Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

JAFO AMALIZA MGOGORO UBWE SEKONDARI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo leo hii Agoust 16 amemaliza mgogoro wa wanafunzi uliokuwa umeota sura mbaya ya kuhatarisha hali ya amani shuleni hapo ambapo mgogoro huo ulianza tangu Augost 10 mwaka huu. Waziri huyo wa TAMISEMI alitoa onyo kwa walimu ambao inaonekana wameshindwa majukumu yao ya kiuongozi hadi shule kuingia katika mapigano makubwa kati ya kidato cha tano na kidato cha sita pamoja na kuchipuka kwa tofauti za mitazamo ya kidini shuleni hapo.

Wanafunzi na walimu wa shule hiyo wamemshukuru sana waziri huyo kwani walikiri kwamba uhasama shuleni hapo ulikuwa mkubwa sana.

Waziri huyo alifanikiwa kuongea na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiwa pamoja na kamati ya Wilaya ya Moshi,Bodi ya shule wakiwa pamoja na walimu wote wa shule hiyo, na kuhitimisha na kikao cha wanafunzi.
Jafo alimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Ngwila kuendelea kufanya uchunguzi wa waanzilishi wa chokochoko hizo ili watakao bainika wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Aidha,Jafo alimaliza ziara hiyo shuleni hapo kwa kuunda timu kumi zenye mchanganyiko mbalimbali ambazo zitashindana katika michezo mbalimbali na kuzipa majina ya Tanzanite,Gold,Diamond,Kilimanjaro, Manyara,Serengeti,Ngorongoro,Mikumi, Nyerere Park, na Ruaha kitendo ambacho kilisababisha shangwe kubwa kwa wanafunzi hao.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AWASILI JIJINI DAR ES SALAAM KUHUDHURIA MKUTANO WA SADC

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb.) kuhudhuria Ufunguzi wa Mkutano wa SADC, unaotarajiwa kufanyika kesho katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijinin Dar es Salaam.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jiji Dar es Salaam, kuhudhuria Ufunguzi wa Mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika kesho katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kulia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Damas D. Ndumbaro, na kushoto Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakielekea katika chumba cha mapumziko Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu)

AIRTEL YASHIRIKI MKUTANO WA SADC, INAHUDUMIA NCHI 5 KATI YA 16 ZA SADC

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imesema inajivunia kuwa sehemu ya mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika –SADC na kutoa huduma bora za mawasiliano kwa wajumbe wanaoshiriki Mkutano huo.

Ushiriki wa Airtel katika Mkutano huo ni pamoja na kutoa line za simu za mtandao huo Bure, kutoa huduma ya Airtel Money yaani kutuma na kupokea pesa kwa wajumbe ambao wanatoka katika nchi ambazo Airtel inatoa huduma na pia wanatoa huduma kwa wateja wakubwa ambao wanahudhuria Mkutano wa SADC.

Mkurugenzi Kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano amesema, kuwa watumiaji wa Mtandao wa Airtel kutoka katika nchi za Zambia, Shelisheli, Malawi, Madagascar pamoja na Tanzania ambao ni wenyeji wanaendelea kufurahia huduma za mawasiliano kupitia mpango wa One Network.

Bi Singano amesema kuwa wameamua kutoa laini za Airtel bure kwa wajumbe wa SADC ili waweze kufurahia huduma za mawasiliano wakiwa hapa nchini na pia kuwawezesha kufurahia huduma nyingine.

Kwa upande wake Mwakilishi wa kitengo cha wateja wakubwa wa Airtel Alice Mashiku amesema, kampuni hiyo inashiriki Mkutano wa SADC ili kuwahudumia wateja wao wakubwa kutoka katika nchi za Zambia, Malawi, Shelisheli na Madagascar na pia kutoa huduma mbalimbali kwa wajumbe wengine wa Mkutano huo.

WEZI WA MBOGA MBOGA MRADI WA TASAF KATIKA SHULE YA MSINGI ELERAI WAKAMATWE

$
0
0
Na Jusline Marco, Arusha

Afisa Tarafa wa Elerai Titho Cholobi ameagiza wezi wa mboga mboga katika bustani za mradi unaofadhiliwa na TASAF katika shule ya msingi ya Elerai wakamatwe na kuchukuliwa hatua kwani wamehujumu fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya kusaidia kaya masikini ziweze kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza katika ziara yake ya kutembelea miradi inayotekelezwa na serikali ikiwemo mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Elerai,Afisa huyo ameshangazwa na kitendo hicho ambacho kinawakatisha tamaa kinamama wanaolima bustani hizo pamoja na wawezeshaji wa mradi huo.

Cholobi amesema kuwa mradi huo hauna haja ya kuwekewa mlinzi maalumu kwani utaongeza gharama za utekelezaji hivyo polisi jamii wanapaswa kuulinda mradi kwa kushirikiana na wananchi kwani fedha hizo niza serikali pamoja na wadau wa maendeleo.

Vilevile ameuagiza uongozi wa kata kukutana na kujadili juu ya namna ya kuwashirikisha wadau wa maendeleo katika kumalizia miradi ambayo bado haijakamilika ili iweze kukamilika ikiwemo ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule hiyo ya msingi.

Naye Mtendaji wa kata ya Lemara Johari Kitara amesema kuwa mradi huo ulianzishwa na Tassaf kwa lengo la kuwakomboa kinamama ili wapate kipato na kujiendeleza hivyo changamoto hiyo itashughulikiwa.
Afisa tarafa Erelai Mkoani Arusha akitoa maelekezo kwa askari polisi kuhusu ulinzi wa bustani hizo.

RAIS WA ZAMBIA EDGAR LUNGU AONGOZA KIKAO CHA SIASA,ULINZI NA USALAMA CHA SADC TROIKA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Rais wa Zambia Mh. Edgar Changwa Lungu,ambaye ni  Mwenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) pichani kati akiongoza kikao cha ulinzi na usalama kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC (SADC) kilichofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika – SADC, Dkt Stergomena Tax.
Rais wa Angola Mh. Joao Lourenco Mwenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) anayemaliza muda wake akiwa katika kikao hicho kilichofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zimbabwe Mh. Emmerson Dambudzo Mnangagwa anayechukua nafasi ya Uenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) akipitia baadhi ya nyaraka za kikao hicho kilichofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Wanaoshuhudi pichani nyuma ni baadhi ya wajumbe wa kikao hicho 
Wanaoshuhudi pichani nyuma ni baadhi ya wajumbe wa kikao hicho.Picha na Michuzi JR.

INDELIBLE MARK YAZINDUA THINNO CHALLENGE KUCHOCHEA UBUNIFU KWA VIJANA

$
0
0
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja

Takribani vijana sitini (60) wanatarajiwa kuwasilisha Mawazo yao ya kibunifu katika shindano la kutekeleza malengo ya Maendeleo endelevu ya dunia hasahasa yakijikita lengo namba tatu, nne, tano, na nane. Malengo hayo yanazungumzia afya bora, elimu bora, usawa wa kijinsia na kazi za staha na ukuaji wa uchumi.

Bw.Naamala Samson akitoa mada kuhusu malengo ya Maendeleo endelevu

Shindano hilo lililopewa jina la THINNO CHALLENGE ikiwa ni muunganiko wa Think and Innovate yaani ‘Tafakari na Ubuni’, limezinduliwa rasmi tarehe 10 Agosti 2019 na shirika la Indelible Mark Movement. Tukio hili lilifanyikia kwenye ukumbi wa BUNI HUB iliyopo jengo la COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam.

Katika uzinduzi huo vijana kutoka vyuo mbalimbali zaidi ya kumi na sita (16) vya ndani na nje ya Tanzania na wajasiriamali mbalimbali waliweza kuhudhuria kupata mafunzo kuhusu malengo ya Maendeleo endelevu ya Dunia pamoja na kuhamasishwa kuwa na ari ya uthubutu na Ubunifu.

Bi.Alice Norberth kutoka Indelible Mark akiongea na washiriki

“Tunapotaka kuwa na kesho njema ni lazima kuhusisha vijana katika michakato yote hivyo ni lazima kuhakikisha wanaelewa vizuri matatizo kwenye jamii na kuja na Mawazo ya kibunifu kuyatatua Matatizo hayo, ndio maana tumeanzisha shindano hili, alisema Bi.Alice Norbeth, mwanzilishi wa shirika la Indelible Mark.

Kwa upande wake mkufunzi wa vijana hao, Bw.Naamala Samson ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Bella Africa, alisema,”Vijana ni zaidi ya asilimia sitini (60) ya idadi ya watu duniani hivyo ni muhimu kutumia vema nguvu kazi hii wajue nafasi yao katika utekelezwaji wa malengo ya Maendeleo endelevu ya dunia ili washiriki bila kuachwa nyuma”.

Mmoja wa washiriki hao, Bw.Issa Chapanga alionesha furaha yake na alisema yamemuwezesha kujitambua zaidi kwani palikuwa na mada kuhusu ‘kujitambua na uthubutu’. Mada hii iliwasilishwa na Dr.Nelsen Amar (PhD). Aliongezea kwamba pindi vijana wasikiapo fursa wasiziachie na wazichangamkie kwa haraka ili kujiletea Maendeleo wao binafsi na jamii kwa ujumla.

Shindano hili la THINNO CHALLENGE linatarajiwa kumalizika ifikapo mwishoni mwa mwezi wa tisa, ambapo washindi watapewa zawadi ikiwemo vyeti, tuzo na mafunzo mbalimbali kuwawezesha kutekeleza Mawazo yao.

Shirika la Indelible Mark Movement linaendesha shindano hili pamoja kwa ushirikiano na Taasisi mbalimbali kama Buni Innovation Hub, Bella Africa Consultancy, Raleigh Tanzania, Bridge For Change, ICS na linakaribisha wadau wengine kuunga mkono jitihada hizi kuongeza hamasa kwa vijana kuwa wabunifu.

SADC YAIPONGEZA TANZANIA KWA KUWA NCHI PEKEE KATIKA JUMUIYA AMBAYO UCHUMI WAKE UNAKUWA KWA ASILIMIA SABA

$
0
0
 Na Said Mwishehe,Michuzi TV
JUMUIYA ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imepongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa nchi pekee ya SADC iliyoweza kufikia kiwango cha asilimia Saba (7) katika ukuaji wa uchumi wake  mwaka 2018 kiwango  kilichowekwa na SADC .

Pongezi hizo za SADC zimetolewa na Katibu Mkuu wake Dk.Stergomena Tax wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 39 wa Jumuiya hiyo ambao umehusisha wakuu wa nchi na viongozi wa Serikali unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Dk.Tax amesema kwa nchi za jumuiya hiyo pamoja na mambo mengine kwenye eneo la uchumi kuna malengo ambayo yamewekwa kwa nchi wanachama na Tanzania ni nchi pekee ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia saba na hivyo wanastahili kupongezwa.

Amefafanua nchi za SADC zimejiwekea lengo la kukuza uchumi na hivyo wameweka vigezo vya kuwa na uchumi mpana na Tanzania imetimiza vigezo hivyo na kuwa nchi ya kwanza kwa ukuaji uchumi ukilinganisha na nchi nyingine ingawa nazo zinapaswa kupongezwa kwani zinafanya vizuri.

"Nchi za SADC uchumi wake unakwenda vizuri sana na takwimu zinaonekana kwenda vizuri katika ukuaji wa uchumi.Hii imetokana na baadhi ya nchi kudhibiti mfumuko wa bei.

" Lakini naomba niseme kwa uchumi mpana wa SADC na nchi wanachama wanafanya vizuri na
Tanzania ni nchi pekee ambayo imefikia asilimia saba
 ya ukuaji wa uchumi,"amesema Dk.Tax.

Wakati huo huo Dk.Tax alipokuwa anazungumzia mikakati ya jumuiya hiyo na hasa katika eneo la sekta ya nishati ya umeme,ametumia nafasi hiyo kuipongeza Tanzania kwa namna ambavyo imeamua kwa vitendo kuhakikisha inakuwa na umeme wa uhakika na unaojitosheleza.

Amesema wanaipongeza Tanzania kutokana na mradi mkubwa wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji ambao ujenzi unaendelea na kuongeza mradi huo utakuwa na tija kwa nchi za jumuiya hiyo kwani wanaamini utakaopatikana mbali ya kutumika Tanzania utaunganishwa katika nchi za SADC.
Baadhi ya Wakuu wa nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wakifuatilia yanayojiri kwenye mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali ulioanza leo Jumamosi Agosti 17,katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wakifuatilia yanayojiri kwenye mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali ulioanza leo Jumamosi Agosti 17,katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.













LIVE:Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na serikali wa SADC, Tanzania.


MWINYI, MKAPA, KIKWETE, KARUME WAHUDHURIA MKUTANO KUSHUHUDIA RAIS MAGUFULI ATAKAVYOKABIDHIWA UENYEKITI WA JUMUIYA YA NCHI ZA SADC

$
0
0
 Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii

MARAISI wastaafu wa Serikali ya Tanzania wamehudhuria Mkutano Mkuu wa 39 unaofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  kushuhudia Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk.John Magufuli akikabidhiwa Uenyekiti wa jumuiya hiyo.

Katika mitandao ya kijamii baadhi ya watu wasiokuwa na njema walikiwa wakizusha kuwa Dk.Magufuli amesusiwa mkutano huo na watangulizi wake.Hata hivyo uzushi wao umekosa mashiko kwani viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo marais hao wote wastaafu wamehudhuria mkutano huo wa kihistoria.

Marais wastaafu ambao wamehudhuria ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye ni Rais ww Serikali ya Awamu ya Pili,Benjamin Mkapa ambaye ni Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu,Jakaka Kikwete aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne na kwa upande wa Zanziabar Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Amani Karume.

Mbali ya wastaafu hao kuwemo kwenye mkutano huo ambao pia wametambulishwa kwa wageni mbalimbali kutoka nchi 15 za jumuiya hiyo,pia viongozi wengine wa Serikali ya Tanzania waliohudhuria ni Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Balozi John Kijazi,mawaziri, viongozi wa ngazi mbalimbali wastaafu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda.Pia wamehudhuria watu mashuri wa ndani na nje ya Tanzania.

Pamoja na shughuli mbalimbali ambazo zinaendelea kwenye mkutano wa jumuiya hiyo ambao utafanyika kwa siku mbili,tukio ambalo linasubiriwa na Watanzania wengi ni kuona Rais Dk.Magufuli anakabidhiwa Uenyekiti wa SADC.
Nafasi hiyo ya Uenyekiti wa SADC kwa Tanzania mara ya mwisho ilishikiliwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa miaka 16 iliyopita na sasa anakwenda kukabidhiwa Rais mchakazi Dk.Magufuli.

Hata hivyo nchi mbalimbali za jumuiya hiyo zimeonesha matumaini na imani kubwa kwa Rais Magufuli hasa kutokana na utendaji wake tangu akiwa Rais ambaye anaamini katika wananchi kufanya kazi na nchi kujitegemea.

Pia amekuwa na kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda ambayo itaipeleka nchi uchumi wa kati.Kwa nchi za SADC moja ya mkakati wao ni kuhamasisha viwanda kwa nchi wanachama kazi ambayo Rais Magufuli ameianza kabla ya kukabidhiwa uenyekiti,hivyo nchi za jumuiya hiyo zinaamini akiwa Rais Magufuli atawafikisha kwenye nchi ambazo uchumi wake utatokana na viwanda.

TBS YAENDELEA KUTOA ELIMU KATIKA WIKI YA UWEKEZAJI KAGERA

$
0
0
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetumia Wiki ya Uwekezaji mkoani Kagera kutoa elimu ya viwango kwa wajasiriamali na umuhimu wa kupata alama ya ubora  ambayo inatolewa bure.

Akizungumza na washiriki wa maadhimisho ya Wiki ya Uwekezaji iliyoanza Agosti 12 ikitarajia kumalizika Agosti 18 Afisa Uhusiano   Neema Mtemvu, alisema gharama za wajasiriamali kupata alama za ubora ni bure, kwani zinalipwa na Serikali.

Alisema wajasiriamali wakishapata barua ya utambulisho kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) na kuipeleka TBS, mchakato wa kuwapatia alama ya ubora unaanza mara moja.

"TBS inatambua mchango wa wajasiriamali katika kukuza pato la taifa na kutengeneza ajira kwa wananchi  wengi, ndiyo maana tuna mchakato endelevu wa kutoa elimu kwa wajasiriamali kwa kuwa na hilo ni sehemu  ya majukumu yetu ili waweze kupata alama ya ubora," alisema Mtemvu.

Alisema katika kuelekea uchumi wa viwanda ni lazima kuzingatia viwango, ndiyo maana wamekuwa wakishiriki maonesho mbalimbali ikiwemo wiki ya uwekezaji mkoani Kagera kwa ajili ya kutoa elimu.

Mtemvu alitoa wito kwa wajasiriamali akisema suala la wao kukidhi matakwa ya viwango vya kitaifa kwa bidhaa wanazozalisha na zinazosindikwa ni la msingi kwa kuwa ndiyo njia pekee ya kupanua wigo wa masoko ya bidhaa zao ndani na nje ya nchi.

Hii ni fursa muhimu ambayo inamlenga kumwinua mzalishaji aweza kushindana na kuuza bidhaa zake bila woga," alisisitiza.

Pia, Mtemvu alisema katika wiki ya uwekezaji wamepata fursa kuwapa taarifa washiriki kuwa baadhi ya majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ya chakula na vipodozi sasa hivi yamehamia TBS.

"Serikali ya Awamu ya Tano imeliona hilo na kwa hatua hiyo sasa inakuwa ni rahisi mno kupata alama ya ubora, kwani ukishapata alama ya ubora utaweza kufanya biashara na vile vile ule mzunguko uliokuwepo awali wa kuzunguka wa kwenda TFDA halafu urudi TBS utakuwa umepungua," alisema Mtemvu na kuongeza kwamba;

"Tunawasisitiza wajasiriamali na wafanyabishara wa mkoa wa kufika ofisi za shirika hizo kupata alama ya ubora." Alitoa mwito kwa Wakazi wa Kagera kuhakikisha wanatumia bidhaa zenye ubora, hasa kwa kuzingatia mkoa huo unapakana na nchi jirani, hivyo bidhaa nyingi zinaingia.
 Afisa Mahusiano Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Neema Mtemtu akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika banda la TBS kwenye Maonesho ya Wiki ya Uwekezaji Kagera inayofanyika katika Viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Bukoba Mkaoni Kagera yatakayofikia tamati  kesho Agosti 18, 2019.

NAIBU WAZIRI BASHE: BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO (CPB) KUWA KIUNGO WA BIASHARA YA MAZAO YA CHAKULA BAINA YA KENYA NA TANZANIA

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kikao cha kwanza baina ya timu ya wataalamu wa masuala ya Mazao ya Chakula hapa nchini ikiongozwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na ya wenzao kutoka Kenya zinakutana hapa nchini leo Agosti 17, 2019 ili kujadiliana namna bora ya kufanya biashara ya mazao hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana usiku Agosti 16, 2019 kwenye ofisi za Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), jijini Dar es Salaam, Mhe. Bashe alisema, kikao hicho ni makubaliano baina ya nchi hizo mbili kukutana na kujadili namna gani wafanyabiashara wa Kitanzania na wenzao wa Kenya watafanya  biashara ya mazao ya chakula na iwe biashara endelevu.
“Biashara tayari imekwisha anza na wakati tunaendelea mpaka sasa wenzetu wa Kenya wamekwishanunua jumla ya tani 34,000 kupitia kwa wafanyabiashara wetu na biashara hiyo inaendelea.” Alifafanua.
Alisema timu ya wataalamu kutoka Tanzania itaongozwa na watu kutoka Wizara ya Kilimo, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) ili wakae chini na wakubaliane utaratibu wa namna gani  wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa Kenya watafanya biashara ya mazao ya chakula.
“Sisi Wizara ya Kilimo jukumu letu ni kufanya mambo makubwa mawili, kuhamasisha uzalishaji wa mazao na kufungua masoko ya wakulima wetu ili waweze kufanya biashara.” Alifafanua.
Alisema katika kikao hicho wametaka mamlaka za viwango za Kenya na Tanzania zijumuishwe kwenye majadiliano hayo ili wazalishaji wa sembe waliosajiliwa Tanzania waweze kusajiliwa Kenya Bureau of Standards ili bidhaa zao ziweze kwenda katika soko la Kenya bila vikwazo vyovyote.“Tunatengeneza Government Agreement ambayo itaonyesha mpango kazi (frame work) ya namna biashara hii itafanyika, tumeshaiteua Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ambayo ndiyo itakayokuwa kiongozi msimamizi na kiungo wezeshi katika biashara hiyo.” Alibainisha Mhe. Bashe.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (katikati), akiwa kwenye kikao baina ya ujumbe kutoka Kenya na wataalamu kutoka Bodi ya Nafaka na Mazao MchanganyikoTanzania (CPB) kwenye kituo cha Uewekezaji Nchini (TIC) jijini Dar es Salaam. Timu ya wataalamu kutoka Kenya na ile ya Tanzania zinakutana leo kujadili namna bora ya kuwezesha wafanyabiashara wa nchi hizo mbili kufanya biashara ya mazao ya chakula kwa njia rahisi na rasmi.
 Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Bw. Valerian Mablangeti (aliyesimama), akizungumza kwenye kikao hicho.
 Naibu Waziri Bashe (katikati), na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Bw. Valerian Mablangeti, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kilimo, kutoka Wizara ya Kilimo Nchini Kenya, Bw.Badu Katelo, wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe kutoka Kenya.
Naibu Waziri Bashe, akiwa katika picha ya pamoja kati ya wataalamu wa CPB na ujumbe kutoka Kenya 

MWENYEKITI ALIYEMALIZA MUDA WAKE SADC DK.GEINGOB AHIMIZA NCHI WANACHAMA KUWASHIRIKISHA VIJANA KULETA MAENDELEO

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MWENYEKITI ambaye amemaliza muda wake wa kuiongoza Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) Rais wa Namibia Dk.Hage Geingob amezitaka nchi wanachama kuhakikisha vijana wanapewa kipaumbele katika nyanja mbalimbali kwa ajili ya kuleta maendeleo.

Amesema robo tatu ya wananchi wa jumuiya hiyo wana umri chini ya miaka 27 na hivyo kundi hilo la vijana likipewa nafasi kwenye zao kuna uwezekano mkubwa kwa nchi hizo kupiga hatua.

Dk.Geingob ameyasema hayo leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kabla ya kukabidhi uenyekiti wa SADC kwa Rais wa Serikali ya Tanzania Dk.John Magufuli.

Ambapo wakati anazungumzia mikakati mbalimbali ya jumuhiyo ili ipige hatua kimaendeleo ameeleza umuhimu wa vijana kupewa nafasi ya kushiriki kikamilifu katika msafara wa maendeleo

Amesisitiza robo tatu ya wananchi wa jumuiya hiyo ni vijana, hivyo wakitumika vizuri itasaidia kuleta maendeleo.

"Ni muhimu nchi zetu zikaweka mkazo na kutia maanani vijana kupata nafasi.Wanao uwezo mkubwa ulioambatana na ubunifu.Hivyo lazima tuwatumie kikamilifu kwa maendeleo yetu.

", Ukweli ni kwamba lazima twende pamoja na vijana wetu, tushirikiane kwa kila hatua.Naamini vijana wakitumika kikamilifu nchi zetu zitapiga hatua kubwa kimaendeleo.Tunayo changamoto ya ajira kwenye nchi zetu,vijana wamekuwa wakikimbilia nchi za Ulaya,umefika wakati wa kuwashirikisha vijana kutatua changamoto zetu," amesema.

Mbali ya kuzungumzia umuhimu wa vijana kutumika kuleta maendeleo,Mwenyekiti huyo aliyemaliza muda wake ameeleza haja ya nchi hizo kuweka mikakati ya kuboresha miundombinu na huduma za jamii kwa ajili ya wananchi huku akihimiza uongezaji thamani kwa mazao yanayozalishwa kwa nchi wanachama.

Pia amesema kuna haja ya kuwepo na mfumo thabiti wa kiabiashara baina ya nchi hizo na kwamba kwa kufanya hivyo uchumi utaimarika na kupiga hatua.

Wakati huo huo amesema kuna kila sababu ya kuongeza jitihada za kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafanikiwa.Ametumia nafasi hiyo kueleza Serikali za jumuiya hiyo kuwa na sera ambazo zinakuza uchumi wa wananchi na kwamba sekta binafsi zipewe nafasi ya kushiriki kuleta maendeleo.

"Sekta binafsi ipewe nafasi yake.Tukizipa nafasi sekta binafsi tutapiga hatua ya maendeleo kwa nchi zetu," amesema Dk.Geingob na kuongeza jambo la kufurahisha nchi hizo zimeendelea kushirikiana hatua kwa hatua.

Akizungumza zaidi kuhusu jumuiya hiyo Dk.Geingob amesema kwamba nchi za SADC zinatambua na kuthamini mchango wa Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Julius Nyerere kwa namna ambavyo alijitoa kufanikisha nchi nyingi za Afrika zinakuwa huru.

Pia amezungumzia ukuaji wa demokrasia kwa nchi za jumuiya na kufafanua ndio maana nchi nyingi marais wake wamepatikana kutokana na chaguzi huru na leo wameshiriki mkutano wa 39 wa SADC.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa historia ya ncho hizo inafanana na kubwa zaidi amani na mshikamano vimeendelea kuimarika.Wakati huo huo amesema pamoja na hatua mbalimbali za kuleta maendeleo,nchi nyingi za jumuiya hiyo zimeendelea kukumbwa na maafa na majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

Hata hivyo amezishukuru nchi za jumuiya hiyo namna ambavyo wamekuwa wakishirikiana na kusaidiana kukabiliana na majanga yanayotokea na hasa vimbunga na mafuriko.

Amezitaka nchi za SADC kuhamasisha wananchi kutunza mazingira kwa kutokata miti hovyo na kuwahamasisha kuoanda miti kwa wingi kama njia mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
 Mwenyekiti amaye amemaliza muda wake wa kuiongoza Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) Rais wa Namibia Dk.Hage Geingob akihutubia kwenye mkutano huo leo uliofanyika Katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere,jijini Dar,Dkt Hage amekabidhi Kijiti kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.Picha na Michuzi JR.

MARAIS WASTAAFU TANZANIA WAMKOSHA RAIS WA NAMIBIA DKT. HAGE GEINGOB

$
0
0
*Kongo yashauri kuundwa na kundi la kikanda kukomesha uovu

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MWENYEKITI aliyemaliza muda wake katika Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye ni Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob amesema Tanzania ni mfano wa kuigwa kutokana ushirikiano na umoja wa viongozi wao.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika ufunguzi rasmi wa mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na serikali uliofanyika leo katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam ,Dkt.Hage amesema;

"Tanzania ni mfano wa kuigwa, ona marais wastaafu wamekaa pamoja na wameonesha ushirikiano mkubwa kwetu na hata mawaziri wastaafu wapo hapa, namwona John Malechela na wengine wengi kweli mnastahili pongezi" ameeleza Hage.

Aidha amempongeza Rais wa Kongo Felix Tshesekedi kwa kufanikisha kubadilishana madaraka kwa usalama nchini humo na kushauri kwa nchi jumuiya lazima zijikite katika kulinda amani na uhimilivu kama msingi mkuu wa maendeleo.

Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ndani ya ukanda huo Dkt.Hage amesema kuwa majanga ya mafuriko na vimbunga yamezikumba baadhi ya nchi za jumuiya hiyo zikiwemo Malawi na Msumbiji ambapo zaidi ya watu 3000 waliathirika.

"Shukrani za dhati ziende kwa nchi wanachama kwa kutoa msaada wa haraka kwa nchi zilizoathirika na majanga hayo na ninashauri tuchukue tahadhari za haraka ikiwa ni pamoja kuwashauri wananchi kupanda na kutokata miti na kutoa taarifa za haraka kwa wananchi kuhusiana mabadiliko ya tabia nchi," ameeleza.

Pia amewahimiza nchi za Jumuiya kuwekeza zaidi katika kundi la vijana ili kuweza kupata maendeleo endelevu ili kufikia malengo ya mwaka 2025 waliyojiwekea kupitia programu mbalimbali zikiwemo za nishati, maji na miundombinu katika ngazi mbalimbali za kitaifa na kimataifa na hiyo ni pamoja na kuwa na kuangalia tafiti na gunduzi ili kuweza kuinua kundi hilo la vijana kupitia sera madhubuti. 

Alisema robo tatu ya wananchi wa Jumuiya hiyo ni vijana,hivyo wakitumika vizuri katika kuleta maendeleo nchi zetu zitapiga hatua kiuchumi.

Awali akihutubia katika mkutano huo Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshesekedi amezishukuru nchi wanachama ikiwemo Tanzania kwa mchango wao wakati wa kubadilishana madaraka kwa amani zaidi na kwa sasa hali ya amani Kongo inazidi kuimarika licha ya eneo la Mashariki mwa nchi hiyo bado kunatishiwa na kundi la kigaidi ambalo ni tishio kubwa ila wametengeneza mkakati wa kuimarisha mamlaka ya serikali ili kuimarisha amani.

Aidha Tshesekedi ameziomba nchi wanachama kuimarisha umoja na mshikamano na kushauri kuwa mwisho wa mkutano huo watoke na tamko la kuwa na kundi la kikanda la kukomesha uovu ili kuzidi kuimarisha nchi wanachama kiusalama na uchumi.

Kuhusiana na kauli mbiu ya mkutano huo wa 39 inayosema "Mazingira wezeshi kwa maendeleo endelevu na Jumuishi ya Viwanda, kuongeza Biashara na Ajira Kikanda" Tshesekedi amesema kuwa jumuiya ya Kongo ina mipaka na nchi nyingi na fursa nyingi hupatikana kupitia mabwawa ya nishati na amehahidi ushirikiano na na kushauri kuondolewa kwa vikwazo vya kibiashara ili wananchi waweze kufanya biashara na kujenga uchumi wa jumuiya kwa ujumla.

Pia ameshauri nchi wanachama kuzingatia kilimo pamoja na ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme ili kuweza kufikia azma ya kufanya mapinduzi ya viwanda na anaamini mkutano huo utafikia malengo makubwa ndani ya jumuiya hiyo.

Tshesekedi amepongeza mwenyekiti anayemaliza muda wake na kueleza kuwa Hana mashaka na mwenyekiti mpya Rais Magufuli na agenda yake wa kujenga Viwanda katika ukanda huo wa SADC wanaamini itafikiwa vyema na kumalizia kwa kusema kuwa lazima jumuiya ijipongeze kwa kukichagua Kiswahili kuwa lugha rasmi ya jumuiya hiyo.
Marais wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Jakaya Kikwete, Mh. Benjamin Mkapa pamoja na Mh Ally Hassan Mwinyi wakifuatilia yanayojiri kwenye mkutano wa 39 wa SADC uliofanyika leo katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam .Picha Michuzi JR

RAIS MAGUFULI AAHIDI USHIRIKIANO SADC, AIPIGIA CHAPUO LUGHA KISWAHILI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Ndani cha Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADIC) uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) akihutubia katika mkutano wa wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi pamoja na Wakuu mbalimbali wa nchi za SADC wakati wa wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa kabla ya kuaza kwa mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Wake wa Marais pamoja na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya ufunguzi wa mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Dar es Salaam


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

RAIS Dkt. John Joseph Magufuli amesema kuwa kwa niaba ya watanzania anaahidi ushirikiano wa hali ya juu na nchi jumuiya wanachama ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea kwa kivitendo zaidi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika ufunguzi rasmi wa mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na serikali Rais Magufuli amesema kuwa tangu jumuiya hiyo ianze mwaka 1980 malengo yalikuwa ni kupambana na ukoloni pamoja na kujenga ushirikiano katika kujenga uchumi miongoni mwetu.

"Ni miaka 20 tangu ufanyike mkutano huu akiwepo mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa niaba ya watanzania tunahaidi ushirikiano ili ndoto za Mwalimu Julius Nyerere na waanzilishi wa jumuiya hiyo yaendeele kufanyika kwa vitendo zaidi" ameeleza Magufuli.

Magufuli amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo lugha ya Kiswahili imekuwa ikitumiwa ndani ya jumuiya katika harakati za ukombozi wa kupambana na ukoloni na aina zote za ubaguzi pamoja na kuwaunganisha wanajumuiya, na kwa sasa lugha ya Kiswahii ni moja kati ya lugha 10 duniani ikizungumza katika nchi kumi duniani na ikizungumzwa katika nchi sita za ukanda wa SADC hivyo Kama wanajumuiya hatuna budi kuichagua lugha ya Kiswahii kuwa lugha Kiswahili kuwa rasmi ya nne ya jumuiya yetu ya SADC.

Awali akizungumza katika mkutano huo katibu mtendaji mkuu wa SADC Dkt. Stergomena Tax ameipongeza Tanzania kwa kuwa nchi pekee kukidhi vigezo katika ukuaji wa uchumi na kufikia asilimia 7 huku akipongeza utekelezaji wa miradi mikubwa ya nishati na miundombinu.

Aidha Dkt. Tax amezipongeza nchi jumuiya kwa kuwa kutunza amani na utulivu na kushauri kushirikiana na taasisi za sekta binafsi ambazo kwa kiasi kikubwa huchangia mapato kwa serikali, kutoa ajira pamoja na kuimarisha hali za uchumi kwa wananchi.

Mkutano huo umehudhuriwa na wakuu wa nchi, viongozi wa serikali, viongozi wastaafu na mabalozi ambapo ndani ya siku mbili watajadili masuala mbalimbali ya kiuchumi na Rais Magufuli atapokea kijiti cha uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa muhula mmoja kutoka kwa Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob.

RAIS DK MAGUFULI AKABIDHIWA UENYEKITI SADC , HOTUBA YAKE GUMZO KWA WAKUU WA NCHI WANACHAMA

$
0
0
*Asema Bara la Afrika lina kila aina ya rasilimali , sio masikini 
*Aiambia Jumuiya ya Kimataifa iondoe vikwazo kwa Zimbabwe 

Na Said Mwishehe, Michuzi TV 

MWENYEKITI mpya wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) Rais Dk.John Magufuli ameziambia nchi za jumuiya hiyo kuwa Bara la Afrika si masikini kwani lina utajiri wa kila aina unatokana na silimali zake. 

Pia ametumia nafasi hiyo kuitaka Jumuiya ya kimataifa kuondolea vikwazo nchi ya Zimbabwe ambayo imewekewa kwa muda mrefu na athari ambazo zinaipata nchi hiyo inaathiri na nyingi nyingine za Afrika. 

Akitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa SADC leo katika Mkutano Mkuu wa 39 wa jumuiya uliofanyika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Rais Magufuli ametoa muelekeo mpya kwa jumuiya huyo kwa kueleza mambo mbalimbali. 

BARA LA AFRIKA SIO MASIKINI 

Mwenyekiti huyo mpya wa SADC amewaambia wakuu wan chi hizo pamoja na viongozi wa Serikali kwamba Afrika sio masikini kwani ina kila kitu zikiwemo rasimali za kutosha ambazo zinatoha kufanya maendeleo. 

“Inasikitisha kuona nchi za Afrika zikiwemo za SADC zinaendelea kujiita maskini wakati zimejaaliwa rasilimali watu, ardhi, maji, madini na misitu. Rasilimali zilizopo zikitumika vizuri Bara hili haliwezi kuendelea kuwa maskini na ombaomba kwani zinahitajika duniani kote. 

Amesema nchi za Bara la Afrika ikiwemo jumuiya ya SADC inayo nafasi ya kuhakikisha kupitia raslimali zilizopo maendeleo yanapatikan.”Afrika sio masikini kwani tunakila kitu.” 

“Nimepokea kijiti cha Uenyekiti kutoka kwa Rais wa Namibia Dk. Hage Geingob na nijipanga kusimamia eneo la viwanda ili kuleta tija kwa maendeleo ya Kanda hiyo. Mwenyekiti aliyemaliza muda wake ameweka mazingira mazuri katika sekta ya miundombinu na vijana, hivyo ni lazima kuwepo na jitihada za kila nchi kujikita katika ujenzi wa viwanda kwa kasi kubwa. 

Amefafanua madhumuni ya waasisi wa SADC yalikuwa yamejikita kupigania amani, ulinzi na siasa na sasa ni jukumu la jumuiya hiyo kuleta maendeleo kwa ajili ya wananchi wake. 

“Nikiwa kama Mwenyekiti mpya nitahakikisha suala la amani na ulinzi linakuwepo lakini ni nipende kueleza tunapaswa kujikita katika viwanda ili kufikia malengo ya kijamii na uchumi kwa haraka,” amesema Dk.Magufuli. 

Amesema mwaka 2018 SADC ilikuwa imejipangia kuwa na uchumi wa zaidi ya asilimia 7 lakini imefikia asilimia 3.1 hiyo ikiwa ni chini ya asilimia ya Umoja wa Afrika (AU) iliyofikia asilimia 3.5 na Afrika Mashariki asilimia 5.7, Afrika Kaskazini asilimia 4.9 na Afrika Magharibi asilimia 3.3. 

“Biashara ya nje ya kanda mwaka 2017 nchi za SADC zenye watu zaidi ya milioni 370 na ukubwa wa heka zaidi ya milioni 9.8 ilisafirisha bidhaa nje ya nchi zake za dola za Marekani bilioni 143 huku ikiwa na rasilimali zote jambo ambalo sio zuri. 

“Haingii akilini kuona nchi mbili Mexico na Vietnam ambazo watu wake hawazidi milioni 132 na eneo lisilozidi ukubwa wa hekta 1.9 ukubwa wa zaidi ya lakini imesafirisha bidhaa zenye thamani zaidi ya dola za Marekani bilioni 403 hali ambayo inaashirikia kuwa SADC haifanyi vizuri,”amesema. 

Hata hivyo amesema kiuhalisia nchi wanachama zinapaswa kujipanga na kufikia malengo yake ikiwa ni kuhakikisha zinajenga viwanda ili kuandaa bidhaa zinazotokana na mazao zinakuwa na viwango vinavyokubalika na kuachana na kuuuza malighafi. 

“Hakuna sababu ya kuficha kwani ndio hali halisi kuwa katika eneo hilo hatujafanya vizuri tunapaswa kujipanga ili kushindana na soko la dunia,”amesema Rais Magufuli. 

Pia amesema jambo la kusikitisha ni kuona nchi wanachama wa SADC zimekuwa zikiagiza bidhaa nyingine kutoka nje ya nchi wanachama hali ambayo inakwamisha mipango ya kuendelea na kukuza uchumi baina yao. 

Ameongeza uchunguzi wake amebaini kitendo cha nchi za SADC kuagiza vyakula kutoka nje ni kutokana na kukosekana kwa taarifa, hivyo kuna mahali ambapo hawapo sawa katika kutoa taarifa. 

Amesema nchi za SADC zinazalisha mazao mengi lakini kinachoonekana ni kuendelea kuewa na mtazamo wa kufikiria kuwa bila kuagiza nje huwezi kupata bidhaa bora. 

“Nilifanya ziara hivi karibuni katika nchi tatu za SADC ambazo amezikuta na ukame na majanga .Nimekuta zikiagiza chakula kutoka nje huku Tanzania, Afrika Kusini, Angola na Mauritius na nyingine zikiwa na akiba ya chakula zaidi ya tani milioni mbili hii si sawa tunapaswa kubadilika,” amesema. 

Ameongeza changamoto nyingine ambayo ameibani kukwamisha maendeleo na kukuwa kwa uchumi kwa nchi wanachama ni kutokana na kuwepo kwa sheria, sera na kanuni ambazo haziwiani hivyo kukwamisha biashara. 

“Ni lazima kuwepo na uhuiwishaji wa sheria na sera za nchi wanachama ili isiwe sababu ya kukwamisha maendeleo yao wenyewe kama ilivyo sasa.Pamoja na hizo changamoto ambazo nimezianisha ipo nyingine ya kukosekana kwa viwanda. 

“Hakuna nchi ambayo imeendelea duniani bila kuwepo viwanda, kwani takwimu zinaonesha nchi zenye viwanda zinauza bidhaa nyingi zaidi ya nchi ambazo hazina viwanda,” amesema. 

Amesema nchi za SADC zinauza malighafi zaidi hali ambayo inakwamisha mipango na mikakati hivyo ni jukumu la kila nchi kuhakikisha kuwa zinakuwa na viwanda vitakavyopandisha thamani ya mazao yao. 

“Suala la viwanda litakuwa kipaumbele changu cha kwanza katika uenyekiti wangu, hivyo naomba ushirikiano, lakini yote hayo yanaweza kufanikiwa iwapo tutadhibiti rushwa na kusimamia makubaliano tunayokubaliana, kwani nchi zetu sio masikini,” amesema. 


AITOLEA UVIVU SEKRETARIETI YA SADC 

Wakati huo huo Rais Magufuli ameitaka jumuiya hiyo kuhakikisha inasimamia vema majukumu yake kwani haridhishwi na utendaji wake na kuitaka ijitathmini upya. 

Amefafanua sekretarieti hiyo imeshindwa kuja na mipango ambayo inaweza kusaidia nchi wanachama kukuwa kiuchumi na maendeleo kama ambavyo inapaswa kufanya. 

Amesema changamoto zote ambazo amezitaja zinapaswa kushughulikiwa na sekretarieti kwa kuja na majibu ikiwa ni pamoja kwanini GDP inashuka kila siku katika kipindi ncha miaka 10 sasa huku miaka ya nyuma ilikuwa inapanda mwaka hadi mwaka. 

“Kuanzia mwaka 2009 uchumi umekuwa ukikua kwa kiwango kisichozidi asilimia 5 tofauti na mwaka 2005 hadi na 2009 ambapo ulifika hadi asilimia 7, hivyo sekretarieti kuitaka ijitafakari na kuja na majibu sahihi wapi imekosea,”amesema. 

ATAKA ZAMBABWE IONDOLEWE VIKWAZO 

Mwenyekiti wa SADC ameziaomba jumuiya za kimataifa kuondoa vikwazo ilivyoweka kwa nchi ya Zimbabwe kwa kuwa vikwazo hivyo vinaumiza nchi za SADC. Amesema vikwazo vya Zimbabwe ni vikwazo ambavyo athari zake zinakwenda kwa Afrika yote, hivyo lazima wawe na kauli moja ili jumuiya ya kimataifa kuondolea vikwazo. 

MWENYEKITI ALITEMALIZA MUDA WAKE 

Kwa upande wake Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Rais wa Namibia Dk. Hage Geingob, amesema anashukuru ushirikiano aliopewa na viongozi wenzake na kufaikisha kusimamia amani kwa kipindi chote. 

Amesema mwaka mmoja ya uogozi wake ameshuhudia chaguzi sita katika nchi za Malawi, DRC Congo, Madagascar, Afrika Kusini, Comoro na Eswatini ambazo zimefanyika kwa uhuru na haki. 

Dk. Geingob amesema nchi za SADC zimefanikiwa kusaidia majanga ya asili yaliyotokea nchi za Msumbiji, Zimbabwe na Madagascar na wamekuwa wakijifunza kila siku namna ya kukabiuliana na hali hiyo. 

“Mwaka mmoja wa uongozi wangu nimefanikiwa kuja na proramu ya kuwezesha vijana katika ushiriki kwenye mijadala na maamuzi ambayo yanagusa jumuiya hiyo. 

“Tumeweza kusimamia utekelezaji wa mkakati wa uwepo wa miundombinu ya viwanda ikiwa ni mkakati wa 2015 hadi 2063.Naamini Mwenyekiti mpya ataendeleza ili siku moja SADC iwe kanda ya viwanda vya kisasa,”amesema.
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Rais Dk.John Magufuli  akitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa SADC leo katika Mkutano Mkuu wa 39 wa jumuiya  hiyo uliofanyika katika kituo cha Kimataifa cha mikutano cha Julius Nyerere,jijini Dar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), aliyemaliza muda wake Rais wa Namibia, Dk Hage Geingob, akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli baada ya kumkabidhi 'kijiti' cha Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kwenye mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi leo Jumamosi Agosti 17, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa jumuiya hiyo, Dk Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), aliyemaliza muda wake Rais wa Namibia, Dk Hage Geingob, akimvisha wadhifa huo Rais Dk John Magufuli kwenye mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi leo Jumamosi Agosti 17, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Mtendaji wa jumuiya hiyo, Dk Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.


HONGERA RAIS DKT. MAGUFULI KWA KUPOKEA KIJITI CHA UENYEKITI WA SADC

Mbunge Gulamali atoa Masada jimboni

$
0
0
 Mbunge wa jimbo la Manongo Seif Gulamali akipokea zawadi ya mchele kutoka kwa mmoja wa wananchi  kama sehemu ya kutambua mchango wake wa maendeleo katika jimbo hilo.
 Mbunge wa  Manongo Seif Gulamali akipokea zawadi ya mbuzi kutoka Kwa wananchi  wake Jimbo hilo Kwa ajili  ya kutambua mchango maendeleo yaliyofanyika katika uongozi.
 Gari maalumu la kubebea wagonjwa lililotolewa na Mbunge wa Jimbo la Manongo kwa ajili ya kituo cha afya cha Simbo kilichopo katika Jimbo hilo la Manongo
Mbunge wa Jimbo la Manongo  Seif Gulamali akionyesha cheti maalum cha kutambua mchango wake maendeleo kilichotolewa na moja ya taasisi I'll liyopo katika Jimbo hilo

Mbunge Gulamali atoa Masada  jimboni.
WANANCHI wa Jimbo la Manonga  lililopo  Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wamempongeza Mbunge wa Jimbo hilo Seif Gulamali kwa hatua anazozichukua katika  kukabiliana na changamoto mbalimbali jimboni humo zikiwemo za kielimu na upatikanaji wa huduma za afya.

Wakizungumza  kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo iliyofanywa na Mbunge huyo jimboni humo ,wananchi hao mbali na pongezi  kwa Mbunge huyo, pia walieleza kuridhishwa  na kasi ya ukuaji wa maendeleo  inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano na kumuomba mbunge huyo kuwafikishia salamu zao kwa Rais John Magufuli.

Wakizungumzia mafanikio hayo, wananchi hao walisema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita Jimbo la Manonga limepiga hatua kubwa za kimaendeleo na hivyo kuleta ustawi wa maisha kwa wananchi wote kutokana na uwepo wa huduma za uhakika za afya, maji, miundombinu ya barabara pamoja na ujenzi wa shule na vyumba vya madarasa katika vijiji mbalimbali.

Mmoja wa wananchi hao Masoud Elias kutoka Kata ya Ndembezi alisema Mbunge amekuwa chachu ya maendeleo ya Jimbo hilo na hasa baada ya kutekeleza ahadi mbalimbali  alizozitoa wakati wa kampeni zake za Mwaka 2015 jambo alilosema kuwa  hujitokeza mara nyingi hasa pale viongozi wanapokuwa wameshaingia madarakani.

Akizungumzia ujenzi wa vituo vya afya katika Jimbo hilo, Masoud alisema mbunge huyo  kwa hamasa yake amewezesha kupatikana kiasi cha Sh Milioni 10 kwa kila zahanati iliyopo katika Jimbo hilo zilizotolewa na Mfuko wa RBF huku wakijiandaa kufungua zahanati mpya katika vijiji vya Itale, Bugingija, Chapela pamoja na kijiji cha  Imalilo kilichopo jimboni humo.

Alisema pamoja na ujenzi wa zahanati hizo, Mbunge huyo pia ameweza kununua gari maalumu kwa ajili ya kubebea wagonjwa katika kituo cha afya cha Simbo na kuwezesha huduma ya upasuaji katika kituo cha afya cha Choma na hivyo kuwa msaada baada ya Hospitali ya Igunga ambayo ilikuwa na jukumu hilo pekee katika suala zima la  huduma ya upasuaji.

“Ukweli ni kwamba hivi sasa changamoto ya ukosekanaji wa huduma za afya katika vijiji mbalimbali ndani ya Jimbo  letu imekuwa siyo tatizo kubwa kwa kuwa maeneo mengi yana vituo vya afya lakini hata huduma zinazotolewa kwa kiasi kikubwa zimekuwa bora, pongezi hizi pia zimfikie Rais John Magufuli kwani kasi yake ya kutuletea maendeleo inaungwa mkono kwa vitendo na Mbunge huyu” alisema Masoud.

Kwa upande wake mkazi wa Kata ya Ziba Shaaban Magengeni alisema kupitia mpango ulioanzishwa na Mbunge huyo wa kuwasomesha wanafunzi wa Jimbo hilo kwa elimu ya kidato cha tano hadi cha sita, umeweza kuleta matokeo mazuri ya ufaulu kwa watoto wao na kuipaisha Manonga kielimu tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

Alisema mpango wa utoaji wa elimu bure chini ya agizo la Rais John Magufuli kwa kiasi kikubwa umesaidia kupatikana wahitimu wengi ambao hujikuta wakibaki mitaani kwa kukosa ada za kuendelea kidato cha tano na sita suala walilodai kuwa Gulamali aliliona na kuamua kulifanyia kazi kwa kuwasomesha wanafunzi wote wanaofaulu.

“Tunamshukuru kwa hatua hii, hivi sasa tunajivunia matokeo mazuri ya ufaulu wa kidato cha nne kwa wanafunzi katika shule yetu ya Ziba na kuifanya kuongoza kiwilaya katika mitihani mbalimbali ukiwemo wa taifa, tuzidi kumuomba Mbunge aweze kuendelea na mpango huu kwa kuwa unaleta akisi ya kimaendeleo” Magengeni.

WAKUU WA NCHI SADC WAIPITISHA LUGHA YA KISWAHILI KUANZA KUTUMIKA RASMI...RAIS MAGUFULI AWASHUKURU

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WAKUU wa Nchi na Viongozi wa Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC)wamepitisha kwa kauli moja lugha ya kuwa lugha rasmi ya nne itakayotumika kwenye jumuiya hiyo.

Kupitishwa kwa lugha hiyo kumetokana na Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais Dk.John Magufuli kuomba lugha hiyo iingizwe kwenye jumuiya hiyo.

Akizungumza leo Agosti 18,2019 kwenye ufungaji wa Mkutano Mkuu wa 39 wa SADC ambao umefanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere Mwenyekiti huyo mpya ametoa taarifa ya kupitishwa kwa lugha ya Kiswahili kuwa rasmi.

"Nianze kutoa hotuba yangu ya kufunga mkutano wa 39 wa SADC kwa kueleza hapa,nilitoa ombi kuhusu lugha ya Kiswahili kutumika kwenye SADC.Wakuu wanachama wameiteua
lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya  nne ya SADC.

"Narudia tena nawashukuru wakuu wa nchi na wakuu wa Serikali kwa kukubali lugha hiyo iwe rasmi kwenye jumuiya yetu.Baba wa Taifa amekuwa na heshima kubwa sana katika Bara la Afrika.Katika maisha wapo wanajitolea kwa mambo mbalimbali, wapo wanatoa figo,wapo wanaotoa fedha na utoaji wa aina nyingine," amesema.

Amefafanua Mwalim Julius Nyerere yeye aliamua kutoa upendo na maisha yake kwa ajili ya wengine na hivyo sehemu kubwa ya maisha aliyatumia kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa salama  na ndio maana nchini Tanzania kuna maeneo mbalimbali ambayo yalikuwa kambi za wapigania uhuru na hasa nchi za Kusini mwa Afrika.

" Mwalimu Nyerere alishiriki kwa vitendo kwa ajili ya kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa huru.Tanzania imekuwa na kambi nyingi za wapigania uhuru na mojawapo ilikuwa eneo la Kongwa ambako anatoka  Spika wa Bunge Job Ndugai.

"Namshukuru Rais wa Afrika Kusini kwani ametemblea eneo la Mazimbo mkoani Morogoro ambako kuna makaburi ya mashujaa wa Afrika Kusini.Rais wa Afrika Kusini alikutana na mabinti wawili ambao walikuwa wanamtafuta baba yao,

"Na majina yao yameonekana katika makaburi hayo.Ni uchungu sana lakini kwa sehemu kubwa inaonesha  ni namna gani Mwalimu Nyerere aliwapenda wengine," amesema Rais Magufuli.

Amefafanua kwamba wote ambao walikuwa kwenye harakati za kupigania uhuru walikuwa wanatumia lugha ya Kiswahili kwa ajili ya kuwasaliana.Hivyo ameshukuru lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya nne rasmi ya nne kwenye jumuiya yetu.Mmemfuta machaozi baba wa Taifa.

"Kwa niaba ya Watanzania tunashukuru sana kwa lugha hii kuwa rasmi.Hivyo uamuzi huu wa kuifanya lugha hii kuwa rasmi itainganisha wananchi wetu.Kwa nchi ambazo hawazungumzi Kiswahili, Serikali ya Tanzania itakuwa tayari kutoa walimu wa somo la Kiswahili kwa ajili ya kuwafundisha wananchi wao," amesema.

TCRA yawaomba mabalozi kutafuta wawekezaji Viwanda vya kuunganisha simu Janja

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imewaomba mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali za nje kutafuta wawekezaji watakaoweza kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha simu janja maarufu Smartphone hapa nchini.

Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba mara baada ya kumaliza kwa ziara ya mabalozi 43 wa Tanzania nje ya nchi walioifanya katika mamlaka hiyo.

Amesema nchi bado inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa simu janja katika maeneo mbalimbali hasa vijijini hivyo fursa ambayo kwa sasa ipo nchini ni kuwa na kiwanda cha kuunganisha simu hizo ili ziweze kupatikana kwa wingi.

“Kutokana na changamoto hiyo ya upatikanaji wa simu janja maarufu Smartphone tumewaomba mabalozi wetu watusaidie kuwatafuta wawekezaji watakowekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha simu hizo hapa nchini,” amesema.

Kilaba amesema mbali na hilo pia ameomba kutafutwa kwa wawekezaji watakaowekeza katika kiwanda kitakachotengeneza simu ambazo zimeharibika au kumaliza muda wake wa matumizi.

“Tuna simu zaidi ya milioni 40 zinazotumika kwa sasa na zipo majumbani mwa watu, lakini tukijuliza tangu tuanze sekta ya mawasiliano ni simu ngapi ambazo hazitumiki watu wameziweka tu, hivyo uwepo wa kiwanda utasaidia hizi kuchukuliwa kwani madini mbalimbali kama dhahabu, shaba yaliyopo kwenye simu yanaweza kuchambuliwa na kupata rasilimali, ila mabaki yakisagwa yatatengeneza kitu kingine,” alisema Kilaba. 

Aidha amesema lengo la ziara ya mabalozi hao ni kuangalia sekta ya mawasiliano inakabiliwa na changamoto na fursa gani ambazo zipo kwa ajili ya wao kwenda kutafutia ufumbuzi maeneo ambayo wanafanyia kazi.


Naye Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Naimi Aziz amesema kuwa wameamua kuja TCRA ili kuweza kujionea kwa macho yao wenyewe jinsi mawasiliano yanavyofanyika hapa nchini.

Amesema yeye na mabalozi wenzake wamefarijika kupata maelezo mazuri na ya kiutalaamu kuhusu shughuli mbalimbali ikiwamo miamala ya simu pamoja na undeshwaji wa mitambo inayofanywa na mamlaka hiyo.

“Tumeweza kufahamu kwa siku ni mawasiliano ya namna gani ambayo yanafanyika hapa nchini kwetu hasa yale yanayoingia na kutoka, tumefarijika kuona kwamba wataalum waliopo TCRA ni watanzania,” alisema Aziz.


Amesema pia wametambua changamoto mbalimbali zinazoikabili TCRA ikiwamo masuala ya mitambo pamoja na wawekezaji na wao kama mabalozi watajipanga namna ya kuweza kuwasaidia kuzitatua.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk. Abadllah Possi amesema watu wanapaswa kuelewa kuwa teknolojia ya mawasiliano ni jambo ya muhimu katika maisha ya binadamu hasa katika sekta ya biashara na usalama nchini.


“Watu wengi wamekuwa wakifanya biashara mitandao huku wengine utumia simu kutuma fedha na wengine ufanya uhalifu wa kimtandao hivyo kama nchi tunatakiwa kujipanga vizuri kudhibiti matumzi mabaya ya mitandao,” alisema.

Hata hivyo amesema katika ziara hiyo wameona uwekezaji mkubwa uliofanyika TCRA hivyo wanaipongeza serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya Rais John Magufuli.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba akizungumza na mabalozi wa Tanzania wanawakilisha nje za Nje walipotembelea mamlaka jijini Dar es Salaam.
 Mabalozi wa Tanzania wanawakilisha nje za nje wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipotembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia Maendeleo yaliyofanyika katika mamlaka hiyo.
 Mhandisi Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Victor Kweka akiwapa maelezo mabalozi namna ya garai la mambo wanapo angalia masafa ya  mawasiliano wakati walipotembelea Mamlaka hiyo.
Balozi wa Tanzania nchini Sweeden Dkt.Wilbroad Slaa akicgangia katika mkutano wa mabalozi wakati walipotembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dar es Salaam.

TIGO YAING'ARISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA SADC JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Rosemary Mroso kutoka kitengo cha huduma kwa wateja Kampuni ya simu za mkononi Tigo Tanzania akimhudumia mteja wa kampuni hiyo Emmanuel Liwimbi Ofisa Huduma za Mikutano Mwandamizi kutoka Sekretarieti ya SADC alipotembelea banda hilo kwenye mkutano wa SADC unaoendelea katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Tigo ni mdhamini wa huduma za intaneti katika Mkutano huo.



Mfanyakazi wa Tigo akitoa huduma ya kusajili kwa alama za vidole kwa wateja waliofika katika banda lake lililopo ndani ya Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam ambapo Mkutano Mkuu wa 39 wa marais wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unafanyika. Tigo ni mdhamini mkuu wa Huduma ya inteneti katika mkutano huo.
Mtaalam wa Mifumo ya Mtandao Kampuni ya Tigo Bw. Kundasen Simon akiwasikiliza wateja wa kampuni hiyo waliotembelea banda la kampuni ya Tigo lililopo kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es salaam ambako Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea , Tigo ni miongoni mwa wadhamini wa intaneti ya bure katika mkutano huo.
Mtaalam wa Mifumo ya Mtandao Kampuni ya Tigo Bw. Kundasen Simon akiwasikiliza wateja wa kampuni hiyo waliotembelea banda la kampuni ya Tigo lililopo kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es salaam ambako Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea , Tigo ni miongoni mwa wadhamini wa intaneti ya bure katika mkutano huo.

Mtaalam wa Mifumo ya Mtandao Kampuni ya Tigo Bw. Kundasen Simon akimsikiliza mteja wa kampuni hiyo Bw. Selemani Kifyoga aliyefika kwenye banda hilo kwa ajili ya kusajili laini yake ya simu kwa mfumo wa kutumia vidole. Tigo ni miongoni mwa wadhamini katika mkutano unaondelea wa SADC
Mtaalam wa Mifumo ya Mtandao Kampuni ya Tigo Bw. Kundasen Simon akiwasikiliza wateja wa kampuni hiyo waliotembelea banda la kampuni ya Tigo lililopo kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es salaam ambako Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea , Tigo ni miongoni mwa wadhamini wa intaneti ya bure katika mkutano huo.

Mfanyakazi wa Tigo akitoa huduma kwa wateja waliofika katika banda lake lililopo ndani ya Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam ambapo Mkutano Mkuu wa 39 wa marais wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unafanyika. Tigo ni mdhamini mkuu wa Huduma ya intaneti katika mkutano huo.
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images