Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA CAG NA MAJAJI NA MAKATIBU TAWALA

$
0
0

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akitangaza uteuzi wa viongozi mbalimbali uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU





WAZIRI KIGWANGALLA KUOGOZA KAMPENI YA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII.

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla akiwa katika kilele cha mlima Kilimanjaro (Uhuru Peak) katika kampeni ya kutangaza utalii mlima Kilimanjaro. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla akizungumza na Menejimenti ya TANAPA na Wakuu wa Kanda wa Shirika hilo jijiini Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla akipanda mlima Kilimanjaro akiwa ameambatana na kunndi la wasanii na wadau mbalimbbali kwa lengo la kuutangaza mlima Kilimanjaro hivi karibuni. 
………………………………………………..

Na.Aron Msigwa – WMU

Waziri wa Malisili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema ataongoza kampeni ya kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika ukanda wa kusini na ukanda wa Kaskazini magharibi kwenye hifadhi mpya za Taifa zilizotangazwa hivi karibuni.

Amesema kampeni hiyo itawahusisha wasanii na watu maarufu wenye ushawishi katika jamii na inalenga kuhamasisha utalii wa ndani na kutangaza vivutio vya utalii vilivyo katika hifadhi za Taifa za Ruaha,Mikumi, Nyerere na Burigi – Chato.

Dkt.Kigwangalla ameyasema hayo alipokuwa akizugumza na Menejimenti ya Shirika la hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) na wakuu wa Kanda wa shirika hilo jijini Arusha.

Amesema hatua hiyo ya kuwatumia wasanii na watu maarufu wenye ushawishi katika jamii inalenga kuogeza hamasa kwa watanzania wavijue na kuvitembelea vivutio vya utalii vilivyopo katika hifadhi hizo hivyo kuogeza idadi ya watalii wa ndani.

Dkt.Kigwangalla amesema wasanii hao na watu maarufu wana wafuasi wengi wanaofuatilia kazi zao na matukio wanayofanya katika jamii kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii hivyo ni vyema wakatumika kutangaza utalii katika maeneo hayo.

Amesema hatua kazi hii ya kuhamasisha utalii wa ndani ni vyema wadau na watumishi walio kweye sekta husika wakawa wa kwanza kuvijua vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo mbalimbali ili iwe rahisi kuvielezea na kuvitagaza.

“Tukitaka kutagaza soko la utalii wa ndani lazima sisi wenyewe tuanze kwanza kuyajua maeneo ya vivutio tuliyonayo ili iwe rahisi kuwafikia watu wengine, tuna marafiki zetu ndani na nje ya Tanzania inakua rahisi kwetu kuwaalika na kuwakaribisha kwenye vivutio hivyo kwa kuwa sisi wenyewe tunavijua” Amesisitiza Dkt.Kigwangalla.

Amesema mkakati wa sasa ni wa kusambaza uelewa kuhusu vivutio vilivyopo ndani ya nchi ili kuwahamasisha watanzania wengi zaidi kutembelea vivutio hivyo akibainisha kwamba mkakati huo utakuwa na matokeo ya haraka na gharama nafuu ya kuhamasisha utalii wa ndani katika maeneo mengine ya nchi tofauti na ilivyo sasa ambapo watu wengi wanayafahamu maeneo machache na hasa yaliyo mikoa ya Kaskazini.

“Nilipoamua kuutangaza mlima Kilimanjaro na mimi mwenyewe kushiriki kupanda mlima kila mtu alishuhudia nini kilichotokea, kila mtu alikua akiuzungumzia mlima na hii inaongeza umaarufu wa mlima ndani ya nchi huu ni mkakati tunaotakiwa kuutumia katika maeneo mengine” Amesema.

Dkt. Kigwangalla ameiagiza TANAPA iendelee kukusanya takwimu za makundi mbalimbali ya watalii wa ndani wanafanya utalii katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo watazania wanaoshiriki mbio za marathon.

Katika hatua nyingine Waziri wa Maliasili na Utalii ameiagiza TANAPA kuifanyia kazi na kuikamilisha miradi ya ujenzi wa magati na ununuzi wa vivuko na Boti zitakazokuwa zikitumika kusafirisha watalii katika ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi kwenye eneo la Hifadhi ya Taifa ya Saadani.

Amesema gati hizo zitajengwa Dar es salaam, Saadani, Pangani, Pangani na Tanga ili kuwezesha boti hizo kusimama katika maeneo hayo yenye vivutio vya utalii na kushusha watalii wanaotaka kutembelea maeneo hayo.

“Hili ni eneo muhimu sana kwetu na rahisi kuuza huduma zetu za utalii wa ndani ya maji kutokana na uwepo wa visiwa na idadi ya watu wanaokwenda kuvitembelea, Ni lazima tujipange kuzitumia fursa hizi kwa kuwa na boti nzuri zitakazowawezesha watu kufanya utalii, mikutano, harusi na sherehe mbalimbali ndai ya maji na hii itakua ni Biashara kubwa kwetu na njia moja nzuri ya kulitumia vizuri eneo la bahari tulilo nalo” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Amesema ili kuitangaza hifadhi ya Taifa ya Saadani ni lazima kuiunganisha na utalii wa fukwe ili kuwavutia watalii wengi zaidi na kuongeza kuwa hifadhi hiyo kutokana na maeneo mazuri yaliyopo,sehemu za kulala na ukaribu wake na Bagamoyo na Dar es salaam.

Dkt. Kigwangalla amefafanua kuwa uanzishaji safari za boti za siku kutokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo na kurudi Dar es salaam utawawezesha watalii kwenda kati katika maeneo hayo kwa haraka na ni rahisi kuuza huduma hiyo kwa wageni watakaokuwa wanakwenda kufanya utalii mwisho wa wiki na kuiwezesha Serikali kupata faida ya kiuchumi kutokana na uwepo wa huduma hizo.

JESHILA MAGEREZA MKOANI SIMIYU MBIONI KUANZA KILIMO CHA PAMBA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Simiyu, alipowasili leo kwa ziara ya kikazi inayohusu Jeshi la Magereza mkoani humo kuanza kilimo cha pamba kwa kutumia ardhi na nguvukazi ya wafungwa walionao.Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya Ulinzi na Usalama baada ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wakwanza kushoto) alipowasili kwa lengo la kujadili Jeshi la Magereza mkoani humo kuanza kilimo cha pamba kwa kutumia ardhi na nguvukazi ya wafungwa walionao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera (aliyevaa nguo ya Kitenge), baada ya kukagua vyumba vya mahabusu na ofisi ya Polisi wilayani hapo.Wengine ni Maafisa wa Jeshi la Polisi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),akitoka kuzungumza na mahabusu waliohifadhiwa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Busega,mkoani Simiyu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

…………………..

Na Mwandishi Wetu, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amelitaka Jeshi la Magereza kutumia jumla ya Ekali Elfu Tatu na Sabini na Moja zilizopo mkoani hapo kwa kilimo cha pamba ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt.John Magufuli la kutaka jeshi hilo kubadilika na kuingia kwenye mfumo wa uzalishaji ili liweze kuondokana na mfumo wa kutegemea bajeti kuu ya Serikali kulisha wafungwa nchini.

Ameyasema hayo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni mkoani hapo lengo ikiwa ukaguzi wa shughuli za taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo na kuangalia fursa zinazopatikana katika mikoa mbalimbali nchini ili kuweza kulibadilisha jeshi la magereza

“Mheshimiwa naibu waziri sisi kama mkoa tuko tayari kushikana na jeshi la magereza kwani kuna ardhi ya kutosha na naomba nikuhakikishie hawa wakilima pamba japo ekali mia moja tu na zikauzwa wataweza kufanya mambo mengi ya maendeleo ikiwemo kujenga nyumba za kuishi askari ambazo zitakua ni za kiwango cha juu,” alisema Mtaka

Akizungumza katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni alisema Serikali imelipokea jambo hilo kwani ndio lengo hasa la serikali kuona jeshi la magereza linajitegemea katika uendeshaji wake pasipo kutegemea bajeti kuu ya serikali

“Mheshimiwa Rais alishatuagiza tulibadilishe jeshi hili la magereza na tayari tushaanza na tumetenga magereza kumi ya kimkakati nchini ambayo yameteuliwa kuleta mapinduzi katika jeshi, ziara hii ni kuona fursa zilizopo katika mikoa mingine kupitia magereza,nakuahidi jambo hilo tumelichukua kama wizara na muda si mrefu litapatiwa ufumbuzi,” alisema Masauni

Naibu Waziri Masauni pia alipata nafasi ya kutembelea Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Busega na kuzungumza na mahabusu waliopo kituoni hapo ambapo akuridhishwa na hali ya uchafu katika chumba cha mahabusu kituoni hapo na kuuagiza uongozi kufanya utaratibu wa kusafishwa kwani waliopo ndani ni binadamu na wana haki zao ikiwepo kukaa sehemu safi ili kulinda afya zao.

WATANZANIA WATAKAOSHINDA KILIMANJARO MARATHON 2020 KUTIA KIBINDONI SH. MIL. 7

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto), akifurahi mara baada ya kufunua pazia kuzindua mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020, kwenye Hoteli ya Coral Beach, Dar es Salaam Mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo wa wizara hiyo, Yusufu Singo na Rais wa Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka na kutoka kulia ni Woinde Shisael Meneja Mawasiliano wa Kamouni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42. Mashindano hayo yatafanyika Machi Mosi mwakani. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto), akifunua pazia ikiwa ni ishara ya kuzindua mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020, kwenye Hoteli ya Coral Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo wa wizara hiyo, Yusufu Singo na Rais wa Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka na kutoka kulia niWoinde Shisael Meneja Mawasiliano wa Kamouni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto), akikabidhiwa zawadi na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42.
Meneja wa Grand Malt, David Tarimo wadhamini wa mbio za Km 5, akielezea kuhusu udhamini huo pamoja na sifa za kinywaji hicho.
Woinde Shisael Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon akielezea kuhusu udhamini wao na kuwaomba watanzania kuisapoti kampuni hiyo kwa kujisajili kwa wingi kujiunga na mtandao huo mkubwa nchini. 
Pamela Kikuli Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42. zielezea kuhusu udhamini wa mbio ndefu na kuitangaza bia ya Kilimanjaro yenye jina linalotukuza Mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio kikubwa cha utalii nchini.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Executive Solutions Waratibu wa mashindano hayo akiongoza hafla hiyo ya uzinduzi na kuelezea umuhimu wa watu kuanza kujisajili ili kushiriki mashindano hayo makubwa nchini na nje ya Nchi.
RAIS WA TOC, FILBERT bAYI AKIELEZEA UMUHIMU WA WATANZANIA KUSHIRIKI NA KUSHINDA MASHINDANO HAYO, ILI WAPATE FURSA YA KUSHIRIKI MASHINDANO YA OLIMPIKI.
Rais wa RT, Anthony Mtaka akitangaza nyongeza ya bonasi kwa wanariadha watanzania watakaoshinda mashindano hayo.
Waziri Dk. Mwakyembe akihutubia katika hafla hiyo
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Leodger Tenga akitoa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo.
Waziri Dk. Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa RT, BMT na wadhamini wa mashindano hayo
Waziri Dk. Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa RT, BMT na wadhamini wa pamoja na waandaji na waratibu wa Kilimanjaro Marathoni.




Na Richard Mwaikenda 

WANARIADHA wa Tanzania watakaoshinda mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020, kuibuka na kitita cha sh. mil. 7 ambapo sh. Mil 4 ni zawadi ya kawaida na sh. mil 3 ni motisha.

Motisha hiyo ilitangazwa na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano hayo, uliofanywa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe katika Hotel ya Coral Beach, Masaki, Dar es Salaam jana.

Waziri Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema kuwa motisha hiyo iwe ni kichocheo kikubwa kwa wanariadha wa Tanzania kushiriki kwa wingi na kushinda mbio hizo.Alisema kuwa huwa inashangaza kuona zawadi ya 1-39 zinakwenda kwa wakimbiaji wa kutoka nje, wakati Tanzania ina watu wenye misuli, mikono na vifua lakini hushindwa, wakati watu hao hao wakikimbizwa na polisi hukimbia sana.

“Nitafurahi sana kuona bahasha nyingi za zawadi zikibaki nchini, naomba wenye uwezo mkubwa tushiriki kwenye mbio hizi zenye jina kubwa kimataifa,” alisema Dk.Mwakyembe.Aliwapongeza waandaji wa mashindano hayo ambayo sasa yamekuwa yanavutia watu wengi kutoka mataifa 56 Ulimwenguni, hali inayochangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania.Alisema kitendo hicho kimesaidia sana kuutangaza Mlima Kilimanjaro na vivutio vingine vya utalii vilivyopo nchini. Pia imesaidia mashindano hayo kuwa na wadhamini wengi.

Rais wa RT, Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, aliwaasa wanariadha wa Tanzania kuachana na kasumba ya kukimbilia kushiriki mashindano ya nje ambako hata zawadi wanazopewa ni sawa na zinazotolewa na Kilimanjaro marathoni na mara nyingine kuzidi.

Aliwataka wajenge tabia ya kupenda kushiriki mashindano ya nyumbani na hasa Kilimanjaro Marathon yenye hadhi kubwa sawa na mengine ya kimataifa. Alisema kuwa waandaji wameamua kutoa motisha ili wanariadha wa kitanzania washiriki kwa wingi na kushinda.

Alisema kuwa wanariadha wakienda nje kushiriki baadhi hulipwa dola 1000 ambayo ni sawa na sh. 2,460,000 za Tanzania na wengine hulipwa dola 500, kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na zawadi ya sh. mil. 4 na nyongeza ya motisha sh. mil. 3, jumla sh. mil 7 kwa mshindi wa mbio za Km 42.

Mshindi wa Tigo Kili Half Marathon Km 21, hulipwa sh. mil. 2 kwa upande wa wanaume na wanawake pia.Mashindano hayo mwaka huu yametimiza miaka 18 tangu ilipoanzishwa 2001.Naye, Rais wa Kamati ya Olympic Tanzania TOC, Filbert Bayi, alisema kuwa wanariadha inabidi wayathamini mashindano ya Kilimanjaro Marathon, kwani ni kipimo tosha cha washindi kupata fursa ya kushiriki mashindano ya Olympic Tokyo, Japan 2020.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Leodger Tenga, alisema hakuna njia ya mkato katika mafanikio, hivyo kuwataka wanariadha kutobweteka, bali wajitahidi sana kufanya mazoezi ambayo ni msingi wa mafanikio ya ushindi.

Hafla hiyo iliwakilishwa pia na Pamela Kikuli Meneja wa Bia ya Kilimanjaro wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42, Woinde Chisael Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo inayodhamini mbio za Km. 21 na David Tarimo Meneja wa kinywaji aina ya Grand Malt wadhamini wa mbio za Km. 5.

TAA yaweka mazingira bora ya kujisomea Ilala sekondari

$
0
0
Mwanafunzi Diana Seth wa shule ya sekondari ya Ilala (kulia) akionesha moja ya majaribio katika maabara ya Biolojia, wakati wageni waalikwa pamoja na mgeni rasmi wa mahafali ya 13 ya shule hiyo, Bi. Harieth Nyalusi kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (wa pili kushoto), akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Julius Ndyamukama walipotembelea maabara hiyo.
Kaimu Meneja wa Biashara na Masoko wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Harieth Nyalusi (aliyesimama), akiwakilisha salamu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Julius Ndyamukama wakati wa mahafali ya 13 ya shule ya sekondari ya Ilala ya Jijini Dar es Salaam, yaliyofanyika hivi karibuni.
Wanafunzi skauti wa shule ya sekondari ya Ilala wakionesha ukakamavu kwa kupasuliwa tofali kichwani katika sherehe za mahafali ya 13 ya shule hiyo yaliyofanyika hivi karibu.
Mmoja wa skauti wa shule ya sekondari ya Ilala ya Jijini Dar es Salaam akizuia pikipiki mbili kwa mikono na kichwa katika sherehe za mahafali ya 13 ya shule hiyo yaliyofanyika hivi karibuni.
Mwanafunzi Salvatory Jeremia (kushoto), akipokea cheti cha kuhitimu kidato cha nne kutoka kwa mgeni rasmi Bi. Harieth Nyalusi, Kaimu Meneja Biashara na Masoko wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Julius Ndyamukama. 





Skauti wa shule ya Sekondari ya Ilala (kushoto) akimvisha skafu mgeni rasmi wa mahafali ya 13 ya shule hiyo, Bi. Harieth Nyalusi, Kaimu Meneja Biashara na Masoko wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Julius Ndyamukama. Mahafali hayo yamefanyika hivi karibuni.

Wahitimu wa kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya Ilala wakiimba wimbo wa kuwaaga wenzao pamoja na walimu katika mahafali yao yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam

WATOTO WAWASHIWA VIFAA VYA KUWASAIDIA KUSIKIA

$
0
0
 Bi. Maria Mosi akionyesha uso wa furaha wakati mtoto wake Gloria Raphael mwenye umri wa miaka mitatu kuanza kusikia sauti kwa mara ya kwanza baada ya kuwashiwa kifaa cha usikivu alichopandikiziwa kwa ajili ya kumsaidia kusikia
 Mtoto Ethan Riziki mwenye umri wa miaka saba akilia baada ya kusikia sauti kwa mara ya kwanza.

Mtaalam wa huduma ya usikivu Muhimbili Bw. Mathayo Majogoro (kulia) akirekebisha sauti kifaa cha usikivu kwa mtoto Uebert Kigala mwenye umri wa miaka saba na nusu.

 Daktari Bingwa wa Upasuaji Masikio, Pua na Koo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, Dkt. Godlove Mfuko (katikati) akizungumzia zoezi la uwashwaji wa vifaa vya usikivu (Switch on) kwa watoto wawili waliopandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia (Cochlear Implant) mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu, kushoto ni Dkt. Aveline Kahinga na kulia ni Dkt. John Masago.

 Mtaalam wa Sauti Bw. Fayaz Jaffer akielezea namna vifaa vya usikivu vinavyofanya kazi.


Watoto wawili wawashiwa vifaa vya kusaidia kusikia

Watoto wawili ambao wamewekewa vifaa vya kusaidia kusikia katika hospiali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo wamewashiwa vifaa hivyo na kuweza kusikia sauti kwa mara ya kwanza tangu wazaliwe.

Mbali na zoezi hilo, pia mtoto Uebert Kigala amerekebishiwa sauti kifaa alichopandikiziwa kwa ajili ya kumsaidia kusikia ikiwa ni mwendelezo wa wataalam kufuatilia maendeleo yake ili kuhakikisha kifaa kinafanya kazi kwa ufanisi.

Akizungumza na waandishi wa habari Daktari Bingwa wa Upasuaji Masikio, Pua na Koo Godlove Mfuko, amesema mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu Hospitali ya Mloganzila ilifanya upasuaji kwa watoto watatu ambapo leo wawili wamewashiwa vifaa vyao ili waweze kusikia sauti.

“Hawa watoto hawajawahi kusikia sauti tangu wazaliwe hivyo leo wataanza kusikia sauti mbalimbali katika mazingira yanayowazunguka baada ya kuunganisha vifaa hivi na kuviwasha’’ amefafanua Dkt. Mfuko.

Sambamba na hilo, Dkt. Mfuko ametoa wito kwa jamii kujenga utamaduni wa kupima afya zao kwa sababu asilimia 20 ya watu wenye tatizo la usikivu ndio wanaokuja hospitali huku asilimia 80 wakibaki nyumbani.

Tangu kuanzishwa kwa huduma hii Juni 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jumla ya watoto 34 wamewekewa vifaa vya kusaidia kusikia (Cochlear Implants) hivyo kufanyika kwa huduma hizi nchini ni mwendelezo wa kuunga mkono jitihada za Mh. Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Joseph Pombe Magufuli za kuhakikisha wananchi wanafikiwa kwa urahisi.


Hadi sasa uwezo wa watalaam wazalendo kufanya upasuji umefikia asilimia 90 huku uwezo wa kuwasha vifaa vya kusaidia kusikia (cochlear implants) watoto waliopandikizwa vifaa hivyo ambao walizaliwa wakiwa hawasikii umeongezeka kufikia asilimia 100.


Gharama za upasuaji kwa mgonjwa au mtoto mmoja kuwekewa kifaa cha kusaidia kusikia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ni Tshs. 36 milioni wakati akipelekwa nje ya nchi kwa matibabu hayo yanagharimu takribani Tshs. 80 hadi Tshs. 100 milioni kwa mtoto mmoja.


HALMASHAURI YA ARUSHA YAPATA CHAKULA KWA AJILI YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE

$
0
0
Na Woinde Shizza globu ya jamii ,Arusha

Kufuatia mkakati wa kuendelea kupandisha kiwango cha taaluma na kuongeza ufaulu wa mitihani ya Taifa ya kidato cha nne, halmashauri ya Arusha imefanikiwa kupata chakula kwaajili ya wanafunzi wa kidato cha nne, katika kipindi chote cha mitihani ya Taifa inayotarajiwa kuanza mapema mwanzoni mwa wiki ijayo.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo wa chakula, kutoka Kanisa la Pentekoste- Ngulelo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Alvera Ndabagoye, licha ya kushukuru waumini wa kanisa hilo, amesema kuwa, uhakika wa uwepo wa chakula kwa wanafunzi, kipindi chote cha mtihani, utawawezesha wanafunzi, kutulia kisaikolojia na kufanya vizuri katika matokeo yao ya mitihani hiyo. 

Ameongeza kuwa, halmashauri inatambua na kuthamini mchango wa wadau wote, kutokana na uhalisia kuwa, Serikali peke yake haiwezi kutatua matatizo yote yanayoikabili sekta ya elimu, hivyo amewataka wadau kuendelea kujitoa kwa hali na mali kuunga mkono juhudi za aserikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Rais John Pombe Makufuli kwa kutoa elimu bila malipo.

Awali, Kiongozi wa Huduma ya Kanisa la Pentekoste Ngulelo, mwalimu Onesmo Anael, amesema kuwa, waumini wa kanisa lake, wameamua kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano, kupitia Sera ya Elimu bila malipo na kuwa jukumu la chakula ni la wazazi, na kuamua kuwasaidia wazazi wasio na uwezo, kuwapa watoto hao chakula, kipindi chote cha kufanya mitihani ya Taifa mwaka 2019.

Amefafanua kuwa, wapo watoto yatima, wanaoshindwa kumudu kuchangia chakula shuleni, lakini pia wapo watoto ambao, wazazi wao hushindwa kuwachangia chakula cha mchana wawapo shuleni, kutokana na kipato chao kidogo, na kusababisha watoto wao kushinda bila kula wawapo shuleni.

"Kama kanisa, tumeguswa na hilo, tukaamua kuelekeza sadaka zetu, kwa wanafunzi wote wanaotegemea kuanza mitihani yao ya kidato cha nne wiki ijayo, kwa shule za ndani ya hamashauri yetu ya Arusha"alisema Onesmo.

Onesmo ameweka wazi kuwa, waumini wa kanisa lake, wamekusanya sadaka zao na kutoa jumla ya magunia 40 ya mahindi yenye kilo 100 na mifuko 20 ya maharage, kwa pamoja vikawasidie wanafunzi wetu wa kidato cha nne.

Naye Afisa Elimu Sekondari, Medard Lupenza, amethibitisha kuwa, kiasi hicho cha mahindi na maharagwe, kimegawanywa kwenye shule 26 za serikali zenye wanafunzi wa kidato cha nne, kwa uwiano kulingana na idadi ya wanafunzi.

Hata hivyo, wakuu wa shule zote 26, wamewashukuru uongozi wa kanisa la Pentekoste Ngulelo, pamoja na waumini wote, kwa kutambua na kuguswa na changamoto ya chakula, inayowakabili wanafunzi wasio na uwezo, na kuamua kujitoa kuchangia chakula ili kuwapa nafasi walimu na wanafunzi kufikiria mirihani tu.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa shule hao, Mwenyekiti wa Wakuu wa shule, Mwalimu Mwamvita Kilonzo, amesema kuwa walimu, hupata wakati mgumu sana pale ambapo, wazazi hushindwa kiwalipia watoto wao chakula, jambo ambalo husababisha unyonge kwa watoto wasiokula shuleni na kuwafanya hata walimu kujisikia vibaya.

Hata hivyo, mwalimu Kilonzo, amesema kuwa, uhakika wa uwepo wa chakula, utasababisha utulivu kwa walimu na wanafunzi, na kutegemea ufaulu kuongeza kwenye matokeo ya mtihani wa Taifa mwaka huu wa 2019.

RC KILIMANJARO AJIFUNZA JAMBO ATHARI YA MAFURIKO YA MVUA WILAYANI HANDENI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mghwira akizawadiwa samaki aina ya Kambare na mwanakijiji wa Suwa Wilayani Handeni Mkoani Tanga. Dkt Mghwira yupo ziarani Handeni kujifunza na kujionea athari ya mafuriko ya mvua yaliyotokea hivi karibuni Mkoani Tanga. Bwawa la Suwa limeathirika kwa kiasi kikubwa sana ambalo ni chanzo cha maji Handeni vijijini.Picha na Jamal Zuberi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga (OMM-Tanga) 

MBUNGE KINGU AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO , AWAHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA

$
0
0
Mbunge Kingu akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wakati akikagua ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kijiji cha Nkenene.
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akiwahubia wananchi wa Kijiji cha Ilowoko wakati akikagua miradi ya maendeleo pamoja na kuwahamasisha kujiandikisha kwa wingi ili waweze kuwachagua viongozi wa vijiji, vitongoji kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katibu Muenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Iyumbu, Lameck Maguni akizungumza kwenye mkutano huo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkenene wakiwa kwenye mkutano huo.
Wananchi wa Kijiji cha Nkenene wakiwa kwenye mkutano.
Mbunge Kingu akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Ilowoko.
Mbunge Kingu akiwa na Wananchi baada ya kukagua ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kijiji cha Ilowoko. 



Na Dotto Mwaibale, Singida

WANANCHI wa Kijiji cha Ilowoko Kata ya Iyumbu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wamesema hawajawahi kumuona mbunge anayewajali wananchi wanaoishi maporini kama Elibariki Kingu.

Hayo waliyasema juzi katika mkutano wa hadhara aliouandaa mbunge huyo wakati akikagua miradi ya maendeleo pamoja na kuwahamasisha kujiandikisha kwa wingi ili waweze kuwachagua viongozi wa vijiji, vitongoji kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)

"Kwa kweli tangu kijiji hiki kianzishwe hatujawahi kumuona kiongozi yeyote anayejali wananchi wanaoishi maporini kama mbunge huyu Elibariki Kingu" alisema mkazi wa kijiji hicho aliyejitambilisha kwa jina moja la Nkuba 

Nkuba alisema viongozi waliowengi wanapenda kuwatembelea wananchi ambao wapo maeneo yanayofikika kiurahisi kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mizuri lakini kwa Kingu amefanikiwa katika hilo.

Kingu akizungumza katika mkutano huo alisema tangu Rais Dkt. John Magufuli aingie madarakani amefanya kazi kubwa ya kuwaletea watanzania maendeleo.Alisema amewapelekea miradi ya maji, ujenzi wa vituo vya afya Ihanja, Sepuka na sasa katoa sh.500 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Kata ya Iyumbu.

Kingu alisema kuwa mbali na miradi hiyo pia amefanikisha kujenga shule, barabara na baadhi ya maeneo yamepata umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA)

Kingu alisema kutokana na kazi hiyo kubwa aliyoifanya Rais Dkt. John Magufuli kwa wananchi hao heshima ya pekee ya kumpa watahakikisha viongozi wote katika uchaguzi wa serikali za mitaa vijiji na vitongoji wanatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)

" Ndugu wananchi heshima pekee ya kumshukuru Rais wetu kwa kutuletea maendeleo haya ni kuhakikisha tunakipa ushindi mkubwa chama chetu naombeni twendeni tukajiandikishe kwa wingi na siku ikifika ya kupiga kura basi tuwachague viongozi watakaounda serikali kupitia CCM" alisema Kingu.


Katika Kata hiyo ya Iyumbu Kingu alitoa zaidi ya sh.700,000 kwa ajili ya kukarabati madawati ya Shule ya Msingi Nkenene na ujenzi wa sakafu wa shule hiyo ambayo imechakaa hivyo kuwafanya wanafunzi kupata elimu kwenye mazingira duni.

NYAVU HARAMU ZENYE THAMANI YA SH.Mil 39.3 ZATEKETEZWA KWA MOTO.

$
0
0
Shehena ya Vyavu haramu aina na Makokoro vilivyokamatwa katika Operesheni   inayoendelea  katika vijiji vinavyolizunguka bwawa la Nyumba ya Mungu vikiwa tayari kwa kuteketezwa kwa moto.

Na.Vero Ignatus,Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga  Thomas Apson,ameteketeza  kwa moto nyavu aina ya makokoro na vyandarua vya kujikinga na mbu, vinavyotumika kwa uvuvi haramu vilivyokamatwa katika oparesheni  inayoendelea  katika vijiji vinavyolizunguka bwawa la Nyumba ya Mungu  vyenye thamani vya shs.39.3mil.

Apson  amesema kuwa  katika oparesheni hiyo  wavuvi haramu 14 katika bwawa hilo wametiwa mbaroni kwa kuwatishia polisi wenye silaha waliokuwa doria na kuwataka waweke silaha ili  wazichape ngumi kavu kavu.

Afisa Tarafa ya Lembeni  Gikila Salisali  amesema, baadhi ya watumishi wa umma  wasiokuwa waaminifu wamekuwa kikwazo katika vita hivyo kwa  wanashirikiana na wavuvi haramu na kuiomba serikali iwape boti ili kuimarisha doria ndani ya  bwawa.

Wananchi wa vijiji hivyo bi Eda Eliakimu na bakari kingazi wakazi wa nyumba ya Mungu wameipongeza serikali kwa kutangaza upya vita hivyo ambavyo wamesema vinaweza kusaidia kupunguza kasi ya uvuvi haramu ambao umekuwa tishio kwa samaki wachanga ambao  wangeweza  kubadili maisha yao.

Benki ya NBC yadhamini Gofu ya Mabalozi visiwani Zanzibar

$
0
0





Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro (kushoto), Mbunge wa Kenya, Kassim Sawa (kulia), na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri (wa pili kulia), wakimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi, Eliah John yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC kama moja ya shughuli za kuisapoti sekta ya michezo na utalii nchini. Mashindano hayo yalifanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar jana.
Meneja wa NBC Tawi la Zanzibar, Ramadhani Lesso (kushoto) akipongezana na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro, huku mchezaji mwenzao Mbunge wa Kenya, Kassim Sawa akiwangalia wakati wa mashindano ya kwanza ya gofu ya Mabalozi yaliyofanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar jana. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Benki ya NBC kama moja ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro (kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi, Issa Mohamed Chaap yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini. Mashindano hayo yamefanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar jana.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro (kushoto) akipokea zawadi ya kushiriki katika Mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri yaliyofanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff Kisiwani Zanzibar jana. Mashindano hayo yalidhaminiwa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini.
Mbunge wa Kenya, Kassim Sawa (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri baada ya kushiriki mashindano ya kwanza ya gofu mabalozi yaliyodhaminiwa na NBC katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff Kisiwani Zanzibar jana ikiwa ni moja ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro akijiandaa kupiga mpira wakati wa Mashindano ya kwanza ya Golf ya Mabalozi yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisapoti sekta ya Michezo na Utalii zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Mashindano hayo yamefanyika katika viwanja vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar jana.
Wacheza gofu wakipozi kwa picha pamoja mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki pamoja na maofisa wa Benki ya NBC wakati wa mashindano hayo mjini Zanzibar jana.




BENKI ya NBC imedhamini mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi visiwani Zanzibar huku ikiahidi kuendelea kusapoti sekta ya michezo na utalii visiwani humo kutokana na mchango wake katika maendeleo ya taifa.

Akizungumza wakati wa mashindano hayo katika Viwanja vya Gofu vya Sea Cliff visiwani humo jana, Mkuu wa Kitengo cha Wateja maalumu binafsi wa Benki ya NBC, Ashura Waziri alisema licha ya kuwa michezo husaidia afya kitu ambacho ni muhimu katika uzalishaji mali, lakini pia michezo yenyewe inaweza kuongeza ajira na kuinua uchumi wa wanamichezo na kwa taifa.

“Naihakikishia Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar kwa kupitia Kamisheni ya Utalii kuwa NBC itaendelea kuisaidia kwenye michezo kama tulivyofanya kwa kudhamini gofu ya mabalozi, tunathamini michezo kwa wafanyakazi wetu pia, tunaihakikishia wizara ya michezo pia tutaendelea kusapoti michezo,” akaongeza.

Naye Meneja wa Tawi la NBC mjini Zanzibar, Ramadhani Lesso alisema NBC imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo visiewani humo na ndio sababu ya kuitikia wito wa Wizara ya Habari na Utalii kupitia Kamisheni ya Utalii kushiriki katika mashindano hayo kwani wamekuwa wakishirikia kwa muda mrefu aatika kusapoti utalii visiwani humo.

“Kama mnavyofahamu benki yetu ina ATM zisizopungua 7 hapa Zanzibar na zote zinatoa huduma ya Visa ambayo ni maalumu kwa ajili ya wananchi wote lakini zaidi kwa watalii. Kwahiyo utakuta watalii wanafaidika sana wanapotumia mashine zetu za kutolea pesa na mashine nyingine zilizopo mahotelini.

“Watalii ni muhimu sana kwetu ndio maaana tulipopata mualiko huu kutoka kwa Mkurugenzi wa Kamisheni ya Utalii tuliona ni sehemu muhimu sana kwetu kwa ajili ya kuunga mkono serikali kwa upande wa maendeleo na vilevile ikiwa ni sehemu ya michezo kama ilivyo sera ya michezo,” aliongeza.

Pamoja na hayo meneja huyo akatoa wito kwa serikali na wadau wa michezo kuunga mkono juhudi za kusapoti mchezo wa gofu ufundishwe mashuleni na sehemu zote ili watanzania wote waweze kuucheza a kuupenda.

Katika mashindano hayo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Damas Ndumbaro, ambaye pia alikuwa mshiriki, Eliah John aliibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza huku Issa Mohamed Chaap wote wa visiwani humo kushika nafasi ya pili.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 4,2019

TRC YAKANUSHA TAARIFA ZILIZOCHAPISHWA NA GAZETI LA TANZANIA MPYA,

SERIKALI KUTOA MILIONI 300 KWA AJILI YA MRADI WA KUSAMBAZIA MAJI WANANCHI KUTOKA BWAWA LA TURA WILAYANI UYUI

$
0
0
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia) akiongozana jana na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Uyui kutoka Bwawa la Tura wilayani Uyui ambapo ametoa milioni 300 kwa ajili ya kuanza ujenzi mradi wa usambazaji maji katika eneo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Igalula Mussa Ntimizi akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa(mwenye kofia) jana wakati kiongozi wakati alipokuwa na ziara ya kukagua Bwawa la Tura wilayani Uyui ili kuona jinsi ya kujenga mradi wa kusambaza maji 

*************************************

SERIKALI imeahidi kutoa milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa usambazaji wa maji kwa wananchi kutoka chanzo cha maji cha Tura wilayani Uyui ili kuwaondolea kero ya upatikanaji wa maji ya uhakika ya muda mrefu kwa wakazi wa eneo hilo.

Fedha hizo ni sehemu zitakazotumika katika kukamilisha mradi huo ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati wa ziara yake Wilayani Uyui Mkoani Tabora kwa ajili ya kutatua kero za maji kwa wananchi wa eneo hilo.

Alisema kukamilika kwa chanzo hicho cha maji kitasaidia kuzalisha lita zaidi ya milioni 2.7 na kuwahudumia wakazi zaidi ya 11,000 na hivyo kuwaondolea usumbufu wa kutembea umbali mrefu kutafuta maji.

Alisema kuwa Serikali haiwezi kuona wananchi wanateseka kutafuta maji kwa umbali mrefu huku kukikwa na chanzo cha maji kizuri ambacho hakitumiki.

Waziri huyo alisema mradi huo utakuwa na hatua tatu ambazo ni ujenzi wa kituo cha kutoa maji kwenye bwawa na kusafisha maji, hatua ya pili ni ujenzi wa tenki la upokeaji wa maji na hatua ya mwisho ni ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji kwa wananchi.

Naye Mbunge wa Jimbo Igalula Mussa Ntimizi alisema kuwa licha ya bwawa hilo kumilikiwa na Shirika la Reli Tanzania(TRL) wamekubaliwa lianze kutumika kutatua kero ya maji kwa wananchi

MBUNGE AYSHAROSE MATTEMBE AONGOZA CHANGIZO UJENZI WA MADARASA NA UFUNGUZI WA SHULE ITIGI

$
0
0


Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe (katikati), akikata utepe kuashiria kufungua rasmi Shule ya Msingi Mitundu 'B' iliyopo wilayani Itigi mkoani humo baada ya kupata usajili wa Serikali ambapo pia aliendesha harambee ya kupata fedha za ujenzi wa madarasa mawili ya shule hiyo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Ally Minja, Mwalimu Mawazo Myabhi, Afisa Mtendaji wa Kata ya Mitundu, Raphael Ackley na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Manyoni, Blandina Mawala. 
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akisalimiana na Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, Timothy Yona.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akiwasalimia wananchi kwa kuwapungia mikono.

Wanafunzi wakipiga makofi wakati wa kumpokea mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe 
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Wanafunzi wakiimba wimbo maalumu.
Wazazi na walezi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, William John akizungumza.
Wanafunzi wakifurahi kwenye hafla hiyo.
Mratibu Elimu wa Kata hiyo, Sister Christina Muro, akizungumza.
Chifu wa Kata hiyo, Mzee Ally Idd Izenzele, akizungumza.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Manyoni, Abel Mtaalamu, akizungumza.
Sister Salome Timothy Nkowi, akimkabidhi zawadi Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe.
Wanawake wa UWT wakimkabidhi zawadi ya kitambaa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Ally Minja, akikabidhiwa zawadi.

Twist ikichezwa.
Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, Timothy Yona, akizungumza.
Katibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Manyoni, Mwadawa Maulid, akizungumza.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Manyoni, Blandina Mawala, akizungumza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Ally Minja, akizungumza.
Watoto nao walikuwepo kwenye hafla hiyo.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe (katikati), akiongoza harambee hiyo. 
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akisisitiza jambo kwenye changizo hilo.
Mshereheshaji wa hafla hiyo (MC) Mwalimu Utukufu Gwimile akiwajibika
Diwani wa Viti Maalumu (CCM) wa kata hiyo, Rose Madumba, akizungumza.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mitundu, Benjamin Lissu, akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake wakati wakichangia harambee hiyo.
Saruji ikiletwa kwenye harambee hiyo.


Mdau wa maendeleo wa kata hiyo, Mhandisi Felix Dagaki, akizungumza kwenye harambee hiyo.







Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akimkabidhi mpira Mwalimu Paul Maduhu kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.



Hafla ikiendelea.



Muonekano wa majengo ya shule hiyo.








Na Dotto Mwaibale, Singida





JAMII imetakiwa kuwekeza kwenye miundombinu ya shule ili wanafunzi waweze kupata elimu katika mazingira bora.





Ombi hilo limetolewa jana na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe wakati akiendesha harambee ya kupata fedha za ujenzi wa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Mitundu 'B' iliyopo wilayani Itigi mkoani humo wakati akiifungua rasmi baada ya kupata usajili wa Serikali.





"Nawaombeni wazazi na walezi wekezeni katika kuboresha miundombinu ya shule ili watoto wapate elimu katika mazingira bora" alisema Mattembe.





Mattembe alisema urithi pekee wa kumpa mtoto ni elimu na sio nyumba wala pesa hivyo kila mwanajamii anapaswa kuguswa katika kuchangia ujenzi wa miundombinu ya shule.





Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Ally Minja alisema bila ya kufanya jitihada za makusudi za ujenzi wa madarasa katika Kata hiyo ya Mitundu hali itakuwa mbaya kutokana na ongezeko kubwa la watoto ambapo kwa mwezi watoto kati ya 80 hadi 95 wanazaliwa.





"Hapa Mitundu pana uchumi mkubwa hivyo tusipo jitoa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa tutashindwa pa kuwapeleka watoto wetu kupata elimu au watalazimika kurundikana katika darasa moja watoto zaidi ya 200" alisema Minja.





Minja alisema idadi ya watoto wanaozaliwa katika kata hiyo ni kubwa ukilinganisha na ongezeko la vyumba vya madarasa na idadi hiyo ni kwa watoto waliosajiliwa baada ya mama zao kujifungua katika kituo cha afya cha kata hiyo.





Mdau wa maendeleo wa kata hiyo, Mhandisi Felix Dagaki ambaye alitoa sh.milioni moja na saruji mifuko 20 kuchangia ujenzi wa madarasa hayo aliwataka wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii na kuwa wao ndio wanategemewa kuwa viongozi wa kesho kwani hata yeye alisoma katika kata hiyo.





Katika harambee hiyo Mattembe alichangia sh.500,000 na fedha taslimu zikiwa ni sh. 215,000 , ahadi ikiwa ni sh. Milioni 2, 215,000 na saruji mifuko 24.

BTI YAAGIZWA KUSHIRIKIANA NA HALMASHAURI KUTOA ELIMU YA UFUGAJI NYUKI

$
0
0
Samwel Samumba Stashahada ya Ufugaji nyuki mwaka wa pili akitoa ufafanuzi wa matumizi ya mizinga ya kisasa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nziku wakati wa maonesho jana ya ufugaji nyuki kwenye sherehe za mahafali ya nane ya Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora.
Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nziku (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa sherehe za mahafali ya nane ya Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nziku akitoa hotuba jana wakati wa mahafali ya nane ya Chuo cha Mafunzo ya ufugaji Nyuki Tabora.
Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nziku (katikati) akishirikiana na Vijana wa Msange JKT kuimba wimbo maalumu wakati wa sherehe za mahafali ya nane ya Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora jana

***********************************

NA TIGANYA VINCENT

CHUO cha Mafunzo ya Ufugaji nyuki Tabora kimetakiwa kushirikiana na Halmashauri mbalmbali ili kuhakikisha kinaifanya sekta ya ufugaji nyuki inatoa mchango na kuwa kichocheo kikubwa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nziku wakati wa mahafali ya nane ya Chuo hicho mjini Tabora.

Alisema ni vema Chuo kihakikishe wa wafugaji nyuki wengi wanapata elimu ili waweze kutumia mbinu za kisasa za uzalishaji wa asali kwa ajili ya kuongeza ubora unaotakiwa na uzalishaji wa asali nchini.

Dkt. Nziku alisema ufugaji wa nyuki hautaji matumizi ya fedha nyingi kwa ajili ya kununulia dawa kama zile za mifugo wengine za kukabiliana na magonjwa bali anachohitaji ni kuwa na eneo la msitu na mizingi iliyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ili kuongeza uzalishaji na ubora wa asali.

Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka wahitimu wa mafunzo ya ufugaji nyuki kutumia elimu waliyopata kwa kujiari wenye kwa kuanzia mashamba darasa ya ufugaji nyuki na uzalishaji asali wa kitalaamu.

Alisema hatua itawasaidia kuepuka lawama za kutokuwa na ajira kwa kuwa chanzo kizuri cha mapato ambayo yatawapelekea kupata fedha nyingi.

“Mwajiriwa Serikalini atasubiri miaka thelathini ifike ndipo alipwe mafano yake ambayo yaweza kuwa milioni 300 au 500 ,lakini mtu aliyejiari mwenyewe fedha hiyo anaweza kuipata kwa muda mfupi” alisema.

Aliwataka wahitimu kuangalia fursa za kuanzisha vikundi na kuwa na andiko ambalo litawasaidia kupata mikopo ambayo itawawezesha kuanzisha miradi ya ufugaji nyuki.

Dkt. Nziku aliongeza kuwa hatua itasaidia sio tu kupata faida bali kutoa utaalamu wa ufugaji nyuki na uhifadhi wa mazingira kwa wananchi wengi na kuwafanya waone kuwa nyuki ni rasilimali nyuki kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Naye Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora Semu Daudi alisema kuwa wanatarajia kutumia msitu wa Simbo uliopo wilayani Uyui kama shamba darasa ili kuwafikia wananchi wengi wanaohitaji mafunzo hayo.

Katika mahafali hayo ya nane ya Chuo hicho jumla ya wahitimu 116 wamehitimu mafunzo ya ufugaji nyuki ambapo astashahada ni 61 na shahada ni 54

Wakulima wa Korosho kunufaika na huduma za NBC msimu mpya wa ununuzi wa zao hilo.

$
0
0



Na Mwandishi wetu,Mtwara
WAKATI wakulima wa korosho wakiendelea na msimu mpya wa korosho kwa mwaka 2019/20 Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesema itaendelea kuwahudumia na kuwahakikishia usalama wa fedha zao huku ikisogeza huduma hizo karibu zaidi badala ya kusafiri umbali mrefu.

Akizungumza wakati wa Kongamano la Uwekezaji na Maonyesho ya Biashara mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki, Meneja wa NBC Mkoa wa Mtwara, Job Nshatsi alisema wameendelea kuwa mstari wa mbele kutuoa huduma za kibenki, ushauri na mafunzo ya kifedha na biashara yanayowezeha wateja wake ikiwemo wakulima na wafanyabiashara wa korosho.

Alisema katika kuhakikisha wakulima wananufaika na huduma zake tayari wameendelea kuongeza mtandao wao wa mawakala katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha wakulima wanapata fedha kwa wakati lakini pia kwa usalama kwa kuepuka kusafiri na fedha umbali mrefu kwenda palipo na tawi la benki hiyo.

“NBC tunatoa huduma za kibenki maalumu kwa ajili ya kukuza na kuendeleza kilimo-biashara (agribusiness) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kilimo nchioni (PASS), tukiangalia sekta ya kilimo na mnyororo mzima wa thamani katika kilimo, na kwa Mtwara tutaendelea kutoa huduma ili kusaidia kukuza uzalishaji, uongezaji wa thamani na uuzaji wa zao la korosho,”alisema Nshatsi

Aidha alisema NBC kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) wanaendelea kutoa elimu za kifedha kwenye vikundi mbalimbali vya wajasiriamali lengo ikiwa ni kuwawezesha wajasiriamali hao kupata mbinu mbalimbali katika kuendesha biashara zao.

Nshatsi alizidi kueleza kuwa ili kuhakikisha watu wengi wanafikiwa na huduma za kibenki wamerahisisha ufunguaji wa akaunti kupitia akaunti ya NBC Fasta ambapo mteja anahitajika kuwa na kitambulisho kimoja au barua ya mtendaji na kufunguliwa akaunti.

Wakizungumza baadhi ya wananchi waliohudhuria kongamano hilo waliziomba taasisi za kifedha kuendelea kuwapa elimu ya matumizi sahihi ya fedha hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mavuno ya korosho.

“Tunapohudhuria makongamano tunatumaini tutapata elimu mbalimbali lakini watu wa benki waendelee kutoa elimu ya matumizi sahihi ya  fedha ili kuwa endelevu hasa kipindi hiki ambacho wakulima wanauza korosho wasaidiwe wajue baada ya kuuza fedha wanazozipata wanatakiwa kuziendeleza kwenye miradi mingine ya maendeleo,”alisema Asha Chimae

Naye mwanachi mwengine Hansi Chilumba alisema “Wananchi wapo tayari kufanya kazi lakini kinachokosekana ni ujuzi na mtaji, ni vizuri benki kuendelea kutuwezesha hata mmoja mmoja ili kutimiza malengo kwa sababu kila mtu anakuwa na malengo yake lakini tunapounda kikundi inakuwa ngumu kwa wote kukubali wazo la mmoja ili kulifanyia kazi.


Ofisa Huduma Wateja wa Benki ya NBC Tawi la Mtwara, Lulu Mutayoba (katikati), akitoa maelezo kuhusu huduma za kibenki zotolewazo na NBC wakati wa Kongamano la Uwekezaji na Maonyesho ya Biashara Mtwara yakiyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Elimu Mtwara mwishoni mwa wiki. 



NMB yatoa msada kwa shule nne za Kinondoni

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (wa tatu kulia), akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 150 kwa Shule ya Msingi, Mkunguni, Hananasif pamoja na Sekondari ya Hananasif. Kulia kwake ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (kushoto), akipokea sehemu ya msaada wa madawati 150 yaliyotolewa na Benki ya NMB kutoka kwa Meneja wa benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Changolo (kulia), akipokea sehemu ya msaada wa mabati 180 kwa ajili ya Shule ya Msingi Turiani kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Benki ya NMB ilitoa madawati 150 kwa shule ya Msingi Hananasif, Mkunguni pamoja na Shule ya Sekondari Hananasif.
Mwanafunzi wa Darasa la V Shule ya Msingi Mkunguni, Jane Shija, akimshukuru Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam baada ya kukabidhi msaada wa madawati 150.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamekaa katika madawati mapya waliyokabidhiwa na Uongozi wa Benki ya NMB.

***********************************


Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo, ameimwagia sifa Benki ya NMB kwa jinsi inavyojitolea katika miradi ya maendeleo nchini wakati alipokuwa akipokewa msaada wa madawati na mabati kwa shule nne za Kinondoni, uliotolewa na Benki hiyo leo jijini Dar es Salaaam.

NMB kupitia Meneja, Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd walikabidhi msaada wa mabati 180 kwa ajili ya Shule ya Msingi Turiani, Madawati 150 kwa shule za msingi, Hananasif, Mkunguni pamoja na shule ya sekondari Hananasif.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hananasif Sekondari Chongolo alisema, Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Benki hiyo kwani imekuwa ikigusa sekta mahsusi za Elimu, Afya na Miundombinu nchini kote.

“Kwa dhati napenda kutoa shukrani zangu kwa Benki ya NMB kwa jinsi ambavyo imekuwa mstari wa mbele kutoa misaada na kuunga mkono juhudi za Serikari ya Awamu ya tano katika kutatua chanagamoto zinazowakabili watanzania.
“Msaada huu wa mabati na madawati kwa shule hizi unaenda kuongeza chachu ya vijana wetu kupata Elimu katika mazingira rafiki kwa kipindi cha miaka mitano.” amesema Chongolo na kuongeza.

“Binafsi napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa NMB kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakiunga juhudi za Serekali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli kwa kutoa misaada katika maeneo mbali mbali ya nchi.

Chongolo alisema shule hizo zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa miundombinu ya kujifunzia kwa wanafunzi na kuahidi kuwa Serikali inayafanyia kazi mapungufu yaliyopo, kwa kushirikiana na sekta binafsi kuzitatua.

Kwa upande wa Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam Badru Idd, amesema misaada hiyo ni sehemu ya misaada ambayo NMB imepanga kuitoa kwa mwaka ambapo kila mwaka hutenga Bilion 1, huku mwaka huu wameshatoa misaada zaidi ya Milioni 800 ikiwemo hiyo waliyoitoa kwenye shule hizo.

“Kama NMB ni utaratibu wetu wa kurudisha kwa jamii katika kile tunachokipata kila mwaka, jamii ndio tunayoihudumia na ndio wateja wetu. Katika Bilioni 1 tunayoitenga kila mwaka hadi sasa tumeshatoa zaidi ya Milioni 800.

“Leo tuko hapa kwa ajili ya kutoa msaada wa Mabati 180 kwa shule ya Tuliani, Madawati 50 kwa Shule ya Msingi ya Hananasif, Madawati 50 kwa Shule ya Sekondari ya Hananasifu na 50 mengine kwa Shule ya Msingi ya Mkunguni.” alisema Idd.

WAKAZI WA KIGWA KUPATA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWA GHARAMA YA BILIONI 10

$
0
0
SERIKALI imeamua kupeleka maji katika Kata ya Kigwa wilayani Uyui kupitia mradi wa ujenzi wa bomba la maji kutoka Ziwa Victoria kwa gharama isiyopungua shilingi bilioni 10.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa baada ya kusikia kilio cha wakazi wa Kigwa cha tatizo la maji akiwa katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi.

Alisema kuwa eneo hilo hakuna mto wala bwawa na ndio maana katika kata hiyo kuna tatizo kubwa la maji na ndio maana Serikali imesikia kilio chao na kuamua kutatua tatizo la wananchi hayo.
Waziri huyo alisema kama Serikali imeweza kutoa maji kutoka Ziwa Victoria haiwezekani kushindwa kupeleka maji kwa wakazi wa Kigwa ambao wako umbali wa Kilometa 29 kutoka bomba kuu.

Profesa Mbarawa amesema mradi huo huo ukikamilika utasaidia kuwanufaisha vijiji 16 vya Jimbo la Igalula.

Alisema utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza Mwezi Desemba mwaka huu na kuongeza kuwa utekelezaji wa ujenzi wake utawahusisha vijana wa Kigwa,

Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Igalula Mussa Ntimizi aliishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kuchukua maji kutoka mradi wa bomba la Ziwa Victoria na kuwapelekea baadhi ya wakazi wa jimbo hilo ambalo lilikuwa limesaulika katika mradi wa kwanza wa kuleta maji mkoani Tabora.

Alisema hatua hiyo na ile ya kutekeleza mradi wa Tura itasaidi kuwatua ndoo wanawake wa Kigwa kama walivyoaahidi kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM yam waka 2015

Naye Mkazi wa Kigwa Dotto Mrisho alisema kuwa 2010 walijengewa tenki la maji ambapo yalitoka siku alipofika Waziri Mkuu wakati ule Mizengo Pinda lakini baada ya kuondoka hakuna maji tena toka siku ile hadi leo.

Alisema kitendo kile kiliwavunja moyo na kuona kila anapokuja kiongozi anapowaambia kuwa wataletewa maji wanajua kuwa wanadanganywa.

Mrisho alisema kuwa anaamini juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano itawasaidia kuwaondolea kero ya maji katika eneo lao la Kigwa.

Semeni Misana alisema tatizo la maji katika eneo hilo ni tatizo kubwa jambo linalowafanya waamuke usiku sana kutafuta maji ambao wakati mwingine wanakabiliwa na matatizo mengi ikiwemo kukataliwa na wenye visima.

RAIS MAGUFULI AMPA MAAGIZO MAZITO CAG MPYA,AMWAMBIA AKACHAPE KAZI

$
0
0
Na Mwandishi wetu Glou ya Jamii
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam leo, ambao ni  Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu  za serikali, Katibu Tawala, Balozi, Kamishna wa kazi katika ofisi ya Waziri Mkuu, na Majaji 12 wa mahakama kuu pamoja na Mwenyekiti, na makamu mwenyekiti na  Makamishna watano wa Tume ya Haki za binadamu na utawala bora.

Akizungumza na viongozi hao wateule, Rais Magufuli amesema kuwa walioteuliwa wasidhani kuwa hizo ndio nafasi zao moja kwa moja, Pia amewashauri majaji wakafanye kazi kwa haki bila kumuonea Mtu, kwani hukumu hutolewa na Mungu tu, ila kwa hapa duniani tunao Majaji. 

"Kuna watu ukiwateua wanadhani hizo ndio nafasi zao moja kwa moja, wewe (CAG) nilipokutoa toka kuwa Mkurugenzi wa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) kwenda kuwa Katibu Tawala mkoa hukusema neno na ulikuwa mtulivu ,wapo wengine ukiwatoa wanasema maneno maneno, wakati huo unapowateua huwa hawasemi" Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amemuasa Mkaguzi Mkuu wa  Hesabu za Serikali kutokuwaonea watu pale anapopewa maagizo na mihimili  mingine kama Bunge na Mahakama, akatekeleze majukumu yake kwani yeye ni mtumishi na asibishane.

"Najua CAG una 'Qualification' nzuri tu na huwa hatufanyi makosa tunapoteua, form four ulitoka na divison one, form six ukatoka na division one hii ni kuonesha wewe ni kipanga sio kilaza, 'Degree'  ya sheria unayo, ukachukua na masters, umefanya kazi sehemu nyingi tu" Amesema Rais Magufuli.
Rais Dkt John Pombe Magufuli leo Novemba 4,2019 amemuapisha  Charles  Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufuatia uteuzi alioufanya hapo jana. Hafla ya kumuapisha Kichere ambaye kabla ya  uteuzi huo alikuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe pamoja na viongozi wengine, imefanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images