Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO (ECHO PROJECT) KATIKA SEKTA YA AFYA

$
0
0
Mafunzo kwa njia ya mtandao (ECHO Project) katika Sekta ya Afya yametajwa kuwa na manufaa makubwa nchini kwani hivi sasa wataalamu wengi wanafikiwa na kupewa mafunzo mbalimbali kwa mara moja kuliko hapo awali.

Hayo yameelezwa leo Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Uchunguzi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Alex Magesa alipokuwa akifungua mafunzo maalum kwa wataalamu wapatao 110 wa sekta ya afya yaliyolenga kuwajengea uwezo zaidi juu ya mfumo huo.

Amesema kupitia mafunzo hayo Serikali imeweza kuokoa gharama za kusafirisha wataalamu wengi kwenda mafunzo, ambapo kupitia program hiyo sasa hutumia wastani wa Sh bilioni 14 kwa mafunzo ya wataalam wapatao 20 hadi 30 kwa mara moja.

Amesema kwa taratibu walizoweka, wamekuwa na dhima ya kutekeleza agizo la Serikali ambapo Rais, Dk. John Magufuli aliwataka kuhakikisha wanaweza kupunguza gharama za uendeshaji wa mafunzo.

Mratibu wa Mradi wa ECHO, Jacob Lusekelo amesema ulianza rasmi kutumika nchini tangu 2016.
“Tanzania ni nchi ya kwanza kusimika mfumo huo barani afrika ni mzuri kwani unasaidia kupunguza sana matumizi ya gharama ambazo tumekuwa tukizitumia kusafiri sehemu moja hadi nyingine kupashana habari za masuala mbalimbali muhimu kwa tiba,” amesema.

Daktari Abuu Maghimbi kutoka Chuo Kikuu cha Maryland amesema wanashirikiana kwa ukaribu na Serikali katika uendeshaji wa mfumo huo na kwamba hadi kufikia 2020 wanakusudia kuvifikia vituo 200.
 Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Uchunguzi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Alex Magesa (kulia) akisoma hotuba alipokuwa akifungua mafunzo maalum ya (ECHO Project)   kwa wataalamu wapatao 110 wa sekta ya afya yaliyolenga kuwajengea uwezo leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza  Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Uchunguzi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Alex Magesa wakati wa akifungua mafunzo maalum ya (ECHO Project) (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Picha ya pamoja

MWAKA HUU TUMEJIPANGA KUSINDIKA KOROSHO NYINGI ZAIDI - WAZIRI HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Wasindikaji Wakubwa na wadogo wa korosho uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma tarehe 9 Septemba 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Wasindikaji Wakubwa na wadogo wa korosho uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma tarehe 9 Septemba 2019.
Sehemu ya wabanguaji wa korosho wakifatilia mkutano wa waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) wakati wakati akizungumza kwenye mkutano wake na Wasindikaji Wakubwa na wadogo wa korosho uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma tarehe 9 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Wasindikaji Wakubwa na wadogo wa korosho uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma tarehe 9 Septemba 2019.


Na Issa Sabuni, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) amewaambia Wasindikaji wadogo na Wakubwa wa korosho kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe Dtk John Pombe Magufuli ni kuongeza kiwango kikubwa cha usindikaji kuliko ilivyokuwa mwaka jana na kwamba Serikali haitanunua tena korosho bali itaweka mazingira mazuri kwa Wafanyabiashara kununua zao hilo kutoka kwa Wakulima bila ya kuwalalia.

Mhe Hasunga ameyasema hayo katika mkutano wake maaalum alioutisha tarehe 9 Septemba 2019 katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma lengo likiwa ni kuzungumza na Wasindikaji hao ili kujiandaa na msimu mpya wa ununuzi wa korosho ambapo taarifa rasmi ya Wizara itatolewa hivi karibuni.

Waziri Hasunga amesema licha ya Serikali kuendelea na azma yake ya kuongeza thamani ya zao la korosho kwa kuwasisitiza Wabanguaji kuongeza ukubwa wa mazao ya korosho kwa kusindika zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita.

“Tumeona kabla ya kutangaza taarifa rasmi ya Wizara yenye kuzindua rasmi msimu mpya wa ununuzi wa korosho, ni vyema tukutane nanyi Wadau ili kujadiliana namna nzuri ya kuboresha biashara ya korosho kwa lengo la manufaa ya Wakulima wetu” Amekaririwa Waziri Hasunga

Katika hotuba yake; Waziri Hasunga ameelekeza kuwa Wabanguaji hao wanapaswa kutoa Taarifa kwa Wizara kwa msimu wa kilimo wa 2019/2020 katika maeneo kadhaa ikiwemo teknolojia wanazotumia katika ubanguaji na usindikaji wa korosho, uwezo wa mashine zao kusindika kwa mwaka, idadi ya Wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda, uwezo wa viwanda kubangua na kusindika korosho kwa mwezi na kwa mwaka vilevile mapendekezo ya bei ya kununulia kabla ya msimu kuanza.

Waziri Hasunga ameongeza kuwa Wasindikaji pia wanapaswa kuwa wa wazi katika kuishauri Serikali namna nzuri ya kuboresha zoezi zima la ununuzi mpya wa korosho na kueleza changamoto wanazokutana nazo.

Awali katika taarifa yake, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Bwana Francis Alfred amesema uzalishaji wa korosho kwa msimu huu unataraji kufikia tani laki 3 na nusu (350,000) na kuongeza kuwa tija itaongezeka ikiwa sehemu kubwa ya uzalishaji itabanguliwa na kusindikwa hapa hapa nchini. 

WAJUMBE WA CCM GANGILONGA WACHANGIA DAMU NA MISAADA KWA WAGONJWA HOSPITALI YA RUFAA IRINGA.

$
0
0
Diwani wa kata ya Gangilonga leonard Raphael Mgina akiwa katika zoezi la kuchangia damu katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuchangia damu
Diwani wa kata ya Gangilonga leonard Raphael Mgina akiwa na wadau wa chama cha mapinduzi wakienda kuwajulia hali wagonjwa katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na kuwapa zaidi mbalimbali
Diwani wa kata ya Gangilonga leonard Raphael Mgina akiwa kwenye picha ya pamojana wadau wa kata ya Gangilonga manispaa ya Iringa mkoani Iringa.


NA FREDY MGUNDA,IRNGA.

WAJUMBE wa chama cha mapinduzi kata ya Gangilonga wamejitokeza kwa kujitolea kuchangia damu na kutoa msaada kwa wagonjwa wa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa kwa lengo la kuadhimisha Gangilonga ya kijani

Akizungumza na blog hii diwani wa kata hiyo leonard Raphael Mgina alisema kuwa katika kuadhimisha Gangilonga ya kijani kwa kujitolea damu na kuwaona wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ili kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo hapa nchini.

“Tumepita kwenye hodi kumi na tatu kuwaona wagonjwa pamoja kufanya zoezi la kujitolea damu kwa lengo la kusaidia kupunguza upungufu wa damu kwa maana mara kwa mara tumesikia hata kwenye vyombo vya habari kuwa kuna upungufu kwenye benki ya damu” alisema Mgina

Mgina alitoa rai kwa wananchi wengine kuendelea kuchangia damu kwa kuwa hakuna aijua kesho yake hivyoni muhimu kuwa na moyo wa kujitolea kutoa damu ili kupunguza upungufu wa damu uliopo katika benki za damu katika hospitali zetu zote hapa nchini.

Naye katibu wa chama cha mapinduzi kata ya hiyo Likotiko Kenyatta alisemalengo ni kuhakikisha wajumbe na wadau wa chama cha mapinduzi nikurudisha fadhila kwa jamii kama ambavyo wamefanya katika siku ya Gangilonga ya kijani.

“Leo tumekuja kufanya shughuli za kijamii, kugawa misaada pamoja nakutoa damu kwa lengo la lakukihusisha chama cha mapinduzi katika shughuli zote za kijamii na kuifanya kata ya Gangilonga kuonekana ya kijani kweli kweli” alisema Kenyatta

Kwa upande wao baadhi ya wadau wa chama cha mapinduzi wa kata hiyo wamempongeza diwani wa kata hiyo kwa kuendelea kuing’alisha Gangilonga ya kijani.

WAANDISHI WA HABARI NCHINI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZINAZOJIHUSISHA NA TAFITI KUPATA TAARIFA SAHIHI

$
0
0


Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania(TALIRI) kwenye ofisi za Kanda inajumuisha mikoa ya Dar,Pwani Morogoro na Tanga Dkt. Zabron Nziku wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari za sayansi na teknolojia yanayofanyika mjini Tanga.
Afisa Utafiti Mkuu kiongozi kutoka Tume ya Sayansi na teknolojia Dkt Bakari Msangi akitoa mada kwenye mafanzo hayo kuhusu umuhimu wa utafiti nchini Tanzania pamoja na umuhimu wa kusambaza matokeo ya utafiti.
Afisa Utafiti Mkuu kiongozi kutoka Tume ya Sayansi na teknolojia Dkt Bakari Msangi akitoa mada kwenye mafanzo hayo kuhusu umuhimu wa utafiti nchini Tanzania pamoja na umuhimu wa kusambaza matokeo ya utafiti.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mtanzania Mkoani Tanga Amina Omari akieleza namna mafunzo hayo yatakayoweza kuwasaidia 
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo hayo
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo hayo
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo katikati ni Mwandishi wa Gazeti la Citizen Mkoa wa Tanga Pascal Mbunga


WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kushirikiana na taasisi zinazojuhusisha na tafiti mbalimbali ili waweze kupata taarifa sahihi kwa kutumia takwimu ili kuweza kuwahabirisha watumiaji wa mwisho.

Hayo yalisemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa Mifugo Tanzania kwenye ofisi za Kanda inajumuisha mikoa ya Dar,Pwani Morogoro na Tanga Dkt Zabron Nziku wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari za sayansi na teknolojia yanayofanyika mjini Tanga.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) kwa ufadhili wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden (SIDA) yanayoendelea kwenye ukumbi wa Veta Jijini Tanga.

Dkt Zabron ambaye pia ni Mtaifiti wa mambo Mifugo lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuona namna waandishi wa habari kuwajengea uwezo kuweza kushirikiana kati yao na watafiti huku wakitegemea watu kwa kutumia teknolojia sahihi zilizotokana na tafiti wanaweza kupiga hatua kubwa na nchi kupata maendeleo. 

Alisema kwamba mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwani mara nyingi waandishi wamekuwa wakiripoti hasa kwenye tasnia nyengine mapenzi na siasa

“Kwa sababu Tanzania inaelekea kwenye uchumi wa viwanda hauwezi kuja bila kuwepo tafiti mbalimbali kwenye Nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo,mifigo,ardhi na maeneo mengine hivyo niipongeze Costec kwa kuja na mpango huo “Alisema

Alieleza kwani waandishi wa habari wamekuwa ni kiungo muhimu kati ya watu na wadau mbalimbali kuweza kupata taarifa sahihi za kuripoti kuhusiana na mambo ya utafiti.“Lakini pia nitoe wito kwa waandishi wa mikoa ambayo imeshiriki mafunzo hayo wayatumie kwa umakini waelewe kwa namna gani wanaweza kuwa na uwezo wa kuripoti taarifa sahihi zinazotokana na mambo ya utafiti”Alisema

Alisema kwamba watafiti wakitafiti na kupata matokeo mbalimbali yanaweza kuwa hayana tija kwa sababu yanatumia fedha kama hawajaweza kuwafikia walengwa na wadau mbalimbali wa hizo tafiti.

“Kwa mfano kwenye eneo ambalo ninafanyia kazi tukiweza kutafiti namna bora au mifugo bora inayoweza kutoa maziwa kwenye ukanda wa pwani huyo mnyama watabaki naye na taarifa zitabaki kituoni lakini kwa kuwatumia waandishi wa habari wanaweza kuzichukua taarifa sahihi zilizofanyiwa utafiti kuweza kuubarisha umma wa watanzania hivyo wanaweza kupata teknolojia sahii inayohusiana na mifugo”Alisema 

Awali akizungumza wakati akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo ya Umuhimu wa Utafiti nchini Tanzania pamoja na umuhimu wa kusambaza matokeo ya utafiti,Afisa Utafiti Mkuu kiongozi kutoka Tume ya Sayansi na teknolojia Dkt Bakari Msangi alisema kwamba ni taalumu muhimu kwenye nchi ambayo inawawezesha kutoa maalumu na wazalishaji kuongeza uzalishaji.

Alisema namna pekee yake ya kutoa maamuzi ambayo yanatija ni baada ya kuwa na taarifa za kitafiti ambazo zina ushahidi ili zitakuongoza kwenye kufanya maamuzi na kuyatumia kwenye kuendeleza Taifa.

Dkt Bakari alisema utafiti ni shughuli ambayo ina mambo mengi ya uwekezaji kwa sababu unatumia fedha nyingi kuwasomesha watafiti na kuandaa maeneo ya utafiti na kufanya utafiti kwa kutumia gharama hivyo ni muhimu kuhakikisha kila ulichokipata kinatumika kuendelea ,kuongeza uzalishaji na tija kwa Taifa.

Mafunzo hayo yanajumuisha waandisi kutoka mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Morogoro na Pwani

OSHA WASHAURIWA KUONGEZA JITIHADA KUSIMAMIA VIWANGO VYA USALAMA NA AFYA SEHEMU ZA KAZI

$
0
0
    Na.Khadija seif, Michuzi tv

WAKALA wa usalama na afya Mahali pa kazi(OSHA)wameshauriwa kuongeza jitihada katika kusimamia viwango vya usalama na afya sehemu za kazi ili kuwezesha utekelezaji wa sera ya serikali ya uchumi wa viwanda kuwa na tija zaidi.

Akizungumza katika kikao kazi hicho,Katibu wa jukwaa la wahariri (TEF) ,Nevelle Meena amesema  wakala wa usalama na afya Mahali pa kazi (OSHA)  ina wajibu mkubwa katika kulinda Afya za wafanyakazi katika sekta ya umma,sekta binafsi pamoja na sekta isiyo rasmi, hivyo ni muhimu kwa taasisi hiyo kuhakikisha kwamba jamii ina uelewa wa kutosha kuhusu usalama wao wawapo kazini.

"Kikao hichi kimekua ni cha muhimu sana kwani wahariri au waandishi wa habari ni watu ambao wanakaa katika taasisi fulani iwe ya binafsi au ya umma au kati ya serikali na wananchi kwa ujumla hivyo wakala wa usalama na afya Mahali pa kazi (OSHA)    wameona kwamba wahariri wanaweza kuelimisha watanzania kuhusu kazi wanazozifanya, manufaa ya kazi wanazozifanya pamoja na faida ya wale wahusika kutekeleza matakwa, sheria ya usalama kazini,"

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala wa usalama na afya Mahali pa kazi (OSHA) Khadija Mwenda ameeleza lengo la kikao hicho ilikua ni kubadilishana uzoefu na kuwafahamisha wahariri kuhusu namna ambavyo  (OSHA) inatekeleza majukumu yake ili kufanikisha suala zima la kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kuzingatia masuala ya usalama na afya sehemu za kazi.

"Changamoto kubwa inayotukabili kwa sasa ni uelewa mdogo kuhusu masuala ya usalama na afya miongoni mwa wadau na kwakutambua mchango mkubwa wa tasnia ya habari katika kuelimisha umma ndio sababu tumewashirikisha ili wao Kwanza wapate elimu ya namna gani sisi tunatekeleza majukumu yetu katika kusimamia nguvu kazi ya taifa na vile vile waweze kujua wanaporipoti masuala ya  (OSHA) basi wanaripoti katika mstakabali gani,"

Naibu Mtendaji Mkuu wa gazeti la jamhuri Manyerere Jackson amesema vikao vya namna hiyo vitasaidia sana kwa sababu wahariri sio malaika hawajui kila jambo na Kama wahabarishaji wakuu wa wananchi ni sharti la kwanza wao kuyafahamu mambo kiundani ili zile taarifa zinazofikiswa kwa jamii ziwe za uhakika.

"Wakala wa usalama na afya Mahali pa kazi (OSHA) ni taasisi kubwa yenye umuhimu wa kipekee katika uhai wa wafanyakazi nchini katika maslahi ya uchumi,"
      Kaimu Mtendaji mkuu wa OSHA Bi. Khadija Mwenda akiongea na wahariri mbalimbali toka Vyombo vya habari nchini

BUNGE LA RIDHIA MKATABA WA MINAMATA KUHUSU ZEBAKI “MINAMATA CONVENTION ON MERCURY”

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akiwasilisha azimio la kuridhia Mkataba wa Minamata kuhusu zebaki mbele ya Bunge hii leo mjini Dodoma. Bunge limeridhia Mkataba wa Minamata kuhusu zebaki na Serikali imeandaa Mpango kazi wa Taifa wa kupunguza matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo ambao umeainisha fursa mbalimbali.


Na Lulu Mussa,Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene amesema inakadiriwa kuwa asilimia 25 hadi 33 ya wachimbaji wadogo wa dhahabu hapa nchini, wameathiriwa na Zebaki kwa kupata magonjwa yakiwemo yale ya mifumo ya neva za fahamu, uzazi, upumuaji, figo, moyo, na udhaifu wa mwili. 

Akiwasilisha azimio la Bunge la kuridhia Mkataba wa Minamata kuhusu zebaki Simbachawene amesema, baadhi ya athari kwa mazingira zilizobainika kutokana na matumizi ya zebaki ni pamoja na kudhoofika kwa ukuaji wa viumbe hai wanaoishi ndani ya maji; uchafuzi wa mfumo mfuatano wa mazao ya chakula, mifugo na samaki; na uchafuzi wa vyanzo vya maji, hewa na udongo. 

“Lengo kuu la Mkataba huu ni kulinda afya ya binadamu na mazingira dhidi ya athari za uchafuzi wa mazingira unaotokana na matumizi ya Zebaki katika hatua za uzalishaji, matumizi na utupaji wake” Simbachawene alisisitiza.

Simbachawene ameainisha sheria ambazo zinatoa mwongozo wa jumla kuhusu usimamizi wa Zebaki ikiwa ni pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (2004); Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Kemikali za Viwandani na Majumbani (2003); Sheria ya Madini (2010); Sheria ya Afya ya Jamii (2009); Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (2003); na Sheria ya Chakula na Dawa (2003) na kusisitiza kuwa zitaandaliwa kanuni za Usimamizi wa Zebaki chini ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (2004) ili kuwezesha utekelezaji wa Mkataba huu.

Tafiti zinaonyesha kuwa zebaki hudumu katika mazingira kwa muda mrefu (miaka 2 hadi 20) na husafiri masafa marefu kwa njia ya hewa, maji (mito, maziwa na bahari) na udongo umbali hadi kilomita 1,000 kutoka kwenye chanzo; na kuathiri afya ya binadamu, viumbe wengine na mazingira. Athari hizi zinajitokeza zaidi katika nchi zinazoendelea ukilinganisha na nchi zilizoendelea kutokana na nchi hizo kupunguza matumizi ya Zebaki. 

Awali akiwasilisha hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Suleiman Ahmed Sadiq amesema Kamati ianona umuhimu wa nchi kuridhia Mkataba huu kwa lengo la kushirikiana na nchi nyingine kutafuta suluhisho la zebaki bila kuathiri shughuli za wachimbaji wadogo.

“Ushauri wa Kamati ni kuwa Serikali ijitahidi kuhakikisha inapatikana teknolojia rahisi na rafiki kwa wachimbaji wadogo kwa gharama nafuu” alisisitiza Mhe. Sadiq.

Zebaki ni miongoni mwa kemikali zinazohatarisha zaidi afya ya jamii duniani kutokana na kudumu katika mazingira kwa muda mrefu, kusafiri masafa marefu kwa njia ya hewa, maji (mito, maziwa na bahari) na udongo na hivyo kuathiri afya ya binadamu na mazingira. Jumla ya nchi 113 zimeridhia Mkataba huu ambao ulianza kutekelezwa rasmi tarehe 16 Agosti, 2017 mara baada ya Nchi 50 kuridhia kama inavyotakiwa na Ibara ya 30 ya Mkataba wa Minamata.

DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA SPIKA WA BUNGE JIMBO LA SHANGHAI NCHINI CHINA

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimkaribisha Spika wa Bunge la Jimbo la Shanghai nchini China Bi. Yin Yicui.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimkaribisha akieleza jambo katika mazungumzo na Spika wa Bunge la Jimbo la Shanghai nchini China Bi. Yin Yicui yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson akipokea zawadi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jimbo la Shanghai nchini China Bi. Yin Yicui baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson na Spika wa Bunge la Jimbo la Shanghai nchini China Bi. Yin Yicui wakiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wabunge kutoka Jimbo la Shanghai China.

………………

Na. Dianarose Shirima- Maelezo

Spika wa bunge la Shengai Yin Yicui,yuko nchini na wajumbe kumi na mbili wa bunge hilo ambapo jiji Dar es Salaam wamekutana na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Akson Mwansasu kwa lengo la kubadilishana uzoefu mbalimbali kwa pande zote mbili. Spika Yin Yicui na wenzake wamefurahishwa na mapokezi na kusema kuwa baada ya kupokea mwaliko kutoka kwa Spika wa Tanzania wakati alipotembelea Shengai, walifurahia kupata mwaliko huo na kuahidi kuja Tanzania.

Spika huyo aliongeza kuwa Tanzania pamoja na jimbo hilo la Shengai limekuwa na uhusiano mzuri toka huko nyuma na kulenga kuendeleza maslahi mapana ya maendeleo ya Tanzania pamoja na jimbo hilo la Shengai.

Katika mazungumzo yao wamejikita zaidi kuona jinsi wanavyoweza kushirikiana katika sekta ya elimu,mazingira na utunzaji wa maliasili na wanyamapori, ambapo watashirikiana katika hatua za utekelezaji.

Kwa upande wa mazingira, Bunge la Shengai linaangalia namna linavyoweza kusaidia uboreshaji wa mazingira, ambapowalipongeza serikali ya Tanzania kwa kupitisha sheria ya kupiga marufuku utumiaji wa mifuko ya plastiki na kuongeza kuwa, nchini kwao jimbo la Shengai wanajiandaa kupitisha sheria ambayo inahitaji utenganishi wa aina za takataka za majumbani. kwamba takataka za nyanya zisichanganywe na makopo. Dkt. Tulia aliongezea kuwa Tanzania inaangalia namna itakavyoitumia hiyo sheria ili kujifunza.

Naibu Spika aliwashukuru jinsi China wanavyoisaidia Tanzania kwa upande wa ufadhili wa masomo ya nje wanafunzi wanaotoka Tanzania, ambapo alisema ufadhili wao ni tofauti na ufadhili wa nchi nyingine, kwamba China huomba wanafunzi kwenda kusoma China wakati mataifa mengine wanafunzi huomba moja kwa moja katika nchi wanazopenda kusoma, pia katika vyuo vya VETA wataangalia ni kwa namna gani wanaweza kushirikiana na Tanzania ikiwemo kusaidia vifaa vya kufundishia kama vile kompyuta

Mwisho walizungumzia namna ya Tanzania kutunza raslimali zilizopo nchini ambapo ni pamoja na wanyamapori na uoto wa asili, na kuahidi kuwa bega kwa bega na Tanzania ili kukuza na kuendeleza rasilimali za nchi.

MAMA TARISHI ASTAAFU UKATIBU MKUU, ASHAURI UTUMISHI WA UMMA WA KIBIASHARA

$
0
0
Aliyekuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Bi. Maimuna Tarishi, akimkabidhi taarifa ya makabidhiano ya Ofisi hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko, tarehe, 9 Septemba, 2019, Jijini Dodoma.
Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Bi. Maimuna Tarishi, akiongea na watumishi wa Ofisi hiyo wakati akiwaaga rasmi baada ya kustaafu kwa mujibu wa sheria, tarehe, 9 Septemba, 2019, Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko akisisitiza jinsi Ofisi hiyo itakavyoendelea kutekeleza ushauri na nasaha zake kwa vitendo wakati wa mkutano na watumishi wa ofisi hiyo wa kumuaga rasm, aliyekuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Bi. Maimuna Tarishi, tarehe, 9 Septemba, 2019, Jijini Dodoma.

Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Bi. Maimuna Tarishi,(hayupo pichani) wakati alipokutana na watumishi hao kuwaaga rasmi baada ya kustaafu kwa mujibu wa sheria, tarehe, 9 Septemba, 2019, Jijini Dodoma.
Aliyekuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Bi. Maimuna Tarishi, (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko, (kulia) wakifuatilia shughuli za ujenzi zinazoratibiwa na Ofisi hiyo, wakati wa kumkabidhi miradi ya Ujenzi aliyokuwa anairatibu, tarehe, 9 Septemba, 2019, Jijini Dodoma.


Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Bi. Maimuna Tarishi, ambaye amehudumu katika ofisi hiyo tangu, tarehe 4 Aprili, 2017, amestaafu rasmi utumishi wa umma, huku akiwashauri watumishi wa umma wanaobaki katika utumishi huo kutekeleza majukumu ya utumishi wa umma kibiashara.

“Ninapozungumzia Utumishi wa Umma wa kibiashara siimanishi kuuza na kununua bidhaa fulani, kimsingi ninachokusudia hapa ni kuwa watumishi wa umma wanaobaki katika utumishi huo nawashauri utendaji wao wa majukumu uwe unajikita katika kuwezesha na sekta nyingine zinastawi ili kupata matokeo chanya yaliyokusudiwa kwa watanzania wanao wahudumia” amesema Tarishi

Bi.Tarishi amefafanua kuwa katika kuhakikisha kuwa utumishi wa umma wa kibiashara unatekelezwa lazima watumishi wa umma watekeleze majukumu yao kwa wakati na kasi inayotakiwa, kutumia weledi na ubunifu pamoja na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu pia kuhakikisha viwango bora vya huduma na lazima matokeo chanya yanapatikane kwa huduma wanazo zitoa kwa wananchi.

Akiongea wakati akiwaaga rasmi, watumishi wa Ofisi hiyo, tarehe 9 Septemba 2019, jijini Dodoma, Bi.Tarishi alieleza kuwa utumishi wa umma ndiyo injini ya kufanyika kwa shughuli zote katika nchi yoyote duniani. Ameeleza kuwa bila utumishi wa umma sekta nyingine zikiwemo sekta binafsi haziwezi kustawi, hivyo utumishi wa umma ukitekelezwa kibiashara huduma zinazotolewa na serikali zitawafikie wananchi wanao wahudumia na zitakuwa na matokea chanya.

Katika hatua nyingine, Bi Tarishi amemshukuru Rais wa Jamhuri yas Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kulitumikia Taifa kwa nafasi ya Katibu Mkuu, Aidha, amemshukuru Mhe. Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, kwa miongozo na maelekezo yaliyomsaidia kutekeleza majukumu yake. Bi Tarishi hakusita kushukuru ushirikiano mzuri aliopata kutoka kwa Mawaziri wa Nchi wa Ofisi hiyo, Mhe. Jenista Mhagama na Mhe. Angellah Kairuki pamoja na Katibu Mkuu anayeendelea kuhudumu kwenye ofisi hiyo, Bi. Dorothy Mwaluko, pia na watumishi wa ofisi hiyo.

Akiongea katika mkutano huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko alifafanua kuwa watumishi wa Ofisi hiyo hawana budi kuwa wabunifu, watiifu na waaminifu na kutumia weledi katika kutekeleza majukumu yao ili kuweza kuhakikisha aliyoyasisitiza Katibu Mkuu mstaafu yanakuwa katika vitendo.

Katibu Mkuu Mstaafu, Bi Maimuna Tarishi aliaza rasmi utumishi wake wa umma tarehe 6 Mei, 1985 na amestaafu utumishi huo tarehe, 7 Septemba, 2017. Awali kabla ya kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu amewahi pia kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Elimu Sayansi na teknolojia kabla ya kuhamia Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) alipostaafia.

CAG MSTAAFU AMTEMBELEA SPIKA NDUGAI

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu Bw. Ludovic Utoh alipomtembelea Ofisi kwake Jijini Dodoma mapema leo.

IGP SIRRO AFANYA ZIARA YA KIKAZI KISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akipita kukagua mradi wa ujenziwa nyumba za askari Polisi zilizopo katika eneo la Fuoni wakati alipofanya ziaraya kikazi ya siku moja leo Kisiwani Zanzibar na kuzungumza na maofisa na askari wa vyeo mbalimbali. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima
wakati alipowasili visiwani Zanzibar leo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja kwalengo la kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za askari pamoja na
kuzungumza na maofisa na askari wa vyeo mbalimbali. Picha na Jeshi la Polisi.

Rais Magufuli amjulia hali Baba Askofu Yuda Ruwaichi aliyelazwa MOI Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) wakimuombea Sala Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika Taasisi hiyo ya MOI mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa Kichwa jana usiku.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Madaktari wa Muhimbili pamoja na MOI mara baada ya kumjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo ya MOI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa MOI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Polisi cha Selander Bridge wakati akitokea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ametembelea Kituo cha Polisi cha Selander Bridge wakati akitokea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka mara baada ya kutembelea kituo hicho. PICHA NA IKULU



RC Wangabo avitaka vyama vya Ushirika kujiepusha na madeni

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amevitaka vyama vya msingi vya ushirika mkoani Rukwa kuhakikisha wanalipa madeni wanayodaiwa na wadau wa kilimo ikiwemo mabenki pamoja na wauzaji mbalimbali wa pembejeo ili wadau hao waweze kuendeleza uaminifu na hatimae kuwa na mahusiano mazuri yatakayoleta maendeleo ya wananchi katika mkoa.

Amesema kuwa kutolipa madeni chama kinajiweka katika mazingira ya kutokopesheka na wadau kukosa uaminifu hata kwa vyama vingine na kunasababisha wadau hao kushindwa kufikisha huduma kwa wakulima na hatimae kilimo kukosa tija, vyama vya ushirika kuyumba na kuongeza kuwa dawa pekee ya kukopa ni kulipa.

“ Vyama vya Msingi vina madeni tena madeni makubwa, kwa mfanokuna kile chama cha Katazi AMCOS pamoja na Rukwa Farmers vyote vipo kule Wilaya ya Kalambo vinadaiwa shilingi milioni 395, vyama viwili sijajua kwengine lakini pale Mpui wanadaiwa Shilingi Milioni 485 au 490, lakini wao wamejipanga nilikuta mzigo mkubwa sana wa mahindi, tani zaidi ya 600, na waliniambia deni wanamaliza, lakini vile vyama viwili hata mahindi yaliyoko kwenye maghala yalikuwa hayazidi magunia 250 sasa watalipaje deni, ukiuliza wanasema kwamba hawakupata mavuno ya kutosha, lakini nje ya hapo wanauza” Alieleza.

Hivyo alitoa rai kwa vyama vya ushirika kuliangalia jambo hilo kwa karibu kwa kuchambua vyama vyote vinavyodaiwa, wadau wanaowadai, siku waliyokopa na siku wanayotakiwa kurudisha mikopo, aina ya mikopo, walichorejesha tangu kukopa ili kuwa na orodha kamili na kuwafuatilia katika urejeshaji wa mikopo hiyo kwani kwa kufanya hivyo watajenga Imani kwa wanaowakopesha na hatimae kukopesha zaidi.

Mh. Wangabo aliyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ufipa Cooperative Union Ltd (UCU) katika mkutano uliowajumuisha wadau wa kilimo katika mkoa ili kuona namna ya kuinua kilimo chenye tija pamoja na kuhuisha ushirika ndani ya mkoa.

Aidha, Wakati akiwasilisha mada yake kwa wakulima Meneja wa Benki ya Manedeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Kanda ya Nyanda za juu Kusini Dickson Pangamawe alisema kuwa viongozi wa shirika ndio nguzo ya wanaushirika, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha kuwa wanachama wanafaidika na ushirika huo na kuhakikisha kuwa mikopo wanayoipata inawafikia wakulima wao.

“ Nyinyi ndio mtakaotujengea uamini kule kwa wakulima, sisi kama benki ya kilimo tuna fursa ya mikopo ya aina zote, kama wakulima wapo ‘serious’ na uongozi wao utasimama imara, tutawakopesha wataweza kufanya shughuli zao za kilimo bila ya shida yoyote, kwahiyo nitoe rai kwa viongozi wa ushirika, mara nyingi kumekuwa na shida na wakulima wanashindwa kuwa waaminifu kwasababu wanashindwa kusimamiana vyema katika vyama vyao, kwahiyo nyie muwe imara ili kuturuhusu sisi tuweze kuwawezesha,” Alisisitiza.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Sumbawanga Abdillahi Nyangasa alishauri kuwa ili wakulima waweze kujikomboa alitaja mambo matatu makubwa ikiwemo Fedha, Masoko na Mkulima mwenyewe na kuongeza kuwa wao kama NFRA wanasimama katika kumhakikishia mkulima masoko na hivyo wakulima wanahitaji fedha za mikopo kutoka katika mabenki na wao kuwa tayari kutumia fedha hizo kwaajili ya manufaa ya kilimo chao.

“Mtazamo wa NFRA ni kuwafanya Wana Rukwa na Watanzania wengine tubadilike tuwe na uwezo wa kuuza bidhaa zetu za mazao ndani na nje ya nchi, bahati nzuri mkoa umeshaweza kulichukua hili na kulifanyia mkakati kwa maana ya ndugu zetu maafisa ugani, kazi ianzie shambani, tuna kiwango kikubwa sana tunachokipoteza cha mahindi tunayolima kwa hatua ya mwisho ya ubora, asilimia 30 mpaka 40 wakati mwingine mazao yanaharibika kwasababu ya kutozingatia kilimo chenye tija,” Alisitiza. 

Mkoa wa Rukwa una matrekta 124 yanayomilikiwa na wakulima binafsi hali iliyopelekea Mh. Wangabo kuvitaka vyama vya ushirika kusimamia kauli mbiu yao ya “ Ushirika, Pamoja tujenge uchumi” kwa kuanza na kumiliki matrekta ili kuwawezesha wanachama wao waweze kulima kwa tija na kuongeza mazao na sio kutegemea kilimo cha majembe au kutumia wanyama.

NABII NA MTUME MWINGIRA AMTEMBELEA SPIKA WA BUNGE

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Nabii na Mtume Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha Ofisi kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisali na Nabii na Mtume Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha pamoja na ujumbe aliombatana nao walipomtembelea Ofisi kwake. Wengine katika picha ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Efatha Dodoma Bi. Frida Nyiti, Mwenyekiti wa Kamati ya Ibada-Bunge Chapel Mhe. Anna Lupembe (Mb), Mzee wa Kanisa la Efatha Winifrida Rutaindurwa na Msaidizi wa Mchungaji Mwingira Bw. Davis Ngowi.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiagana Nabii na Mtume Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha mara baada ya kuzungumza naye Ofisi kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai katika picha ya pamoja na Nabii na Mtume Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha mara baada ya kuzungumza naye Ofisi kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Nabii na Mtume Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha pamoja na ujumbe aliombatana nao. Kushoto kwa Mchungaji Mwingira ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Efatha Dodoma Bi. Frida Nyiti na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ibada-Bunge Chapel Mhe. Anna Lupembe (Mb).PICHA NA BUNGE

WANANCHI HALMASHAURI YA KIGOMA KUNUFAIKA NA UJENZI WA MADARAJA YA MAWE KWA UFADHILI WA UBELGIJI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Pendo E. Mangaliakiwa na wataalam kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA),wakati wa Ukaguzi wa daraja la Rubumba lililopo Kijiji cha Nyarubanda Kata yaNyarubanda.
Wananchi wa Kijiji cha Nyabigufa Kata ya Mkongoro katika Halmashauri ya
Wilaya ya Kigoma wakiwa wanaendelea na ujenzi wa Daraja la Nyabigufa lililopoMto Kaseke, Kata ya Mkongoro.
Daraja la Nyabigufa linaloendelea kujengwa na Wakala wa Barabara za Vijijinina Mijini (TARURA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma,Serikali ya Ubelgiji chini ya Mradi wa Sakirp – Enabel pamoja na wananchilililopo katika mto Kaseke, Kijiji cha Nyabigufa Kata ya Mkongoro.
Daraja la Nyabigufa linaloendelea kujengwa na Wakala wa Barabara za Vijijinina Mijini (TARURA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma,Serikali ya Ubelgiji chini ya Mradi wa Sakirp – Enabel pamoja na wananchilililopo katika mto Kaseke, Kijiji cha Nyabigufa Kata ya Mkongoro.

*****************************

Geofrey A.Kazaula na Bebi Kapenya – Kigoma

Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wanatarajia kunufaika na Ujenzi wa Madaraja ya mawe unaofadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji chini ya mradi wa Kilimo endelevu katika Mkoa wa Kigoma (Sakirp – Enabel) na kusimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kigoma Bi. Pendo E. Mangali ameeleza kuwa mradi huo uliibuliwa na wananchi baada ya kueleza changamoto wanayokutana nayo katika kusafirisha mazao yao kutoka mashambani hadi majumbani na kwenye masoko.

Kiongozi huyo amebainisha kuwa mradi huo wa Ujenzi wa madaraja ya mawe unalenga kutatua kero ya usafiri na usafirishaji wa mazao na kwamba wananchi walihamasishwa na wakakubali kujitokeza katika kusomba mawe na kushiriki kujenga madaraja hayo.

“Nitumie fursa hii kuwapongeza sana wananchi wa Halmashauri ya Kigoma kwani wanafanya kazi sana, baada ya kugundua kuwa wanashindwa kusafirisha mazao yao kutoka mashambani hadi sokoni kwa pamoja tuliamua kuanza ujenzi wa madaraja ya mawe”, amesema kiongozi huyo.

Kiongozi huyo amebainisha kuwa baada ya kukamilika kwa madaraja hayo kazi itakayokuwa imebaki ni Kufungua barabara za kuunganisha mashamba na hatimaye kuwezesha wananchi kufikisha mazao yao sokoni kwa urahisi na kukuza kipato chao.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mhandisi Pharles E. Ngeleja ameeleza kuwa Ujenzi wa madaraja kwa teknolojia ya kutumia mawe ni wa gharama nafuu na kwamba una washirikisha wananchi moja kwa moja kwa kukusanya vifaa vinavyopatikana katika mazingira yao hususani mawe na wafadhili wanatoa vifaa vya viwandani visivyopatikana kwenye mazingira mfano simenti huku TARURA wakisimamia shughuli za ujenzi .

Akiongea kwa niaba ya wananchi wanaoshiriki katika ujenzi wa madaraja hayo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyabigufa Ndg. Johnphace Kabora Tunzwe amesema kuwa changamoto ya usafiri ni kubwa hasa kipindi cha masika na hivyo tayari wameamua kujitolea kwa kukusanya mawe ili kujenga madaraja .

“Kwanza nawashukuru TARURA, Sakirp Enabel na Halmashauri ya Kigoma kwani mwanzo tulidhani kuwa kazi hii ni ngumu sana na haiwezekani lakini sasa kama mnavyoona tayari tumeanza kukamilisha ujenzi wa daraja” amesema Kiongozi huyo.

Aidha ameongeza kuwa baada ya kukamilisha ujenzi wa daraja, kazi itakayokuwa imebaki ni Kufungua barabara za kufika mashambani ili kuwasaidia wananchi kusafirisha mazao yao na kwamba anaimani kuwa Serikali kupitia TARURA watafungua barabara .

Naye Meneja mshauri wa mradi huo chini ya Serikali ya Ubelgiji Ndg. Steven Hollevoet ameeleza kuwa Teknolojia ya ujenzi wa madaraja ya mawe ni ya muda mrefu hasa katika nchi za Ulaya na Asia na sasa wameileta Tanzania ili kuwafundisha wananchi kujenga madaraja kwa gharama nafuu kwasababu vifaa vinavyotakiwa kama mawe na mchanga vinapatikana kwa urahisi.

Hadi sasa madaraja sita yamekamilika na madaraja tisa yapo katika hatua mbalimbali huku lengo likiwa ni kukamilisha madaraja kumi na tano ifikapo mwezi Desemba, 2019.

CCM Z'BAR YASEMA SERA ZAKE ZIPO RAFIKI KULINDA HAKI ZA WATOTO.

$
0
0
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao,akiwa amembeba Mtoto Hajra Abdillahi Abdalla aliyetupwa na Mama yake Kichakani baada ya kuzaliwa na akaokotwa na Mbwa hivi sasa analelewa na Serikali katika Nyumba ya kulelea Watoto Mazizini.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao(kulia),akimkabidhi zawadi Mdhamini wa Nyumba ya kulelea Watoto ya Mazizini Bi.Chumu Ali Abeid katika ziara hiyo ya Katibu Mwenezi.
BAADHI ya Watoto wanaolelewa katika Nyumba ya kulelea Watoto ya Mazizini Zanzibar baada ya kutembelewa na KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao.

…………….

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao, amesema CCM inasimamia vyema Ilani yake kwa kuhakikisha kundi la Watoto wanapata haki zao za msingi zikiwemo kupatiwa Malezi bora,Huduma bora za Afya,Elimu na kulindwa.

Kauli hiyo ameitoa katika ziara yake ya kumtembelea Mtoto Hajra Abdillahi Abdalla, aliyeokotwa na Mbwa baada ya Mama yake kumzaa na kumtupa kichakani huko Pemba miezi kadhaa iliyopita kwa sasa analelewa katika Kituo cha kulelea Watoto cha Mazizini Unguja.

Alisema CCM imeweka Sera bora na rafiki za kulinda maisha ya watoto ili wapate huduma muhimu zinazowawezesha Watoto kupata mazingira bora ya Kimalezi.

Akizungumzia Tukio la kutupwa kwa Mtoto Hajra alisema vitendo vya aina hiyo vinatakiwa kupingwa vikali na jamii na yeyote atakayebainika achukuliwe hatua kali za klisheria kwani Mtoto anakuwa hana kosa lolote la kupelekea kutupwa.

Alisema Mtoto huyo aliyetupwa na Mama yake vichakani mara tu baada ya kuzaliwa kisha akaokotwa na Mbwa na kumpeleka sehemu salama za Watu ni kitendo cha kumshukru Mwenyezi Mungu.

Aliishukru Serikali kwa kuchukua hatua za haraka za kulinda Maisha ya Mtoto huyo sambamba na kumpatia huduma bora za kimalezi kama walivyo Watoto wengine katika Jamii.

Katibu huyo aliwataka Walezi wa Watoto hao katika Nyumba hiyo,kuhakikisha wanawalea katika misingi Bora ya Kimaisha hasa ya Kidini na kuwajengea mazingira ya kupenda kusoma ili watakapoanza kujitegemea wawe na uwezo wa kujimudu kimaisha.

Amewasihi Watoto hao kujilinda dhidi ya Vitendo vya udhalilishwaji kwani kuna baadhi ya Watu wanatumia mbinu mbali mbali za kuwaadaa watoto kwa nia ya kuwadhalilisha.Alitoa wito kwa Serikali kuendelea kuthibiti Vitendo vya Udhalilishaji kwani vinaharibu Maisha ya Watoto ambao ndio Viongozi na Wataalamu wa Taifa wa baadae.

Naye Mdhamini wa Nyumba ya kulelea Watoto Mazizini Bi.Chumu Ali Abeid, aliwapongeza Viongozi hao kwa kutembelea Watoto wanaolelewa katika Nyumba hiyo.Alisema kuwa hali ya Mtoto Hajra inaendelea Vizuri na kwa sasa anapewa huduma bora kwa uangalizi mkubwa hali inayochangia Afya yake kuimarika kila siku.

“Tunawalea Watoto wa aina mbali mbali na Afya zao zipo vizuri kutokana na Malezi Bora wanayopatiwa wakati wote”,alisema Mdhamini huyo Bi.Chumu.
Katibu huyo alifuatana na Viongozi mbali mbali Wanawake wa UWT pamoja na Makatibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Zanzibar, walitoa zawadi mbali mbali kwa Watoto wanaolelewa katika Nyumba hiyo.

WANANCHI WILAYA YA KAKONKO WASHAURIWA KUCHAGUA VIONGOZI WATAKAOLETA MAENDELEO

$
0
0

Na Rhoda Ezekiel, Kigoma


WANANCHI wilayani Kakonko mkoani Kigoma wameshauriwa kuacha kwenda kwenye shughuli za Kilimo wakati wa uchaguzi ili kufika katika vituo kuchagua viongozi watakao waletea maendeleo na kuepuka kuchaghuliwa viongozi wanaotafuta uongozi kwa matakwa yao binafsi.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, wakati akiwahamashisha wananchi hao kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu na kuhakikisha kuwa wanachagua viongozi waadilifu, wasiopenda rushwa bali wapenda maendeleo na kuimarisha ulinzi na usalama wa eneo analoliongoza.

Amesema kumekuwa na wananchi wengi Vijijini kutoshiriki katika chaguzi mbalimbali hususani wakati huu msimu wa Kilimo ambapo wananchi wengi wanahamia mashambani; hivyo wananchi wanapaswa kutenga muda wao wa kushiriki katika kuchagua na kuchaguliwa katika uongozi mbalimbali katika uchaguzi huo, na ili shughuli wanazozifanya ziweze kuwaletea maendeleo lazima kupata viongozi wazuri.

Aidha, ameeleza kuna baadhi ya viongozi wa vijiji vilivyoko mpakani wanajihusisha na vitendo rushwa kwa kugawa ardhi kwa wananchi ambao inasadikia siyo raia wa Tanzani na kushiriki kuhifadhi mifugo yao na pia kuwanyanyasa wannanchi.

Yote yametoke kwa kuwa wananchi hawakujipanga kujua ni nani kiongozi atakae waongoza kwa misingi ya uzalendo na uadilifu. 

" Nitoe mwito kwenu Wananchi ni haki ya kila raia kushiriki katika uchaguzi iwe kuchaguliwa au kuchagua; na tutakapo jitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi itatusaidia kupata viongozi watakao tuongoza katika Misingi ya uadilifu na uwajibikaji, ni jukumu letu kuhakikisha uchaguzi huu tunatenda haki, tuhudhurie mikutano ya wagombea na tusikilize sera zao ili kujua ni kiongozi gani anatufaa,'amesema.

Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Masumbuko Magang'hila aliwataka wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ilikuweza kushiriki kikamilifu katika kuchagua viongozi.

Amesema daftari hilo litahusisha wale ambao hawakujiandikisha katika daftari la awali la kupigia kura, waliofikia umri wa kupiga kura, waliopotelewa vitambulisho vyao na waliohama makazi yao ya mwanzo na kuhamia sehemu ambayo hawakujiandikishia.

Alieleza kuwa uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu na watakaoshiriki ni wale waliojiandikisha, na wale ambao wanasifa za kugombea na kuwataka Wananchi wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali na wasiogope.

Kwa upande wake Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Kakonko, Ladisraus Ibrahim msaki Aliwataka Wananchi kutoa taarifa kwa yeyote atakaye kuwa anajihusisha na vitendo vya rushwa kwa ajili ya kupata uongozi ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria na kuepuka kupata viongozi wasiofaa watakao kuwa wapenda rushwa na wasiopenda maendeleo.

Nao baadhi ya Wananchi walikuwa na maoni tofauti juu ya uchaguzi, Joackim Antony ni mkazi wa kijiji cha Kabingo alisema Wanatambua ni haki ya kila mwananchi kushiriki katika uchaguzi na wao kama vijana watahakikisha wanashiriki kikamilifu kuhakikisha wanapata viongozi walio bora.

Amesema changamoto ambayo inayowakatisha tamaa ni pale wao wanapochagua viongozi harafu wanajitokeza baadhi wanawapitisha wagombea wanaowataka wao bila kushinda hivyo wanaiomba serikali kuwa makini katika uchaguzi huu ili kuweza kuondokana na changamoto hizo.

Mwananchi wa kijiji Kabingo Nezia Kasiano amesema atahakikisha wanashiriki katika uchaguzi huo na kwamba hakuna jambo litakalo wazuia kushiriki, endapo watapata viongozi wazuri itawasaidia hata kupanga mipango ya maendeleo katika vijiji vyao
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza na Wananchi hao 

MAHAKAMA INAYOTEMBEA DAR YAENDELEA NA KAZI

$
0
0
Mwananchi, Zubeda Abdallah Kombo akielekezwa na Karani wa Mahakama ya Mwanzo, Kimara,Judith Mwakyalabwe jinsi ya kupata hati ya kiapo.
Karani wa Mahakama ya Mwanzo, Kimara, Judith Mwakyalabwe, akiendelea na utendaji kazi ndani ya Mahakama Inayotembea wakati Mahakama hiyo ikitoa huduma eneo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, iliyopo Kibamba jijini Dar es Salaam.
Gari ya Mahakama Inayotembea likiwa katika eneo ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ubungo, iliyopo Kibamba jijini Dar es Salaam likiendelea kutoa huduma za kimahakama.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo ya Kimara, Mhe. Geiza Mbeyu, akimsikiliza kwa makini mwananchi ambaye alikuwa akiuliza jambo kuhusu Mahakama Inayotembea katika eneo la Stendi ya Kibamba iliyopo jijini Dar es Salaam.Picha na Aziza Muhali (SJMC)

SERIKALI YAKUSANYA SHILINGI BIL.1.9 KUPITIA MAUZO YA MAZAO YA MISITU KWA NJIA YA MNADA .

$
0
0
Mkurugenzi wa TFS Mohamed Kilongo akizungumza kuhusiana na mnada wa mazao ya misitu uliofanyika Longuza wilaya ua Muheza mkoa wa Tanga


Na.Vero Ignatus,Muheza.

Zaidi ya sh 1.9 Billioni Serikali imekusanya,kupitia mauzo ya mazao ya misitu yaliyouzwa kwa njia ya mnada katika Wilaya za Kilosa Mkoa wa Morogoro na Muheza mkoa wa Tanga.

Mohamed Kilongo ni Mkurugenzi waMipango na Matumizi ya Misitu wa Wakala wa huduma za misitu (TFS),Akizungumza wakati wa mnada kwenye shamba la Longuza, amesema kuwa kisasi hicho cha fedha kimekusanywa kwenye misitu ya Mtibwa Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro na Longuza lililopo Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.

Amesema kuwa zaidi ya sh 453.milioni zilikusanywa katika mnadawa shamba la Mtibwa na zaidi ya sh 1.5 Bilioni zilipatikana kwenyeuuzwaji wa miti ya shamba la Longuza baada ya kuuzwa ujazo wa 2100kati ya elfu 12 zilizopangwa kuuzwa.

Aidha amesema Serikali imepanga kuuza miti ya eneo la ujazo wa Mill 1.62.8
katika misiti yake 13 iliyopo kote nchini na kwamba miti iliyouzwa Longuza ni ya aina ya Misaji yenye umri wa miaka 48.

Amesema mwaka 2012 mpango wa uuzwaji wa mazao ya misitu ulianza mara baada ya kuanzishwa kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Misiti nchini (TFS)ambapo aina tatu za kuuzwa mazao hayo zinatumika ikiwemo utumaji maombi yaani mnunuzi,kutangazwa kwa mnada na mali zitakazo uuzwa na ule wa mazungumzo na mnunuzi husika.

Dkt. Cellina ni afisa misitu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Misitu na
Nyuki, Mongo amesema minada hiyo inaendeshwa kwa mujibu wa
sheria ya misitu sura 323, kanuni za misitu za mwaka 2004 na tangazo
la serikali namba 255/2017.

Dkt.Mongo ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa mnada huo alisema sheriahiyo inaelekeza namna ya uuzwaji wa miti hiyo aina ya misaji na kwambautazingatia hali ya bei ya soko iliyopo.

Yusuff Ngage wa Kampuni ya Prime Timber iliyoshiriki mnada huo aliipongeza TFS kwa kuuza misitu kwa njia ya mnada kwa kuwa kila hatua inafanyika kwa uwazi na hivyo kuondoa malalamiko ambayo yalikuwa yakipokea awali"Utaratibu huu utasaidia kuboresha viwanda vya ndani ambavyo vinahitaji bidhaa hizi kwa wingi ili kutekeleza kwa vitendo mpango wa Taifa wa uchumi wa viwanda".Alisema Yusuff.
Aidha Mnada huo uliendeshwa chini ya usimamizi wa viongozi waandamizi wa Idara ya Misitu ya Wiza.ra ya Maliasili na Utalii.

JAFO ATANGAZA WATUMISHI WA UMMA WALIOTEULIWA KUSIMAMIA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MATAA

Timu ya Vijana wa Taifa kushiriki mashindano ya Kuogelea nchini Tunisia

$
0
0





Timu ya Taifa ya vijana ya kuogelea imeondoka nchini kwenda Tunisia kushiriki katika mashindano ya Afrika ya kuogelea.

Timu hiyo inajumuisha jumla ya waogeleaji wanne ambao ni Yuki Omori anayetokea klabu ya Mis Piranhas ya mkoa wa Morogoro, Khaleed Ladha (Mwanza), Aaron Akwenda (Bluefins) na Mohameduwais Abdullatif wa klabu ya Taliss-IST.

Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Asmah Hilal alisema kuwa waogeleaji wapo tayari kuiwakilisha nchi

Katika mashindano hayo ambayo yatajumuisha waogeleaji zaidi ya 1000 kutoka bara la Afrika.

Alisema kuwa waogeleaji hao wamechaguliwa baada ya kufikia vigezo vya mashindano.

Hilal alisema kuwa timu hiyo itakuwa chini ya mkuu wa msafara, Amina Mfaume ambaye ni mkurugenzi wa ufundi wa TSA na kocha mkuu Samwel Mtupo kutoka klabu ya Mwanza.

“Tunatarajia kupata matokeo mazuri katika mashindano hayo pamoja na ugumu wake. Watanzania zaidi ya milioni 50 wanatarajia kuona mnarejea kishujaa,” alisema Hilal.

Kocha wa timu hiyo, Mtupo alisema kuwa wanajua ushindani katika mashindano hayo na kufanya maandalizi kwa lengo la kufanya vyema.

“Tumejiandaa kwa ajili ya kushindana na tunaamini tutafanya vyema. Naamini waogeleaji waliochaguliwa ambao wana ubora wa hali ya juu, tutajitahidi kuiwakilisha nchi vizuri,” alisema Mtupo.

Nahodha wa timu hiyo, Mohameduwais Abdullatif alisema kuwa wamejiandaa kwa ajili ya kushinda na siyo vinginevyo.

“Tumefanya maandalizi kwa muda mrefu kwa lengo la kuleta matokeo ambayo Watanzania watayafuraia, ” alisema Abdulatif.

 Makamu Mwenyekiti wa chama cha kuogelea Tanzania (TSA), Asmah Hilal (kushoto) akimkabidhi bendera nahodha wa timu ya vijana Mohameduwais Abdullatif.
Waogeleaji wa timu ya Taifa ya vijana wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi, viongozi wa chama cha kuogelea na wadau mara baada ya kukabidhiwa bendera.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images