Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AWAONYA WANAOMILIKI SILAHA KUTISHA WENGINE...JESHI LA POLISI KUTUMIKA KUTOA MAFUNZO MATUMIZI YA SILAHA

$
0
0

*Ni baada ya video kusambaa mtandaoni akionesha mtu akitishwa kwa bastola

*Waziri asema hata kiwembe nacho ni silaha,marufuku kumtisha nacho mtu

Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii

BAADA ya kuwepo picha ya video mtandaoni inayoonesha kuna mtu ameshika silaha aina ya bastola akimtisha mtu mwingine, Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema ni kosa kisheria kwa anayemiliki silaha kutaka kuitumia kinyume na sheria na atakayekamatwa atachukuliwa hatua kwani hakuna aliyekuwa juu ya sheria.

Akizungumza leo Novemba 2,2019 jijini Dar es Salaam ,Waziri Lugola amesema ni kosa kisheria kutumia silaha kumtisha mtu au kutaka kumdhuru nayo ." Kwetu sisi wembe,kisu,upinde na aina nyingine ya silaha ni marufuku kumtisha nayo mtu.

"Ipo sheria ya kumiliki silaha, kuitumia na namna ya kuihifadhi.Hivyo kwa wanaomiliki silaha za moto lazima waheshimu sheria ,ni vema Watanzania wote wakawa makini na matumizi ya silaha,'amesema Waziri Lugola.

Hata hivyo amesema kuna mkakati unaandaliwa kupitia Kampuni ya Jeshi la Polisi watatoa mafunzo kwa watu wote wanaomiliki silaha za moto ili kuhakikisha wanazitumia kwa matumizi sahihi na mafunzo hayo yanaweza kutolewa kwa gharama ndogo ya fedha.

"Kila anayemiliki silaha lazima apewe mafunzo ya matumizi bora ya silaha. Hiyo itasaidia kuwakumbusha silaha inahifadhiwa vipi na inatumika vipi.Hata sisi Polisi tumekuwa na utaratibu wa kwenda mafunzo ya mara kwa mara.

"Ambapo huko pia tunakumbushana kuhusu matumizi ya silaha,hivyo lazima na raia ambao wanamiliki silaha wapate mafunzo,"amesema na kuongeza mafunzo hayo yatahusu na ulengaji shabaha.
Hata hivyo amesema sheria ya kumiliki silaha ya moto iko wazi,hivyo yoyote ambaye atakiuka atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria,"amesema Waziri Lugola.

Wakati huo huo amesema katika ziara yake ya kikazi ambayo ameifanya katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ameona kazi zinavyofanyika kwa weledi,umakini  na ujuzi huku akisifu namna askari Polisi wanavyotekeleza majukumu yao ya kila siku na kwamba wanastahili pongezi.

Akiwa katika ziara hiyo amepata nafasi ya kuona kazi zinazofanywa na jeshi hilo katika Kitengo cha kuzuia uhalifu mtandaoni ambapo amesema kuna mambo ambayo wamekubaliana ili kufanikisha utendaji kazi.Hata hivyo amesema Polisi wamefanikiwa Kudhibiti matukio ya uhalifu yakiwemo ya wizi mtandaoni .

DKT TULIA ASHIRIKI TAMASHA LA KUIMARISHA JUMUIYA YA UVCCM MKOANI MBEYA

$
0
0
November 2, 2019 Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson alikuwa Mgeni rasmi katika Tamasha la kuimarisha Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Mbeya lililofanyika katika viwanja vya Sokoine ambapo kupitia taasisi yake ya Tulia Trust ametoa michango mbalimbali kwa makundi tofauti yalishoshiriki katika tamasha hilo.

Miongoni mwa michango hiyo ni pamoja na kituo cha Afya cha Makongolosi Chunya ambacho kimepata Shilingi Milion tano (Tsh 5,000,000/-), Umoja wa Wanawake Tanzania mkoa wa Mbeya waliopewa Computer mpakato yenye thamani ya Milion mbili (Tsh 2,000,000/-), 

Umoja wa vijana CCM mkoa wa Mbeya waliopewa Pikipiki moja yenye thamani ya shilingi Milion mbili na laki mbili (Tsh 2,200,000/-), Murua Group wamepewa Milion mbili (Tsh 2,000,000/-) pamoja na Umoja wa Machifu Igawilo waliopewa jumla ya shilingi Milion moja (Tsh 1,000,000/-) ambapo jumla ya Shilingi Milion kumi na mbili na laki mbili zimetolewa zimetolewa na taasisi hiyo ili kuwawezesha kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.

Katika hotuba yake Dkt. Tulia amesema >>>“Kama mnavyofahamu kwamba mimi sio Mbunge wa sehemu moja hivyo basi hata kwenye Wilaya nyingine huko tumekwishafanya wote kazi na tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha chama chetu lakini kwa leo wenyeji wetu walikuwa ni Mbeya jiji na lazima jumuiya zetu zifanye kazi vizuri na kwa ufanisi.” 



CHUO CHA IFM CHAFANYA KUMBUKIZI CHA MAREHEMU PROFESA JOSHUA DORIYE

$
0
0

*WANATAALUMA WAJADILI MIKAKATI YA KUFIKIA UCHUMI WA KATI WA VIWANDA
Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimefanya  kumbukizi ya aliyekuwa Mkuu wa chuo  hicho  Marehemu Profesa  Joshua Doriye katika kutengamanisha  utumishi wake pamoja taaluma  ya utumishi wake uliotukuka .
Kumbukizi ya Profesa   Doriye  kitaaluma kwa wanafamilia ya IFM katika kuenzi na kufuata utumishi wake katika kufanya kazi sehemu mbalimbali kutokana na umahiri wake katika taaluma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha  Usimamizi wa Fedha Profesa Tadeo Satta amesema kuwa katika kuangalia kumbukizi ya Profesa Doriye  ni pamoja na kuangalia taaluma katika kwenda katika uchumi wa viwanda  kwa kufungua fursa ya wanafunzi wanaohitimu kuingia katika uanzishaji wa viwanda.
Profesa Satta amesema serikali ya awamu ya Tano imechukua wataalam wengi ili kuweza kusaidia  na kushauri serikali kwenda katika mipango yake ya kuipeleka Tanzania kwenda katika uchumi wa kati wenye viwanda.
Amesema  kuwa wanafunzi wanaohitimu  kwa sasa ndio wanaweza kufikisha mipango ya serikali ya uchumi wa viwanda kwa kwenda na mawazo yao katika kufungua viwanda na kuzalisha ajira zingine ambapo serikali itakuwa imepiga hatua ya maendeleo inayoitaka.
Profesa Satta amesema kuwa kama wataalam wanaangalia pamoja na kushirikiana na nchi ambazo zimepiga hatua za kimaendeleo ikwemo India  ambayo imepiga hatua  kutokana na sera walizozianzisha zikazaa maendeleo.
Aidha amesema serikali imekuwa na mikakati mbalimbali ikiwemo na ya kisera katika kuandaa wataalam kuwa wazalishaji wa fursa za ajira kwa kuanzisha viwanda ambavyo vitazalisha ajira kwa watu wengine.

Katika Kumbukizi ya Marehemu Profesa Doriye mwenyekiti aliyeongoza  majadiliano ni Profesa Samuel Wangwe wa Daima Associate Limited  na mwasilishaji mada Profesa Arunaditya  Sahay  wa Taasisi ya Usimamizi wa Teknolojia ya Bibla nchini India.
 Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta akizungumza na waandishi habari katika kumbukizi ya aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho Marrehemu Profesa Joshua Doriye iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 mwasilishaji mada  wa Taasisi ya Usimamizi wa Teknolojia ya Bibla nchini India Profesa Arunaditya  Sahay akitoa mada katika kumbukizi ya aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho Marrehemu Profesa Joshua Doriye iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti majadiliano ni wa Daima Associate Limited  Profesa Samuel Wangwe akiendesha majadiliano katika mada katika kumbukizi ya aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho Marrehemu Profesa Joshua Doriye iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi na IFM na wataalam wakiwa katika mada katika kumbukizi ya aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho Marrehemu Profesa Joshua Doriye iliyofanyika jijini Dar es Salaam

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MWANAMWEMA SHEIN AZINDUA HUDUMA YA UPIMAJI WA AFYA NA KUKABIDHI VIFAA KWA WAZEE WA SEBLENI NA WELEZO ZANZIBAR.

$
0
0
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akihutubia wakati hafla ya Uzinduzi wa Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee wa Nyumba za Wazee Sebleni na Welezo Zanzibar,huduma hiyo imetolewa na Madaktari Bingwa wa Kichina, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Nyumba za Wazee Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja.kushoto Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar.Mhe.Maudline Castico, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Uwezeshaji wa Wazee, Wanawake na Watoto Zanzibar.Bi. Fatma Gharib Bilal, Naibyu Waziri.Mhe.Shadya Mohammed na Mkuu wa Wilaya ya Mjini.Bi.Marine Thomas Joe.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akihutubia wakati hafla ya Uzinduzi wa Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee wa Nyumba za Wazee Sebleni na Welezo Zanzibar,huduma hiyo imetolewa na Madaktari Bingwa wa Kichina, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Nyumba za Wazee Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja.kulia Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar.Bi.Liu Jie, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi na Makamu Mwenyekiti wa UWT.Bi. Thuwaiba Editin Kisasi.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akishuhudia huduma ya Uchunguzi wa Afya kwa Wazee wa Sebleni na Welezo ikitolewa na Daktari Bingwa kutoka Jamuhri ya Watu wa China.Dr.Yang Xiaodong wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa nyumba za Wazee Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja, (kulia kwa Mama Mwanamwema Shein) Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mama Asha Suleiman Iddi.(Picha na Ikulu)
WAZEE wa Nyumba ya Wazee Sebleni na Welezo Zanzibar wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar.Mama Mwanamwema Shein, akihutubia na kuzindua Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee inayotolewa na Madaktari Bingwa wa Kichina katika ukumbi wa Sebleni kwa Wazee.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akikabidhiwa baadhi ya Vifaa vya Afya kwa Ajili hya Nyumba za Wazee za Welezo na Sebleni na Mke wa Mdogo wa Jamuhri ya Watu wa China Anayefanyia Kazi zake Zanzibar.Bi. Liu Jie, wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee wa Nyumba ya Sebleni na Welezo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa makaazi yua Wazee Sebleni Wilaya ya Mjiniu Unguja, kushoto Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar.Mhe. Maudline Castico.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akikabidhiwa baadhi ya Vifaa vya Afya kwa Ajili hya Nyumba za Wazee za Welezo na Sebleni na Mke wa Mdogo wa Jamuhri ya Watu wa China Anayefanyia Kazi zake Zanzibar.Bi. Liu Jie, wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee wa Nyumba ya Sebleni na Welezo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa makaazi yua Wazee Sebleni Wilaya ya Mjiniu Unguja.(Picha na Ikulu).



MKE wa Rais wa Zanzibar, mama Mwanamwema Shein amesema kwa
kuzingatia umuhimu wa wananchi kuwa na afya bora, Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar imeweka kipaumbele katika sekta ya Afya, kwa kuimarisha
huduma mbali mbali .

Mama Mwanamwema amesema hayo katika uzinduzi wa huduma za
upimaji afya kwa wazee wanaoishi katika nyumba za wazee Sebleni na
Welezo, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Sebleni, mjini hapa.

Timu ya madaktari bingwa kutoka Jamuhuri ya watu wa China,
wakishirikiana na madaktari wazalendo wameendesha zoezi la upimaji wa
Afya kwa wazee wanaoishi katika nyumba hizo na kutoa huduma za
uchunguzi, dawa na ushauri.

Alisema ili kufanikisha dhamira hiyo, Serikali imechukuwa hatua mbali
mbali, ikiwa pamoja na kuimarisha miundombinu, kununua vifaa vya kisasa
vya uchunguzi, kuongeza bajeti ya dawa, kuongeza madaktari pamoja na
kusomesha vijana wake ndani na nje ya nchi.

Alisema hivi sasa huduma za za Afya katika hospitali na vituo vya Afya
kote nchini zimeimarika na kutolewa bure , ikiwa ni hatua ya kufanikisha
malengo ya muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, marehemu mzee Abeid
Amani Karume.

Alieleza kuwa hatua ya washirika wa maendeleo, ikiwemo Jamuhuri ya
Watu wa China, kuunga mkono juhudi hizo kwa wataalamu wake kupima
afya za wazee hapa nchini, ni jambo la kutia moyo na linalopasa
kupongezwa.

“Kuwapima afya wazee wetu ni kuendeleza jitihada za kuwaenzi na
kuwahudumia wazee wetu, hakika wazee hawa walifanya kazi ya kutulea
na kuijenga nchi yetu, hii ni kuonyesha tunawathamini, tunawajali na
tunawapenda”, alisema.

Aliwataka wazee hao kuitumia vyema fursa waliyoipata na kutoa
ushirikiano kwa wataalamu hao, ili kufikia malengo yaliokusudiwa.
Aidha, alitowa wito kwa wazazi na walezi kote nchini kusimamia vyema
malezi ya watoto wao kwa kuzingatia maadili mema, utamaduni na silka za
Wazanzibari, ili hatiame waweze kuwa raia wema.

Mama Mwanamwema alisitiza haja ya kuwahimiza watoto kuzingatia
masomo yao ya skuli na madrasa pamoja na kuwafuatilia nyendo zao ili
kuwaepusha na vitendo viovu, udhalilishaji na matumizi ya dawa za
kulevya.

Alitowa shukrani kwa timu hiyo ya madaktari kwa mara ya pili kukubali
kutoa huduma za upimaji wa afya, hatua aliyobainisha inaonyesha mapenzi
makubwa na urafiki uliopo kati ya wananchi wa China na Zanzibar.

Aidha, mama Mwanamwema alitowa ombi maalum kwa Ubalozi mdogo wa
China uliopo Zanzibar akiomba huduma hizo zifikishwa kisiwa Pemba kwa
ili wazee wanaoishi katika nyumba za wazee Limbani, nao waweze
kufaidika.

Altowa pongezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa kutimiza miaka tisa ya uongozi
wake na kubainisha maendeleeo makubwa ya kiuchumi na kijamii
yaliofikiwa.

Mapema, Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha
Suleiman Idd, aliwashukuru madaktri hao kwa moyo wao wa kujitolea na
kuona umuhimu wa kuwaenzi na kuwahudumia wazee wa Zanzibar.
Aidha, aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya Chama cha
Mapinduzi kwa kuwajali na kuwathamini wazee.

Nae, Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, wazee, wanawake na watoto, Moudline
Castico alipongeza juhudi endelevu za Mama Mwanamwema na Mama
Asha Suleiman , ambapo kwa nyakati tofauti wamekuwa mstari wa mbele
kutoa misada mbali mbali ya kijamii kwa wazee na watoto wanaolelewa
katika nyumba za Serikali.

Alisema wazee wamekuwa wakikabiliwa na magonjwa mbali mbali,
ikiwemo sukari, shinikizo la damu, kiharusi, macho, masikio na mengineyo,
hivyo akabainisha hatua ya Ubalozi wa China kuedesha zoezi hilo kuwa ni
ya kupongezwa.

Alimpongeza Mke wa Balozi mdogo wa China Bi Liu Jie kwa juhudi kubwa
alizochukuwa kufanikisha kazi ya kuwapima afya wazee, hatua aliyoeleza
inayonesha imani na mapenzi kwa wazee hao.

Aidha, Mke wa Balozi mdogo wa China aliopo Zanzibar, Liu Jie aliipongeza
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya uongozi wa Dk. Shein kwa
juhudi mbali mbali inazozichukuwa kudumisha amani na kuimarisha
uchumi.

Alisema China itaendelea kuiunga mkoni Zanzibar katika dhamira zake za
kuimarisha uchumi, sambamba na kuendeleza mashirikiano yaliopo kati ya
nchi mbili hizo.

Alisema ushirikiano kati ya China na Zanzibar ni wa kihistoria, hivyo
akaahidi kuendelezwa na kubainisha upimaji wa afya kwa wzee hao ni
hatua inayoonesha heshima na upendo.

Nao, wazee mbali mbali waliopatiwa huduma hizo, wameishukuru Serikali,
Ubalozi mdogo wa China pamoja na Mke wa Rais wa Zanzibar kw
akufanikisha zoezi hilo muhimu.

Wamesema wamefurahishwa kupata fursa hiyo, kwani imemwawezesha
kueleeza changamoto mbali mbali za maradhi yanayowakabili na
kuchunguzwa na hatiame kupata dawa na ushauri wa kitaalamu.
Katika hafla hiyo Mke wa Balozi wa China aliopo nchini Bi Liu Jie aliikabidhi
zawadi na vifaa mbali mbali kwa wazee wanaoishi nyumba za wazee
Welezo na Sebleni.

Nyumba za kutunzia wazee ziliopo Welezo na Sebleni zina jumla ya
wazee 71 wa kike na kiume, ambao hupatiwa huduma zote muhimu,
ikiwemo Chakula, malazi, matibabu na Serikali.

Dkt. Gwajima Aweka reheni Vyeo vya Watumishi Makore Dodoma

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Dkt. Dorthy Gwajima, akizungumza katika zoezi la ufatiliaji kwenye kituo cha Afya Makore.
Mmoja wa Wafamsia katika kituo cha Afya Makore, akisajili dawa kwenye kitabu cha kupokelea Ledger.





Wananchi walikutwa katika kituo cha Afya makore wakipata huduma siku ya tareh 02,Novemba, 2019

Watumishi wa Kituo cha Afya Makore wakiwa wanapewa somo wakati wa Ziara hiyo na Naibu Katibu Mkuu.

Eneo la Stoo yakutunzia dawa katika kituo cha Afya Makore.

Mtekinolojia Maabara kama alivyokutwa wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu.


Godfrey Mahundi Msimamizi wa Maabara katika kituo cha Afya Makore akitoa maelezo mbele ya naibu katibu Mkuu wakati wa ziara hiyo ya kikazi. 

*********************************

Na. Atley Kuni- OR-TAMISEMI

Baadhi ya watumishi wa Afya katika Kituo cha Afya Makore mkoani Dodoma wamejikuta kwenye wakati mgumu mara baada ya kubainika kufanya kazi kinyume na taratibu zinavyo elekeza. Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Daktari Dorothy Gwajima amesema, kutokana na kukithiri kwa utendaji wa mazoea kwa baadhi ya watumishi wanaopima upepo sasa kaguzi zote zitaanza kufanyika kwa mwelekeo wa kutathmini jinsi gani kila mtumishi wa kada husika ametekeleza majukumu yake kama yalivyoelekezwa kwenye muundo wake wa utumishi.

Aidha, amewaeleza watumishi hao kuwa, inaonekana maboresho yanayoonekana katika kituo hicho yakawa yanafanywa na watumishi wachache wanaofidia utegaji wa wengi hivyo, kutokana na mwenendo huo sasa hatasita kuwashtaki wazembe wote kwa Katibu Mkuu utumishi ili hii habari ya kupandishana vyeo iende sambamba na chujio makini la ufanisi wa kila mtumishi na kiongozi mahala pa kazi.

Hatua hiyo imekuja kufuatia ufuatiliaji endelevu unaofanywa na Naibu Katibu Mkuu na jopo la wataalamu kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI katika kituo hicho na vingine nchini ambapo, kituo cha afya Makore ni mojawapo ya vituo vinavyojengewa uwezo viwe vya mfano katika mabadiliko ya mifumo ya uwajibikaji mahala pa kazi. Mwelekeo huu ni utekelezaji wa mojawapoa ya Azimio la Kikao cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kilichofanyika Agosti, 2019 kuwa, kila halmashauri iteue vituo 4 vya mfano.

“Sitasita kumshauri Katibu Mkuu Utumishi asiridhie baadhi ya watumishi miongoni mwa 80 mnaowaombea wapandishwe vyeo iwapo nitabaini ufanisi wao hautoshi kupitia kaguzi tunazofanya. Nitamwambia Katibu Mkuu hawa watumishi hawastahili kupanda vyeo kwakuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo na hapa msisingizie eti mko wachache wakati idadi yenu ni mara mbili ya wanaotakiwa hapa,” alisema Gwajima na kusisitiza kuwa,“haiwezekani zaidi ya miezi mitatu wataalamu wa kitengo cha dawa eti hawajahuisha taarifa za dawa kwenye kitabu husika (Ledger) yaani mnajifanyia fanyia tuu bila utaratibu halafu mnasema dawa hazitoshi huku mmeotesha vichaka vyenye utata wa kujua wapi mmezitumia?” alihoji Gwajima.

Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu pia, alifanya uhakiki wa hadi ujazo wa kila kitendanishi cha maabara kwamba kilitakiwa kupima sampuli ngapi na mwisho kimepima ngapi ambapo, alibaini wataalamu wa maabara wamepima sampuli nyingi zaidi kuliko walizotakiwa kupima huku wakiwa hawana kumbukumbu za kiofisi kuhusu wapi walikopata vitendanishi vya ziada, ‘inakuwaje ulitakiwa kwa kitendanishi hiki upime sampuli 50 badala yake umepima 350”? Gwajima alihoji.

Naye mtaalamu wa Maabara katika kituo hicho Ndugu Godfrey Mahundi hakuwa na majibu yakina juu ya wapi hasa alitoa ziada hiyo ya vitendanishi na kama ipo sehemu alikotoa kwa nini hakuna rekodi ya aliyempa wala yeye kukiri mapokezi.

Dkt. Gwajima alisema, kwa kawaida taratibu za uchukuaji dawa lazima ziwe zinaandikishwa kutoka eneo moja hadi lingine yaani kutoka hifadhi kuu, hifadhi ya kati, hifadhi ndogo mpaka zinapomfikia mgonjwa na hata kama amepewa toka kwenye kituo kingine lazima kuwe na rekodi za aliyetoa na aliyepokea.

“Hapa Kituo cha Afya Makore baadhi ya watumishi wameelewa somo hasa eneo la huduma za kitabibu na kiuguzi ila nyie watu wa maabara na dawa ndiyo bado mnapima upepo mnajifanyia mambo kienyeji kwa kutoandika kumbukumbu za matumizi ya raslimali za dawa na vitendanishi na nani katumia, nasema nyie pamoja na wengine wote nchi nzima wanaofanya mambo kama yenu ambayo, yanayoruhusu kushamiri kwa vichaka vya matumizi mabaya ya raslimali za vituo sasa wakati umefika wa kuamua kurudi kwenye mstari ama mtausikia tu utumishi wa umma kwenye redio. Aliendelea kusisitiza Katibu Mkuu.

Amesema kituo hicho ni cha mfano na watakaofanya hapa lazima wawe wa mfano na si vinginevyo, huwezi kuwa mtumishi wa kituo cha mfano huku wakitoa fursa ya majizi kujificha kwenye kazi zao. Ameongeza kuwa ijulikane kuwa hizo ni salamu zake kwa vituo vyote vya afya nchini.

Katika hatua nyingine Watumishi hao walionesha kutambua uzembe walioufanya na kukiri kuzembea katika utendaji wao huku wakiomba msamaha na kuahidi kubadilika.

Akikiri kufanya uzembe Mfamasia wa Jiji la Dodoma George Hondi, kwa niaba ya watumishi wengine, alisema wanaona fedheha na aibu kwani yote yaliyobainishwa na Naibu Katibu Mkuu hakuna hata moja la kusingiziwa wala kuonewa.

“Ni kweli hatujatekeleza na kusimamia majukumu yetu na hili ni kosa na sisi tuseme tu na kunaahidi kubadilika” alisema Hondi.

Kwa mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Namba 1 wa Mwaka 2009 unaoeleza juu ya Miundo ya Utumishi kwa Kada za Afya chini ya Wizara ya Afya yapo mambo mengi ambayo yameendelea kugundulika kupitia ziara hii na zingine za Naibu Katibu Mkuu na timu yake na yanayotokana na baadhi ya watumishi kujifanyia kazi kienyeji mfano, Mfamasia Daraja la Pili anayo majukumu yake ikiwemo kutunza kumbukumbu za dawa na vifaa tiba na kutekeleza maelekezo ya wizara kuhusu ufanisi wa Kamati ya Dawa kwenye kituo husika lakini wengi hawafanyi na sababu hawana lakini wanadai wapandishwe vyeo Hii haiwezekani” amesema Dkt Gwajima. .

Chini ya OR-TAMISEMI imeundwa timu rasmi ya kuwa inafanya ukaguzi wa utekelezaji wa majukumu ya kila mmoja tutajua huko huko wapi hawatoshi na wapi wako idadi kubwa lakini hawana tija.

Dkt. Gwajima amewataka Makatibu wa Afya kutokuwa makarani wa kuorodhesha tu majina ya watu kupanda vyeo kisa mtumishi kaajiriwa siku nyingi bali wapime ufanisi ili kumtendea haki anayejituma na mzembe naye apate haki yake ya kutopandishwa cheo au kushushwa. Amesema wataimarisha mifumo na taratibu za kujipima na kuwapima watumishi ili haki itendeke haraka kwa wale wanaojituma na wasiojituma pia wapate haki yao mapema tu kila mtu abebe mzigo wake.

Mapema juma lililopita, Naibu Katibu Mkuu akifungua Kikao cha Wafamasia wa Mikoa mjini Dodoma, aliwarushia lawama wataalam wa Afya hususani kada ya Famasia kwamba, wizi wa dawa unaoshamiri unachangiwa na usimamizi mbovu eneo lao kiasi kwamba dawa hizo zinapotea bila taarifa kwa kuwa hawazingatii au kwa makusudi wanafanya kazi huku wakitoa fursa nzuri kwa wezi na wadokozi kutekeleza azma yao na hii ni kusaliti juhudi za Serikali za kuongeza bajeti ya dawa na kufikia bilioni 269, hivyo akaapa kupambana nao kwa kuomba nguvu za wananchi kuwafichua wote watakaobainika kuhujumu jitihada hizo.

Ofisi ya Rais TAMISEMI, kwa mujibu Muongozo wa sasa ndio msimamizi Mkuu wa Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati kote nchini.

Glitters Car wash washerehekea mwaka moja wa kazi

$
0
0
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kuosha Magari ya Glitters Car Grooming Bays ya jijini Dar es Salaam wakishangilia wakati wa kutoa huduma ya uoshaji magari bure leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo. 
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Glitters Abdallah Motto amesema changamoto kubwa wanazozipitia ni kukimbiwa na wafanya kazi ambao kabla huwapa elimu ya namna ya uoshaji magari lakini baadaye hukimbia.

Aidha katika sherehe hiyo kulikua na utoaji wa elimu kwa namna ya uendeshaji magari kwa kuzingatia usalama wa muendeshaji na abiria wawapo barabarani.

UTATUZI MGOGORO WA ARDHI MBEYA WAFIKIA PAZURI

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akikagua ramani wakati wa kutatua mgogoro wa Ardhi baina ya Kijiji cha Nanyala na kiwanda cha Saruji cha Mbeya, Waziri Lukuvi aliambatana na Ma naibu waziri wa Wizara za Tamisemi, Madini na Viwanda na Biashara.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiambatana na Ma naibu waziri wa Wizara za Tamisemi, Madini na Viwanda na Biashara kukagua eneo lenye Mgogoro kati ya Kijiji cha Nanyala Wilaya ya Mbozi na Kiwanda cha Saruji cha Mbeya.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi eneo linalotumika kuchimba madini ya Marumaru ambalo pia liko kwenye mgogoro wa Ardhi baina yao na kiwanda cha Saruji cha Mbeya, Waziri Lukuvi aliambatana na Ma naibu waziri wa Wizara za Tamisemi, Madini na Viwanda na Biashara.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya(kushoto), Naibu Waziri Madini Stanlaus Nyongo na Naibu Waziri OR TAMISEMI Josephat Kandege wakisikiliza maelezo kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya Kiwanda cha Saruji cha Mbeya na Kijiji cha Nanyala cha Wilaya ya Mbozi.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela (aliyevaa kofia), akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kutatua mgogoro wa ardhi kati ya kiwanda cha Saruji cha Mbeya na Kijiji cha Nanyala.

***********************************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliagiza Wizara za Ardhi, Madini, Tamisemi na Viwanda zishughulikie mgogoro wa Ardhi baina ya Kijiji cha Nanyala na kiwanda cha Saruji cha Mbeya.

Mgogoro unahusisha ekari 2315 ambapo ekari 1475 zipo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe na ekari 840 ziko wilaya ya Mbeya.Leo tumekuja kama alivyoagizwa kujionea hali halisi ikiwa lengo letu ni kuumaliza mgogoro huo na tutafuata sheria taratibu na kanuni zote katika kutatua mgogoro huu.

Kufikia Jumatatu Kiwanda cha Saruji kiondoe kesi tatu zilizoko mahakamani baina ya kiwanda na wana kijiji cha Nanyala kama alivyo agiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, hii si hiyari, haiwezekani Mkuu wa Nchi anaagiza jambo halafu kuna mtu anajivuta kutekeleza.

Utoaji wa leseni za madini katika eneo lenye mgogoro usitishwe, Kijiji cha Nanyala, Wilaya za Mbozi na Mbeya zisitishe utoaji wa hati za kimila katika eneo lenye mgogoro.

Wakulima na wafugaji ambao wanalima na kufuga katika eneo hilo, mgogoro huu hauna maslahi nao hivyo wasizuiliwe kuendelea na shughuli za kilimo na ufugaji.Wachimbaji wadogo wadogo wa chokaa wanaofanya shughuli zao kwa msimu katika eneo lenye mgogoro wasizuiliwe waendelee kufanya kazi zao.

Naibu Waziri Madini Stanslaus Nyongo

Wataalamu waangalie namna ya kubalidisha Sheria ya Service Levy ili halmashauri za Mbeya na Mbozi waweze kufaidika kwa pamoja na sio halmashauri moja kufaidika huku nyingine ikipunjwa.

Kiwanda cha Saruji cha Mbeya kama wanataka kutunza eneo kwa ajili ya matumizi ya baadaye waangalie namna bora inayotambulika kisheria na sio kukwepa gharama kwa kutofuata taratibu na sheria.

Naibu Waziri OR TAMISEMI Josephat Kandenge

Halmashauri ambayo haikupata service levy na ilistahili kupata ilipwe kwakuwa tusirekebishe ya mbele bila kuangalia stahiki zilizopita za Halmashauri hizi.Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya.

Wizara ya Viwanda na Biashara ingependa kuona mgogoro huu unaisha kwakuwa kiwanda cha Saruji na vingine vilivyopo katika eneo hilo vina mchango katika maendeleo ya taifa.Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila

Migogoro inapoendelea sana lazima kuna upande unakuwa hauna uelewa hivyo wataalamu watusaidie katika hilo pia tusiingie sana katika mgogoro wa mapato kuwa yaende kwa nani isipokuwa tujielekeze kuumaliza mgogoro huo.Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela

Mkoa wa Songwe tunaomba kesi zifutwe ili wananchi waendelee kufanya shughuli zao kwa uhuru.Mkoa wa Songwe tunataka wawekezaji na tunawakaribisha waje kwakuwa sisi tuna mali ghafi za kutosha ila tu wajue kuwa lazima sheria na taratibu zifuatwe.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 3,2019


MWONGOZO WA UWEKEZAJI WA MKOA WA MWATARA WAZINDULIWA

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mtwara

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amezindua Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Mtwara (MIG) katika Kongamano la Uwekezaji na Maonyesho ya Biashara lililofanyika kwenye viwanja vya Chuo Cha Ualimu Mtwara.

Mwongozo huo umetayarishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Mkoa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

“Kuja kwenu Mtwara leo hii hamjapoteza nauli na muda wenu, mmekuja Mtwara mahali sahihi kwa uwekezaji na mtatumia nafasi ya leo kusikia nini kimeandaliwa kwa ajili ya kuwaambia fursa zipi zinapatikana mkoani Mtwara.” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa

Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuiondoa Tanzania kwenye uchumi wa chini kwenda Uchumi wa Kati na hakuna njia nyingine isipokuwa ni kuvutia uwekezaji, Serikali inakaribisha wawekezaji kuwekeza hapa nchini iwe ni Mtanzania au mgeni kutoka nje ya nchi atapokelewa ili aweze kuwekeza hapa nchini. 

“Wakati nikizungumza na wakuu wa mikoa Juni 18, 2018 jijini Dodoma nilitoa maelekezo na dira ya kila mkoa kupata wawekezaji, niliagiza kila mkoa lazima ujipange kuhakikisha unatangaza fursa zilizopo katika mkoa.” Alifafanua Waziri Mkuu. 

Mheshimiwa Majaliwa alisisitiza Mikoa ambayo bado haijaandaa miongozo ya uwekezaji ifanye hivyo mara moja kabla mwaka huu haujaisha. Pia aliwaonya watumishi wanaokuwa vikwazo kwa wawekezaji waache mara moja na wanaobainika wachukuliwe hatua stahiki.

“Niipongeze Taasisi ya ESRF chini ya Mkurugenzi wake Dkt. Tausi Kida imefanya kazi kubwa na nzuri, baada ya kufanya utafiti imetoa tathmini ya nini kifanyike, wapi tufanye nini ili tuweze kufanikisha uwekezaji hapa nchini” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa na kuongeza….Kila ninapokwenda kuzindua Miongozo ya Uwekezaji nimekuwa nikukutana na ESRF ikiongozwa na Dkt. Tausi Kida, hongera sana kwa kazi nzuri mnayofanya.” Alipongeza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu pia ameipongeza UNDP kwa kufanya kazi kwa pamoja na Serikali na kuahidi kuwa Serikali itaunga mkono shughuli za UNDP ambazo Serikali ya awamu ya Tano na zile zilizotangulia daima zimekuwa zikifanya kazi kwa pamoja na UNDP na zinatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hii ya kimataifa.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki. Wakati akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia, Mhe. Kairuki alieleza hatua ambazo Serikali imechukua kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kupelekea Tanzania kupanda kutoka nafasi ya 144 hadi 141 kwenye urahisi wa kufanya biashara duniani. 

Mawaziri wengine waliohudguria na kutoa neno ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga.

Wakati akitoa salaamu, Mwenyeji wa Mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa aliwakaribisha wageni waalikwa na kuelezea jinsi Mkoa ulivyojipanga kuwapokea na kuwasaidia wawekezaji. Pia alitoa fursa kwa Wakuu wa Mikoa jirani walihudhuria halfla hiyo ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Mtwara kutoa neno. Waliohudhuria ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Chrintina Mdema na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bi.Christine Musisi alisema UNDP itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi. Alisema UNDP itaendelea kusaidiana na Mikoa katika utekelezaji wa miongozo hii kwa kutoa ushauri wa kitaalam na rasilimali fedha panapohitajika.

Awali akiwasilisha Muhtasari wa Fursa za Uwekezaji katika Mkoa wa Mtwara katika Kongamano la Uwekezaji, Mtafiti Mkuu Mshiriki kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Oswald Mashindano alisema ESRF ilifanya utafiti kwenye halmashauri zote za Mkoa wa Mtwara na utafiti huo ulibaini uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji. Dkt. Mashindano alitaja timu ya wataalam kutoka ESRF walioshiriki kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji ikijumuisha Prof. Haidari Amani, Bi. Margareth Nzuki, Bw. Mussa Mayala Martine, na Bw. James Kasindi.

Dkt. Mashindano alitaja fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo zimepewa kipaumbele na mkoa. Fursa hizi ziko katika makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwekezaaji katika kilimo hasa korosho, kilimo cha umwagiliaji wa mpunga na miwa, ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji wa mpunga na mazao ya bustani; uwekezaji katika mifugo hasa ranchi na unenepeshaji wa mifugo; uwekezaji katika uvuvi hasa uvuvi ndani ya bahari kwa kutumia nyenzo na teknolojia za kisasa pamoja na ufugaji wa samaki; uwekezaji katika viwanda hasa Kuchakata Korosho na mazao mengine kama mhogo, nazi, choroko, mbogamboga na matnda, kuchakata na kufungasha chimvi, Chakula cha Mifugo, Kuchakata Samaki, Kiwanda cha Kutengeneza Maji ya Chupa nk.

Fursa za uwekezaji katika eneo la miundombinu zilijumuisha ujenzi wa jengo kwa ajili ya matengenezo na maegesho ya ndege, stendi za kisasa, ujenzi wa kituo cha michezo ikijumuisha uwanja wa mpira, masoko ya kisasa nk. Aidha Dkt. Mashindano alitaja makundi mengine ya fursa za uwekezaji kuwa ni pamoja na uwekezaji katika utalii akilenga uwekezaji kwenye fukwe, michezo ya baharini, ujenzi wa hoteli, majumba ya starehe, kambi za watalii, kuendeleza maeneo ya kihistoria nk. Pia zilibainishwa fursa za uwekezaji katika huduma za kijamii zikijumuisha afya na elimu. Kwa upande wa afya kuna fursa ya ujenzi wa hospitali na kiwanda cha kutengeneza maji ya wagonjwa na vifaa tiba. Kwa upande wa elimu alitaha fursa ya kuendesha chuo maalum cha ujuzi pamoja na shule binafsi za kisasa.

Baada ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji washiriki walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uwekezaji Mkoani Mtwara.
Maonesho ya biashara na Uwekezaji yanafikia kilele leo Novemba 3, 2019.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (katikati), akionyesha nakala za Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Mtwara (MIG), baada ya kuuzindua kwenye Chuo Cha Ualimu Mtwara Novemba 1, 2019. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki (wapili kulia), Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bi. Christine Msisi (wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Gelasius Byakanwa (wakwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida. 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (watatu kushoto), akikata utepe, kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara (MIG), kwenye Chuo Cha Ualimu Mtwara Novemba 1, 2019. Wanaoshuhudia ni kutoka kulia ni Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bi. Christine Msisi na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Gelasius Byakanwa. 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki (katikati) akishuhudia, mara baada ya Waziri Mkuu kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara Novemba 1, 2019.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki (katikati) akishuhudia, mara baada ya Waziri Mkuu kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara Novemba 1, 2019.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia kongamano hilo na kisha kuzindua Mwongozo huo Novemba 1, 2019.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara (MIG) Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bi. Christine Msisi akitoa hotuba yake.
Viongozi waandamizi wa ESRF walioshiriki katika utafiti huo kutoka kushoto,Bw. Mussa Mayala Martine, Dkt. Oswald Mashindano na Bi. Margareth Nzuki.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara (MIG), Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga huku Mhe. Kairuki (katikati) akishuhudia. 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara (MIG), Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa huku Mhe. Kairuki (katikati) akishuhudia. 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara (MIG) Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bi. Christine Msisi. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angela Kairuki (wapili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida. Mwongozo huo umetayarishwa na (ESRF) kwa kushirikiana na Mkoa wa Mtwara chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Zaidi Ya Shilingi Bilioni Mbili Kukarabati Machinjio

$
0
0
Na, Editha Edward-Tabora .

Halmashauri ya Manispaa ya Tabora inatarajia Kutumia zaidi ya Shilingi bilioni mbili kufanya ukarabati mkubwa wa machinjio ya mifugo mjini Tabora baada ya kukamilisha nyaraka za upembuzi yakinifu kwa mwaka wa fedha 2019/2020 

Wajumbe wa kamati ya fedha halmashauri ya manispaa ya Tabora wametembelea machinjio hayo ya mkoa wa Tabora na kuweza kujionea kile ambacho tayari walisomewa na wataalam kwenye nyaraka za upembuzi yakinifu ya kuomba fedha hivyo wa ajili ya ukarabati mkubwa wa machinjio hayo

Nae Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Joseph Kashushula amewaeleza Wajumbe wa kamati hiyo ya fedha hatua za mwanzo zilizotumika za kufanya ukarabati mdogo wa machinjio hiyo kuwa uligharimu zaidi ya shilingi milioni kumi na tano huku akisema mapato yatokanayo na tozo ya machinjio hiyo ambayo kwa siku inachinja kati ya ng'ombe sitini na tano hadi Sabini

"Tuna mipango mizuri ya kuhakikisha kwamba machinjio hii tunaikarabati na inakuwa ni ya kusasa zaidi tunategemea kupata pesa kutoka central government au kama itakuwa Siyo huko tutaweza kupata fedha kwa wafadhili na tayari maandiko tumeshaandika"Amesema Kashushula

Kwa upande wake Naibu meya wa manispaa ya Tabora Hahaha Muhamali amesisitiza umuhimu wa chanzo hicho cha mapato ya ndani ya halmashauri "sasa hivi tunatengeneza hizi kuta tunazowekea tailizi lakini hizi sakafu Siyo salama kiafya kwa Sababu nyama zinakaa chini haziko katika hali nzuri mimi nadhani tutajadili kwenye kikao chetu tutajadili tuone ni jinsi gani tuweze kufanyia ukarabati na hii sakafu"Amesema Muhamali 

Aidha machinjio hiyo ya manispaa ya Tabora imekuwa ikiingiza mapato ya wastani wa Shilingi milioni kumi na laki tano kwa mwezi kwa tozo ya uchinjaji wa ng'ombe pekee ukiachilia mbali na makusanyo ya tozo ya ushuru wa damu baada ya ng'ombe kuchinjwa.
Muonekano wa machinjio kwa ndani ambayo hapo awali yalikarabatiwa kwa kiasi cha shilingi milioni kumi na tano. 
Wajumbe wa kamati ha fedha halmashauri ya manispaa ya Tabora wakitembelea machinjio hayo ya mkoa wa Tabora. 
Muonekano wa machinjio kwa ndani.
Wajumbe wa kamati ya fedha halmashauri ya manispaa ya Tabora wakiwa ndani ya machinjio hayo wakielekezwa jambo

Rais Magufuli aagiza kufanyika mabadiliko Halmashauri ya Mji Ifakara na Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero

WAFANYAKAZI ZAIDI YA 100 WAMLILIA RAIS MAGUFULI ,WAMUOMBA AWASAIDIE ILI WALIPWE STAHIKI ZAO

$
0
0
Na Woinde Shizza,michuzi Tv,Arusha

Wafanyakazi zaidi ya 100 wakiwemo 22 waliofukuzwa kazi hivi karibuni bila kulipwa stahiki zao, wamemwomba Rais John Magufuli kusikia kilio chao cha muda mrefu baada ya kukosa msaada kwa uongozi wa mkoa kutokana na mkurugenzi wa ya hotel ya Naura Springs na Impala,Randy Mrema kudaiwa kuwaweka mfukoni

Wakiongea kwa masikitiko baadhi ya wafanyakazi hao waliodai kufanyakazi kwa zaidi ya miaka kumi,wamesema kuwa uongozi wa hotel hizo uliwaandikia barua ya ukomo wa ajira Ifikapo oktoba 31 mwaka huu kwa kile kilichodaiwa ni kampuni kushindwa kujiendesha .

Kutokana na hatua hiyo walipaswa kuandaa malipo yetu ikiwemo mishahara ya miezi minne tunayoidai ,makato ya NSSF na malipo ya kusitisha ajira kuliko walivyofanya kwa sasa na kusababisha familia zetu kuteseka kwa njaa"

Wakiongea kwa niaba ya wenzao baadhi ya wafanyakazi waliofukuzwa kazi, Grayson Mwanga na Kisuno Bernard wamedai kwamba uongozi wa hotel hizo umeshindwa kuwalipa stahiki zao na wamekuwa wakiwadharau wafanyakazi pindi wanapoulizia malipo ya mishahara yao.

"Hapa tulipo hatujalipwa mishahara ya miezi minne ,makato ya mfuko wa hifadhi nssf ambayo wamekuwa wakikatwa kila mwezi lakini mwajiri wao hapeleki kwenye mfuko huo jambo ambalo tunataka rais Magufuli aingilie kati" Wamesema Mwanga.

Wamemtuhumu mkurugenzi wa Hotel hizo,Randy Mrema kuwa na mahusiano na viongozi wote wa mkoa wa Arusha ,wakiwemo wa idara ya kazi jambo ambalo wamekosa mtu wa kusikiliza kilio chao na hivyo kumtaka rais Magufuli,TAKUKURU idara ya usalama,waziri mwenye dhamana, kuingilia kati kuchunguza jambo hilo.

"Awali Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqaro alitusaidia sana na kuwezesha kulipwa kwa mishahara ya nyuma lakini naye kwa sasa wamejiweka kando na suala letu hali ambayo tumekosa mtu sahihi wa kutusaidia" Alisema Mwanga

Akiongea sakata hilo afisa wa Idara ya kazi Mkoa wa Arusha, Wilfred Mdumi anayedaiwa kuwekwa mfukoni na mkurugenzi wa hotel za Impala na Naura,Randy Mrema amekanusha kurubuniwa kwa kitita cha fedha na kigogo huyo ili apindishe haki ya walalamikaji,ila amesema kuwa suala hilo analishughulikia kwa umakini mkubwa kwa mujibu wa Sheria za kazi.

" Tumefanya mazungumzo na uongozi wa hotel hiyo na kutoa maelekezo lakini kumekuwepo na suala la utovu wa nidhamu kwa wamiliki wa hotel hizo kukiuka makubaliano ya wazi"Amesema Mdumi

"Ofisi yangu imewashauri wafanyakazi hao pamoja na wale walioachishwa kazi kufungua kesi mahakamani kulalamikia kuachishwa kazi bila kupewa stahiki zao ikiwemo kukatwa makato ya mfuko wa hifadhi wa NSSF bila kupelekwa katika mfuko huo"amesema Mdumi

Vyombo Vya Habari waliomtafuta Mkurugenzi wa hotel hizo RANDY MREMA kupata ufafanuzi wa jambo hilo ,mkurugenzi huyo hakutoa ushirikiano badala yake alitimua mbio na kuingia kwenye gari lake la kifahari na kutokomea kusikojulikana na kuwaacha waandishi waliokuwa wamejazana katika hotel ya Impala wakishangaa

Amesema mpaka sasa wamepeleka maombi Mahakamni kuomba itoe amri kukamatwa kwa Mali za kampuni hizo ili iweze kulipa mishahara baada ya kushindwa kutekeleza Maelekezo ya Idaya ya kazi mpaka sasa kampuni hizo zina kabiliwa na kesi namba 83 / 2019/ kwa Naura Spring na Impala kesi namba 84 / 2019 kwa impala Hotel 

Hotel za Impala na Naura Springs zimeachwa na marehemu Faustine Mrema aliyefariki mwaka 2017 na kukabidhi Mali hizo zisimamiwe na mtoto wake mkubwa aitwaye Joan Mrema lakini baada ya msiba wa marehemu kumalizika dada wa marehemu pamoja na mama yake na Randy walifanya mapinduzi matakatifu(Kupindua Meza) na kujimilikisha hoteli hizo.
  Afisa wa Idara ya kazi Mkoa wa Arusha, Wilfred Mdumi  akiwa ofisini kwake 

 baadhi ya wafanyakazi wakionyesha barua walizosimamishiwa nazo kazi

WAITARA AWAONYA WATAKAOFANYA UDANGANYIFU MITIHANI YA KIDATO CHA NNE

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imetoa onyo kwa wale wote watakaojaribu kufanya vitendo vya udanganyifu kwenye mitihani ya kidato cha nne inayoanza kesho.

Onyo hilo limetolewa leo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Mwita Waitara alipokua akitoa salami zake za heri kwa wanafunzi zaidi ya Laki Nne wanaotarajiwa kumaliza mitihani yao ya kidato cha nne.

Mhe Waitara amewapongeza wanafunzi hao kwa uvumilivu wao kwa kipindi chote walichokua shuleni na kuwataka kufanya vizuri mitihani hiyo ili kumpa sifa Rais Dk John Magufuli kwa kutoa elimu bila malipo.

Amesema kumekuepo na vitendo vya udanganyifu kwenye vipindi vya mitihani ya Kitaifa na kuwataka wazazi na wanafunzi kutodanganyika na kushiriki vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na sheria.

" Niwapongeze Wanafunzi wote wanaotarajia kufanya mitihani hii, Sisi kama Serikali tunawatakia kila la heri, wakamtangulize Mwenyezi Mungu na kuzingatia yale yote ambayo wamefundishwa kwa miaka minne.

Lakini pia niwasihi Walimu, Wazazi na Wanafunzi kutojaribu kushiriki vitendo hivi kwa kununua mitihani kutoka kwa watu ambao wamekua wakiwalaghai kwamba wanauza mitihani. Kufanya hivyo ni kujihatarisha kwani Serikali iko makini na tukiwabaini tutawafutia mitihani,* Amesema Mhe Waitara.

Amesema tayari wameshatoa maelekezo kwa vyombo vya usalama kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaokutwa wakifanya udanganyifu huo kwani hauna tofauti yoyote na rushwa na wizi.

Waitara pia amezungumzia mafanikio ya elimu bure ambapo wanafunzi hawa wa kidato cha nne ndio zao la kwanza la elimu bure na kusema Serikali itaendelea kufanya maboresho katika sekta ya elimu na kutatua changamoto zote ambazo zipo ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira bora ya wanafunzi pamoja na walimu.

" Toka Rais atangaze elimu bila malipo hawa ndio wanafunzi wa kwanza ambao wanamaliza wakiwa wamesoma miaka minne bila malipo. Kwetu sisi ni mafanikio makubwa kuona ndoto ya Rais Magufuli ya kupambana na ujinga ikifanikiwa kwa kasi. 

Serikali imekua ikitenga zaidi ya Bilioni 23 kila mwezi kwa ajili ya elimu bure, lakini pia kuonesha mafanikio yao idadi ya wanafunzi wanaomaliza mwaka huu ni kubwa kulinganisha na ya mwaka jana. Mwaka huu wanafunzi waliosajiliwa na wanatarajiwa kufanya mitihani ni 485,000 ambapo mwaka jana waliofanya mitihani ni 427,000," Amesema Mhe Waitara.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Mwita Waitara akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma kuhusiana na mitihani ya kidato cha nne itakayoanza kesho.

BREAKING NEWZZZZZ: RAIS MAGUFULI ATEUA CAG MPYA

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli leo , Novemba 03, 2019 amemteua Ndugu Charles Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akichukua nafasi ya Prof Mussa Assad

Prof. Assad aliteuliwa na Rais Mstaafu, Dkt.Jakaya Kikwete wakati wa utawala wake na kuapishwa Novemba 2014

Kabla ya uteuzi wa leo, Kichere alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Njombe na awali alishawahi kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

TAARIFA MUHIMU KWA UMMA KUHUISHA TAARIFA ZA MAKAMPUNI NA MAJINA YA BIASHARA NDANI YA SIKU 90


TZUK DIASPORA INAWALETEA SHEREHE ZA KUAZIMISHA MIAKA 58 YA UHURU

Mwenyekiti wa Tahliso afanya Kikao Kazi na Balozi wa Tanzania Nchini China

$
0
0
Mwenyekiti wa Tahliso Ndg.Peter Niboye akiwa na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania Nchini China Mh.Balozi Mbelwa Kairuki

Beijing China

Mwenyekiti wa Tahliso Ndg.Peter Niboye amefanya leo kikao cha kazi na Balozi wa Tanzania Nchini China Mh.Balozi Mbelwa Kairuki na kujadiliana kwa pamoja jinsi ya Kuhakikisha Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu Nchini Tanzania na Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma China wanaweza wakanufaikaje na Fursa zilizopo Nchi ya China na Kuzileta Tanzania na hii yote ni kuhakikisha Vijana wa Tanzania tunaisaidia Serikali ya Awamu ya Tano Kutekeleza kwa pamoja Sera ya Viwanda kwa Vitendo.

Lakini Pia kwenye Kikao hicho Balozi ameahidi Ushirikiano wa Kutosha kwa Tahliso na kuahidi kuendelea kuhakikisha Fursa za Scholarships kuendelea kupatikana na kama Tahliso tuendelee kusaidia kuzitangaza Fursa hizi ili Watanzania wengi wapate fursa ya kusoma lakini Pia Balozi ameahidi kuendelea kushirikiana na Jumuiya za Wanafanzi kwani ndo think tankers wa Taifa letu na kuhakikisha Fursa za Viwanda zitakazopatikana tuzitumie vizuri kwa manufaa mapana ya Tanzania.

Mwenyekiti wa Tahliso aliwasilisha salamu kutoka Tanzania pamoja na Tahliso kwa ujumla na kuomba kuendeleza Ushirikiano baina ya Tahliso na Ubalozi wa Tanzania Nchini China na kuahidi Ushirikiano ulioanza utadumu na lazima Vijana sasa tuanze kufanya Kazi kwa Bidii na kutafuta fursa zilizopo kwa wenzetu ili kuhakikisha tunazileta Nyumbani na kuzitekeleza kwa Wakati.

Lakini pia tumekubaliana Kuhakikisha Changamoto zote za Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma China wanazokumbana nazo tutazishughulikia kwa Pamoja ili kuhakikisha wanapata mazingira mazuri ya Kusoma wawapo Nchini China.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wanaosoma Beijing China pamoja na Maafisa Ubalozi wa Tanzania Nchini China.

Tanzania na China ni Marafiki wakubwa na sisi kama Vijana wa Taifa letu tunakila Sababu ya Kuhakikisha tunatumia fursa zilizopo kwa Kufanya kazi kwa Bidii.




Rais Dkt Magufuli amteua Mhandisi Aisha Amour kuwa Balozi nchini Kuwait

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli leo Novemba 03.2019 amemteua Mhandisi Aisha Amour kuwa Balozi nchini Kuwait.Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Aisha Amour alikuwa  katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro.

WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAAJIRI (ATE) NA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI (TUCTA)

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na viongozi wa Chama cha Waajiri (ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) walipokutana kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya Wafanyakazi na Waajiri, Novemba 2, 2019 Jijini Dodoma.
Sehemu ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokutana nao Bungeni, Jijini Dodoma. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akifafanua jambo wakati wa kikao hicho cha Utatu kilichowakutanisha kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya Wafanyakazi na Waajiri.

Baadhi ya wajumbe kutoka Chama cha Waajiri (ATE) na Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia majadiliano wakati wa mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akieleza jambo wakati wa mkutano huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipitia taarifa wakati wa mkutano na viongozi wa Chama cha Waajiri (ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) walipokutana kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya Wafanyakazi na Waajiri, Jijini Dodoma.
Mkuu wa Huduma za Kisheria kutoka Chama cha Waajiri (ATE) Bi. Suzan Ndomba akichangia mada wakati wa mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe.

Benki ya NBC Yatangaza kupata ongezeko la faida kwa asilimia 300

$
0
0
Benki ya NBC Yatangaza kupata ongezeko la faida kwa asilimia 300

Dar es Salaam, 3 Novemba, 2019: BENKI ya NBC imeonyesha ufanisi mkubwa katika utendaji wake baada ya kutangaza kupata ongezeko la faida (baada ya kodi) la asilimia 367 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka huu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Mafanikio hayo yanatajwa kusababishwa na ufanisi wa benki hiyo katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika usimamizi wa mizania, kuongezeka kwa mapato yatokanayo na ada ya mihamala na kuboreshwa kwa huduma za mikopo, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw Theobald Sabi.

Kwa mujibu wa ripoti yake ya kifedha ya robo ya tatu ya mwaka 2019 iliyotolewa hivi karibuni, hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu, benki hiyo ilikuwa na jumla mikopo yenye thamani ya TSh 987 bilioni huku ikiwa na amana za wateja zenye thamani ya Tsh 1.717 Trilioni

"Jumla kuu ya Mikopo yetu imeongezeka katika kipindi cha robo mwaka kwa asilimia 3.7, hasa ikichangiwa na ongezeko la uombaji wa mikopo kutoka kwa wateja wetu wakubwa, wa reja reja na wa kati huku amana zetu (customer deposits) kwa ujumla ziliongezeka kwa asilimia 19.3" Aliongeza Bw Sabi.

"Umakini na ufanisi wetu katika suala zima la utoaji wa mikopo limeanza kutupa faida kwa kuwa hata kiwango cha mikopo chechefu kimeendelea kupungua hadi kufikia asilimia 6.9 kutoka asilimia 10.1 katika kipindi kama hiki mwaka uliopita,’’ alibainisha Bw Sabi.

Aliongeza kuwa mkakati wa mabadiliko ya kidigitali unaotekelezwa na benki hiyo umeendelea kuzaa matunda ya ukuaji huo huku akibainisha kuwa mfumo wa miamala kwa njia ya simu umekua kwa asilimia 50 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka jana.

“Ongezeko hili ni ishara kwamba wateja wetu wanapokea vizuri mabadiliko ya uboreshaji wa huduma zetu hasa kidigitali na hivyo kutupunguzia kiasi cha muda ambao tungeutumia kuwahudumia kupitia matawi yetu na hivyo tunajikuta tunapata muda wa kutosha kubuni na kutekeleza huduma nyingine bora zaidi kwa ajili yao,’’ alisema.

Alihamasisha zaidi wateja wa benki hiyo wakiwemo wa reja reja na wateja wakubwa yakiwemo mashirika na taasisisi (corporates)kuendelea kutumia huduma hizo za kidigitali kwa kuwa ni salama na zinatoa huduma ya malipo ya ya aina zote yakiwemo malipo makubwa kwa ndani na nje ya nchi.

Aidha Bw Sabi aliitaja huduma nyingine ya kielectronic inayokua kwa kasi kuwa ni NBC Wakala ambayo kwasasa ina mtandao wa mawakala zaidi ya 2,000 waliotapakaa nchi nzima.

“Wateja sasa wana uwezo wa kuzifikia akaunti zao na hufanya mihamala kwa urahisi zaidi kupitia maelfu haya ya mawakala nchi nzima.’’

“Mawakala wa NBC kwasasa wamefuzu kufanya mihamala kupitia mfumo wa kielectronic wa malipo serikalini (GePG) na hivyo wateja wanaweza kuwatumia kufanya malipo yao kwenye taasisi na mashirika ya serikali na ndio sababu Benki ya NBC sasa ni moja wapo ya benki inayoongoza kwa Makusanyo ya Mapato ya Serikali kupitia GePG.’’Alisema. 


 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Bw  Theobald Sabi.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images