Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC Wafanyika JIANGSU

$
0
0
Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC kutoka Jimbo la Jiangsu umefunguliwa leo jijini Nanjing na Naibu Gavana wa Jimbo hilo Ndugu Ma Qiulin. Mkutano huo umehudhuriwa na Mabalozi 11 wa nchi za SADC na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa SADC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Miundombinu wa Sekretariat ya SADC Bi Mapolao Mokolena.

Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo Balozi wa Tanzania Mhe. Mbelwa Kairuki alitoa hotuba kwa niaba ya Jumuiya ya Mabalozi wa Nchi za SADC nchini China ambapo pamoja na mambo mengine aliyakaribisha makampuni ya SADC kuchangamkia fursa za uwekezaji katika nchi za SADC kutokana na fursa za soko kubwa la SADC lenye idadi ya watu wanaokadiliwa kuwa milioni 345 na uchumi wa GDP 600 Billioni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miundombinu wa SADC Bi Makolane alipokuwa akitoa mada alielezea mazingira mazuri yaliyopo ya biashara na uwekezaji katika nchi za SADC. Aidha, Mabalozi wa nchi za SADC walielezea fursa zilizopo katika nchi za SADC katika sekta za miundombinu, kilimo, viwanda; madini; utalii nk. 

Jiangsu ni jimbo la pili kwa ukubwa wa uchumi nchini China likiwa na GDP ya USD 1.2 Trillion na idadi ya watu milioni 80. Jimbo hilo linaongoza nchini China katika sekta ya viwanda. Makampuni kutoka Jimbo la Jiangsu yamefanya uwekezaji nchini Tanzania katika sekta ya viwanda.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Afrika na wenyeji China mara baada kuhitimisha mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC uliofanyika jimbo la Jiangsu nchini China 
Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki akitoa hutuba kwenye ufunguzi wa Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC ulifanyika Jiangsu, China 
Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki (mstari wa mbele katikati) akifuatilia Mkutano wa kuvutia uwekezaji uliokuwa ukiendelea 
Wajumbe kutoka chi za SADC na Wenyeji tao China wakifutilia Mkutano uliokuwa ukiendelea 

Wananchi watakiwa kunywa maziwa yaliopita viwandani

$
0
0
Na Woinde Shizza globu jamii,Arusha

Unywaji wa maziwa ya ng'ombe  ambayo hayajapimwa na mtaalamu husababisha magonjwa mbalimbali kwa binadamu ikiwemo ugonjwa wa kifua kikuu pamoja na brusela. 

Hayo yameelezwa na daktari wa mifugo ambaye pia ni mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha  Grande Demam ,Dr Deo Temba wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo alibainisha kuwa wakati huu kumekuwa na wananchi wengi wanaokubwa na magonjwa haya ,huku wengi wao ukiwachunguza unakutwa magonjwa yao yametokana na unywaji wa maziwa

Alibainisha kuwa ipo haja ya serikali kuunda sheria itakayo muamrisha mwananchi kununua maziwa yaliopimwa na yale ambayo yamepita kiwandani ili kuweza kusaidia kupunguza tatizo hili

"kumekuwepo na wananchi wafugaji ambao sio waaminifu unakuta kabisa anajua ng'ombe wangu ni mgonjwa au nimempa dawa sitakiwa kukamua na kwenda kuuza lakini kwavile anauroho wa fedha anakamua na kwenda kuuza na akifika kwa mnunuzi ananunua na kutumia bila kujua"alisema Temba

Alibainisha kuwa maziwa ambayo yanapita viwandani hupimwa kwanza kabla  ya kuingizwa kiwandani,huku akifafafanua kuwa hupimwa kama yamewekwa maji au kama mnyama huyo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wowote  naikibainika ni mazuri ndipo harakati zingine hufanyika  

"kuna wananchi ambao wanachukuwa maziwa uko mtaani hayaja chekiwa ubora ,hayajapimwa lakini pia wakifika majumbani kwao hawayachemshi kama inavyotakiwa wanachemsha kwa muda mchache hivyo iwapo maziwa yale au ng'omb e yule alikuwa na magonjwa vile vijidudu vilivyopo kwenye maziwa havifi na ndio vinasababisha magonjwa haya yanayotoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu"alifafanuaTemba 

Aidha alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wanakunywa maziwa ambayo hayanaubora kwani asilimia kubwa ya wauzaji wa maziwa haya wamekuwa wanayaweka maji kitu ambacho kinasababisha maana halisi ya maziwa haya kupotea na ubora wake pia kuisha kabisa kutokana na maji wanayoyaweka huku wengine wakiwa wanajaza maji nakuchanganya vitu vingine kama unga wa ngano ili maziwa yao yaonekane mazito

Alimalizia kwakuwataka wananchi kuacha kutumia maziwa yanauzwa kiolela badala yake watumie maziwa yaliotoka viwandani kwani yamechemshwa vizuri ,yameangaliwa kama yanaubora,pia Baada ya kuletwa nawateja  yameangaliwa kama mnyama huyo anamagonjwa au kama alikuwa anatumia madawa.

Kwaupande wa mwananchi aliejitambulisha kwa jina la  Japheti Mwahakila alisema kuwa nikweli wao kama wananchi wamekuwa wananunua maziwa kiholela bilakujua kama ng'ombe huyo ni mzima au la kitu ambacho kinawafanya baadhi yao kupata magonjwa mbalimbali yawanyama.

Aliomba serikali kupitia mamlaka ya chakula na dawa kutoa elimu zaidi kwa wafugaji juu ya mazara yanayoweza kutokea iwapo atauza maziwa ambayo mnyama wake ni mgonjwa ili kuweza kuwasaidia wananchi kwani anaamini wakipewa elimu ya kutosha tatizo hili litamalizika kabisa.
Picha ikionyesha meneja masoko wa  kiwanda cha Grande Demam  Japheti Mwahakila akionyesha namna kampuni hiyo inavyosindika siagi kabla ya kwenda kwa mteja(picha na Woinde Shizza ,Arusha)


THE GRANDE DEMAM KIWANDA CHA MAZIWA KINACHOWANUFAISHA KIUCHUMI WAFUGAJI 2000

$
0
0
Na Woinde Shizza michuzi blog,Arusha.

Wilaya ya Meru ni moja kati ya Wilaya maarufu zinazoongoza kwa uzalishaji mkubwa wa maziwa mkoani Arusha,maziwa ambayo huuzwa maeneo ya miji ikiwemo viunga vya Jiji la Arusha na nje ya jiji hilo.

Licha ya uzalishaji huo wa maziwa bado wafugaji hao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa masoko ya uhakika ya kununua maziwa hayo hivyo kupelekea maziwa wanayoyazalisha kuharibika baada ya kukaa muda bila kununuliwa.

Kufuatia Changamoto hiyo Daktari wa Mifugo Dokta Deo Temba aliona changamoto hiyo kama fursa ya uwekezaji kwani malighafi ya maziwa inapatikana kwa wingi ,kwa kuwa wafugaji walikua wakiyamwaga maziwa yao yaliyokua yakiharibika kwa kukosa soko la uhakika na hawakua na namna yoyote ya kuongeza thamani maziwa hayo ili yaweze kukaa kwa muda bila kuharibika.

Dokta Deo Temba aliacha kazi ya kuajiriwa mwaka 2001 na kuamua kufuga ng`ombe 1 baadae watatu ambao walikua wakitoa lita 30 kila siku huku yeye na familia yake wakitumia lita 1 hivyo maziwa mengine kuharibika baada ya kukaa kwa muda.

Suala hili lilimfikirisha sana Dokta Deo ambaye alimtafuta mtaalamu kutoka nchini Kenya atakayemfundisha jinsi ya kuongeza thamani maziwa yake ,kuyafungasha na kuyauza .Mtaalamu huyo alimfundisha ndipo akaianza kazi ya kuongeza thamani maziwa hayo nyumbani kwake.

Baada ya muda majirani zake wafugaji walianza kuvutiwa na jinsi anavyoongeza thamani maziwa yake na walimletea maziwa ili ayaongeze thamani ndipo alipoanza kununua maziwa na kuongeza thamani takribani lita 100,150 mpaka sasa anazalisha lita 200000 kwa siku.

Baada ya hapo akafungua kiwanda kidogo ambacho kilikua na uwezo wa kusindika lita 200 kwa siku huku wafugaji wakileta maziwa mengi zaidi ndipo alipoongeza uzalishaji na kwa sasa anazalisha lita 200000 kwa siku.

Kutokana na ongezeko hilo lauzalishaji kwa sasa Dokta Deo pamoja na Wakurugenzi wenzake wa kiwanda hicho cha The Grande Demam wameongeza wigo na kununua maziwa zaidi kwa wafugaji ambao walikua wakiteseka kupata masoko na wakati mwingine kumwaga maziwa yao yanayoharibika kwa kukaa muda mrefu bila kununuliwa.

Kiwanda hicho kinanunua maziwa bora kutoka kwa wafugaji na kuyaongezea thamani ikiwa ni pamoja na kuyafungasha vyema.“Maziwa ambayo hayajaongezwa thamani hukaa kwa muda wa masaa 13 lakini maziwa yaliyoongezwa thamani yanaweza kukaa hadi mwezi mmoja jambo ambalo linaleta unafuu hasa kwa kipindi kifupi kabla hayajafika sokoni” Alisema Dokta Deo

Dokta Deo anaeleza kuwa maziwa yaliyosindwa ni maziwa mazuri kwa afya ya binadamu yamekua yameondolewa bacteria hatarishi na kuongezewa bacteria rafiki kwa afya.Mtu anayetumia Maziwa ambayo hayajasindikwa anakua yuko hatarini kupata magonjwa mbalimbali ikiwemo Tb,Typhoid na Brusela.Pia maziwa yaliyosindikwa kiwandani yanasaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yanayoweza kuambukizwa kutoka wanyama kwenda kwa binadamu.

Mkurugenzi wa kiwanda hicho Dokta Deo amesema kuwa maziwa ni bidhaa yenye faida kubwa sana katika mwili wa binadamu ikiwemo virutubisho aina ya Protini,Madini,Fat pamoja na wanga.Dokta Deo anashauri unywaji wa maziwa uhamasishwe kwa wingi katika jamii ili kuwa na jamii yenye afya bora inayoweza kushiriki katika shughuli za uzalishaji.

Anaeleza kutokana na ubora wa maziwa yanayozalishwa na kiwanda hicho wateja wamekua wakiyafurahia hivyo wanafirikiria kuongeza uzalishaji na kuboresha zaidi ili kuwafikia wateja wengi zaidi.

“Tuna mpango wa kuzalisha mpaka lita laki tano kwa siku ,uzalishaji huu utaleta tija kwa kiwanda pamoja wafugaji ambao tumekua tukinunua maziwa kwao tutanunua maziwa mengi zaidi hivyo kukuza kipato cha wafugaji waweze kunufaika na shughuli zao za ufugaji” Alisema Dokta Deo

Ni vyema Watanzania wakajifunza kunywa maziwa haya bora yanayozalishwa nchini badala ya kunywa maziwa kutoka nje kwani kwa kufanya hivyo utakua unainua uchumi wa nje.

Biashara hiyo ya maziwa imesaidia vijana wengi waliojiriwa na kiwanda hicho katika sekta ya uzalishaji na usambazaji jambo ambalo linaonyesha mnyororo wa wanufaika wa kiwanda hicho unavyoongezeka.

Kwa sasa bidhaa za maziwa,Yogat na Siagi za The Grande Demam imefika katika mikoa ya Dar es Salaam ,Manyara ,Tanga ,Kilimanjaro ,Dodoma na Morogoro ambapo alibainisha kuwa wanampango wa kuongeza wigo na kuuza bidhaa zao nchi nzima

Afisa masoko wa kiwanda hicho Faraja Kiliba amesema kuwa kiwanda hicho kinaweza kuwanufaisha watu zaidi ya 4500 kutokana na mzunguko wa uzalishaji mpaka kumfikia mlaji.
 Baadhi ya Wafanyakazi na Viongozi wa Kiwanda cha Maziwa cha The Grande Demam wakihakiki ufungashaji wa bidhaa za maziwa zinazozalishwa kiwandani hapo.Picha na Woinde Shizza
 Baadhi ya Wafanyakazi na Viongozi wa Kiwanda cha Maziwa cha The Grande Demam wakihakiki ufungashaji wa bidhaa za maziwa zinazozalishwa kiwandani hapo.Picha   na Woinde Shizza

 Baadhi ya Viongozi wa kiwanda cha maziwa cha  The Grande Demam wakinywa maziwa yanayozalishwa na kiwanda hicho
Uongozi wa kiwanda cha maziwa cha  The Grande Demam


Anaeleza kuwa licha ya kiwanda hicho kujikita na uzalishaji wa maziwa bado kinatoa huduma za ushauri wa ufugaji bora,matibabu ya mifugo pamoja na madawa ili waweze kufanya ufugaji wenye tija pia wamekuwa wakiwakopesha wafugaji madini ya ngombe kwaajili ya kuzuia magonjwa mbalimbali

Pia anashauri serikali na taasisi binafsi kuunga mkono juhudi za Wawekezaji wanaowekeza kwenye viwanda ikiwamo kiwanda cha maziwa kwani kinagusa maisha ya watu wengi moja kwa moja.“Kama unavyojua katika maziwa hakuna kinachosalia unatoa maziwa,siagi,yogati,samli,mtindi hivyo hakuna kinachotupwa kila kitu kina thamani kubwa” alisema Mshauri huyo

Rafael akyooo ni moja kati ya Wafugaji ambao maziwa yao yananunuliwa na kiwanda hicho wamesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kiwanda hicho wamekua wakipata soko la uhakika la maziwa yao hivyo kuondokana na tatizo la maziwa kuharibika kwa kukosa soko.

Anaeleza kuwa uwepo wa kiwanda hicho umewasaidia wafugaji wengi ambao walikua hawana pa kuyapeleka maziwa yao lakini kwa sasa wanafika katika kiwanda hicho na kuyapeleka maziwa yao

KWANDIKWA AAGIZA BILIONI 32 ZILIPWE TEMESA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Mhandisi Elias Kwandikwa kushoto akikagua mojawapo ya vitendea kazi vya karakana ambavyo vimenunuliwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa ajili ya kusambazwa kwenye karakana na vituo 12 nchini, vifaa hivyo vimegharimu jumla ya shilingi milioni 260. Katikati ni Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Japhet Maselle.
Muonekano wa baadhi ya vitendea kazi vya karakana vilivyonunuliwa na TEMESA, vitendea kazi hivyo vimegharimu jumla ya shilingi milioni 260 na vitasambazwa katika vituo 12 ikiwemo karakana ya Dodoma, Ruvuma, Geita, Kigoma, Rukwa, Pwani, Shinyanga, Katavi, Mwanza, Songwe, Same na Kahama.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Mhandisi Elias Kwandikwa akiwa ndani ya karakana inayotembea (Mobile Workshop Track) ambayo ni kwa ajili ya matengenezo ya magari yaliyo mbali na karakana za mikoa na magari yaliyopata hitilafu yakiwa safarini. TEMESA imenunua gari mbili zitakazotumika kama karakana za dharura ambazo pamoja na vifaa vyake zimegharimu jumla ya shilingi milioni 115.

Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Mhandisi Elias Kwandikwa kushoto akipewa maelezo wakati akikagua vitendea kazi vya karakana ambavyo vimegharimu jumla ya shilingi milioni 260. Vitendea kazi hivyo vitasambazwa katika karakana na vituo 12 nchini.

PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)

……………………….

NA ALFRED MGWENO (TEMESA)

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Elias Kwandikwa ameziagiza taasisi zote za serikali zinazodaiwa madeni na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) yanayofikia jumla ya shilingi bilioni 32 kuhakikisha zinalipa madeni hayo haraka iwezekanavyo ili kuusaidia Wakala huo kutimiza majukumu yake. 

Mhandisi Kwandikwa ametoa maagizo hayo leo wakati akikagua vitendea kazi vipya vilivyonunuliwa na TEMESA kwa ajili ya kuvisambaza kwenye karakana zake.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kwandikwa alisema anaelewa changamoto zinazoukabili Wakala ikiwemo kutolipwa madeni kwa wakati ambapo alisema Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2019/20 imetoa fedha zote zilizokuwa kwenye bajeti zinazohusu karakana ili TEMESA ikamilishe ukarabati wa karakana na ununuzi wa vitendea kazi ambapo alielekeza miradi yote iliyokuwa imepangwa na imepelekewa fedha, utekelezaji wake ukamilike kwa wakati.

‘’Ninaelekeza Taasisi zote za Serikali zilipe madeni zinazodaiwa na TEMESA kiasi cha Shilingi bilioni 32’’. Aliongeza Naibu waziri.

Awali Naibu waziri alipata wasaa wa kukagua vitendea kazi hivyo vipya vya karakana pamoja na karakana mbili mpya zinazotembea (Mobile Workshop Track) kwa ajili ya matengenezo ya magari yaliyo mbali na karakana za mikoa na magari yaliyopata hitilafu yakiwa safarini.

Aidha alitoa wito kwa watumishi wa Wakala kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha magari yanafungwa vipuri halisia na hivyo kuondoa malalamiko yaliyozoeleka kuwa magari yakitoka katika karakana za TEMESA huharibika baada ya muda mfupi.

‘’Ninaagiza kudhibiti gharama za matengenezo ambazo nazo hulalamikiwa. Mnapaswa kununua vifaa (vipuri) kwa pamoja (Bulk procurement) ili kupata punguzo la bei’’. 

Naye Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Japhet Maselle, akisoma taarifa fupi katika hafla hiyo, alisema Vitendea kazi hivyo vimegharimu jumla ya shilingi milioni 260 na vitasambazwa katika vituo 12 ikiwemo karakana ya Dodoma, Ruvuma, Geita, Kigoma, Rukwa, Pwani, Shinyanga, Katavi, Mwanza, Songwe, Same na Kahama. Vilevile, gari itakayotumika kama karakana ya dharura pamoja na vitendea kazi vyake imegharimu jumla ya shilingi milioni 115 na gari hiyo itafanya kazi sambamba na magari madogo mawili

‘’Tutafanya ununuzi wa vitendea kazi kwa ajili ya karakana zingine 14 pamoja na hayo tunaishukuru serikali kwani tumepokea shilingi bilioni 12.4 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya karakana pamoja na vivuko, nakuahidi fedha hizi zitatumika kama zilivyokusudiwa na kwa ufanisi mkubwa’’, alisema Mhandisi Maselle.

Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA una jumla ya karakana 26 katika makao makuu ya mikoa kote nchini pamoja na karakana moja ngazi ya wilaya katika mji wa Ifakara katika wilaya ya Kilombero.

KIVUKO CHA BILIONI 5.3 KUTUA MAFIA NYAMISATI FEBRUARI MWAKANI

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Elias Kwandikwa akichomelea chuma kuashiria kuanza kwa ujenzi wa kivuko kipya cha Mafia Nyamisati. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 sawa na tani 100, kinajengwa kwa shilingi bilioni 5.3 za Kitanzania na kitakamilika ifikapo mwezi Februari mwakani.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle kushoto akisoma taarifa fupi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Mhandisi Elias Kwandikwa wa (pili kushoto)wakati alipokua akizindua ujenzi wa kivuko kipya cha Mafia Nyamisati, tukio lililofanyika katika yadi ya Songoro Kigamboni. Kutoka kulia ni Lazaro Vazuri na mbunge wa Mafia Mbaraka Dau.

AKINA MAMA WASHAURIWA KUWANYONYESHA WATOTO WAO MIEZI SITA KUPATA AFYA BORA

$
0
0
KINA mama wameshauriwa kuwanyonyesha watoto wao kuanzia umri 0 hadi miezi sita ili waweze kupata afya bora ambayo itamsaidia kumjenga kimwili na kiakili katika ukuaji wake.

Hayo yalisemwa na Mratibu Lishe Mkoa wa Dar es Salaam, Neema Kweba ambapo alisema kuwa kitendo cha kuacha kuwanyonyesha kabla ya muda kwa kisingizio cha maziwa hayatoki kunaweza kusababisha udumavu wa mwili na akili.

Alisema mtoto anatakiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama kuanzia anapozaliwa (umri 0) hadi umri wa hadi umri wa miaka miwili na zaidi huku akifikisha miezi sita anatakiwa kupewa vyakula mchanganyiko yakiwamo maziwa ya mama yake.

Alisema maziwa ya mama yana virutubisho vingi ambavyo vinasaidia katika ukuaji wake jambo ambalo linawamfanya mtoto kuwa na afya bora Na kuendelea kukua bila ya matatizo yoyote.

"Kuna baadhi ya kina mama wana tabia ya kuwaachisha watoto kunyonya kabla ya wakati kwa kisingizio cha maziwa hayatoki, jambo ambalo ni uongo na kwamba linaweza kusababisha udumavu kwa mtoto kwa kushindwa kukua ipasavyo," alisema Kweba.

Aliongeza kuwa, hivyo basi wanapaswa kubadilika na kunyonyesha watoto wao kuanzia umri 0 hadi miaka miwili na kwamba wakifikisha umri wa miezi sita wanapaswa kuwaanzishia vyakula mchanganyiko vyenye virutubisho huku akiendelea kunyonya,hali ambayo itaimarisha afya yake.

"Ninawasihi wanawake wenzangu acheni tabia ya kusingizia maziwa hayatoki ili muweze kuwaachisha watoto wenu kabla ya wakati, kufanya hivyo kunaweza kusababisha udumavu kwa mtoto au kukosa afya bora, kwa sababu maziwa ya mama ni muhimu kwa afya yake na kwamba yanamsaidia katika ukuaji wa afya ya mwili na akili," alisema Kweba.

Aliongeza kuwa, mtoto anapokosa afya bora, madhara yake ni makubwa ikiwa ni pamoja na kupata udumavu au utapiamlo, ukosefu wa kinga za mwili ,jambo ambalo linaweza kusababisha ubongo wake kushindwa kukua ipasavyo.

Alisema kuwa kila mzazi anayenyonyesha ana wajibu wa kuhakikisha anamnyonyesha mtoto hadi afikie umri wa miaka miwili au zaidi huku akiendelea kumpa chakula mchanganyiko, jambo ambalo litamsaidia mtoto kuwa na afya bora pamoja na kumkinga na maradhi.

Alisema mkakati wa Mkoa ni kuhakikisha kuwa wanaendelea kutoa elimu ya lishe kwenye vituo vya afya, zahanati na hospitali pamoja na majumbani ili kuwaelimisha wazazi au ndugu wanaobaki na watoto ili waweze kuzingatia elimu ya lishe bora kwa mtoto.

MISS WORLD VANESSA PONCE AGAWA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI MOSHONO

$
0
0
Na Woinde Shizza michuzi blog,Arusha

Mlibwende wa dunia 2019 (miss World)Vanessa Ponce kwa kushirikiana na Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian leo wametoa elimu ya hedhi salama pamoja na kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wanawake zaidi ya 100 wa shule ya sekondari ya Moshono iliopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha mkoani hapa.

Vanessa ambaye ni Raia wa Mexico kwa sasa yuko mkoani Arusha,kwa ziara ya siku nne ambapo akiwa mkoani hapa amezindua mashine ya kutengeneza Taulo za kike zinazojulikana kwa jina la Uhuru Pads na kugawa taulo za kike 1000 kwa wasichana wa shule ya sekondari Moshono iliyopo katika halmashauri ya jiji la Arusha.

Akiongea wakati wa kutoa taulo hizo za kike mrembo wa dunia Sylivia Sebastian alisema kuwa amefurahi kushiriki kampeni hii ya kumsitiri mtoto wa kike ,kwani ni jambo ambalo limemgusa sana na linawaumiza watoto wengi wa kike.

"wanafunzi wengi wa kike wamekuwa wanafeli masomo yao kutokana na kuwa na wasiwasi wanapokuwaga katika hedhi,wengine wamekuwa hawaji shule katika kipindi cha hedhi hivyo tumeona tuje kutoa taulo hizi za kike ili matatizo haya yanaowakumba watoto wa kike yanaisha pia tumewapa elimu kuhusiana na hedhi salama"alisema Sylivia

Akiongelea kampeni hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alishukuru mrembo huyo kwa kutembelea nchi yetu na kuipongeza kamati nzima na waandaji wa miss Tanzania kuwezesha kumleta na kuanzisha kampeni hiyo ya kugawa taulo za kike kwa wasichana wa shule za sekondari 

Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na Michezo,Dkt Harrison Mwakyembe amesema ujio wa Mrembo wa dunia(Miss World)hapa nchini katika jiji la Arusha,Venessa Ponce De Leon utasaidia kuitangaza Tanzania kibiashara ya utalii kupitia kampeni yake ya kuhamasisha matumizi ya taulo za kike kwa wanafunzi wa kike.

"pia tumpongeze Rais wetu kwa kuzia matumizi ya mifuko ya plastiki kwani zuio hilo ndio limesababisha hata wenzetu kuja na kutuletea taulo hizi za kike ambazo sio za mfuko wa plastiki kwani zinauzo na ata vifungashio vyake vinaoza na pia hata ukitupa katika choo maligafi yake inalainika na kuoza "alisema mwakimbe

Alibainisha kuwa serikali itakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha wanafanikisha kampeni hii ya kumsitiri mtoto wa kike kwakutafuta wadau ambao watanunua mashine kwa ajili yakuzalisha taulo hizo za kike ili ziweze kukithi maitaji ya watoto wakike wa sekondari zote hapa nchi . 

Naye mkurugenzi mwendeshaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Basila Mwanukuzi amesema hii ni mara ya kwanza kwa Mrembo anayeshikilia Taji la urembo la Dunia mwaka 2018/2019 kuitembelea Tanzania tangu kuanzishwa kwa mashindano ya miss Tanzania mwaka 1994 hapa nchini. alisema kuwa ujio wa miss dunia pamoja na muanzilishi wa shindano hili la miss World Julia Morlye ni bahati ya kipekee kwa nchi yetu ya Tanzania Kwani hii ni mara ya kwanza kwa mrembo huyu kufika hapa nchini hususa ni nchi ya Tanzania.

Alibainisha kuwa hivi karibuni mrembo wetu anatarajiwa kuondoka kuelekea nchini uingereza kwenda kushiriki shindano la mrembo wa dunia ambalo fainali yake inatarajiwa kufanyika huko hivyo watanzania wajitaidi kumpigia kura ili aweze kushinda na hata wageni hawa waendelee kuona umuhimu wa kuja nchini Tanzania huku akitaja kauli mbiu ya mashindano haya kwa mwaka 2019 inasema urembo ni heshima hivyo kila miss Tanzania ambaye amewahi kushiriki shindano hili na anaetarajiwa kushiriki anatakiwa kutambua kauli hii na kuifanyia kazi aidha aliongeza kuwa ni jinsi gani mrembo anaweza kurudisha fadhila kwa jamii kwa kuwasaidia

kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Uhuru Sanitary pads Sara Gunda Alisema kuwa wameamua kuwapa wasichana nafasi nao wajisikie kwamba kuna watu wanawajali katika swala zima la kuvunja ungo na itambulike kuwa uwezi kuwa mwanamkekamili kama ujavunja ungo na ndio maana wakaamua kufanya hivi .

"awali kampuni yetu ilipata mthamini na kuanza kujenga mabweni kwa ajili ya wasichana na katika kutembelea mabweni yale mthamini yule aliona iko aja ya kusaidia zaidi watoto wa kike na akaona atusaidie kutengeneza taulo za kike kwa ajili ya wasichana wetu ,tulianza na kutengeneza taulo za kike zinazo fuliwa na tulivyogawa tukaona pia katika shule zetu zipo changamoto ya shule nyingi kutokuwa na maji na ndio maana tukaamua kutoa taulo hizi ambazo sio zakufuliwa ili wanafunzi wetu wasiteseke "alisema Gunda

Alibainisha kuwa hadi sasa wameshatoa taulo za kike kwa wanafunzi elfu nne waliopo katika shule za sekondari za halmashauri ya wilaya ya Arumeru ,Monduli pamoja na jiji la Arusha na hawataishia hapa bali watagawa kwa wanafunzi wa kike katika shule zote za mkoa wa Arusha , Amesema lengo ni kuendelea kutengeneza na kugawa bure taulo hizo ziweze kuwafikia wanafunzi wengi zaidi wa kike na kuondoa changamoto walionayo

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake mwanafunzi wa shule ya sekondari ya moshono Neema Msuya alishukuru kwa ujio wa miss world na kubainisha kuwa misaada waliopewa itawasaidia sana kwani kuna wanafunzi ambao wamekuwa hawaji shuleni pindi wanapokuwa katika kipindi cha hedhi kwani wengi wao wanaofia kuchafuka kitu kinachowasababishia kukosa masomo na kupelekea kufeli mitiani yao.o
 Picha ikionyesha Mlibwende wa dunia 2019 (miss World)Vanessa Ponce akiwa anatoa mafunzo ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Moshono wakati alipotembelea shuleni hapa leo na kugawa taulo za kike kwa wanafunzi hao
 mmoja wa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya moshono akiwa anauliza swala kuhusiana ya elimu waliopewa ya hedhi salama wakati miss World na miss Tanzania walienda shuleni kwao kutoa elimu
 
 mfanyakazi wa kampuni ya uhuru Amina Msuya akiwa anagawa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya sekondari moshono hii leo




Muanzilishi wa shindalo la miss world Julia Morlye akiwa anaongea na wanafunzi wa shule ya sekondari moshono wakati walipotembelea shule hiyo leo kugawa zawadi za taulo za kike pamoja na kutoa elimu ya hedhi salama
 miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian akiendelea kutoa elimu ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari mushon

MY LIFE, MY PURPOSE: MEMOIR BY RETIRED PRESIDENT BENJAMIN WILLIAM MKAPA - COMING SOON

$
0
0
UONGOZI Institute: Former President Benjamin William Mkapa's memoir is set to be released on 12th November, 2019. In the book he shares on his childhood, his political maturation, and his time as the 3rd President of Tanzania



Dkt. Mwakyembe: Ni heshima kutembelewa na Miss World 2018

$
0
0

 Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian (kulia) akisistiza jambo wakati wa uzinduzi wa taulo za kike (Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa taulo za kike (Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akimkaribisha Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico wakati wa uzinduzi wa taulo za kike (Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.

Mwenyekiti na Mwendeshaji wa Shindano la Miss World Bi Julia Morley (kushoto) akisisitiza kufurahishwa kwake na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania ambapo ni mara ya kwanza kwake kuja nchini. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico (kushoto) na Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian (kulia).
 Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico (kushoto) na Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian (kulia) wakiwa katika moja ya matukio wakati wa uzinduzi wa taulo za kike (Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.
 Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa taulo za kike (Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.
 Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian (kulia) akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa taulo za kike (Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.

Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico (kushoto) na Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian (kulia) wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa taulo za kike (Uhurupads) uliofanyika katika shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.

(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Arusha)

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Arusha

NI HESHIMA kubwa kwa Tanzania kutembelewa na Mwenyekiti na Mwendeshaji wa Shindano la Miss World Bi Julia Morley pamoja na Mshindi wa Miss World 2018 Vanessa Ponce.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa taulo za kike zinazojulikana kama Uhurupads uliofanyika leo katika shule ya sekondari Moshono iliyopo jijini Arusha.

“Ujio wao leo hapa Arusha, ni heshima kwa taifa. Katika mataifa yote duniani, wameichagua Tanzania, hii ni heshima kubwa na wametuletea zawadi ya Uhurupads ambazo zitawaweka huru watoto wetu katika kutimiza ndoto zao hasa wanapokuwa shuleni” amesema Waziri Dkt. Mwakyembe.


Aidha, Waziri Dkt. Mwakyembe amesema kuwa bidhaa ya taulo hizo alizozindulia leo ni rafiki kwa mazingira kwa kuwa zinaweza kutunzwa mahali popote na zisiwe na madhara kwenye mazingira kwa kuwa haina  mchanganyiko wowote wa plastiki. Taulo hizo zinazotengenezwa na kikundi cha wanawake 12 kiachojulikana kama timu ya Uhuru Kit Ltd ambao wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kutunza mazingira kwa marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki nchini Julai, 2019.


Katika kuhakikisha Tanzania inatumia vema fursa ya ujio wa Mshindi wa Miss World 2018 Vanessa Ponce wa Mexico, Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Serikali itaandaa ziara maalum kwa Uongozi wa Miss World ukiongozwa na Mwenyekiti na Mwendeshaji wa Shindano la Miss World Bi Julia Morley kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini ikiwemo mbuga za Serengeti, hifadhi ya Ngorongoro pamoja na mji wa kihistoria wa Zanzibar.


“Uwepo wa Miss World 2018 Vanessa Ponce, dunia nzima macho yao yapo hapa nchini, ni vema kuitangaza nchi yetu kimataifa kupitia ujio wake” amesema Waziri Dkt. Mwakyembe.


Kwa upande wake Mwenyekiti na Mwendeshaji wa Shindano la Miss World Bi Julia Morley amesema kuwa amefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania ambapo ni mara ya kwanza kwake kuja nchini.


“Nimefurahi sana Tanzania ni nchi nzuri, nilipopanda ndege kuja hapa nilipata matangazo yanayosisitiza marufuku ya kutumia mifuko ya plastiki, Serikali imefanya vizuri kujali kutunza mazingira” alisema Bi Julia Morley.


Nao Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico pamoja na Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian wamesema kuwa urembo ni heshima, UhuruPads zitawasaidia wasichana kupata elimu wakiwa huru wakizingatia kauli mbiu ya ‘Uzuri wenye malengo.’


Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Mwenyekiti na Mwendeshaji wa shindano la Miss World Bi Julia Morley, Mshindi wa Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico, Mshindi wa Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian Bebastian Bebwa pamoja, mwandaaji wa Mashindano ya Miss Tanzania Bi. Basilla Mwanukuzi pamoja na walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Moshono ya jijini Arusha.

LEAH AWAONYA WAZAZI WA KILOLO WANAOKATISHA MASOMO WANAFUNZI

$
0
0
Na Fredy Mgunda Kilolo
MJUMBE wa halmashauri Kuu (CCM) Mkoa wa Iringa, Leah Mwamoto amewaonya wazazi wanaokatisha masomo watoto kuwa serikali itawachukulia hatua kali pindi watakapobainika kufanya kosa hilo.


Mwamoto ameyasema hayo katika mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Mlafu iliyopo katika kijiji cha Mlafu wilayani Kilolo alipomuwakilisha mbunge wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto.


Akiwaonya wazazi katika mahafali hayo Mwamoto amewaeleza wazazi juu ya mazingira mabaya wanayoyakuta watoto wanaokwenda kufanya kazi za ndani katika miji mikubwa.


Hata hivyo amewaomba watendaji wa kata kuendelea kuwafutilia watoto ili kuwaepusha kujiingiza katika mazingira hatarishi yatakayoharibu ndoto zao.


Aidha Mwamoto amepongeza uongozi wa shule ya sekondari Mlafu kwa matokeo mazuri pamoja na mbunge wa jimbo la Kilolo, Mhe Venance Mwamoto kuchangia bati 180 na mifuko 100 ya saruji kwa ujenzi wa zahanati kijiji cha Mlafu.

Awali akisoma taarifa fupi ya shule mwalimu mkuu wa shule hiyo Emmanuel Mbangwa ameomba wadau kujitokeza kuboresha mazingira katika shule hiyo hususani kujenga nyumba za walimu na mabweni.


Nae diwani Mlafu Isidory Kiyenge amewataka wazazi wa kata hiyo pamoja na wadau kuwa tayari kuchangia katika sekta ya elimu ili kuongeza mazingira ya ufaulu.


Kayenge amewataka wanafunzi kujiandaa kwa mitihani ya kidato cha nne huku alito ahadi ya kuwaandalia chakula wakati wa mitihani.Mjumbe wa halmashauri Kuu (CCM) Mkoa wa Iringa, Leah Mwamoto akiongea na wazazi wa shule ya sekondari ya Mlafu iliyopo katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
 Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mlafu iliyopo katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wakicheza nyimbo mbele ya mgeni Rasmi

WAZIRI JAFO AAGIZA KUWAPELEKA WANAFUNZI KATIKA SHULE WATAKAZOZICHAGUA

$
0
0

 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) Suleiman Jafo akizungumza wakati wa kutoa tunzo  za Elimu kwa wanafunzi, walimu na shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kidato cha sita na darasa la saba 2019.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) Suleiman Jafo amemuagiza Katibu Mkuu Tamisemi, kuwapeleka wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao katika shule watakazochagua ili kuwawezesha kutimiza ndoto zao.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati tamasha utoaji tunzo kwa za Elimu kwa wanafunzi, walimu na shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kidato cha sita na darasa la saba 2019 zilizoratibiwa na Global Education Link kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani Tanzania.

Amesema, serikali inafanya yote hayo katika kutoa hamasa, kukuza na kuongeza ushindani katika elimu kwani siyo vizuri kukatisha ndoto za vijana hao.

"Yule  kijana Tanzania one nilimsikia anasema anatamani kwenda shule ya sekondari ya Iliboru nitashangaa sana kama hataenda huko, hawa ni vijana special waambieni wachague shule wanazotaka waende kusoma, ..Naomba niwahakikishie, Rais Magufuli anawapenda sana, mtachagua shule zile mnazotaka nyinyi kwenda kusoma, katibu mkuu shughulikiia hilo. Amesema Jafo.

Aidha, amesema kwa, wale wa kidato cha sita kwa kuwa Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako yupo basi atalishughulikia hilo.

" Hawa ni vijana special, kwa vile katibu mkuu wa elimu yupo hapa na kuna vijana wa kidato cha sita, msiharibu ndoto za watu. Lazima tujifunze kutafsiri utashi wa watu, nini wanataka hawa vijana.". Amesema.

Aidha, Waziri Jafo amewataka wataalamu wanaotunga miongozo ya elimu kuweka yenye manufaa ambayo itakuwa inaangalia taifa linapoelekea.

"Hizi ni tuzo ya kwanza kutolewa na Serikali kwani vijana na walikumu waliofanya vizuri kwenye mtihani hiyo wanastahili pongezi ili waendelee kufanya vizuri na tunaamini itaongeza ubora zaidi kwa shule zetu kuendelea kufanya vizuri," amesema Jafo.

Jafo amesema baada ya kupata wazo la utoaji wa tuzo hiyo kazi ya kuratibu walipewa Global Education Link kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani Tanzania.

Amesema, tuzo hizo mpya ni za historia ndani ya nchi . Kwani Serikali ya Awamu ya Tano kwa upana wake imeamua kufanya kitu cha pekee kwa kuwatambua walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kwa kiwango kikubwa.

Amesema, Serikali ilikuwa ikitoa zawadi mbali mbali huko nyuma lakini utaratibu huu mpya wa tuzo ambao ndio mara ya kwanza unafanyika, utaongeza chachu ya elimu na kuiwezesha nchi kufikia katika uchumi wa viwanda. 

"Mafanikio makubwa ya kuwekeza kwenye elimu yanaonekana hasa katika ufaulu kwa ngazi zote kuanzia darasa la saba hadi kidato cha sita, mfano mwaka jana, katika shule bora 100, shule 64 zilikuwa za umma na shule 52 zilikuwa za kata, hii ilikuwa ni mara ya kwanza ndipo nikaamua kutambua shule bora. Amesema Jaffo

Aidha amesema, mwakani licha ya kuthamini waliofanya vizuri, pia mwakani vijana watakaofanya vizuri katika fani ya michezo,  wataingizwa katika tuzo hizo ambapo watabainisha mchezaji na msanii wa mwaka ili kutambua kazi kubwa wanayoifanya kwani elimu ni pamoja na michezo

Katika tuzo hizo zilizojumuisha, walimu wakuu, walimu wa masomo, shule, wilaya na mikoa iliyoongoza kwa ufaulu huo pia wasimamizi wa mitihani kutoka mikoa mbali mbali nao wamejumuishwa.

Kwa upande wake, mratibu mkuu wa tuzo hizo, Mkurugenzi wa Global Education Link Abdalmalik Mollel amesema ili walimu na wanafunzi wafanye vizuri darasani wanahitaji motisha.

" Watoto wengi nimeongea nao hawana matamanio makubwa ya mamilioni, wanataja tu aina za shule wanazozitaka, waende,  pia wale wa vyuo vikuu wanasema teyari wamepata nafasi vyuoni ila wanaomba bodi ya mikopo isiwasahau kuwapa mikopo na mimi kama mratibu ninasema wanastahili. Walimu nao hawako nyuma wanahitaji wakiwa wamefanya vizuri serikali isimame na kusema tunakutambua hongera., amesema Mollel.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania Charles Msonde amesema utoaji wa tuzo hizo utaongeza kiwango cha ufaulu.

"Ushindani wa tuzo hizi ni heshima kwa Baraza la Mitihani," amesema.

BEI YA MADAFU

DKT.KAWAMBWA ATOA MIL.30.8 ZA MFUKO WA JIMBO KUPIGA TAFU VIKUNDI 30 VYA UJASIRIAMALI

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo,Dkt Shukuru Kawambwa akikabidhi fedha kwa vikundi 30 vya wajasiriamali wanawake na vijana na wazee.

Na Mwamvua Mwinyi Bagamoyo
MBUNGE  wa Jimbo la Bagamoyo,Dkt Shukuru Kawambwa amekabidhi sh.milioni 30.801 kwa vikundi 30 vya wajasiriamali wanawake, vijana na wazee ili ziwasaidie katika shughuli zao za ujasiriamali.

Hafla ya kukabidhi fedha hizo ambazo ni ruzuku toka mfuko wa Jimbo, imefanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ambapo wawakilishi wa vikundi vilivyonufaika vimekabidhiwa fedha hizo ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo kugawa fedha za mfuko wa jimbo kwa vikundi vya wajasiriamali wadogo kwa ajili ya kuchochea maendeleo kwenye shughuli za kiuchumi wanazofanya.

“Katika ugawaji wa fedha hizi kila kikundi kimeangaliwa vizuri, vikundi vya vijana, wazee na wanawake, hakukuwa na ubaguzi, lengo likiwa ni kuhakikisha tunawafikia walengwa na kuwasaidia kuzifikia ndoto zao kwa kuwawezesha kidogo ili kujiinua kiuchumi” alieleza Kawambwa.

Aliongeza baada ya ugawaji wa fedha hizo, atashirikiana na madiwani na wataalamu wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, kuwatembelea wanavikundi hao ili kuona kama fedha zilizotolewa zimekwenda kufanya kazi iliyokusudiwa.

Aliwahamasisha wananchi wa Bagamoyo, kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali vya wanawake, wenye ulemavu na vijana katika maeneo yao.

“Katika mwaka wa fedha 2019/2020, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, imetenga sh.211.915  toka mapato yake ya ndani kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wanawake, vijana na wenye ulemavu, robo ya fedha hizi hutolewa mara moja kila baada ya miezi 3,"

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Fatuma Latu ,alifafanua kwa miaka minne mfululizo mfuko wa Jimbo la Bagamoyo, umekuwa ukitoa wastani wa sh. milioni 30 kwa taasisi za serikali na vikundi vya wajasiriamali wadogo ndani ya halmashauri.

Mmoja wa wanufaika wa ruzuku hiyo ya mfuko wa Jimbo, mzee Golden Mwenda, toka kikundi cha Unjacha kilichopo Chasimba, Kata ya Yombo, ambao wanajihusisha na kilimo cha muhogo, amepongeza hatua hiyo ya utoaji fedha za ruzuku kwa vikundi vya wajasiriamali wadogo ambazo zitawawezesha kuinua biashara zao.

MLIMWENDE WA DUNIA ATOA ELIMU YA HEDHI SALAMA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MOSHONO

$
0
0
 Mlibwende wa dunia 2019 (miss World)Vanessa Ponce akiwa anatoa mafunzo ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Moshono wakati alipotembelea shuleni hapa leo na kugawa taulo za kike kwa wanafunzi.
Mlibwende wa dunia 2019 (miss World)Vanessa Ponce kwa kushirikiana na Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian wakiwa wanapanda mti wa matunda kama ukumbusho katika shule ya sekondari ya  moshono.

Na Woinde Shizza michuzi blog,Arusha 
MLIMBWENDE wa dunia 2019 (miss World)Vanessa Ponce kwa kushirikiana na Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian leo wametoa elimu ya hedhi salama pamoja na kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wanawake zaidi ya 100 wa shule ya sekondari ya Moshono iliopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha mkoani hapa.

Vanessa ambaye ni Raia wa Mexico kwa sasa yuko mkoani Arusha, kwa ziara ya siku nne  ambapo amezindua mashine ya kutengeneza Taulo za kike zinazojulikana kwa jina la Uhuru Pads na kugawa taulo za kike 1000 kwa wasichana wa shule ya sekondari Moshono iliyopo katika halmashauri ya jiji la Arusha.

Akiongea wakati wa kutoa taulo hizo za kike mrembo wa dunia Sylivia Sebastian amesema kuwa amefurahi kushiriki kampeni hii ya kumsitiri mtoto wa kike, kwani ni jambo ambalo limemgusa sana na linawaumiza watoto wengi wa kike.

"Wanafunzi wengi wa kike wamekuwa wanafeli masomo yao kutokana na kuwa na wasiwasi wanapokuwaga katika hedhi, wengine wamekuwa hawaji shule katika kipindi cha hedhi hivyo tumeona tuje kutoa taulo hizi za kike ili matatizo haya yanaowakumba watoto wa kike yanaisha pia tumewapa elimu kuhusiana na hedhi salama"alisema Sylivia

Kampeni hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amemshukuru mrembo huyo kwa kutembelea nchi yetu na kuipongeza kamati nzima na waandaji wa miss Tanzania kuwezesha kumleta na kuanzisha kampeni hiyo ya kugawa taulo za kike kwa wasichana wa shule za sekondari 

Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na Michezo,Dkt Harrison Mwakyembe amesema ujio wa Mrembo wa dunia(Miss World)hapa nchini katika jiji la Arusha,Venessa Ponce De Leon utasaidia kuitangaza Tanzania kibiashara ya utalii kupitia kampeni yake ya kuhamasisha matumizi ya taulo za kike kwa wanafunzi wa kike.

"Pia tumpongeze Rais wetu kwa kuzia matumizi ya mifuko ya plastiki kwani zuio hilo ndio limesababisha hata wenzetu kuja na kutuletea taulo hizi za kike ambazo sio za mfuko wa plastiki kwani zinaoza na ata vifungashio vyake vinaoza na pia hata ukitupa katika choo maligafi yake inalainika  na kuoza "amesema mwakyembe.

Alibainisha kuwa serikali itakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha  wanafanikisha kampeni hii ya kumsitiri mtoto wa kike kwakutafuta wadau ambao watanunua mashine kwa ajili yakuzalisha taulo hizo za kike ili ziweze kukithi maitaji ya watoto wakike wa sekondari zote hapa nchi   . 

Naye Mkurugenzi mwendeshaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Basila Mwanukuzi amesema hii ni mara ya kwanza kwa Mrembo anayeshikilia taji la urembo la Dunia mwaka 2018/2019 kuitembelea Tanzania tangu kuanzishwa kwa mashindano ya miss Tanzania mwaka 1994 hapa nchini. amesema kuwa ujio wa miss dunia pamoja na muanzilishi  wa  shindano hili la miss World  Julia Morlye ni bahati ya kipekee kwa nchi yetu ya Tanzania Kwani hii ni mara ya kwanza kwa mrembo huyu kufika hapa nchini hususa ni nchi ya Tanzania.


Alibainisha  kuwa hivi karibuni mrembo wetu anatarajiwa kuondoka kuelekea nchini uingereza kwenda kushiriki shindano la mrembo  wa dunia ambalo fainali yake inatarajiwa kufanyika huko hivyo watanzania wajitaidi kumpigia kura ili aweze kushinda na hata wageni hawa waendelee kuona umuhimu wa kuja nchini Tanzania  huku akitaja kauli mbiu ya mashindano haya kwa mwaka 2019 inasema urembo ni heshima hivyo kila miss Tanzania ambaye amewahi kushiriki shindano hili na anaetarajiwa kushiriki anatakiwa kutambua kauli hii na kuifanyia kazi  aidha aliongeza kuwa ni jinsi gani mrembo anaweza kurudisha fadhila kwa jamii kwa kuwasaidia

 kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Uhuru Sanitary pads Sara Gunda amesema kuwa wameamua  kuwapa wasichana nafasi nao wajisikie kwamba kuna watu wanawajali katika swala zima la kuvunja ungo na itambulike kuwa uwezi kuwa mwanamkekamili  kama ujavunja ungo na ndio maana wakaamua kufanya hivi .

Amebainisha kuwa hadi sasa wameshatoa taulo za kike kwa wanafunzi elfu nne waliopo katika shule za sekondari za halmashauri ya wilaya ya Arumeru ,Monduli pamoja na jiji la Arusha na hawataishia hapa bali watagawa kwa wanafunzi wa kike  katika  shule zote za mkoa wa Arusha , Amesema lengo ni kuendelea kutengeneza na kugawa bure taulo hizo ziweze kuwafikia wanafunzi wengi zaidi wa kike na kuondoa changamoto walionayo

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake mwanafunzi wa shule ya sekondari ya moshono Neema Msuya ameshukuru kwa ujio wa miss world na kubainisha kuwa misaada waliopewa itawasaidia sana kwani kuna wanafunzi ambao wamekuwa hawaji shuleni pindi wanapokuwa katika kipindi cha hedhi kwani wengi wao wanaofia kuchafuka kitu kinachowasababishia kukosa masomo na kupelekea kufeli mitiani yao.

CHUO CHA SUZA CHATANGAZA WALIOCHAGULIWA KUJINGA NA CHUO MWAKA WA MASOMO 2019/2020

$
0
0
CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR KINAPENDA KUUTANGAZIA UMMA NA WOTE WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2019/2020 KWA NGAZI YA CHETI, STASHAHADA NA SHAHADA YA KWANZA KUWA, ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KATIKA AWAMU ZOTE.

INAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA CHUO www.suza.ac.tz.
IKIWA KUNA MWANAFUNZI AMECHAGULIWA NA KWA BAHATI MBAYA JINA LAKE HALIKUTOKEA KATIKA ORODHA HII, ANAOMBWA AFIKE KATIKA KAMPASI YOYOTE YA CHUO ILIYO KARIBU NAE, AU AWASILIANE

 NA MAAFISA HUSIKA KWA UTATUZI WA HARAKA.
AIDHA, CHUO KINAPENDA KUUJUULISHA UMMA KUWA, TAREHE 4/11/2019 NDIO TAREHE RASMI YA KURIPOTI CHUO.

 WANAFUNZI WOTE WALIOCHAGULIWA WANAOMBWA KUWASILI CHUONI KATIKA KAMPASI KUU (TUNGUU) SAA MBILI KAMILI ZA ASUBUHI KATIKA UKUMBI WA DR. ALI MOHAMED SHEIN.

SAMBAMBA NA HILO, ZOEZI LA UPIMAJI WA AFYA KWA WANAFUNZI WOTE WALIOCHAGULIWA AMBALO LIMEANZA TAREHE 28/10/2019 LINAENDELEA HADI TAREHE 8/11/2019 MUDA WA SAA ZA KAZI.

TANBIH
WANAFUNZI WOTE WALIOCHAGULIWA WANASHAURIWA KUJA NA NYARAKA ZOTE WALIZOTUMIWA KATIKA AKAUNTI ZAO ZA UDAHILI KWA UFAFANUZI ZAIDI ILI KUONDOWA USUMBUFU USIO WA LAZIMA.

KARIBUNI SANA.

Muungano wa Tigo na Zantel kuboresha soko la mawasiliano nchini

$
0
0
SEKTA ya mawasiliano ya simu za mkononi imekua kwa kiasi kikubwa sana katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Katika kipindi hiki cha ukuaji huu makampuni ya simu yametanua wigo wa huduma na matumizi ya simu za mkononi imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku kwa mamilioni ya Watanzania tofauti na zamani ambapo simu ilikuwa kama anasa na ni wachache tu waliweza kuwa nazo. Maendeleo haya yanazidi kukua siku hadi siku kutokana na kuongezeka kwa ubunifu katika teknolojia. 

Simu ya mkononi sasa imebadilika na kuwa si tu kifaa cha kupiga, kupokea na kutuma meseji baina ya watumiaji lakini pia imeleta mapinduzi katika namna tunavyoweka akiba ya fedha, kulipana, kulipa bili mbalimbali na kuendesha maisha yetu ya kila siku. 
Mfano wa namna ambavyo simu za mkononi zimebadili maisha yetu ni kampuni ya Tigo Tanzania. Mfumo wa Tigo Pesa wa kutuma na kupokea pesa unatupa nafasi ya kutumiana na kupokea pesa bila haja ya kwenda na kupanga foleni benki. 

Vivyo hivyo wenye maduka na biashara mbalimbali nao wametengenezewa mfumo wa Tigo Pesa Merchant ambao unawapa uwezo wa kupokea malipo kutoka wateja wote wa Tigo Pesa ambao kwa sasa ni zaidi ya watu milioni 16.   

Tigo Tanzania pia ni moja ya makampuni yanayoongoza kwa kutoa huduma ya 4G ambayo ni teknolojia yenye ina kasi zaidi katika mawasiliano nchini.

 Huduma hii inakupa uhakika wa kutazama vitu kama videos mtandaoni bila wasiwasi wa kukwama kwama au hata kufanya mikutano kwa njia ya video (conferencing)

Hata hivyo katika siku za karibuni umekuwepo wasiwasi kwamba sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi imejaa watoa huduma ambao wengi hawana tija na wasiolipa soko afya katika kuhudumia wateja. 

Hali hii inaelezwa kuleta changamoto kwa ubunifu na utoaji huduma wenye tija na viwango bora kwa wateja. 

Katika sekta nyingi za uchumi uwepo wa watoa huduma wengi huwa ni faida kwa mteja. Bahati mbaya ukweli huu haupo kwenye sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi. Utafiti unaonyesha kuwa kupunguza idadi ya watoa huduma katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi huwezesha makampuni machache yalipo sokoni kuongeza faida ambayo huwawezesha kuwekeza zaidi katika mitambo na teknolojia yenye kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake. 

Katika soko la Tanzania, siku za karibuni zimekuwepo hatua mbalimbali za kibiashara kupunguza watoa huduma ili kuongeza uwekezaji kwenye teknolojia na ubora wa huduma kwa wateja. 

Makampuni mawili ya Tigo Tanzania na Zantel yamekuwa na mjadala kuungana. 

Hatua hii ya Tigo Tanzania na Zantel kuungana ni habari njema sana kwa wateja wa Zantel. Maana yake ni kwamba sasa wateja hao wa Zantel wataweza kufurahia huduma zote ambazo sasa wateja wa Tigo Tanzania wanazipata. 

Muungano huo pia utasaidia sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini kuendelea kuwa bunifu na kutoa huduma bora kwa mamilioni ya wateja wake nchi nzima.

Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC Wafanyika JIANGSU

$
0
0
Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC kutoka Jimbo la Jiangsu umefunguliwa leo jijini Nanjing na Naibu Gavana wa Jimbo hilo Ndugu Ma Qiulin. Mkutano huo umehudhuriwa na Mabalozi 11 wa nchi za SADC na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa SADC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Miundombinu wa Sekretariat ya SADC Bi Mapolao Mokolena.

Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo Balozi wa Tanzania Mhe. Mbelwa Kairuki alitoa hotuba kwa niaba ya Jumuiya ya Mabalozi wa Nchi za SADC nchini China ambapo pamoja na mambo mengine aliyakaribisha makampuni ya SADC kuchangamkia fursa za uwekezaji katika nchi za SADC kutokana  na fursa za soko kubwa la SADC lenye idadi ya watu wanaokadiliwa kuwa milioni 345 na uchumi wa GDP 600 Billioni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miundombinu wa SADC Bi Makolane alipokuwa akitoa mada alielezea mazingira mazuri  yaliyopo ya biashara na uwekezaji katika nchi za SADC. Aidha, Mabalozi wa nchi za SADC walielezea fursa zilizopo katika nchi za SADC katika sekta za miundombinu, kilimo, viwanda; madini; utalii nk.  

Jiangsu ni jimbo la pili kwa ukubwa wa uchumi nchini China likiwa na GDP ya USD 1.2 Trillion na idadi ya watu milioni 80.  Jimbo hilo linaongoza nchini China katika sekta ya viwanda. Makampuni kutoka Jimbo la Jiangsu yamefanya uwekezaji nchini Tanzania katika sekta ya viwanda.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Afrika na wenyeji China mara baada kuhitimisha mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC uliofanyika jimbo la Jiangsu nchini China
Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC ulifanyika Jiangsu, China
Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki (mstari wa mbele katikati) akifuatilia Mkutano wa kuvutia uwekezaji uliokuwa ukiendelea 
Wajumbe kutoka nchi za SADC na Wenyeji wao China wakifuatilia Mkutano uliokuwa ukiendelea

ACHA,TRW KUWAPELEKA WAANGALIZI 215 UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2019, KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA

$
0
0

Na Ripota Wetu, Michuzi TV

ASASI mbili za kiraia za Action for Change(ACHA) na The Right Way (TRW) zinatarajia kupeleka waangalizi jumla ya 215 katika Wilaya zote za Tanzania Bara kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba mwaka huu.

Pia imeelezwa ACHA na TRW kwa pamoja wanadhamiria kuendesha mpango wa pamoja wa kutoa elimu ya uraia na uangalizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa mwaka 2019 sanjari na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ili kuzifanya chaguzi hizo kuwa huru zaidi, za haki za kuaminika Tanzania.

Akizugumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020,Ofisa Mradi wa ACHA Jackson Sikahanga amesema wanatarajia kupeleka waangalizi hao kuhakikisha wanafuatilia mchakato mzima wa uchaguzi wa Serikali za mitaa.

"ACHA TRW tuna matarajio kwamba uchaguzi huu utakuwa huru, haki , kuaminika , tulivu na wenye amani.Pia utakuwa wa uwazi na utakaoshirikisha makundi maalumu , mfano watu wenye ulemavu, wanawake, vijana na wazee.

"Ni dhahiri kuwa uangalizi wa uchaguzi huu utafanyika pia kwa kutumia vifaa vya teknolojia ya kisasa na mafunzo bora yatakayotolewa kwa wakati katika nyanja zote za michakato ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi,"amesema na kuongeza uangalizi na umakini huo katika utoaji taarifa vitabainisha maeneo yenye ucdhaifu kwa marekebisho kwa siku zijazo

Sikahanga amesema ACHA na TRW zinalenga kuona mchakato wa uchaguzi unaofuata viwango vya kitaifa na kimataifa, kama ambavyo Tanzania imeridhia na zile zilizopo kwenye sheria za manispaa , kanuni na miongozo kutoka vyombo mbalimbali vya kusimamia uchaguzi ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC).

Pia amesema uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu mwaka 2020 ni fursa nyingine kwa Watanzania kushuhudia ukuaji wa utawala wa demokrasia. Aidha amesema ipo haja ya ushiriki mpana wa wananchi wote katika mchakato wa uchaguzi, kaunzia kipindi kabla ya uchaguzi kwa mfano uandikisha waji wa wapiga kura, elimu ya mpira kura na uteuzi katka vyama.

"Mchakato huu unahitaji mfumo wa mwenendo thabiti wa elimu kwa wananchi katika zoezi zima, ambalo litafanya elimu kwa mpiga kura kuwa thabiti na wenye tija , mwamko huu wa wananchi kupitia elimu kwa umma na programu ya mpiga kura , ambayo imeandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwadaidia wananchi kutambua kuwa ushiriki katika uchaguzi ni haki yao,"amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TRW Rhoda Kamungu amesema upo ushahidi usiojitosheleza unaunga mkono umuhimu wa vyombo katika kuhakikisha Serikali inawajibika juu ya utawala bora ,haki na misingi yote ya haki za binadamu na kwa wananchi wake.

"Ni jukumu letu kuwajulisha wananchi kama nguzo muhimu kupitia vyombo vya habari katika kutoa jukwaa jumuishi la mjadala wa umma na majadiliano kuhusu kuhamasisha mijadala kwa kuzingatia Katiba,sheria,sera ,taratibu na miongozo.Utafiti unadhihirisha kuwepo idadi kubwa ya wapiga kura wasiofahamu kuhusu mchakato na utaratibu wa uchaguzi,"amesema.

Kuhusu kwanini elimu ya uraia, elimu ya mpiga kura na ungalizi ni muhimu, Kamungu amejibu kuwa ACHA na TRW kwa pamoja wanatamani kuona mchakato wa uchaguzi ambao unaongozwa na wananchi, shirikishi , wenye uwazi , huru na haki. "ACHA na TRW tutatoa elimu ya uraia, mpiga kura na uangalizi wa michakato ya uchaguzi kwa kuzingatia vigezo vilivyopo.
 Mkurugenzi wa The Right Away ,Rhoda Kamungu  akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam,mambo mbalimbali ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi mkuu,sambamba na namna  Asasi hizo zilivyojipanga kupeleka waangalizi  Wilaya zote za Tanzania Bara,ambapo ameeleza kuwa waangalizi wa Muda mrefu  wapatao 215 watapewa jukumu hilo ngazi ya majimbo na Waangalizi wa muda mfupi wapatao 3600 watapelekwa kwenye vituo mbalimbali vya uangalizi nchi nzima.
 Ofisa Mradi wa Action for Change   (ACHA) Jackson Sikahanga akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu  namna walivyodhamiria kuendesha mpango wa pamoja wa kutoa elimu ya uraia,na uangalizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa mwaka 2019 sanjari na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ili kuzifanya chaguzi hizo kuwa huru zaidi, za haki na kuaminika Tanzania.



 Ofisa Mipango wa ACHA na TRW akitolea ufafanuzi wa baadhi ya mambo yalitozungumza na Watangulizi wake kwenye mkutano huo na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana leo OKtoba 29,2019 katika Ukumbi wa TAMISEMI Jijini Dodoma.   
 (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MKUU WA MKOA SINGIDA DKT. REHEMA NCHIMBI ATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akizungumza na wananchi wenye kero mbalimbali dhidi ya serikali mjini hapa jana, ambao walimuonesha mabango ya kero hizo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani hapa mapema mwezi huu.
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani)
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani)
 Mkutano ukiendelea
 Mama akitoa kero yake kwa maofisa wa idara za serikali mkoani Singida katika mkutano huo.
Maofisa wa idara za serikali mkoani Singida, wakipokea kero za wananchi hao (hawa pichani
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amekutana na wananchi wenye kero mbalimbali dhidi ya serikali ambao walimuonesha mabango ya kero hizo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani hapa mapema mwezi huu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kuyaona na kupokea mabango hayo alimuagiza mkuu wa mkoa kutatua changamoto za wananchi hao ambapo jana alikutana nao akiwa na viongozi wa idara za serikali kwa ajili ya kuwasikiliza na kutafuta njia ya kuzitatua kwa pamoja.
Hata hivyo ilitokea sintofahamu baina ya wananchi hao na mkuu wa mkoa huo pale walipotakiwa kusikilizwa na viongozi wa idara za serikali ambao walishindwa kuzitatua hapo awali na kufikia uamuzi wa kumuonesha mabango waziri mkuu.
Pamoja na sintofahamu hiyo baadae wananchi hao walikubali kusikilizwa  ambapo mkuu huyo wa mkoa aliwagiza viongozi hao hasa wa Manispaa ya Singida kupanga tarehe za kukutana na wananchi hao wengi wakiwa na malalamiko ya migogoro ya ardhi.

Baadhi ya malalamiko waliyoyatoa kwa Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ni pamoja na madai ya fidia ya viwanja namba 23 na eneo lililoko nyuma ya moja ya kiwanja cha Ginnery, kupinga rufaa ya kesi ya ardhi iliyotoleea hukumi na baraza la ardhi la wilaya ya Singida.
Madai mengine ni kiwanda cha mafuta ya alizeti kumilikiwa na wajanja wachache, kutokamilika kwa mradi wa ujenzi wa matundu ya vyoo na mabweni shule ya msingi Mtinko tangu mwaka 2017 na mkopo wa Saccos fedha kutoka NSSF 160 milion zilizokuwa wakopeshwe wanachama wamekopeshwa vigogo kutoka Singida mjini.
Mkazi wa Kata ya Mwankoko Rochard Katyani ambaye ana malalamiko ya fidia ya ardhi aliomba serikali kumaliza malalamiko ya migogoro ya ardhi ambayoimedumu kwa mda mrefu.
Kati ya migogoro 27 iliyowasilishwa kwa waziri mkuu kwa njia ya mabango migogoro zaidi ya 20 inahusu masuala ya ardhi hasa fidia baada ya ardhi za wahusika kudaiwa kuchukuliwa na serikali kwa matumizi mengine.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images