Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

Prof Ndalichako amuagiza Mkurugenzi wa Kasulu kumhamisha kazi Mkuu wa shule ya Sekondari ya Kasangezi

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akikagua ujenzi moja ya jengo katika shule ya sekondari Kasangezi iliyoko Halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
 Prof Ndalichako amuagiza Mkurugenzi Kasulu kumhamisha kazi Mkuu wa Sekondari ya Kasangezi.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako ametilia shaka matumizi ya fedha za serikali zaidi ya shilingi milioni mia tano zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa shule ya sekondari Kasangezi iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Akizungumza mara baada ya kukagua utekelezaji wa  mradi huo waziri Ndalichako amesema shule hiyo imepatiwa zaidi ya shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 4, mabweni 4 yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 katika kila moja, matundu ya vyoo 10, bwalo pamoja na ukarabati wa maabara.

Ndalichako amesema  kazi iliyofanyika haiendani na fedha iliyotolewa kutokana na miundombinu hiyo kujengwa chini ya Kiwango.

“ milango ya madarasa na hata ya mabweni mmetengeneza kwa mbao laini tofauti na BOQ pamoja na kuwa laini ina uwazi hii nataka itolewe, tazama sakafu imeshaharibika hapa hata mwaka haujaisha mabweni mliambiwa ya watu themanini mmejenga ya watu sitini" 

Kufuatia hali hiyo ndalichako ameagiza kuwa ujenzi wa mabweni urudiwe kwa kuzingatia BoQ na ameaguza ujenzi huo uwe umekamilika ifikapo desemba.

 "..nitakuja mwenyewe mwezi wa kwanza kukagua  kama hayo yatakuwa hayajatekelezwa mengine yatafuata,”
 amesema waziri Ndalichako.

Aidha waziri Ndalichako amemuagiza  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu Mhandisi  Godfrey Kasekenya  kumuondoa  mara moja shuleni hapo mkuu wa shule hiyo kwa kushindwa kusimamia  vizuri kazi hiyo na hivyo kuisababishia hasara serikali.

“Kwanza ujenzi wa mara ya kwanza hata matofali hukununua ulichukua kwenye benki ya wananchi na tayari nilikuwa nimeleta fedha sasa kwanini hukujiongeza hata ukarekebisha ofisi ya Mkuu wa Shule ambayo iko katika hali isiyoridhisha vitu vingine ni kudhalilisha Serikali, Mkurugenzi muahamishe huyu katika shule hii,” alisema waziri Ndalichako.

Waziri Ndalichako pia ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na  Rushwa (TAKUKURU) wilayani Kasulu   kufuatilia muenendo wa upatikanaji wa madawati miamoja themanini yaliyonunuliwa katika mradi huo kama yametimia na yamenunuliwa kwa kufuata utaratibu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Saimon Anange amekiri kuwepo uzembe katika kusimamia miradi hiyo na kumuhakikishia waziri Ndalichako kuwa ofisi yake itafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa katika ziara hiyo.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolijia Prof. Joyce Ndalichako yupo mkoani Kigoma Kwa ziara ya Kikazi akikagua miradi ya elimu inatekelezwa kupitia fedha za Programu ya lipa kwa matokeo EP4R.

TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada yawafikia wakazi wa Nyehunge Wilayani Sengerema

$
0
0
Mhandisi Francis Mihayo akizungumza na wananchi wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika katika Viwanja vya Nyehunge Sengerema.

Wananchi wakipata huduma ya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa katika Viwanja Nyahunge.
Wananchi wakisoma vitabu vya muongozo wa TCRA katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Nyehunge Sengerema.

MAJALIWA AKAGUA MAANDALIZI YA OFISI ZA MUDA ZA HALMASHAURI YA MTAMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maadalizi ya Ofisi za muda za Halmashauri ya Mtama mkoani, Lindi, Oktoba 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Mtama baada ya kukagua maandalizi ya ofisi za muda za halmashauri hiyo Oktoba 17, 2019. Kushoto ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maandalizi ya Ofisi za muda za Halmashauri ya Mtama Oktoba 17, 2019. Wa pili kulia ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na Wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama, M. Matei.

WANAUME WAASWA KUWASAIDIA WANAWAKE KATIKA UZALISHAJI NA UTUNZAJI WA CHAKULA

$
0
0
 Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bi. Coletha Shayo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Gehandu kuhusu umuhimu wa wanaume kushirikiana na wanawake katika kuzalisha chakula wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
 Katibu Tawala Wilaya ya Hanang Bw Paulo Bura akizungumza na wananchi wa kijiji cha Gehandu na kusisitiza wanaume kutouza chakula na kuicha familia ikiwa na njaa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
 Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, na Watoto Bw. Abel Palapala akitoa elimu kwa wanakijiji wa Gehandu kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi kwa wananchi wanaoishi vijijini wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
 Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, na Watoto Bi. Silvia Siriwa akieleza uhusisano ulipo kati ya uzalishaji na mwanamke kwa wananchi wanaoishi vijijini wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara. Pix 5 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Gehandu wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW


Wanaume nchini Tanzania wameaswa kuwasaidia wanawake katika shughuli za maendeleo hasa katika uzalishaji wa chakula katika kaya ili kuondokana na upungufu wa chakula katika familia.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bi. Coletha Shayo katika Kijiji cha Gehandu kilichopo katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ikiwa na kauli mbiu isemayo " Lishe Bora kwa Ulimwengu usio na njaa"

Bi. Coletha ameongeza kuwa wanaume ni nguzo muhimu kwa familia na kuwataka wanaume kutelekeza familia zao wakati wa uhaba wa chakula bali kujipanga pamoja kwa kuweka chakula cha akiba.

Amewataka wanawake na Wanaume wa Kijiji cha Gehandu kuchangamkia fursa zilizopo ikiwemo uwepo wa ardhi nzuri na wataalam wa kilimo na mifugo ili kulima kilimo cha bora na kuwa na ufugaji wa kisasa.

Aidha amewataka wananchi hao kushirikiana katika kuhakikisha wanakuwa na mafanikio katika shughuli za kilimo na ufugaji ili kusaidia kuleta maendeleo katika kijiji chao.

"Niwatake wananchi wa kijiji hiki kuzingatia utunzaji wa chakula hasa suala la lise bora katika familia ili kuondokana na tatizo la udumavu kwa Watoto" alisisitiza Bi. Coletha

Naye Katibu Tawala Wilaya ya Hanang Bw Paulo Bura amesisitiza wanaume kushirikiana na wanawake kuzalisha chakula kwa ajili ya chakula na kuuza ili kujenga uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa wanaume walio wengi wamekuwa wakiona fahari kuwa na mifugo mingi huku familia zao zikiwa katika hali duni hivyo amewataka kuitumia mifugo kuwasaidia kupata chakula, kununua mashamba na kusomesha watoto.

"Kuna mila za kuwa na mifugo mingi katika jamii nyingi za wafugaji huku wakikosa huduma nyingine kama chakula elimu na afya tusiifanye mifugo fahari itusaidie katika kuendeleza familia zetu" alisema Bw. Bura

Akielezea mikakati ya Wizara yenye dhamana kwa wanawake Mratibu wa Maadhimisho kutoka Wizara husika Bi. Silyvia Siriwa amesema Wizara imejikita katika utoaji wa elimu kwa wanawake itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na pia kuondokana na vitendo vya ukatili katika jamii.

"Mwanamke akiwezeshwa kiuchumi katika jamii anaondokana na vitendo ukatili wa kijinsia na kuisaidia jamii inayowazunguka" alisisitiza Bi. Silyvia

Naye Mkazi wa Kijiji cha Gehandu Bi. Pili Mussa amesema kuwa wanaume wamekuwa wakiuza mazao bila kuwashirikisha na kusababisha njaa katika familia nyingi na hata kuzikimbia familia zao wakati wa uhaba wa chakula kwa kigezo cha kwenda kutafuta maisha.

Kwa upande Mkazi wa Kijiji cha Gehandu Bw. Samwel Arajiga amesema kuwa baadhi ya wanaume wamekuwasababu ya kuleta njaa katika familia kwa kuuza mazao yote na kutumia pesa kunywe pombe hivyo ameomba elimu zaidi kutolewa kuhusu umuhimu wa kutunza chakula katika familia.

Amesisitiza utolewaji wa elimu ya kilimo bora na lishe bora kwa wananchi wa vijijini ili kuondokana na tatizo la udamavu kwa kuzingatia ulaji bora kwa watoto na familia zao.

WAASWA KULINDA AMANI, MASHEIKHE 20 WAKIHUDHURIA MAULIDI YA MTUME MUHAMMAD S.A.W

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
WAUMINI wa Dini ya Kiislamu Jiji la Mwanza wameaswa kulinda amani, utulivu na usalama wa nchi pamoja na wageni wakati wote wa sherehe za Maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W, kwani amani ikivunjika wote watahusika.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Masheikhe wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Haruna Kichwabuta, kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa BAKWATA kwa niaba na masheikhe hao wakati wa kupokea taarifa ya maandalizi ya maulidi uliofanyika,kwenye Ukumbi wa Sheikhe Salum Ferej.

Sheikhe huyo wa Mkoa wa Kagera, alisema suala la amani na utulivu ni muhimu, lakini ikivunjika waislamu wote watahusika,hivyo lazima wajichunguze na kuwachunguza wengine wenye nia ovu wanaoweza kujipenyeza ili kuvuruga amani, utulivu ili kuharibu jina la Uislamu na Maulidi yenyewe.

“Waislamu tuhakikishe tunakuwa macho na watu wenye nia ovu wanaoweza kujipenyeza miongoni mwetu wakati wa Maulidi ili kuchafua Uislamu.Tunahitaji watu watakaokuja hapa watusaidie kulinda amani na utulivu wa nchi yetu na kuhakikisha usalama unakuwepo.Pia tutakuwa na wageni , tuwaangalie na kusimamia usalama wao licha ya kuwepo kwa vyombo vya ulinzi na usalama,”alisema Sheikhe Kichwabuta.

Alisisitiza kwa vile waislamu wanayo dhamana kubwa ya kulinda amani na utulivu wahakikishe sherehe hizo za kihistoria za maulidi ya Mtume S.A.W. yanafanyika kwa amani, usalama, mshikamano na upendo miongoni mwa waumini Kiislamu na jamii ya Watanzania.

Sheikhe Kichwabuta pia ahimiza waumini kushiriki na masheikhe kuendelea kusema na kukutangaza jambo hilo la heri kwenye mimbari (msikitini) na kushughulika na watu wanaoyahitaji maulidi,waachane na wasiyoyataka ili mwisho wa siku yafanyike kulingana na hadhi ya Jiji la Mwanza.

Aidha, Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza alhaji Hasani Kabeke alisema Kitendo cha Mufti Abubakar Zuberi kuipa BAKWATA mkoani humu jukumu la kuandaa Maulidi ya Mtume S.A.W. Kitaifa baada ya miaka 29 ni mtihani, ili kuufaulu ni kuyafanikisha.

Alisema kwa sababu Watanzania waislamu na wasio waislamu wanashirikiana kwa mambo mbalimbali ya kijamii, washirikiane kwa wenye uwezo,wajitoe hali na mali, wenye magari ama nyumba za wageni wasaidie kuwahifadhi wageni hao wa Mtume S.A.W. na kuwasafirisha.

Tunashirikiana na waislamu na wasio waislamu, hivyo wasio waislamu hawajaweewa pazia (mipaka), wanayo haki ya kuchangia Maulidi.Wajitokeze na watusaidie kuwahudumia wageni wa Mtume Muhammad S.A.W. na si BAKWATA.Watakachotoa ni kwa ajili ya wageni hao wa mtume,”alisema.

Kwa mujibu wa Sheikhe Kabeke jumla ya watu 10,000 wanaratajiwa kuhudhuria kwenye sherehe hizo wakiwemo masheikhe 20 kutoka nchi za Burundi, Kenya, Uganda na Rwanda, kuanzia Novemba 4 hadi 9, mwaka huu huku shilingi milioni 171 zihitajika kwa shughuli hiyo.ssss
 Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke (mwenye kanzu nyeupe), akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu Maalumu wa BAKWATA wa kupokea taarifa ya maandalizi ya sherehe za Maulidi ya Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza Novemba 9, mwaka huu.
 Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke (katikati),akizungumza kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa BAKWATA wa kupokea taarifa ya maandalizi ya sherehe za Maulidi ya Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza Novemba 9, mwaka huu.
 Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W. Sadiki Mshola akitoa taarifa fupi ya fedha za maandalizi kutoka vyanzo mbalimbali.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Miundombinu na Mapambo, Musa Mkumbi, akitoa taarifa kwenye mkutano Mkuu Maalum wa BAKWATA mikoa ya Kanda ya Ziwa kuhusu hatua iliyofikiwa pamoja na bajeti inayohitajika.
 Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa BAKWATA mikoa ya Kanda ya Ziwa baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya Maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W. yanayotarajiwa kufanyika kitaifa jijini humu Novemba 4-9, mwaka huu.
 Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke akifunga mkutanoMkuu Maalumu wa BAKWATA mikoa ya Kanda ya Ziwa baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya Maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W. yanayotarajiwa kufanyika kitaifa jijini humu Novemba 4-9, mwaka huu. Picha zote na Baltazar Mashaka


Llaki tano kutolewa na Biteko kwa kila mwanafunzi atakayepata daraja la kwanza mtihani wa Kidato cha Nne 2019

$
0
0

 Wahitimu wa Shule ya Sekondari Busangi wakiimba wimbo wa kuwaaga wenzao kwenye Mahafali hayo.
 Mgeni Rasmi, Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini akiwasili Mahafali ya 15 ya Shule ya Sekondari Busangi iliyopo Halmashauri ya Msalala, Wilaya Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 16, 2019.

Akizungmza kwenye Mahafali hayo, Biteko alitoa ahadi ya mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo huku akiungwa mkono na viongozi wa Serikali na taasisi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala aliyeahidi kupeleka Tsh. 25,000,000 (milioni 25) kwa ajili ya ujenzi huo.


Aidha Biteko aliahidi kutoa Tsh. 500,000 (laki tano) kwa kila mwanafunzi atakayefaulu kwa daraja la kwanza katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne katika Shule hiyo ya Sekondari Busangi.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko akipungia wananchi mkono alipokuwa akiwasili kwenye Mahafali hayo.
 Kijana wa Skauti akimvisha Skafu Mgeni Rasmi, Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko.
 Viongozi mbalimbali meza kuu.
 Mgeni Rasmi, Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko akizungumza kwenye Mahafali hayo.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari Busangi akisoma taarifa ya Shule hiyo.
 Katibu Tawala Mkoa Shinyanga akitoa salamu za Serikali kwenye Mahafali hayo.
 Wahitimu.
 Mgeni Rasmi, Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko akikabidhi vyeti kwa wahitimu pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo taaluma.
Tazama Video hapa chini

SAMIA -SERIKALI HAITOMVUMILIA ATAKAETHUBUTU KUINGIZA BIDHAA FEKI AMA KUKWAMISHA UWEKEZAJI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

SERIKALI imesema haitomvumilia mtu yeyote atakaethubutu kukwamisha ujenzi wa viwanda ,ikiwa ni pamoja na kuzalisha ama kuingiza bidhaa bandia zinazochafua taswira ya viwanda vya ndani ya nchi na sifa ya nchi kijumla.

Aidha imezielekeza mamlaka za ukaguzi na udhibiti wa ubora ikiwemo Shirika la viwango Tanzania(TBS )na NEMC kutoa huduma stahiki kwa wawekezaji pasipo urasimu.

Akifungua maonyesho ya mara ya pili ya viwanda kwa niaba ya makamu wa Rais ,katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani, Naibu Waziri Wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ,Stella Manyanya alisema haitowezekana kuwafumbia wale wachache wanaokwamisha juhudi za serikali za kukimbilia uchumi wa kati.

Alieleza ,serikali pia inaangalia utitiri wa kodi unaotozwa na tozo zinazotozwa na mamlaka za ukaguzi na udhibiti ubora unaolalamikiwa na wawekezaji."Hatua ya ushuru na tozo kuzifuta zimechukuliwa ,kati ya 114 zinazotozwa na taasisi za ukaguzi na udhibiti wa ubora wa bidhaa ,ambapo mwaka 2019 tozo 54 zimefutwa "

Stella alifafanua, licha ya viwanda kuzalisha bidhaa zenye viwango na ubora zinakumbana na ushindani sokoni.Wakati huo huo ,alibainisha serikali inaendelea kuboresha reli na kujenga reli ya kisasa ili kusafirisha mizigo kwa kasi,kununua ndege kubwa kwaajili ya mizigo na kurahisisha sekta ya usafirishaji .

Pia Stella alisema, kuwekeza upatikanaji wa umeme wa uhakika vijijini na mijini na kuongeza ufanisi na utoaji mizigo bandarini.Awali mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM ,mkoani Pwani Ramadhani Maneno alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,ameonyesha dhamira ya kufufua sekta ya viwanda na kupigania kuinua sekta ya uwekezaji.

Alisema kauli ya mh.Rais imetekelezwa kwa vitendo mkoani Pwani na mkuu wa mkoa huo ameitendea haki utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema,kauli mbiu ya maonyesho hayo ni  IJENGE TANZANIA,WEKEZA PWANI MAHALI SAHIHI KWA UWEKEZAJI .

Alisema, mkoa huo umevunja rekodi ya kuinua sekta ya uwekezaji na ujenzi wa viwanda zaidi ya 1,000 na kati ya hivyo 300 vimejengwa katika awamu ya tano na hii imetokana na kutokuwa na urasimu kwa wawekezaji na kutenga maeneo mengi kwa ajili ya viwanda.

"Malengo ya maonyesho haya ni kuonyesha kwamba mkoa umedhamiria kuwa ukanda wa viwanda,wenye viwanda kupata masoko ya uhakika,kupanua wigo wa soko la ndani ya mkoa kufikia kimataifa na ,kuvutia wawekezaji wapya"alisema Ndikilo.Ndikilo alisema hali ya ushiriki imeimarika tofauti na mwaka jana ambapo mwaka huu wamefikia washiriki 329 na mwaka uliopita walikuwa 166.

Hata hivyo Ndikilo alibainisha, ,maonyesho hayo yataambatana na kongamano la uwekezaji litakalofanyika octoba 19 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Wazir Mkuu Kassim Majaliwa.Naibu Wazir wa Nishati,Subira Mgalu anatambua kuna maeneo yenye tatizo la kukatika umeme ila wanafanya kila linalowezekana kuwe na umeme wa uhakika.

Alisema tatizo hilo litakuwa historia baada ya kukamilisha miradi mikubwa ya Peri urban,ujazilizi ,stigo huko Rufiji wa megawatt 2,100 ili kupunguza tatizo la umeme maeneo ya vijijini na kwa wawekezaji.Waratibu wa maonyesho hayo ni kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) pamoja na mamlaka ya maendeleo ya viwanda (TANTRADE) .

Maonyesho hayo yanatarajia kufungwa octoba 23 mwaka huu na Waziri Mkuu Mstaafu ,Mizengo Pinda.

Vodacom Tanzania PLC Yaendelea kupanua Huduma Mkoani Tabora

$
0
0
Mgeni rasmi mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Tabora, Katibu Tawala msaidizi anayeshughulikia Utawala, Hamisi Mkunga akizungumza na wananchi katika hafla ya uzinduzi wa duka la Vodacom mjini Tabora.
Mgeni rasmi mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Tabora, Katibu Tawala msaidizi anayeshughulikia Utawala, Hamisi Mkunga akipata maelezo toka kwa wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom ndani ya duka 
Baadhi ya wateja wa kampuni ya Vodacom wakiendelea kupata huduma ndani ya duka jipya lililoko mjini Tabora 
Baadhi ya watumishi wa duka la Vodacom lililopo mjini Tabora wakifungua champagne wakati wa uzinduzi wa duka hilo.
Baadhi ya Watumishi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania wakiwa katika maandamano ya amani wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Vodacom mjini Tabora.

DC ILEJE AZINDUA CHANJO YA POLIO NA SURUA

$
0
0
 Na Daniel Mwambene, Ileje
Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe leo amezindua zoezi la chanjo ya surua,lubela na polio akiwataka wananchi kutoficha watoto ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la soko katika kijiji cha Itumba huku zoezi hilo la kitaifa likifanyika tangu saa mbili asubuhi kwenye maeneo mengine ya wilaya hiyo na nchi nzima.
Awali,akisoma taarifa kwa Mgeni Rasmi Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo,Dkt.Enock Mwambalaswa alisema kuwa zaidi ya watoto 28 wataweza kufikiwa na zoezi hilo likitarajiwa kufanyika kwa siku tano.

Dkt.Mwambalaswa alisema kuwa wakati wa zoezi hilo watoto 17,783 watapata chanjo ya surua  huku watoto 10795 wakipata chanjo ya polio wote wakiwa na umri wa miezi tisa hadi 59.
Zoezi hilo lilitanguliwa na mafunzo ya siku moja kwa wahudumu wa afya 83 yaliyofanyika Itumba kwa Tarafa ya Bulambya na Isoko kwa Tarafa ya Bundali.

Wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Herman Njeje aliwataka wahudumu hao kutoa huduma itakayowezesha Wizara kufikia malengo yake.
 Mkuu wa Wialaya ya Ileje Ndg. Joseph Mkude akizindua zoezi la chanjo ya polio,surua na lubela,hapa ni katika eneo la soko Itumba,mbele yake ni mzazi akiwa na mtoto wake aliyekuwa wa kwanza kuchanjwa siku hiyo.
 Dc wa Ileje Ndg.Joseph Mkude akiwa amembeba mtoto Ivan Lukumay aliyekuwa wa kwanza kuchanjwa siku ya uzinduzi wa chanjo kiwilaya mjini Itumba.
 Wazazi na walezi wa Itumba-Ileje wakiwa kwenye foleni wakisubiri watoto wao wapewe chanjo ya polio,lubela na surua.
 Dc mkude wa Ileje akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa chanjo kiwilaya katika mji wa Itumba.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ileje wakifurahia jambo siku ya uzinduzi wa chanjo ya polio,surua na lubela.

SERIKALI YAPONGEZA UWEZESHAJI WA BENKI YA MAENDELEO YA TIB KATIKA VIWANDA

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Kibaha
Serikali imepongeza uwekezaji unaofanywa na Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kuwezesha uwekezaji kwa viwanda na makampuni ya wazawa hivyo kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
Pongezi hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya wakati alipotembelea Banda la Benki ya Maendeleo TIB wakati wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda ya Mkoa wa Pwani yanayoendelea mjini Kibaha.
Mhandisi Manyanya aliyekuwa akimwakilisha Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa maonesho hayo alisema kuwa uwekezaji unaofanywa na Benki ya Maendeleo TIB umechangia kwa kiasi kikubwa kuondoa utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi na kutoa ajira kwa Watanzania.
Kwa upande wake Naibu wa Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wazalishaji wa nyaya na vifaa vya umeme kuwa waendelee kuzalisha vifaa bora, kwa kuwa soko la bidhaa hizo lipo hasa kwa kuzingatia uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya nishati.
“Naomba niwahakikishie kuwa soko la bidhaa zenu lipo na kama mnavyofahamu Serikali imezuia uingizaji wa bidhaa kutoka nje ambazo zinaweza kuzalishwa na wawekezaji wa ndani ya nchi,” alisema.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Patrick Mongella alisema kuwa TIB ikiwa benki ya kisera inatekeleza kwa vitendo juhudi za serikali kwa kuwezesha uwekezaji wa viwanda nchini ili kuongeza ajira na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje.

“Benki ya Maendeleo TIB ni taasisi ya kifedha ambayo imekuwa ikisaidia nchi katika ukuaji wa uchumi na maendeleo katika sekta za kimkakati, hivyo tunatekeleza mikakati ya Serikali inayolenga kuchagiza maendeleo ya haraka ya kiuchumi,” alisema.
Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Patrick Mongella (wapili kulia) akitoa maelezo kwa Mgeni Rasmi wa Ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda ya Mkoa wa Pwani, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya (watatu kushoto). Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wapili kushoto).
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya (watatu kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wapili kushoto) wakiangalia nyaya za umeme zinazozalishwa na Kampuni ya Konnectt Wire moja ya wateja waliowezehswa na Benki ya Maendeleo TIB.
Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Patrick Mongella akimkabidhi zawadi Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.

Abdallah Hussein awabeba Watanzania kwenye Pool Afrika Mashariki

$
0
0
Mkurugenzi wa Cuespory Maaters Limited, James Nderitu Kuria (kulia) Akimkabidhi Amos Ndyagumanawe pesa taslimu shilingi 50,000 ya Kenya sawa na 1,000,000/= ya Tanzania mara baada ya kuibuka bingwa kwenye mashindano ya pool yajulikanayo kama "East Africa Chinise 8 Ball Competitions 2019" yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Moran Lounge & Grill Nanyuki nchini Kenya.
Bingwa wa Mashindano ya Pool yajjulikanayo kama "East Africa Chinise 8 Ball Competitions 2019" , Amos Ndyagumanawe kutoka Uganda akishangilia na kikombe pamoja na pesa taslimu shilingi 50,000 ya Kenya sawa na 1,000 000/= ya Tanzania yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Moran Lounge and Grill Nanyuki nchini Kenya.
Mkurugenzi wa Cuespory Maaters Limited, James Nderitu Kuria (kulia) Akimkabidhi Abdallah Hussein pesa taslimu shilingi 5,000 ya Kenya sawa na 100,000/= ya Tanzania mara baada ya kushinda kuingia robo fainali ya mashindano ya Pool yaliyojulikana kwa "East Africa Chinise 8 Ball Competitions 2019" yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Moran Lounge & Grill Nanyuki nchini Kenya. 

MCHEZAJI wa Pooltable, Abdallah Hissein(Sniper) amewabeba Watanzania kwa kutinga robo fainali  ya mchezaji mmoja mmoja(Singles) katika fainali za mashindano ya East Afrika ya mchezo huo yaliyojulikana kwa "East Africa Chinise 8 Ball Competitions 2019" yaliyo malizika mwishoni mwa wiki Nanyuki nchini Kenya.

Mashindano hayo yalijumuisha wachezaji kutoka Nchi tatu ikiwani Tanzania, Uganda na Tanzania kwa siku mbili ambapo yalifungukiwa rasmi octoba 12 hadi 13,2019 yakikutanisha jumla ya wachezaji 64 kwa udhamini wa Moran Lounge & Grill.

Bingwa alieibuka katika mashindano hayo ni Amos Ndyagumanawe kutoka nchini Uganda ambapo alizawadiwa shingi 50,000 ya Kenya sawa na 1,000 000/= ya Tanzania.
Msindi wa pili ni John Kyalo kutoka Kenya ambaye alizawadiwa shilingi 30,000 ya Kenya sawa na 600,000/= ya Tanzania, mshindi wa tatu ni Dennis Kimani kutoka Kenya ambaye alizawadiwa shilingi 20,000 ya Kenya sawa na shilingi 400,000/= ya Tanzanian na mshindi wa nne ni Collins Tuwei kotoka Kenya ambaye alizawadiwa pesa taslimu shilingi 10,000 ya Kenya sawa na 200,000/= ya Tanzania na wasindi wengine walioingia nane bora ni Abdallah Hussein kutoka Tanzania, Henry Mwangi kutoka Kenya, David Njane kutoka Kenya na Martin Mwangi kutoka Kenya ambao walizawadiwa shilingi 5,000 ya Kenya kila mmoja sawa na 100,000/= ya Tanzania.

Akizungumza na Wanahabari,Wachezaji pamoja na wadai waliojitokeza kushuhudia mashindano hayo, Mkurugenzi wa Cresports Masters Limited
James Nderitu Kuria kwanza aliwapongeza wachezaji kutoka nchi mbalimbali kuja kuungana na wenyeji Kenya kwenye mashindano hayo na kuwaomba sasa ni wakati wa kujikita kuwekeza katika mchezaji mmoja mmoja na si team.

Alisema Kuria kuwa alifurahiswa sana na mwitikio wa wachezaji wengi waliojitokeza na kuahidi mashindano haya leo yamefanyika Kenya awamu ijayo yatakuwa nchi nyingine ili kuleta hamasa zaidi.

Mwisho alimpongeza bingwa Amos Ndyagumanawe kwa kufanikiwa kupata ubingwa huo 2019 kwani kwa uwezo aliouonyesha hakika alistaili kuwa bingwa na pengine maandalizi aliyoyafanya.Lakini pia aliwapongeza washindi wengine wote na kuwaomba wakafanye mazoezi kwa maandalizi ya mashindano yajayo ambayo watatangaziwa.

Nae mratibu wa Mkurugenzi wa Athletes Committee (ICEA) ,Peter Gichuhi Kinyua aliwapongeza wachezaji wote na wadau wa Chinise 8 Ball kwa kujitokeza kushiriki na kuwapongeza walifanikiwa kushinda na kuwaomba walioshindwa wakajipange kwa mashindano yajayo.

Katika Mashindano hayo ya Chinise 8 Ball yaliwakilishwa na wachezaji wanne kwa udhamini wa Kampuni ya kutengeneza meza za Pool ya Kenice ambao ni Abdallah Hussein(Dar), Baraka Jackson(Manyara), Amos Bonophace (Dar) na Michael Machellah(Dar).

SEKTA BINAFSI: MATAMKO YA SERIKALI KIKWAZO KIUWEKEZAJI.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janet Bitegeko akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa kilimo ilikujadili ushiriki wa Sekta Binafsi katika utekelezaji ASDP II, pamoja na masuala mengine amesema Baraza la Kilimo litaendelea kuwasemea wakulima. 
Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo Tanzania Bw. Enock Ndondole akichangia wakati wa mkutano huo wa wadau wa Sekta ya Kilimo, Mkutano huo uliandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania na kufanyika Mjini Morogoro
Mratibu wa Ubia wa Kilimo Kanda namba 4 chini ya Baraza la Kilimo Tanzania BI Mwajuma Sizya akichangia katika warsha ya wadau wa kilimo ilikuona ushiriki wao katika utekelezaji wa Mpango wa ASDP II, Mkutano huo umefanyika Mkoani Morogoro.
Mratibu wa Ubia wa Kilimo Kanda namba 4 chini ya Baraza la Kilimo Tanzania BI Mwajuma Sizya akichangia katika warsha ya wadau wa kilimo ilikuona ushiriki wao katika utekelezaji wa Mpango wa ASDP II, Mkutano huo umefanyika Mkoani Morogoro.



Na Mwanandishi wetu.

WADAU wa Sekta Binafsi nchini wamesema Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili ASDP II bado kunachangamoto nyingi za ufanyaji biashara ikiwa ni pamoja na uwepo wa matamko yanayozui usafirishaji wa mazao nje ya nchi.

Wakizungumza wakati wa Warsha ya kujadili ushiriki wa Sekta Binafsi katika utekelezaji wa ASDP II iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania na kufanyika jana Mkoani Morogoro wamesema ni muhimu Mpango huo ukawa jumuishi si tu kwenye makaratasi, bali iwe jumuishi kwenye utendaji, maamuzi ya kila siku ya kisera ili sekta binafsi iweze kushiriki vema zaidi katika Mpango huo.

“Tumekuwa tukiathiriwa sana na matamko mengi hasa ya ufungaji wa mipaka, mfano SUMRI alikuwa na tani 5,000 za Mahindi ghafla likatoka TAMKO la kuzui kuuza nje, unaweza kuona namna tamko la mtu mmoja linavyoathiri saana , unakuta mtu mmoja anatoa tamko ambalo athari yake ni kubwa sana kiuchumi kwa mtu mmoja na jamii nzima.

“Lakini pia unakuta mtu anamkataba wake wa kuuza mazao nje ya nchi katafuta wakulima amewapa Mbolea, Mbegu mwisho wa siku mavuno yanakomaa na muda huo huo unakutana na,

“Tamko la kutokutoa mazao Wilaya moja hadi nyingine, sasa unaona ambavyo mazingira yanavyoiathiri sekta binafsi kwa hiyo ni muhimu changamoto hizi zikafanyiwa kazi vizuri na serikali ili tuweze kushiriki vizuri katika ASDP II” alisema Bw.Joseph Massimba kutoka kampuni ya SUGECO.

“Kimsingi changamoto ni nyingi hasa haya mazuio ya usafirishaji wa mazao nje ya nchi yanaathiri saana, sisi tunategemea masoko ya nje sasa unapozuiwa unajikuta unabaki na mzigo mkubwa sana ambao soko la ndani haliwezi kuumudu mzigo ulipo, lakini pia ni muhimu tuwe tunashirikishwa kama sekta binafsi “ alisema Bi Sifa Gerana ambaye ni Msindikaji wa Bidhaa za Mchele na Mahindi.

Kwa upande wake Mtafiti Mshauri aliyefanya utafiti kuhusu changamoto zinaikabili Sekta Binafsi kushindwa kushiriki kikamilifu katika ASDP II Bw. Apromius Mbilinyi amesema ni wakati muafaka kwa Sekta Binafsi kuanza kuwekeza katika Sekta ya Kilimo kwani kuna fursa nyingi hasa katika uongezaji wa thamani.

“Asilimia 70 ya mbegu zinaagizwa nchi ya nje, hii ni fursa kwa Sekta Binafsi kuwekeza lakini pia lazima wajitokeze kuwekeza katika ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula kwa sababu asilimia 30 ya mazao nchini yanaharibika baada ya kuvunwa kwa hivyo ni muhimu Sekta binafsi ikazitazama fursa hizi” alisema.

Alisema kuwa Sekta Binafsi kwa sasa inachangia asilimia 65 ya ajira na kwamba kupitia asdf ii ajira nyingi zaidi zinaweza kupatikana hasa katika uongezaji wa thamani wa bidhaa za mazao na kusema ni muhimu serikali ikazifanyia kazi changamoto kadhaa zinazoikabili sekta ya kilimo.

Kwa upande wake Afisa Sera Mwandamizi kutoka Baraza la Kilimo Tanzania ambao ndio waandaaji wa Mkutano huo Bi Laetitia Wiliam alisema waliamua kufanya utafiti huo baada ya kuona wadau wengi wa Sekta binafsi wakiwa na ukakasi katika kushiriki katika utekelezaji wa mpango huo ambapo sekta binafsi inatarajiwa kutoa asilimia 59 huku seriklai ikitoa asilimia 41 katika kukamilisha mpango huo.

“Ni kweli ndani ya ASDP II kuna fursa nyingi saana, ila kunavikwazo vya kisheria na kikanuni ambavyo vinaleta changamoto kidogo kiutekelezaji hasa kwa sekta binafsi , lakini sisi kama Baraza la Kilimo Tanzania baada ya mkutano huu tutaandika andiko letu la Kisera ilikuweza kuishauri Serikali ili iweze kufanyia kazi changamoto hizo na tumekuwa tukifanya hivyo na serikaLi imekuwa ikifanyia kazi” alisema Bi Laetitia Wiliam.

Akizungumza katika mkutano huo Mchumi kilimo dawati la ASDP II kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw Militon D.Manyara licha ya kukiri uwepo wa changamoto kadhaa za kiutekelezaji wa ASDP II na kwamba Serikali bado inaendelea kuzifanyia ili kukifanya kilimo kiwe na tija.

“Zaidi ya asilimia 78 ya tozo ambazo wadau wamekuwa wakizilalamikia tayari serikali imekwisha kuzifanyia kazi na kupitia BLUE PRINT tunaamini changamoto nyingi zinazoelezwa hapa zitafanyiwa kazi kikamilifu” alisema Bw. Militon.

“Serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto zote inapitia sera na taratibu na kanuni ili kukifanya kilimo kiwe chenye tija na iweze kumsaidia mkulima aweze kunufaika na sekta ya kilimo” alisema.

Mkutano huo wa siku moja uliofanyika mjini Morogoro na kuandaliwa na Baraza la kilimo Tanzania ulihudhuriwa na wadau wote wa sekta binafsi ikiwa ni pamoja na maafisa wa ACT/TAP pamoja na Maafisa kutoka wiraza za kilimo na viwanda na biashara.

KATIBU MWENEZI AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA KIGOMA UJIJI

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole (Katikati) akizungumza na wananchi wa Ujiji Mkoani kigoma leo na kukagua miradi ya maendeleo ya manispaa ya Kigoma Ujiji pamoja na Jengo la Mahakama ya Tanzania pamoja na Utandaji wa Mabomba ya Kusambazia maji.

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole  amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Mkoa wa Kigoma katika Manispaa ya Kigoma Ujiji leo.

Katika ziara hiyo Polepole ametembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Mahakama ya Tanzania ambalo limekamilika na litaanza kutumika hivi karibuni. Jengo hilo la Mahakama linakuwa sehemu ya utekelezwaji wa Ilani ya CCM inayotaka kusogezwa kwa huduma za utolewaji haki kwa wananchi na kuhakikisha haki za umma zinatolewa kwa wakati.

Ameihakikishia Mahakama kwamba Chama Cha Mapinduzi na Serikali wanataendelea kuiwezesha Mahakama ikiwamo ujenzi wa miundombinu  na nyenzo za kufanyia kazi.

Hata hivyo Polepole ametembelea na kukagua kazi inayoendelea Kigoma Ujiji ya Utandikaji wa mabomba na usambazaji wa maji katika magati yaliyo katika makazi ya wananchi pembezoni mwa mji wa Kigoma ujiji ikiwa ni sehemu ya kukamilisha mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Tanganyika.

"Huu ni muendelezo wa ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM inayotekelezwa na CCM chini ya Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Amesema polepole.

Polepole ataendelea na ziara yake Mkoani Kigoma na kuihitimisha kwa kutoa darasa la itikadi na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kwa Viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Kigoma.

TANZANIA KUWA MWENYEJI MKUTANO WA MAWAZIRI SEKTA ZA MAZINGIRA ,MALIASILI NA UTALII NCHI ZA SADC.

$
0
0
Katikati ni Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt,Aloyce Nziku akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Oldonyo Lengai ulipo katika kituo cha Kimataiofa cha Mikutano cha AICC Jijini Arusha leo 0ktoba 17,2019.kushoto kwake ni Agnes Kayoka ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uahirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika ya mashariki,Kulia kwake ni Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zamaradi Kawawa 
Agnes Kayoka ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uahirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika ya mashariki


Na.Vero Ignatus -Arusha.

Tanzania inatazamia kuwa mwenyeji wa mkutano wa Mawaziri wa Sekta za mazingira ,Maliasili na Utalii wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC ambapo mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha AICC,Kuanzia Oktoba 21 hadi 25 mwaka huu 2019.

Dkt.Aloyce Nzuki ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii akifungua mkutano huo leo 17oktoba2019 Jijini Arusha amesema lengo la mkutano huo kuangalia mwenendo wa hali ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi,kubainisha utekelezaji wa mikakati ya hifadhi na usimamizi wa mazingira kupitia mkakati wa SADC,uchumi wa Bahari na kutathimini maendeleo katika sekta za misitu wanyamapori na Utalii.

Agnes Kayoka ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uahirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika ya mashariki amesema kuwa mikakati ya nchi katika Uenyekiti wa SADC ni kuhakikisha kuwa wanafanikisha matumizi ya lugha ya kiswahili kama lugha mojawapo katika nchi hizo 16 kwenye vikao vya SADC.

Kayoka amesema sambamba na hayo ni kuandaa kamati ya kitaifa ya kushughulikia maswala ya Jumuiya na Mtangamano. 

Tanzania ni miongoni mwa nchi 16 wananchama wa SADC wanaotekeleza mkakati wa SADC kuhusu usimamizi wa sheria juu ya vita dhidi ya ujangili wa wanyamapori,programu za uhifadhi yaliyovuka mpaka wa nchi moja hadi nyingine kwenye maeneo ya misitu ,uvuvi,mazimgira na mabadiliko ya tabianchi,utalii,ukuzaji viumbe maji na mkakati wa ubora wa wanyama wa majini.

Aidha mkutano wa Mawaziri wa sekta za mazingira ,Maliasili na Utalii ni muendelezo wa mikutano itakayofanyika katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho Tanzania ni mwenyeji wa Jumuiya hiyo.

Mkutano huo wa Mawaziri ,Maliasili na Utalii utatanguliwa na mikutano ya wataalam wa sekta ya wanyamapori utakaofanyika Oktoba 18 hadi 19 ambapo makatibu wakuu wa sekta za mazingira Maliasili utafanyika Oktoba 21 -24 ,2019 ambapo mikutano hiyo miwili itajadili mapendekezo yatakayowasilishwa katika kikao cha Mawaziri Oktoba 26 ,2019 kwa maamuzi na maelekezo.

Mapema mwezi Agosti mwaka huu, Serikali ya Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Dar es Salaam, Katika Mkutano huo,Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikabidhiwa na kupokea rasmi jukumu la uenyekiti wa Jumuiya hiyo.

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ni moja kati ya jumuiya za kikanda katika bara la Afrika ambayo iliundwa kwa dhumuni la kuimarisha ushirikiano katika nyanja za uchumi, ulinzi, siasa na usalama,ambapo inaundwa na nchi wanachama 16 ambazo ni Angola, Botswana, Comoros,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Eswatini, Lesotho, Madagascar,Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Tanzania,Zambia na Zimbabwe.

Aidha Mkutano huo wa Mawaziri unatarajiwa kufunguliwa na Mhe.Samia Suluhu Hassani Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo mkutano wa Makatibu wakuu unatarajiwa kufunguliwa na Dkt.Hamis Kigwangalla ,Waziri wa Maliasili na Utalii 21Oktoba 2019 Jijini Arusha.

DC asema ni msimu wa mavuno kwa wakazi wa Dodoma, awataka kutumia vizuri fursa

$
0
0


Dodoma.Oktoba 19, 2019. Wafanyabiashara mbalimbali katika Mkoa wa Dodoma wameeleza namna ambavyo wamejiandaa kutumia fursa za kibiashara zinazotokana na msimu wa tamasha la Tigo Fiesta ikiwamo kukuza na kuboresha huduma zao ili kukidhi mahitaji ya wateja.
Mkuu wa Wilaya, Patrobas Katambi asema ni msimu wa mavuno kwa wajasiriamali huku akiwataka kutumia vema fursa za kibiashara.

Tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako litarindima Jumamosi hii tarehe 19 katika uwanja wa Jamhuri likiwa na dhumuni la kuchochea shughuli za kiuchumi pamoja na kutoa burudani kwa wateja wa Tigo na wakazi wa mkoa huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti jana, wafanyabiashara hao wamesema msimu wa Tigo Fiesta huleta fursa nyingi za kiuchumi kutokana na namna ambavyo linawakusanya watu kutoka maeneo mbalimbali ambao hugeuka kuwa wateja wa bidhaa na huduma kama chakula, malazi pamoja na usafiri.

Samuel Kakolanya ambaye ni dereva wa bajaji wa eneo la Chako ni Chako, alisema ni fursa ya kipekee kwa madereva na wasafirishaji kwani hali ya biashara huwa nzuri kutokana na mahiataji kuongezeka hasa nyakati za usiku.

“Kwanza nawapongeza sana waandaaji wa tamasha hili kwasababu ukiangalia mwaka jana biashara ilikuwa nzuri sana, tunapata wateja wengi tofauti na siku za kawaida kwahiyo msimu huu pia tunategemea mambo mazuri zaidi,” alisema Kakolanya.Naye, Juma Yusuph ambaye ni dereva wa pikipiki maarufu ‘bodaboda’ eneo la Jamhuri alisema msimu huo hugeuka kuwa neema kwao kutokana na biashara kuwa ya kasi.

“Sisi shughuli zetu zinategemea zaidi wingi wa watu na ukiangalia kama Fiesta ya mwaka jana niliona ongezeko kubwa la biashara tofauti na siku zote na hii inaonesha kukiwa na Fiesta hali inakuwa nzuri kutokana na Population ‘watu’ kuwa kubwa,” alisema.

Mbali na wasafirishaji, wafanyabiashara wa huduma za vyakula maarufu kama mama tilie walieleza kuwa kutokana na manufaa ya tamasha hilo wamejiandaa kuboresha huduma zao ili kukidhi mahitaji ya wateja.

“Tunachokifanya ni kujiongeza kiuchumi na kikubwa ni kuhakikisha naweka huduma za aina mbalimbali kama supu, chips pamoja kuboresha hili banda langu ili kuwavutia zaidi wateja siku hiyo,” alisema Mariam Meshack.

Aidha, watoa huduma za malazi (hoteli) walieleza namna ambayo wameanza kuboresha huduma ili kukidhi mahitaji ya wateja siku ya tamasha la Fiesta.

Meneja wa hoteli ya Los Angelos iliyopo mtaa wa Mji mpya, Benedicta Simon alisema.“Tunapokea wageni kutoka mikoa jirani kama Singida na pia wasanii mbalimbali wanafikia hapa, tumeanza kwa kubadilisha muenekano wa hoteli na ndani ya wiki hii tutaweka huduma ya intaneti ili kuwapa mazingira rafiki wateja wetu,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi aliwataka wakazi wa Dodoma kuchangamkia fursa akisema kuwa msimu wa Tigo Fiesta hugeuka kuwa msimu wa mavuno kwa wafanyabiashara.

“Ujio wa Fiesta hapa Dodoma itakuwa ni fursa ya ajira kwa vijana kwakuwa italeta fursa nyingi, wawe bodaboda, madereva teksi na mama lishe hivyo watu wategemee kuneemeka zaidi na fursa hii na Tigo imekuwaa rafiki wa vijana na kwa hapa Dodoma imeajiri vijana zaidi ya 600,” alisema.

Aliwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo zaidi kwa kusajili namba za simu kwa mfumo wa alama za vidole kwakuwa Tigo wanashirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kutoa namba na vitambulisho kwaajili ya zoezi hilo.


WATOTO 8,082,838 KUPATIWA CHANJO YA SURUA-RUBELLA

$
0
0
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na wazazi waliofika kwenye uzinduzi wa chanjo iliyofanyika kwenye viwanja vya jamhuri mkoani morogoro
Muuguzi Tumaini Majoji.kutoka kituo cha afya Uhuru akimpatia chanjo mmoja wa mtoto aliyepelekwa kwenye uzinduzi huo ambapo chanjo hiyo itatolewa kwa siku tano kwa watoto wenye umri wa miezi tisa hadi miaka mitano 
.Waziri Ummy Mwalimu akihutubia wakazi wa Morogogo(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa kampeni shirikishi ya chanjo
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Lowata Olesanare akiongea na wananchi walofika kiwanjani hapo
Waziri.Ummy Mwalimu akiongea na mmoja wa mzazi ambaye alipeleka watoto wake mapacha kupatiwa chanjo kwenye uzinduzi huoMwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) nchini Tanzania Dkt.Tigest Mengestu akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Muuguzi Tumaini Majoji akichanganya dawa wakati wa zoezi hilo


*******************

Na. Catherine Sungura-Morogoro


Inakadiriwa watoto wapatao 8,028,838 wenye umri wa miezi tisa hadi umri wa chini ya miaka mitano (miezi 59) wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Surua-Rubella kwenye kampeni shirikishi ya chanjo itakayotolewa nchi nzima.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoro Ummy Mwalimu wakati akizindua kampeni hiyo iliyofanyika kitaifa mkoani hapa.

“Kampeni hii inaanza leo na itamalizika tarehe 21 mwezi huu na itatolewa bila malipo tanzania bara na itaendeshwa katika vituo vya kutolea huduma za afya na vituo maalam vitakavyoundwa na kubainishwa na halmashauri katika kipindi hiki ili kusogeza huduma karibu na walengwa”. Alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha, kwa upande wa kuzuia ugonjwa wa kupooza kwa watoto wenye umri wa mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na nusu, Waziri huyo alisema inakadiriwa kuwa watoto 4,041,934 watapata chanjo hiyo.

“Lengo kuu ni kushiriki katika mkakati wa kitaifa wa kutokomeza ugonjwa wa surua na rubella ili kuchangia katika kupunguza vifo vya watoto hapa nchi,Zoezi hili la kampeni linatarajiwa kugharimu takribani shilingi za kitanzania billion 11.9 sawa na dola za kimarekani milioni 4.59”.

Hata hivyo alisema kuwa chanjo hupunguza gharama kubwa ambazo familia na taifa kwa ujumla lingetumia katika kutibu magonjwa yanayozuilika kwa chanjo“kuna faida kubwa katika uchumi wa taifa tunapowekeza kwenye chanjo,kwani imethibitishwa kwamba kila dola moja unawekeza kwenye chanjo unapata faida ya dola kumi na sita”.

Naye Mwakili Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tigest Mengestu alisema kuwa Tanzania inatoa chanjo hii kwa asilimia 95 na hivyo kampeni hii inasaidia kuimarisha afya za watoto nchini na kuwakinga na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

KIWANDA CHA CHUMVI GEREZA KIWANDA CHUMVI MTWARA KUBORESHWA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua shamba la chumvi la Gereza Kiwanda Chumvi Mtwara pamoja na sehemu ya mkondo wa maji ya bahari ambapo hivi karibuni mvua kubwa zilizonyesha katika maeneo hayo ya Gereza ziliharibu kingo za mashamba ya chumvi.
Sehemu ya matofali ya saruji ambayo yatatumika katika ujenzi wa nyumba za makazi ya askari katika Gereza Kuu Lilungu. Pichani ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua tofali hizo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiagana na Mkuu wa Wilaya Newala, Mhe.Aziza Mwanwasongo alipomtembelea Ofisi kwake kwa mazungumzo katika ziara yake ya kikazi Wilayani Newala, Mkoani Mtwara(Picha na Jeshi la Magereza).
Askari wa Gereza Kuu Lilungu wakiwa timamu katika Paredi wakati Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(hayupo pichani) alipowasili katika viwanja vya gereza hilo leo Oktoba 17, 2019 katika ziara yake ya kikazi.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiangalia chumvi ambayo ipo tayari kwa matumizi katika ghala la kuhifadhia chumvi la Gereza Kiwanda Chumvi Mtwara alipotembeleakatika ziara yake ya kikazi leo Oktoba 17, 2019.



Na ASP. Lucas Mboje, Mtwara

JESHI la Magereza lina mpango wa kukiboresha Kiwanda chake cha uzalishaji chumvi katika Gereza Kiwanda Chumvi Mtwara ili kupanua shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho kilichopo Mkoani Mtwara.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ameelezea adhima hiyo leo Mkoani Mtwara wakati akizungumza na uongozi wa Gereza hilo katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utendaji kazi wa Jeshi hilo.

Amesema kuwa kiwanda hicho lazima kiboreshwe kwa kuwekewa miundombinu mizuri ili kukidhi mahitaji halisi ya soko la chumvi hapa nchini.

“Mradi huu wa uzalishaji chumvi ni fursa kubwa ndani ya Jeshi letu hivyo ni lazima tukiboreshe kwa kukijengea miundombinu mipya pamoja na kufanya maboresho ya shughuli za uzalishaji wa chumvi ili kuongeza uzashaji,” amesisitiza Jenerali Kasike.

Katika hatua nyingine, Kamishna Jenerali Kasike ameupongeza Uongozi wa Gereza Kuu Lilungu kwa kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya Rais kuhusu kutatua changamoto ya makazi ya askari ambapo gereza hilo tayari limefyatua matofali 7,600 ya saruji pamoja na matofali ya kuchoma 25,000 ambayo yatatumika kujengea nyumba za watumishi wa Jeshi hilo.

“Nitumie fursa hii kumpongeza sana Mkuu wa Gereza Lilungu pamoja na maeneo mengine ya magereza yetu kwa mwitikio mzuri wa kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais Magufuli katika kutatua changamoto hii ya uhaba wa makazi ya askari,” Amesema Kamishna Jenerali Kasike.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kiwanda cha Gereza Chumvi Mtwara, SP. Wambura Kitoka amesema kuwa kiwanda hicho kinao uwezo wa kuzalisha chumvi ambayo inaweza kulisha magereza yote nchini ikiwa miundombinu ya uzalishaji itaboreshwa na kwa sasa kiwanda hicho kinao uwezo wa kuzalisha tani 300 za chumvi.

“Hivi sasa kiwanda chetu kinao uwezo wa kuzalisha tani 300 za chumvi, aidha malengo yetu nitani 700 za chumvi,” Amesema SP. Wambura.

Aidha, Mkuu huyo wa Kiwanda ameelezea baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwemo uchakavu wa miundombinu pamoja na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo kunyesha kwa mvua kubwa hali ambayo inawaletea changamoto kubwa katika uzalishaji wa chumvi.

Gereza Kiwanda chumvi Mtwara lilianzishwa mwaka 1975, lina eneo lenye ukubwa wa ekari 265 na shughuli kubwa zinazofanywa na Gereza hilo ni mradi wa uzalishaji wa chumvi.

WASTAAFU WAKABIDHI MAPENDEKEZO YA KUBORESHA ZAIDI SEKTA YA MIFUGO NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (Kushoto), akipokea ripoti yenye mapendekezo sita ya namna ya kuboresha zaidi sekta ya mifugo nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati Teule


Na. Edward Kondela

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel amepokea mapendekezo ya wataalamu wa mifugo wastaafu na wadau wa sekta ya binafsi yaliyotolewa ili kuboresha zaidi sekta ya mifugo nchini.

Akizungumza wakati akimkabidhi Katibu Mkuu Prof. Gabriel mapendekezo hayo katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo jijini Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati Teule ya wajumbe sita Dkt. Jonas Melewas, amemwambia katibu mkuu huyo kuwa mapendekezo yaliyotolewa ni Sita na kamati anayoingoza ambayo yanatokana na maazimio 14 yaliyotolewa kwenye kikao kilichofanyika Tarehe 7 Mwezi Oktoba 2019.

Dkt. Melewas ametaja mapendekezo hayo sita kuwa ni: Kusimamia tozo mbalimbali ikiwemo ya zao la ngozi na kuimarisha usimamizi wa Sheria na Kanuni kwa kuboresha mifumo ya ukaguzi ya uendeshaji, uzalishaji na biashara katika sekta ya mifugo.

Aidha Dkt. Melewas amefafanua pendekezo la tatu ni matumizi sahihi ya dawa za uogeshaji kudhibiti kupe na magonjwa yaambukizwayo na kupe kuzuia usugu na hasara kwa wafugaji.

Amebainisha mapendekezo mengine ni udhibiti wa magonjwa ya mifugo, kuongeza uzalishaji na tija katika ufugaji mbari za mifugo, mifumo ya ufugaji, uvunaji, biashara na masoko.

Akipokea mapendekezo hayo Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel amesema wizara itatumia taratibu mbalimbali kuhakikisha mapendekezo yaliyotolewa na wastaafu hao na wadau wa sekta binafsi yanafanyiwa kazi na kwamba wizara pia inafanya kila jitihada kuhakikisha afya ya watanzania inaimarika kwa kutumia mazao ya mifugo ikiwemo nyama na maziwa kutoka kwenye mifugo isiyo na magonjwa.

Prof. Gabriel amefafanua kuwa Asilimia 60 ya magonjwa ya binadamu yanasababishwa na mifugo hivyo wizara itahakikisha inadhibiti magonjwa ya mifugo pamoja na kuhakikisha inasimamia vyema soko la mifugo nje ya nchi.

DC SIMANJIRO AHAMIA KWENYE LANGO LA UKUTA WA MAGUFULI

$
0
0
MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mhandisi Zephania Chaula ameagiza vituo vya kuandikisha wapiga kura katika vituo vya vitongoji 24 vya Mji mdogo wa Mirerani kuhamia kwa muda kwenye lango la kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite ili kuwapa watu wengi fursa ya kujiandikisha. 

Mhandisi Chaula alisema shughuli ya uandijishaji imehamishiwa kwa muda kwenye eneo hilo ila vituo husika vitaendelea na kazi hiyo baada ya kukamilika kwa uandijishaji katika lango hilo. 

Alisema tangu asubuhi ya leo wamefanikisha kuandikisha watu 2,111 kupitia vitongoji 24 vya kata mbili za Mirerani na Endiamtu katika mji mdogo wa Mirerani. 

“Baada ya kuona shughuli ya uandikishaji inasuasua kwenye mji mdogo wa Mirerani na Orkesumet kamati ya usalama ikaamua kuweka mikakati ya kufanikisha uandikishaji,” alisema mhandisi Chaula. 

Alisema hadi hivi sasa watu 81,400 wamejiandikisha wilayani humo kati ya makisio ya wananchi 105,052 wanaotarajiwa kujiandikisha sawa na asilimia 85.Alisema anatarajia wananchi wengi watajiandikisha na hadi sasa wanatarajia kufikia asilimia 90 na leo watamalizia zilizobakia. 

“Nawashukuru wananchi wote kwa kujitokeza kujiandikisha na wasimamizi wa uandikishaji huo kwani agizo la Rais John Magufuli la kutaka wenye sifa washiriki uchaguzi huo linafanikishwa,” alisema mhandisi Chaula. 

Hata hivyo, ameagiza vitongoji na vijiji vya wilaya hiyo kufanya mikutano yao siku ya mwisho ya kujiandikisha ili wakamilishe kwa kila mmoja kutumia haki yake ya kujiandikisha. Mmoja kati ya waliojiandikisha kwenye lango hilo Mohamed Hassan alisema yeye ni mkazi wa Kitongoji cha Zaire na ameshajiandikisha kabla hajaingia ndani ya lango hilo. 

“Kuna baadhi ya watu wanaopanda kwenye migodi ya Tanzanite wamepata fursa ya kujiandikisha baada ya mkuu wa wilaya kuagiza shughuli hiyo ifanyike hapa kwa muda,” alisema Hassan.

HAKIKISHENI KILA KAYA INAKUWA NA UMEME HADI IFIKAPO NOVEMA 16-KALEMANI

$
0
0
Na Woinde shizza, Simanjiro

Waziri wa  Nishati  Dkt Medard Kalemani  amewataka wakuu wa wilaya, wakurugenzi, mameneja wa tanesco   kuwahamasisha wananchi waliopo katika Wilaya zao kulipia umeme ili waweze kuvutiwa umeme katika kaya zote. 

Aidha alimtaka Mkandarasi ambaye ni Angelique International Ltd kwa kushirikiana na shirika la Umeme Tanesco wilaya ya Simanjiro na mkoa wa Manyara kwa ujumla kuhakikisha wananchi wote wilaya ya Simanjiro katika vijiji vyote pamoja na vitongoji vyote vinapata umeme na sio mradi Umeme tu bali ni Umeme wa uhakika. 

Aliyasema hayo jana wakati akiongea na wananchi  wa Kijiji cha  Naepo kilichopo katika kata ya Naisinyai wilayani simanjiro mkoani Manyara ambapo mbali nakuongea na wananchi hao pia alizindua mradi na kuwasha Umeme katika Shule ya msingi Naepo pamoja na shule ya sekondari ya Shambarai zote zipo katika Wilaya hiyo. 

Kalemani alisema kuwa anafahamu katika kijiji cha naisinyai kimeshapata Umeme lakini haujatosheleza, lakini pia katika vijiji vingine pia vimepata umeme ,ambapo alibainisha kuwa anafatilia katika vijiji vyote ambapo avina umeme vinapata Umeme 

"napenda kutoa maelekezo kwa Mkandarasi pamoja na Tanesco wilaya ya simanjiro hadi ikifika November 16 vijiji vyote pamoja na kaya zote za Kata ya Naisinyai viwe vimepatiwa Umeme ,namaanisha kitongoji cha naepo kiwekimejaa Umeme ,kambi ya chokaa kulipelekwa Umeme lakini bado ujaja sasa napenda kukwambia Mkandarasi kabla ujatoka hapa hakikisha kaya zote, vijiji vyete pamoja na kitongoji cha kibaoni kiwe kimejaa Umeme  zinaumeme"alisema Kalemani 

Aliwataka Wananchi kujitokeza kwa kasi sawa ya muheshimiwa Rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania John Magufuli kuunganisha Umeme katika nyumba zao ,alibainisha kuwa Umeme huu hautaruka Nyumba ,kitongoji, kijiji na hata kaya  na wajibu wao wananchi ni kulipia tu kiasi cha shilingi elfu 27000 na kuunganishiwa Umeme. 

"napenda kuwaambia wananchi kama nyumba yako niyamakuti ,ni tembe ama ni yaudongo au ya gorofa zote zinastaili kuwekewewa umeme ,hakuna nyumba isiofaa kuwekewe Umeme na olewake Mkandarasi au muhandisi au Meneja aruke nyumba eti kwasababu ni mbaya ,hoho utakuwa wewe ni mbaya nanapenda kukuhakikisha autabaki salama "alisema  Kalemani 

Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Naepo Kaika  Mevukori aliishukuru serikali kwa kuwaletea umeme katika Kijiji chao Kwani umeme uwo utawasaidia kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo Kufunga mashine za kusaga na kukoboa, Kupungua maduka ya kuuza vifaa vya umeme pamoja na kuendeleza shughuli mbalimbali ambazo Zilikuwa zikitegemea Umeme. 

Naye  Lazaro Charles alisema wakati hakuna Umeme walikuwa wanatembea kilimeta kumi na mbili kwenda kufata huduma za umeme kama vile kuchaji simu ,pia walikuwa wanatembea umbali mrefu kwenda kusaga mahindi kwa ajili ya chakula ,aidha pia alisema pia Umeme huu uliowashwa katika shule hizi utawawezesha wanafunzi kupata muda wa ziada wa kujisomea na  hata Waalimu kupata muda wakuandaa Vipindi namitiani kwaajili ya mwanafunzi 

Kwa upande wake Laitiness Lowasa Sainyei aliomba serikali iongeze kasi zaidi ya kusambaza umeme ili vijiji ambavyo avina viweze kupata na wananchi waweze kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo zinategemea umeme

Kwa upande wake Meneja wa Tanesco wilaya ya Simanjiro, Zakaria Masatu aliishukuru serikali kupitia Wizara ya Nishati Kwa kuendelea kuwa karibu na Shirika katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali na hivyo kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya maendeleo ya wananchi wa wilaya ya simanjiro na Tanzania kwa ujumla 

Alisema kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali iliwemo udogo wa wigo wa mradi kulinganisha na mahitaji ya wananchi, pia alibainisha kuwa changamoto ingine inayolikabili  shirika hilo wilaya ya simanjiro ni pamoja na hujuma katika miundo mbinu hasa kuibiwa nyaya za copper kwenye transfoma na baadhi ya Watu wasio waadilifu. 

Alibanisha kuwa wao kama shirika wanaendelea kumsimamia Mkandarasi ili kuhakikisha anajenga miundombinu yenye ubora pia akamilishe Kazi katika muda uliopangwa.
Waziri Wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na Wananchi Wakijiji cha Naepo kilichopo katika Kata ya Naisinyai jana mara baada ya kuzindua mradi wa umeme na kuwasha umeme katika Shule ya msingi ya Naepo iliopo katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara (picha na Woinde shizza, Manyara) 
Meneja wa Tanesco wilaya ya Simanjiro Zakaria Masatu akiongea mbele ya Waziri wa nishati
Waziri Wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na Wananchi Wakijiji cha Naepo kilichopo katika Kata ya Naisinyai jana mara baada ya kuzindua mradi wa umeme na kuwasha umeme katika Shule ya msingi ya Naepo iliopo katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara (picha na Woinde shizza, Manyara) .
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live




Latest Images