malengo ya serikali kufikia uchumi wa kati.

Nae Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)Profesa Tadeo Satta amesema kuwa wanawataalam wa ushauri katika chuo hicho wa kutosha na wanaendelea kuzalisha.

Amesema katika Chuo kimeweka msingi wa utoaji wa elimu ambayo itafanya vijana wajiajiri katika sekta mbalimbali kutokana na ubunifu wanaofanya wa mahitaji ya jamii.
 Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akizungumza katika Kongamano la Kitaaluma katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha kuelekea mahafali yatakayofayika Nov3mba 29 jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta akizungumza katika Kongamano la Kitaaluma  katika kuwaandaa wahitimu kwenda kutumia taaluma walizopata katika maendeleo jijini Dar es Salaam
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi Fedha(IFM) Dkt Imanuel Mnzava akitoa kuhusiana na chuo kilivyojipanga katika mahafali na utoaji tuzo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na wanafunzi wa Chuo hicho katika kongamano la Kitaaluma jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akiwa katika picha ya pamoja wanafunzi waliopata  tuzo mbalimbali  na vyeti vya kufanya vizuri katika masomo yao ya mwisho

WANAFUNZI WAJASIRIAMALI SHULE YA HOCET WASIITWE YATIMA- ASKOFU MWAMFUPE

$
0
0
Wanafunzi pamoja na baadhi ya wananchi wakicheza ngoma ya asili ya Maasai wakati wa sherehe za Mahafali ya kumaliza kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Hocet, iliyopo Kata ya Shungubweni,wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani hivi karibuni. Kulia ni Mkurugenzi wa na Mwasisi wa Hocet, Hezekiah Mwalugaja.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Good For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe ambaye alikuwa mgeni rasmi, akijumuika pamoja na wanafunzi Angel Kiphutu na Tibet Eliya kukata keki wakati wa mahafali hayo.
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondary Hocet, Hezekiah Mwalugaja akilishwa keki na mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne, Angel Kiphutu. 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Good For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe, akilishwa keki na mwanafunzi Tibeti Eliya.

Na Richard Mwaikenda, Mkuranga.

MKURUGENZI wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Edger Mwamfupe ameupongeza uongozi wa Shule ya Sekondari ya Hocet, kwa kuwanusuru Watoto Yatima kutoka kwenye hali ya mateso, kuwabadilisha tabia ya awali hadi kuwa na furaha ya maisha.

Kwa hatua nzuri waliyofikia, Mwamfupe aliutaka uongozi kuachana na mazoea ya wanafunzi hao kuwaita yatima au shule hiyo kuiita ya Yatima, bali iitwe ya shule maalumu kwa vile mambo mengi waliyofundishwa hapo yakiwemo ya ujasiriamali yameyatoa kwenye uyatima.

Mwamfupe ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akihutubia katika sherehe za mahafali ya Kidato cha Nne ya shule hiyo iliyopo wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

“Nawasihi kuanzia sasa muache kutumia jina Yatima, msiwarudishe watoto kwenye unyonge, kwani mmefanya kazi kubwa ya kuwafundisha mambo mbalimbali ya kujitegemea, hawa sasa si sawa na watu wanaotegemea kila kitu kutoka kwa watu wengine. Hawa ni tofauti wana uwezo wa kujitegemea, Hivyo nashauri shule hii iitwe ya wanafunzi maalumu si Yatima tena,” alisema Mwamfupe, huku akipigiwa makofi.

Alitoa ushauri kwa uongozi kushirikiana na Taasisi yake kuweka mpango maalumu wa kuwawezesha wahitimu kubaki shuleni hapo kwa kuendesha miradi ya ujasiriamali kwa kutumia elimu waliyopata badala ya kuwaachia kurudi mitaani walikotoka ambako ni rahisi kurudia tena katika hali waliyokuwa nayo awali ya maisha hatarishi..

Mkurugenzi wa shule hiyo, iliyoanzishwa mwaka 2007, Mchungaji Hezekiah Mwalugaja, alisema kuwa wanafunzi wanaojiunga na shule ni yatima pamoja na wanaoishi kwenye mazingira magumu ambapo huwabadilisha tabia na mwenendo na hatimaye kuwa na tabia nzuri.

Alisema hufundishwa masomo ya kawaida, stadi za kazi, ujasiriamali, kilimo cha mbogamboga, matunda na mazao mbalimbali ambayo baadhi hutumika shuleni hapo kwa mahitaji ya chakula.

Naye, Diwani wa Kata ya Shungubweni, Kamwiri Omari aliyekuwa mmoja wa wageni waalikwa katika mahafali hayo yaliyohudhuriwa pia na baadhi ya wananchi wa kata, alifurahia uwepo wa shule hiyo katika kata hiyo, ambapo aliahidi kutoa ushirikiano kutatua kero zinazoikabili. 

Alisema kuwa tayari amewasiliana na Wizara ya Nishati ili umeme wa Rea ufike shuleni hapo na kwamba nguzo zinaletwa na umeme unaweza kuwashwa kabla ya Januari mwakani. Hivi sasa shule inatumia umeme wa jua.

Pia, ameahidi kumpeleka shuleni hapo,Ofisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, akawapatie wahitimu 43 elimu ya mikopo kuunda vikundi ili wawezeshwe kupata mikopo kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali.

Wahitimu Leila Mketo, Rahel Sarakikya na Fatuma Kalanje kila mmoja alikabidhiwa zawadi ya cherehani na kupata wasaa wa kuonesha kwa waalikwa nguo walizozishona.

Mahafali hayo yalihanikizwa kwa kwaya, ngoma za asili, shoo ya mitindo ya nguo na walioshinda michezo mbalimbali walizawadiwa ikiwemo mbuzi iliyotwaliwa na timu ya Shungubweni FC iliyoishinda timu ya Mamba FC. Zote kutoka kata hiyo ya Shungubweni.

Pia palifanyika michezo ya kuvuta kamba, kukimbia na yai likiwa kwenye kijiko mdomoni, kula apple zilizoning’inizwa kwenye kamba, Mr & Miss Hocet na mingineyo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Good For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe akihutubia katika mahafali hayo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.

WAHITIMU CBE WASHAURIWA KUTUMIA MAARIFA WALIYOPATA KUJIAJIRI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WANAFUNZI 2439 wa ngazi za Astashahada, Shahada, na Shahada za Uzamili kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara nchini (CBE) tawi la Dar es Salaam wanatarajiwa kuhitimu rasmi masomo yao Novemba 16 mwaka huu katika mahafali ya 54 ya Chuo hicho.

Akihutubia katika sherehe za Convocation zilizofanyika Chuoni hapo na kuwakutanisha wanafunzi na wahitimu (Alumni) wa chuo hicho, mgeni rasmi na Mkurugenzi wa kampuni ya Vision Investment Ally Mchahanga amesema kuwa ndani ya miaka 54 Chuo hicho kimepiga hatua kubwa sana hasa katika taaluma ambapo wataalamu wengi wametoka hapo pamoja na kuboresha miundombinu ya elimu.

Amesema kuwa Serikali imeendelea kushirikiana na Chuo hicho katika kuhakikisha elimu inayotolewa Chuoni hapo inakidhi mahitaji ya wanajamii hasa ukizingatia kwa sasa nchi imedhamiria kujenga uchumi wa kati na hiyo ni fursa kwa wahitimu hao kutumia maarifa waliyopata katika kuleta tija kwa wanajamii hasa katika uchumi.

Vilevile amewashauri wahitimu wa vyuo hivyo (Alumni) kusaidia maendeleo ya chuo hicho ili kuzidi kuendelea kukiweka katika nafasi bora zaidi na hiyo ni pamoja na kuwasaidia wanafunzi wanaoendelea na masomo Chuoni hapo na hiyo ni pamoja na kuwashauri.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Emmanuel Mjema amesema kuwa mipango ya chuo hicho inaendelea kutekelezwa vyema na hali ya chuo hicho hasa katika taaluma na miundombinu inaridhisha.

Mjema amesema kuwa mafunzo, elimu na tafiti za kibiashara zilizofanywa na Chuo hicho zimeleta tija hasa kwa kutoa wataalamu na washauri wa kibiashara katika sekta mbalimbali.

"Chuo pia kimeendelea kutoa shahada za uzamili katila masuala mbalimbali ikiwemo tehama na mnyororo wa ugavi na hiyo yote ni katika kupanua wigo wa utoaji wa elimu na wahitimu wote wanaweza kurudi Chuoni hapa ili kuendelea na masomo zaidi" amesema.

Vilevile amesema kuwa katika kwenda na kasi ya Serikali ya awamu ya tano Chuo hicho kimefanya marekebisho ya miundombinu ikiwemo jengo la maktaba ya kisasa pamoja na kuboresha maabara ya kompyuta kwa kununua kompyuta zitakazokidhi mahitaji.

Pia amewashauri wahitimu wote kutumia vyema maarifa na elimu ya ujasiriamali waliyoyapata Chuoni hapo na kubadili mitizamo yao kwa kuweka mbele mawazo ya kijiajiri na sio kutegemea kuajiriwa pekee.

"Dunia ya sasa inatawaliwa na sayansi na teknolojia na matatizo yote mnayoyaona yanazunguka dunia myatumie kama fursa na pia msimamie maamuzi yenu pamoja na kujituma, kamwe msikatishwe tamaa kuhusiana na ndoto na malengo yenu" ameeleza.

Makamu mwenyekiti wa umoja wa wahitimu wa chuo hicho (Alumni) Peter Mayunga amesema kuwa wataendelea kushirikiana zaidi ili kuleta maendeleo ya Chuo hicho ikiwa ni sehemu ya azma ya maendeleo ya chuo hicho cha biashara.

Amewashauri wanafunzi kuzingatia masomo yao pamoja na kuwa na mawazo ya kibiashara na sio kutegemea kuajiriwa pekee na hiyo ni pamoja na kutumia mawazo wanayopewa na taasisi hiyo ya biashara katika kuleta maendeleo yenye tija katika jamii.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Vision Investment na mgeni rasmi wa Convocation ya 54 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Ally Mchahanga akizungumza katika hafla hiyo na kueleza kuwa Alumni wataendelea kushirikiana na Chuo hicho ili kukipeleka mbele zaidi, leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara nchini (CBE) tawi la Dar es Salaam, Dkt. Emmanuel Mjema akizungumza katika hafla hiyo ambapo amewashauri wahitimu hao kutumia changamoto zilizopo kama fursa na hiyo ni pamoja na kusimamia ndoto na mawazo yao, leo jijini Dar es Salaam.

Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Edda Tandi Luoga akisoma hotuba yake wakati wa Convocation ya 54 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dar es Salaam iliyowakutanisha wahitimu na Alumni kutoka Chuo hicho ambapo amewashauri wanafunzi kuyatumia maarifa wanayoyapata kwa kutengeneza ajira zao wenyewe, leo jijini Dar es Salaam.

Makamu mwenyekiti wa jumuiya ya wahitimu wa Chuo cha CBE (Alumni) Peter Mayunga akizungumza katika hafla hiyo ambapo amewashauri wahitimu hao kushirikiana wao kwa wao na kuinuana ili waweze kutimiza malengo yao, leo jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Kampuni ya Vision Investment na mgeni rasmi wa Convocation ya 54 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Ally Mchahanga akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kufanya vizuri katika masomo yake Mhitimu wa Shahada ya Uzamili ya masuala ya Tehama Juma Masoud katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Vision Investment na mgeni rasmi wa Convocation ya 54 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Ally Mchahanga akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kufanya vizuri katika masomo yake Mhitimu wa Shahada ya Uzamili ya masuala ya Kompyuta Maria Charles katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Vision Investment na mgeni rasmi wa Convocation ya 54 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Ally Mchahanga akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kufanya vizuri katika masomo yake Mhitimu wa Shahada ya Uzamili ya masuala ya biashara za kimataifa Philipo Clemence katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Vision Investment na mgeni rasmi wa Convocation ya 54 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Ally Mchahanga akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kufanya vizuri katika masomo yake Mhitimu wa Shahada ya Uzamili ya masuala ya ununuzi na ugavi Ibrahimu Mussa katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images