Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

TAARIFA KWA UMMA; KITUO CHA SANAA NA UTAMADUNI KWA VIZIWI TANZANIA( KISUVITA )

$
0
0
KISUVITA NI NINI?

Kituo cha Sanaa na Utamaduni kwaViziwi Tanzania, (KISUVITA), ni asasi isiyo ya kiserikali na isiyolenga faidai na yoongozwa na viziwi kwa ajili ya viziwi, ambao imejikita katika kuimarisha maisha ya wanachama viziwi kupitia sanaa, utamaduni, mawasiliano ya lugha ya alama na uwezeshaji wa kiuchumi.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka2007, KISUVITA imeendeleza vipaji vya viziwi katika Sanaa na utamadun inakusaidia kutengeneza ajira na fursaza mafunzo mbalimbali kwa viziwi nchini Tanzania

TASNIA YA UREMBO NA MITINDO

Kwa kutambulika wajibu wake huo, ndani na nje ya nchi, KISUVITA imekuwa ikipokea mialiko ya kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa ya urembo na mitindo. Hata hivyo, changamoto ya rasilimali fedha kwa kipindi kirefu tangu ianzishwe ili sababisha ilishindwe kuyashiriki hadi ilipoweza kufanya hivyo mara ya kwanza mwaka huu.

Shukrani za kufanikiwa kushiriki mara ya kwanza tena katika mashindano makubwa ya viziwi ya urembo na mitindo katika ngazi ya kimataifa; Miss & Mister Deaf International yaliyofanyika mjini St. Petersburg, Urusi Julai 5- 17, 2019 zinawaendea wadau kadhaa hasa Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Mali asili na Utalii, Wizara ya Habari na Michezo bila kusahau Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Ushirikiano huo si tu ulituwezesha kushiriki nakufanya vyema baada ya mmoja wa warembo wetu Winfrida Brayson kuingia bora katika mashindano hayo na kushinda kipengele cha utamaduni katika shindano la onesho la mavazi bali pia kung’ara katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni Afrika Mashariki (JAMAFEST) lililomalizika mwishoni mwa Septemba 2019.

Kwa kushiriki kwao, warembo wetu walipata fursa si tu ya kusafiri na kukutana na viongozi kadhaa wa dunia na kuitangaza nchi yetu, bali pia kuwa kiwakilishi na mfano mzuri katika kuhamasisha maadili ya kielimu, kijamii na kiuchumi kwa wanawake na wanaume kupitia tasnia hii popote pale walipo pamoja na kujenga mwamko kwa jamii kuhusu Kiziwi, vipaji na uwezo wao kuleta maendeleo kwa jamii na Taifa lao.

Ushiriki huu ulikuwa wenye wenye tija kwa washiriki wetu binafsi, jamii ya viziwi na Tanzania kwa ujumla, ambao matunda ataonekana siku za usoni. Warembo na waandaaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika na kimatraifa wamepanga kuzuru nchini na hivyo kutoa fursa ya kuchangia kulitangaza Taifa ikiwa mosekta ya utalii. Si hivyo tubali itakuza biashara zetu kwa kuzitangaza kampuni mbalimbali zitakazojitokeza kudhamini matukio ya nayohusu viziwi katika tasnia hii adhimu.


KIFUATACHO BAADA YA KUCHOMOZA KATIKA TASNIA HII

• KISUVITA imeanzisha Shindano la Miss & Mister viziwi Tanzania, ambao watapata tiketi ya kushiriki Miss & Mister viziwi Afrika mjini Nairobi, Kenya mwaka ujao, kabla ya kushiriki Miss & Mister viziwi Dunia ni nchini Marekani

• Inapanga kuwa mwenyeji wa mashindano ya Miss na Mister viziwi ngazi ya Afrika na Dunia siku za usoni

USHIRIKIANO WAKO NI MUHIMU

Hata hivyo, mipango na mikakati hiyo, ambayo si t u itaisaidia jamii ya viziwi bali pia Taifa kwa ujumla wake, itawezekana tukiwa ushirikiano wa wadau mbalimbali kuanzia serikalini hadi sekta binafsi hasa kupitia udhamini.

Kwa sababuhiyo, tunaomba wadau hasa kampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini mashindano au ushiriki wetu katika mashindano ya kimataifa;

• Miss & Mister Deaf Tanzania itakayofanyika mjini Dar es Salaam (Februari 2020)-Dar es salaam

• Miss & Mister Deaf Afrika mjini Nairobi, Kenya (Juni,2020)

• Miss & Mister Deaf International nchini Marekani (Julai,2020)

Katika shindano tutakalo andaa Februari 2020 mjini Dar es Salaam likishirikisha vijana wa kike na kiume ili kupata wa wakilishi wetu, pia litashuhudiwa na warembo na waandaaji wa kimataifa kutoka ndani na nje ya Afrika wakiwamo waandaaji wakuu wa Miss & Mister Deaf International wa Marekani.


FAIDA ZA UDHAMINI

Kuna faida nyingi za kudhamini mashindano haya, kwa kutaja chache ni pamoja na;

• Kulitangaza jina na nembo ya kampuni kupitia vyombo vya habari ndani na nje ya nchi

• Kuhesabiwa ukarimu unaochochea mahusiano mema na jamii hasa watu wenye ulemavu

• Usamaria wema wa kusaidia jamii ya watu wenye ulemavu nchini

• Kuwa sehemu ya mafanikio wachangiaji wa mafanikio ya watu wenye ulemavu hasa katika awamu hii, ambayo Serikali inawapa kipaumbele.

Faida hizo moja kwa moja si tu zitakuza jina la kampuni bali pia kuongeza mapato ya kampuni katika dunia hii ya ushindani wa kibiashara.

Asante sana kwa ushirikiano, wote mnakaribishwa.


Habibu Mrope
Mkurugenzi Mkuu
Kisuvita
+255688744482 -SMS
kisuvita@yahoo.com











BODI YA MIKOPO YATANGAZA AWAMU YA KWANZA WALIOPATA MKOPO ELIMU YA JUU

$
0
0
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675 wa Mwaka wa Kwanza kwa mwaka wa masomo 2019/2020 waliofanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya TZS 113.5 bilioni.

Katika mwaka huu wa masomo, Serikali imetenga TZS 450 bilioni zinazolenga kuwanufaisha jumla ya wanafunzi 128,285. Kati yao, zaidi ya wanafunzi 45,000 ni wa mwaka wa kwanza na wengine 83,285 ni wenye mikopo wanaoendelea na masomo. Mwaka 2018/2019, fedha zilizotengwa na kutolewa zilikua TZS 427.5 bilioni na ziliwanufaisha jumla ya wanafunzi 123,283 wakiwemo 41,285 wa mwaka wa kwanza.

Akizungumza na wanahabari leo (Alhamisi, Oktoba 17, 2019) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, amesema katika orodha hiyo, wanaume ni 19,632 (64%) na wanawake ni 11,043 (36%).

Badru amefafanua kuwa waombaji mikopo wafungue akaunti zao binafsi (SIPA – Student’s Individual Permanent Account) walizofungua kuomba mkopo kupitia mfumo wa HESLB (olas.heslb.go.tz) ili kupata taarifa za mikopo. 

Makundi Maalum –Yatima, Wenye ulemavu n.k

Kuhusu makundi maalum yenye uhitaji, Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema katika orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675, wapo wanafunzi 6,142 ambao ni yatima au wamepoteza mzazi mmoja, wenye ulemavu 280 na wengine 277 wanaotoka katika kaya zinazofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

“Katika makundi maalum pia tuna wanafunzi 1,890, sawa na asilimia 6 ya wanafunzi 30,675 wa awamu ya kwanza ambao walisoma shule binafsi lakini kutokana na hali duni ya uchumi, walifadhiliwa na walithibitisha kwa kuweka nyaraka sahihi,” amesema Badru.

Kutangazwa orodha ya awamu ya pili

Kuhusu awamu ya pili, Badru amesema HESLB kabla ya Oktoba 25 ya wiki ijayo baada ya kukamilishwa kwa uchambuzi wa maombi ya mikopo kutoka kwa wanafunzi waliochelewa kukamilisha taratibu za udahili au kuchelewa kurekebisha maombi yao ya mkopo mtandaoni.

Wito kwa wanafunzi
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchambuzi na Upangaji Mikopo wa HESLB Dr. Veronica Nyahende amewataka wanafunzi ambao taarifa zao hazijakamilika, kukamilisha ili wenye sifa wapangiwe mkopo.

“Kuna kama wanafunzi 1,000 ambao maombi yao hayajakamilika, watumie muda huu hadi tarehe 19 kukamilisha ili wenye sifa nao tuwapangie mkopo,” amesema.


MAJINA YA WALIOPATA MKOPO ELIMU YA JUU HAYA HAPA

$
0
0
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675 wa Mwaka wa Kwanza kwa mwaka wa masomo 2019/2020 waliofanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya TZS 113.5 bilioni.

Akizungumza na wanahabari leo (Alhamisi, Oktoba 17, 2019) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, amesema katika orodha hiyo, wanaume ni 19,632 (64%) na wanawake ni 11,043 (36%).


Badru amefafanua kuwa waombaji mikopo wafungue akaunti zao binafsi (SIPA – Student’s Individual Permanent Account) walizofungua kuomba mkopo kupitia mfumo wa HESLB (olas.heslb.go.tz) ili kupata taarifa za mikopo. 

Mgogoro wa mudamrefu wa kugombea mali katika familia ya marehemu bilionea erasto Msuya wachukuwa sura mpya

$
0
0
Na Woinde shizza Michuzi Tv , Arusha 

Mgogoro wa Muda mrefu uliokuwa ukifukuta baina ya familia za Marehemu bilionea Erasto Msuya wa kugombea Mali umechukua sura mpya mara baada ya serikali ya Mkoa kuingilia kati kwa lengo la kupata suluhu ya kudumu nje ya Mahakama.

Mgogoro huo ambao umedumu kwa takribani miaka 7 tangia kifo cha Marehemu mwaka 2013, upande wa wazazi wa marehemu Erasto msuya na upande wa Mke wa marehemu  Erasto aitwaye Miriam  Erasto ambaye kwa sasa yupo mahabusu Gerezani kwa tuhuma ya mauaji ya WiFi yake,wameshindwa kuelewana juu ya rasilimali zilizoachwa na marehemu.

Akiongea na familia hizo katika nyumba aliyokuwa akiishi Marehemu Erasto iliyopo Kwa Iddy wilayani Arumeru,Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro amewataka watoto wa marehemu  waliokuwa wameikimbia nyumba ya marehemu baba yao wakihofia kuuawa kurejea katika nyumba hiyo kuanzia Leo wakati wakiendelea na utatuzi wa mtafaruku uliopo.

Aidha Muro amezitaka pande hizo mbili kufika ofisini kwake siku ya jumatatu SAA 4 asubuhi wakiwa wameambatana na vielelezo mbalimbali ili kufikia mwafaka wa mgogoro huo nje ya Mahakama.

"Si nia ya serikali kuingilia jambo lililopo mahakamani ila kama serikali tunamamlaka ya kusuluhisha jambo iwapo pande zote zipi tayari kuketi kwani suala la kutafuta msindi mahakamani si suluhu ya kuleta amani" Amesema Muro

Akiongea mgogoro huo mtoto mkubwa wa marehemu , aitwaye Kervin Erasto  alimweleza mkuu huyo wa Wilaya kuwa wazazi wa marehemu baba yake( bibi) aitwaye Ndeshu Msuya na babu yake aitwaye Elisaria Elia Msuya pamoja na shangazi zake wanataka kumpokonya Mali za Marehemu baba yake .

Akijibu tuhuma hizo,Mama wa marehemu Erasto,Ndeshu Msuya amesema kuwa wao kama wazazi wa marehemu Erasto hawana nia ya kutaka urithi wa mali yoyote ya marehemu  mtoto wao ila wanasikia uchungu kuona Mke wa Erasto akiuza Mali ovyo za Marehemu mtoto wao ili kumaliza suala la kesi ya mauaji inayomhusu wakati ugawanyo wa Mali bado haujafikiwa.

Mama huyo amedai kuhofika watoto wa marehemu kupoteza rasilimali hizo kutokana na Mali hizo ndugu wa Mke  kujimilikisha ambao wamejipa kipaumbele kusimamia jambo ambalo linawapa mashaka kwamba huenda watoto hao wakadhulumiwa.

Naye baba wa marehemu aitwaye Elisaria Msuya amesema  madai yanayotolewa kuwa amejimilikisha mgodi wa marehemu Erasto hayana msingi wowote kwani wakati anamzaa Erasto alikuwa anamiliki migodi huko Mererani na ubilionea wa Msuya umetokana na yeye kumpa mgodi wa kuchimba madini ya Tanzanite.

Marehemu Erasto alifariki agosti,7mwaka  2013 kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 eneo la Mijohoroni,wilaya ya Hai ,mkoani Kilimanjaro na watu ambao baadae walikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela Mara baada ya Mahakama kuwatia hatiani.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro (pili kushoto) akiwa na familia ya marehemu bilionea Erasto Msuya

SERIKALI YATENGA BILIONI 450 KWAAAJIRI YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru

KATIKA  mwaka wa masomo wa 2019/2020, Serikali imetenga TZS 450 bilioni zinazolenga kuwanufaisha jumla ya wanafunzi 128,285. Kati yao, zaidi ya wanafunzi 45,000 ni wa mwaka wa kwanza na wengine 83,285 ni wenye mikopo wanaoendelea na masomo. Mwaka 2018/2019, fedha zilizotengwa na kutolewa zilikua TZS 427.5 bilioni na ziliwanufaisha jumla ya wanafunzi 123,283 wakiwemo 41,285 wa mwaka wa kwanza.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675 wa Mwaka wa Kwanza kwa mwaka wa masomo 2019/2020 waliofanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya TZS 113.5 bilioni.

Akizungumza na wanahabari leo (Alhamisi, Oktoba 17, 2019) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, amesema katika orodha hiyo, wanaume ni 19,632 (64%) na wanawake ni 11,043 (36%).

Badru amefafanua kuwa waombaji mikopo wafungue akaunti zao binafsi (SIPA – Student’s Individual Permanent Account) walizofungua kuomba mkopo kupitia mfumo wa HESLB (olas.heslb.go.tz) ili kupata taarifa za mikopo. 

Makundi Maalum –Yatima, Wenye ulemavu n.k
Kuhusu makundi maalum yenye uhitaji, Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema katika orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675, wapo wanafunzi 6,142 ambao ni yatima au wamepoteza mzazi mmoja, wenye ulemavu 280 na wengine 277 wanaotoka katika kaya zinazofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

“Katika makundi maalum pia tuna wanafunzi 1,890, sawa na asilimia 6 ya wanafunzi 30,675 wa awamu ya kwanza ambao walisoma shule binafsi lakini kutokana na hali duni ya uchumi, walifadhiliwa na walithibitisha kwa kuweka nyaraka sahihi,” amesema Badru.

Kutangazwa orodha ya awamu ya pili
Kuhusu awamu ya pili, Badru amesema HESLB kabla ya Oktoba 25 ya wiki ijayo baada ya kukamilishwa kwa uchambuzi wa maombi ya mikopo kutoka kwa wanafunzi waliochelewa kukamilisha taratibu za udahili au kuchelewa kurekebisha maombi yao ya mkopo mtandaoni.

Wito kwa wanafunzi
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchambuzi na Upangaji Mikopo wa HESLB Dr. Veronica Nyahende amewataka wanafunzi ambao taarifa zao hazijakamilika, kukamilisha ili wenye sifa wapangiwe mkopo.

“Kuna kama wanafunzi 1,000 ambao maombi yao hayajakamilika, watumie muda huu hadi tarehe 19 kukamilisha ili wenye sifa nao tuwapangie mkopo,” amesema.

RAIS MAGUFULI KUWA MGENI RASMI UFUNGUZI WA MAONESHO YA UTALII (SITE)

$
0
0
Na Zainab  Nyamka, Globu ya Jamii

Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maonesho ya Swahili International Tourism Expo (SITE) kesho Ukumbi wa Mlimani City.

Maonesho hayo yatakayoanza leo Oktoba 18 yatamalizika Oktoba 20 mwaka huu yakitarajia kuwa na kampuni za waoneshaji 210 kutoka nchi 60, Jumla ya mawakala wa utalii na waandishi wa habari takribani 333.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Aldof Mkenda amesema lengo la maonesho ya SITE ni kuwaunganisha wafanyabiashara wadogo na wa kati wa utalii Tanzania pamoja na wafanyabiashara kutoka masoko makuu ya utalii duniani.

Mkenda amesema, kwa mara ya kwanza maonesho hayo yalianza mwaka 2014, yakiandaliwa na Bodi ya Utalii Nchini (TTB) na yamekuwa yanakuwa kwa kasi kila mwaka.

Mkenda amewashukuru balozi za Tanzania nje ya nchi kwani wameweza kufanya kazi kubwa sana ya kufanya usaili wa mawakala wa utaliu pamoja na waandishi wa habari watakaoshiriki kwenye maonesho hayo kutoka nchi wanazosimamia.

"SITE imeendelea kupata mafanikio makubwa bapo ni jambo la kujivunia kama Wizara, wadau wa sekta ya utalii  na nchi kwa ujumla kuona onesho hili limeendelea kukua mwaka hadi mwaka na kuvutia washiriki wengi kutoka kila kona duniani," amesema Mkenda

Aidha, ameeleza kuwa TTB imeandaa ziara kwa ajili ya mawakala wa utalii na waandishi wa habari wa kimataifa Oktoba 21, kwenda kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya asili ikiwemo Hifadhi ya Taifa Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.

Maeneo mengine ni Fukwe za Tanga na mapango ya Amboni, Misitu ya Magoroto, Mlima Kilimanjaro na miradi ya utalii wa utamaduni katika Mkoa wa Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Riaha na Mji wa Iringa. Pia Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa na Mikumi, Visiwa vya Zanzibar na Mafia.

Pia, katika maonesho hayo kutakuwa na semina  zitakazoendeshwa na wataalamu waliobobea kwenye masuala ya utalii kukiwa na mada mbalimbali.

INAKULETEA VICHWA VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 18,2019

DHAMIRA YA SERIKALI NI KUHAKIKISHA MTAMBO WA KUZALISHIA UMEME HALE UNAREJEA KWENYE HALI YAKE YA KAWAIDA-KALEMANI

$
0
0
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kushoto katikati akionyeshwa kitu ni Mhandisi Mkuu wa Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Pangani Hydro System Jackline Mtolela wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo hicho
 Mhandisi Mkuu wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Pangani Hydro System Jackline Mtolela  kulia akimuonyesha kitu Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani kushoto wakati wa ziara yake kwenye kituo hicho
Mhandisi Mkuu wa Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Pangani Hydro System Jackline Mtolela  kushoto akiwa na  Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani kulia chini ya mgodi wa Hale  wakati wa ziara yake kwenye kituo hicho
 Sehemu ya mitambo iliyopo kwenye kituo hicho cha kuzalisha umeme
Meneja wa Tanesco mkoa wa Tanga Julius Sabu kulia akipitia taarifa wakati wa ziara hiyo 

WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amesema serikali itahakikisha mtambo wa kuzalisha umeme wa hale unarejea kwenye hali yake ya kawaida ili uweze kutoa megawatts 21 kama ilivyosanifiwa na kuanza kufanya kazi mwaka 1964.

Dkt Kalemani aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme cha Hale wilayani Korogwe mkoani Tanga ambapo pia alitembelea mgodi wa kufua umeme.

Akiwa kwenye kituo hicho Waziri Kalemani alisema kwamba ametembelea mradi huo kwenye maeneo makubwa mawili ya mashine na trasfoma huku akieleza kwamba kwenye mashine mbili ambazo zipo eneo hilo hazifanyi kazi kwa sasa maanake hatupati megawati hata moja kutoka kwenye mtambo huo.

Alisema kwamba ingawa mtambo mmoja unafanyiwa marekebisho kwa maana ya kufungwa vifaa na wataalamu hivyo watahakikisha unakamilika na tayari alikwisha kutoa maekelezo kazi hiyo ikamilike ili megawatts 10.5 zirejee.

“Hapa katikati mlikuwa mnapata megawatts 8 zilikuwa hazifiki hata kumi ..wakati huu matengenezo makubwa yanafanyika hivyo ni matumaini yake kwamba hata mkandarasi ambaye anatafutwa kwa ajili ya kufanya matengenezo ya mitambo yote miwili utafanyika haraka “Alisema Dkt Kalemani 

Hata hivyo alisema lazima wahakikisha wanakuwa na umeme wa kutosha ambao utapatikana kwenye mradi huo ambao ni wa miaka mingi kwani ulijengwa mwaka 1964 hiyo mitambo kila wakati lazima ifanyiwe ukarabati hasa wakati unapopita.

“Mwaka juzi nilipita hapa na kutoa maekelezo kutokana na kuwepo dalil za mitambo iliyochakaa nikawaambia muanze utaratibu wa kufanya marekebisho ya mitambo yote wakati wa ziara yangu kupita kwenye mitambo ni kujihakikisha umeme unapatikana na wa uhakika”Alisema

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mhandisi Mkuu wa Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Pangani Hydro System Jackline Mtolela alimueleza Waziri Kalemani kwamba hali ya mitambo iliyopo kwnye kituo hicho ni chakavu ya mwaka 1964ina hitaji matengenezo makubwa.

Alisema kutokana na hali hiyo hivi sasa wapo kwenye mchakato wa kupata wakandarasi ili waweze kufanya ukarabati kwani kwa sasa wana uwezo wa kuzalisha megawatts 10.5 kwa mashine moja ila kutokana na uchakavu wa mashine wanazalisha megawatts 8 lakini mashine ipo kwenye matengenezo.


WAZEE TUNU YA TAIFA,TUWATUNZE- KIKWETE.

$
0
0

Na Shushu Joel

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete amewataka vijana nchini kuwalinda,kuwatunza na kuwajali Wazee ambao ndiyo Walezi wa Jamii yetu.

Ombi hilo amelitoa alipokuwa akizungumza na baadhi ya Wazee wa kata ya Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

"Wazee wamelipigania taifa hili , na sasa ni Muda muafaka wa sisi kupambana ili kulinda maslahi yao. Wazee hawa walipambana sana kutufikisha tulipo leo. Amani tunayoiona na maendeleo haya ni kazi waliyoasisi na hivyo juhudi zao zimetufanya sisi kuwa na amani kubwa na kuwa Mfano wa kuigwa na baadhi ya mataifa"Alisema Kikwete.

Aliongeza kuwa serikali ya Tanzania imejipanga ili kuhakikisha wazee wanaenziwa na kunufaika na nchi yao kutokana na kile walichokifanya wakati wa ujana wao. Wamekuwa mstari wa mbele kushauri hivyo amewataka vijana kuongea na wazee mara kwa mara kwani wanaushauri mzuri juu ya mwenendo wa maisha yetu kama vijana.

"Vijana wengi tumeshindwa kujua na kutambua historia ya wazee wetu kutokana na kutokuwa karibu nao ili kujua jinsi wao walivyokuwa wakiishi na hivyo kujifunza toka kwao", Alisema 

Kwa upande wake Mzee Said Bwilingu (87) alisema kuwa amempongeza Mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete Kwa jinsi anavyowajali wazee Kwa kuwatembelea kila wakati na kuwajulia hali zao."Hivyo wazee tumefarijika sana kutembelewa na mjukuu wetu . Sisi tuliishi na Wazee wake na hivyo Analolifanya mbunge ni kufuata mwenendo ulioasisi na wazee wake."

Aliongeza kuwa amani ya nchi yetu inatokana na jinsi tulivyokuwa na umoja na mshikamano wenye nia ya kujenga taifa letu la Tanzania. Wazee musiwatenge. Watembeleeni ili muweze kufaidika na mawazo yao japo vijana mnaona wa kizamani.

Aidha mzee huyo alisema kuwa anafarijika kuona jimbo la chalinze linavyozidi kupata maendeleo makubwa ambayo kipindi hicho ilikuwa ni historia lakini kwa sasa mambo mengi yanafanyika na kuleta neema kwa wananchi. 


Pia amempongeza mbunge Ridhiwani Kikwete kwa ufanisi wake katika kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kwani wakati wetu maji,umeme,huduma za afya na miundombinu vilikuwa ni changamoto kubwa.

Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na baadhi ya wazee

SAMIA -SERIKALI HAITOMVUMILIA ATAKAETHUBUTU KUINGIZA BIDHAA FEKI AMA KUKWAMISHA UWEKEZAJI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

SERIKALI imesema haitomvumilia mtu yeyote atakaethubutu kukwamisha ujenzi wa viwanda ,ikiwa ni pamoja na kuzalisha ama kuingiza bidhaa bandia zinazochafua taswira ya viwanda vya ndani ya nchi na sifa ya nchi kijumla.

Aidha imezielekeza mamlaka za ukaguzi na udhibiti wa ubora ikiwemo Shirika la viwango Tanzania(TBS )na NEMC kutoa huduma stahiki kwa wawekezaji pasipo urasimu.

Akifungua maonyesho ya mara ya pili ya viwanda kwa niaba ya makamu wa Rais ,katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani, Naibu Waziri Wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ,Stella Manyanya alisema haitowezekana kuwafumbia wale wachache wanaokwamisha juhudi za serikali za kukimbilia uchumi wa kati.

Alieleza ,serikali pia inaangalia utitiri wa kodi unaotozwa na tozo zinazotozwa na mamlaka za ukaguzi na udhibiti ubora unaolalamikiwa na wawekezaji."Hatua ya ushuru na tozo kuzifuta zimechukuliwa ,kati ya 114 zinazotozwa na taasisi za ukaguzi na udhibiti wa ubora wa bidhaa ,ambapo mwaka 2019 tozo 54 zimefutwa "

Stella alifafanua, licha ya viwanda kuzalisha bidhaa zenye viwango na ubora zinakumbana na ushindani sokoni.Wakati huo huo ,alibainisha serikali inaendelea kuboresha reli na kujenga reli ya kisasa ili kusafirisha mizigo kwa kasi,kununua ndege kubwa kwaajili ya mizigo na kurahisisha sekta ya usafirishaji .

Pia Stella alisema, kuwekeza upatikanaji wa umeme wa uhakika vijijini na mijini na kuongeza ufanisi na utoaji mizigo bandarini.Awali mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM ,mkoani Pwani Ramadhani Maneno alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,ameonyesha dhamira ya kufufua sekta ya viwanda na kupigania kuinua sekta ya uwekezaji.

Alisema kauli ya mh.Rais imetekelezwa kwa vitendo mkoani Pwani na mkuu wa mkoa huo ameitendea haki utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema,kauli mbiu ya maonyesho hayo ni  IJENGE TANZANIA,WEKEZA PWANI MAHALI SAHIHI KWA UWEKEZAJI .

Alisema, mkoa huo umevunja rekodi ya kuinua sekta ya uwekezaji na ujenzi wa viwanda zaidi ya 1,000 na kati ya hivyo 300 vimejengwa katika awamu ya tano na hii imetokana na kutokuwa na urasimu kwa wawekezaji na kutenga maeneo mengi kwa ajili ya viwanda.

"Malengo ya maonyesho haya ni kuonyesha kwamba mkoa umedhamiria kuwa ukanda wa viwanda,wenye viwanda kupata masoko ya uhakika,kupanua wigo wa soko la ndani ya mkoa kufikia kimataifa na ,kuvutia wawekezaji wapya"alisema Ndikilo.Ndikilo alisema hali ya ushiriki imeimarika tofauti na mwaka jana ambapo mwaka huu wamefikia washiriki 329 na mwaka uliopita walikuwa 166.

Hata hivyo Ndikilo alibainisha, ,maonyesho hayo yataambatana na kongamano la uwekezaji litakalofanyika octoba 19 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Wazir Mkuu Kassim Majaliwa.Naibu Wazir wa Nishati,Subira Mgalu anatambua kuna maeneo yenye tatizo la kukatika umeme ila wanafanya kila linalowezekana kuwe na umeme wa uhakika.

Alisema tatizo hilo litakuwa historia baada ya kukamilisha miradi mikubwa ya Peri urban,ujazilizi ,stigo huko Rufiji wa megawatt 2,100 ili kupunguza tatizo la umeme maeneo ya vijijini na kwa wawekezaji.Waratibu wa maonyesho hayo ni kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) pamoja na mamlaka ya maendeleo ya viwanda (TANTRADE) .

Maonyesho hayo yanatarajia kufungwa octoba 23 mwaka huu na Waziri Mkuu Mstaafu ,Mizengo Pinda.

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA 18 WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NCHI ZA AFRIKA NA NORDIC KUANZIA TAREHE 7-8 NOVEMBA 2019

$
0
0
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic (Norway, Denmark, Finland, Sweden na Iceland) unaotarajiwa kufanyika tarehe 08 Novemba 2019 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano huu kufanyika hapa nchini tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Msagariki, mkutano huu unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki takribani 250 ambao kati yao thelathini na nne (34) ni Mawaziri wa Mambo ya Nje akiwemo Mhe. Prof. Palamagamba J.A.M. Kabudi (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (pichani juu).
Kadhalika, Mabalozi wa nchi shiriki za Afrika katika nchi za Nordic, Mabalozi wa nchi za Nordic hapa nchini, watendaji kutoka Wizara za Mambo ya Nje za nchi shiriki, wawakilishi wa taasisi za biashara na uwekezaji na Wafanyabiashara za hapa nchini wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, lengo la kuanzishwa kwa mkutano huu, ambao kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka 2000, ilikuwa ni kutoa nafasi kwa nchi za Nordic na nchi chache za Afrika marafiki zao wa karibu, kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili, kuainisha vipaumbele katika ushirikiano huo na kuweka mikakati ya pamoja ya kutekeleza vipaumbele hivyo. Nchi za Afrika na Nordic zimekuwa zikipokezana uenyeji wa mikutano hii kila mwaka. Mwaka 2017, mkutano huu ulifanyika Abuja, Nigeria na mwaka 2018 ulifanyika Copenhagen, Denmark na mwaka huu, utafanyika Tanzania.
Kwa mwaka huu, taarifa hiyo imesema. mkutano huu utajadili namna ya kuimarisha mahusiano yenye tija kwa maendeleo ya nchi washiriki hususan namna ya kukuza ushirikiano kwenye sekta ya biashara na uwekezaji kwa maendeleo endelevu. Aidha, ushirikiano kwenye masuala ya ulinzi na usalama unatarajiwa kupewa kipaumbele kwenye mkutano huu ikizingatiwa kuwa utekelezaji wa shughuli za maendeleo unategemea uwepo wa amani na usalama. 
Tanzania ni nchi ya kipaumbele kwa nchi za Nordic. Ushirikiano kati ya Tanzania na nchi za Nordic ulianza hata kabla ya uhuru wa Tanganyika ambapo wamisionari kutoka nchi hizo walikuja kufanya kazi hapa nchini kwenye sekta za afya na elimu. Katika sekta ya elimu, nchi hizo zilianzisha Kituo cha Kilimo cha Uyole na Kituo cha Elimu cha Kibaha kupitia Mradi wa Nordic-Tanganyika Project. Ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na nchi za Nordic ulichangiwa kwa kiwango kikubwa na falsafa zilizokuwa zinafanana kuhusu maendeleo ya watu, ukombozi wa Afrika, urafiki miongoni mwa viongozi wetu na nafasi ya kimkakati ya Tanzania katika Bara la Afrika. 
Hadi sasa, Tanzania ni nchi pekee iliyopokea msaada mkubwa kifedha kutoka katika nchi za Nordic. Kuanzia mwaka 2013 hadi 2019, Tanzania imepokea takribani shilingi za kitanzania bilioni 900 kutoka kwa nchi za Nordic. Nchi hizo zimekuwa zikisaidia sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo: elimu; afya; miundombinu; nishati; TEHAMA; utafiti; ukusanyaji wa kodi; bajeti; misitu; usawa wa jinsia; hali ya hewa; na ukuzaji wa sekta ya biashara. Kufuatia ushirikiano huu wa kihistoria kati ya Tanzania na nchi za Nordic, nchi hizo ziliiomba Serikali ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka huu na Serikali kuridhia kwa minajili ya kuendelea kuboresha ushirikiano kati ya pande hizi mbili kwa manufaa ya pande zote.

RC SHIGELLA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAMILIKI WAPYA WA KIWANDA CHA KUZALISHA SARUJI CHA RHINO JIJINI TANGA

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wamiliki wapya wa kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Rhino kilichopo Jijini Tanga ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji 
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akizungumza na wamiliki wapya wa kiwanda cha Kuzalisha Saruji cha Rhino kilichopo Jijini Tanga ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa 
VIONGOZI mbalimbali wakifuatilia mazungumzo hayo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na aliyevaa miwani kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) faidha Salim

KAMATI YA UKIMWI YAPOKEA TAARIFA YA HALI YA KIFUA KIKUU NCHINI

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Mheshimiwa Oscar Mukasa akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati hiyo walipokutana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi wakifuatilia Taarifa ya majukumu ya Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma kwa mwaka 2018/2019 iliyowasilishwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakari Kambi Jijini Dodoma hi leo. 
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakari Kambi akiwasilisha Taarifa ya majukumu ya Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma kwa mwaka 2018/2019 kwenye Kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi Jijini Dodoma hii leo.(Picha na Ofisi ya Bunge)

SHIRIKA LA INADES FORMATION TANZANIA LAITAKA JAMII KUTAMBUA HAKI NA SHERIA ZA MNYAMA PUNDA

$
0
0

Mnyama aina ya Punda ambaye anapiganiwa kupata haki na sheria zake na Shirika la Inades Formation Tanzania (IFTz)


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Shirika la Inades Formation Tanzania (IFTz) limeitaka jamii kutambua haki na sheria za mnyama punda pamoja na kutambua mchango wa punda katika maisha ya jamii.

Akizungumza na vyombo vya habari mratibu wa kuboresha maisha kupitia ustawi wa mnyama kazi punda Fadhili Nyingi ambapo amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuboresha maisha ya watu waishio vijijini kupitia mnyama punda pamoja na kurasimisha sekta ya punda katika halmashauri ya wilaya ya iringa.

Lengo la kwa la mradi ni kuongeza uelewa wa watu juu ya haki za wanyama na ufugaji bora wa Punda,mwisho wa siku watu wanatakiwa kujua punda anatakiwa kula nini,analala wapi na anahaki gani za msingi kutoka kwa binadamu” alisema Nyingi

Nyingi alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaongeza uelewa kwa wananchi juu ya mnyama punda na kuwa sekta rasmi kama zilivyo sekta nyingine.Aidha ameeleza mafanikio waliyopata kutokana na mradi huo ikiwa ni pamoja na kubadili mitizamo ya wananchi na kupunguzwa ukatili dhidi ya mnyama punda.

“Mafanikio yapo toka tumeanza mradi huu,maana wananchi wengi waliopo vijijini wameanza kubadilika kimtadhamo juu ya mnyama punda ndio maana sasa wameanza kuacha kuuza punda” alisema Nyingi

Kwa upande wake afisa mfawidhi nyanda za juu kusini bwana Nong’ona Solomoni amebainisha baadhi ya magonjwa yanayokumkumba mnyama punda ni pamoja na pepo punda,homa ya farasi na vidonda.

Hata hivyo kupitia mradi huo wa Inades Formation Tanzania wamefanikiwa kuunda vikundi 6 vya kukopeshana pamoja kutoa elimu juu ya haki za wanyama.

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUENDANA NA WAKATI KIUTENDAJI

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakiungana na wanafunzi na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora na wageni wengine kucheza muziki uliokuwa ukitumbuizwa na bendi ya Msange JKT wakati wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970. Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika.
Mkufunzi Msaidizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora, Bw. Alex Massengo akiwaonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg matukio mbalimbali katika picha yakiwemo yanayohusu ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden katika kujenga Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora wakati wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho.



Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri akielezea historia fupi ya Mkoa wa Tabora kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg walipomtembelea ofisini kwake jana kabla ya kutembelea Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini, Mhe. Kitwala Komanya.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg kuingia Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970. Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika.

Mkuu wa Idara ya Uhazili, Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora, Bw. Given Simkwai akiwaonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg umuhimu wa matumizi ya hati mkato wakati wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970.

***********************************

Na Mary Mwakapenda, Tabora

18 Oktoba, 2019

Watumishi wa Umma nchini wametakiwa kubadilika kiutendaji ili kuendana na
kasi ya mabadiliko mbalimbali yanayotokea hivi sasa duniani kwa lengo la
kuliletea taifa letu maendeleo.

Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara
yake ya kikazi na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg
iliyolenga kuangalia maendeleo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya
Tabora kilichojengwa mwaka 1970 kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania
na Sweden.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema hivi sasa kila kitu kinabadilika duniani
ikiwemo uchumi, maisha na teknolojia, hivyo watumishi wa umma hawana
budi kubadilika kulingana na wakati uliopo, kwa mantiki hiyo ni lazima wawe
wabunifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea hatimaye taifa liweze
kunufaika na mchango wao.

“Kama katika sekta binafsi wanafanya kazi ipasavyo kwanini katika Sekta ya
Umma tushindwe? ikizingatiwa kuwa wananchi ambao ndio walengwa wakuu
wanahitaji huduma kutoka serikalini na waliopewa dhamana ya kuwahudumia
ni sisi,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa alihoji na kuongeza kuwa, ndio maana Serikali
ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi makini wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli inasisitiza na kuiishi
kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu ili watumishi wa umma wawe na tija kwa taifa.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewasisitiza watumishi na wanafunzi wa Chuo
cha Utumishi wa Umma kila mmoja kwa nafasi yake kutekeleza wajibu wake
ipasavyo ili kutimiza malengo waliyojiwekea.

“Ukiwa mwanafunzi soma kwa bidii na mtumishi fanya kazi kwa bidii ili
kutimiza ndoto yako kwani Serikali inataka Chuo cha Utumishi wa Umma
Tanzania kiendelee kutoa mchango katika maendeleo ya taifa na kuwa mfano
bora wa kuigwa na vyuo vingine” Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliongeza.

Akitoa salamu za Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey
Mwanri amemshukuru Naibu Waziri na Balozi Sjoberg kwa ujio wao kwani
unaendelea kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na Sweden ambao
ulianza tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza mpaka sasa.

Mhe. Mwanri amewaasa wanafunzi wa chuo hicho kutumia vema ujuzi
watakaoupata kwa manufaa yao na maslahi ya taifa na kuongeza kuwa chuo
hicho kina historia ya kutoa viongozi bora huku akitoa mfano wa baadhi ya
viongozi waliosoma hapo na kupata mafanikio makubwa akiwemo Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu na Mke
wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Hayati Robert Mugabe, Mama Grace
Mugabe.

Kwa upande wake, Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg
alishukuru kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na kuwaasa wanafunzi na
watumishi wa chuo hicho kutekeleza wajibu wao ipasavyo, na hakusita
kupongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania za kukiendeleza
chuo hicho.

Ziara hiyo ilitoa fursa kwa viongozi hao kutembelea maktaba ya kumbukumbu,
maktaba, chumba cha Kompyuta, darasa la kupiga chapa, mabweni ya
wanafunzi na jengo jipya la utawala linalojengwa kwa fedha za ndani ambalo
limekamilika kwa asilimia 94 kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7.

Serikali ya Awamu ya Tano Kuendelea Kuboresha Maisha ya Wananchi Kwa Kutumia Takwimu

$
0
0
Mtakwimu mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akieleza faida za kutenga maeneo ya kuhesabia watu kwa kutumia mfumo wa kidigitali kwa ajili ya Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwaka 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi na usambazaji wa taarifa ya kutenga maeneo hayo iliyofanyika Wilayani Bahi mkoani Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Bw. Adam Mgoi akizungumza Wilayani Bahi mkoani Dodoma Oktoba kwa niaba ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo wakati wa hafla ya uzinduzi na usambazaji wa taarifa ya kutenga maeneo ya kuhesabia watu kwa ajili ya Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwaka 2022.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamis Munkunda akizungumza Jafo wakati wa hafla ya uzinduzi na usambazaji wa taarifa ya kutenga maeneo ya kuhesabia watu kwa ajili ya Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwaka 2022.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Bw. Wilfred Ochan akieleza kuhusu mikakati ya Shirika hilo kuunga mkono mikakati ya Serikali kufanikisha Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwaka 2022.
Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia Bi. Elizabeth Talbert akizugumzia umuhimu wa sense na zoezi ya kutenga maeneo ya kuhesabia watu kwa ajili ya Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwaka 2022.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Bw. Adam Mgoi akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambapo alimuwakilisha Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo kuzindua taarifa ya Wilayani Bahi mkoani Dodoma baada ya kukamilika kwa zoezi za kutenga maeneo ya kuhesabia watu kwa ajili ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ,hafla hiyo iliyofanyika Oktoba 17, 2019 wilayani humo.

………………

Na Mwandishi Wetu- Bahi

Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuboresha maisha ya wananchi kwa kutumia takwimu zinazokusanywa ili kuwezesha kupangwa kwa mipango ya maendeleo inayoendana na mahitaji ya wananchi katika huduma za jamii.

Akizungumza Oktoba 17, 2019 huko Bahi mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi na usambazaji wa taarifa ya kutenga maeneo ya kuhesabia watu ya Wilaya ya Bahi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo alisema kuwa taarifa zinazotokana na takwimu zitasaidia katika upangaji wa mipango unaoendana na mahitaji ya wakati.

Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoi, Waziri Jafo alieleza ili kutekeleza dhamira ya serikali ya kuwatumikia vyema wananchi ni lazima kufahamu idadi ya wananchi wake, hali zao za kiuchumi, mahali walipo, elimu yao, afya zao na mahitaji yao ya msingi.

Aliueleza mkutano huo kuwa Takwimu zinazokusanywa wakati wa Sensa ni nyenzo muhimu kwa utayarishaji wa sera za kiuchumi na maendeleo, na inatumika katika kuangalia uboreshaji wa hali ya maisha ya watu.

Alipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar kwa kufanya kazi kwa weledi na ikiwemo kufanya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi miaka mitatu kabla ya zoezi la kuhesabu watu kufanyika kama miongozo ya kimataifa inavyoelekeza.

“Mataifa mengi ya Afrika yanakuja kujifunza hapa Tanzania jinsi Ofisi ya Taifa ya Takwimu inavyotekeleza majukumu yake kwa ufanisi hali iliyowezesha hata kuanza kwa zoezi hili la utengaji wa maeneo ya kuhesabia watu kwa ajili yan Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022” Alisisitiza Mgoi

Akifafanua amesema kuwa viongozi Viongozi katika ngazi zote hapa nchini wanapaswa kutoa ushirikiano kwa watafiti kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakapokuwa wakitekeleza jukumu la utengaji wa maeneo ya kuhesabia watu ikiwa ni maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 itakayofanyika hapa nchini.

Aliongeza kuwa Sensa hiyo inatarajiwa kufanyika kwa kutumia mifumo ya kisasa ya TEHAMA na hivyo kupunguza gharama kuanzia katika hatua za utengaji wa maeneo hadi utekelezaji wa zoezi la sensa mwaka 2022.

Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt Albina Chuwa aliishukuru Serikali na wadau wa maendeleo kwa kuendelea kuwezesha utekelezaji wa majukumu yake kwa ufanisi ikiwemo kuanza kwa zoezi la kutenga maeneo ya kuhesabia watu kwa ajili ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

Aliongeza kuwa Ofisi yake inapata ushirikiano wakutosha katika mamlaka za Serikali za Mitaa hali inayowezesha kutekelezwa kwa ufanisi kwa zoezi hilo katika Wilaya ya Bahi, Kondoa na Chamwino ambapo kwa Bahi tayari limekamilka pamoja na Sehemu ya Wilaya ya Kondoa.

Naye Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bi Elizabeth Talbert amesema kuwa wataendelea kusaidia juhudi za Serikali katika kufanikisha Sensa ya mwaka 2022 ili kuchochea maendeleo kwa kuwa Benki hiyo hutumia takwimu hizo katika kusaidia miradi ya maendeleo.

Zoezi la kutenga maeneo ya kuhesabia watu kwa ajili ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 mkoani Dodoma limekamilika katika Wilaya za Bahi na Chamwino pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Vijijini na hivi sasa linaendelea katika Halmashauri ya Kondoa mjini. 

Kwa kawaida, Sensa ya Watu na Makazi hufanyika kila baada ya miaka kumi. Sensa ya mwisho kufanyika humu nchini ilikuwa mwaka 2012

TAKUKURU MWANZA YAOKOA NA KUDHIBITI UPOTEVU WA ZAIDI YA SH. MILIONI 50

$
0
0
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Stenga, akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa waandishi wa habari jana, katika kipindi cha Julai-Septemba mwaka huu.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Stenga, akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari jana,yaliyolenga utendaji wa taasisi hiyo katika kipindi cha Julai-Septemba mwaka huu.
Waandishi wa habari baadhi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Emmanuel Stenga (mwenye tai nyekundu) wakiwemo watumishi wa taasisi hiyo jana.
Picha na Baltazar Mashaka
…………………………..

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

TAASISI ya Kupamba na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza imeokoa na kudhibiti upotevu wa fedha zaidi ya sh. milioni 50 mkoani humu huku kati ya fedha sh. milioni 30 zikirejeshwa kwenye akaunti maalumu ya serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkuu wa TAKUKURU mkoani humu Emmanuel Stenga alisema kuwa uokoaji na udhibiti wa upotevu wa fedha hizo ulifanyika katika kipindi cha Julai-Septemba mwaka huu. 

“TAKUKURU Mkoa wa Mwanza katika mapambano ya rushwa, udhibiti wa ubadhirifu wa fedha za umma kwa kipindi cha Julai hadi Septemba, 2019 imefanikiwa kuokoa sh.42,529,840 na kudhibiti upotevu wa sh.8,294,560.Kati ya fedha hizo sh.30,206,840 zemerejeshwa BOT kwenye akaunti maalumu ya serikali,’alisema Stenga.

Alisema kiasi kingine cha sh.11,413,000 zilizobainika kufanyiwa ubadhirifu kwenye mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Salongwe wilayani Magu pia kimerejeshwa kwenye akaunti ya serikali ya kijiji hicho.

Pia Stenga alisema, sh. 640,000 zimerejeshwa baada ya ukaguzi wa taasisi hiyo kufanyika kwenye mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Kakerege wilayani Ukerewe baada ya kubainika kuwa madirisha yaliyowekwa kwenye vyoo vya shule hiyo kutolingana na thamani ya fedha iliyolipwa.
Aidha, taasisi hiyo ilikagua miradi nane ya maendeleo katika sekta za elimu, maji na afya yenye thamani ya sh.2,152,600,000 ili kuona fedha za serikali zinatumika kwa usahihi na miradi inatekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa kulingana na thamani ya fedha.

Stenga alifafanua kuwa kati ya miradi iliyokaguliwa sita ni yelimu yenye thamani ya sh. milioni 806.6, maji mradi mmoja wenye thamani ya milioni 986 na afya wenye thamani ya sh. milioni 360 na walifuatilia na kukagua fedha za ruzuku zinazotolewa na serikali kwa shule za msingi ambapo 70 zilikaguliwa katika halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza.

“Lengo kuu la ufuatiliaji huu kwenye miradi inayotekelezwa, ni kuzuia mianya ya rushwa na upotevu wa rasilimali ama kudhibiti fedha za serikali inapobidi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ili itekelezwe kwa kiwango kinachotakiwa na thamani ya fedha ionekane,”alisema Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoani humu

UMEME UPO WA KUTOSHA WEKEZENI PWANI KATIKA VIWANDA

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,(kushoto) na mhandisi Stella Manyanya wakipata maelezo kutoka kwa mfanyabiashara mwenye kiwanda aliyeshiri katika maonesho ya viwanda na wafanyabiashara yaliyofanyika mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,(wa pili kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo ( kulia), wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanakijiji( hayupo pichani) baada ya kushindwa kufika katika Kijiji cha Kitima wilayani Bagamoyo kilichokubwa na mafuriko,baada ya barabara kuharibika na kujaa maji kufuatia mvua zinazonyesha katika Mikoa ya Ukanda wa Pwani.

…………………..

Na Zuena Msuya, Pwani

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka wafanyabiashara, wenye viwanda na wadau mbalimbali wa maendeleo kuendelea kujenga na kuwekeza katika viwanda mkoani Pwani kwa kuwa umeme upo mwingi na wa kutosheleza mahitaji ya viwanda hivyo.

Mgalu alisema hayo Oktoba 17,2019 wakati wa ufunguzi wa maonesho ya pili ya wafanyabiashara na wenye viwanda yanayofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, ambapo Mgeni Rasmi katika maonesho hayo alikuwa ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, kwa niaba ya Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.

Maonesho hayo yanayofanyika kwa siku 7, yamewashirikisha wafanyabisha, wenye viwanda pamoja na wadau mbalimbali ndani na nje nchini, ambapo zaidi wa washiriki zaidi ya 300 wamejitokeza katika maonesho hayo.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Mhandisi Manyanya aliwahakikishia wafanyabiashara na wenye viwanda kuwa, Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza, pia serikali imeweka mazingira rafiki katika uwekezaji na uwezeshaji wa namna yeyote hususani katika viwanda.

Mhandisi Manyanya pia alisema kuwa, wafanyabiashara na wenye viwanda wasiwe na wasiwasi juu ya upatikanaji wa nishati ya umeme kwa kuwa Tanzania ina miradi mikubwa ya kuzalisha umeme: Akijata visima vya gesi mkoani Mtwara na Lindi pamoja na Mradi Mkubwa wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere kwa kutumia maporomoko ya maji katika Bonde la Mto Rufiji utakaozalisha zaidi ya Megawati zaidi ya 2000 za umeme mwingi ,wa kutosha na wa bei nafuu. 

Akizungumzia hali ya upatikanaji wa umeme kwa Mkoa wa Pwani, Mgalu alisema kuwa kwa sasa mradi mkubwa wa kusambaza umeme katika vijiji 150 unatekelezwa ili kurahisisha usambazaji wa umeme katika viwanda vitakavyojengwa na vinavyojengwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Vilevile Mkoa wa Pwani utanajenga kituo cha kupoza umeme cha Uruguni pamoja kutanua kituo cha kupoza na kupokea umeme cha Mlandizi na Chalinze ambavyo vitakuwa na njia zake za kusafirisha umeme kwenda viwandani.

Sambasamba na hilo, kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ubungo pia kitatanulia na kuongezewa nguvu na kuzalisha Megawati 800 za umeme kwa lengo la kuimarisha na kuboresha upatikani wa umeme katika wa Mkoa wa Dar es salaam na Pwani.

Alilitaka Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kuendelea kuboresha miundombinu ya usafirishaji na usambazji wa umeme ili kuepuka changamoto ya kukatika umeme pasipo sababu ya msingi.

Kuhusu malalamiko ya bei ya gesi yaliyokuwa yametolewa na wenye viwanda, Mgalu alitumia hadhara hiyo kuwaeleza wenye viwanda na wafanyabiashara kuwa , Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini ( TPDC) limepewa kazi kusikiliza na kujadiliana na wafanyabiasha na wenye viwanda ili kupata mapendekezo ya kuboresha na kupunguza bei ya gesi kwa manufaa ya watumiaji na taifa kwa ujumla.

Serikali ilitenga shilingi Bilioni 17 na Dola za Kimarekani milioni 4, kwa ajili ya usambazaji wa umeme katika Mkoa wa Pwani na shilingi bilioni 64 kwa ajili ya mradi wa usambazaji umeme wa Peri Urban katika maeneo 186 mkoani humo, ambapo mahitaji ya umeme kwa sasa ni megawati 82.

Katika hatua nyingine, baada ya kushiriki katika ufunguzi wa manesho hayo, Naibu Waziri Mgalu, aliungana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Kamati ya ulinza na usalama ya mkoa huo, kutembelea maeneo ya kijiji cha kitima wilayani bagamoyo ambayo yamekubwa na mafuriko kufuatia mvua zinazoendela kunyesha katika Mikoa ya Pwani ya bahari ya hindi ikiwemo Mikoa ya Dar es salaam na Pwani. 

Ilielezwa kuwa wananchi wanaoshi katika kijiji hicho kukumbwa na mafuriko kwakuzingirwa na maji hivyo kuhatarisha usalama wa maisha yao, ambapo serikali ilifanya juhudi ya kuwaokoa na kuwahamishia katika sehemu salama.

Hata hivyo zoezi la viongozi hao kufika katika kijiji hicho kilichokubwa na mafuriko hazikuzaa matunda baada ya maji kujaa na kuharibu barabara na hivyo kushindwa kufika katika eneo la tukio.

WATANZANIA TUNASUMBULIWA NA UMASIKINI WA KIFIKRA-DC HANANG

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mhe. Joseph Mkirikiti akizungumza na wananchi wa kijij cha Gehandu wakati wa hitimisho la Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika kijiji hapo.
Wananchi wa kijiji cha Gehandu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mhe. Joseph Mkirikiti wakati wa hitimisho la Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika kijiji hapo.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya- Idara Kuu ya MAendeelo ya Jamii (kulia) akicheza ngoma ya Kibarabaigi na wanakijiji wa Kijiji cha wakati wa hitimisho la Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika kijiji hapo.Picha zite na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

………………

Na Mwandishi Wetu Hanang Manyara

Tanzania iliungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuondoa umasikini duniani huku ikisemekana kuwa watanzania walio wengi wanakabiliwa na umasikini wa kifikra zaidi kwa kukosa kutambua firsa za kimaendeleo unaosababisha kuleta umasikini wa kipato.

Hayo yamebainika wakati wa hitimisho la Maadhimisho ya siku tatu mfululizo ikiwa ni Siku ya Mwanamke anayeishi kijijini,Siku ya Chakula Duniani na Siku ya kuondoa Umasikini Dunaini yaliyofanyika katika Kijiji cha Gehandu Wilaya ya Hanang mkoa wa Manyara yaliyoratibwa na Wizara ya Afya, Idara Kuu ya MAendeleo ya Jamii.

Akizungumza wakati wa hitimisho ya maadhiisho hayo Mkuu waWilaya ya Hanang Mhe. Joseph Mkirikiti amesema kuwa watanzania waliowengi wanasumbuliwa na umasikini wa kifikra zaidi unaopelekea umasikini wa kipato.

“Nitolee mfano katika Wilaya ya Hanang utakuta katika jamii sio watu wanakosa pesa ila ni kukosa kutambua fikra za kuweza kujiwezesha kiuchumi na kuondokana na umasikini wa kipato” alisisitiza Mhe. Mkirikiti
Ameongeza kuwa jambo kubwa linaloanisha umasikini ni ukosefu wa fursa za kimaendeleo kwa jamii nyingi za kitanzania hivyo elimu inahitajika kwa wananchi hasa wa vijijini hasa katika kutambua fursa za kimaendeleo na kuzifanyia kazi.

Mhe. Mkirikiti amesema kuwa kwa upande wa Wilaya ya Hanang umasikini wa kipato haupo ili kuna hitajika elimu wananchi ya jinsi ya kutumia fursa za kimaendeleo kwa kutumia kipato wanachopata kujileta maendeleo kwa kujenga nyumba bora na kupeleka watoto shule.

Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Mratibu wa maadhimisho kutoka Wizara hiyo Bi.Silyvia Siriwa amesema kuwa mwanamke akiwezeshwa kiuchumi na kuondokana na umasikini ana uwezo wa kulea familia na kupunguza masuala ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji.

“Sisemi kama wanaume hawalei familia ila mwanamke akiwa na uwezo wa kiuchumi kwa kiasi kikubwa anaweza kuiangalia familia kwa ukaribu hasa katika malezi ya watoto” alisema Bi. Silyvia.

WAZIRI MKUU AELEZA JINSI YA KUFIKIA NCHI YA KIPATO CHA KATI

$
0
0
Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela kutambua mchango wa benki hiyo katika sekta ya viwanda kwa kudhamini Tuzo za Rais kwa wazalishaji bora viwandani zilizofanyika jana kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kushoto ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye viwanda nchini (CTI) Bw. Subash Patel na katikati ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Innocent Bashungwa.



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ili Tanzania ifikie lengo la kuwa nchi ya kipato cha kati inayoongozwa na uchumi wa viwanda, haina budi kuhakikisha kuwa inatimiza vigezo kadhaa, kikiwamo cha ukuaji wa uchumi kwa kiwango cha asilimia 12 kwa mwaka.

Amesema vigezo vingine ni mchango wa viwanda katika Pato la Taifa usiopungua asilimia 15; utoaji ajira rasmi na za moja kwa moja uongezeke na kufikia asilimia 40 ya ajira zote; na sekta ya viwanda iweze kuiingizia nchi mapato ya fedha za kigeni zaidi ya asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni.

Alitoa kauli hiyo jana usiku (Alhamisi Oktoba 17, 2019) wakati akizungumza na wageni na washiriki waliohudhuria hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa mwaka 2018 iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli alisema: “Ili kufikia vigezo hivyo na kuongeza kasi ya ukuaji wa sekta ya viwanda, ni lazima tujizatiti na kuimarisha ushirikiano wa karibu baina ya sekta ya umma na sekta binafsi,” huku akiwasihi washiriki katika hafla hiyo waitumie fursa hiyo kutafakari mbinu mpya za kufikia vigezo hivyo muhimu vya kuijenga Tanzania mpya ya viwanda.

“Kila mmoja wetu anatambua umuhimu wa sekta ya viwanda katika kukuza uchumi wa nchi yoyote duniani. Viwanda ndivyo vimekuwa chimbuko la maendeleo ya haraka ya nchi mbalimbali duniani na mhimili mkuu wa kutegemewa katika kuondoa umasikini kwa kutoa ajira nyingi na za uhakika kwa wananchi. Maendeleo ya sayasi na teknolojia yanategemea sana sekta ya viwanda.”

“Takwimu pia, zinaonesha kwamba katika mwaka 2018, sekta ya viwanda imetoa ajira rasmi 306,180 ikilinganishwa na ajira 280,899 za mwaka 2017; sawa na ongezeko la asilimia tisa. Tutaendelea kuchukua hatua zinazostahiki ili kuwezesha sekta hii ikue kwa haraka na kutoa mchango mkubwa zaidi katika Pato la Taifa na hivyo kuchangia katika kukuza uchumi na kuondoa umaskini wa wananchi wetu,” alisema Waziri Mkuu.

Aliema kutokana na jitihada kubwa zinazoendelea kufanywa na Serikali za kujenga uchumi wa viwanda, jumla ya viwanda vipya zaidi ya 4,000 vimejengwa katika mikoa mbalimbali. “Viwanda vilivyojengwa vinazalisha bidhaa za ujenzi (saruji, nondo, vigae, mabomba, marumaru, n.k); pamoja na viwanda vya kusindika mazao ya kilimo ikiwemo nafaka, matunda, mafuta ya kupikia na bidhaa za ngozi,” alisema.

Alisema viwanda vingi vimeanzishwa nchini na ni faraja kuona wawekezaji wa ndani nao wanaendelea kufungua viwanda vipya pamoja kuongeza uwekezaji wao. “Moja ya viwanda vinavyohamasishwa ni vile vinavyochochea uzalishaji wa ajira kwa wingi. Ujenzi wa viwanda vipya nchini, katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano, umechangia kupatikana kwa ajira mpya 482,601 nchi nzima,” alisema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wenye viwanda na washiriki wa hafla hiyo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw. Innocent Bashungwa alisema wizara yake kwa kushirikiana na sekta binafsi itaendelea kuondoa kero zinazokwamisha ufanisi na ukuaji wa sekta ya viwanda zikiwemo kero kubwa zinazolalamikiwa na sekta hiyo.

Alizitaja baadhi ya kero hizo kuwa ni ucheleweshaji wa malipo ya madai ya kodi za ongezeko la thamani (VAT) na asilimia 15 ya ziada inayolipwa na waagizaji wa sukari ya viwandani; ushindani usio na uwiano na bidhaa za bei nafuu kutoka nje ya nchi kama vile nondo, mabomba ya plastiki, nguo na mavazi, bidhaa za ngozi na marumaru.

“Pia tutaangalia upya uwepo wa utitiri wa tozo na ada za juu zinazotozwa na taasisi mbalimbali za Serikali, ongezeko la kodi ya kuagiza mali ghafi kutoka nje ya nchini, na kucheleweshwa upatikanaji wa vibali vya kufanya kazi kwa wataalam wa kigeni wasiopatikana hapa nchini (expetriates employees),” alisema.

Kuhusu usajili wa makampuni, Waziri Bashungwa alisema Wizara hiyo kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imekamilisha kuweka mifumo ya kusajili majina ya biashara kwa njia ya mtandao. “Mifumo hiyo inawawezesha wafanyabiashara kusajili jina la biashara, uandikishwaji wa makampuni, usajili wa alama za biashara na usajili wa viwanda mahali popote walipo kupitia tovuti ya wakala (www.brela.go.tz).”

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Bw. Subhash Patel, alisema CTI inaunga mkono azma ya Rais Magufuli ya kuleta viwanda nchini. “Hakuna nchi itakuwa imefanikiwa duniani bila kuwekeza kwenye viwanda,” alisema.

Akielezea uwepo wa fursa za biashara kwa wawekezaji wa Kitanzania, Bw. Patel alisema Tanzania ina majirani ambao hawana bandari na hiyo ni fursa tosha ya kuwekeza na kuendeleza biashara kwenye nchi jirani.

Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images