Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

Vivutio vya Utalii vya Tanzania Kuanza Kuonekana Baidu Septemba Hii

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devota Mdachi (wa kwanza kulia) akikabidhi zawadi kwa mtaalam wa mtandao wa Baidu kutoka China katika Hafla ya kuwaaga wageni hao iliyofanyika Ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania TTB Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB), Jaji Thomas Mihayo akikabidhi zawadi ya kanga kwa mtaalam wa mtandao wa Baidu kutoka China katika Hafla ya kuwaaga wageni hao iliyofanyika Ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania TTB Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB), Jaji Thomas Mihayo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devota Mdachi wakiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa mtandao wa Baidu kutoka China katika Hafla ya kuwaaga wageni hao iliyofanyika Ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania TTB Jijini Dar es Salaam.(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

*****************

Na. Paschal Dotto-MAELEZO
1-09-2019

Tanzania imeelekeza juhudi zake katika kuvutia watalii hasa wale kutoka nje ya nchi na ikilenga zaidi kuliteka soko la china lenye watu wengi duniani, ambapo kwa siku za karibuni Bodi ya utalii Tanzania ilifanya ziara kubwa ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika Miji ya Beijing, Shanghao, Chengdu, Guangzhuo, Hong Kong, Najing na Changsha.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi wa Boti ya Utalii Tanzania (TTB) Jaji Thomas Mihayo, alisema kuwa matunda ya Ziara nchini China sasa yameanza kuonekana kwa kitendo cha kampuni ya Baidu kuja nchini kufanya mradi wa upigaji picha jongevu na mnato wa vivutio vya utalii Tanzania ili kuweza kuvitangaza katika mtandao huo wenye wafuasi zaidi ya milioni 700.

“Matunda ya ziara iliyofanyika katika Miji ya China yameanza kuonekana ambaposafari hii timu ya wataalam 11 kutoka katika kampuni kubwa za kimtandao nchini humo (Baidu) waliwasili nchini tarehe 22 Agosti ,2019 na kutembelea baadhi ya maeneno ya vivutio vya utalii hapa nchini kwa lengo la kupata picha jongevu na mnato ili kutangaza vivutio hivyo kwenye soko la utalii wa zaidi ya watu milioni 700 wanaoufuatilia mtandao huu wa Baidu”, Alisema Jaji Mihayo.

China ni moja ya nchi duniani ambao wanatumia mtandao wao wa baidu, kwa hiyo ni dhahiri kuwa utengenezaji wa makala na picha mbalimbali walizopata kutoka katika vivutio hapa nchini vitaweza kuongeza watalii kutoka China kwani picha hizo zitaonekana kwa watumiaji zaidi ya milioni 700 wa mtandao huo.

Aliongeza kuwa lengo la TTB ni kuiwezesha sekta ya utalii kupata watalii wengikutoka China na kuongeza idadi ya watalii wa kigeni wanakuja kuitembelea Tanzania kutokana na kuona vivutio vitakawekwa kwenye mradi huo wa Wander Planet kutoka katika kampuni ya BAIDU, kuanzia Septemba 2019 na kuendelea.

Mihayo alisema kuwa kati ya nchi saba duniani Tanzania imeibuka kuwa nchi yakwanza katika Mradi huo na ndiyo nchi pekee kutoka bara la Afrika na nchi zingine zinazolengwa na mradi huo ni kutoka mabara ya Amerika, Asia na Ulaya.

Wakiwa nchini wataalam hao wa mambo ya Picha jongevu na picha mnato walipata wasaa wa kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii nchini ikiwemo Mji wa kihistoria Bagamoyo, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Makumbusho ya Oldvuai Gorge, Hifadhi ya Taifa Serengeti, ziwa Manyara, Mji wa Mwanza na Zanzibar. Na maeneo hayo yote yamechukuliwa picha ili kuweza kutangazwa katika mtandao huo mkubwa wenye wafuasi milioni 700 nchini China.

Aidha, Jaji Mihayo alisema kuwa lengo la ziara ya wataalam hao ni kupiga pichajongevu na mnato na kuandika taarifa za vivutio mbalimbali vya utalii katika maeneo waliyotembelea na kisha kuziweka kwenye mtandao wao, na wameahidi kutekeleza kama walivyolenga katika kutangaza utalii wa Tanzania nchini China ambapo baadhi ya taarifa za Shirika la Utalii Duniani(UNWTO) zinaeleza jinsi China ilivyo na soko kubwa la utalii Duniani.

“Takwimu za Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) zinaonesha kuwa China ni nchi ambayo ina soko kubwa la utalii duniani, mwaka 2018 wachina Milioni 130 walisafiri nje ya nchi huku Tanzania ikipokea watalii 32,773 idadi ambayo ni ndogo ukilinganisha na idadi ya watalii hao kutoka China kwenda nchi zingine, kwa hiyo juhudi hizi zinafanyika ili kuliteka soko la China kwenye sekta hii muhimu” Alisema Jaji Mihayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi alisema kuwa kampuni ya Baidu kutoka China imefanya vyema kuwaletawataalam hao ili kutekeleza kazi ya kupiga picha jongevu na mnato na kuwezakutangaza utalii wa Tanzania nchini China kwenye soko la watu milioni 130 wanaotoka nje ya nchi kwenda kutalii sehemu mbalimbali Duniani.

“Tunaishukuru kampuni ya Baidu kutoka China kwa kuwaleta wageni hawa, kwani wameona na walichokiona kinatosha kabisa kwenda kukieleza nyumbani kwao China, Tanzania tuna vivutio vingi sana kwa hiyo picha na video zilizopigwa kwenye vivutio ambavyo kila mtu duniani anatamani kuviona na kuitembelea Tanzania zitasaidia kuleta watalii wengi kutoka China ”, alisema Mdachi.

Naye kiongozi wa msafaro huo Bibi Jin Xiaping, alisema kuwa kampuni ya Baiduimefanya kitu muhimu kwa kuwaleta wataalam hao, kwani wamekuja Tanzania ilikuona jinsi gani wataweza kutekeleza mradi huo(Wonder planet) kupiga picha jongevu na mnato na sasa wamefanya kazi yao, kwa hiyo kuanzia Septemba hii wataweza kuweka kwenye mtandao wao wa Baidu na kutangaza uzuri wa Tanzania kwenye soko la utalii China.

“Wataalam hawa 11 kila mmoja anazaidi ya wafuasi milioni mbili kwenye mitandao ya kijamii, kwa hiyo wamepiga picha jongevu, mnato na wataandika makala mbalimbali ili kuziweka kwenye mitandao yao na kuwezesha wafuasi wao kufahamu vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania”,Alisema Xiaping

YAMTAKIA MUNGE MBILINYI (SUGU) KILA LAKHERI KATIKA MAISHA YAKE MAPYA YA NDOA

0
0
  Mbunge wa Jimbo la Mbeya  Mh.Joseph Mbilinyi (Sugu)  akiwa na Mkewe Hapynes Masonga
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila (kulia )akiwa Naibu Waziri Utumishi Dkt Mary Mwanjelwa (kushoto) wakiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Joseph Mbilinyi (Sugu) na Mkewe Hapynes Masonga katika sherehe ya kufunga ndoa katika Hotel Desideria inayomilikiwa na Mbunge huyo iliyopo katika mtaa wa Uzunguni jijini Mbeya ndoa hiyo ilifungwa katika kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Ruanda Jimbo Kuu la Mbeya Agosti 31 Mwaka huu

AFRECO KUIPA BASI HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA

0
0
TAASISI ya Association of African Economy and Development in Japan (AFRECO) imeahidi kuipatia Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Chuo Kikuu cha Dodoma basi ambalo ni hospitali kamili litakalotoa huduma za matibabu kwa Manispaa ya Dodoma, Mikoa na Wilaya zinazoizunguka Mkoa wa Dodoma.

Basi hilo litakapowasili nchini kutoka Japan linatarajiwa kuwa ni mkombozi kwa wananchi waishio vijijini na katika maeneo ambayo hayana hospitali kwani kila litakakokwenda kutoa huduma litakuwa na madaktari waliobobea katika utaalamu wa tiba mbalimbali, vifaa tiba, maabara pamoja na dawa.

Hayo yamebainishwa leo (Jumapili, Septemba 1, 2019) na Rais wa AFRECO, Bw. Tetsuro Yano katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa yaliyofanyika kwenye hoteli ya Yokohama Bay nchini Japan.

Bw. Yano amesema wameamua kuanza kutoa misaada na huduma zao nchini Tanzania baada ya kufurahishwa na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Ameongeza kuwa anaamini siku moja Tanzania itakuwa nchi ya mfano kwa Afrika Mashariki na Afrika yote kwa kutoa huduma bora za tiba kwani itakuwa na vituo vingi vya Afya na hospitali zenye uwezo wa kutibu magonjwa kama vile ya moyo na figo. Hata hivyo tayari wagonjwa toka nchi jirani wameanza kuja kutibiwa nchini.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amesema mbali na kutoa basi ambalo litakuwa linatoa huduma za matibabu, pia taasisi hiyo ya AFRECO itasaidia katika kupandisha hadhi hospitali ya Benjamin Mkapa ya Chuo Kikuu cha Dodoma kuwa Shule kamili ya tiba.

Amesema hospitali hiyo ya Benjamin Mkapa ya Chuo Kikuu cha Dodoma itapatiwa vifaa mbalimbali vya tiba ambavyo vitaifanya hospitali hiyo kuwa ni shule bobezi kwa utoaji wa tiba mbalimbali nchini Tanzania na Barani Afrika.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuwa wamekubaliana na AFRECO kuanzisha kitivo maalum cha Uhandisi wa Vifaa Tiba ambacho kitafundisha uhandisi wa vifaa tiba ili nchi yetu iwe na watalaamu wa kukarabati vifaa tiba pindi vinapoharibika badala kuvipeleka nje ya nchi au kuagiza wahandisi na watalaamu kutoka nje ya nchi kuja kuvitengeneza.

“Hivi sasa yanafanyika makubaliano ya kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vifaa tiba na kwa kuanzia wataanza kutengeneza maji ya drip ambayo huongezwa kwa wagonjwa kwa maeelekezo ya madaktari na baadae watengeneza dawa mbalimbali.”

Naye,Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Mipango, Utawala na Fedha, Profesa Donald Mpanduji amesema wametia saini hati ya makubaliano kati ya AFRECO na Chuo Kikuu cha Dodoma ambayo yanalenga kuboresha hospitali ya Chuo Kikuu cha Dodoma.

Awali, Dkt. Omary Ubuguyu kutoka Wizara ya Afya amesema maboresho yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika huduma za tiba yameiwezesha Tanzania kupunguza wagonjwa wanaopelekwa nchi za nje kwa matibabu kutoka 800 hadi 42 ambalo ni punguzo la asilimia inayotajwa kuwa 200.

Amesema hatua hiyo imeongeza nafasi kwa watalaamu wetu wa tiba kujifunza zaidi pamoja na kuwapunguzia wananchi gharama za kusafiri kwenda nje ya nchi kutafuta tiba na pia imeipunguzia Serikali gharama ya fedha za kigeni ambazo zingetumika kuwatibu wagonjwa nje ya nchi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA RAIS WA AFRECO NCHINI JAPAN

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa The Association of African Economy and Development in Japan (AFRECO), Bw. Tetsuro Yano kabla ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Yokohama Bay nchini Japan September 1, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Rais wa The Association of African Economy and Development in Japan (AFRECO), Bw. Tetsuro Yano (kushoto) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Mipango, Utawala na Fedha, Profess Donald Mpanduji (kulia) wakishikana mikono ikiwa ni ishara ya makubaliano yanayolenga kuboresha hospitali ya Chuo Kuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa kati ya Chuo hicho na AFRECO baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Yokohama Bay nchini Japan, Septemba 1, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAHAKIMU WATAKIWA KUTOAIHIRISHA KESI MARA KWA MARA

0
0
JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA (KUSHOTO) AKIMKABIDHI MKUU WA WILAYA YA MUFINDI MHE. JAMHURI WILLIAM KITABU CHA MPANGO WA MIAKA MITANO WA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA YA TANZANIA ALIPOMTEMBELEA OFISINI KWAKE AKIWA KATIKA ZIARA YA KIKAZI MKOANI IRINGA.
JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MKUU WA WILAYA YA MUFINDI MHE. JAMHURI WILLIAM (WA PILI KULIA) PAMOJA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA MUFINDI ALIPOMTEMBELEA OFISINI KWAKE AKIWA KATIKA ZIARA YA KIKAZI MKOANI IRINGA


JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WATUMISHI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA MUFINDI BAADA YA KUZUNGUMZA NAO ALIPOTEMBELEA MAHAKAMA YA WILAYA YA MUFINDI KUKAGUA SHUGHULI ZA MAHAKAMA AKIWA KATIKA ZIARA YA KIKAZI MKOANI IRINGA
MKUU WA WILAYA YA MUFINDI MHE. JAMHURI WILLIAM AKIMUELEZEA JAMBO JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA WAKATI JAJI MKUU ALIPOENDA KUKAGUA KIWANJA CHA UJENZI WA JENGO LA MAHAKAMA YA MWANZO MJINI MAFINGA AKIWA KATIKA ZIARA YA KIKAZI MKOANI IRINGA.

********************



Lydia Churi-Mahakama Iringa

Mahakimu wametakiwa kusimamia uendeshaji wa mashauri na kuzuia maahirisho ya mara kwa mara ya kesi bila ya sababu za msingi kwa lengo la kuhakikisha kesizinamalizika kwa wakati Mahakamani.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema hayo wakati wakikao cha majumuisho mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi ya siku tano katikamikoa ya Iringa na Njombe aliyoifanya kwa lengo la kukagua shughuli zaMahakama pamoja na kubainisha kwa wadau changamoto zilizoibuliwa wakati wakikao cha Mahakama ya Rufani kilichomalizika leo mjini Iringa.

Jaji Mkuu amewata Mahakimu kutokubali kuahirisha mashauri kwa muda mrefukwa ajili ya kuandaa maamuzi madogo yanayotokana na pingamizi ambazo nyingihutumiwa vibaya kwa lengo la kuchelewesha mashauri.

“Maafisa wote wa Mahakama ni jukumu lenu pia kuzipa nguvu za kimahakamavifungu vya sheria zinazolinda haki ya Mwananchi aliye mahabusu kwakuhakikisha hakuna mwananchi atashikiliwa bila kufikishwa mahakamani ndani yasiku zilizowekwa na sheria”, alisema.

Alitoa rai kwa Mahakimu kutokuwa wepesi kukubali hoja za waendesha mashitakaza kusema kuwa upelelezi bado unaendelea bila ya kufafanua ni kitu gani katikaupelelezi bado kinatafutwa na ni kwa muda gani.

“Ni umakini wa Mahakama ndiyo utahakikisha kuwa shughuli za upelelezi
haziwanyimi wananchi haki yao ya kikatiba ya kutochelewesha haki yao ya
kusikilizwa kesi dhidi yao bila sababu za kimsingi,” alisisitiza Jaji Mkuu.

Akizungumzia dhamana, Jaji Mkuu amesema ni wajibu wa Mahakama kutoa
dhamana kwa makosa yenye dhamana kwa kuwa Mahakama ni msimamizi wahaki ya kila mtu kuwa huru na kuishi kama mtu huru.

Alivitaja vigezo vya kutumiwa katika kutoa dhamana kuwa ni pamoja na
vitambulisho vya Taifa, na vitambulisho vinavyokubalika. Aliongeza kuwa
Mahakama pia ziwaruhusu washtakiwa kujidhamini wenyewe pale Hakimu
anapojiridhisha na utambulisho wao kuwa watahudhuria mahakamani.

“Mashauri ambayo washtakiwa wamekosa dhamana yasikilizwe mfululizo, kwayale makosa yasiyo na dhamana na yako ndani ya mamlaka ya Mahakama,matumizi ya sheria yatumike ili kuyaondosha”, alisema.

Katika kupunguza msongamano magerezani, Jaji Mkuu amesema Maafisa waMahakama hawana budi kutumia adhabu mbadala kwa makosa madogo madogokwa kuzingatia sheria zilizopo.

WAFANYABIASHARA WA TANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KONGAMANO LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA UGANDA

0
0
Dkt John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania amemualika Mhe Yoweri Kaguta Museveni Rais wa Jamhuri ya Uganda kuzindua kongamano la kwanza la biashara kati ya Tanzania na Uganda linalotarajiwa kufanyika tarehe 6-7 Septemba, 2019 katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. 

Hayo yamesemwa na Mhe Innocent Bashungwa, Waziri wa Viwanda na Biashara wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa Mhe Yoweri Kaguta Museveni Rais wa Jamhuri ya Uganda ataambatana na wafanayabiashara kutoka nchini kwake ili kukutana na wafanyabaishara wa Tanzania. 

Mhe Bashungwa ameeleza kuwa lengo la kongamano hilo ni kutangaza fursa na kuhamasisha biashara na uwekezaji zilizoko Tanzania na Uganda. Pia Serikali itapata fursa ya kuongea na wafanyabiashara hao ili kuangalia changamoto za kufanya biashara katika nchi hizo mbili. Vilevile Serikali zetu zitashirikiana kuzitatua, kuangalia fursa zilizopo, kuongeza biashara katika nchi hizo mbili na kuhamasisha uwekezaji. 

“Sisi Tanzania tumekuwa tunawauzia chakula na vifaa vya viwandani, kwakuwa tunajenga uchumi wa viwanda ni fursa kwa watanzania kushiriki kwenye kongamano hilo ambalo litakuwa na tija kubwa kwetu kama nchi. Rais wetu analeta wakuu wa nchi mbalimbali ikiwemo Uganda ili kuwaonesha fursa tulizonazo pamoja na kujenga mtandao mpana wa biashara”, amesema Mhe Bashungwa 

Mhe Bashungwa ameeleza kuwa kutakuwa na Maonesho ya bidhaa za Tanzania ambapo Watanzania watapata fursa ya kuonesha bidhaa za kilimo na za viwandani, taasisi za umma na sekta binafsi zinazosaidia katika mnyororo wa thamani za biashara. Ujio wa Rais wa Jamhuri ya Uganda pamoja na wafanyabiashara toka nchini humo itakuwa ni fursa ya kuunganisha wafanyabiashara wetu na wafanyabiashara wa Uganda kukuza wigo wa biashara, kupata masoko mapya pamoja na kutatua changamoto na kujenga mazingira mazuri zaidi ya kufanya biashara. Amewahamasisha wazalishaji wa bidhaa za kilimo, wafanyabaishara na wamiliki wa viwanda kutoka Mikoa yote ya nchini kujitokeza kushiriki. 

“Wafanyabaishara waelewe kuwa ni mwanzo mzuri wa kupenya katika soko la Sudani ya Kusini kwasababu wapo wafanyabiashara wa Uganda wanafanya biashara nchini Sudani ya Kusini” amesema Mhe Bashungwa. 

Ameendelea kusema kuwa mwelekeo wa Serikali ya Tanzania ni kujenga uchumi wa viwanda hivyo ni fursa kwa Watanzania kutumia kongamano hili kwasababu Serikali inazidi kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara nchini, kujenga viwanda na kufuatilia masoko mbalimbali lengo ni kutaka uuzaji wa bidhaa nchini Uganda uongezeke. 

Imetolewa na: 
Theresa Chilambo 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano-TanTrade

RC MBEYA 'ALIANZISHA' KWA MADEREVA WA BAJAJI WASIO NA LESENI

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila leo  Septemba 2,2019 ameongoza kufanya ukaguzi maalumu kwa madereva wa Bajaji wenye leseni Jijini Mbeya ,ukaguzi huo umehusisha Jeshi la Polisi

Waziri Mbarawa afanya ziara Mbulu, awaahidi wananchi kumaliza tatizo la Maji

0
0

Waziri wa Maji, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) akiwa na Mbunge wa Mbulu vijijini Mhe. Flatei Gregory Massay na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Bw. Chelestino Mofuga pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Babati Mhandisi Iddy Msuya wakielekea kukagua mradi wa Tumati uliopo Mbulu vijijini.
Waziri wa Maji, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) akipata maelezo ya mradi wa Arri Harsha kutoka kwa Mhandisi Maji wa Halmashauri ya Mbulu Philemon Kamar. 
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Maji, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) hayupo pichani.

……………….

Waziri wa Maji, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) amefanya ziara ya kukagua miradi ya maji yenye changamoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara. 

Waziri Mbarawa amefanya ziara hiyo ili kubaini changamoto zilizopo katika miradi ya maji ili serikali iweze kutafuta ufumbuzi wa haraka na wananchi wa Mbulu waweze kupata majisafi na salama na kutekeleza azma ya kumtua mama ndoo kichwani. 

Waziri Mbarawa amesema changamoto kubwa iliyokuwepo ni kuwa wakandarasi wanaopewa kazi hizo za kutekeleza miradi, wanaweka gharama kubwa za ujenzi na kujenga miradi chini ya viwango. 

Mhe. Mbarawa amesema kwa muda mrefu Serikali imekuwa inalipa gharama kubwa za kujenga miradi ya maji nchini kutokana na ubabaishaji wa wakandarasi wa kuweka gharama kubwa, kujenga miradi isiyokuwa na ubora na miradi kutokamilika kwa wakati hivyo kuwafanya wananchi wakose majisafi na salama.

“Kuanzia sasa Serikali imekuja na utaratibu mwingine wa kuwatumia wataalam wake wa ndani na Mamlaka za Maji za eneo husika katika utekelezaji wa miradi ya maji ili kupunguza gharama kubwa zilizokuwa zinawekwa na wakandarasi”, Prof. Mbarawa amesema

Miradi iliyokaguliwa ni mradi wa maji wa vijiji vya Mongahay, Tumati, mradi wa maji wa vijiji vya Arri, Yaeda Ampa, Haseng, Harsha Bashay na Yaeda. Mhe. Mbarawa ameahidi kupeleka kiasi cha fedha Tsh. 150 milioni kwa mradi wa Tumati na Tsh. 300 milioni kwa mradi wa Arri Harsha ambazo zimeshafika katika Mamlaka ya Maji Babati kwa ajili ya kuanza kazi za kukamilisha kazi zilizobaki.

Mhe. Waziri Mbarawa akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Mbulu na kusikiliza kero zao amewaahidi kwamba kero zao zitafanyiwa kazi ili kuhakikisha wanapata majisafi na salama. 

Waziri Mbarawa amewataka wananchi wa Mbulu kutunza miundombinu ya miradi ya maji na kutunza vyanzo vya maji ili viwe endelevu kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

Nilivyopokewa kwa tabasamu, kushuhudia mengi Thailand

0
0


 Na Bakari Kimwanga,aliyekuwa Bangkok, Thailand

SAWADIKA ni salamu ambayo hutolewa kwa mwanamke, na Sawadikrapu
hutolewa kwa mwanamume ikimaanisha habari pindi uingiapo nchini
Thailand.

Unaponunua au kumpa mtu chochote basi utajibiwa kwa neno Koponhka,
likiwa na maana ya ahsante sana.

Haikuwa kazi rahisi kufika katika Jiji la Bangkok nchini Thailand,
lakini tu kwa uwezo wa Mungu, nami nilibahatika kufika nchini humo.

Ilikuwa Agosti 17, mwaka huu, ilipofika saa 7 mchana nilianza safari
kutoka nyumbani na kueleka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, ambapo nilisoma maelezo ya tiketi yangu ya ndege ya Shirika
la Ndege la Qatar ikiniambia kwamba ninataka kuwa uwanja wa ndege mpya wa Terminal III kuanzia saa 9:5 alasiri kwa ajili ya safari.

Nilifika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa 8 mchana, ambapo mimi
na wasafiri wenzangu ambao tulikuwa tukisafiri na ndege ya Qatar
tulipewa maelezo ya kututaka kuanza kukaguliwa kuanzia saa 9:5
alasiri. Nikiwa nimekaa kwenye viti na abiria wenzangu nilianza kuvuta
taswira nzito kuhusu safari itakavyokuwa kutoka Dar es Salaam hadi
katika Jiji la Bangkok nchini Thailand.

Hakika muda ukafika tukakaguliwa na kuingia ndani ya uwanja mpya wa
ndege huku mawazo yaliyoambatana na usingizi yalikuwa ni jinsi
nitakavyoshuhudia mji huo.

Naam; ilipofika saa 11 jioni abiria tulitangaziwa kwamba sasa tunaaza
kuingia ndani ndege awamu kwa awamu, ambapo mimi nakumbuka tiketi
yangu ilikuwa imeandika ‘Zone 3’ tukaitwa nami nikajongea huku nikiwa
na picha sasa tunaanza safari lakini je, ndani ya ndege itakuwaje?

Nikiwa ndani ya ndege kwenye kiti changu namba 24 E huku jirani yangu
akiwa ameketi mwenzangu, Exper Pius, ambaye ni mtaalamu wa mazingira
na mtumishi wa Taasisi ya Kimataifa ya RTI iliyo chini ya USAID
Protect Tanzania, chini ya mradi wa Wildlife Combating Crime, ikiwa
inaangazia masuala ya usafirishaji haramu wa wanyama.

Ndani ya ndege nikaanza kumuuliza maswali kadhaa je, hii safari yetu
itakuwaje? Jibu lake lilikuwa jepesi, tuombe Mungu tutafika salama
Thailand, hakika tunakwenda mashariki ya mbali, ambapo tutafika kesho
mchana wakati huku kwetu itakuwa ni asubuhi.
Licha ya wahudumu kupita na kunipa viburudisho, lakini bado akili
yangu ilikuwa ikipiga picha Thailand hasa Bangkok ikoje!

Ilipofika saa 12 jioni abiria wote tuliokuwamo ndani ya ndege,
tukatangaziwa tena umuhimu wa kufunga mikanda huku wahudumu wa ndegewakiwa wanapita katika kila kiti na kumkagua abiria kama amefunga
mkanda.

Kazi hiyo ikakamilika likatoka tangazo ya kwamba sasa tunaanza safari,
mara ndege ikachochewa injini kelele zikawa nyingi, huku mitetemo
ikitamalaki watu tukiwa vitini kwa utulivu huku kila mmoja amefunga
mkanda.

Ndege ukajisogeza taratibu kwenye njia yake na kuanza kupaa angani,
huku nikiwa kitini na kazi ya kusima ramani kupitia ‘tv ndogo ya
kwenye kiti’ na kuona tunamaliza anga ya Tanzania kuingia Kenya na
kisha Somalia, baada ya muda usingizi ukanipitia na ilipofika saa 7:30
usiku tulitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamadi mjini Doha nchini
Qatar.

Tukashuka na kuanza kutafuta ndege nyingine ya kuelekea Bangkok nchini
Thailand, ukubwa wa unjwa wa Kimataifa wa Hamadi Doha, ulinishangaza
na kuona alaa kumbe dunia ina mambo mazuri na kila mtu yupo mbio na
baada ya kutembea kwa umbali mrefu hatimaye tulilifikia geti namba
nane, tulilotakiwa kupita ili kuanza safari yetu ya pili.

Mungu alitusaidia na tulitimiza wajibu wetu ikiwamo ukaguzi na kukaa
mapumziko kidogo na ilipofika saa 8 usiku tulitangaziwa na abiria
kuanza ukaguzi wa tiketi zetu kwa ‘zone’ ambayo nami ilinifikia tena
zone namba tatu huku nikiwa na tikiti yangu.

Tulikamilisha taratibu na kuingia ndani ya ndege tukafunga mikanda na
ilipofika saa 8:30 usiku safari ikaanza ya kukata anga na na
tukafanikiwa kufika saa 7 mchana ya siku ya pili na kutua katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Suvarnabhumi ambao ni mkubwa huku
ukiwa unapokea idadi kubwa ya ndege za kimataifa na wageni kutoka
mataifa mbalimbali.

Tuliposhuka tu, wahudumu tuliowakutana nao walianza na salama
Sawadikrapu, wote wakiinamisha mikono yao kwenye kifua na kuinama nami
nikajibu Sadika, kwa kuwa alikuwa ni mwanamama.

Lakini cha kuashangaza kila tulipokuwa tunapita pale uwanjani, raia wa
Thailand nyuso zao zilijawa na tabasamu kiasi kwamba hata mgeni
kujihisi nipo eneo salama na kila nikiulizwa swali na maofisa wa
uhamiaji pale uwanjani nalijihisi kwamba sina tatizo kwa kuwa hawakuwa
ni wenye kukunja uso kama tulivyozoea kwa askari wengine wawapo katika
majukumu yao.

Tulikamilisha taratibu na kuanza kutoka pale uwanjani, kwa kweli
ilikuwa ni safari nzuri huku wenyeji wetu wakiwa ni wenye furaha mno
kwetu wakati wote.

Tulifika hadi Hoteli ya Grande Centre Point na kupokewa na wahudumu
wenye tabasabu wakati wote huku nikiwa na shauku kubwa ya kujua kwa
undani kwa nini watu wake ni wakarimu wakati wote.

Mwenyeji wetu Dararat Weerapong, akatuchukua hadi katika moja ya
mgahawa na kupata mlo wa mchana, lakini wale wahudumu muda wote
wakizunguka kuhakikisha natimiziwa mahitaji yangu.
Siku zangu zote nilizokuwa Thailand nilipata maelezo kadhaa kutoka kwa
mmoja wa marafiki zangu Pratch Rujivanarom, akaniambia kwamba moja yautamaduni kwa watu wa Taifa la Thailand ni tabasamu wakati wote, kwanihata historia inaonesha kwamba Thailand ni nchi ya ‘tabasamu’.

Pia alikwenda mbali zaidi na kunieleza kwamba wananchi wa taifa hilo
wengi wao ni watu wachakarikaji si wa kukaa na kuletewa na hata pindi
wanapokuwa katika biashara zao, muda mwingi huongozwa na ukarimu
unaombatana na tamasabu kiasi cha kujenga imani kwa wateja wao wakati
wote.

“Tabasamu ni sifa kubwa kwetu kwani Thailand ni ‘Business Hub’ kwa
nchi zote za Asia ya Kusini. Ndio maana hii Bangkok ina watu asilimia
30 ya watu wote wa Thailand ambao kwa sasa wanakadiriwa kufikia zaidi
ya milioni 67.

“Lakini hata hivyo, hapa tumeweza kuendelea, tuna treni ya umeme
ambayo inachukua watu wengi mno, pia tuna barabara nyingi zikiwamo za
juu lakini zipo pia njia ya kulipia ‘By pass’, ambazo zimekuwa ni
msaada mkubwa mno,” anasema Rujivanarom.

Kidogo akanipeleka kwenye historia ya taifa hilo na kusema kuwa  nchi
hiyo ilijulikana kama Uthai (Siam) ni nchi ya kifalme katika Asia ya
Kusini – Mashariki.

Imepakana na Laos, Kambodia, Malaysia na Myanmar.

Ina pwani kwenye Ghuba ya Uthai ya Bahari ya Kusini ya China, upande
wa Kusini na Bahari Hindi upande wa Magharibi. Nchi hiyo ina wakazi
zaidi ya milioni 67 hivyo, inashika nafasi ya 20 duniani.

Mji Mkuu na mkubwa ni Bangkok, ukiwa na wakazi zaidi ya milioni nane.
Nchi iliitwa rasmi Siam hadi mwaka 1939, tena kati ya 1945 na 1949.

Neno Thai  linamaanisha ‘uhuru’ kwa Kithai, pia ni jina la kundi kubwa
la watu nchini ambao ni Wathai asilimia 75 – 85, mbali na
Wathai-Wachina asilimia 12.

Tangu Septemba 19, 2006 nchi imekuwa ikitawaliwa na kamati ya jeshi.
Jeshi ilipindua Serikali ya Waziri Mkuu Thaksin Shinawatra, bila
kumwaga damu. Viongozi wa kijeshi walipatana na mfalme kwamba
wataandaa uchaguzi mpya.

Nchini Uthai kuna lugha za asili 73 kati yake, Kithai ndiyo lugha rasmi.

Wathai walio wengi, asilimia 94.6 hufuata dini ya Ubuddha katika
madhehebu ya Theravada. Kusini, mpakani kwa Malaysia, kuna Waislamu
asilimia 4.6 na Wakristo ni asilimia 0.7.

Kwa hakika nimefika Thailand na kushuhudia kuwa ni nchi ya tabasamu
wakati wote huku maendeleo yakishika kasi.

SHIRIKA LA PURPLE PLANET LAAZISHA PROGRAM YA MAFUNZO KWA WANAWAKE NCHINI KOTE

0
0
SHIRIKA lisilo la kiserikali linalojihusiasha na maendeleo ya wanawake kijamii na kiuchumi nchini Purple Planet imetambulisha programu ya mafunzo kwa mwanamke sahihi kwa mwaka 2019 ambayo itahamasisha wanawake kwa nadharia na vitendo kuelekea uchumi wa Viwanda.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa kampuni ya Purple Planet, Hilda Kisoka amesema kuwa Programu hii itawakusanya wanawake pamoja kwaajili ya kuwainua kiuchumi.

"Programu hii kwaajili ya mwanamke sahihi kwa 2019 italenga kuhamasisha wanawake na inalengo la kugusa makundi zaidi ya wanawake 2000 katika sekta binafsi kwa awamu ya kwanza katika mikoa mbalimbali hapa nchini".

Hilda amesema kuwa wanawake wa kanda mbalimbali hapa nchini wajiandae kwaajili ya Program hiyo ambayo itakuwa katika mikoa mbalimali kulingana na kanda zao. 

Kanda ya Pwani ambayo inajumuisha mikoa ya Pwani na Morogoro itafanyika jijini Dar es Salaam, Kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma na Singida programu hiyo itafanyika jijini Dodoma, kanda ya kati kasikazini inayojumisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha itafanyika Arusha, Kanda ya ziwa itafanyika jijini Mwanza.

Hilda amesema kuwa kampuni ya purple planet kwa awamu ya kwanza itaanza kutoa mafunzo kwa miezi mitatu kisha itaendelea tena kwa awamu nyingine.

Program ambazo watakazotoa mafunzo ni fasheni na kubuni ambayo itatolewa na speshoz, Mapishi ambayo yatafanyika kwa Maanjumati na BRAGEN CATERING, Mambo ya Saloon na urembo, itafanyika Dage na Lavy, Uokaji wa Keki itafanyika Melisa School of Bake, Upangaji wa Matukio na urembo yatafanyika Sabrionce event na Bragen, na The Event Crop COMESAVE Dodoma.

Pia usindikaji wa vyakula na bidhaa za majumbani itafanyika kusiga Product, First R&R Supermarkets kwaajili ya masoko, ufugaji na kilimo itafanyika Malemo Farm, Ufugaji wa kuku nutafanyika kuku Project pamoja na kuandda Rasilimali watu itafanyika Top Taget na kazi point.

Hilda amesema katika kufanikisha hiyo Purple Plane wanashirikia na mamlaka za serikali ili kuleta ufanisi katika mafunzo mbalimbali yatakayotolewa ikiwemo, NEEC, JUWADA, SIDO, GS1,TBS, na UTT. 
Hata hiyo Hila amesema kuwa changamoto kubwa wanayokumana nayo ni kuwa na wanawake wachache ambao wanahitaji kujikwamua kiuchumi.

Pia amewaalika wanawake kuhudhulia programu ya mafunzo hayo ili waweze kutatua changamoto zao za masoko, ujuzi na mitaji hata changamoto za kijamii kwa kutumia rasilimali walizonazo bila kusubiri serikali kuelekea uchumi wa viwanda.
,Mkurugenzi wa kampuni ya Purple Planet, Hilda Kisoka akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutamulisha uprogramu ya m,afunzi wa wanawake ili kujikwamua kiuchumi na changamoto za kijamii. kulia ni  Mkufunzi Taasisi ya Purple Planet,Violet Konyani.
Mkufunzi Taasisi ya Purple Planet,Violet Konyani akizungumza na waandishi wa habari jijni Dar es Salaam leo wakati wa kutamulisha programu ya mafunzo kwa wanawake yatakayo fanyika katika mikoa kikanda nchini kote.
Mkufunzi wa mafunzo yanayotolewa na Purple Planet, Breatice Nyalandu  akizungumza na waandishi wa badari wakati wa kutambulisha programu ya mafunzo kwa wanawake yatakayofanyika nchini kote. Amesema mafunzo hayo hayatabagua dini yatakuwa kwa watu wote. 
Mkufunzi wa Shirika la Purple Planet, Sara Pima akifafanua jamo wakati wa kutambulisha wa programu ya mafuzo kwa wanawake wote hapa nchini yatakayomwenzesha mwanamke kujikwamu kiuchumi na changamoto ja kijamii. amafunzo yatakayotolewa kwenye kanda za mikoa yote ya hapa nchini.

Baadhi ya wajumbe na viongozi wa Purple Planet

KONGAMANO LA KIBIASHARA KUFANYIKA JIJINI DAR

0
0
 Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kongamano la biashara baina ya Tanzania na Uganda.
Mratibu wa Kongamano la biashara baina ya Tanzania na Uganda Ali Gugu akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema Jijini Dar es salaam

Na Mwandishiwetu             
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kujitokeza Kwa wingi kushiriki katika kongamano la biashara la Tanzania na Uganda linalotaraji kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema leo Jijini hapa Bashungwa amesema kongamano hilo ambalo litafunguliwa na kuhudhuliwa na wakuu
 wa nchi zote Mbili Tanzania na Uganda.

"Rais Magufuli amemualika Rais Museveni  wa Uganda katika ufunguzi wa mkutano hii ambao utawashirikisha wafanyabiashara zaidi ya 1000 ambao  watapata nafasi ya kujadili namna ya kuongeza  biashara mpya baina ya nchi hizi Mbili" amesema Waziri Bashungwa.

Aidha Waziri Bashungwa ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mikoa ya kanda ya ziwa ambao wengi wao ndio wamekuwa wakifanya biashara Moja kwa Moja na nchi za jirani hili waweze kupata mtandao mpya wa kibiashara.

Ametaja muungano wa kimtandao baina ya Tanzania na Uganda utafungua njia mpya ya Biashara hadi Sudan ya kusini ambao wamekuwa wakifanya biashara na Uganda kila uchwao.

Ametaja muungano wa kibiashara baina ya nchi hizi Mbili utaongeza mabilioni kwa nchi yetu ya Tanzania kwani mpaka Sasa sisi ndio tumekuwa tukiuza zaidi kwao kuliko wao kuuza kwetu.

Amesema kuwa Uganda imekuwa ikitegemea mazao ya chakula kutoka hivyo wauzaji wa nafaka na Wasindikaji wa vyakula wanatakiwa kutumia fursa hii vizuri kwa kutanua masoko yao.

Amemaliza kwa kutoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza Kwa wingi katika kongamano hili.

Rais Dkt. Magufuli azungumza na Watendaji Kata Ikulu Jijini Dar es Salaam

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Watendaji wa Kata zote za mikoa ya Tanzania Bara Ikulu jijini Dar es Salaam.
Watendaji wa Kata zote za mikoa ya Tanzania Bara wakiimba Wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa Mkutano wao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Watendaji wa Kata zote za mikoa ya Tanzania Bara wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Watendaji Kata wakiwa katika mkutano wao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU

MAENEO YA YATAKAYOJENGWA TAASISI ZA UMMA KUWEKWA MIUNDOMBINU YA UMEME

0
0

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wanakijiji wa Lole kabla ya kuwasha umeme katika kijiji hicho katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, mkoani Njombe.
Baadhi wa wanakijiji wa Lole, katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, mkoani Njombe, wakimshuhudia, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( haonekani pichani) akiwasha umeme katika moja ya nyumba za ibada katika kijiji hicho.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Lupembe,Joram Hongoli (kushoto) wakipitia orodha ya vijiji vilivyopata na visivyopata katika jimbo hilo ili vile ambavyo bado viweze kupatiwa umeme

Wanakijiji wa Kijiji cha Ninga, katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, mkoani Njombe,wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kuhusu mradi wa usambazaji wa umeme vijiji (REA), kabla ya kuwasha umeme katika kijiji hicho.


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kulia) akitoa maelekezo ya kuboresha na kuharakisha utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijiji ( REA) kwa wakandarasi wanaotekeleza mradi huo wa Kampuni ya JV Mufindi Power Service Ltd na Hegy Engineering Service Ltd, Shirika na Umeme nchini (Tanesco), na Wakala wa Nishati vijijini REA. 


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (kushoto) akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Ninga, huku watoto nao wakimsikiliza kwa shauku ya kupata umeme.




Baadhi ya wanakijiji wa Ninga, wakipiga pushapu kwa furaha ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli ya kuwapatia wananchi maendeleo ikiwemo nishati ya umeme.

……………………..

Na Zuena Msuya , Njombe

Waziri Nishati, Dkt. Medard Kalemani, amewagiza wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Usambazaji umeme Vijijini, kuweka miundombinu ya umeme katika maeneo yaliyoidhinishwa na Serikali za Vijiji kujengwa taasisi za umma kama vile shule, nyumba za ibada, vituo vya afya pamoja na masoko , hata kabla ya ujenzi kuanza.

Dkt. Kalemani alisema kwa kufanya hivyo kutarahisisha upatikanaji wa huduma ya umeme katika taasisi hizo pindi ujenzi wa majengo utakapokamilika hata baada ya mradi wa usambazaji umeme vijijini kukamilika.

Dkt.Kalemani alitoa agizo hilo, Septemba 1,2019, wakati akiwasha umeme katika Kijiji cha Lole na Ninga pamoja na kukagua maendeleo ya mradi wa usambazaji umeme vijijini katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe mkoani Njombe.

“Wakandarasi wote nchini mnaotekeleza Mradi wa REA, hakikisheni maeneo yaliyoidhinishwa na serikali kujengwa taasisi za umma yanawekewa miundombinu ya umeme,hatutaki kuona taasisi zinajengwa lakini hakuna umeme wakati tayari mradi wa umeme ulikwishapita katika kijiji husika, hii itaendeleza azma ya serikali ya kuwapatia wananchi huduma bora zaidi”, alisema Dkt. Kalemani.

Wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA, awamu ya Tatu Mzunguko wa kwanza katika Mkoa wa Njombe ni Kampuni ya JV Mufindi Power Service Ltd na Hegy Engineering Service Ltd,

Kalemani aliweka wazi kuwa kumekuwa na changamoto kwa taasisi nyingi za umma,Vituo vya Afya pamoja na nyumba za ibada kukosa umeme na maeneo mengine miundombinu ya umeme kupita mbali zaidi, hivyo wahusika kushindwa kuunganishwa na huduma hiyo licha ya mradi wa usambazaji wa umeme vijijini kutekeleza katika maeneo hayo.

Vilevile alisema baada ya changamoto hiyo kutokea, wamebaini kuwa taasisi nyingi zilizokosa umeme ni zile zilizokuwa bado hazijajengwa ama ujenzi wake ulikuwa haujakamilika, kipindi ambacho wa mradi wa usambazaji umeme vijijini unatekelezwa.

Waziri wa Nishati. Dkt.Kalemani alieleza kuwa, maeneo yote yatakayoidhinishwa na serikali kujengwa taasisi za umma, vituo vya afya na nyumba za ibada lazima yawekewe miundombonu ya umeme wakati wa utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijiji unaoendelea sasa.

Aidha ameendelea kuwakumbusha wananchi wote nchini hasa waliopo vijijini kuendelea kulipia shilingi 27,000 ikiwa ni gharama ya kuunganishiwa umeme pia kutandaza nyaya katika nyumba zao kurahisisha zoezi la kuwaunganishia umeme utakapowafikia.

Aliendelea kusisitiza kuwa serikali imetumia gharama kubwa kuhakikisha mradi huo unawafikia na kuwanufaisha wananchi wote hasa wale walio vijijini kwa gharama nafuu, hivyo haitakuwa busara endapo walengwa wa mradi huo watashindwa kuchangamkia fursa hiyo.

Waziri Kalemani, alisesema hadi kufikia Januari, 2020,tayari vijiji vyote vilivyokuwa katika mpango wa kupata umeme wa mradi wa REA awamu ya tatu Mzunguko wa kwanza vitakuwa tayari vimeunganishiwa umeme nchini kote na kuendelea na REA mzunguko wa tatu awamu ya pili ambao ukomo wake ni Juni, 2020. 

VIJANA WATAKIWA KUCHUKUA FOMU KUGOMBEA NAFASI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

0
0

Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Msakuzi Kaskazini Humphrey Shao akizungumza na Vijana Wakati wa maaadhimisho ya Msakuzi Kaskazini ya Kijani.
Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi wa Kata ya Magomeni ambaye ni Muwakilishi wa Iddi Azan akitoa salamu kwa vijana.

Katibu wa umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Msakuzi Kaskazini,Haroun NKanjamba akisoma Lisala kwa Mgeni rasmi.
Vijana walioshiriki katika mkutano wa Msakuzi Kaskazini ya Kijani wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti.

……………….

Na Mwandishiwetu

Wito umetolewa kwa vijana kuchukua fomu na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa,ili kuwa kuwa sehemu ya kuipatia jamii maendeleo na sio kulalamika

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Msakuzi Kaskazini Humphrey Shao alipokuwa akihutubia katika mkutano wa Msakuzi Kaskazini ya Kijani uliyofanyika katika Viwanja vya CCM Makamba.

“Huu ni Wakati wetu vijana hakuna kulalamika na kuwa wabeba mabegi  kwa watu ambao wameshindwa kutatua kero zetu za muda mrefu,sisi kama kundi muhimu kwenye jamii,shime vijana sasa tujitokeze tuchukue fomu na tugombee tuwaoneshe namna ya kutatua matatizo ya jamii yetu”amesema Shao.

Shao ametaja vijana wengi wamekuwa wakirudi nyuma katika nafasi mbalimbali kwa kutishwa ama kuamini kuwa uongozi ni wa Kundi la wazee jambo ambalo Rais wetu Dkt.John Pombe Magufuli amelipiga Vita.

“Rais Magufuli ametuamini Vijana ndio maana katika awamu hii ya tano wapo vijana wengi waliopewa dhamana na wanaendelea kufanya vizuri hivyo sasa tujitokeze tokeze kwa wingi kila mtu katika mtaa wake” Amesema Shao.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Vijana Kata ya Mbezi,Marry Biita ameagiza vijana wote kuendelea kusimama imara na kuyasema yale yote yaliyofanywa na Rais wetu Dk.John Pombe Magufuli katika Kata yetu na nchi nzima kwa ujumla.

Biita ameweka wazi kuwa maboresho ya miundombinu katika Kata ya Mbezi ni zawadi tosha kwa vijana wa CCM katika kata hiyo ambao watapata fursa ya kujiongezea kipato na kujiajiri.

Ametaja mradi wa kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani utapokea watu zaidi ya 5000 kwa siku katika kata ya Mbezi, hivyo vijana  wakae tayari kuhudumia kundi hilo kubwa ili uchumi wetu uzidi kukua .

Nae Mgeni rasmi katika mkutano huo Mh Idd Azzan kupitia mwakilishi wake aliahidi aidi jezi na kiasi cha shilingi laki tatu mara baada ya kununua keki ya Harambee kwa ajili ya ujenzi na maboresho ya ofisi ya chama.

NG'OMBE 22 WAFARIKI PAPO HAPO BAADA YA KUPIGWA NA RADI

0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

NG'OMBE 22 wenye thamani ya shilingi milioni 12 ,wamekufa baada ya Kupigwa na radi iliyoambatana na upepo mkali pamoja na Mvua,katika kijiji cha Kaziramihunda kata ya Gwanumpu wilayani Kakonko mkoani kigoma.

Wakizungumzia tukio hilo wamiliki wa Ng'ombe hizo Abdul Kasungu ,alisema septemba 1 mwaka huu majira ya saa kumi na moja, vijana walikuwa wametoka kuwanywesha maji Ng'ombe katika Kijiji cha msenga ,walipokuwa njiani ulitokea upepo mkali ulioambatana na radi na kuwapiga Ng'ombe 22 ambao walikufa papo hapo.

Alisema kati ya Ng'ombe 20 alizokuwanazo amepoteza Ngombe 16 ambao kila moja alikuwa amuuze kwa shilingi laki sita, alisema wanashukuru kwa kuwa watu waliokuwa wakiwachunga walibaki salama kwa kuwa imetokea ni bahati mbaya hawanabudi ya kulipokea hilo.

Filbert Chibedese alisema yeye Ng'ombe wake sita ndio walikufa wengine walipona,  alisema tukio hilo limewasikitisha kwa kuwa litawarudisha nyuma sana kiuchumi, lakini hawana namna kwa kuwa ni majanga ya kiasili yanayojitokeza bila kutarajia.

Akizungumza na Wananchi hao wakati alipofika katika eneo la tukio Mkuu wa Wilaya ya Kakonko,Kanali Hosea Ndagala alisema tukio hilo ni kama matukio mengine halikutegemea litokee, hivyo watu wanatakiwa kuwa wavumilivu na kutambua kuwa mambo hayo ni mpango wa Mwenyezi Mungu,Kanali Ndagala alitoa pole kwa wote waliokutwa na janga hilo.

" nitoe pole kwa wote mliondokewa na mifugo,ni kweli inaumiza sana na ni hasara kubwa mmeipata, jambo kubwa ni kumshukuru Mungu kwa kuwaponya watu waliokuwa wanawachunga Ng'ombe hao, kikubwa ni uvumilivu msikate tamaa muendelee kupambana haya mambo yanatokea hatuna sababu ya kukata tamaa katika utafutaji poleni sana", alisema Kanali Ndagala.

Aidha aliwataka Wananchi katika kipindi hiki ambacho Mvua zimeanza kunyesha wawe makini na kuepuka kukaa chini ya miti wakati wa radi na Mvua ili kukwepa kupigwa na radi na kusababisha maafa makubwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko,Kanali Hosea Ndagala  akishuhudia NG'OMBE 22 wenye thamani ya shilingi milioni 12  wakiwa wamekufa baada ya Kupigwa na radi iliyoambatana na upepo mkali pamoja na Mvua,katika kijiji cha Kaziramihunda kata ya Gwanumpu wilayani Kakonko mkoani kigoma. 
 Baadhi ya Wananchi wakishuhudia tukio hilo 

  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko,Kanali Hosea Ndagala akizungumza na Wananchi kufuatia NG'OMBE 22 wenye thamani ya shilingi milioni 12 kufa baada ya Kupigwa na radi iliyoambatana na upepo mkali pamoja na Mvua,katika kijiji cha Kaziramihunda kata ya Gwanumpu wilayani Kakonko mkoani kigoma.


RAIS MSTAAFU WA AFRIKA KUSINI THAMBO MBEKI AKUTANA NA VIONGOZI WAANDAMIZI WASTAAFU WA TANZANIA JIJINI DAR

0
0
Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (wa pili kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri Mstaafu, Prof. Mark Mwandosya, Balozi Mstaafu Juma Mwapachu (kulia) pamoja na Balozi Mstaafu Ami Mpungwe walipokutana jijini Dar es salaam hivi karibuni. wa pili kushoto ni Max Boqwana, Afisa Mtendaji Mkuu wa Thabo Mbeki Foundation.

Vodacom yazindua mtandao wa 4G visiwani Zanzibar

0
0

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc imezindua huduma ya intaneti yenye kasi ya 4G visiwani Zanzibar (Pemba na Unguja), ambapo wakazi wa visiwa hivyo sasa watapata fursa ya kipekee kufurahia mtandao wenye kasi zaidi nchini. 

Katika visiwa hivyo Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc ina minara zaidi ya 53 yenye kasi ya 4G, 3G na 2G ambayo inawezesha wakazi hao kufurahia huduma kutokana na uwezo wa vifaa vyao. 

Akizungumza juu ya maendeleo hayo, Mkurugenzi wa kitengo cha Network wa Vodacom, Alec Mulonga alisisitizia kwamba, kampuni hiyo imejikita katika kuipeleka Tanzania kwenye zama za kidijitali na kuhakisha kwamba kila mtu anaunganishwa. 

“Vodacom Tanzania inaamini katika nguvu ya teknolojia kwenye kuleta maendeleo na kutoa fursa mpya. Kuunganisha ngome hii ya utalii – Zanzibar na huduma yetu ya 4G kutaleta fursa mpya za maendeleo kwani tutakuwa tumeifungua katika soko la dunia na huduma nyingine za kimtandao kama elimu, afya, kilimo na usalama pamoja na kukuza uchumi wa Wazanzibari,” alisema Mulonga. 

Uwepo wa intaneti umebadilisha namna ya upatikanaji wa taarifa na ufanyaji biashara. Na kwa upande wa utalii, intaneti ina uwezo wa kuwafanya watalii kufurahia zaidi safari zao nchini Tanzania na vile vile kuwaongezea uwezo wa kupata huduma za malazi kwa gharama nafuu kupitia mtandao. Pia ni chombo cha kuwezesha utangazaji wa biashara na mawasiliano kati ya watoa huduma na watu wengine. 

Kwa zaidi ya miaka 20, Vodacom Tanzania imewekeza katika kuboresha mtandao wao ili uweze kuwafikia na kuwaunganisha mamilioni ya Watanzania. Upatikanaji huu wa mtandao wenye kasi utawezesha ufanisi wa utendaji kazi wa sekta ya utalii visiwani Zanzibar. 

Kwa sasa, kampuni inajivunia kutoa huduma za kimtandao kwa asilimia 90% ya idadi ya watu nchini Tanzania, ikiwa inamiliki zaidi ya minara 3000 ya 2G, 2500 ya 3G na 1000 ya 4G, kati ya hiyo minara 57 ikiwa ya 4G+ ambayo hutoa mtandao wenye kasi kuliko zote hapa nchini. 

Kwa upande wake, Mwanakheri Abdulswamadu, mkazi wa Mchambawima Unguja alieleza furaha yake kuhusu upatikanaji wa mtandao huo wenye kasi zaidi, “Ninafanya biashara na nina wateja ambao wako katika sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi, na hivyo kupitia mtandao huu wenye kasi itakuwa rahisi kwangu kuwasiliana nao na kuwashawishi kununua bidhaa zangu.” 

“Tunachokiona leo ni matokeo ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa mtandao wetu, Mfano; mwaka uliopita tuliingia mkataba wa kukodisha mkongo wa Taifa (NICTBB) na kuboresha vituo vyetu kote nchini. Tumedhamiria kuwekeza kwenye miundombinu ya mtandao ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu upande mawasiliano na pia kupunguza utofauti wa kidijitali, pia kuimarisha uwezo wa ushindani kati ya mashirika ya mawasiliano hapa nchini,” alihitimisha Mulonga.

Waziri HASUNGA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU WA MAFUNZO YA AGRO STUDIES MJINI JERUSALEM NCHINI ISRAEL

0
0
Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi Cheti Dayana Novat wakati wa mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ICC (Jerusalem International Conventional Center) mjini Jerusalem nchini Israel, leo Tarehe 2 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal,Wizara ya Kilimo).
Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akishiriki mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika mjini Jerusalem nchini Israel, leo Tarehe 2 Septemba 2019.
Sehemu ya washiriki wakifuatili mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ICC (Jerusalem International Conventional Center) mjini Jerusalem nchini Israel, leo Tarehe 2 Septemba 2019. 
Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi Cheti Bazil Materu wakati wa mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika (Jerusalem International Conventional Center) mjini Jerusalem nchini Israel, leo  Septemba 2,2019. 
Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na mawaziri, Naibu Mawaziri na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali waliohudhuria mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika mjini Jerusalem nchini Israel, leo Tarehe 2 Septemba 2019. 


Na Mathias Canal, Jerusalem-Israel

Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo Tarehe 2 Septemba 2019 ameshiriki mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika mjini Jerusalem nchini Israel na kuwatunuku vyeti vya kuhitimu wanafunzi 45 kutoka Tanzania.

Katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa ICC (Jerusalem International Conventional Center), Waziri Hasunga amewapongeza vijana hao kwa kuhitimu masomo yao hivyo amewaahidi kuwa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipanga kuboresha mazingira wezeshi kwenye sekta ya kilimo hivyo wanayo nafasi nzuri kuutumia ujuzi walioupata kuboresha kilimo watakaporejea nchini Tanzania.

Mahafali hayo yatajumuisha vijana 1600 kutoka mataifa zaidi ya 12 ambapo kati ya hao vijana 45 ni watanzania, miongoni mwao wanawake wakiwa ni 9 na wanaume ni 36.

Waziri huyo wa kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepewa jumla ya nafasi 100 kwa ajili ya kupeleka vijana wa kitanzania kujifunza kilimo cha kisasa nchini Israel hivyo fursa hiyo ni muhimu kwani vijana hao wa Tanzania wamepata ujuzi wanachotakiwa kufanya ni kutumia ujuzi huo kwa manufaa makubwa nchini mwao.

Akizungumza na mtandao wa WazoHuru Blog mara baada ya kuwakabidhi vyeti wahitimu hao Mhe Hasunga amesema kuwa kupatikana kwa nafasi hizo 100 ni kutokana na ombi la Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa serikali ya Israel ili kuwawezesha vijana wengi wa kitanzania kujifunza mbinu na teknolojia za kilimo cha kisasa.

Kadhalika, Waziri Hasunga atakutana na kurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Agro Studies ambapo miongoni mwa mazungumzo muhimu itakuwa ni pamoja na kumuomba uwezekano wa kuongezewa nafasi zaidi ili vijana wengi wa kitanzania waende kujifunza mbinu mpya za kilimo nchini Israel.

Pia, Mhe Hasunga atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo nchini Israel kujadiliana nae maeneo mbalimbali na fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya kilimo nchini Tanzania.Katika mkutano mwingine, Mhe Hasunga atakutana na kufanya mazungumzo na wadau wawekezaji wakubwa wa sekta ya kilimo nchini Israel ili kuwaeleza fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.

Katika ziara hiyo tarehe 4 Septemba 2019 Mhe Hasunga atashiriki mapokezi ya vijana 100 ambao wapo nchini Israel kwa ajili ya kuanza mafunzo yao.Leo tarehe 2 Septemba 2019 ni siku ya pili ya ziara ya kikazi ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga nchini Israel kati ya siku sita atakazokuwa nchini hapa.

RAIS DKT SHEIN AHUTUBIA MKUTANO WA 50 WA MABUNGE YA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika leo unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika leo unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
BAADHI ya Wajumbe wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi rasmi wa Mkutano huo unaofanyika Hotelini hapo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Zubeir Ali Maulid na Spika wa Bunge la Kenya pia Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji Chama cha Mabunge Justin Maturi (katikati) wakiongozwa na Mpambe Mwinyi Haji Abu(mwenye Siwa) wakati leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiingia katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kufungua Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Spika wa Mabunge wa Nchi mbali mbali wakisimama wakati Wimbo wa Taifa wa Ukipigwa katika ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai (kulia) Spika wa Bunge la Kenya pia Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji Chama cha Mabunge Justin Moturi (katikati) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Zubeir Ali Maulid (wa pili kushoto) na Spika wa Bunge la Uganda Rebecca Alitwala Kadaga wakisimama wakati Wimbo wa Taifa wa Ukipigwa katika ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
BAADHI ya Wajumbe wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika wakiwa katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar uliofunguliwa leo rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.Picha na Ikulu

J FILM 4 LIFE KUTAFUTA VIPAJI VYA WATOTO SEPTEMBA 14 LIDERS JIJINI DAR

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa J FILM 4 LIFE, Jenifer Kyaka, alimaarufu kama Odama akizungumza mara baada kuzindua siku ya kuanza kutafuta vipaji vya watoto watakao igiza filamu ya watoto. Siku ya kuanza kutafuta vipaji vya watoto Septemba mwaka huu 14 katika viwanja vya Club Liders jijini. 

Mkurugenzi Mtendaji wa J FILM 4 LIFE, Jenifer Kyaka, alimaarufu kama Odama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

KATIKA kuendeleza tasinia ya filamu nchini kampuni ya J FILM 4 LIFE inaendeleza dhamila hiyo kwa kutafuta vipaji vya watoto wa kuanzia miaka mnne hadi miaka 14. 

Mkurugenzi Mtendaji wa J FILM 4 LIFE, Jenifer Kyaka, alimaarufu kama Odama, amesema kuwa katika sekta ya filamu kwa mara ya kwanza wanampango wa kuvumbua na kukuza vipaji vya watoto hapa nchini. 

“Sote tunafahamu kuwa tasnia ya filamu nchini kwetu imeendelea kukua na kuboreka hasa katika miaka ya hivi karibuni. Sisi wasanii wa Tanzania na ubora wa kazi zetu za sanaa umeimarikaa mara dufu kupelekea kuweza kuaminika zaidi ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu”. Amesema. 

“Kundi kubwa la watoto wanatakiwa kushirikishwa katika jamii ili kusiwepo na ubaguzi wa kuwa umri gani unaweza kutoa ujembe kwenye jamii kupitia sanaa”. Amesema Jenifer. 

Jenifer amesema kuwa tamthilia hiyo ambayo itakayohusu watoto italenga maudhui ya watoto pia na waigizaji ni watoto wenyewe ndio maana wameona umuhimu wa kutafuta vipaji vya watotoili maudhui yaendane na waigizaji. 

Tamthilia hiyo italenga watoto na ikielezea zaidi maisha ya watoto katika mambo mbalimbali kama vile elimu, afya, migogoro ya kifamilia kwa watoto, dini, miradhi, mila na utamaduni pamoja na mila mbalimbali, unyanyasaji wa watoto ubakwaji watoto ikiwa pamoja na watoto wa mitaani itagusa maisha ya uhalisia wa maisha ya mtaani na familia nyingi hapa nchini. 

Mchakato wa kupata watoto wenye vipaji wa kuigiza filamu ya watoto utafanyika katika viwanja vya clabu liders Septemba 14 kuanzia saa tatu kamili jijini Dar es Salaam. 

Pia Jenifer amewaomba wazazi kuwaruhusu watoto wao kwaajili ya kuja kufanya usahili wa mchujo wa watoto watakasoigiza filamu hiyo. Hata hivyo amewaalika wadau wa masuala mbalimbali ya watoto kuja kukutana na wadau wengine kama wadau wa elimu. 
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images