Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

KAMATI YA USALAMA BARABARANI MOROGORO YAFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU WA CCM SHAKA OFISINI KWAKE

$
0
0
Kamati ya Usalama Barabarani mkoa wa Morogoro wamekutana na nakufanya mazungumzo na Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka ofisini kwake.

Kamati hiyo ikiongozwa Mwenyekiti wake Ndugu Johanes Kakiziba pamoja na mambo mengine waliwasisha mpango mkakati wao wa utekelezaji wao katika kipindi cha miezi sita ijayo.

“Sisi tuna makundi ya mjumuiko wa watu katika jamii, ili muweze kufanikisha majukumu wenu lazima sisi tuwe mabalozi wenu wazuri kwa vile mara nyingi hukutana nao katika shuhuli mbali mbali, vyengine kazi yenu itakuwa ngumu”

“Naelekewa zipo changamoto za usalama barabarani katika mkoa wetu Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Morogoro tuko pamoja na nanyi”

“Endeleeni nasi tutawaunga mkono ushauri wangu kwenu mipango yenu isishie kwenye makaratasi lazima mjipange vizuri katika usimamizi na utekelezaji wake, punguzeni urasimu wa kuwa mbioni kukamilika kila siku hatamfanikiwa na mwisho wa siku mtaonekana nanyi ni mizigo isiyobebeka mbele ya mamlaka hata wananchi” Shaka Hamdu Shaka.
Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro.

BAKWATA Waishukuru Serikali ya Mkoa kufanikisha kupata hati za viwanja vyao

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akimkabidhi hati za viwanja viwili vya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania vilivyopo Manispaa ya Sumbawanga Shekhe wa Mkoa Shekh Rashid Akilimali wakati wa hafla fupi ya Makabidiano hayo.
Picha ya pamoja ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (waliokaa katikati) pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Bernard Makali (wa pili Kutoka kulia) na Shekhe wa Mkoa Shekh Rashid Akilimali (wa pili toka Kushoto) Kamati ya Ulinzi na Usalam ya mkoa pamoja na viongozi wengine wa Wilaya na Halmashauri. 

……………………………………………………………………….

Shekhe wa Mkoa wa Rukwa Shekhe Rashid Akilimali amepongeza juhudi za serikali ya mkoa wa Rukwa chini ya mkuu wa mkoa huo Mh. Joachim Wangabo kwa kuweza kufanikisha kupatiwa viwanja viwili vyenye jumla ya ekari 18 vilivyopo katika Manispaa ya Sumbawanga baada ya kupita miaka 13 ya mgogoro baina ya Taasisi hiyo na uongozi wa serikali ya mkoa.

Amesema kuwa Serikali hii ya awamu ya tano ndio inayotakiwa kwani inawajali wanyonge na kuwapa haki wale wanaostahiki kupewa haki hiyo na kuongeza kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kweli anajua kuwateua watu wake na hakukosea kumteua Mh. Wangabo kuuongoza mkoa wa Rukwa

“Kwahiyo mheshimiwa nikushukuru kwa niaba ya waislamu wa mkoa wa Sumbawanga, hili linatoka Moyoni kwangu rasmi, miaka 13 leo tunakabidhiwa hati hizi, imetugonga mioyo, imeleta farka ya jamii, unapomchangisha sadaka mtu halafu isionekane imefanya kazi fulani anabaki anajenga hoja ambayo haipo, wewe ni mfano wa kuigwa kwa wakuu wa mikoa wengine kwa jambo hili, lakini nitakuwa mnyimi wa fadhila kutokumshukuru Mkurugenzi wa Manispaa, kijana Madhubuti kabisa huyu, amejitoa muhanga akasema ardhi hii ipo na mtapata lakini kwa usimamizia wako,” Alisisitiza

Aidha, Shekhe Akilimali alitumia nafasi hiyo kuiomba radhi serikali ya mkoa kwa niaba ya waislam wa mkoa huo katika eneo ambalo uongozi wa taasisi uliwakwaza katika kufuatilia hati hizo na kuonekana ni tatizo katika ofisi za serikali.

Kwa upande wake Mh. Wangabo alisema kuwa ni dhamana ya viongozi katika maeneo mbalimbali ya kiutawala kuhakikisha kuwa hakuna migogoro baina ya serikali na wananchi wanaoongozwa na kuongeza kuwa viongozi kwa namna yoyote ile ni lazima wawe tayari kuitatua migogoro hiyo kwasababu madhara yake ni makubwa na isiposhughulikiwa kwa wakati itapelekea kukosekana kwa utulivu na amani na hatimae maendeleo yanadumaa.

“Tnapotatua migogoro ya namna hii tunawezesha serikali kupita hatua za kimaendeleo pamoja na wananchi kwa ujumla wanapiga hatua za kimaendeleo, mgogoro huu wa viwanja umekuwepo tangu miaka hiyo ya 2006, miaka mingi sana lakini sasa leo tumekata mizizi ya fitina, tunaamini kabisa kwamba kuanzia sasa hivi tutakwenda kwa amani na utulivu na madhehebu ya dini zote sit u waislamu hata wakristo ambapo nao kulikuwa na mgogoro mzito tangu 1985 ambapo nao tumekwishautatua,” Alieleza.

Halikadhalika, Mh. Wangabo alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kufanya haraka katika kuwafikisha viongozi hao wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)katika maeneo hayo ambayo wamepatiwa hati ili waweze kutambua mipaka yao huku kukiwa na muwakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga.

Awali akitoa taarifa ya mgogoro huo Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Rukwa Ust. Mohamed Adam alisema kuwa kuna wakuu wa mikoa kadhaa ambao wamepita katika mkoa huo lakini hawakuweza kujaaliwa kuumaliza mgogoro huo ambao umemalizika leo tarehe 30.8.2019 na kusisitiza kuwa jambo hilo litabaki kuwa historia kwa waislamu wa Mkoa wa Rukwa.

“Sisi Waislamu wa Mkoa huu kwa jambo hili ulilolifanya tutaendelea kukumbuka katika maisha yetu yote na Mwenyezi Mungu akujaalie sana Mheshimiwa mkuu wa mkoa kwa alama hii uliyoiweka katika mji wetu,” Alisema.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mhe. Joachim Wangabo kwa niaba ya Serikali amekabidhi hati za Viwanja viwili vyenye namba 50074 na 50075 kwa Shekhe wa Mkoa Shekhe Rashid Akilimali kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Taasisi nunuzi zasisitizwa kujiunga na Mfumo wa manunuzi ya umma kwa njia ya Mtandao (TANePS)

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo akikabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo kwa mmoja wa washiriki
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo akiwahutubia washiriki wa mafunzo kuhusu matumizi ya mfumo wa TANePS yaliyofanyika jijini Arusha
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mafunzo kwa vitendo kuhusu matumizi ya mfumo wa TANePS .


Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imetoa wito kwa Taasisi nunuzi kuwaruhusu watumishi wa vitengo vya usimamizi wa manunuzi pamoja na mifumo ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kushiriki kwenye mafunzo kuhusu matumizi ya Mfumo wa Manunuzi ya Umma kwa njia ya Mtandao ili ziweze kuunganishwa na kufanya manunuzi yake kwa kutumia mfumo huo. 

Wito huo umetolewa jijini Arusha na Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo, alipokuwa akifunga mafunzo ya siku sita kuhusu matumizi ya Mfumo huo unaojulikana kwa jina TANePS (Tanzania National e-Procurement System) kwa maafisa 110 wa vitengo vya usimamizi wa manunuzi na Tehama kutoka Taasisi 44. 

Mhandisi Kapongo amezisisitiza Taasisi nunuzi kuhakikisha zinaunganishwa na kisha kufanya manunuzi yake kwa kutumia mfumo huo wa TANePS ili kukidhi matakwa ya sheria ya manunuzi ya umma pamoja na uamuzi wa Serikali kutaka taasisi zote za umma kuunganishwa na TANePS ili ziweze kufanya manunuzi yote kupitia mfumo huo kwa lengo la kurahisisha michakato ya manunuzi kufanyika kwa ufanisi na tija zaidi na kuhakikisha upatikanaji wa thamani halisi ya fedha. 

Amezitaja baadhi ya faida za mfumo wa TANePS unaosimamiwa na PPRA kuwa ni kupunguza gharama na muda kwenye michakato ya manunuzi serikalini pamoja na kuongeza uwazi, ushindani na usawa kwa wazabuni na watoa huduma wanaoshindania zabuni mbalimbali zinazotangazwa na Taasisi za Umma. 

“TANePS inawezesha mchakato wote wa manunuzi serikalini kufanyika kielektroniki ambapo hakutakuwa na sababu ya wazabuni kutumia muda mwingi kutembelea ofisi za Taasisi za Umma pale wanapotaka kushindania zabuni, pia hawawezi kukutana ana kwa ana na watumishi wa taasisi za umma kwa kuwa kila kitu kinafanyika mtandaoni,”alisema Mhandisi Kapongo. 

Aidha, Mhandisi Kapongo ametoa wito kwa wafanyabiashara, wazabuni na watoa huduma kuhakikisha wanajisajili kwenye mfumo huo ili waweze kushiriki au kushindania zabuni mbalimbali zinazotangazwa na taasisi za umma. 

Tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti, 2019, wataalamu kutoka PPRA wamepiga kambi jijini Arusha kwa ajili ya kutoa mafunzo kuhusu matumizi ya TANePS kwa awamu tofauti, programu inayotarajiwa kuwa endelevu ili kutoa fursa kwa wataalamu wa manunuzi kwenye taasisi zote za umma kupata fursa ya mafunzo hayo. Tangu kuanza kwa programu hii kabambe jumla ya watumishi 204 kutoka taasisi za umma 75 wameshapatiwa mafunzo hayo, ambapo wahusika wanapaswa kutembelea tovuti ya mfumo (www.taneps.go.tz) au tovuti ya PPRA (www.ppra.go.tz) ili kupata zaidi maelezo ya namna kujisajili kushiriki. 

Mafunzo haya yanagharamiwa na Serikali pamoja na ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).

RAIS DKT. MAGUFULI NA MKEWE JANETH WASHIRIKI MISA TAKATIFU DOMINIKA YA 22 MWAKA “C” KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA OYSTERBAY JIJINI DAR

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli, Mama Marry Majaliwa (Mke wa Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa) pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 22 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Dkt. Alista Makubi, Septemba 01,2019. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali  katika Misa Takatifu Dominika ya 22 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Dkt. Alista Makubi, Septemba 01,2019.



PICHA NA IKULU


"ADHABU ZA SHULENI NI ADHABU ZA UPENDO";PADRI JISO

$
0
0

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

“ADHABU mnazopewa shuleni ni adhabu za upendo, zinalenga kuwarekebisha ili akili ziweze kupokea maarifa mnayopewa na walimu na hatimaye muwe raia wema wenye uwezo wa kuztumikia taifa na jamii, tofauti na adhabu mtakazopewa baada ya kumaliza elimu, huko mitaani mtakutana na adhabu za chuki zinazotokana na maarifa kidogo mliyonayo.” Hayo ni maneno yaliyosemwa na Padri Jiso kutoka Mtakatifu Vincent wakati wa mahafali ya saba ya darasa la saba shule ya Carmel Convent iliyoko Vikindu, Wilayani Mkuranga

Padri Jiso ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo ambayo ni ya saba kufanyika katika shule hiyo, aliwaasa wanafunzi kuendeleza yale mema waliyojifunza katika kipindi cha miama saba waliyokuwa shuleni.

Alisema binadamu wametunukiwa zawadi kubwa na Mwenyezimungu ya kutumia maarifa na akili katika kuyatawala mazingira, licha ya kwamba sayansi inaonyesha miaka mingi ya nyuma binadamu ambaye yuko katika kundi la wanayama, na kama walivyo wanayama wengine aliishi porini.

“Lakini kutokana na upendo wa Mungu, alituongezea maarifa na vipaji mbalimbali vilivyotuwezesha kutawala mazingira kwa manufaa yetu na viumbe vingine ndio maana leo hii binadamu licha ya kutokuwa na maguvu kama walivyo wanyama wengine Tembo na Simba tumeweza kujenga majumba kuishi kwenye mazingira mazuri na yakliyo bora, kupata huduma za afya na elimu.” Alifafanua na kuongeza Tembo na mahguvu yake, Simba na magubvu yake wao bado wako pori ni na hawajabadilika kwa miaka yote hiyo.

Alitoa mfano wa ndege aitwaye Tai (Eagle) ambaye ana nguvu nyingi, kucha kali zenye uwezo wa kuchakura na kupokonya, mdomo wenye chongo kali na anakadiriwa kuishi hadi miaka 50, lakini watafiti wengi wanase kabla ya kufikisha miaka hiyo 50 Tai ama Eagle hufa kabla ya kufikisha umri huo kutokana na viungo vyake vinavyomuwezesha kupata chakula, kutishiwa nguvu hizo, kwani nkucha hupinda na hivyo hushindwa kupokonya na kuchakura vyakula, mdomo nao hupinda na hivyo uwezo wake wa kudonoa nao hupungua na hatimaye hufa kwa sababu hawezi tena kujitafutia chakula.

“Hii ndiyo tofauti ya wanyama wengine na binadamu kwani sisi tumejengewa maarifa kwa hivyo tunatumia maarifa hayo kutatua kero mbalimbali na hivyo kishi kwa furaha.” Alisema Padri Jiso.

Kwa kutumia mfano huo Padri Jiso alisema ndio maana watoto hujengewa msingi mzuri wa maarifa kwa kupatiwa elimu ili hatimaye baadaye waweze kutawala mazingira wanayoishi kwa kuwa wananachi wazuri na wenye faida kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Padri huyo aliwaonya wanafunzi hao kuwa lazima watambue, adhabu walizokuwa wanapata wakiwa shuleni ni adhabu za upendo zilizolenga kuwarekebisha ili kujaza maarifa kwenye vichwa vyao kwa faida ya baadaye na kwamba nje ya mazingira ya shule adhabu wataakazopata ni za “chuki” na hazina upendo wowote zaidi ya kuwuadhibi ili kuleta majuto.

Katika mahafali hayo pamoja na mambo mengine, wanafunzi walikabidhiwa vyeti (Living certificates) na kushuhudia burudani mbalimbali zilizoporomoshwa na wanafunzi wenzao.Mtihani wa taifa wa darasa la saba unatarajiwa kufanyika nchini kote kuanzia Septemba 11, 2019.
Mlulu Khalfan Said (kulia), akipokea cheti cha kuhitimu elimu ya msingi (Darasa la VII) kutoka kwa Padri Jiso kutoka Mtakatifu Vincent wakati wa sherehe za Mahafali ya Saba Shule ya Carmel Convent iliyoko Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani Agosti 31, 2019.

WAZEE WATAKIWA KUTOA NAFASI KWA VIJANA,KUACHA KUWATISHA NA KUWAZUIA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

WAZEE wametakiwa kutoa nafasi kwa vijana kugombea katika nafasi za uongozi, kuacha tabia ya kuwatisha na kuwazuia vijana ili kuwajengea msingi mzuri ikwemo kuwapima katika nafasi mbali mbali ili kuweza kujenga viongozi watakao ongoza kwa hekima na busara.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James Mkoani Kigoma wakati wa uzinduzi wa Oparesheni ya Kigoma ya Kijani , alisema Nchi inahitaji utayari wa vijana na uongozi wa vijana hivyo lazima wazeee wawaachie vijana kugombea na wasiwanyime nafasi iliwaweze kuwapima na kuwajengea weredi wa uongozi na busara kwa kipindi hiki ambacho bado kunawazee wenye busara iliwaweze kuwapa bisara hizo na waweze kubaki viongozi wazuri.

Alisema Vijana wakipewa nafasi kwa kipindi hiki ambacho bado kuna wazee wa kuwapima kutokana na busara zao namna gani ya kuongoza, itasaidia kutengeneza Taifa lenye uongozi ulio bora na unaozingatia misingi ya waasisis wa Taifa la Tanzania na kuepuka kuacha taifa la watu wanaofanya maamuzi bila kutumia busara.

Sambamba na hilo James aliwataka Wananchi wa mkoa wa Kigoma kuwapuuza wanasiasa wanaotumiwa na watu wa Nje kuivuruga Nchi, kwa kusema kwamba Tanzania kunamatatizo na hakuna kilichofanyika jambo ambalo sio kweli kwa kuwa mambo yaliyofanywa na Serikali iliypo madarakani yanaonekana .

Alisema Siasa hazifai kutweza juhudi zinazofanywa na serikali kwa maslahi ya Taifa letu hivyo wanasiasa wanatakiwa kujua kazi yao ni kukosoa pale jambo linapoonekana haliendi sawa na kupongeza pale serikali inapofanya vizuri na sio kutumiwa na watu wa Nje kuwakatisha tamaa viongozi wanaoifanya Nchi isongembele kwa kuwa uchumi ukikua ni wawatanzania wote na ajira zikipatikna ni kwa wote kwa kuwa nchi hii imejengwa kwa uzalendo na Usawa. 

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma, Amandus Nzamba alisema watajitahidi kutoa nafasi kwa vijana, ili na wao waweze kujifunza namna ya kuongoza na kuiletea nchi maemdeleo.

Aidha aliwaomba vijana kujitokeza kwa wingi kugombea uongozi kuanzia ngazi ya serikali za mitaa hadi uongozi wa juu, kwa kuwa vijana wengi wanaogopa kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali hivyo sasa ni wakati wao.

Nae katibu wa Umoja wa Vijana(UVCCM) kigoma Rashidi Semindu alisema Vijana Kigoma wamejipanga katika Chaguzi zinazokuja ikiwa ni pamoja na kulirudisha jimbo la kigoma mjini kwa chama cha mapinduzi na kuhakikisha vijana wote wanajitokeza na kupambana na upinzani kwa Mkoa wa Kigoma.

Alisema wamefanikiwa kuwarudisha kwenye chama cha mapinduzi vijana 82 wakiwemo waliokuwa Viongozi wa chama cha ACT wazarendo, wataendelea kuwashawishi Vijana kutokana na mambo Makubwa yanayofanywa na viongozi wa CCM Kwa kuleta maendeleo Tanzania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM)Taifa Kheri James pembeni ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kigoma Silvia Sigula akikaribishwa na Vijana wa umoja huo Mkoani kigoma jana.

IGP SIRRO: WANANCHI WASHIRIKIANE NA JESHI LA POLISI KUDHIBITI MAUAJI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amemuagiza kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora kuhakikisha anashirikiana na wananchi katika kudhibiti vitendo vya mauaji yanayotokana na imani za ushirikina, ubakaji pamoja na uhalifu wa uvunjaji. 

IGP Sirro amesema hayo wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi katika wilaya za Igunga na Nzega mkoani humo ziara yenye lengo la kuona utayari wa askari Polisi wakati wanapotekeleza majukumu yao. 

Aidha, IGP Sirro amesema kuwa, ni vyema pia viongozi wa kidini na wa kisiasa kuzungumzia madhara ya mauji na uvunjaji katika maeneo yao.

KATIBU MKUU UVCCM TAIFA AZINDUA KONGAMANO LA MTWARA YA KIJANI KWA KISHINDO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala leo amezindua rasmi Kongamano ya Mtwara ya Kijani lililofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Mkoa wa Mtwara.

Akizungumza na Maelfu ya Wananchi waliohudhuria Ufunguzi huo Katibu Mkuu Mwl Mwangwala amewataka Kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi kwani ndio Chama pekee kisichokuwa na Misingi ya Kiubaguzi wa Matabaka mbalimbali.

Pia, Katibu Mkuu Ndugu Mwl Raymond Mwangwala akizungumza katika Mkutano huo ametuma salama kwa Viongozi mbalimbali wa Vyama vya Upinzani kujiandaa kuachia ngazi kwani hakuna mwananchi wa sasa atakae acha kuipigia kura CCM kutokana na kasi ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Aidha, Ndg Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa amewapongeza Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Mkoa wa Mtwara kwa Kazi kubwa wanayoifanya ya kuendelea kuwa karibu na kuwasaidia Vijana wote wa Mkoa huo kuendelea kutatua Changamoto zao kwa kutimiza moja ya lengo la kuundwa kwa  jumuiya hiyo.

Akizungumza awali akimkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara Ndugu Yusuph Nanila amemuhakikishia mgeni rasmi hali ya Kisiasa ya Chama na Serikali Mkoa wa Mtwara ipo vizuri na kutumia fursa hiyo kuwapongeza Watumishi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe Gelasius Byakanwa  kwa kuendelea kuwatumikia Wananchi kwa Haki na Usawa.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala akiwasili katika uwanja wa Uwanja wa Nangwanda Mkoa wa Mtwara kuzindua rasmi Kongamano la Mtwara ya Kijani . 
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala akizungumza mbele ya Wananchi waliohudhuria Ufunguzi huo 



Mbunge Kingu aunga mkono kampeni ya kuhamasisha Taifa Stars

$
0
0
Mbunge wa Singida Magharibi, Mhe Elibariki Kingu ameupokea msafara wa kundi la waandishi wa habari wanaoenda nchini Burundi kuiunga mkono Timu ya Taifa 'Taifa Stars' katika mchezo wake wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Mhe Kingu pamoja na kuupokea msafara huo wenye watu 35 pia ameuandaliwa kifungua kinywa pamoja na kuchangia kiasi cha Shilingi Laki Mbili kama sehemu ya kuunga mkono kampeni hiyo ya kuhamasisha Timu ya Taifa.

" Niwashukuru Sana ndugu zangu wanahabari kwa kuamua kujitolea kuunga mkono Timu yetu ya Taifa. Historia lazima iwakumbuke mmefanya jambo ambalo halijawahi kufanywa hapo awali. Nyinyi ni mashujaaa wa Taifa hili.

" Niwahikikishie Mimi ni sehemu ya kampeni yenu, nitashirikiana nanyi kwa kila Jambo, lengo likiwa kumuunga mkono Rais wetu Dk John Magufuli kupitia Michezo na haswa Timu yetu ya Taifa. Twendeni pamoja.," Amesema Mhe Kingu.

Kampeni hiyo ambayo imeandaliwa na wandishi wa habari za michezo na ilianza katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN, dhidi ya Kenya ambapo Taifa Stars ilifuzu kwenda hatua inayofuata.

LUKUVI ATAKA MARC KUHARAKISHA UANZISHAJI OFISI ZA ARDHI ZA MIKOA

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitekeleza majukumu katika gari yake wakati wa ziara yake mkoani Tanga mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shighela, wa tatu kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daud Mayeji na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Idara ya Mipago Miji Ofisi ya Ardhi Kanda ya Kaskazini Nickson Mjema (Kulia).(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shighela (Kushoto) wakati akikagua moja ya itakayokuwa ofisi ya Ardhi mkoa wa Tanga wakati ziara yake katika mkoa huo mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daud Mayeji.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mipago Miji Ofisi ya Ardhi Kanda ya Kaskazini Nickson Mjema (Kulia) wakati akikagua moja ya sehemu ya kuhifadhia nyaraka za ardhi wakati akikagua inayotarajiwa kuwa ofisi ya ardhi mkoa wa Tanga akiwa katika ziara yake mkoani humo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shighela.
………………………………………………………

Na Munir Shemweta, WANMM TANGA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka Wakuu wa mikoa nchini kuhakikisha wanaharakisha uanzishwaji Ofisi za Ardhi za mikoa ili kusaidia upatikanaji huduma za ardhi katika mikoa hiyo.

Lukuvi alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki mkoani Tanga wakati alipokagua ofisi zinazotarajiwa kuwa za ardhi katika mkoa huo ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilolitoa la kuanzisha ofisi za ardhi kila mkoa kwa ajili ya kusogeza huduma za ardhi kwa wananchi.

Katika Mkutano wa Wataalamu wa sekta ya ardhi uliofanyika hivi karibuni jijini Dodoma Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitangaza kuanzisha ofisi za ardhi katika kila mkoa ili kurahisisha huduma za sekta hiyo ambapo sasa zinapatikana katika Kanda tisa ikiwemo ile Maalum ya Morogoro.

Lukuvi alisema, uharakishwaji uanzishaji ofisi za ardhi katika mikoa utasaidia wananchi kupata huduma za ardhi katika mikoa yao tofauti za sasa ambapo hulazimu baadhi yao kutembea umbali mrefu kufuatilia nyaraka ofisi za kanda jambo aliloeleza linawakatisha tamaa.

Alimpongeza mkuu wa Tanga Martine Shighela kwa kuwa Mkuu wa mkoa wa kwanza kukubali na kupokea agizo la kuanzishwa ofisi hizo za ardhi mapema kwa lengo la kuhakikisha migogoro ya ardhi inaondolewa katika mkoa wake.

Alisema, pamoja na uwepo ofisi za Kanda ambazo baadhi yake zinahudumia zaidi ya mikoa miwili lakini kero kwa wananchi kuhusiana na masuala ya ardhi zinaendelea ndiyo maana Wizara yake imeona ianzishe ofisi za mikoa zitakazokuwa zikitoa huduma kama zile zinazotolewa katika kanda.

Alizitaja huduma hizo kuwa ni Upimaji, Uthamini, Mipango Miji, Usajili na Utoaji Hati za ardhi aliloueleza kuwa ulikuwa ukipatikana ofisi za kanda pekee jambo lililokuwa likiwalazimu wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo na kufafanua kuwa, uwepo ofisi za mikoa utaongeza ari ya wananchi kuchukua hati kutokana na ukaribu wa ofisi.

‘’Mtu atoke Korogwe afuate hati Moshi, trend ya kuchukua hati inapungua kutokana na umbali maana maeneo mengine mtu anavuka mikoa miwili kwenda kuifuata Hati na Kamishna aliyeko Moshi ni vigumu kusimamia mikoa iliyo mbali’’ alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, binafsi alitaka mikoa yote 26 kuanzisha ofisi za ardhi za mikoa kufikia Oktoba mwaka huu na Hati zitolewe katika mikoa hiyo jambo alilolieleza kuwa litapunguza kero na kuongeza wigo mpana wa makusanyao ya kodi ya pango la ardhi.

Lukuvi alibainisha kuwa, baada ya kuanzishwa ofisi za mikoa sasa ramani zote na historia ya masuala ya ardhi katika mikoa husika zitarudi katika ofisi hizo na Wakuu wa Mikoa hawatakosa msaada katika masuala ya ardhi kwa kuwa watalaamu wa ardhi watakuwa wakifanya kazi chini yao.

Kabla ya kukagua ofisi hizo Waziri Lukuvi alielezwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shighela kuwa, mkoa wake ulipokea kwa shauku kubwa uamuzi wa Serikali kuanzisha ofisi za ardhi katika mikoa na tayari umeshatenga ofisi hizo kwa ajili ya kuanza kazi ili kupunguza migogoro ya ardhi pamoja na kusogeza huduma karibu kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daud Mayeji alisema, uanzishwaji ofisi ya ardhi katika mkoa wa Tanga utausaidia sana mkoa huo kwa kuwa wamekuwa wakitumia muda mwingi kushughulika na masuala ya ardhi na hufanya zaidi ya safari 50 katika kipindi cha miezi mitatu kufuata huduma ya ardhi katika ofisi za kanda zilizoko Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Jiji la Tanga, uwepo wa ofisi za Ardhi za Mikoa itakuwa rahisi kwa jiji lake kushughulika na masuala mengine badala ya kujikita katika ardhi pekee suala alilolieleza lilikuwa likichukua muda mwingi.

KALEMANI AAGIZA MSIMAMIZI WA REA AONDOLEWE

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani, akipeana mikono na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Idunda wilayani Ulanga mkoani Morogoro mara baada ya kuwapa kifaa cha Umeme Tayari ( UMETA).
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani ( kushoto) na akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Ngolo Malenya,Waziri alifika wilayani hapo kuwasha umeme na kukagua utekelezaji wa REA awamu ya tatu, mzunguko wa kwanza.
Baadhi ya akina mama wa kijiji cha Makanga wakifurahia jambo, wakati Waziri wa Nishati ,Dkt.Medard Kalemani ( hayupo pichani)akizungumza kuhusu kuwasha umeme wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza katika kijiji chao. 






Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani,( kushoto) akizungumza na wanakijiji wa Kijiji cha Makanga( hawapo pichani) mara baada ya kuwasha umeme wa REA Awamu ya tatu mzunguko wa kwanza, kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Ulanga , Ngolo Malenya.

Baadhi ya wanakijiji wa Idunda wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alipofika kijijini hapo kuwasha umeme wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza.
………………………………………………..

Na Zuena Msuya, Morogoro,

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, ameagiza Afisa aliyekuwa akisimimamia Mradi wa Umeme Vijijini (REA), Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Seif Abdallah, aondolewe kwenye nafasi hiyo kutokana na utendaji kazi usioridhisha.

Aidha Dkt. Kalemani ametoa siku 20, kwa Kampuni ya Ukandarasi ya State Grid inayotekeleza mradi huo kuwasha umeme katika vijiji vya Wilaya ya Ulanga la sivyo atakatwa asilimia kumi ya malipo yake kutokana na kazi hiyo.

Dkt.Kalemani alitoa kauli hiyo Agosti 31,2019, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa REA na kuwasha umeme katika Vijiji vya Makanga na Idunda wilayani Ulanga, mkoani Morogoro.

Waziri wa Nishati alifikia hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na usimamizi unaofanywa na mhandisi huyo kutoka Wakala wa Nishati Vijiji ( REA) pamoja na utekelezaji wa mradi usioridhisha.

“Huyu Mhandisi Seif Abdallah, utendaji wake wa kazi hauridhishi kabisa, hayupo katika maeneo ya kazi yanayotekelezwa mradi, anamuacha mkandarasi afanye kazi anavyojitakia yeye mwenyewe hakuna usimamizi wowote, ninamuagiza Mkurugenzi wa REA amuondoe huyu mhandisi hafai kuwa msimamizi”,alisisitiza Dkt.Kalemani.

Katika hatua nyingine, Dkt.Kalemani alitoa siku 20 kuanzia, Septemba 1 hadi 20, 2019 kwa kampuni ya ukarandari ya State Grid kuwasha umeme katika vitongoji vinne kabla ya kukamilisha Mradi wa REA awamu ya tatu, mzunguko wa kwanza unaotarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu nchini kote.



Alifafanua kuwa, utekelezaji wa Mradi wa REA awamu ya tatu umegawanyika katika mizunguko miwili ambayo ni mzunguko wa kwanza ulioanza kutekelezwa mwezi Juni, 2019 na utakamilika Desemba mwaka huu.

Aidha mzunguko wa pili wa REA awamu ya tatu unatarajiwa kuanza mwezi Januari na kukamilika mwezi Juni ,2020, hivyo alimtaka kila mkandarasi aliyepew kazi ya kutekeleza mradi huo ahakikishe anakamilisha mzunguko wa kwanza wa kazi yake kwa mujibu wa makubaliano ya mikataba na sheria.

Alisisitiza kuwa haridhishwi na hatua ya utekelezaji wa mradi huo katika Mkoa wa Morogoro ambao mpaka sasa umefikia asilimia 56 tu ya utekelezaji wake ambao hauendani na kasi ya utekelezaji wa mradi huo.

Sambamba na hilo alimtaka mkandarasi huyo,kuongeza nguvu kazi ya makundi ya vijana ili kuharakisha shughuli za utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza kama ilivyoelekezwa katika mkataba wa kazi hiyo.

“Sitakubali kukwamishwa na ninyi State Grid katika utekelezaji wa mradi huu kwa kuwa mnafanya kazi kwa kusuasua sana kasi yenu hairidhishi kabisa, na nyie ndiyo mko nyuma kabisa katika kasi ya kutekeleza mradi wa huu REA awamu ya tatu, mzunguko wa kwanza ikilinganishwa na wakandarasi wote wanaotekeleza miradi hii nchini, kama hamtatimiza makubaliano ya mkataba, tutawakata asilimia 10 ya malipo yenu”, alisema Dk.Kalemani.

Hata hivyo, Dkt.Kalemani alirejea kauli yake ya kuwataka wananchi kuwa wasinunue miundombinu ya umeme kama vile nguzo, pamoja Luku kwa kuwa vifaa hivyo vinatolewa bure kwa kila mwananchi aliyepitiwa mradi wa umeme vijijini.

Pia aliwataka wananchi kutumia umeme kwa faida kama vile kuongeza thamani ya mazao kwa kufanya usindikaji wa mazao yao ili kujiletea maendeleo zaidi.

Serikali imetenga shilingi Bilioni 42 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa REA awamu ya tatu, mzunguko wa kwanza kwa Mkoa wa Morogoro.

KATIBU MKUU MWAKALINGA ATOA ONYO KWA WATENDAJI WA MIZANI NCHINI

$
0
0
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Eng. Matari Masige, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, wakati alipowasili mkoani humo kwa ajili ya ukaguzi wa barabara, madaraja na mizani.Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akipita juu ya Daraja la Msingi lililopo sasa wakati alipokuwa akikagua hatua za ujenzi wa Daraja jipya la Msingi litakalokuwa na urefu wa mita 75 na barabara unganishi za KM 1 kwa kiwango cha lami, mkoani Singida.Mkandarasi Mzawa wa kampuni ya M/s Gemen, Eng. Eradius Raphael, akimwonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, mchoro wa Daraja jipya la Msingi litakalokuwa na urefu wa mita 75 na barabara unganishi za KM 1 kwa kiwango cha lami, mkoani Singida.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Bw. Emmanuel Magandi, ambaye ni Msimamizi wa Mzani wa Nala wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mizani hiyo, jijini Dodoma.Mtaalam wa Mzani wa Nala Bw. Noel Gabriel, akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, kuhusu mfumo wa namna ya upimaji wa uzito wa magari katika mizani hiyo, wakati Katibu Mkuu huyo alipokagua utendaji kazi wake, jijini Dodoma.Gari likipima uzito katika mzani wa Njuki uliopo katika barabara ya Singida – Shelui, mkoani Singida. Mzani huo ni moja kati ya mizani mitatu iliyopo mkoani humo ambapo mizani mingine ni Mzani wa Itigi katika barabara ya Manyoni – Itigi – Chaya na Mzani wa Mughamo katika barabara ya Singida – Babati.


……………………
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, amekemea vikali vitendo vya rushwa kwa watendaji wote wanaosimamia mizani hapa nchini na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayehusika.

Kauli hiyo ametoa mjini Dodoma wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua hali ya miundombinu ya barabara, madaraja, mizani, Magari na Mitambo ya Serikali ambapo alianzia mkoani humo katika mzani wa Nala na kusisitiza kwa wafanyakazi wa mizani kuacha kucheza na mizani, kupokea rushwa na kuzembea kazini.

“Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwani barabara nyingi zinaharibika kutokana na kubeba mizigo mizito na nyie watu wa mizani hamfanyi kazi yenu kikamilifu”, amesisitiza Arch. Mwakalinga.

Arch. Mwakalinga, amesema elimu elekezi itatolewa kwa wafanyakazi wa ngazi zote hata maaskari wanaolinda katika mizani ili kuepusha vitendo vya rushwa na kuingizia gharama kubwa Serikali.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo amekagua mzani wa Njuki uliopo mkoani Singida ambapo Serikali iliamua kujenga mzani huo wa kupima uzito wa magari katika mwendo (Weigh in Motion) ili kupunguza tatizo la msururu mrefu wa magari wakati wa kupima uzito na kuagiza kupatiwa taarifa ya utendaji wa mzani huo kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) wa mkoani humo.

Aidha, amekagua ujenzi wa daraja jipya la Msingi lenye urefu wa mita 75 na barabara za maingilio zenye urefu wa KM 1 kwa kiwango cha lami linalojengwa na mkandarasi mzawa Gemen Engineering na kusimamiwa na Kitengo cha TECU kwa gharama ya shilingi bilioni tisa na kumtaka mkandarasi huyo kuongeza kasi ya ujenzi kabla ya majira ya mvua kuanza.

Kwa upande wake Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida Eng. Matari Masige, amemueleza Katibu Mkuu huyo kuwa ujenzi wa daraja hili utakamilika kwa muda wa miezi 24 na mkandarasi yupo katika hatua za awali za kuandaa msingi wa daraja na kuahidi kuusimamia kwa ukaribu mradi huo ambao una miezi mitatu toka kuanza kwake.

Ameongeza kuwa daraja hilo likikamilika litaunganisha wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida na Wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu na hivyo kuendelea kufungua mtandao wa barabara kwa kiwango cha lami hapa nchini.

Kuhusu miradi mingine ya kitaifa ya ujenzi Eng. Masige, ameendelea kumueleza Katibu Mkuu huyo kuwa ujenzi wa daraja la Sibiti umekamilika na magari yanapita juu ya daraja na wananchi walioathiriwa na mradi washalipwa fidia wote na hakuna mwananchi yeyote anayedai fidia.



Ujenzi wa Daraja la Msingi ni ahadi ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wananchi wa wilaya ya Mkalama na wilaya jirani na likikamilika litapunguza umbali wa safari kwa watu wanaoelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa.

WAZIRI LUGOLA AAGIZA BODABODA ZOTE ZISAJILIWE NCHINI, AWATAKA TRAFIKI KUACHA VISINGIZIO UGUMU UKUSANYAJI FAINI BARABARANI ZINAPOFANYA MAKOSA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akimsikiliza Katibu wa Chama cha Wamiliki na Waendesha Bajaj na Bodaboda Mkoa wa Kilimanjaro (CWBK), Rashid Omary, alipokuwa anatoa pongezi kwa Waziri huyo, kuwasaidia kupata eneo la maegesho ya Bajaj na Bodaboda Shairifu, Mjini Moshi, leo. Mwezi uliopita, Lugola alitatua mgogoro uliopo kati ya Manispaa ya Moshi na CWBK kuhusiana na maeneo ya maegesho. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Khamis Issa, na wapili kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani humo, Zauda Mohammed. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (aliyevaa Kaunda suti), akikagua eneo la maegesho ya Bodaboda na Bajaj, Sharifu, Mjini Moshi, leo. Lugola aliambatana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Khamis Issa (kulia), kukagua maeneo ya Aghakan na Shairifu ambalo lilileta mgogoro kati ya Manispaa ya Moshi na Chama cha Wamiliki na Waendesha Bajaj na Bajaj Mkoani humo (CWBK), na kutatuliwa na Waziri huyo mwezi uliopita, mjini humo. Wapili kushoto ni Katibu wa CWBK, Rashid Omary. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimuaga Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki na Waendesha Bajaj na Bodaboda Mkoa wa Kilimanjaro (CWBK), Rashid Omary, mara baada ya kumaliza kukagua vituo vya Sharif una Aghakan vya maegesho ya Bodaboda na Bajaj, Mjini Moshi, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimuaga Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro, Zauda Mohammed (kushoto), mara baada ya Waziri huyo, kumaliza kukagua vituo vya Sharif una Aghakan vya maegesho ya Bodaboda na Bajaj, Mjini Moshi, leo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa huo, Khamis Issa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

…………………………………………………..

Na Felix Mwagara, Moshi (MOHA).

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelitaka Jeshi la Polisi Kikosi Usalama Barabarani washirikiane na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuzisajili bodaboda na bajaj zote nchini ili ziweze kudhibitiwa katika ukusanyaji wa faini pamoja na matukio mbalimbali ya kiuhalifu zinapofanya makosa.

Lugola alisema ushirikiano kati ya viongozi au askari waliopo chini ya halmashauri nchini ipo ndani ya sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi Sura namba 322, hivyo Jeshi lake linapaswa kushirikiana na Polisi Wasaidizi waliopo chini ya halmashauri ya Miji, Wilaya, Manispaa na Jiji kwa mujibu wa sheria. 

Waziri Lugola ameyasema hayo Mjini Moshi, leo, wakati alipokuwa anakagua vituo vya bodaboda na bajaj mjini humo ambapo mwezi uliopita alifanya mkutano na wamiliki na waendesha bodaboda na bajaj mkoani humo kwa lengo la kutatua migogoro mbalimbali waliokuwa wanailalamikia Manispaa ya Moshi kuwanyanyasa pamoja na kuwafukuza kuegesha kituo cha Sharif una Aghakan mjini humo ambapo Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabara Mkoani humo aliwaelekeza wawepo katika eneo hilo. 

“Askari wa usalama barabarani, muache visingizio kuwa ukamataji wa bodaboda ni mgumu hasa mnapowaandikia makosa walipe baada ya siku saba, mara usingizia bodaboda hazipo katika mfumo wa TRA kama magari, tukiziachia tuzipate wapi, nilishawaelekeza mshirikiane na viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijijini, Miji, Manispaa na Jiji kuanzisha kanzi data, kwenye mfumo wa kuwasajili waendesha bodaboda wote sehemu mbalimbali nchini, na taarifa za bodaboda hizo endapo zinafanya makosa inakua rahisi kuzikamata kwasababu zipo kwenye mfumo,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, lengo la usajili wa bodaboda huo, ni kutokana na kuepuka kuzikamata hovyo na kuziweka vituoni jambo ambalo analipinga kuepusha mlundikano wa boaboda vituoni na pia kuwasababishia bodaboda hao kuwaongezea umaskini zaidi.

“Naomba niendelee kurudia tena agizo hili, bodaboda zinazopaswa kuwepo vituo vya polisi ni za aina tatu, moja bodaboda zilizotumika katika matukio ya uhalifu, mbili zilizohusika katika ajali, na tatu bodaboda zilizookotwa, mbali na makundi hayo zinapaswa kulipwa faini,” alisema Lugola. 

Pia Lugola aliwataka baadhi askari na wananchi kuacha tabia ya kuwatuhumu viongozi wanapowatetea waendesha bodaboda wanaambiwa kuwa wanasiasa ndiyo wanasababisha ajali kuongezeka.

Amesema kauli hiyo sio sahihi, kwani wanaosababisha ajali asilimia 76 kwa mujibu wa utafiti wa ajali zinazotokea barabarani zinasababishwa na makosa ya wanadamu na sio bajaj na bodaboda peke yao, na asilimia 24 za ajali zinatokea zinasababishwa na ubovu wa miundombinu.

“Kumekuwa na dhana potofu kwamba wanasiasa kama mimi tunasababisha ajali za bodaboda, kwasababu tunawatumia bodaboda kwa mgongo wa siasa, sasa nataka niwaambie, wanaosababisha ajali barabarani ni asilimia 76 ni makosa ya wanadamu ambao ni wanadamu watembea kwa miguu, waendesha baiskeli, wenye mikokoteni, wanafuga mifugo barabarani na madereva ndio wanasababisha ajali, na sio bodaboda wala bajaj peke yao,” alisema Lugola.

Lugola amesema hakuna mahali popote ambayo tumesema baodaboda wakifanya makosa wasikamatwe, tunachosema na kusimamia nikupunguza umaskini kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo inaelekeza Bodaboda na Bajaj wafanye biashara ili wapunguze umaskini. 

Aidha, Lugola amesema Serikali ya Magufuli inataka wananchi Watanzania wajiajiri hivyo sekta ya bodaboda lazima iheshimika kwakua nao wanatafuta ridhiki kama ilivyo kwa watanzania wengine.

KAMATI ZA CHAMA CHA WABUNGE CPA KANDA YA AFRIKA ZAKUTANA MJINI ZANZIBAR

$
0
0
Mhe. Job Ndugai na Katibu wa CPA Kanda ya Afrika, Ndg. Stephen Kagaigai
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati ya Marekebisho ya Sheria Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika walipokaa leo Septemba 1, 2019 katika hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa Mjini Zanzibar. Kushoto ni Mjumbe wa kamati na Naibu Spika wa Bunge la Afrika ya kusini, Mhe. Lechesa Tsenoli na Mwenyekiti wa kamati ya Wawakilishi wa Kanda Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, Mhe. Bernard Sibalatani 






Wajumbe Kamati ya Wawakilishi wa Kanda Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Bernard Sibalatani (katikati) wakati wa kikao kilichofanyika leo Septemba 1, 2019 katika hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa kamati ya Fedha na Mipango Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola (CPA) Kanda ya Afrika, Mhe. Elijah Okupa (katikati) akiongoza kikao hicho kilichofanyika leo Septemba 1, 2019 katika hoteli ya Madinat Al Bahr Mjini Zanzibar. Kushoto ni Spika wa Bunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bodi ya Kampuni ya uwekezaji CPA Kanda ya Afrika


WATAALAMU WA CHAKULA WANAJUKUMU KUBWA LA KUTUMIA UMAHIRI NA WELEDI WAO KUSAIDIA JAMII - JAMES NDEGE

$
0
0
Mgeni Rasmi,Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Wakutubi Tanzania (TLA), Bw. James Ndege, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Wahitimu wa shahada ya sayansi na teknolojia ya chakula, leo Katika ukumbi wa kitivo cha historia, Chuo Kikuu cha Dar es salaam.amabpo mesema wataalamu wazalendo wa chakula, wanajukumu kubwa la kutumia umahiri na weledi wao kusaidia jamii na kutatua changamoto mbalimbali za kijakijamii. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Wahitimu wa Shahada ya Sayansi na Teknolojia ya Chakula,Bw.Jasson Kyaruzi,akisoma hotuba yake katika ufunguzi wa kongamano hilo lilifanyika Katika ukumbi wa kitivo cha historia, Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakiwa makini kumsikiliza Mgeni Rasmi,Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Wakutubi Tanzania (TLA), Bw. James Ndege,
Mgeni Rasmi,Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Wakutubi Tanzania (TLA), Bw. James Ndege,(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

MBUNGE WA JIMBO LA SAME MAGHARIBI AJA NA STAIL MPYA YA KUTATUA KERO ZA WANANCHI PAPO KWA PAPO

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Dkt. Mathayo David Mathayo ameendelea na ziara yake ya kutekeleza ilani ya uchaguzi katika jimbo lake huku akija na staili mpya ya kutatua kero za wananchi kwa mtindo wa papo kwa papo.

Licha ya kutekeleza ahadi alizoahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa Same Magharibi mbunge huyo amekuwa akitekeleza wakati mwingine kutoa fedha taslim  pale anapoombwa na wananchi wa kata husika nje ya ahadi anazotekeleza katika kila kata.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Vudee na Bangalala mbele ya mbunge huyo diwani wa Kata hiyo Ngomoi Ntarishwa pamoja na kumshukuru mbunge huyo kwa utekelezaji wa ahadi zote alizoahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza wanachi hao.
“mhe mbunge wananchi wa Vudee wanakushukuru sana kwa utekelezaji wa ahadi uliahidi na umetekeleza,sisi wanannchi wa Vudee tuna Imani kubwa na wewe hivyo pamoja na kuwa umetelekeza bado tuna changamoto kadhaa ambazo tunaomba pia utusaidie”alisema Ntarishwa

Mbunge huyo ambae licha ya kutekeleza ahadi za mabilioni amekuwa akipandwa na mzuka pale wananchi wake wanapomlilia shida na kuhakikisha hawaachi hivyo hivyo wala kuahidi bali amekuwa akizitatua papo kwa papo.

Ndugu zangu leo nimekuja kutekeleza ahadi zote nilizoahidi wakati nilipokuja kuwashukuru kwa ushindi wa kishindo ambao mlinichagua,lakini nasikia kuna watu wanapitapita wakisema kuwa Mathayo hajarudi,hivi niwaulize swali ilani inatekelezwa ndani ya kipindi gani,si ni kwa miaka mitano?hivi mtoto akiaanza shule akafika kidato cha pili utasema basi kabla hajafika kidato cha nne?
Mathayo amewataka wananchi hao  kutokubali kurubuniwa na kuendelea kuwa na Imani na chama cha mapinduzi ambacho kupitia Rais John Magufuli kimeleta maendeleo makubwa kwa wananchi wake tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani.

Akiwa katika kata ya Vudee na Bangalala mbunge huyo ametekeleza ahadi zake kwa kutoa mifuko ya fedha taslimu saruji  350 kwa ajili ya ujenzi wa shule,zahanati,vyoo vya wanafunzi,,mabomba ya maji,mabati 200,matanki ya maji,comyuta,mashine za photokopi,mipira ya kuchezea,key bord,nondo,meza na viti,huku akiahidi kuleta katapila kwa ajili ya ujenzi wa barabara korofi ya Kisesa,vyote kwa ajili ya kata ya Vudee.

Baadhi ya ahadi mpya alizozitoa na kuzitatua papo kwa papo katika kata ya Vudee ni kompyuta,mashine ya photokopi,jiko la shule ya sekondari masheka,mabati 30,na upande wa zahanati ya kiji cha kisesa bati 100.

Ombi jingine alilolitekeleza papo kwa papo katika kata ya Bangalala ni kukubali kutoa gari la kubebea wagonjwa kwa ajili ya kata hiyo, kuleta katapila kwa ajili ya kutengeneza barabara za kata hiyo,tenki la kuhifadhia maji,ambapo pia ametoa fedha taslimkwa ajili ya kunua mipira ya maji 20 na nyinginezo.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi dr.Mathayo David Mathayo akimkabidhi diwani wa kata ya Bangalala George Mshana mipira kwa ajili ya ligi itakayoshindanisha vijiji vyote ambapo mshindi kwa upande wa wanawake atapatiwa shilingi milioni mbili na wanaume timu mshindi atapatiwa shilingi milioni mbili wakati wa mkuatano wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya utekelezaji wailani ya uchguzi ya CCM mwaka 2015-2020 kama alivyoahidi kwa jailia ya kata hiyo.


Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Mathayo David Mathayo akikabidhi Mabati 200 na mifuko ya saruji kwa uongozi wa kata ya Vudee kama alivyoahidi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na zahanati ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi yam waka 2015-2020 mbele ya wananchi wa kata hiyo.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi dr.Mathayo David Mathayo akimkabidhi fedha taslim diwani wa kata ya Bangalala George Mshana mbele ya wananchi wa kata hiyo wakati wa mkuatano wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya utekelezaji wailani ya uchguzi ya CCM mwaka 2015-2020 kama alivyoahidi kwa jailia ya kata hiyo.

IDARA YA UHAMIAJI YATAKIWA KUJIIMARISHA KATIKA KUVUTIA WAWEKEZAJI NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Kangi Lugola ameitaka Idara ya Uhamiaji kuimarisha uwekezaji nchini. Wito huo umetolewa leo Mjini Moshi wakati akifungua Mkutano wa Maafisa Uhamiaji Waandamizi  unao lenga kujadili na kutathmini utendaji kazi wa Idara ya Uhamiaji.

 Akizungumza na Maafisa hao, Waziri Lugola amesisitiza kuwa nchi yetu inazo fursa nyingi za kiuchumi na Utalii hivyo kuwavutia wageni na wawekezaji wengi kuiingia na kuwekeza nchini.

“Katika utendaji kazi wake,Idara ya uhamiaji ndio kioo/taswira ya nchi yetu hivyo  tufanye kazi kwa weledi na kuweka mazingira bora ya uwekezaji na kuwahudumia wageni kwa ukarimu, lugha za staha na msiwe kikwazo cha uwekezaji na utalii nchini” alisema Waziri Lugola.

Aidha, Waziri Lugola amemuagiza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kusimamia kikamilifu Ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali na kudhibiti mianya inayopelekea upotevu wa maduhuli.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjro, Mhe. Anna Mghwira ametoa wito kwa Idara ya Uhamiaji kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji na utoaji wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

“Mkoa wa Kilimanjaro una idadi kubwa ya Wahamiaji haramu kutokana na jiografia yake pamoja na kuwepo kwa fursa mbalimbali za uwekezaji na utalii. Ili kukabiliana na changamoto hii, Idara iimarishe udhibiti wa mipaka ya nchi yetu ikiwa ni sambamba na kuwatambua Watanzania na raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini”, aliongeza Mhe. Mghwira.

Mhe. Mghwira ameitaka pia Idara ya Uhamiaji kujenga mahusiano na Wananchi ili kupata taarifa za haraka na sahihi kutoka kwa wananchi hao.

“Nitoe wito kwa Idara ya Uhamiaji kubuni mbinu na mikakati kwa Maafisa wake kushuka chini kwa Wananchi ili kuwa karibu zaidi na jamii na Watanzania kwa ujumla. Kwa kufanya hivyo Wananchi watajua haki zao ikiwa pamoja na kufahamu vielelezo vinavyotakiwa katika kupata huduma za Idara ikiwamo Pasipoti sanjali na kutoa taarifa juu ya uwepo wa wahamiaji haramu katika maeneo yao  amesisitiza Mhe. Mghwira.

Awali akimkaribisha Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi katika Mkutano huo, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala amesema kuwa Idara imezindua mpango mkakati wa kudhibiti Uhamiaji nchini. Mpango huo unalenga kuwatambua na kuwaorodhesha wahamiaji wote nchini na zoezi hilo litafanyika nchi nzima kwa kuanzia Mkoa wa Dar es Salaam.

Katika utekelezaji wake, mpango huo utahusisha Viongozi wa Serikali za Mitaa au Vijiji (MEO/VEO), Maafisa Watendaji wa Kata (WEO) na kuratibiwa na Idara ya Uhamiaji. Kupitia Mpango huo Idara itaimarisha udhibiti na usimamizi wa mipaka yetu, kuimarisha ulinzi na Usalama na pia kulipatia ufumbuzi suala la Wahamiaji Walowezi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Kangi Lugola akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Uhamiaji Waandamizi mara baada ya kufungua Mkutano wa Maafisa Uhamiaji Waandamizi  unaolenga kujadili na kutathmini utendaji kazi wa Idara ya Uhamiaji.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Uhamiaji Waandamizi  unaolenga kujadili na kutathmini utendaji kazi wa Idara ya Uhamiaji.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjro, Mhe. Anna Mghwira akitoa toa wito kwa Idara ya Uhamiaji kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji na utoaji wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Uhamiaji Waandamizi  unaolenga kujadili na kutathmini utendaji kazi wa Idara ya Uhamiaji.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akizungumza kuhusu Idara hiyo ilivyozindua mpango mkakati wa kudhibiti Uhamiaji  hapa nchini wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Uhamiaji Waandamizi  unaolenga kujadili na kutathmini utendaji kazi wa Idara ya Uhamiaji.
Baadhi ya maofisa wa Uhamiaji wakiwa kwenye Mkutano wa Maafisa Uhamiaji Waandamizi  unaolenga kujadili na kutathmini utendaji kazi wa Idara ya Uhamiaji.

WAZIRI HASUNGA AWASILI NCHINI ISRAEL KWA AJILI YA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU SITA

$
0
0


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa pamoja na mwenyeji wake Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Israel Brigedia Jenerali Kahema Juni Mziray (Mwambata wa Jeshi) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Ben Gurion katika mji wa Telaviv nchini Israel kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku sita, leo tarehe 1 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa pamoja na mwenyeji wake Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Israel Brigedia Jenerali Kahema Juni Mziray (Mwambata wa Jeshi) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Ben Gurion katika mji wa Telaviv nchini Israel kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku sita, leo tarehe 1 Septemba 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa pamoja na mwenyeji wake Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Israel Brigedia Jenerali Kahema Juni Mziray (Mwambata wa Jeshi) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Ben Gurion katika mji wa Telaviv nchini Israel kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku sita, leo tarehe 1 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo). Wengine pichani ni Afisa mambo ya nje Ndg Davis Byarugaba na Msaidizi wa Waziri wa Kilimo Ndg Steven Kihwele.


Na Mathias Canal, Telaviv-Israel

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 1 Septemba 2019 majira ya jioni amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Ben Gurion katika mji wa Telaviv nchini Israel kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku sita.

Katika uwanja huo wa ndege wa kimataifa wa Ben Gurion, Mhe Hasunga amepokelewa na mwenyeji wake Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Israel Brigedia Jenerali Kahema Juni Mziray (Mwambata wa Jeshi) kwa niaba ya Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima.

Katika ziara hiyo ya kikazi ya siku sita waziri Hasunga atashiriki mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yatakayofanyika mjini Jerusalem tarehe 2 Septemba 2019.

Mahafali hayo yatajumuisha vijana 1600 kutoka mataifa zaidi ya 12 ambapo kati ya hao vijana 45 ni watanzania, na kutoa vyeti kwa vijana hao wa Tanzania 45 watakaohitimu.

Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini Israel Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepewa jumla ya nafasi 100 kwa ajili ya kupeleka vijana wa kitanzania kujifunza kilimo cha kisasa nchini Israel.

Alisema kuwa kupatikana na kwa nafasi hizo 100 ni kutokana na ombi la Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa serikali ya Israel ili kuwawezesha vijana wengi wa kitanzania kujifunza mbinu na teknolojia za kilimo cha kisasa.

Kadhalika, Waziri Hasunga atakutana na kurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Agro Studies ambapo miongoni mwa mazungumzo muhimu itakuwa ni pamoja na kumuomba uwezekano wa kuongezewa nafasi zaidi ili vijana wengi wa kitanzania waende kujifunza mbinu mpya za kilimo nchini Israel.

Pia, Mhe Hasunga atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo nchini Israel kujadiliana nae maeneo mbalimbali na fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Katika mkutano mwingine, Mhe Hasunga atakutana na kufanya mazungumzo na wadau wawekezaji wakubwa wa sekta ya kilimo nchini Israel ili kuwaeleza fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.

Katika ziara hiyo tarehe 4 Septemba 2019 Mhe Hasunga atashiriki mapokezi ya vijana 100 ambao wapo nchini Israel kwa ajili ya kuanza mafunzo yao.

Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Israel Brigedia Jenerali Kahema Juni Mziray (Mwambata wa Jeshi) akizungumza kwa niaba ya Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima mara baada ya kumpokea mwenyeji wake amesema kuwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Israel uliorejea mwaka 1995 baada ya kuvunjika mwaka 1963 unazidi kuimarika hivyo kutoa fursa kwa watanzania kujifunza mbinu bora za kilimo nchini Israel.

Alisema kuwa Tanzania kupitia nafasi za kimasomo zinazotolewa na Israel, itazidi kunufaika kwani nchi ya Israel ni moja ya nchi zinazoongoza katika utafiti wa maendeleo ya Kilimo na Teknolojia (Agriculture Research and Development).

MKUTANO WA CPA ZANZIBAR

$
0
0

Spika wa Bunge na Mwenyekiti wa Bodi ya Uwekezaji ya Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika , Mhe. Job Ndugai wa pili (kulia) akizungumza katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya CPA, Kanda ya Afrika, anayefuata kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA, Mhe. Justin Muturi, Naibu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Aaron Mwansa Mbulakulima, Mhe. Emilia Monjowa Lifaka, Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimataifa (CPA – INTERNATIONAL), Mhe.Elijah Okupa, Naibu Mweka Hazina wa CPA Kanda ya Afrika na kushoto kwa Mhe. Spika ni Katibu wa CPA Kanda ya Afrika, Ndugu Stephen Kagaigai. kikao hicho kimefanyika katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa Hoteli iliyoko visiwani Zanzibar
Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA)Kanda ya Afrika wakiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ,wa kwanza kulia ni Katibu wa CPA Kanda ya Afrika, Ndugu Stephen Kagaigai, Mhe. Job Ndugai, Mwenyekiti wa Bodi ya Uwekezaji ya Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika , Mhe. Justin Muturi Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA, Kanda ya Afrika, Mhe. Aaron Mwansa Mbulakulima, Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Afrika, Mhe. Emilia Monjowa Lifaka, Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kimataifa (CPA – INTERNATIONAL) na Mhe . Elijah Okupa, Naibu Mweka Hazina wa CPA Kanda ya Afrika .Kikao hicho kimefanyika katikaa Hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa Hoteli iliyoko visiwani Zanzibar
Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Jumuiya ya Madola (CPA) Kimataifa (CPA – INTERNATIONAL), Mhe. Emilia Monjowa Lifaka, akizungumza katika akizungumza katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya CPA, Kanda ya Afrika, anayefuata kushoto kwake ni Mhe. Aaron Mwansa Mbulakulima, Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Afrika, Mhe. Justin Muturi Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA, Kanda ya Afrika Mhe. Job Ndugai, Mwenyekiti wa Bodi ya Uwekezaji ya CPA Afrika, Ndugu Stephen Kagaigai, Katibu wa CPA Kanda ya Afrika na kushoto kulia kwa Mhe Lifaka ni Mhe . Elijah Okupa, Naibu Mweka Hazina wa CPA Kanda ya Afrika.
Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Jumuiya ya Madola (CPA) Kimataifa (CPA – INTERNATIONAL), Mhe. Emilia Monjowa Lifaka, akizungumza katika akizungumza katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya CPA, Kanda ya Afrika, anayefuata kushoto kwake ni Mhe. Aaron Mwansa Mbulakulima, Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Afrika, Mhe. Justin Muturi Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA, Kanda ya Afrika Mhe. Job Ndugai, Mwenyekiti wa Bodi ya Uwekezaji ya CPA Afrika, Ndugu Stephen Kagaigai, Katibu wa CPA Kanda ya Afrika na kushoto kulia kwa Mhe Lifaka ni Mhe . Elijah Okupa, Naibu Mweka Hazina wa CPA Kanda ya Afrika. Kikao hicho kimefanyika katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa Hoteli iliyoko visiwani Zanzibar

PROGRAMU YA KITALU NYUMBA YAWAPA HAMASA VIJANA KUSHIRIKI SEKTA YA KILIMO

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Vijana walioshiriki katika mafunzo ya ukuzaji ujuzi kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba (Green House) katika Kijiji cha Ihemi alipotembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya mafunzo hayo Mkoani Iringa.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Bi. Lucy Nyalu akieleza jambo kuhusu ushirikishwaji wa vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo walioshiriki katika mafunzo hayo.

Baadhi ya Vijana wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea vijana hao kwa lengo la kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba.
Mratibu wa Mradi huo katika Halmashauri ya Iringa Vijijini Bw. Daniel Mlay akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ukuzaji ujuzi kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Holly Green Bw. Octavian Laswai alipokuwa akikagua kitalu nyumba wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya kilimo cha kisasa kupitia kitalu nyumba, Mkoani Iringa.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ihemi Bw. Antony Akata (wa pili kutoka kushoto) akimfafanulia jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea eneo hiyo kwa lengo la kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga Bi. Saada Mwaruka alipokuwa akikagua chanzo cha maji yanayotumika kumwagilia Kitalu nyumba hicho. (Katikati) ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Venerose Mtenga.

******************

Programu ya ukuzaji ujuzi kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu nyumba (Green house) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imewapa hamasa vijana kushiriki kwa wingi kwenye sekta ya kilimo ikiwa ni chanzo cha kimoja wapo cha ajira nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Ziara yake ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba, Mkoani Iringa.

Waziri Mhagama alieleza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu iliamua kuanzisha programu hiyo kwa lengo la kuwawezesha vijana kushiriki kwa wingi kwenye masuala ya kilimo ili waweze kujiajiri wao wenyewe na kuajiri vijana wenzao kupitia teknolojia hiyo.

“Mradi huu unatekelezwa kwenye Halmashauri 185 nchini katika awamu hii ya kwanza ikiwa na lengo la kuwawezesha vijana kuwa na ujuzi pamoja na stadi za kilimo cha kisasa kupitia kitalu nyumba ambacho kina tija katika kuwapatia mazao bora na mengi yatokanayo kwenye eneo dogo,” alieleza Mhagama

Alieleza kuwa Serikali imeendelea kuwawezesha na kuwajengea uwezo vijana wa masuala ya ukuzaji ujuzi ili waweze kuongeza tija kwenye shughuli wanazozifanya na zitakazo wakwamua kiuchumi.

“Vijana wanaweza kupata ajira bora katika kilimo endapo watawekewa mazingira bora kama kuimarisha teknolojia na mbinu za kilimo,” alisema Mhagama.

Hata hivyo aliwasihii vijana kuhakikisha wanatunza vitalu nyumba hivyo kwa kuwa watanufaika navyo na vitawasaidia kufanilisha malengo yao sambamba na kuleta maendeleo endelevu katika sekta ya kilimo.

Aidha alitoa wito kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakiksha wanawasilisha njia bora zaidi za kuwapata vijana stadi zitakazo wajengea uwezo kupata teknolojia za kisasa zitumikazo katika kilimo pamoja na kuwapatia mitaji ambayo itawawezesha kujenga vitalu nyumba vyao binafsi.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Venerose Mtenga alisema kuwa Ofisi hiyo inatekeleza programu mbalimbali zitakazo wawezesha vijana kupata ujuzi na stadi stahiki zitakazo wasaidia kuondokana na changamoto ya ajira.

Naye Mratibu wa Mradi huo katika Halmashauri ya Iringa Vijijini Bw. Daniel Mlay alisema kuwa jumla ya vitalu nyumba vinne vimejengwa na vijana 431 wameweza kunufaika na mafunzo hayo.

“Tutaendelea kuwahamasisha vijana washiriki kwa kikamilifu katika mradi huu kwa kuwa una manufaa mazuri kwao,” alisema Mlay 

Pia mmoja wa vijana walionufaika kupitia Mradi huo Bw. Ramadhani Haule alieleza kuwa mradi huo wa Kitalu Nyumba umewasaidia kupata elimu bora ya kilimo na umesaidia vijana kuondoka kwenye makundi ya wasiokua na ajira.

“Tunaishukuru Serikali kwa kutuamini na kutupatia ujuzi huu, tunaahidi tutaendelea kushirikiana vijana wengi ili kujikwamua kiuchumi,” alisema

Katika ziara hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alitembelea Vitalu Nyumba vilivyopo katika eneo la Ihemi na Halmashauri ya Mafinga.



Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images