Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

EQUITY BANK YAJA NA MUONEKANO MPYA

$
0
0
Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Equity, Dk. James Mwangi, akiwaonesha Logo mpya ya Benki ya Equity, Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo Uganda, Apollo Makubuya (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Logo hiyo iliyozinduliwa Makao Makuu ya benki hiyo Upperhill, Nairobi nchini Kenya Oktoba 2 mwaka huu. 
************************************

NAIROBI, Kenya

BENKI ya Equity imezindua muonekano mpya wa logo ya benki hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuboresha utendaji kazi wa benki hiyo katika huduma na uboreshaji wa maisha ya watu ikidhamiria kuwa benki ya mfano Barani Afrika.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Equity, Dk. James Mwangi, zilisema kuwa muonekano mpya utaleta ufanisi katika huduma za kifedha, hasa kwenye uwanja wa utoaji wa huduma kielektroniki.

Alisema logo hiyo ni ya kipekee na imekuja wakati mwafaka katika kuleta mapinduzi kwa wateja wao, baada ya kupata ujuzi kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mjini hapa, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu, Dk. James Mwangi alisema, 

“Muonekano wetu mpya una akisi mtazamo mpya wa kibiashara, wateja na kuleta matokeo bora kwenye benki kuelekea katika mafanikio ya baadae pasipo na kusahau tulikoanzia”.

Alisema Benki ya Equity imedhamiria kuwa na ubora wake kwa kuzingatia malengo na dhamira ya kuwahudumia wateja kwa kuwawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali kupitia huduma zenye ubunifu na za kisasa. Uimarishaji wa huduma za kielektroniki pia utasawadia wateja wa Equity Bank kufungua fursa mpya za kibenki katika mfumo wa kielektroniki kwa kuangazia kuleta ufanisi katika ugunduzi wa huduma zake za kibiashara.

Equity Bank iliyoanza kutoa huduma miaka 35 iliopita na hadi sasa inatoa huduma za kimkakati katika nchi 9 za Afrika ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, South Sudan, Rwanda, Democratic Republic of Congo (DRC), Zambia, Msumbiji na Ethiopia.
Mwenyekiti wa Bodi ya Makampuni ya Equity, Mhandisi. Raymond Mbilinyi (kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti (katikati) na Mkurugenzi asiyekuwa na majukumu, Dino Stengel wakifurahia jambo wakati wakipiga picha ya pamoja mbele ya bango lenye Kogo mpya ya Benki hiyo ya Equity wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika Oktoba 2, mwaka huu Makao Makuu ya benki hiyo, Upperhill, Nairobi nchini Kenya.

Wasichana Tabora Kuwania Uongozi

$
0
0
Na, Editha Edward-Tabora 

Baadhi ya Wasichana Mkoani Tabora wamesema hawata kuwa nyuma kuwania nafasi za uongozi katika chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi mkuu ujao wakiamini Kuwa kupata uongozi kutasaidia kuimarisha nguvu Katika Kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyodaiwa kuja ndoto za maisha yao

Wameyasema hayo katika kongamano la ajenda ya msichana ya 2019 lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Msichana Initiative lililofanyika chuo cha utumishi wa Uma mjini Tabora ambapo limehusisha  wasichana 800 kutoka katika wilaya tatu za mkoa wa Tabora ambazo ni Uyui, Nzega, na Tabora mjini 

Akifungua kongamano hilo mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema Serikali itaendelea Kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo kimsingi vinadaiwa kuwaathiri wasichana kimwili na Kisaikolojia na hivyo kusababisha kuwadhorotesha kifikila na kiuchumi ikiwemo kuwania uongozi

"Jitihada za shirika la msichana initiative pamoja na serikali hazotaishia hapa kwa Sababu tunataka mtoto wa kike asome hadi elimu ya juu ili aepukane mimba za utotoni na ndoa za utotoni ili baadae akawe kiongozi bora wa kesho"Amesema Mwanri 

Aisha Uledi ni miongoni mwa wasichana walio hudhuria kwenye kongamano hilo amesema semina hiyo imewasaidia kwa kiasi kikubwa kwa wasichana na kujitambua na kuweza  kuwania nafasi za uongozi

Kwa Upande wake  Mkurugenzi mtendaji wa shirika la initiative msichana Rebeca Gyumi amesema kongamano hilo litaweza kusaidia jamii kuona ni jinsi gani msichana ataweza kuonesha na Kutumia nguvu zake mwenyewe kama chachu ya maendeleo kukomesha ukatili wa kijinsia 

Aidha mkoa wa Tabora ni miongoni mwa mikoa mitatu nchini inayoongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo shirika lisilo la kiserikali la Msichana Initiative linatekeleza Mpango wa kuwajengea uwezo wasichana  ili iwe kichocheo cha Kushiriki vita dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani Mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni.
 Pichani ni wasichana walioshiriki katika kongamano hilo la ajenda ya msichana mkoani Tabora.
Pichani ni mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza na wasichana (Pichani hawapo)  katika kongamano la msichana lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Initiative.

TRC YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU FURSA ZA AJIRA ZAIDI YA 200 TRC

MABULA AVUTIWA KASI YA UJENZI MRADI WA MACHINJIO YA VINGUNGUTI

$
0
0
Mhandisi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Elisante Ulomi akimuonesha maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Machinjio ya Vingunguti Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa mradi huo jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Machinjio ya Vingunguti kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa Muungano Saguya (kulia) na kushoto ni Mhandisi wa mradi huo Elisante Ulomi.

********************************

Na Munir Shemweta, WANMM

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametembelea mradi wa ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti na kuvutiwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo inayofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo alilitaka shirika hilo kuhakikisha linajenga jengo lenye ubora.

Akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo jana, Dkt Mabula alisema pamoja na mradi huo kutakiwa kukamilika katika kipindi cha miezi mitatu badala ya 12 ya awali lakini hatarajii kuona Shirika la Nyumba linajenga jengo lililo chini ya kiwango.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, NHC ni shirika la umma lenye kila fani katika masuala ya ujenzi hivyo basi ujenzi wa mradi huo ujenge imani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watanzania kwa kukamalisha mradi huo katika kipindi cha miezi mitatu.

Dkt Mabula alisema, Maelezo ya Rais kuhusiana na mradi wa machinjio ya Vingunguti ubadilishe fikra za Shirika la Nyumba la Taifa katika miradi yake mbalimbali sambamba na kuonesha uwezo katika miradi waliyopewa kwa kujenga kwa kasi na kwa muda mfupi ukilinganisha na makampuni mengine ya ujenzi.

‘’Tuondoke katika fikra tuliyokuwa nayo huko nyuma, tujenge trust kwa mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’’ alisema Dkt Mabula

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Muungano Saguya alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa shirika hilo limejipanga kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha linakamilisha ujenzi katika muda uliopangwa.

Alisema ujenzi wa mradi huo wa machinjio ya Vingunguti umefikia hatua nzuri na ana imani kutokana na jinsi shirika lilivyojipanga katika mradi huo, ujenzi wake utakamilika katika muda uliopangwa kama ilivyoelekezwa na rais

WATENDAJI SERIKALINI WATAKIWA KUTENDA HAKI WAKATI WA UJAZAJI WA FOMU ZA OPRAS ZA WATUMISHI ILI KUEPUKA KUSHUSHA ARI YA UTENDAJI KAZI

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Simiyu (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
Katibu Msaidizi Ajira na Nidhamu, Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Celina Maongezi akiwasilisha mada, wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma na Watumishi wa Mkoa wa Simiyu kilichofanyika katika Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa ufafanuzi wa hoja, wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kushoto), Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma na Watumishi wa Mkoa wa Simiyu kilichofanyika katika Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini wakati wa kikao kazi kati yake na Watumishi wa Mkoa wa Simiyu kilichofanyika katika Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
Baadhi ya Watumishi wa Umma kutoka Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.

****************************



Na Happiness Shayo- SIMIYU (Bariadi)

Serikali imewataka Watendaji katika taasisi za umma kuacha vitendo
vya upendeleo wakati wa ujazaji wa fomu za OPRAS kwa watumishi
wa umma nchini ili kupima utendaji kazi wao, lengo likiwa ni kuepuka
kushusha morali ya utendaji kazi kwa watumishi hao.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa
(Mb) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa umma mkoani
Simiyu kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Bariadi
Alliance mkoani humo.

“Hakikisheni mnajaza fomu za OPRAS kiuhalisia bila upendeleo ili
kila mtumishi apate haki yake anayostahili, epukeni kuwakatisha
tamaa watumishi wanaofanya kazi kwa bidii” Dkt. Mwanjelwa
amesisitiza.

Dkt. Mwanjelwa ameweka bayana kuwa, watumishi wanaofanya kazi
pamoja wanajuana kiutendaji, hivyo si jambo zuri kwa mtendaji
kumpendelea mtumishi wakati wa ujazaji wa fomu za OPRAS.

“Serikali inahitaji OPRAS ambayo itaziba kabisa mianya ya
upendeleo”, Dkt. Mwanjelwa amehimiza.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa amefafanua kuwa, ujazaji wa fomu za OPRAS
unatakiwa uzingatie uchapakazi wa mtumishi ikiwa ni pamoja na
tabia na mwenendo wa mtumishi kwa ujumla.

“Kuwa mtumishi wa umma ni pamoja na kuwa na mwenendo bora.
Mtumishi mwenye mwenendo mbaya hafai kuwa katika utumishi wa
umma”, Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Dkt. Mwanjelwa amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa
kutoa mafunzo ya OPRAS kwa watumishi wa mkoani humo na
kuwataka kuendelea kuwaelimisha watumishi ili kila mtumishi atambue haki na wajibu wake.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa kikao kazi hicho, Mkaguzi
Mkuu wa Nje wa mkoa huo, Bw. Costantine Mabirika amemshukuru
Dkt. Mary Mwanjelwa kwa kutoa elimu na maagizo ya kiutendaji,
hivyo ameahidi kuwa yatatekelezwa ipasavyo ili kuboresha utendaji
kazi wao.

Kikao kazi hicho ni muendelezo wa ziara ya Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt.
Mary Mwanjelwa (Mb) mkoani Simiyu yenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji kwa watendaji na watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na
kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.

WAZIRI MKUU AKAGUA SHAMBA LA KOROSHO MANYONI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua shamba la mfano la korosho lenye ukubwa ekari 12,000 lililopo kijiji cha Misigati, wilayani Manyoni na kusema kuwa ameridhishwa na uamuzi wa wilaya hiyo kuwa na zao mbadala la biashara.

Akizungumza na wananchi na baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo waliokuwepo eneo hilo jana (Ijumaa, Oktoba 4, 2019), Waziri Mkuu alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi kwa kulibeba wazo hilo na kuhakikisha linatimia.

“Nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa kulibeba jambo hili, lakini nikuombe wewe na viongozi wenzako mhamasishe wengine walime zaidi zao hili kwa sababu korosho ni zao kubwa duniani na tena zao hili lina bei nzuri kimataifa,” alisema.

Alisema anatambua kwamba timu ya wataalamu kutoka kituo cha utafiti wa kilimo cha Naliendele, Mtwara imeshawasili Manyoni ili kufanya utafiti za zao hilo na jinsi linavyoweza kuzaa mara mbili kwa mwaka.

“Kwa kawaida, mkorosho mmoja hutoa kilo 40 za korosho kwa msimu mmoja, kwa hiyo kwa misimu miwili mtapata kilo 80. Ninawasii limeni korosho kwa ajili ya watoto wenu ambao wako darasa la pili au la tatu. Mkulima ukianza kuvuna, utaendelea kuvuna kwa miaka 20 mfululizo na kwa hiyo hao watoto hawatahitaji kulipiwa ada wakiwa chuo kikuu sababu korosho itakuwa inawalipia,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wakulima wanaolima zao hilo wilayani Manyoni, waunde Ushirika wao ambao utawasaidia kuagiza dawa kwa pamoja ama kuuza kwa pamoja.Hivyo, amemwagiza Afisa Ushirika wa Wilaya hiyo, Bi. Yusta Philipo ahakikishe anasimamia jambo hilo kuanzia sasa.

Mapema, akitoa taarifa juu ya mradi huo, Meneja wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Kanda ya Kati, Bw. Ray Mtangi alimweleza Waziri Mkuu kwamba mradi wa kilimo cha korosho unajumuisha mashamba makubwa mawili ambapo shamba la Misigati lina ukubwa wa ekari 7,000 na lile la Mikwese lenye ukubwa wa ekari 5,000.

Alisema watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kitaifa wamekuwa wakifika shambani hapo ili wajifunze mbinu mpya za kuzalisha korosho kwenye maeneo yao. “Wiki mbili zilizopita, Mheshimiwa Spika na madiwani wa Kongwa walipita hapa ili kujifunza zao hili,” alisema.

Pia alisema Halmashuri yao imetenga eneo la ujenzi wa viwanda na kwamba hadi sasa wanazo ekari 50 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kubangua korosho.Mapema, Waziri Mkuu alikagua shamba hilo na kujionea hali halisi ya shambani ikoje. Pia alioneshwa mabibo na korosho ambazo zimevunwa kutoka kwenye shamba hilo la mfano, kutoka kwenye mashamba ya wakulima ambao walipanda miche tangu Januari, mwaka jana.

WANANCHI HALMASHAURI YA MJI NEWALA KUNUFAIKA NA ZAHANATI ILIYOJENGWA NA TASAF

$
0
0
Mwenge wa Uhuru ukiwa mbele ya Zahanati ya Tupendane iliyojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mara baada ya ujumbe wa Mwenge huo kuitembelea Halmashauri ya Mji Newala ili kukagua na kujiridhisha na ujenzi wa zahanati hiyo. Kiongozi wa Kitaifa wa Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2019, Ndugu Mzee Mkongea Ali ameweka jiwe la msingi katika zahanati hiyo.
Sehemu ya viongozi na wananchi wa kijiji cha Tupendane katika Halmashauri ya Mji Newala waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru mara baada ya ujumbe wa Mwenge huo kuwasili kwa ajili ya ukaguzi wa ujenzi wa zahanati katika kijiji hicho.
Mwenge wa Uhuru ukiwa mbele ya Zahanati ya Tupendane iliyojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mara baada ya ujumbe wa Mwenge huo kuitembelea Halmashauri ya Mji Newala ili kukagua na kujiridhisha na ujenzi wa zahanati hiyo. Kiongozi wa Kitaifa wa Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2019, Ndugu Mzee Mkongea Ali ameweka jiwe la msingi katika zahanati hiyo.

WANAFUNZI WAELEZA UELEWA MDOGO WA JAMII AFYA YA UZAZI IMEKUWA NI CHANZO CHA NDOA NYINGI ZA UTOTONI

$
0
0
Na Jusline Marco-Arusha

Vijana wa shule ya sekondari Musa, halmashauri ya Arusha, wameweka wazi kuwa, uelewa mdogo wa jamii kuhusu afya ya uzazi, imekuwa ni chanzo cha ndoa nyingi za utotoni.

Wakizungumza katika mdahalo wa Afya ya uzazi kwa vijana, uliofanyika kwenye shule ya sekondari Musa iliyopo wilayani Arumeru,mdahalo uliohusisha wanafunzi wa shule hiyo, wamesema kuwa, licha ya changamoto nyingi zinazowakabili vijana, bado uelewa mdogo wa vijana juu ya afya ya uzazi unasababisha ndoa za utotoni na vijana kujikuta kwenye changamoto nyingi za kimaisha.

Wamefafanua kuwa mara nyingi vijana hushauriana wao kwa wao, juu ya mabadiliko ya kimwili yanayoambatana na kuanza mahusiano ya kimapenzi, kwa kupeana taarifa zisizo sahihi, jambo ambalo husababisha mimba zisizotarajiwa pamoja na ndoa za utotoni. 

Wameongeza kuwa kutokana na mila na desturi za jamii zao, inaonesha wazi kuwa hata wazazi hawana uelewa wa kutosha juu ya afya ya uzazi kwa vijana pamoja na mabadiliko ya kimwili kwa vijana jambo ambalo linasababisha vijana kubaki njia panda na pengine kushindwa kufikia malengo yao kwa kukatiza ndoto zao.

Wanafunzi hao wakwenda mbali zaidi na kusema kuwa endapo wazazi wangekuwa na uelewa sahihi juu ya afya ya uzazi kwa vijana wasingewalazimisha wasichana kuolewa wakiwa na umri mdogo kwa kuhofia wasichana hao kupata mimba kabla ya ndoa.

Kadhalika katika mdahalo huo vijana walipata fursa ya kujadili kwa kina juu ya afya ya uzazi na changamoto za mabadiliko ya kimwili zinazosababisha mihemko na namna ya kukabiliana na hisia.

Hata hivyo halmashauri ya Arusha kupitia mradi wa TCI - TUPANGE PAMOJA , unaotekelezwa na shirika la Jhpiego Tanzania wameanzisha huduma Rafiki kwa Vijana, huduma zinazotolewa bure kwenye zahanati na vituo vya afya na kuwataka vijana kwenda kwenye zahanati kupata elimu zaidi juu ya afya ya uzazi kwa vijana.

MEYA MSTAAFU KINONDONI YUSUFU MWENDA AWAOMBA WADAU KUCHANGIA SEKTA YA ELIMU ILI KULETA USTAWI BORA KATIKA JAMII

$
0
0
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni akimlisha keki mmoja wa watoto wa darasa la awali katika Shule ya Mikocheni A ikiwa ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akiwapongeza mmoja wa watoto aliyesoma vizuri risala kwa niaba ya watoto wenzake
Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni akikagua darasa kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la awali linalokarabatiwa kwa ufadhili wake.
Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akipata viburudisho na wanafunzi.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akiwapongeza mmoja wa watoto aliyesoma vizuri risala kwa niaba ya watoto wenzake.

******************************

MEYA Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda amewaomba wadau mbalimbali nchini kujitokeza kwa namna mbalimbali kuchangia elimu ili kuleta ustawi bora katika jamii .

Ametoa rai hiyo jana wakati alipokuwa akikabidhi moja ya darasa katika shule ya Msingi Mikocheni ‘A’ alilolikarabati kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la awali hatua iliyoendana na hafla fupi na watoto hao ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.

Mbali na ukarabati huo Meya huyo mstaafu pia alikabidhi viti na meza kwa ajili ya wanafunzi hao wa darasa la awali ili kuwaondolea changamoto ya ukaaji pindi wanapokuwa darasani.

Mwenda alisema kama jamii itajenga utamaduni wa kuzikumbuka shule walizosoma na kwenda kutoa misaada inayohitajika katika shule hizo kwa kiasi kikubwa watakuwa wametoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya shule hizo na sekta nzima ya elimu nchini.

“Serikali inafanya mambo mengi sana katika elimu lakini nasi kama wananchi hatuna budi kujitokeza na kuiunga mkono ili iweze kutimiza azma yake kikamilifu kwa kuchangia japo kidogo kwa kile tunachojaaliwa kuwa nacho” alisema Mwenda

Awali Mwenda alipata fursa ya kutembelea mazingira ya shule hiyo na kujionea hali ya uchakavu mbalimbali wa majengo hatua iliyotokana na kujengwa miaka mingi huku uongozi wa shule hiyo ukimuomba kuwasaidia ukarabati wa ofisi ya walimu.

Walisema kutokana na uchakavu wa majengo ya shule hiyo wamelazimika kutumia moja ya darasa kuwa ofisi yao licha ya kukosa sifa zinazotakiwa na kwamba wanafanya hivyo kutokana na uwepo wa changamoto ya majengo mahali hapo

Aidha Mwenda alilikubali ombi hilo na kuhahidi kulifanyia kazi ili kuwaondolea walimu hao adha wanayoipata wakati wanapotekeleza majukumu yao.

MAKAMU WA RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MENEJMENTI YA OFISI YAKE JIJINI DODOMA

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Menejmenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira katika kikao cha kazi ikiwemo Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Mazingira, kikao hicho kimefanyika leo Octoba 05,2019 katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtumba Jijini Dodoma.

Wananchi washauriwa kujiepusha na vichocheo vya maradhi ya Moyo

$
0
0
Wananchi wametakiwa kupunguza utumiaji wa vileo, uvutaji wa sigara pamoja na vyakula vyenye mafuta mengi ikiwemo chapati, mandazi na vitumbua kwani vinavyochochea ongezeko la maradhi ya moyo na badala yake wamehimizwa kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara.


Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji wa Maradhi ya Moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando iliyopo jijini Mwanza, Prof. William Mahalu ametoa rai hiyo Oktoba 05, 2019 kwenye mazoezi/ matembezi ya afya yaliyofanywa na wafanyakazi wa hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho kilele ya Siku ya Moyo Duniani 2019.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wakiwa kwenye mazoezi ya afya katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara.
Wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wakihitimisha kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani 2019 kwa kufanya mazoezi ya afya.
Wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wameweka utaratibu wa kufanya mazoezi ya afya mara mbili kila mwezi ili kutoa hamasa kwa wananchi wengine kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi.
Matembezi/ mazoezi ya afya kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Rifaa ya Kanda ya Ziwa Bugando iliyopo jijini Mwanza.
Maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani hufanyika kila mwaka Septemba 29.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani 2019 ni "ahadi ya moyo wangu, moyo wako na mioyo yetu sote" ikilenga kuhamasisha kila mmoja katika jamii kuwa balozi wa kuzingatia kanuni za kiafya ikiwemo mazoezi na ulaji wa vyakula ili kuepukana na maradhi ya moyo.
Mratbi wa Mazoezi kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa Bugando akisisitiza umuhimu wa kufanya mazoezi.
Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando, Prof. William Mahalu (kushoto) akizungumza baada ya mazoezi/ matembezi hayo kufikia tamati.
Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando, Prof. William Mahalu (katikati) akizungumza na wanahabari.
Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando, Prof. William Mahalu (kulia) akionesha baadhi ya nembo za wafadhili waliosaidia upatikanaji wa tisheti kwa ajili ya matembezi hayo.

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA ZAMBIA EDGAR LUNGU,WAFUNGUA KITUO CHA PAMOJA CHA HUDUMA ZA MPAKANI (ONE STOP BORDER POST)

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kufungua Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Nakonde Zambia



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda mti pamoja na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kufungua Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Nakonde Zambia . PICHA NA IKULU


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshma iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika eneo hilo la Tunduma mkoani Songwe.

 Wafanyakazi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania na Zambia wakiwa tayari kwa kutoa huduma katika eneo hilo la mpakani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kuwasili katika eneo la Nakonde Zambia.




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu wakati wakisalimia wananchi mara baada ya kuwasili katika Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania. 
 Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu akifurahia hotuba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu wakati wakisalimia wananchi mara baada ya kuwasili katika Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

 Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu akizungumza kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.



 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kuwasili Tunduma mkoani Songwe kwa ajili ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.


MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YAMEPUNGUA TANDAHIMBA-DC WARYUBA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema maambukizi ya virusi vya ukimwi yamepungua kwenye Wilaya ya Tandahimba na amewataka wananchi kujiepusha na maambukizi mapya

Ameyasema hayo leo asubuhi wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa  Uhuru Mzee Mkongea Ally  katika Kijiji cha Nanyhanga 

Mwenge  wa Uhuru umepitia miradi ya maendeleo  yenye thamani ya zaidi ya Bil 1.7 Wilayani humo na yote imeridhiwa.

WAZIRI MKUU AAGIZA DED MKALAMA ACHUNGUZWE

$
0
0
*Agoma kuweka jiwe la msingi la hospitali ya wilaya hiyo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Singida, Bw. Adili Elinipenda amchunguze Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkalama, Bw. Godfrey Sanga kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.

Baadhi ya tuhuma alizonazo ni kujilipa posho ya safari Machi mwaka huu bila kusafiri, kuwasainisha watumishi wa chini yake vocha na kisha kuwapa ‘asante kidogo’ kwa madai fedha hizo zinaenda mkoani, kujilipa stahiki kabla ya wakati na kuagiza gari liende gereji kwa matengenezo bila nyaraka zozote.

Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumamosi, Oktoba 5, 2019), wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmshauri hiyo.

“Kuna watumishi wanne uliwaambia wasaini vocha ya sh. 1,320,000. Hii ni kwa safari iliyopangwa kati ya tarehe 15 na 24 Septemba, mwaka huu; ukawapa asante ya sh. 30,000 ukidai kuwa zinatakiwa mkoani. RAS ni kweli hela hiyo ililetwa mkoani?” Alihoji Waziri Mkuu na kujibiwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Dkt. Anjelina Lutambi kwamba hakutoa hayo maagizo.

Alipoulizwa Mweka Hazina wa Wilaya hiyo, Bw. Peniel Mbula kwamba fedha alilipwa nani, mweka hazina huyo alijibu kwamba alikuwa Dodoma kikazi. Mhasibu aliyekaimu nafasi yake, Bi. Lulu Hamadi aliwataja watumishi hao kuwa ni Stella Mawa, Godfrey Mnubi, Richard Laizer na Method Kafuku.

Waziri Mkuu aliwasimamisha watumishi hao na kuwauliza walilipwa hiyo posho ili waende wapi lakini walikosa majibu. Ndipo akawaeleza kwamba walimkabidhi Mkurugenzi na wakalipwa asante ya sh. 30,000.

Alipoulizwa kuhusu malipo ya sh. 1,090,000 ambayo yalilipwa Septemba 9, mwaka huu yalikuwa ya nini, Mkurugenzi huyo alijibu kuwa ni ya stahiki zake za kila mwezi ambapo kati ya hizo, sh. 600,000/- ni za malipo ya nyumba; sh. 230,000  ni za umeme na sh. 260,000 ni za simu. Lakini hakuweza kujibu ni kwa nini amejilipa kabla mwezi haujaisha.

Kuhusu gari la elimu lenye namba za usajili STK 913 lililopelekwa gereji kupakwa rangi kwa gharama ya sh. milioni saba, Waziri Mkuu alitaka aoneshe dokezo lililotumika kupitisha idhini hiyo na malipo hayo lakini akajibiwa kwamba hakuna utaratibu wa kuandika dokezo pindi magari ya Halmashauri yanapoenda kufanyiwa matengenezo bali wanapeana taarifa kwa mdomo tu.

“Kamanda wa TAKUKURU leta maafisa kutoka mkoani waje wafanye ukaguzi wa kila jambo ambalo limeainishwa. Hatuwezi kuacha Halmashauri iendeshwe kienyeji bila kufuata taratibu. Mkalama inaonekana chafu kumbe tatizo ni mtu mmoja, mnasaini vocha halafu mnamsingizia RAS,” alisema.

“Ajenda ya kikao changu nanyi watumishi wenzangu, nilitaka tuambiane kwamba ni lazima tutunze mali na fedha za Serikali. Waheshimiwa Madiwani ni lazima msimamie Halmashauri yenu na mhoji kila senti imetumika vipi. Kama ni jengo nendeni mkakague, kama ni kisima nendeni mkaangalie,” alisisitiza.

“Pia niwasihi Waheshimiwa Madiwani wenzangu, msikubali kutumika kupitisha matmizi ya fedha ambayo si sahihi,” aliongeza.

Watumishi wa Halmashauri hii mfanye kazi, muache ubabaishaji sababu Serikali hii iko makini sana. Msiishi kwa mazoea, kwa sababu wakati siyo wenyewe na tena muache kutengezeza syndicates,” aliwaonya.

Pia amemuonya Afisa Manunuzi wa wilaya hiyo, Bw. Dickson Mataramba aache kutumika na kufanya kazi kwa mazoea kwa kupandisha bei ya sh. elfu 2000 hadi 3,000 kwenye vifaa wanavyoagiza.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amekataa kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya kwa sababu lilikataliwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge na uchunguzi wake bado haujakamilika.

“Jiwe la msingi mlilonipangia kuweka leo kwenye hospitali ya wilaya siweki hadi TAKUKURU wakamilishe kazi ya uchunguzi kuhusu mikataba iliyotumika. Mkikamilisha uchunguzi mniite, nitakuja kulizindua likiwa limekamilika,” amesema.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,  akizungumza na Watumishi wa Halmashauri pamoja na Madiwani, katika ukumbi wa Halmashauri ya Mkalama, mkoani Singida. Oktoba 5.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,  akimhoji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Godfrey Sanga, kutokana na matumizi mabaya ya fedha za Umma, Oktoba 5.2019. wakati alipozungumza na Watumishi wa Halmashauri pamoja na Madiwani, katika ukumbi wa Halmashauri ya Mkalama, mkoani Singida. 

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,  akiwahutubia wananchi wa Nduguti, wilayani Mkalama, kwenye mkutano wa hadhara Oktoba 5.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 Wananchi wa Nduguti, wilayani Mkalama, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati  akihutubia, kwenye mkutano wa hadhara Oktoba 5.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

DAWASA YAWEKA MALENGO YA KUKUSANYA BILIONI 12 KWA MWEZI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) imejiwekea malengo ya kufikia Kiasi cha Shilling Bilioni 12 kwa mwezi katika makusanyo ya ankara za maji kwa wateja wake Dar es Salaam na Pwani.

Ndani ya Mwaka mmoja Dawasa wameweza kuongeza ukusanyaji wa ankara za maji kwa kukusanya Shilingi Bilioni 11. 11 mwezi Septemba mwakaa hu.

Mkurugenzi wa Biashara na Huduma kwa Wateja, Ritamarry Lwabulinda amesema kabla ya  kuunganishwa kuwa Dawasa moja, Makusanyo ya mwezi Agosti mwaka jana ankara za maji kwa mwezi yalikuwa Bilioni 9.2.

Amesema, kiwango cha mapato ya ndani ya mwaka mmoja wa Dawasa kimekuwa kutoka wastani wa makusanyo ya Sh. Bil 9.2 kwa mwezi hadi sasa wanakusanya wastani wa Sh. Bil. 11 kwa mwezi.

“Kwa mwaka wa fedha uliokwisha Dawasa ilikusanya Sh. Bil. 135 sawa na asilimia 95 ya lengo” alisema

Ritamarry amesema kuongezeka kwa mapato ndani ya mamlaka yanatokana na wateja ambao ni waaminifu, kudhibiti mivujo na mamlaka kuzidi kutanua wigo wa utoaji huduma kwa wateja wa zamani na wapya.

"Upotevu wa maji umepungua kwa asilimia kubwa ambapk mwaka 2015 upotevu ulikuwa asilimia 53 na Shirika la DAWASCO ilikuwa inakusanya kiasi cha Tsh Bil 3.2 kwa mwezi ila kwa sasa hali ya upatikanaji maji Jijini imepanda hadi asilimia 85 na kwa mwezi wa Agosti mwaka huu upotevu umefikia asilimia 39 ya kiwango cha Maji yasiyolipiwa," amesema.

 Amesema anawashukuru wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na Miji ya Kibaha na Bagamoyo kwa mwitikio wao kwenye kulipa bili zao kwa wakati na hata wale wenye malimbikizo pia wameweza kupunguza jambo lilifanya kupanda kwa makusanyo kwa mwezi. 

"Kwa sasa  Dawasa inatekeleza miradi zaidi ya 40 kwa pesa za ndani ambapo ni asilimia 35 ya mapato ya kila mwezi, hivyo kupanda kwa makusanyo kutaiwezesha mamlaka hiyo kutekeleza miradi ya maji mingi zaidi itakayowezesha kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji,"

Ameongeza kuwa kwa upande wa huduma kwa wateja imefanikiwa kuboresha namna ya ulipaji wa Ankara. “wateja wetu wamerahisishiwa namna ya ulipaji wa ankara za maji kupitia mtandao, hiyo imewarahisishia wananchi kulipia huduma na  wamekuwa wakikumbushwa mara kwa mara njia za malipo ili kuweza kulipa kwa wakati huduma muhimu ya Maji.

Mpendwa Mteja, tunakushukuru kwa kulipia bili yako ya September kwa wakati, Umeiwezesha DAWASA kukusanya Tshs.11.11 Billion. Ahsante sana, Tunakusihi kuendeelea kulipia Bill zako Kwa wakati. Piga (0800110064)," Taarifa ya Dawasa kwa wateja wake.
Afisa Mtendaji Mku wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa pongezi kwa baadhi ya wafanyakazj waliofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ili kufikia malengo ya kukusanya Bilioni 12 kwa mwezi


RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS LUNGU WA ZAMBIA WAZINDUA KITUO CHA MPAKANI CHA TUNDUMA-NAKONDE ONE-STOP BORDER POST

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Edgar Lungu wa Zambia wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Mpakani cha Tunduma-Nakonde One-Stop Border Post upande wa Tanzania Leo Jumamosi Oktoba 5, 2019
 Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Edgar Lungu wa Zambia wakipeana mikono baada ya kuzindua kwa pamoja wa Kituo cha Mpakani cha Tunduma-Nakonde One-Stop Border Post upande wa Tanzania Leo Jumamosi Oktoba 5, 2019
 Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Edgar Lungu wa Zambia wakiwa na wafadhili wa mradi wakipanda mti kama kumbukumbu baada ya kuzindua Kituo cha Mpakani cha Tunduma-Nakonde One-Stop Border Post upande wa Tanzania Leo Jumamosi Oktoba 5, 2019
 Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Edgar Lungu wa Zambia wakiondoka baada ya kuzindua Kituo cha Mpakani cha Tunduma-Nakonde One-Stop Border Post upande wa Tanzania Leo Jumamosi Oktoba 5, 2019
 Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Edgar Lungu wa Zambia wakikata utepe wakiwa na mawaziri wa nchi Zao kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Mpakani cha Nakonde-Tunduma One-Stop Border Post upande wa Zambia Leo Jumamosi Oktoba 5, 2019
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsihi Mkuu wa Wilaya ya Nakonde Bw. Alex Sinkala kusimama baada ya kumpigia magoti kumshukuru kwa masada wa shilingi milioni tano taslimu ili kusaidia ujenzi wa Shule ya Sekondary ya Nakonde wakati akihutubiua wananchi wa Zambia Katika mkutano wa hadhara baada ya uzinduzi wa Kituo cha Mpakani cha Nakonde-Tunduma One-Stop Border Post upande wa Zambia Leo Jumamosi Oktoba 5, 2019
 Rais Dkt John Pombe Magufulii akihutubiua wananchi wa Zambia Katika mkutano wa hadhara baada ya uzinduzi wa Kituo cha Mpakani cha Nakonde-Tunduma One-Stop Border Post upande wa Zambia Leo Jumamosi Oktoba 5, 2019
  Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Edgar Lungu wa Zambia wakikata utepe wakiwa na mawaziri wa nchi Zao kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Mpakani cha Tunduma-Nakonde One-Stop Border Post upande wa Tanzania Leo Jumamosi Oktoba 5, 2019
 Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Edgar Lungu wa Zambia wakipeana mikono baada ya kukada utepe wakiwa na mawaziri wa nchi Zao kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Mpakani cha Tunduma-Nakonde One-Stop Border Post upande wa Tanzania Leo Jumamosi Oktoba 5, 2019 PICHA NA IKULU

Hospitali kuwajengea vyoo shule ya msingi Mloganzila

$
0
0
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi (aliyesimama) akizungumza katika mahafali ya 14 ya darasa la saba ya Shule ya Msingi Mloganzila yaliyofanyika hii leo. 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mloganzila Geofrey Magembe akielezea jambo katika mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wakiwa na walimu wao katika mahafali yaliyofanyika shuleni hapo.
Zubeda Fadhili(kushoto) pamoja na Innocent Johanes wakisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Mloganzila.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi akiwatunuku vyeti wanafunzi vya kuhitimu elimu ya msingi.
Dkt. Magandi akikata keki maalum iliyoandaliwa na uongozi wa shule kwa ajili ya harambee ya kuchangisha fedha ya ukarabati wa majengo chakavu katika shule hiyo. 



Na Neema Wilson Mwangomo

Hospitali ya Taifa Muhimbili –Mloganzila imedhamiria kujenga vyoo matundu matano katika Shule ya Msingi Mloganzila ikiwa ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na uongozi wa shule hiyo ya kuboresha mazingira ya shule ili wanafunzi wasome katika sehemu safi na salama.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi alipokua akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru katika mahafali ya 14 ya darasa la saba ya Shule ya Msingi Mloganzila.

Dkt. Magandi ameeleza kuwa ujenzi wa vyoo utagharimu shilingi milioni 10 na kwamba utaanza mara moja ambapo vyoo vinne vitakua vya wasichana na kimoja ni kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.

“Tulielezwa kuna hitajika matundu kumi ya vyoo hivyo kama taasisi tukaona ni vema kusapoti suala hili ili kuhakikisha watoto wetu wanasoma katika mazingira safi, pia tumefanikiwa kutafuta mfadhili ambaye amekubali kujenga matundu mengine matano kwa maana hiyo matundu kumi yaliyohitajika yatakua yamekamilika” amefafanua Dkt. Magandi.

Dkt. Magandi ametumia fursa hiyo kuikumbusha jamii kwamba jukumu la maendeleo ya elimu ni la wananchi wote hivyo kila mmoja anapaswa kushiriki kikamilifu.

Pia ametoa wito kwa wazazi katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wanasubiri matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi waendelee kuwalea na kuwalinda watoto ili wasijihusishe katika vitendo viovu ambavyo vitaharibu maisha yao.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mloganzila Mwalimu Geofrey Magembe ameishukuru Muhimbili-Mloganzila kwa msaada wa ujenzi wa vyoo na kueleza kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa vyoo na uchakavu wa majengo.Katika mahafali hayo takribani wanafunzi 100 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2019.

Mahafali ya 41 ya NBAA yafana, Naibu Waziri Dkt. Kijaji atoa neno kwa wahitimu

$
0
0
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa mradi wa kituo cha uhasibu kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam ulibuniwa kwa weledi mkubwa katika kuongeza wigo na fursa za mapato ya ndani sambamba na kuondoa matumizi yasiyo ya lazima ya kukodi majengo kwa ajili ya ofisi, kumbi na madarasa katika kuendesha shughuli zao.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mahafali ya 41 ya Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) yaliyofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam Dkt. Kijaji amesema kuwa utaalamu wa viongozi katika masuala ya fedha uliwasaidia na kutumika kama kichocheo kikubwa cha kubuni mradi huo ambao utawanufaisha watanzania wengi.

Aidha amewapongeza Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi ambao wamekuwa wabunifu katika utendaji kazi na kupambana na changamoto na kuhakikisha sekta hiyo nyeti inaendelea kufanya vizuri zaidi.

Kwa upande mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Prof. Isaya Jairo amesema kuwa Serikali ya awamu tano chini ya Rais Dkt. John Joseph Magufuli kupitia Wizara ya Fedha imeendelea kuwahudumia katika mambo mbalimbali ikiwemo uwezeshaji wa fedha na ushauri.

Amesema kuwa wahitimu wameendelea kuongezeka kutoka mwaka hadi mwaka na hiyo ni kutokana na mafunzo bora yanayotolewa na kituo hicho, na wameweza kutoa viongozi wahasibu katika sekta mbalimbali.

Awali akieleza mafanikio ya kituo hicho Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Pius Maneno amesema kuwa mazingira ya kusomea katika kituo hicho ni faafu na wataendelea kushirikiana na bodi ya wakurugenzi katika kusimamia maadili ya taaluma hiyo kwa kuzingatia sheria.

Vilevile amewataka wahitimu hao kuwa mabalozi bora wa Bodi hiyo pamoja na kuzingatia maadili na mafunzo waliyopewa katika maeneo ya kazi wanakoenda kutumikia.

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akisoma hotuba yake kwa wahitimu kwenye mahafali ya 41 ya Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) yaliyofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Profesa Isaya Jairo  akizungumzia mafanikio pamoja na changamoto zinazowakabili kwa Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati wa mahafali ya 41 ya Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) yaliyofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno akitolea ufafanuzi kuhusu Bodi hiyo inavyofanya kazi zake wakati wa mahafali ya 41 ya Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) yaliyofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wahitimu wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji aliyokuwa akiitoa kwa wahitimu hiyo kwenye mahafali ya 41 ya Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji  akiwapingeza baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya  Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakati wa mahafali ya 41 ya Bodi hiyo yaliyofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji(kulia) akiwatunuku wahitimu wa  Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakati wa mahafali ya Bodi hiyo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Profesa Isaya Jairo.
Wahitimu wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakisoma viapo vyao wakati wa mahafali ya 41 ya Bodi hiyo yaliyofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kulia) akiwasili huku akiwa ameambatana na wenyeji wake wakiongozwa na  Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Profesa Isaya Jairo(kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno(wa pili kushoto) pamoja na Afisa Masoko na Mawasiliano kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Magreth Kageya(kushoto)

WATENDAJI SERIKALINI WATAKIWA KUTENDA HAKI WAKATI WA UJAZAJI WA FOMU ZA OPRAS ZAWATUMISHI ILI KUEPUKA KUSHUSHA ARI YA UTENDAJI KAZI

$
0
0
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Simiyu  (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
 Baadhi ya Watumishi wa Umma kutoka Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mataka (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipotembelea ofisini kwake kabla ya kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Simiyu kilichofanyika katika  Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
 Katibu Msaidizi Ajira na Nidhamu, Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Celina Maongezi akiwasilisha mada, wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma na Watumishi wa Mkoa wa Simiyu  kilichofanyika katika  Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa ufafanuzi wa hoja, wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kushoto), Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma na Watumishi wa Mkoa wa Simiyu  kilichofanyika katika  Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini wakati wa kikao kazi kati yake na Watumishi wa Mkoa wa Simiyu  kilichofanyika katika  Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu. 

TMDA ITAHAKIKISHA DAWA NA VIFAA TIBA VINAVYOPITA MPAKANI NI SALAMA NA VYENYE UBORA-WAZIRI UMMY

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Mh.Ummy Mwalimu ameeleza jana mbele ya Rais Dkt John Pombe Magufuli na Wananchi kwa ujumla kuwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) itahakikisha Dawa na Vifaa Tiba vinavyopitia mpaka wa Tunduma,Tanzania na Nakonde,Zambia ni salama,fanisi na vyenye ubora unaotakiwa.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images