Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Darasa la saba kuanza mtihani kesho, shule zilizofutiwa mitihani 2018, kutumia vituo mbadala

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema vituo nane vilivyofungiwa mwaka jana baada ya kufanya udanganyifu katika mitihani ya darasa la saba vitaendelea kutumia vituo mbadala vilivyopangiwa  hadi baraza hilo litakapojiridhisha kuendelea kutumia vituo hivyo.

Katika mwaka huu 2019, watahiniwa 947,221  wamesajiliwa kufanya mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) unaotarajiwa kuanza kesho (Septemba11 na 12 mwaka huu) huku wakuu wa shule zote nchini wakipewa onyo kutojihusisha na udanganyifu wa mitihani hiyo.

Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Charles Msonde ameyasema hayo leo Septemba 10,2019 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema mwaka jana  baraza ilifuta matokeo  ya Shule za Msingi zote za halmashauri ya Chemba mkoani Dodoma, Shule za Msingi Hazina, New Hazina (Kinondoni), Aniny Nndumi, Fountain of Joy (Ubungo), Alliance, New Alliance na  Shule ya Msingi Kisiwani zote za Mwanza Jiji) na Shule ya Msingi Kondoa integrity (halmashauri mji wa Kondoa) kwa kufanya udanganyifu.

Amesema shule hizo zilifungiwa kufanyiwa au kusimamia mitahani zitaendelea kupangiwa vituo mbadala ambavyo vitaendelea kutumiwa na  watahiniwa wanaoanza mtihani leo.

Aidha, Dk. Msonde amevitaja vituo vitakavyotumiwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam, kuwa ni shule ya Hazina na New Hazina itatumia Shule ya Msingi Oysterbay, Shule ya Fountain of Joy na Aniny Nndumi zitatumia Shule ya Msingi Mbezi, mkoani Mwanza, Shule ya Kisiwani itatumia Kituo cha Shule ya Msingi Kakebe, Shule ya Msingi Alliance na New Alliance za Halmashauri Kondoa Mji  mkoani Dodoma kituo kitakuwa Shule ya Msingi  Mahina.

Dk. Msonde amesema kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa 451,235 ambao ni sawa na asilimia 47.64 ni wavulana na watahiniwa 495,986 ambao no sawa na asilimia 52.36. Waliosajiliwa ni wasichana na kuongeza kuwa kati ya hao, watahiniwa 902,262 watafanya mtihani kwa lugha ya kiswahili na watahiniwa 44,959 watafanya mtihani kwa lugha ya kiingereza ambayo wamekuwa wakiitumia kujifunzia ambapo mtihani huo utakuwa na masomo ya Kiswahili, English  Sayansi, Hisabati na Maarifa ya Jamii.


Pia ametaja watahiniwa wenye mahitaji maalum ni 2,678 kati yao 81 ni wasioona, 780 wenye uoni hafifu, 628 wenye ulemavu wa kusikia, 325 ni wenye ulemavu wa akili na 864 ni wenye ulemavu wa viungo," amesema Dk Msonde.

Dk. Msinde pia ametoa wito kwa Kamati za Mitihani za Mikoa Halmashauri na Majiji kuhakikisha kuwa taratibu za uendeshaji wa mitihani ya taifa zinazingatiwa kwa kuhakikisha mazingira ya vituo kuwa salama, tulivu na kuzuia mianya inayoweza kusababisha kutokea kwa udanganyifu na wasimamizi wot walioteuliwa wameaswa kufanya kazi kwa umakini na uadilifu kulingana ja kanuni za mitihani na miongozo waliyopewa.

"Baraza halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kujihusisha au kusababisha udanganyifu wa mitihani kufanyika kwa kujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma. Tunaomba wadau kutoa taarifa katika vyombo husika kila mnapobaini uwepo wa mtu au kikundi cha watu kujihusisha na udanganyifu wa mitihani wa aina yoyote ile," amesema Dk Msonde.


Baraza hilo limewataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi cha kufanyika mtihani huo kwani hawatasita kufuta kituo chochote endapo litajiridhisha pasipo shaka kuwa uwepo wake unahatarisha usalama wa mitihani hiyo.

pia wasimamizi, wametakiwa kuhakikisha wanalinda haki za watahiniwa wenye mahitaji maalum kwa kuwapa mitihani yenye maandishi ya nukta nundu kwa watahiniwa wasioona na maandishi yaliyokuzwa kwa watahiniwa wenye uoni hafifu.
Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania ( NECTA), Dkt. Charles Msonde akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kufanyika kwa mitihani ya kumaliza elimu ya  msingi mwaka 2019 unaotarajiwa kuanza kesho Septemba 11 na kumalizima Septemba 12 mwaka huu.

HAKUNA RASILIMALI ITAYOPOTEA WALA KUTOROSHWA - DC KYERWA

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus - Michuzi TV, Kagera.
Jeshi la Polisi Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera, limefanikiwa kukamata Madini ya Bati Tani 2.152 yenye thamani zaidi ya Shilingi Milioni 46 tayari kusafirishwa Nchi za jirani kwa njia za Magendo.

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu amesema Rasilimali hiyo imekamatwa kwa nyakati tofauti kufuatia taarifa za wananchi wema, walioshirikiana na jeshi la polisi wilayani Kyerwa waliokuwa katika Doria mpakani kwa ajili ya kuhakisha rasilimali za Nchi hazitoroshwi.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ambae ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya  amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya magendo na wale  wote wanojihusisha na magendo ya aina yoyote ikiwemo Kahawa, Ng'ombe, madini n.k hawatabaki salama na hakuna chochote kitakachopelekwa nje Kupitia Kyerwa.

Kuhusu watuhumiwa na madini yaliyokamatwa Mhe. Mwaimu amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika, na tayari wamewasiliana na Ofisi ya Madini Mkoa wa Kagera ambapo itahusika kutafuta Soko na mwisho hela itayopatikana itaingizwa katika mapato ya Serikali tayari kupangiwa kazi Nyingine.

Itakumbukwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera Brig. Jen. Marco Gaguti amekuwa akisisitiza ulinzi wa rasilimali za Nchi hususani Mkoa Kagera, na kuahidi kutoa asilimia za mauzo ya kile kitakachokamatwa kama magendo, kwa kikundi au mtu mmoja atakayetoa ushirikiano au taarifa za kukamatwa kwa magendo husika. Hivyo katika kuongeza motisha Wilaya ya Kyerwa inandaa zawadi kwa waliofanikisha zoezi hilo.
 Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kyerwa ikiendelea kupima uzito wa Madini yaliyokamatwa yakitoroshwa, zoezi lilifonyika katika kituo Kidogo cha Polisi Kagenyi Wilayani humo.
 Jiwe la madini aina ya Bati miongoni mwa madini yaliyokuwa yakitoroshwa ikidaiwa kuwa na ubora wa juu sana.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kyerwa Rashid Mwaimu akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya ukamataji Rasilimali madini.
Mifuko iliyofungashwa madini ya Bati yenye zaidi ya Tani 2 baada ya kupimwa uzito huo katika kituo cha Polisi Kagenyi Wilayani Kyerwa.

DKT. KIJAJI: WADAU WA KILIMO WAWASILIANE NA BENKI YA TADB KUPATA MIKOPO

$
0
0
Na. Peter Haule na Saidina Msangi, WFM, Dodoma

Serikali imetoa wito kwa wadau wote wa kilimo nchini kuwasiliana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo –TADB ili waweze kupata maelekezo sahihi ya uandaaji wa miradi itakayokidhi vigezo vya kupatiwa mikopo na benki hiyo. 

Wito huo umetolewa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Mbeya Vijijini , Mhe. Oran Njeza, aliyetaka kujua mkakati wa Benki ya Kilimo kuwafikia wakulima wadogo wa Wilaya ya Mbeya.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, Benki ya TADB imefikisha huduma zake mkoani Mbeya na kuongeza kasi ya utoaji wa mikopo kutoka Sh. milioni 799.9 mwezi Desemba 2017 hadi Sh. bilioni 2.54 kufikia Aprili, 2019.

Alisema kuwa mikopo imetolewa kwa miradi 7 ya kilimo na kuwanufaisha wakulima 509 wa Nyanda za Juu Kusini katika wilaya za Mbozi, Momba na Mbalali.

“Benki ya TADB imefanikiwa kufungua Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya, lengo likiwa kuhakikisha Benki hiyo inasogeza huduma zake karibu zaidi na wateja ambao ni wakulima wote wa Nyanda za Juu Kusini, ikiwa ni pamoja na wakulima wadogo wa Wilaya ya Mbeya Vijijini”, alieleza Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji alisema kuwa ili kuhakikisha kuwa Benki ya TADB inakuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wakulima, Serikali imeipatia benki hiyo kiasi cha Sh. bilioni 103, kupitia mkopo wa gharama nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB.

Aidha kwa sasa Benki hiyo inaendelea na mchakato wa kukamilisha masharti ya kupatiwa awamu ya pili ya mkopo wa Sh. Bilioni 103 kutoka Benki hiyo ya Maendeleo ya Afrika.

Benki ya TADB tangu ilipoanza rasmi shughuli zake mwaka 2015, TADB imefanikiwa kujiendesha na kukuza mtaji wake hadi kufikia Sh. Bilioni 67.5 zilizo rekodiwa mwishoni mwa robo ya kwanza ya mwaka 2019 kutoka Sh. Bilioni 60 mwezi Novemba, 2014.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).

UZINDUZI MPANGO SHIKIRISHI WA KUTOKOMEZA KIPINDUPINDU ZANZIBAR

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa Hutuba ya Uzinduzi wa mpango shirikishi wa kutokomeza Kipindupindu Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Idris Abdulwakil Vuga Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa Hutuba ya Uzinduzi wa mpango shirikishi wa kutokomeza Kipindupindu Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Idris Abdulwakil Vuga Mjini Zanzibar.[Picha na Ikulu.] 10/09/2019.

NAPE AJISALIMISHA KWA RAIS MAGUFULI KUOMBA MSAMAHA, RAIS AMABWAMBIA AMSAMEHE...SASA AMTAKA AENDE KUFANYA KAZI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

HATIMAYE Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi Nape Nnauye(CCM) amejisalimisha kwa Rais Dk.John Magufuli kwa kwenda kumuomba msamaha kufuatiakuhusikakwake katika mazungumzo yasiyofaa dhidi ya Rais.

Siku za karibuni sauti ya Nape ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo sehemu ya mazungumzo yake yalisikika akitoa maneno ya kejeli kwa Rais Magufuli.Hivyo leo Septemba 10,2019 amekutana na Rais kwa ajili ya kuomba msamaha.Wiki iliyopita Rais Magufuli atangaza kumsamehe Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Januari Makamba na Mbunge wa Sengerema William Ngeleja ambao nao sauti zao zilisikika wakimsema vibaya Rais.Wabunge hao walimuomba Rais msamaha na baada ya hapo Rais akatangaza kuwaseheme.

Taarifa iliyotolewa leo na Ikulu kwa vyombo vya habari imesema kuwa baada ya mazungumzo hayo Nape amemshukur Rais Magufuli kwa kukubali ombi lake la kukutana nae na kumsikiliza, na pia kumsamehe kwa makosa aliyoyafanya kutokana na taharuki iliyoibuka baada ya kuvuja kwa sauti za mawasiliano yake na wanasiasa wengine wakimsema Rais Magufuli.

"Kwa hiyo baada ya kupata fursa nimekuja, nimemuona, na mle ambamo nilimkosea kama Baba yangu nimezungumza naye na Baba amenielewa.Ameniambia amenisamehe na amenipa ushauri ambao nitaufanyia kazi na naamini baada ya hapa mambo yatakwenda vizuri.

"Na kwa kweli kwa dhati ya moyo wangu nimshukuru sana sana, amenipa fursa kubwa, ndefu na ameongea maneno mengi kwangu na ushauri wake nimeuchukua,"amesema Nape.

Mbali ya kumuomba msamaha Rais Magufuli na kusamehewa,Nape ametumia nafasi hiyo kuzungumzia maendeleo yanayofanywa nchini kwetu, ambapo amempongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa inayofanywa na Serikali na amesema ana matumaini kuwa CCM itapata ushindi katika chaguzi kutokana na kazi hiyo.

Kwa upande wake, Rais Magufuli amesema Nape amekuwa akiomba kukutana nae mara nyingi na tangu siku nyingi kupitia kwa watu mbalimbali wakiwemo wasaidizi wake, viongozi wastaafu na viongozi wa CCM, na baada ya kukutana nae na kumuomba radhi ameamua kumsahehe.

Rais Magufuli amemtaka Nape kwenda kufanya kazi za kuhudumia wananchi wa Jimbo lake la Mtama na kukitumikia vyema chama chake cha CCM."Yote nimesamehe, huyu bado ni kijana mdogo, ana matarajio makubwa katika maisha yake, mimi nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu kwanza ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu na tumefundishwa katika maandiko yote tusamehe saba mara sabini.

"Kwa hiyo nimemsamehe na Mungu amsaidie katika shughuli zake akafanye kazi zake vizuri, akalee Mke wake na familia yake, akakitumikie chama, akawatumikie wananchi wa Jimbo lake vizuri, mimi nimemsamehe, labda kama yeye atakengeuka hiyo itakuwa ni juu yake,"amesema Rais Magufuli.

Pia ameongeza "Lakini mimi kutoka moyoni mwangu nimeshamsamehe na nimemsaheme kweli. Nape nenda ukafanye kazi, Mungu akujaalieee.

Nape alisikika akizungumza kwenye simu ambapo kwa sehemu kubwa mazungumzo yake yalina kumuomba msamaha baada ya sauti yake kusikika akimteta Rais kwenye simu ya mkononi siku za karibuni. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumuomba msamaha Rais Dkt. Magufuli  kufuatia tukio  lililotokea miezi iliyopita.

 Mbunge wa Mtama Nape Nnauye akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao pamoja na kusamehewa kosa aliliofanya Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Mbunge wa Mtama Nape Nnauye akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao pamoja na kusamehewa kosa aliliofanya Ikulu jijini Dar es Salaam.

 
 Mbunge wa Mtama Nape Nnauye akizungumza na Wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU 

MAAFISA WA SERIKALI YA NIGERIA WAANZA ZIARA NCHINI KUJIFUNZA SHUGHULI ZA TASAF.

$
0
0
Na Estom Sanga - TASAF 

Ujumbe wa Maafisa wa Serikali ya Nigeria wapatao 33 umeanza ziara ya siku Nane nchini kujifunza namna Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF unavyotekeleza majukumu yake kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini-PSSN. 

Akiwakaribisha Maafisa hao, Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF ,Bwana Amadeus Kamagenge amesema Mkakati wa Serikali ya Tanzania kupambana na umaskini kupitia TASAF umekuwa na mafanikio makubwa na umeamsha ari ya wananchi kuboresha maisha yao. 

Bwana Kamagenge amesema mkazo mkubwa umewekwa katika uhamasishaji wa Walengwa kushiriki kwenye kazi za uzalishaji mali huku sekta ya elimu na afya hususani kwa watoto kutoka katika kaya za Walengwa zikipewa msukumo mkubwa zaidi kwenye shughuli za Mpango. 

Aidha Mkurugenzi huyo wa Miradi wa TASAF amesema mafanikio yaliyopatikana tangu kuanza kwa shughuli za Mpango yamechangiwa kwa kiwango kikubwa na ushiriki wa Walengwa na Mchango mkubwa wa Serikali na Wadau mbalimbali wa Maendeleo. 

Kwa upande wao Maafisa hao kutoka nchini Nigeria wamesema uamuzi wa kuja Tanzania kujifunza umetokana na taarifa walizonazo juu ya mafanikio makubwa ambayo Serikali ya Tanzania kupitia TASAF imepata kwa kuzifikia Kaya za Walengwa na kuzihudumia kwa mafanikio makubwa katika kupunguza kero ya umaskini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao ni wa aina yake kupata kutekelezwa barani Afrika. 

Ujumbe huo wa Maafisa kutoka Nigeria, mbali na kupata maelezo ya shughuli za TASAF katika Ofisi ndogo za Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam pia utapata fursa ya kutembelea Unguja ambako utakutana na Maafisa wa Serikali na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kisiwani humo . Hii ni mara ya Pili kwa Maafisa wa serikali kutoka Nigeria kutembelea Tanzania kujifunza namna TASAF inavyotekeleza majukumu yake kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF,Amadeus Kamagenge(aliyesimama) akizungumza katika hafla ya kuwakaribisha Maafisa wa Serikali kutoka Nigeria ambao wako nchini kujifunza utekelezaji wa shughuli za TASAF. Kulia kwake ni mkurugenzi wa Fedha wa TASAF Bi. Chiku Thabit.
Baadhi ya Maafisa wa Serikali ya Nigeria wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF katika ofisi ndogo zilizoko jijini Dar es Salaam wakisikiliza maelezo ya utekelezaji wa Shughuli za TASAF wakiwa katika ziara ya mafunzo ya namna Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unavyotekelezwa.
Mmoja wa Maafisa wa Serikali ya Nigeria (aliyesimama) akizungumza kwenye kikao cha kuukaribisha Ujumbe huo ikiwa ni mwanzo wa ziara ya kujifunza shughuli za TASAF zinavyotekelezwa.
Baadhi ya Maafisa kutoka Nigeria wakimsikiliza Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF (hayupo pichani) katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi Ndogo ya TASAF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watendaji wa TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Nigeria ambao wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya namna Mfuko wa Maendeleo ya Jami – TASAF unavyotekeleza majukumu yake kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

ASKARI POLISI WATANO NA MWANAJESHI MMOJA WAFIKISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv.,

ASKARI Polisi watano na Mwanajeshi mmoja wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka matatu likiwamo la wizi wa mafuta ya ndege na Utakatishaji wa zaidi ya Sh. Milioni nne.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Koplo Shwahiba(38), MT. 74164 SGT Ally Chibwana (47), wa jeshi la wananchi Tanzania, PC Elidaima Paranjo (38), PC Simon (28), PC Dickson na PC Hamza.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa na wakili wa serikali , Faraji Nguka akisaidiana na Saada Mohammed mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Mwaikambo imedai washtakiwa wote hao wakiwa ni watumishi wa umma walikiuka maadili ya kazi zao na kupanga genge la uhalifu na kuiba lita 2180 za mafuta ya ndege( Jet A-1/Ik yenye thamani ya sh. 4,647,760.

Katika shtaka la pili imedaiwa, Julai 30,2019 huko katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere uliopo katika Wilaya ya Ilala jijini Darvea Salaam, watuhumiwa hao(askari), waliiba lita 2180 za mafuta ya ndege( Jet A-1/Ik yenye thamani ya sh. 4,647,760 malibya shirika la ndege Tanzania ATCL

Katika shtaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo washtakiwa hao wote walifanya uwizi wa mafuta hayo na kutakatisha kiasi hicho cha sh. Milioni 4.6 ambapo walikuwa wakijua kiwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la wizi kinyume na Sheria.

Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo husikilizwa mahakama kuu au pale DPP atakapotoa kibali cha mahakama hiyo kusikiliza.

Washtakiwa hao ambao wanatetewa na wakili Hasaan Kiangio wmerudishwa rumande hadi Septemba 24 mwaka huu kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

TAEC YASAINI MUENDELEZO UJENZI WA MAABARA AWAMU YA PILI NA KAMPUNI YA DEVELOPMENT CONSTRUCTION LTD

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) Profesa Lazaro Busagala akibadilishana mkataba wa muendelezo wa ujenzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa maabara ya TAEC, ujenzi wenye thamani ya shilingi Bilioni 10,447,749,433.24 na Mkurugenzi wa Kampuni ya M/S LI JUN DEVELOPMENT COMPANY LTD. maabara hiyo itajengwa kwenye makao makuu ya TAEC yaliyopo Njiro jijini Arusha 


Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imesaini mkataba wa shilingi bilioni 10,447,749,423.24 na kampuni ya ujenzi ya M/S LI JUN DEVELOPMENT CONSTRUCTION LTD kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya pili maabara ya kisasa. 

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) Profesa Lazaro Busagala ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha inajenga maabara hiyo kwa kiwango cha hali ya juu kulingana na makubaliano ya mkataba husika. 

Maabara hiyo ni mwendelezo wa maabara ya awamu ya kwanza iliyozinduliwa mwezi April mwaka huu na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa. Ujenzi huu wa maabara ni juhudi zingine za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuendelea kuleta maendeleo nchini. 

Imetolewana; 

Peter G. Ngamilo 
Mkuuwa Kitengo cha Mawasiliano 
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania

WAZIRI MHAGAMA AMPONGEZA KATIBU MKUU MSTAAFU MAIMUNA TARISHI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama amempongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi.Maimuna Tarishi kwa utendaji wenye weledi kwa kipindi cha miaka 34 alichotumikia katika utumishi wa umma.

Ametoa pongezi hizo wakati wa hafla fupi ya kumuaga na kumpongeza katibu mkuu huyo aliyestaafu utumishi wake wa umma kwa mujibu wa sheria za utumishi nchini mapema mwanzoni mwa mwezi Septemba Jijini Dodoma.

“Kwa dhati nachukua nafasi hii kumpongeza Bi. Tarishi kwa namna alivyotumikia Taifa hususani akiwa katika Ofisi hii ya Waziri Mkuu, amefanya vizuri na alijitahidi sana kusimamia vyema ofisi kuhakikisha ofisi inaenda vizuri na hakika unastahiri pongezi kwa kuzingatia ulivyotekeleza majukumu yako kwa busara na weledi wa hali juu,”

Waziri aliongezea kuwa, mchango wa Katibu mkuu huyo ni mkubwa kwa kuzingatia namna alivyotumika kwa miaka mitatu katika ofisi hiyo kwa kuhudumia Ofisi binafsi ya Mhe.Waziri Mkuu pamoja na Uratibu wa Shughuli zote za Bunge.

“Umekuwa ni kiungo muhimu katika kuhakikisha shughuli za Mhe.Waziri Mkuu pamoja na bunge zinatekelezwa katika viwango vya hali ya juu kwa kusimamia vyema hivyo tutakumbuka mchango wako kwa kipindi chote ulichokuwa nasi,”alisema Waziri Mhagama

Aidha Waziri alipongeza timu ya menejimenti ya ofisi hiyo na kukiri kuridhishwa na utendaji wao wenye ufanisi na weledi wa hali ya juu kwa kuzingatia misingi, kanuni na sheria za utumishi wa umma.

“Kipekee ninawapongeza timu ya menejimenti kwa usimamizi wenu mzuri wa ofisi hii hivyo niwatie moyo muendelee kutekeleza majukumu yenu ili kuzaa matunda yanayoonekana kwa kuzingatia ofisi hii ni mratibu wa shughuli zote za serikali,”Alisisitiza Waziri Mhagama

Kwa upande wake aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi.Maimuna Tarishi alishukuru Ofisi ya Waziri mkuu kwa namna walivyochangia katika utekelezaji wake wa majukumu kwa muda aliotumikia katika ofisi hiyo toka tarehe 4 Aprili 2017 alipoteuliwa kusimamia shughuli za Bunge na Waziri Mkuu.

Aidha Tarishi aliiasa timu ya menejimenti kuendelea kuwatumia watumishi vijana katika kutekeleza majukumu kwa kuzingatia uwezo waliona katika kufiri, kutenda na kujituma kwa dhati.

“Nishauri Watendaji mnaobaki wekezeni kwa vijana kwa kuzingatia wanauwezo mkubwa wa kufikiri kwa haraka, wepesi kutenda na wakiaminiwa wanatekeleza kwa juhudi ili kuthibitisha uwezo wao hivyo muwatumie kwa tija na maendeleo ya nchi yetu’”alisema Tarishi

Aidha aliongezea kuwa, uwepo wa vijana katika ofisi za umma unamchango mkubwa kwa kuzingatia uwezo walionao wa kubuni mbinu mbalimbali zinazorahisisha utendaji kazi kwa kuzingatia ukuaji wa sayansi na teknolojia hivyo  wekezeni nguvu kwa kundi hilo.

“Chukue fursa ya ukuaji wa sayansi na teknolojia katika kuboresha ufanishi na ubunifu katika kutekeleza majukumu yenu ya kila siku kwa kuwekeza kwa vijana, kwa kuwatia moyo na kuwaelekeza pindi inapobidi ili kuleta matokeo chanya katika kutekeleza majukumu ya kila siku,”alisisitiza Tarishi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Timu ya Menejimenti ya Ofisi yake wakati wa hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi yake (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi Septemba, 2019 Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi zawadi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi wakati wahafla fupi  ya kumuaga iliyoandaliwa na ofisi yake.
 Katibu Mkuu Msaafu wacOfisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akieleza historia yake katika utumishi wa umma (Miaka 34) kwa timu ya menejimenti ya ofisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyoongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi.Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa halfa hiyo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimpongeza Katibu Mkuu Msataafu wa ofisi yake Bi.Maimuna Tarishi wakati wa hafla hiyo.
 Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Maimuna Tarishi (Mstaafu) wakati hafla hiyo.
 Katibu Mkuu Mstaafu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) hiyo Bi. Maimuna akizungumza na timu ya Menejimenti ya ofisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kumuaga kwa kustaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria za utumishi.
 Mhasibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Anthony Chayeka akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Bunge na Siasa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Raymond Kaseko akiungumza jambo wakati wa hafla hiyo
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Paul Sangawe akieleza jambo wakati wa hafla hiyo.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

TAASISI YA MOI WAMFANYIA UPASUAJI MKUBWA, ASKOFU MKUU JIMBO KATOLIKI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mhashamu Yuda Thadeus Rwaichi.

 Na Said Mwishehe, Michuzi Blogu 
MADAKTARI na wauguzi wa Taasisi ya MOI wamemfanyia upasuaji mkubwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Rwaichi kwa saa tatu na kwamba hali yake inaendelea vizuri.

Taasisi ya MOI imeuarifu umma wa Watanzania kwamba jana Septemba 9,2019 , saa tano usiku  walimpokea Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwaichi baada ya huduma katika ya hospitali ya KCMC.

Taarifa iliyotolewa leo Septemba 10,2019 na Patrick Mvungi wa Kitengo cha Uhusiano  MOI  amesema kuwa baada ya kupokelewa ,wataalam wa MOI walimfanyia uchunguzi na vipimo na kubaini alihitaji upasuaji wa dharura.

"Jopo la madaktari bingwa pamoja na wauguzi wa taasisi ya MOI walimfanyia upasuaji mkubwa kwa muda wa saa tatu kuanzia saa saba usiku hadi saa 10 alfajiri .Upasuaji huo ulifanyika kwa mafanikio makubwa .Baada ya upasuaji hali ya Mhashamu Askofu Ruwaichi inaendelea vyema na bado yuko kwenye chumba cha uangalizi maalum (ICU),"amesema Mvungi.

Hata hivyo taasisi hiyo ya MOI imesema inawatoa hofu watanzania wote hususani waumini wa Kanisa Katoliki kwamba hali ya Mhashamu Askofu Rwaichi inaendelea vizuri na kikubwa ni kuendelea kumuombea ili apone mapema na kurejea kwenye majukumu yake ya utumishi.

JUKWAA LA WADAU WANAOTUMIA RASILIMALI YA MAJI LAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
* Yaelezwa kuwa  asilimia 90 ya viwanda vinategemea huduma ya maji kutoka bonde la Wami/Ruvu

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
LEO Septemba 10, jukwaa  maalumu la wadau wanaotumia maji katika bonde la Wami/Ruvu limezinduliwa rasmi na hiyo ni pamoja na kujadili hali ya maji katika bonde hilo pamoja na kujadili changamoto na utatuzi wake ili kuendelea kutunza hazina hiyo ya maji kwa kizazi cha sasa na baadaye.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali za maji kutoka Wizara ya maji Rosemary Rwebugisa  amesema kuwa jukwaa hilo limewahusisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali na wananchi ambao ndio walengwa wakubwa wa rasilimali hiyo, na kueleza kuwa ili malengo yaweze kufikiwa lazima wataalamu na wananchi washirikiane ili kuweza kuleta maendeleo endelevu hasa ya kiviwanda kupitia rasilimali ya maji.

Amesema kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na sekta na wadau mbalimbali katika kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa na kuhifadhiwa na hiyo ni pamoja na mamlaka husika kusimamia matumizi ya maji kulingana na uwepo wake pamoja na kutatua migogoro inayohusu  rasilimali ya hiyo.

Mwenyekiti wa bonde la Wami/Ruvu Hamza Sadick amesema kuwa bonde hilo la Pwani ambalo ni moja kati ya mabonde tisa yanayopatikana Tanzania bara ni muhimu sana katika kukuza na kuendeleza viwanda na hiyo ni kutokana na maeneo mengi kutegemea maji kutoka bonde hilo na hiyo ni pamoja na jiji la Dar es Salaam, Dodoma na miji ya Kibaha na Bagamoyo ambayo imesheheni viwanda ambavyo hutegemea rasilimali maji katika kujiendesha.

Hamza amesema kuwa wataendelea kuimarisha usimamizi madhubuti wa maji yaliyokuwepo kwa kizazi cha sasa na kijacho na kueleza kuwa changamoto kubwa inayokabili usimamizi wa rasilimali hiyo ni pamoja na uvamizi katika hifadhi za maji, ukataji miti, uchimbaji wa madini na mchanga katika hifadhi za maji pamoja na kuendesha shughuli za kilimo katika hifadhi za maji na kupitia jukwaa hilo hilo wanaamini changamoto hizo zitakomeshwa ili kuendelea kuhifadhi vyanzo vya maji.


Amesema kuwa matumizi ya maji yamekuwa makubwa majumbani na viwandani huku changamoto ya uchafuzi wa vyanzo hivyo ukipelekea maji kupungua, maji kubadilika na kuwa ya chumvi pamoja na kuchafuliwa kwa vyanzo hivyo kupitia maji ya viwandani na chemba za maji taka zilizoelekezwa kwenye vyanzo vya maji, ambapo amewashauri wananchi kutojihusisha na shughuli ambazo zitapelekea kuharibu vyanzo hivyo na watakaokiuka taratibu kwa kuharibu vyanzo hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Bonde la Wami/Ruvu lilianza mwaka 2002 likihudumia Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Manyara na jiji la Dodoma pamoja na Mbuga za Mikumi, Selous, Saadan na milima ya Tao na limeendelea kuhudumia na kuhakikisha viwanda na wananchi wanaotegemea bonde hilo wanapata huduma faaafu kulingana na matumizi yao na uwepo wa rasilimali hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Maji Rosemary Rwebugisa akizungumza wakati uzinduzi wa jukwaa la watumiaji maji lililofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mwenyikiti wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Hamza Sadiki akitoa maelezo kuhusiana na bonde  na wanavyotekeleza katika Uhifadhi wa vyanzo vya maji  katika uzinduzi Jukwaa la watumiaji maji lililofanyika jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani akizungumza kuhusiana hali ya Maji na hatua wanazozichukua kwa watumiaji  katika uzinduzi wa Jukwaa la watumiaji Maji lililofanyika jijini Dar es Salaam.

 Mhandisi wa Bonde la Wami/Ruvu Halima Abdallah akitoa maada katika mkutano wa Jukwaa la watumiaji maji lililofanyika jijini Dar Salaam.
 Baadhi wadau katika uzinduzi wa Jukwaa la watumiaji maji lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Maji Rosemary Rwebugisa na watendaji wa Wami/Ruvu pamoja na wadau katika uzinduzi wa Jukwaa la watumiaji maji lililofanyika jijini Dar es Salaam.

NAPE AMWAMBIA RAIS DKT. MAGUFULI ALIKUWA HANA AMANI, HAPATI USINGIZI

$
0
0
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye akipeana mkono na Rais Dkt. John Magufuli mara baada ya kuomba msamaha leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MBUNGE wa Mtama Nape Nnauye amemwambia Rais Dkt. John Magufuli kuwa hakuwa na amani, wala hakuwa anapata usingizi lakini sasa moyo wake unaamani na atalala usingizi.

Nape ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na Rais na kufanya naye mazungumzo ambayo kwa sehemu kubwa ilikuwa ni kumuomba msamaha Rais kwa mambo yaliyotokea siku za karibuni.

Akizungumza mbele ya Rais Magufuli akiwa Ikulu leo Septemba 10, 2019 jijini Dar es Salaam Nape amesema kuwa "Leo nimefurahi sana kumuona baba yangu, Mwenyekiti wangu wa CCM na Rais wangu. Baada ya kumuomba msamaha na kunisamehe hakika moyo wangu unaamani kubwa, nilikuwa sipati usingizi, ilifika mahali naamka saa nane ya usiku  usingizi unakata, leo nitalala na nina amani moyoni," amesema Nape.

Amefafanua "Mimi kama mtoto wa CCM, kama mwanaye nikasema ni vizuri nije niongee na baba yangu ,amenipa fursa ya kuja kuniona, ameniambia amenisamehe na amenipa fursa kubwa.

"Kwa hiyo mheshimiwa Rais kama baba yangu, kama mzee wangu nashukuru kwa fursa uliyonipa na pia  kwa kunisikiliza, kwa kunisamehe, pia kwa kunishashauri na kunielekeza ninafanyaje huko mbele ninako kwenda."

Wakati Nape anajiandaa kuondoka Ikulu akiwa ameshikana mkono na Rais Magufuli na kumwambia hakuwa anapata usingizi na moyo wake haukuwa na amani lakini sasa anayo amani moyoni mwake baada ya Rais kumsamehe.

Rais Magufuli baada ya kumsikiliza Nape, amesema hivi "mimi nishamsemehe, nimemsamehe kwa dhati  ya moyo wangu, Nape amekuwa hata akiandika meseji nyingi, ameshaandika meseji ya kuomba msamaha saa nane usiku.

"Amekuwa akiniomba msamaha, na ukiangalia meseji zake unaona kabisa huyu mtu anaomba msamaha. na leo aliniomba aje anione na hata wasaidizi wangu wamekuwa wakipata hiyo habari, amejaribu kwenda kwa mzee Mangulla, kwa mzee Apson na amefika mpaka kwa mama Maria Nyerere." ameeleza Rais Magufuli.

"Amehangaika kweli lakini sisi tumeumbwa kusamehe, na leo umemuoana asubuhi amekuja, nikasema siwezi kuzuia kumuoana. Nikasema ngoja niache shughuli zangu na kubwa zaidi, ameniambia baba nisamehe." amesema Rais

"Kusamehe kunaumiza lakini nasema kwa dhati kabisa nimemsamehe, nimesamehe kabisa. Ameeleza yaliyokuwa yanamsibu lakini pia ameeleza watu waliokuwa wanamhubiri, wengine wako kwenye chama.

"Lakini nimesema yote nimemsamehe, huyu bado ni kijana mdogo na ana maono mazuri katika maisha yake, nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu kwanza ni dhambi kubwa kwa Mwenyezi Mungu na tumefundishwa katika maandiko yote kusamehe saba mara sabini.

"Mungu amsaidie katika shughuli zake, akafanye kazi vzuri, akalee mke wake na familia yake, akakitumie chama, akawatumikie wananchi wa jimbo lake," amesema Rais Magufuli na baada ya maelezo hayo Nape alimwambia Rais hakuwa na amani katika moyo wake.

Hata hivyo Rais Magufuli alimuuliza  hakuwa na amani? Nape akajibu ndio, na wakati mwingine hakuwa anapata usingizi. Wakati anaondoka Rais alimshauri Nape awe anasali sana na kumuomba Mungu, ambapo Nape naye akasikika akimueleza Rais kuwa anasali. Baada ya hapo kicheko kikachukua nafasi yake na Nape akaondoka Ikulu.

WANANCHI KIGOMA KUNUFAIKA NA UJENZI WA MADARAJA YA MAWE

$
0
0
 Daraja la Nyabigufa linaloendelea kujengwa na  Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kushirikiana na  Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Serikali ya Ubelgiji chini ya Mradi wa Sakirp – Enabel  pamoja na wananchi lililopo katika mto Kaseke, Kijiji cha Nyabigufa Kata ya Mkongoro.
 Wananchi wa Kijiji cha Nyabigufa Kata ya Mkongoro katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wakiwa wanaendelea na ujenzi wa Daraja la Nyabigufa lililopo Mto Kaseke, Kata ya Mkongoro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Pendo E. Mangali akiwa na wataalam kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), wakati wa Ukaguzi wa daraja la Rubumba lililopo Kijiji cha Nyarubanda Kata ya Nyarubanda.
Geofrey A.Kazaula na Bebi Kapenya - Kigoma
WANANCHI wa halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wanatarajia kunufaika na Ujenzi wa Madaraja ya mawe unaofadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji chini ya mradi wa Kilimo endelevu katika Mkoa wa Kigoma (Sakirp – Enabel) na kusimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kigoma Bi. Pendo E. Mangali ameeleza kuwa mradi huo uliibuliwa na wananchi baada ya kueleza changamoto wanayokutana nayo katika kusafirisha mazao yao kutoka mashambani hadi majumbani na kwenye masoko.

Kiongozi huyo amebainisha kuwa mradi huo wa Ujenzi wa madaraja ya mawe unalenga kutatua kero ya usafiri na usafirishaji wa mazao na kwamba wananchi walihamasishwa na wakakubali kujitokeza katika kusomba mawe na kushiriki kujenga madaraja hayo.

“Nitumie fursa hii kuwapongeza sana wananchi wa Halmashauri ya Kigoma kwani wanafanya kazi sana, baada ya kugundua kuwa wanashindwa kusafirisha mazao yao kutoka mashambani hadi sokoni kwa pamoja tuliamua kuanza ujenzi wa madaraja ya mawe”, amesema kiongozi huyo.

Kiongozi huyo amebainisha kuwa baada ya kukamilika kwa madaraja hayo kazi itakayokuwa imebaki ni Kufungua barabara za kuunganisha mashamba na hatimaye kuwezesha wananchi kufikisha mazao yao sokoni kwa urahisi na kukuza kipato chao.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mhandisi Pharles E. Ngeleja ameeleza kuwa Ujenzi wa madaraja kwa teknolojia ya kutumia mawe ni wa gharama nafuu na kwamba una washirikisha wananchi moja kwa moja kwa kukusanya vifaa vinavyopatikana katika mazingira yao hususani mawe na wafadhili wanatoa vifaa vya viwandani visivyopatikana kwenye mazingira mfano simenti huku TARURA wakisimamia shughuli za ujenzi .

Akiongea kwa niaba ya wananchi wanaoshiriki katika ujenzi wa madaraja hayo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyabigufa Ndg. Johnphace Kabora Tunzwe amesema kuwa changamoto ya usafiri ni kubwa hasa kipindi cha masika na hivyo tayari wameamua kujitolea kwa kukusanya mawe ili kujenga madaraja .

“Kwanza nawashukuru TARURA, Sakirp Enabel na Halmashauri ya Kigoma kwani mwanzo tulidhani kuwa kazi hii ni ngumu sana na haiwezekani lakini sasa kama mnavyoona tayari tumeanza kukamilisha ujenzi wa daraja” amesema Kiongozi huyo.

Aidha ameongeza kuwa baada ya kukamilisha ujenzi wa daraja, kazi itakayokuwa imebaki ni Kufungua barabara za kufika mashambani ili kuwasaidia wananchi kusafirisha mazao yao na kwamba anaimani kuwa Serikali kupitia TARURA watafungua barabara .

Naye Meneja mshauri wa mradi huo chini ya Serikali ya Ubelgiji Ndg. Steven Hollevoet ameeleza kuwa Teknolojia ya ujenzi wa madaraja ya mawe ni ya muda mrefu hasa katika nchi za Ulaya na Asia na sasa wameileta Tanzania ili kuwafundisha wananchi kujenga madaraja kwa gharama nafuu kwasababu vifaa vinavyotakiwa kama mawe na mchanga vinapatikana kwa urahisi.

Hadi sasa madaraja sita yamekamilika na madaraja tisa yapo katika hatua mbalimbali huku lengo likiwa ni kukamilisha madaraja kumi na tano ifikapo mwezi Desemba, 2019.

JUMA CHOKI AJIFUA KUMKABIRI MWAKYEMBE SEPTEMBA 15

$
0
0
Bondia Juma Choki kushoto akioneshana umwamba na bondia wa Kimataifa ambaye alishawai kuishi nchini Marekani miezi takribani 8 kwa ajili ya mchezo wa masumbwi nchini humu Ibrahimu Class 'KING CLASS MAWE' Choki anajiandaa na mpambano wake wa fainal dhidi ya Emanuel Mwakyembe septemba 15 katika ukumbi wa bucket club uliopo Masaki Dar es salaam
Bondia Juma Choki kushoto akioneshana umwamba na Ibrahimu Makubi wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Super D Coach iliyopo kariakoo
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kamba ya Super D coach Shule ya Uhuru Dar es salaam Jana
Bondia Alex Kachelewa kushoto akitupiana makonde na Juma Choki wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Super D coach shule ya Uhuru 
Bondia wa Kimataifa nchini Tanzania ambaye alishawai kuka nchini Marekani kwa Takribani ya miezi nane kwa ajili ya mcheszo wa masumbwi Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto' akioneshana umwamba na Juma Choki anayejiandaa na mpambano wake dhidi ya Emanuel Mwakyembe utakaofanyika septemba 15 katika ukumbi wa Backet club ulipo masaki.
Bondia wa Kimataifa nchini Tanzania ambaye alishawai kuka nchini Marekani kwa Takribani ya miezi nane kwa ajili ya mcheszo wa masumbwi Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto' akioneshana umwamba na Juma Choki anayejiandaa na mpambano wake dhidi ya Emanuel Mwakyembe utakaofanyika septemba 15 katika ukumbi wa Backet club ulipo masaki

Na Mwandishi Wetu
BONDIA Juma Choki anaye jiandaa na mbambano wake dhidi ya Emanuela Mwakyembe septemba 15 katika ukumbi wa bucket Clab uliopo Masaki jijini Dar es es salaam amejinasibu kumtwanga bondia huyo na kuchukuwa ubingwa wa king of The Ring 

akijinasibu bondia huyo alivyotembelewa kambini kwake kwa Super D Coach iliyopo shule ya Uhuru Jijini Dar es salaam 

Amesema kuwa mwakembe ana uwezo wa kukanyaga moto wake ata siku moja huko alikutana na viande sasa kaja kwenye kazi kazi hapo ndipo pa kuoneshana uwezo kama anavyosemaga kocha Super D Kazi Kazi No Pain No Gain yani siku hiyo patachimbika hivyo mwakyembe ajipange sana kwana mazoezi ninayofanya na mbinu ninazofundishwa sio za kitoto hatari tupu

Nae kocha wa bondia huyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema hii ni vita kubwa sana kwa kuwa kocha wa mwakyembe Edward Lwiyakwipya wamesoma nae pamoja katika ngazi kubwa ya kozi ya kimataifa hata hivyo mimi nina mbinu nyingi zaidi yake ata hivyo nita akikisha napata ushindi usiokuwa wa kuwachosha majaji hivyo matumaini yangu ni kumpiga k,o mbaya zaidi

ikumbukwe kuwa mabondia wote wenye viwango vya juu nchini wanatoka kwangu ukiangalia mabondia wote wakubwa wanatoka kwangu na wana viwango vya kimataifa hivyo najivunia kwa hilo ukiangalia mabondia wanaotoka kwangu akuna ata mchovyu mmoja alijinasibu Super D

Ameongeza kwa kusema mikono yake wamepita mabondia wengi sana akiwemo Sanday Kiwale, Idd Mkwera Vicent Mbilinyi Ibrahimu Class' King Class Mawe' Shomali Milundi Shabani Kaoneka na mabondia mbalimbali nchini wote wamepita katika mikono yangu kwa njia moja au nyingine hapa ndio No Pain No Gain kazi kazi hivyo wapenzi wa ngumi muje kwa wingi kuangalia kazi hii ambayo aita muacha mtu salam.

KIFUSI CHA UDONGO CHAUA MCHIMBA MADINI, WENGINE TISA WAJERUHIWA WILAYANI MISINGWI

$
0
0
amanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Mulilo Mulilo 

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MCHIMBAJI mdogo wa madini ya dhahabu aliyefahamika kwa jina la Ndaki Juma(45), amefariki dunia huku wengine nane wamejeruhiwa baada gema la machimbo ya madini ya dhahabu katika duara namba 50 yaliyopo Kata ya Inonelwa wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza kuangukiwa na kifusi wakati wakiendelea na shughuli za uchimbaji madini.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Mulilo Mulilo amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo limetokea Septemba 9,2019 saa moja asubuhi katika machimbo hayo ya dhahabu Shilalo, yaliyopo kata ya Inonelwa wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza wachimbaji wadowadogo wakiwa kwenye shughuli zao za kawaida za uchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu katika duara namba 50 mali ya Deogratius Ushanga na duara namba 47 g mali ya Peter Charles, duara zilizo kuwa na wachimbaji takribani 10.

Amewataja wachimbaji waliokuwa kwenye machimbo hayo ni Ndaki Juma (45) , Nyamikoma-busega, Keo Werema (34)John Katwale( 35), Mwita George (27), Masanja Charles ( 42) Abdallah Abdu(38), Bengwe Clenent(29), Songa Charles(28) Emmanuel Mathias(34) na Mang’era Meki(40).

"Wakati wakiendelea na uchimbaji ndani ya maduara hayo ghafla gema la udongo lilimeguka, likaporomoka na kuanguka kisha kufunga njia za maduara hayo. juhudi za haraka zilifanyika na kufanikiwa kuwaokoa watu wanane wakiwa hai,wakiwa na majeraha mbalimbali na mtu mmoja alikutwa amefariki ambae ni Ndaki Juma na jitihada za kumuokoa mtu aitwaye Keo Werema zinaendelea kufanyika. Majeruhi walifikishwa hospitali ya wilaya Misungwi kwa matibabu na maiti imehifadhiwa hospitalini kwa hatu za uchunguzi,"amesema Kamanda Mulilo.

Katika tukio lingine Kamanda Mulilo amesema tarehe 06/08/2019 ,saa saba maeneo ya Mtaa Kagera jirani na Shule ya msingi Kagera wilayani Ukerewe kulitokea tukio la mauaji ambapo Euzebia Didakus Malas (16) ambaye ni mwanafunzi kidato cha tatu shule ya sekondari Nansio aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani.

Amesema Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata Joseph Msafiri Anthon(30) mkazi wa mtaa wa Kagera Nansio ambaye ni Mwalimu wa shule ya msingi Namabugo, uchunguzi wa awali unaonesha kumtuhumu mwalimu huyo kuhusika na mauaji hayo.

Wakati tukio la tatu limetoa Septemba 7, mwaka 2019 huko wilayani Sengerema katika ufuatiliaji walikamatwa watuhumiwa wanne kuhusiana na tukio la kuvunja nyumba usiku na kuiba silaha aina ya rifle lililotokea Septemba 2 mwaka 2019 huko kijiji cha Isaka kata ya Nyehunge ambapo silaya yenye namba nyg/ir/95/2019 imekamatwa na watuhumiwa James Juma(20) , Alex Panda( 49), Shaban Mohamed (42) na mapambano Charles( 35).

"Baada ya kuwakamata watuhumiwa waliwapeleka askari katika eneo la Isaka Nyehunge na kupelekea kupatikana kwa silaha rifle yenye namba a 6986 ambayo ni kilelezo kilicho ibiwa katika tukio tajwa,"amesema Kamanda.

Pia Kamanda Mulilo amesema Agosti 15 mwaka huu wa 2019 katika eneo la Mahina mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Mahina Martha Joseph(16) alikutwa ameuawa baada ya kubakwa na kisha mwili wake kutelekezwa sehemu yenye mawe mengi. 

"Watuhumiwa wafuatao wamekamatwa na kukiri kuhusika na mauaji hayo ambapo ni Sospeter Kazumari (37), Jastine John ( 24), Amos Andrea(36) na Rebeka Bukindu (35,"amesema.

BENKI YA CRDB YAANDAA KONGAMANO LA UWEZESHAJI WAKANDARASI MIRADI YA MAENDELEO NCHINI

$
0
0
Benki ya CRDB imeandaa kongamano maalum la uwezeshaji kibiashara kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wa ujenzi wa miradi ya maendeleo nchini ikiwamo ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge Railway) na mradi wa uzalishaji umeme wa bonde la mto Rufiji (Rufiji Hydropower Project).

Akizungumza wakati wa kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na makampuni zaidi ya 400 ya ukandarasi na watoa huduma mbalimbali, Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts alisema kongamano hilo limelenga katika kuwajengea uwezo wakandarasi nchini ili kuwasaidia kutekeleza miradi yao kwa ufanisi zaidi.

“Benki yetu ya CRDB imeweka mikakati mikubwa katika kuhakikisha tunaisaidia Serikali yetu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo, tulianza kwa kutoa mikopo na dhamana katika miradi mbalimbali ikiwamo mradi wa reli ya kisasa ya SGR na mradi wa umeme wa maji wa Rufiji (RHPP). Sasa hivi tumejipanga kuongeza wigo wetu katika kuwasaidia wakandarasi na watoa huduma katika miradi hii, kwani hawa ndio watekelezaji wenyewe,” alisema Dkt. Witts.

Dokta Witts alisema benki hiyo kupitia kauli mbiu yake ya “Tupo Tayari” imejipanga vilivyo kuwahudumia Wakandarasi hao nchini huku akitaja baadhi ya huduma ambazo benki hiyo inazitoa kwa ajili ya wateja kupitia idara yake ya wateja wakubwa.

“Benki yetu sasa hivi inatoa huduma ya dhamana kwa wakandarasi au wateja ambao wanatafuta kazi ijulikanayo kama ‘Bid Guarantee’ hii inatuwezesha kumjengea mkandarasi uwezo wa kupata kazi, lakini vilevile tunatoa dhamana za utekelezaji wa miradi ‘Performance Guarantee’ na dhamana za malipo ya awali ‘Advance Payment Guarantee’,” alisema Dkt. Witts.

Dkt. Witts alisema Benki hiyo imeboresha taratibu zake za utoaji mikopo akiwataka wakandarasi hao kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo, pamoja na kujiunga na huduma za bima ili kujikinga na majanga yanayoweza kutokea. “Benki ya CRDB ni Benki yenu, na sisi tupo hapa kuwahudumia niwahakikishie tu sisi Tupo Tayari kuwahudumia,” alihitimisha Dkt. Witts.

Kwa upande wake Msajili Mkuu wa Wakandarasi nchini (CRB), Rhoben Nkori aliipongeza Benki ya CRDB kuwa mstari wa mbele kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini huku akiwataka wakandarasi wote kuchangamkia fursa hiyo inayotolewa na Benki ya CRDB katika kukuza na kuboresha utendaji wa kazi zao.

Wakandarasi na wadau mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo waliipongeza Benki ya CRDB kwa hatua hiyo ya kuwakutanisha wadau wa sekta ya ujenzi nchini huku wakieleza fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB zitakwenda kuleta sura mpya katika utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu nchini.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akizungumza katika Kongamano la uwezeshaji kibiashara lililoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini, lililofanyika leo kwenye ukumbu wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Wateja wa Kati na Wadogo wa Benki ya CRDB, Boma Raballah akizungumza katika Kongamano la uwezeshaji kibiashara lililoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini, lililofanyika leo kwenye ukumbu wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa Benki ya CRDB, Tully Ester Mwambapa akizungumza jambo wakati alipokuwa akiongoza Kongamano la uwezeshaji kibiashara lililoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini, lililofanyika leo kwenye ukumbu wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya CRDB, Toyi Ruvumbagu akizungumza wakati alipowasilisha mada yake katika Kongamano la uwezeshaji kibiashara lililoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini, lililofanyika leo kwenye ukumbu wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa makandarasi nchini, Consolata Ngimbwa akichangia mada katika Kongamano la uwezeshaji kibiashara lililoandaliwa na benki ya CRDB kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini, lililofanyika leo kwenye ukumbu wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.






























MWANDISHI SEBASTIANI ATILIO AFIKISHWA MAHAKAMANI ,APELEKWA MAHABUSU

$
0
0
Sebastian Atilio akiwa katika mahakama ya Wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa kabla ya kusomewa mashtaka yake leo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo.

MWANDISHI wa habari wa kujitegemea anayeandika habari zake katika ukurasa wa kitabu sura (face Book )katika wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa Sebastian Atilio amefikishwa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Mufindi kwa makosa mawili likiwemo la kuandika habari za uongo na kufanya kazi bila kusajiliwa na bodi anaripoti mwandishi Francis Godwin kutoka mkoani Iringa.

Akisoma mashtaka haya leo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Edward Uforo .mwendesha mashitaka wa jamhuri Victor Kitamale alisema kuwa Sebastian anashitakiwa kwa kosa la kwanza kufanya kazi bila kusajiliwa katika bodi ya uandishi na kosa la pili ni kuandika habari za uongo juu ya wananchi wa kijiji cha Ifupila kuhamishwa .

Hata hivyo msitakiwa huyo alikana mashitaka yote yanayomkabili huku mahakama hiyo ikisema kuwa makosa hayo kisheria yanadhamana .

Wakati mwendesha mashtaka wa jamhuri alipinga dhamana hiyo chini ya kifungu namba 148(5) D) cha sheria na mwenendo wa makosa ya jinai (sura 20) ambapo jamhuri imefaili kiapo cha kuzuia dhamana kutolewa.

Huku upande wa mashtaka umepewa na mahakama hiyo nafasi ya kufaili hati kinzani Septemba 16 mwaka huu ili Septemba 18 mwaka huu maombi ya kutolewa ama kutotolewa kwa dhamana yatajulikana.

Wakili wa mwanahabari huyo Emmanuel Chengula kutoka mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC) alisema kuwa hatua ya kufikishwa mahakamani kwa mteja wake ni mwanzo wa haki yake kupatikana kwani polisi walikuwa wakimzuia mahabusu mteja wao toka jumamosi iliyopita bila kumpeleka mahakamani.

Wakili Chengula alisema katika kesi hiyo kuna maombi ya kuzuia dhamana ambayo ni maombi namba 10/2019 na kesi yenyewe ya msingi ni kesi namba 208/2019.

Mshitakiwa huyo amepelekwa katika mahabusu ya Isupilo Mufindi hadi septemba 18 atakapofikishwa mahakamani hapo tena kwa ajili ya kusikiliza maamuzi ya dhamana yake.

TANZANIA YAWEKEZEA MKAKATI WA KUTOKOMEZA UKATILI KWA WATOTO NA WANAWAKE

$
0
0
 Dr Naftari Ng'ondi kamishina wa ustawi wa jamii nchini Tanzania  amesema serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza mkakati wa miaka mitano wa kutokomeza  ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (Mtakua) ili kumaliza tatizo hilo ifikapo mwaka 2021.
 Baadhi ya wajumbe kutoka nchini Tanzania waliowakilisha mkutano wa msaada wa kisaikolojoa kwa watoto uliofanyika nchi Namibia.
 Baadhi ya wajumbe kutoka nchini Tanzania waliowakilisha mkutano wa msaada wa kisaikolojoa kwa watoto uliofanyika nchi Namibia.

Tumaini Godwin, Namibia.
 SERIKALI ya Tanzania inaendelea kutekeleza mkakati wa miaka mitano wa kutokomeza  ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (Mtakua) ili kumaliza tatizo hilo ifikapo mwaka 2021.


Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini Tanzania, Dk Naftari Ng'ondi amesema hayo  wakati akiwasilisha mkakati huo kwenye mkutano wa kimataifa wa msaada wa kisaikolojia kwa watoto(PSS FORUM) unaofanyika Windhoek nchini Namibia.


Dk Ng'ondi amesema mkakati huo ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2016  umetamka wazi kuwa pamoja na mambo yote, tatizo la mimba na ndoa za utotoni linapaswa kushughulikiwa.


"Mimba za utotoni maana yake kuna ubakaji umefanyika na  kwa Tanzania hilo ni kosa la jinai, tumeimarisha sheria ya mtoto na yeyote anayekutwa na kosa la kumpa mimba mwanafunzi anafungwa jela miaka 30," amesema Kamishna huyo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.


Amesema mbali na sheria, wanatekeleza mkakati huo kwa kuikarisha kamati za ulinzi wa mtoto kwenye kata kwa kuzipatia nguvu ya kupokea, kuchunguza na kuchukua ikiwa ni pamoja na kufungua kesi.


Dk Ng'ondi amesema nguvu kubwa imewekwa katika kutoka  elimu kwa Jamii na vijana kupitia kampeni mbalimbali.


"Na sasa hivi tunaendesha kampeni inayoitwa Twende pamoja, tokomeza ukatili," amesema.


Awali Balozi wa Umoja wa Mataifa wa Mpango wa kutokomeza mimba za utotoni, Nyaradzayi Gumbonzvanda alisema nchi za Afrika zinapaswa kufanya kampeni ya kuhakikisha tatizo la mimba za utotoni linaisha.


Amesema nchi nyingi za Afrika zinakutana na changamoto ya mimba za utotoni huku umaskini ukichangia tatizo hilo.


"Tuandae mkakati ya kumalizaa tatizo,inawezekana," amesema Gumbonzvanda.


Mkutano huo unaoendeshwa na Shirika la Msaada wa Kisaikolojia kwa Watoto (REPPSI) umezikutanisha zaidi ya nchi 24 kutoka kusini mwa Afrika.

TANZANIA YAPOKEA FARU TISA KUTOKA MFUKO WA GRUMET

$
0
0
 Ndege iliyowabeba Faru kutoka nchini Afrka Kusini ikishusha baadhi ya mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA, Faru hao wametolewa na Mfuko wa Grumet (GF) kwenda Serikali ya Tanzania
PIX 3: Baadhi ya maboksi yaliyobeba Faru walitolewa na Mfuko wa Grumet.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu akisaini nyaraka muhimu za makabidhiano ya Faru na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Grumet (GF), Stephen Cunliffe mara baada ya kupokelewa kwa Faru kutoka nchini Arusha. 

Na Mwandishi Wetu, KIA
SERIKALI ya Tanzania imepokea Faru Tisa kutoka Mfuko wa Grumet (GF) nchini Afrika Kusini.

Faru hao wamepokelewa alfajiri Saa 9 jana katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), na kusafirishwa kwa ndege kuelekea Ikolongo-Grumet iliyopo Hifadhi ya Serengeti.

Aidha wakati Faru hao wakiwasili nchini, ilielezwa Faru mmoja alifariki akiwa Afrika Kusini wakati wa harakati za kuwasafirisha kuja nchini.

Hafla ya kuwapokea Faru hao ilihudhuriwa na viongozi mbalimabli wa Serikali wakiwamo Wakuu wa Mikoa ya Kilimanjaro Anna Mghwira na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Makamishna wa Uhifadhi wa Taasisi za TANAPA, TFS, NCAA na TAWA, Wenyeviti wa Bodi wa mashirika hayo na viongozi wengine.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano kati ya serikali na Mfuko wa Grumet, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu alisema, serikali itahakikisha inawalinda wanyama hao kwa gharama yeyote.

“Faru hawa tutawalinda kwa gharama zozote iwe za kisanyansi au kienyeji,” alisema Naibu Waziri Kanyasu.

Kwa upande Kamishna Uhifadhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), Dk. James Wakibara alisema wanyama hao walikuwapo muda mrefu

Kutoweka kwao ni kwasababu ya matatizo ya ujangiri, baada ya juhudi kubwa zinazofanywa na Wizara ya Maliasili hatua inayofuatana sasa ni kuanza kuwarudisha,” alisema Dk. Wakibara.

Kamishna Uhifadhi wa Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA Dk. Allan Kijazi alisema wamefarijika kupata Faru watakaoongeza idadi kwenye mfumo wa Ikolojia ya Serengeti.

Naye Kamishna Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dk. Fredy Manongi alisema kwa miaka mingi idadi ya Faru ilikuwa ikishuka Tanzania kwa hivyo mkakati uliowekwa mwaka huu ni kuongeza idadi ya Faru.

“Tunaamini mkakati wetu utafanikiwa kwa sababu nia ni kuongeza idadi ya Faru nchini,” alisema Dk. Manongi.

Serikali yawakamilisha mchakato wa kuwasomesha wataalam 100 wa Kilimo Israel

$
0
0

Serikali imekamilisha zoezi la kuwapeleka wataalam 100 wa kilimo nchini Israel kujifunza mbinu bora na teknolojia za kisasa za kuendeleza kilimo cha umwagiliaji nchini.

Akiongea na wataalam hao wakati wa hafla ya kuwaaga jana jioni, Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe alisema kuwa nafasi hizo za masomo ya kilimo nchini Israel zitatoa fursa kwa wataalam hao kuongeza ufanisi katika Sekta ya kilimo nchini na kukifanya kilimo kuwa na tija zaidi hapa nchini mara baada ya kukamilisha mafunzo hayo.

Aidha, Dkt. Mnyepe alibainisha kuwa, Tanzania na Israel wana uhusiano wa muda mrefu na umeendelea kuimarika siku hadi siku katika Sekta mbalimbali za kiuchumi na maendeleo nchini. Sekta hizo ni kama vile Kilimo, TEHAMA, Afya na mafunzo katika fani mbalimbali. Fursa za mafunzo zinazotolewa na nchi mbalimbali ikiwemo Israel zinasaidia kuongeza ujuzi kwa wataalam wetu nchini ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

"Kupitia uhusiano huo, tarehe 8 Novemba 2018, Rais Dkt. John Magufuli, alifanya mazungumzo na Mhe. Noah Gal Gendler, aliyekuwa Balozi wa Israel na baada ya mazungumzo hayo alitangaza kuwa Serikali ya Israel imeipatia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nafasi za mafunzo ya Kilimo yatakayofanyika nchini Israel kuanzia Septemba 2019 ambapo mara baada ya kutangazwa kwa fursa hizo Mhe Rais ilielekeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuratibu upatikanaji wa nafasi hizo" Alisema Dkt. Mnyepe

Aliongeza kuwa, zoezi la uratibu wa kupata nafasi hizo ilifanyika kwa ushirikiano wa karibu na Wizara za Sekta ya Kilimo na Mafunzo nchini pamoja na Wizara na Taasisi zinazohusika na masuala ya uendelezaji wa ujuzi kwa vijana kwa lengo la kutumia fursa ya mafunzo hayo kuongeza uzoefu na kuwa ni chachu ya kuchochea ajira  kwa vijana watakohitimu mafunzo hayo. Katika mchakato huo jumla ya wanafunzi 1440 waliomba nafasi hizo na kuchujwa hadi kufikia 100 ambao wameanza kusafiri kwenda nchini Israel.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana, Kazi na Ajira, Antony Mavunde aliwataka wataalamu hao kuhakikisha kuwa wanatumia mafunzo hayo vyema ili kuweza kupata na kuweza kuanzisha shughuli mbalimbali za kilimo watakaporejea nchini. 

"Kama mnavyofahamu, Israel ni moja ya mataifa yaliyopiga hatua kubwa ya Teknolojia katika Sekta ya Kilimo hivyo mafunzo haya ni fursa adhimu ya kuboresha sekta yetu ya kilimo ambayo ni muhimu katika uendelezaji wa viwanda. Ni matarajio ya serikali kuwa mafunzo haya yatawawezesha kuanzisha shughuli mbalimbali za Kilimo watakaporejea nchini, vinginevyo hakuna sababu ya ninyi kwenda" Alisema Mavunde. 

Aliongeza kuwa fursa hiyo ni hatua kubwa ambayo itapelekea kupata ujuzi ambao utapelekea mapinduzi ya kilimo nchini. Niwakumbushe tu kuwa, sekta ya kilimo ni sekta ambayo hutoa ajira nyingi sana ambapo huchangia asilimia 12 katika pato la taifa, 

"Ni matumaini ya serikali kuwa mtakuwa wataalam bora na wakuigwa katika matumizi ya ujuzi na uzoefu juu ya kilimo kwa maslahi ya taifa na kusaidia watanzania wengi zaidi,"Aliongeza Mavunde, huku akipongeza juhudi za Rais Magufuli ambazo alizofanya hadi kupatika kwa nafasi hizi za mafunzo. 

Mafunzo hayo hutolewa kwa vitendo kwa wanafunzi kutoka nchi zinazoendelea kama vile Asia, Amerika ya Kusini na Afrika ikiwemo Tanzania, ambao tayari wanamsingi wa elimu ya masuala ya Kilimo, kwa madhumuni ya kuwaongezea ujuzi katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji kama vile mbogamboga na matunda, mifugo, uongezaji thamani mazao, kutunza ubora, kutumia teknolojia ya kisasa kama vile umwagiliaji na usindikaji pamoja na ubunifu katika biashara ili kutumia vyema mnyororo wa thamani katika shughuli za kilimo. 
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana, Kazi na Ajira, Antony Mavunde akiongea na wataalam wa kilimo jijini Dar es Salaam jana kabla ya kuondoka kwenda Israel kwa mafunzo zaidi juu ya kilimo. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana, Kazi na Ajira, Antony Mavunde pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe wakiwakabidhi baadhi ya wataalamu hati za kusafiria.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images