Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

JENGO LA KITUO CHA UMAHIRI LAKABIDHIWA KWA WIZARA YA MADINI.

$
0
0

Anaandika Abdullatif Yunus, Michuzi TV KAGERA.

Miongoni mwa majengo saba ya Vituo vya Umahiri (Centers of Excellence) yanayojengwa hapa Nchini, chini ya Wizara ya Madini likiwemo jengo lililojengwa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, limekabidhiwa rasmi na kupokelewa na Waziri mwenye Dhamana Mhe. Dotto Biteko mapema Oktoba 04, 2019.

Jengo hilo lenye Orofa tatu, lenye thamani ya Sh. Bilioni 1.081 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyetaka kuona mabadiliko katika Sekta ya madini kwa kuweka mazingira wezeshi.

Akizungumza kabla ya kukabidhiwa jengo hilo, Waziri wa Madini  Dotto Biteko amepongeza usimamizi wa Jengo hilo kwa ujumla, huku akikumbusha nia ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutaka kujengwa kwa Vituo hivyo Saba, lengo likiwa kuifanya Sekta ya madini iwe sekta ya wadau na wachimbaji wa uhakika, na kuondokana na ujanja ujanja uliokuwa ukifanywa awali, kufuatia nia hiyo pamoja na mambo mengine tayari leseni 12000 zimefutwa na zitagawiwa Kwa wachimbaji wadogo, huku miongoni mwa hizo leseni, leseni 156 ni kutoka Mkoani Kagera.

Aidha Waziri Biteko ameongeza kuwa mpaka sasa Masoko zaidi ya 28 yameanzishwa na vituo vidogo zaidi ya 18 vya kununua madini vimefunguliwa,  ambapo utaratibu mwingine wa kupata cheti cha uasilia kwa ajili ya kuanza kupeleka madini hayo nje yakiwemo ya TIN  umekamilika na kufikia mwishoni mwa Mwaka huu Wizara itaanza kusafirisha madini nje ya Nchi, Hivyo kukamilika kwa jengo hilo ni fursa kwa wachimbaji na wafanyabiashara kuongeza ufanisi katika shughuli zao, na kuwataka kulitumia jengo hilo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema nia ya Mkoa ni kuongoza Mikoa yote katika ukusanyaji madini, kwa kutoa elimu kwa wachimbaji wa madini wadogo na wakubwa bila kutumia nguvu kubwa, ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi huku suala la kudhibiti utoroshaji wa madini likizidi kuimarishwa, na wito ukizidi kutolewa kwa wawekezaji wa biashara ya Madini kuendelea kwekeza katika Sekta hii ya Madini Mkoani Kagera.

Jengo hilo lenye Ofisi za Maafisa madini na wataalamu, Ukumbi wa mikutano, eneo la mafunzo, Chumba maalumu la kuhifadhi madini (strong room) pamoja na huduma nyinginezo tayari limekabidhiwa kwa Wizara ya Madini kutoka kwa Wajenzi wa Jengo hilo Shirika la Suma JKT, na tayari Wizara imekabidhi kwa Tume ya Madini Mkoa wa Kagera tayari kwa matumizi.
 Pichani Waziri wa Madini Dotto Biteko akikabidhi funguo kwa Tume ya Madini mara baada ya kukabidhiwa toka Suma JKT ambao ndio wajenzi 
 Pichani In meneja mradi kutoka shirika la Suma JKT Kapteni Fabian Buberwa akiwasilisha taarifa yake mbele ya Viongozi kabla ya kukabidhi mradi wa jengo la umahiri.
 Pichani Waziri wa Madini Dotto Biteko akipokea funguo toka kwa Meneja mradi Kapteni Fabian Buberwa kama ishara ya kukabidhiwa Jengo la umahiri mara baada ya Kumalika ujenzi wake.
 Pichani Ni Msafara wa Waziri wa Madini Dotto Biteko ukiwasili kukabidhiwa jengo la Umahiri, baada ya kukamilika kwa ujenzi.
Pichani ni Mhe. Ditto Biteko Waziri wa Madini akitoa nasaha zake mapema kabla ya kukabidhiwa Jengo la umahiri.
 Pichani Bi Veronica Nangale Kaimu Meneja Mradi akiwasilisha taarifa ya Ujenzi kwa Viongozi mapema kabla ya kukabidhiwa kwa Jengo la umahiri.
Pichani ni Muonekano wa Jengo la Orofa Tatu lenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.081 lilojengwa Mkoani Kagera, chini ya Wizara ya Madini likiwa tayari kwa matumizi baada ya kukabidhiwa.


RC MAKONDA AWAPA SIKU SITA WATUMISHI WA TAMISEMI WANAOHUSIKA NA MIRADI YA DMDP KUHAKIKISHA MIRADI YA UJENZI WA MIFEREJI INAANZA, ATISHIA KUFANYA MAANDAMANO ENDAPO WATAKAIDI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Paul Makonda ameelekeza Watumishi wa TAMISEMI wanaohusika na Miradi ya ujenzi wa Mifereji na Mito kupitia DMDP kuhakikisha kabla ya October 10 mwaka huu miradi yote ya Ujenzi wa Mifereji Wilaya ya Ilala iwe imeanza na endepo watakaidi atahitisha maandamano ya wakazi wa Kata 5 kwenda Wizara ya TAMISEMI.

RC Makonda ametoa maagizo hayo baada ya kutembelea Mfereji wa Kisiwani kata ya Buguruni ambao tangu mwezi May mwaka huu aliagiza ufanyiwe maboresho kutokana na mfereji huo kuwa chanzo cha mafuriko kwenye makazi ya watu lakini ameshangazwa kuona hadi leo anafika site anakuta hakuna chochote kilichofanyika licha ya mkataba kusainiwa tokea mwezi wa Saba mwaka huu.

Jambo hilo lilimlazimu RC Makonda kumpigia simu Mratibu wa Miradi ya DMDP Bwana Emmanuel Ndyamkana ambae alijitetea kuwa miradi hiyo inakwama kutokana na wizara ya fedha kuchelewa kutoa fedha jambo ambalo RC Makonda amesema ni uzembe.

Aidha RC Makonda ameitaja baadhi ya Mifereji na Mito inayotakiwa kufanyiwa maboresho ni pamoja Mfereji wa Tabata kanisa la Roman catholic, mfereji wa Kiwalani na baadhi ya Mito yenye urefu wa Km 19 ambayo ujenzi wake utagharimu takribani Shilingi Bilioni 32.

Pamoja na hayo RC Makonda ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Machinjio mpya ya Vingunguti na kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambapo amewataka NHC kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa muda uliopangwa.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Mh Paul Makonda pichani kulia akiwa  ameambatana na Naibu Meya wa Manispaa ya  Ilala,Mh Omary Kumbilamoto .


WAZIRI MKUU AKAGUA MRADI WA MAJI MANYONI

$
0
0
*Unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi. bilioni 10

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa mradi wa maji wa Kintiku – Lusilile ulioko Manyoni ambao awamu yake ya kwanza inatarajiwa kukamilika ifikapo Novemba 22, mwaka huu.

Akizungumza na watumishi na wakadarasi leo (Ijumaa, Oktoba 4, 2019) mara baada ya kukagua mradi huo akiwa njiani kuelekea Manyoni, Waziri Mkuu alisema ameridhishwa na ujenzi huo pamoja na kasi ya mkandarasi.

Waziri Mkuu ambaye ameanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Singida, alielezwa kwamba mradi huo utahudumia vijiji 11 vya Kintinku, Lusilile, Maweni, Mvumi, Ngaiti, Chikuyu, Mwiboo, Mbwasa, Mtiwe, Makutupora na Chilejeho ambavyo viko kando ya barabara kuu itokayo Singida kwenda Dodoma.

Akitoa taarifa ya mradi mbele ya Waziri Mkuu, Meneja wa RUWASA, Injinia Gabriel Ngongi alisema wananchi zaidi ya 55,000 watanufaika na mradi huo pindi utakapokamilika. Alisema awamu ya kwanza imegharimu sh. bilioni 2.46.

Akizungumzia halia halisi ya utekelezaji wa mradi huo, alisema ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji la lita 300,000 limekamilika lakini bado liko kwenye hatua ya umaliziaji. “Birika la kuhifadhia maji lemye ujazo wa lita milioni mbili limekamilika, bado shughuli za umaliziaji,” aliongeza.

Alisema ujenzi wa uzio, nyumba ya kuhifadhia mitambo na nyumba ya mlinzi umekamilika licha ya kuwa bado kuna kazi ndogo za umaliziaji.

Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake wilayani Itigi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mkandarasi wa mradi wa maji Kintinku/Lusilile, Injinia Jumanne Werema, uliyopo katika Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida, Oktoba 4, 2019. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi. Waziri Mkuu yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku nne. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

RAIS DKT. MAGUFULI AWAHUTUBIA WANANCHI WA VWAWA MKOANI SONGWE

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi Mbozi katika mkutano uliofanyika katika mji wa Vwawa mkoani Songwe.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Mbozi wakati akitoka kuweka jiwe la msingi mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji  Vwawa mkoani Songwe.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vikundi vya ngoma za asili kabla ya kuwahutubia wananchi wa Vwawa mkoani Songwe.



 Wananchi wa Mbozi wakifurahia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli  wakati akiwahutubia katika mji wa Vwawa. 
 Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akicheza ngoma ya kiasili wakati kikundi cha Vwawa kikitumbuiza mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika eneo hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Momba (Chadema) David Silinde mara baada ya kuwahutubia wananchi Mbozi katika mkutano uliofanyika katika mji wa Vwawa mkoani Songwe. PICHA NA IKULU

WADAU SEKTA YA MIFUGO ARUSHA WAITAKA JAMII KUACHA IMANI POTOFU YA KUTHAMINI BIDHAA ZA NJE KWA KUONA NI BORA KULIKO ZA TANZANIA

$
0
0

Na Woinde shizza, Arusha 

WADAU wa sekta ya Mifugo katika Halmashauri ya Arusha wameitaka jamii  kuachana na dhana potofu ya kuthamini bidhaa za nje ya nchi ni bora kuliko zinazotengenezwa hapa nyumbani, badala yake kuanza kuthamini na kutumia bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vya nyumbani, ili kuunga mkono jitihada za Serikali na utekelezaji wa uchumi wa viwanda, kuelekea uchumi wa kati.

Wakizungumza leo Oktoba 4,mwaka 2019 wadau hao wamewaambia waandishi wa habari changamoto kubwa inayokabili wawekezaji wa sekta ya mifugo, ni uelewa duni wa jamii,kuhusu mtumizi ya bidhaa zao za ndani na kuthamini zaidi bidhaa kutoka viwanda vya nje ya nchi. 

Wamefafanua wafugaji wengi wameanza kuamka na kuanza kufuga kibiashara kwa kutumia malighafi za mifugo, kuanzisha viwanda, ikiwemo viwanda vya kuchakata ngozi, kufungasha maziwa na nyama, teknolojia ya gasi itokanayo na kinyesi cha ng'ombe, na kuongeza kuwa changamoto kubwa ni ushindani mkubwa wa bidhaa za nje, unaotokana na dhana potofu ya jamii ya watanzania kutokununua bidha zinazotengenezwa nchini.

Msimamizi wa kiwanda cha Uchakataji Nyama, 'Maasai Exports Butchery', Frenk Mollel, amesema kuwa licha ya kuwa kiwanda hicho, huzalisha bidhaa za nyama zenye ubora wa kimataifa, lakini bado wananchi hawatumii bidhaa hizo kwa wingi, jambo linalosabisha soko la ndani kusuasua.

"Watu kutoka mataifa ya nje wananunua ng'ombe hapa nchini, wanasafirisha nje ya nchi, kule wanatumia mashine kama tunazo tumia sisi, lakini wakiingiza nchini bidhaa hizo, watanzania wananunua bidhaa hizo zaidi na kwa bei ya juu, wakidhani ni bora zaidi, ilihali kiwango cha ubora kinafanana na bidhaa ambazo tunazalisha hapa nchini," amesema Mollel.

Aidha, Mollel ameishauri Serikali na Taasisi zake, kuwa mfano kwa kutumia bidhaa za ndani, ikiwemo nyama inayozalishwa hapa nchini, kwa kufanya hivyo kutawapa hamasa wananchi kutumia bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi.

Kwa upande wake  mfugaji Leah Sangawe amesema ng'ombe ni zaidi ya biashara, kwa kuwa  ana uwezo wa kutoa malighafi nyingi tofauti, zinazoweza kuzalisha bidhaa ikiwemo chakula, mavazi, dawa, pamoja na mapambo na kuwashauri wafugaji kutokukatishwa tamaa na changamoto za masoko na kuendelea kuzalisha bidhaaa zenye ubora wa kushindana kwenye soko la kimataifa.

"Ng'ombe hutoa kwato kwaajili ya gundi, mifupa kwa ajili ya mapambo, ngozi kwa ajili ya viatu, maziwa na nyama kwa ajili ya chakula, kinyesi kwa ajili ya nishati hivyo unapamuuza ng'ombe nje ya nchi unapoteza faida nyingi ambazo zingesaidia kukuza uchumi wa taifa" amesema mfugaji huyo.

Sambamba na hayo, Ofisa Mifugo Halmashauri ya Arusha, Charles Ngiloriti, amesema, halmashauri imejipanga kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili wafugaji, ikiwa ni pamoja na kuwatembelea maeneo yao ya kazi, kuwapatia elimu wafugaji ili kuongeza thamani ya bidhaa zitokanazo na mifugo.

"Tumekuwa tukiwashirikisha wadau mbalimbali wa mifugo kwenye maonesho, semina na mikutano pamoja na kuwatembelea ili kubaini changamoto pamoja na kuwapatia elimu juu ya ufugaji bora wenye tija katika jamii" amesema Ngiloriti.

Daktari wa mifugo Halmashauri ya Arusha, Dk. Yohana Kiwone amewaambia wadau hao kuwa, halmashauri ipo kwa ajili ya kuwasaidia wafugaji wote, hivyo wanatakiwa kutumia fursa hiyo, kutatua changamoto zinazowakabili na kufanya uzalishaji bora unaokidhi viwango vya soko la kimataifa.

SHIRIKA LA SMILE TRAIN LAWAUNGA MKONO CCBRT KUSAIDIA WENYE WATOTO WANAOZALIWA NA TATIZO LA MDOMO WAZI

$
0
0

Ofisa wa maliasili watu na maendeleo wa hospitali ya CCBRT, Anastansia Melis akikabidhiwa mashine ya kufanyia upasuaji kwa watoto waliozaliwa na mdomo wazi kutoka Mkurugenzi wa Afrika Mashariki wa shirika la Smile Train's, Jane Ngige katikati ni Daktari wa upasuaji wa hospitali ya CCBRT, Zainab Ilonga. 

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Smile Train limetoa msaada wa mashine za kufanyia operesheni kwaajili ya kuwatibu watoto wanaozaliwa wakiwa na mdomo (Mdomo Sungura)katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kurejesha furaha kwa watoto hao.

Mkurugenzi wa Smile Train Afrika Mashariki Jane Ngige amesema leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wazazi wa watoto waliozaliwa na mdomo wazi (Mdomo Sungura) wakati akitoa mashine hizo.

Ngige amesema kuwa watoto wanatakiwa kuhudhuria shuleni bila kutengwa wala kuchekwa kwasababu tu ya kuzaliwa na tatizo la mdomo wazi, hivyo mashine ambazo wamezitoa kwa hospitali hiyo zitasaidia kufanya operesheni kwa watoto na hatimaye kurejesha furaha na kutobaguliwa na wenzao.

"Habari njema ni kwamba hali hii inaweza kuondolewa kwa kufanyiwa operesheni ya kawaida tu na wengine huenda wakafanyiwa operesheni zaidi ya mara moja, hivyo Smile Train tutaendelea kuiunga mkono CCBRT kwa kuwapa furaha maelfu ya watoto wanaozaliwa na tatizo la mdomo wazi,"amesema.

Kwa upande wake Dk.Zainau Ilonga kutoka CCBRT ameeleza tatizo la mdomo wazi linavyokuwa ambapo amefafanua mtoto mwenye tatizo hilo anazaliwa akiwa na uwazi kwenye sehemu ya juu ya mdomo au ya chini.

Amesema sababu za tatizo hilo huwa linatokea pale mtoto akiwa tumboni, sehemu ya mdomo juu au chini zinashindwa kuungana."Ni rahisi mtoto kuzaliwa akiwa na mdomo wazi wa chini au juu au yote miwili, na hili tatizo lipo katika nchi nyingi duniani ambapo kila watoto 500 hadi 700 mmoja anazaliwa na mdomo wazi lakini inategemea na eneo na shughuli za kiuchumi ndani yenyewe,"amesema.

 Dk. Ilonga amesema kwa Tanzania watoto wasiopungua 2500 wanazaliwa na mdomo wazi na sababu zake kwa hapa nchini haijafahamika lakini kuna sababu mbalimbali ambazo zinachangia mtoto kuzaliwa akiwa na mdomo wazi.

Ametaja baadhi ya sababu hizo ni uvutaji sigara kwa mama mjazito, uzito kupita kiasi na wakati huo huo zipo sababu zinazotokana na utumiaji wa dawa.

Awali Ofisa Rasilimali Watu na Maendeleo wa CCBRT Anastazia Melis amesisitiza kuwa kwa watoto wanaozaliwa na mdomo wazi wanapopata huduma ya operesheni ya kuondoa tatizo hilo wanakuwa na amani ya moyo kwani hawatakuwa kuwa katika kundi la kuchekwa au kubaguliwa.

Pia ametumia nafasi hiyo kuwashukuru Smile Train kwa kusaidia mashine 3259 ndani ya miaka saba. Pia amewaasa wananchi kwa ujumla wenye midomo wazi wwaende latika hospitali ya CCBRT wakafanyiwe Operesheni kwani huduma hiyo ni bure kabisa.
 Mkurugenzi wa shirika la Smile Train's Afrika Mashariki,  Jane Ngige(Katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya siku ya maadhimisho ya siku ya furaha ambayo hufanyika kila ifikapo Oktoba 5 kila mwaka.
Katika Kusheherekea siku hii shirika la Smile Train's wametoa mchango wa mashine za kufanyia upasuaji watoto wanaozaliwa na mdomo wazi katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam leo ili kushiriki furaha na watu wote bila kuwatenga watu katika siku mhimu kama siku ya furaha.
 Kushoto Daktari wa upasuaji wa hospitali ya CCBRT, Zainab Ilonga akizungu na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa maadhimisho ya siku ya furaha ambayo hufanyika kila ifikapo Oktoba 5 kila mwaka ili kushiriki furaha na watoto pamoja na watu wazima waliozaliwa na mdomo wazi na kufanyiwa oparesheni ili kuondoa hali ya kuwa na mdomo wazi. Na kulia ni Mkurugenzi shirika lisilo la kiserikali Afrika Mashariki wa shirika la Smile Train's, Jane Ngige
 Mmoja wa mzazi ambaye mtoto wake alizaliwa na mdomo wazi na akafanyiwa upasuaji katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari jinsi mtoto wake alivyotibiwa katika hospitali hiyo bila gharama zozote.
 Baadhi ya wazazi wa mzazi wa mtoto mwenye mdomo wazi, Veronika Joseph akizungumza na waandishi wa habari wakati akisubiria matibabu ya mtoto wake aliyezaliwa na mdomo wazi. Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema kuwa jamii kwa ujumla ijue kuwa matibabu ya watoto wanaozaliwa na mdomo wazi waende katika Hospitari ya CCBRT jijini Dar es Salaam kwani matibabu ni bure.
Pia amesema kuwa jamii kwa ujumla ionapo mtoto mwenye mdomo wazi wasimnyanyapae kwani hiyo hali watoto huzaliwa nayo.

JKCI KUTOA MAFUNZO YA DHARURA KWA WATAALAMU WA MUHIMBILI, MOI NA AMANA

$
0
0
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya kutoa huduma za dharula na jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo. Jumla ya washiriki 75 kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa MOI, Amana, Mwananyamala, Temeke na Mloganzila walihudhuria mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Idara ya usingizi na wagonjwa walioko katika uangalizi maalum.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akieleza umuhimu wa mafunzo ya kutoa huduma za dharula na jinsi ya kuwahudumia wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanavyoweza kuokoa maisha ya mgonjwa. Jumla ya washiriki 75 kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa MOI, Amana, Mwananyamala, Temeke na Mloganzila walihudhuria mafunzo hayo yaliyoandaliwa na JKCI Idara ya usingizi na wagonjwa walioko katika uangalizi maalum. Picha na JKCI
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi Daktari Bingwa wa usingizi na wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya mifupa MOI Asha Abdulla cheti cha ushiriki wa mafunzo ya siku mbili ya kutoa huduma za dharula na jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum. Jumla ya washiriki 75 kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa MOI, Amana, Mwananyamala, Temeke na Mloganzila walihudhuria mafunzo hayo yaliyoandaliwa na JKCI Idara ya usingizi na wagonjwa walioko katika uangalizi maalum.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi Daktari wa usingizi na wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Nsia Mushi heti cha ushiriki wa mafunzo ya siku mbili ya kutoa huduma za dharula na jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum. Jumla ya washiriki 75 kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa MOI, Amana, Mwananyamala, Temeke na Mloganzila walihudhuria mafunzo hayo yaliyoandaliwa na JKCI Idara ya usingizi na wagonjwa walioko katika uangalizi maalum.
 Daktari Bingwa wa usingizi na wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya mifupa MOI Asha Abdulla akitoa neno la shukrani wakati wa kufungwa kwa mafunzo ya siku mbili ya kutoa huduma za dharula na jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum. Jumla ya washiriki 75 kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa MOI, Amana, Mwananyamala, Temeke na Mloganzila walihudhuria mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Idara ya usingizi na wagonjwa walioko katika uangalizi maalum.

RAIA WA CHINA-SIJAANDIKA BARUA YA KUKIRI MAKOSA

$
0
0
RAIA wa China, Cheng Guo, anayeshuka kwenye gari, ameiarifu mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa yeye hajaandika barua ya kukiri makosa yake ila ameandika barua ya kulalamikia kucheleweshwa kwa kesi yake na kuomba msamaha. 

Katika kesi hiyo, mshtakiwa anakabiliwa na mashitaka ya kukutwa na nyara za serikali ambazo ni meno ya Tembo na kucha za Simba ambapo vyote vina thamani ya zaidi ya sh. Milioni 267. 4.

Mshitakiwa Guo amedai hayo leo Oktoba 4, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi wakati alipoletwa mahakamani hapo kwa hati ya kutolewa gerezani.

"Nimeandika barua nimesema kesi imechukua muda mrefu pia ninaomba msamaha, sijasema nataka kulipa pesa", amedai mshitakiwa Guo.

MIAKA 20 BILA BABA WA TAIFA NA MSAMAHA WA WAHUJUMU UCHUMI WA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Judith Mhina-Maelezo

Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni kati ya Marais wachache duniani ambao walikuwa  na utaratibu wa kusamehe watu wanaomkosea binafsi  na Taifa, kama vile wahujumu uchumi  na wahaini ambao walikuwa na fikra za kupata madaraka isivyo halali.

Baba wa Taifa tunamkumbuka  kwa matendo yake yaliyotukuka ambayo ni darasa tosha kwa viongozi hapa Tanzania na duniani kwa ujumla hususan Barani Afrika. Wapo viongozi wengi na wana zuoni ambao hawalali usiku na mchana kuchimba fikra za Mwalimu Nyerere na kuhimiza zifuatwe na kutekelezwa kwa kuwa zilikuwa na lengo la kuwaendeleza Waafrika na zina tija mpaka sasa.

Kati ya matendo hayo ni pale Mwalimu Nyerere anapowasamehe  watu mbalimbali walliomkosea hata kama sheria ilielekeza wafungwe maisha, kunyongwa hadi kufa  na adhabu nyinginezo lakini binafsi dhamira yake ilimtuma kuongea nao na kuwasamehe.

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli alitoa ushauri wakati akiwaapisha baadhi ya viongozi uliowateua tarehe 22 Septemba 2019, kuhusiana na watuhumiwa ambao wako tayari kukiri na kukubali kurejesha fedha za Watanzania katika kesi za madai za uhujumu uchumi.

“Rais Magufuli amesema siwezi kuongoza Taifa la watu wenye machozi, hivyo natoa rai wale wote ambao wapo mahabusu kwa tuhuma ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha nashauri  waandike barua ya kuomba radhi na kukiri makosa ili warejeshe fedha za umma walizochukua ili zikajenge shule, hospitali barabara na masuala mengine ya maendeleo”

Akimuelezea Rais Magufuli juu ya walioandika barua ya kuomba msamaha na kukiri makosa Muendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga amesema jumla ya watuhumiwa 467 wenye kesi za uhujumu uchumi wameandika barua na kuomba kukiri makosa yao. 

“Kati ya hao waliokiri, jumla ya shilingi Bilioni saba mia nane themanini na nne elfu mia tisa na moja na mia tano ishirini na sita (7,884, 901, 526) fedha za Tanzania, wako tayari kurudisha muda wowote kuanzia sasa”.

Aidha, kwa wale ambao walichukua fedha za kigeni ni jumla ya Dola za Amerika, elfu mbili mia tano sitini na tatu elfu, mia saba na nne na senti hamsini na nane,( 2, 563,704.58)  sawa na fedha za Tanzania Bilioni  tano milioni mia saba kumi na saba elfu sitini na moja na mia tatu na kumi na nne. (5, 717, 061, 314) zinarejeshwa alisema Mganga.

Watanzania waliowengi wanaona ni maajabu na ni kitu kisichewezekana katika dunia hii lakini la hasha, hata Baba  wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati wa vita vya uhujumu uchumi mwaka 1982-1984 watuhumiwa  wa Uhujumu uchumi  walitupa bidhaa mali na vitu kadhaa kwa kuhofia kukamatwa.

Aidha, wahujumu uchumi walio wengi walikamatwa na kukiri makosa yao na kuahidi hawataficha bidhaa, mali na vitu vinavyohitajika katika maisha ya kila siku ya Mtanzania au kuuza kwa bei ya juu (wakatu ule bei ya kuruka) ili kuihujumu serikali ya Tanzania. Lengo likiwa kuifanya Tanzania ikosolewe Kimataifa na kumpaka matope Baba  wa Taifa ambaye alikuwa na heshima ya kipekee duniani aonekani hafai. 

Hivyo, sio ajabu kwa Rais Dkt Magufuli kuhujumiwa na kulaumiwa kwa mema anayoyafanya na wasioitakia mema nchi yetu. Eti analaumiwa kwa kitendo chake cha kushauri na kuwapa nafasi wahujumu uchumi kukiri makosa yao na kurejesha fedha za Watanzania, ni ukweli usiopingika watu wanaokosoa  msamaha huu wanafanya hivyo kwa masilahi  yao binafsi.

Akiwasilisha kundi la pili ambalo lipo tayari kulipa fedha walizochukua kwa awamu Biswalo Mganga  amesema “Jumla ni Bilioni tisini na nne mia mbili arobaini mia moja hamsini elfu na tano elfu  watarejesha kwa awamu  (94,240, 155, 000) na kufanya jumla kuu ya fedha zote ambazo wahujumu uchumi walioomba na ambao wako tayari kuzirudisha ni Bilioni 107,842,112,744: 04”

Hii , ikiwa ni pamoja na mdaiwa wa Dola za Amerika laki nne na nusu (4,500) ambazo mtuhumiwa  alikuwa mahakamani ijumaa tarehe 27 Sept, 2019 na kukubali kuitikia wito wa kukiri na kurejesha fedha. Ambazo zina dhamani ya fedha za Tanzania Bilioni moja thelathini  na sita elfu mia sita sabini na mbili milioni (Bilioni  1, 036, 672, 000) ambazo zimelipwa pamoja na faini ya milioni tano zaidi. Alimalizia Biswalo Mganga.

Huu ni ujasiri  na utayari wa Watanzania wanapotenda kosa na kuonekana kihalali kweli wamelitenda wanapewa nafasi ya kukiri na kurejesha walichochukua. Hii yote inafanyika kwa masilahi ya Watanzania kwa kuwa hata kama akifungwa haitakuwa na mantiki kwa kuwa fedha ambazo zingewaletea maendeleo Watanzania hazitarudi.

Matendo yote haya yanaiwekea Tanzania katika ramani ya dunia  kuwa nchi ya Amani, Upendo na Mshikamano kwa kuwa kila mmoja anapewa nafasi ya kuongea kukiri na kurejeshwa katika jamii. Hii ina maana kubwa jamii inakuwa radhi  na ndio matokeo ya sasa kila Mtanzania kuona fahari kulipa kodi, ambayo inawanufaisha watu wote.

Tukubali  funzo hili tunalolipata kutokana na zoezi zima la Watuhumiwa kukaa ndani kwa siku kadhaa, na kuona adha waliyoipata wakiwa mahabusu, pamoja na kuishia kurejesha kile ambacho walidhani wana uhalali wa kuwadhulumu Watanzania. Hali hii italeta nidhamu ya fedha na mali za serikali kutochezewa hovyo na kudhani itawanufaisha Wahujumu uchumi na familia zao. 

Bado Rais Magufuli alitoa tahadhari kwa kuongeza siku saba za msamaha na baada ya hapo wale wote ambao hawataomba wasijewakidhani watahusika na masuala ya uhujumu uchumi, bali sheria itachukua mkondo wake. Aidha, alisisitika kesi zote mpya za uhujumu uchumi hawatahusika na msamaha huu, hii ikiwa ni onyo kwa wanaotaka kuhujumu nchi kuacha.

Watanzania tuwapokee kwa mikono mawili watanzania wenzetu waliokiri na kurejesha fedha  kwa roho safi. Tushirikiane nao katika hali na mali na kuhakikisha tunaijenga nchi yetu, nina hakika nchi ya maziwa na asali tutaifikia hivi punde kwa kuwa dalili za mvua ni mawingu. 

Tukumbuke  yaliyotokea serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo baadhi ya watanzania walikula njama za kuingia madarakani isivyo halali mwaka 1971. Wahusika takribani nane walikamatwa na kuwekwa ndani na kuhukumiwa kifungo cha maisha japo adhabu yake ilikuwa kunyongwa na miezi kadhaa baadaye alitoa msamaha na kuwaachia huru bila masharti yeyote.

Hii ilimletea sifa ya pekee duniani ni kiongozi aliyeongoza kwa kusamehe watu waliotaka kumuondoa madarakani  isivyo halali . Fatilia historia ya wahaini popote duniani hakuna aliyewaachia huru bali Babawa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Ambapo pia aliamua kuondoka madarakani kwa hiari yake mwenyewe mwaka 1985 na kumuachia kijiti cha uongozi Rais wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi, kitu ambacho kwa serikali za Afrika ilikuwa ni ndoto ya mchana kamwe hakikuwahi kutokea. Huyu ndiye Baba wa Taifa la Tanzania Pumzika kwa Amani Mwalimu.
04 Oktoba 2019

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AKUTANA IDARA YA MAZINGIRA NA MENEJIMENTI YA NEMC

$
0
0
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akiongoza kikao kazi alipokutana na Idara ya Mazingira pamoja na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) leo katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.
Watendaji kutoka Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiwa katika kikao na Katibu Mkuu Mhandisi Joseph Malongo.

DIT YAAMUA KUPELEKA WALIMU WAKE KATIKA MIRADI MIKUBWA YA SERIKALI

$
0
0
KATIKA kuhakikisha Tanzania inaendesha miradi yake mikubwa inayojengwa sasa na serikali ya awamu ya tano, taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) imepeleka walimu katika miradi hiyo kujifunza kwa vitendo na baadaye wawafundishe wanafunzi uendeshaji na ukarabati.

Baada ya walimu hao kujifunza itasaidia kupata ujuzi na maarifa ya kutosha kurudi kufundisha wanafunzi wa fani mbalimbali chuoni hapo hasa ikizingatiwa chuo hicho kimejikita katika masuala ya sayansi, teknolojia, uhandisi na tafiti.

Aidha, kwa walimu hao kujifunza itasaidia katika kipindi cha uendeshaji miradi kunakua na wataalamu wa kutosha kuendesha na kukarabati bila kutegemea tRNA wataalamu kutoka nje.

Miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), Mradi Mkubwa waUmeme wa Rufiji (Stiegler’s Gorge) na katika viwanda mbalimbali kupata ujuzi wa kufundishia.

Mkuu wa Idara ya Mahusiano Viwandani na Mhadhiri  wa Taasisi ya DIT, Dk.John Msumba akizungumza jijini Dar es Salaam amesema mpaka sasa walimu 30 wa fani mbalimbali zinazofundishwa katika taasisi hiyo wamepelekwa katika viwanda na miradi kujifunza kwa vitendo ili kuboresha kile wanachofundisha.

Dk.Msumba amesema kati ya walimu hao 30, sita wapo kwenye mradi huo wa reli ya kisasa
Amesema kutoa wanafunzi mahiri ni muhimu kuwa na wafundishaji mahiri ambapo DIT katika kuboresha elimu wanayoitoa wanaangalia kwa jicho la pekee suala la kuendeleza walimu wake pia.

“Katika kuboresha elimu tunayoitoa tunatazama kwa upande wa wanafunzi pia kwa watumishi wetu ambao ndio wafundishaji, kwa upande wa watumishi tumeanzisha utaratibu wa kuwapeleka katika viwanda na kwenye miradi mikubwa,” amesema Dk.Msumba.

Amefafanua walimu hao  kuna mambo ambayo wanayajua lakini kuna utaalamu mwingine kama vile wa kupasua miamba inahitaji kujifunza kwa ukaribu zaidi  ili itakapohitajika huduma hiyo wakati mwingine hapa nchini tayari tuwe na wajuzi wa kutosha bila kuhitaji kuchukua wataalamu kutoka nje.

“Pia kuna mainjinia ambao wako katika ujenzi wakijifunza kama kupasua miamba, ili tutakapohitaji kujenga miradi ya namna hii tusihitaji tena wageni kutujengea, tukihitaji ukarabati tuwe tunajua nini cha kufanya” ameongeza.

Aidha, amesema baada ya miradi hiyo kukabidhiwa kwa serikali kwaajili ya uendeshaji inabidi kujipanga kuwa na wataalamu katika maeneo mbalimbali ambao watashiriki kuendesha miradi hiyo pamoja na kufanya ukarabati .

“Sisi kama Taasisi tumesema tunataka kushiriki kwa kuandaa wataalamu ili itakapokuja katika uendeshaji wake, utafiti na kutatua matatizo mbalimbali ya kiteknikali tushiriki moja kwa moja," amesema Dk.Msumba.

Malengo ya Taasisi ya DIT ni pamoja na kutoka taaluma bora ya Uhandisi, Utafiti na ushauri wa kitaalamu ndani ya nchi na Afrika Mashariki kiujumla.

WATOA HUDUMA ZA MAJI WAKABIDHIWA VYETI, WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA MPYA YA 2019

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wamewataka watoa huduma za majisafi kuzingatia sheria mpya ya maji na usafi wa mazingira namba 5 ya mwaka 2019.

Hayo yamesemwa leo wakati wa hafla fupi ya utoaji vyeti kwa watoa huduma za maji kwenye maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam.

Lengo la hafla hiyo ni pamoja na kuwatambua na kuwapa vyetu vya uendeshaji iliyoandaliwa na DAWASA.

Akizungumza kabla ya kukabidhiwa vyeti hivyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Shabani Mkwanywe amesema sheria mpya ya maji inawataka kutoa huduma yenye ubora unaofanana na inayotolewa na DAWASA.

Amesema, baada ya kukabidhiwa vyeti hivyo watoa huduma za maji watakuwa na uhuru wa kusambaza majisafi katika maeneo yao na wanatambulika na DAWASA kwenye maeneo yao.

"Watoa huduma watatakiwa kutunza miundo mbinu katika hali ya ubora na usafi, kupima ubora wa maji na kutunza orodha ya wateja.,"amesema Mkwanywe na kuongeza kuwa masharti hayo siyo magumu kwa mtoa huduma yoyote makini´

"Naamini hakuna atakayeshindwa kuyatekeleza hasa ukizingatia kwa sasa hapatakuwa na kodi wala tozo lolote kutoka DAWASA, usumbufu wala changamoto ya kuongeza muda wa cheti endapo masharti yote yakifuatwa"

"Nafurahi kusikia kuwa mmepima na kujihakikishia ubora wa maji pamoja na miundo mbinu yenu imekaguliwa na taarifa muhimu za kiundeshaji zimepatikana, hivyo sasa mpo tayari kuwa wawakilishi wetu wazuri maeneo mnayoyahudumia,"amesema.

Mkwanywe amewaasa watoa huduma kufuata sheria hususani baada ya kupata vyeti na kuwa upo mkono wa sheria kwa wale wachache ambao watakwenda kinyume na taratibu za nchi za usimamizi wa huduma ya majisafi na wale watakaokiuka hawataongezewa muda wa cheti baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Neli Msuya akitoa mafunzo kabla ya utoaji wa vyeti alisema, kutakuwa na utaratibu wa kuratibu huduma za maji safi, ubora wa maji, usawa na upatikanaji, udhibiti wa usafi wa mazingira.

DAWASA wamekuwa wanafanya semina ili kutoa elimu na ufahamu wa jinsi DAWASA wanavyofanya kazi na pia kuelelezana njia bora za kuboresha ubora wa huduma za DAWASA.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Shabani Mkwanywe akizungumza na watoa huduma za Majisafi kwenye maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar ikiwa ni hafla maalumu ya kuwatambua na kuwapa vyeti vya uendeshaji.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii, Neli Msuya akizungumza na watoa huduma za Majisafi kwenye maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar ikiwa ni hafla maalumu ya kuwatambua na kuwapa vyeti vya uendeshaji.
Mtaalamu wa maabara Maliweza Shusha akizungumzia ubora wa maji kwa watoa huduma za maji na umuhimu wa kupima na kujihakikishia ubora wa maji ikiwemo kusafisha visima na matanki pale inapohitajika. Hayo aliyasema wakati wa hafla fupi ya utoaji vyeti kwa watoa huduma za maji kwenye maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Shabani Mkwanywe akikabidhi vyeti kwa watoa huduma za Majisafi kwenye maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar ikiwa ni lengo la kuwatambua na kuwapa vyeti vya uendeshaji. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii, Neli Msuya.

Watoa huduma za maji wakiendelea kupata elimu ya maji na kufahamu sheria mpya ya mwaka 2019 kabla ya hafla fupi ya utoaji vyeti kwa watoa huduma za maji kwenye maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam.
Picha zote na Zainab Nyamka.

ALIYEKUWA MHASIBU TAKUKURU AKIRI KOSA, KULIPA FAINI YA SHILINGI MILIONI 100

$
0
0
Mfanyabiashara Yasin Katare, wa mbele mwenye tisheti nyekundu, anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, pamoja na aliyekuwa Mhasibu wa Takukuru, Godfrey Gugai wa nyuma mwenye tisheti ya mistari ya punda milia na wenzao wakitoka katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Yasin kukiri kosa na kuhukumiwa kulipa faini ya shilingi Milioni 100. Washtakiwa wengine wamekana makosa hayo

Hatimaye Mwili wa nahodha wa mtumbwi uliozama ziwa Momela wapatikana

$
0
0


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Hatimaye mwili wa nahodha wa mtumbwi Samwel mhina (29)aliyezama kwa dhoruba ya upepo katika ziwa Momela mkoani Arusha siku nne zilizopita umepatikana.

Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha ACP Koka Moita amethibitisha kupatikana kwa mwili wa marehemu Samwel Gelda Mhina akiwa ameshafariki.

"Kwa kushirikiana na Jeshi la uokoaji na zimamaoto tumefanikiwa tumefanikiwa kuupata mwili wa marehemu Samwel Gelda Mhina,akiwa ameshafariki tayari" alisema Kamanda Moita.

Mkuu huyo wa wilaya ya Arumeru ametoa pole kwa familia na kusema kuwa huo ni msiba mzito,ambapo serikali ya awamu ya tano imefanya kila jitihada na ndani ya siku nne mwili huo umeweza kupatikana.

“Hili lilikuwa ni hitaji la ndugu wa samweli kwamba wanahitajika wawepo wazamiaji na sisi tulifanya kila jitihada za kuwapata wazamiaji kutoka dare s salaam waliingia jana na leo alfajiri tukaanza zoezi na ndani ya saa moja, tukadfanikiwa kuupata mwili wa Samweli akiwa ameshafariki.”alisema Jerry

Murro ametoa wito kwa jamii wasisubirie matukio yatokee ndipo wachukue tahadhari,bali amewataka kuchukua tahadhari wakati wowote,.
" Wazamiaji waliangalia chini zaidi kuona kama kuna mtu mwingine yeyote aliyekwama ziwani kwa bahati mbaya,kwa taarifa walizotupatia ni kwamba hakuna mtu mwingine anayehofiwa kuwa katika zile ziwa dogo la momela"alisema Murro.

Dedis Samwel Mhina ni baba mdogo wa marehemu wameishukuru serikali kwa kuwasaidia kuupata mwili wa ndugu yao,mwili umehifadhiwa katika hospital ya Mount Meru,taratibu za mazishi zitakapokamilika wanatarajia kumzika ndugu yao mkoani Tanga. 

Ikumbukwe kuwa tukio hilo la kuzama kwa mtubwi lilitokea majira ya saa 8:45 mchana oktoba 1,2019 katika kijiji cha Olkungwando,kitongoji cha Momela ,kata Ngarenanyuki,tarafa ya King'ori wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.

Mtalii Rosenbever Heike alifanikiwa kujiokoa kwa kuogelea ,nahodha Samwel Mhina akazama ziwani ambapo mwili wake umeoatikana leo octoba 4,2019 akiwa amefariki.

TIMU 14 DAR ZATINGA HATUA YA NUSU FAINALI MASHINDANO YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS NYEREE

$
0
0
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Utegi Enterprises (T)LMT Otieno Igogo (kulia) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu  udhamini wa michuano ya mchezo wa mpira wa miguu kuelekea katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere Octobar 14 mwaka huu.Kushoto ni Mratibu wa  mashindano hayo Shaban Mparure.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV
 TIMU 14 kutoka Kata ya Msigani Kinondoni jijini Dar es Salaam zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kuwania kombe la kumbukumbu ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

 Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo yaliyoanza Septemba 14 mwaka huu kwa kuwa na  timu 48 na kwamba timu ambazo zimeingia hatua ya nusu fainali  ambayo itaanza kutumia vumbi kuanzia Jumamosi ya wiki ijayo.

Katika kuhakikisha ushindani unakuwa mkubwa kwenye michuano hiyo Zawadi za vikombe na medani zitatolewa katika  timu ambazo zitashika nafasi ya kwanza na ya pili ambapo timu hizo zitafanyika katika makundi matatu na kila kundi linatimu nne.

Akizungumza zaidi leo Oktoba 4 ,mwaka huu jijini Dar es Salaam  mmoja wa waandaaji wa  mashindano hayo Shaban Mparure amesema katika kuhakikisha michuano inakuwa na ushindani walishirikisha timu  hizo 48 na timu  12 kati ya hizo ndio zimefanikiwa kuingia  hatua hiyo ya  nusu fainali.

Amesema kuwa mashindano hayo yamedhaminiwa na Mwenyekiti Mtendaji  wa kampuni ya UTEGI Techical Enterprises (T) LTD Otieno Igogo ambaye ndio ametoa vikombe na zawadi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini Mashindano hayo ya  kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Mparure amesema fainali za mashindano hayo zinatarajia kufanyika katika Uwanja wa  wa Uhuru jijini Dar es Salam kuazia Oktoba nane hadi Oktoba tisa na kwamba  kadri siku zinavyozidi kwenda watatoa ratiba kamili ya fainali hizo.

Kuhusu zawadi za washindi amesema mshindi wa kwanza atapata  Kombe kubwa na mpira mmoja na  zawadi wa mshindi wa pili itakuwa mpira mmoja.Pia kutakuwa na zawadi ya mchezaji bora.

Mparure amesema  lengo kubwa la kufanya mashindano hayo ni mwendelezo wa  kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alikuwa mpenda michezo na mzalendo wa nchi yake na Afrika kwa ujumla.

Awali akizungumzia udhamini wake Mwenyekiti huyo wa Kampuni ya Utegi interprises (T) LTD Otieno Igogo  amesema kuwa Mwalimu  alikuwa zawadi ya pekee  kwa ajili ya kuikomboa Afrika na mzalendo wa nchi yake na kwamba alihamasisha watu kuwa katika misingi hiyo pia aliweza kuunganisha nchi katika misingi ya umoja wa kitaifa.

Igogo amesema kwamba Nyerere alijenga misingi mizuri ya kikatiba na uhuru wa habari pia aliruhusu uwepo wa  mfumo wa vyama vingi na msingi mzuri wa kielimu.

Igogo amesema wao kama Kampuni wamejikita kwenye biashara ya forodha na zaidi ya miaka 35 ana endelea na kazi hiyo kuazia Mwaka 1984 .na amekuwa alifanya kwa nidhamu kubwa mno ikiwamo kulipa stahiki zote za Serikali.

Ameongeza kuwa yote ambayo anaya fanya ni katika kuendelea kumuenzi Mwalimu Nyerere na hasa kwa kutambua Oktoba 14 mwaka huu Watanzania tuna adhimisha miaka 20 ya kukumbuka ya kifo chake.

Amesema  ni matumaini yake kupitia mashindano hayo ya kumuenzi Mwalimu Nyerere vijana watapa nafasi ya kutambua mchango wa Mwalimu katika kuhakikisha  nchi yetu inakuwa na umoja,upendo na mshikamano na leo hii hakuna anayezingumzia ukabila wala udini.

ASKALI POLISI WATANO WA JWTZ WAHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILION 7.6

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu  Askari  Polisi watano na Mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kulipa faini ya Shilingi milioni 7.6 ama kutumikia kifungo cha mwaka miaka saba gerezani baada ya kukiri kosa la kuiba mafuta ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Washitakiwa hao, Koplo Shwahiba(38), MT. 74164 SGT Ally Chibwana (47) wa JWTZ, PC Elidaima Paranjo (38), PC Simon (28), PC Dickson  na PC Hamza ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi walifutiwa mashtaka ya utakatishaji fedha na kupanga genge la uhalifu na kubaki na mashtaka ya wizi.

Kabla ya kufutiwa mashtaka yao, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Renatus Mkude alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo kuwa, wameingia makubaliano na washitakiwa hao kumaliza shauri hilo hivyo, aliomba makubaliano hayo yawe sehemu ya shauri hilo.

Hakimu Mwaikambo alisema ni lazima mahakama ijiridhishe kama ni kweli washitakiwa waliweka makubaliano hayo kwa hiari bila kulazimishwa ndipo wakasema kuwa, waliandika makubaliano hayo wenyewe.

Akisoma adhabu, Hakimu Mwaikambo amesema amezingatia kwamba washitakiwa ni wakosaji wa kwanza na kuwa amezingatia msamaha uliotolewa na rais wa washitakiwa kukiri makosa yao na kupunguziwa kiwango cha makosa yao.

"Kila mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh 500,000 au kifungo cha miaka saba jela, pia mtatakiwa kulipa thamani yote mliyosababisha hasara kwa ATCL yaani Sh 4,647,760. Pia magaloni yote ya mafuta yanataifishwa na kuwa mali ya serikali," amesema Hakimu Vick.

Mapema kabla ya kusomwa hukumu hiyo,  Wakili Mkude aliieleza mahakama kuwa hawana taarifa ya nyuma ya washitakiwa hao na kwamba shauri hilo limeingia utaratibu wa makubaliano hivyo, suala la adhabu tunaiachia mahakama lakini pia tunaomba warudishe hasara waliyosababisha na kutaifisha madumu 109 ya mafuta ya ndege.

Kwa upande wake, wakili wa utetezi, Nestory Wandiba amedai washitakiwa wameokoa muda wa mahakama kwa kukubali kosa na kwamba kosa linalowakabili adhabu yake ni kifungo cha miaka saba au faini.

Katika kesi hiyo inadaiwa Julai 30, mwaka huu huko katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere uliopo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washitakiwa  waliiba lita 2180 za mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik) yenye thamani ya Sh  4,647,760 mali ya ATCL.

Bonanza la michezo Kufanyika kila baada ya Miezi Miwili

$
0
0
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo amesema kuwa Bonanza la Michezo litaendelea kufanyika kila baada ya miezi miwili na litahusisha michezo mbalimbali.

Bw.Singo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma alipozungumza wakati akishukuru Watumishi wa Serikali na wananchi wa Jijini la Dodoma waliojitokeza kushiriki Bonanza hilo.

“Bonanza hili litafanyika kila baada ya miezi miwili lengo ikiwa ni kuimarisha afya zetu pamoja na kuimarisha upendo,amani na mshikamano tulionao Tanzania”alisema Bw.Singo.

Aidha Bw.Singo amesema kuwa Bonanza hilo litashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo mbio za taratibu,mazoezi ya viungo, mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na michezo mingine.

Naye Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Bw.Daudi Manongi amesema kuwa Bonanza hilo limekuwa na faida nyingi kwani limewakutunisha Watumishi wa Serikali na Wananchi wa Jiji la Dodoma katika kuimarisha afya zao na kubadilishana uzoefu katika kutekeleza kazi zao.

Katika bonanza hilo timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya habari,Elimu na timu ya Joggin kutoka Dodoma ziliibuka washindi ,huku timu ya mpira wa miguu ya Serikali ikiifunga magoli matatu timu ya Boabao Queens ya Jiji la Dodoma iliyoambulia goli moja.
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.
Muongozaji wa mazoezi Bw.Simba akiongoza mazeozi ya viungo wakati wa Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.


Baadhi ya Watumishi wa Serikali na wananchi wa jiji la Dodoma wakifanya mazeozi ya viungo wakati wa Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.
4.Timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ikiwa uwanjani ikishindana na timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo timu hiyo iliibuka kidedea katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara hiyo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.
Timu za Mpira wa miguu za Serikali na Baobao Queens ya Jijini Dodoma zikichuana vikali katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma ambapo timu ya Serikali ilishinda kwa magoli matatu dhidi ya goli moja.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA PAMOJA NA UJENZI WA BARABARA YA MPEMBA-ISONGOLE KM 50.3 TUNDUMA MKOANI SONGWE

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ili kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma katika eneo la Mpemba Tunduma mkoani Songwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya majengo ya Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma katika eneo la Mpemba Tunduma mkoani Songwe.
Ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma katika eneo la Mpemba Tunduma mkoani Songwe ukiwa katika hatua za mwisho.
Mfano wa hospitali hiyo ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma utakavyokuwa mara baada ya kukamilika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Viongozi wengine kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa barabara ya Mpemba-Isongole km 50.3 itakayojengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili Mpemba mkoani Songwe .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mtoto Joan Schinga mmoja wa wanakwaya ya Watoto ya Light Angels ya Kanisa la Moravian Tunduma ambao waliimba wimbo wa kukemea Rushwa mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa barabara ya Mpemba-Isongole km 50.3 itakayojengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mpemba mkoani Songwe mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa barabara ya Mpemba-Isongole km 50.3 itakayojengwa kwa kiwango cha lami.
Wananchi wa Mpemba wakiwa katika shamrashamra za mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mbozi wakati akielekea Mpemba mkoani Songwe.
Wanakwaya ya Light Angels ya Kanisa la Moravian Tunduma mkoani Songwe wakiimba wimbo maalum wa kukemea Rushwa katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa barabara ya Mpemba-Isongole km 50.3 itakayojengwa kwa kiwango cha lami. PICHA NA IKULU.

Waziri Mkuu Majaliwa, aweka jiwe la msingi, katika kituo cha kupozea umeme 400/220/33kV, Shinyanga, Singida Dodomana Iringa awamu ya pili

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, katika kituo cha kupozea umeme 400/220/33kV, Shinyanga, Singida Dodoma na Iringa awamu ya pili, eneo Misuna, katika Wilaya ya Singida Oktoba 5.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Meneja Mradi wa kituo cha kupozea umeme 400/220/33kV, Shinyanga, Singida Dodoma na Iringa awamu ya pili, Peter Kigadye, kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo, eneo Misuna, katika Wilaya ya Singida Oktoba 5.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

UHAKIKI TAASISI ZA KIDINI NA JUMUIYA ZA KIJAMII KANDA YA ZIWA KUANZA OKTOBA 7 HADI 18

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, MOHA 

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kijamii na Taasisi za Kidini, itaanza kufanya uhakiki wa Jumuiya na Taasisi hizo awamu ya nne. Uhakiki huo utahusisha Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kagera na Shinyanga kuanzia Oktoba 7-18, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, ilisema uhakiki katika mikoa hiyo utafanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. “Katika uhakiki huo, Jumuiya na Taasisi husika zinapaswa kuwasilisha nyaraka mbalimbali, huu ni mchakato endelevu ambao unahusisha mikoa yote nchini,” alisema.

Alisema nyaraka hizo ni cheti halisi cha usajili na kivuli cha cheti hicho, stakabadhi ya mwisho ya malipo ada iliyolipwa hivi karibuni, katiba ya Jumuiya au Taasisi husika. Katiba hiyo ni ile iliyopitishwa na Msajili, barua ambayo inathibitisha uwepo wa Jumuiya, Taasisi husika kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa, Kata mahali ilipo ofisi ya Jumuiya, Taasisi, taarifa ya Mkutano Mkuu wa Mwaka na fedha ya mwaka.

“Fomu ya uhakiki inapatikana katika tovuti ya Wizara hiyo sambamba na kwenye kituo cha uhakiki,” alifafanua.

Meja Jenerali Kingu alisema taasisi ambazo zitashindwa kuhakikiwa kwa mujibu wa ratiba ya eneo husika zitalazimika kwenda Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma kwa ajili ya uhakiki na kama zitashindwa kufanyiwa uhakiki kwa muda uliopangwa zitaondolewa kwenye Daftari la Msajili.

Alisema Taasisi za dini na Jumuiya ambazo hazijasajiliwa zinatakiwa kufika wakati wa uhakiki ili ziweze kupewa utaratibu wa kupata usajili.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images