Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live

WASAIDIZI WAPYA WA SHERIA WA MAJAJI WAPATIWA ‘ABC’ ZA UTENDAJI KAZI

$
0
0
 Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (katikati) akizungumza na Wasaidizi wapya wa Sheria wa Majaji wa Mahakama ya Rufani (T) (hawapo pichani), wa pili kushoto ni Naibu Msajili Mwandamizi-Mahakama ya Rufani, Mhe. Elizabeth Mkwizu, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Bi. Patricia Ngungulu, wa kwanza kulia ni Afisa Utumishi/Msaidizi wa Mtendaji-Mahakama ya Rufani, Bi. Vivienne Kishimbo na wa pili kulia ni Hakimu Mkazi na Msaidizi wa Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Upendo Ngitiri. 
Mhe. Mkwizu akiwaonyesha Maafisa hao Ofisi ya Mapokezi ya Mahakama ya Rufani.

Na Mary Gwera, Mahakama
JUMLA ya Wasaidizi wa Sheria 21 wa Majaji wa Mahakama ya Rufani (T) walioteuliwa hivi karibuni wamepatiwa utangulizi wa masuala muhimu ya kuzingatia katika ufanyaji kazi kwenye Mahakama hiyo.

Akizungumza na Maafisa hao mapema Agosti 15, 2019 katika Ukumbi ya Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati amewaasa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Mahakama imewaamini, hivyo basi ni vyema mkafanye kazi kwa uadilifu na unyenyekevu,” alieleza Msajili Mkuu.

Mbali na masuala hayo, Mhe. Revocati aliongeza kwa kuwataka Maafisa hao kutojihusisha na vitendo vya upokeaji wa rushwa wanapotekeleza majukumu yao.

“Siku hizi hakuna rushwa isiyojulikana pindi unapojihusisha katika vitendo hivi utajulikana tu, hivyo ni vyema kutojihusisha ili kuwa salama,” alisisitiza Mhe. Revocati.

Wasaidizi hao wa Sheria ambao kwa taaluma ni Mahakimu wameteuliwa kutoka Mahakama mbalimbali nchini lengo likiwa ni kuwasaidia Waheshimiwa Majaji katika kufanya tafiti ambazo zitawawezesha katika utoaji wa maamuzi ya rufaa mbalimbali.

Kabla ya kuanza kazi rasmi Maafisa hao watapatiwa Mafunzo elekezi yatakayowawezesha kuwapa kwa kina misingi ya ufanyaji kazi katika Mahakama hiyo.

MABALOZI WASIFU JUHUDI ZA SERIKARI YA AWAMU YA TANO KWA UJENZI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA, UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE

$
0
0

 Mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali Ulimwenguni wakiapata maelekezo kuhusu ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kutoka kwa Meneja wa Jengo hilo, Mhandisi Burton Komba

 Mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali Ulimwenguni wakiwasili katika Jengo la Tatu la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam na kupokewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale wakati wa ziara yao ya kikazi katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.




Mabalozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbroad Slaa na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza, Dkt. Asha-Rose Migiro wakisikiliza maelekeo ya Jengo la Tatu la Abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MABALOZI wa Tanzania katika nchi mbalimbali wamesifu juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwenye ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Mabalozi hao wametoa sifa hizo wakati wa ziara yao ya kikazi katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayoratibiwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Balozi wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda ambaye hivi karibuni Shirika la Ndege nchini (ATCL) imezindua safari zake nchini humo, amesema Jengo hilo la Tatu la Abiria linatuleta katika sura mpya ya Kimataifa na kututambulisha.

Balozi Luvanda amesema Wajumbe mbalimbali wa Mkutano wa Nchi wa Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wataondoka na sura nyingine ya kimaendeleo katika Taifa la Tanzania, amesema Uwanja huo umefunguliwa muda mwafaka na maboresho yanayoendelea kufanyika yataiweka Tanzania katika Ramani ya Dunia kwa inavyostahili.


"Kwanza ujio wa ATCL (Dream Liner) nchini India kutoka Dar es Salaam umepunguza muda wa safari, kulikuwa na Wagonjwa wanakuja India lakini wengine walikuwa watunia masaa 13 au 14 kwa sababu ya umbali, lakinj kwa sasa wanatumia masaa matano tu kufika Mumbai", amesema Balozi Luvanda.

Amesema atatumia fursa hiyo kuutangaza Uwanja huo nchini India kutokana na uwezo wake wakuchukua idadi kubwa ya abiria kwa mwaka ambao ni Milioni 6, ameahidi kutangaza ili kupata idadi kubwa ya Ndege na Mashirika mbalimbali.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dkt. Abdallah Posi amesema miradi hiyo ni muhimu kwa wageni wanaoingia nchini, amesema Ujenzi wa Jengo hilo utarahisisha usafiri kwa watu wa mataifa mbalimbali wanaoingia nchini, Dkt. Posi amesema anaona mafanikio makubwa zaidi kwa utofauti uliopo kati ya Jengo hilo la Tatu la Abiria pamoja na Jengo la Kwanza na la Pili la Uwanja wa Ndege.

"Wengi wetu tumefurahishwa sana na utekelezaji wa miradi hii, kwa yale tunayoyaona huko nje ni mafanikio, walichotuzidi wenzetu labda wao wana hela nyingi", amesema Dkt. Posi.

Naye, Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wibroad Slaa ametoa wito kwa Mabalozi hao kuitangaza zaidi Tanzania Kimataifa, amewataka kutoa woga katika kulitangaza Taifa katika maendeleo yanayofanyika chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

"Tusiogope kuitangaza Tanzania Kimataifa kama tunaendelea katika miradi mablimbali, wenzetu huko wanatumia sana Pesa katika masuala mbalimbali ikiwemo miradi ya ujenzi", amesema Dkt. Slaa.

Mabalozi hao wapatao 42 wametembelea Miradi mbalimbali ya Serikali ikiwemo Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge, Ujenzi wa Daraja la Surrender na Ujenzi wa Interchange ya Ubungo inayosimamiwa na Serikali Kuu ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

SHIRIKA LA SMCCT LAUNDA KAMATI ZA ULINZI KUMLINDA MAMA NA MTOTO DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la SMCCT, Evalyen Lyimo, akitoa mafunzo kuhusu lishe na chakula kwenye mkutano wa kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto na mama katika Kata sita zilizopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida. Mafunzo hayo yalikuwa na lengo ya kuzijengea uwezo kamati za ulinzi wa mama na mtoto ngazi ya wilaya hiyo.
Wadau na wanafunzi wakiwa kwenye mkutano huo wa kuunda kamati hizo
Wajumbe wa kamati za ulinzi wa mama na mtoto ngazi ya kata kutoka kata sita za wilaya ya Ikungi za Ihanja,Iseke,Iglanson,Minyughe na Muhintiri wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuundwa kwa kamati hiyo.
Mgeni rasmi wa mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akisalimiana na mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.
Mgeni rasmi wa mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akisalimiana na wanafunzi walioshiriki mkutano huo.
Mgeni rasmi wa mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa kamati za ulinzi wa mama na mtoto kutoka ngazi ya Wilaya ya Ikungi wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Mpogolo (katikati aliyevaa miwani).



Na Dotto Mwaibale, Singida

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Save the Mother and the Children of Central Tanzania (SMCCT), limeunda kamati za ulinzi wa mama na mtoto katika kata sita na vijiji 18 katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida. 

Imeelezwa kwamba majukumu ya kamati hizo ni kumlinda mama na mtoto dhidi ya vitendo vya ukeketaji na ukatili wa kijinsia. Hayo yalisemwa na mwezeshaji wa mradi wa utetezi dhidi ya mila potofu, Japhet Kalegeya wilaya ni hapa juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la Foundation for Civil Society ambalo limetoa shilingi milioni 40 kwa mradi utakaofanyika kuanzia mwezi Julai hadi Machi 2020. 

Alisema wamefikia uamuzi wa kuanzisha kamati hizo ili ziweze kuharakisha kutokomeza kabisa vitendo hivyo ambavyo vipo kinyume na haki za binadamu kama vile ukatili dhidi ya wanawake na watoto, mimba za utotoni, ndoa za utotoni ,ubakaji ,ulawiti,ukeketaji na udhalilishaji wa kijinsia katika wilaya hiyo. 

“Mradi huu wa utetezi dhidi ya mila potofu ikiwemo ukeketaji na ukatili wa kijinsia,unalenga kuwafikia wanawake na wasichana wapatao 7,200 katika wilaya ya Ikungi ambapo hali ya unyanyasaji wa kijinsia ni mbaya”,alisema Kalegeya.

Akitolea mfano wa hali hiyo alisema kuanzia Januari hadi oktoba 2018 jumla ya wanafunzi 37 waliokuwa kati ya kidato cha kwanza na nne walipachikwa mimba.

Naye mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Sekondari ya Masinda, Rosemary Seith, amelishukru na kulipongeza shirika la SMCCT kwa kushirikisha baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuwapa elimu juu ya madhara ya ukeketaji na ukatili wa kijinsia. 

“Sisi tuliohudhuria mafunzo haya yametusaidia kujua kwa mapana madhara ya vitendo hivyo vya ukeketaji na ukatili wa kijinsia sasa tunaenda kuwaelimisha na wenzetu ambao hawakubahatika kupata mafunzo haya hapa leo”, alisema. 

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la SMCCT, Evalyen Lyimo, ametaja baadhi ya malengo ya mradi huo kuwa ni kuongezeka kwa uelewa kwa jamii kuhusu kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukeketaji na kuimarisha mfumo wa utoaji wa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii hadi ifikapo Machi mwaka 2021.

Kata zilizounda kamati hizo ni Ihanja, Iglansoni,Iseke, Minyughe na Muhintiri.

Wizara ya Kilimo yatiliana saini kushirikiana na Taasisi ya ICRAF ya nchini Kenya

$
0
0
Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe kwa niaba ya Wizara leo, ametiliana saini ya makubalianao ya kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa masuala ya Kilimo Misitu (International Centre for Research in Agro-Forest - ICRAF). Taasisi ya ICRAF imekwa ikifanya tafiti zinazolenga kuboresha uhifadhi wa mazingira na uzalishaji wa nishati jadidifu ambayo ni muhimu katika shughuli za kilimo. 

Akizunzungumza baada ya kusaini hati za makubaliano Katibu Mkuu, Mhandisi Mtigumwe amesema kimsingi Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo imesahini makubaliano kwa ajili ya lengo la kushirikiana na ICRAF kwenye maeneo ya ugunduzi wa misitu inayopatikana kwenye ikolojia maalum, usimamizi wa misitu kwa lengo la kuongeza tija kwenye eneo hilo. 

Mhandisi Mtigumwe ameongeza kuwa Wizara itashirikiana na ICRAF katika eneo la ufuatiliaji wa madhara kwenye afya ya udongo, mabadiliko ya tabianchi kwenya ardhi ya kilimo ili kufanya tafiti zitakazokuja na majibu ya changamoto katika maeneo hayo. 

Mhandisi Mtigumwe ameongeza kuwa eneo moja la ushirikiano ni kujengeana uwezo wa kitaasisi pamoja na kubadilishana Wataalam, uzoefu katika tafiti mbalimbali pamoja na kubadilishana vinasaba vya mimea na mazao ya kilimo na misitu. 

Akiongea kwa niaba ya Taasisi ya ICRAF, Bi. Catherine Muthuri ambaye ni Msimamizi wa Shughuli la Taasisi hiyo iliyopo Jijini Nairobi amesema Tanzania na Kenya ni majirani wa muda mrefu na kwamba changamoto zinazowakuta Wakulima wa Kenya, zinawakuta pia na Wakulima wa Tanzania na kusisitiza kuwa lengo la nchi hizi mbili ni kuhakikisha mambo mazuri kama ya kushirikiana katika tafiti; yanafanyika kivitengo kwa lengo la kuboresha Sekta ya Kilimo.

Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe kushoto kwa niaba ya Wizara akimkabidhi hati ya makubaliano ya kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya ICRAF mara baada ya kusaini ya makubalianao ya kushirikiana kulia ni Msimamizi Mkuu wa Taasisi hiyo Bi. Catherine Muthuri, katika Ofisi za Wizara ya Kilimo katika eneo la Mtumba, Jijiji Dodoma leo tarehe 16/08/2019.

KAMATI YA PAC YAPEWA MAFUNZO NA OFISI YA MSAJILI WA HAZINA

$
0
0
Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Ndg. Lightness Mauki akifafanua jambo alipokuwa akitoa Mada kuhusu Changamoto za usimamizi wa Matumizi ya Mashirika ya Umma nchini kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma hii leo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC wakifuatilia jambo kwa karibu kwenye Semina kuhusu Changamoto za usimamizi wa matumizi ya Mashirika ya Umma nchini iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge).

WADAIWA SUGU KODI YA ARDHI SIKONGE KUBANWA

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM SIKONGE

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameiagiza idara ya ardhi katika halmashauri ya Sikonge mkoani Tabora kuhakikisha inawafikisha kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya wadaiwa wote sugu wa kodi ya pango la ardhi katika wilaya hiyo wanaodaiwa kiasi cha takriban milioni 150.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo tarehe 15 Agosti 2019 katika halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi sambamba na kukagua masiajala ya ardhi na mifumo ya ukusanyaji kodi kwa njia ya kielektroniki mkoani Tabora.

Dkt Mabula alishangazwa na idara ya ardhi katika halmashauri hiyo kushindwa kuwafikisha wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba wakati sheria inaelekeza baada ya siku kumi na nne mdaiwa asipotii wito afikishwe kwenye Baraza.

Alisema, katika halmashauri ya Sikonge kuna baadhi ya wamiliki wa ardhi ambao kwa mara ya mwisho walilipa kodi ya ardhi mwaka 2000 lakini idara ya ardhi imeshindwa kuwadai ama kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria jambo alilolieleza kuwa halikubaliki.

Kaimu Afisa Ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Sikonge Martin Ukongo alieleza kuwa ofisi yake tayari ilishasambaza ilani 105 kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi kuanzia januari hadi machi 2019 lakini baadhi yake pamoja na kushindwa kulipa hawajafikishwa kwenye Baraza la Ardhi jambo lililomfanya Naibu Waziri kuagiza hatua za kuwafikisha kwenye Baraza zifanyike.

Dkt Mabula pia ameigiza halmashauri ya wilaya ya Sikonge kupitia idara ya ardhi kuhakikisha inapima mashamba yote yaliyopo katika halmashauri hiyo na kueleza kuwa kutopimwa kwa mashamba hayo kunatoa fursa kwa wamiliki wake kutolipa kodi ya ardhi.

‘’Sikonge mna mashamba hayajapimwa wakati ni ya wafanyabiashara wakubwa hapa wanakwepa kulipa kodi why hamjawapimia na kuwapatia hati ili walipe kodi?’’ Alihoji Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula

Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Denis Masami alisema kuwa Wizara yake kwa sasa imeimarisha mfumo wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kurahisisha ukadiriaji na kufanya malipo kupitia kupitia simu ya mkonini jambo linalowarahisishia wamiliki kuepukana na usumbufu wa kufika ofisi za ardhi kwa ajili ya malipo.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa katika kipindi cha mwaka 2018/2019 wilaya hiyo ilifanikiwa kukusanya kodi ya pango la ardhi shilingi milioni 29,127,334.50 sawa na asilimia 87.55 wakati lengo ilikuwa kukusanya milioni 33.2. Hata hivyo Magiri alisema wilaya yake imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kama vile kutoa matangazo na kuelimisha jamii kupitia mikutano umuhimu wa kulipa kodi kwa wakati.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Sikonge Joseph Kakunda alimpongeza Naibu Waziri Dkt Mabula kwa uamuzi wake wa kufanya ziara katika wilaya hiyo na kueleza kuwa huyo ni Waziri wa Ardhi wa kwanza kuitembelea wilaya hiyo toka ianzishwe.

Hata hivyo, Kakunda alimueleza Dkt Mabula kuwa wilaya ya Sikonge ni wilaya iliyoko nyuma katika suala la Mapango wa Matumizi Bora ya Ardhi na kuomba Wizara ya Ardhi kuipa kipaumbele katika upimaji ili kuepusha migogoro ya ardhi hasa ile ya wakulima na wafugaji. 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoka katika ofisi za Masijala ya Ardhi Halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora wakati wa ziara yake mkoani Tabora jana.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Sikonge Joseph Kakunda. 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya wilaya ya Sikonge Martin Ukongo (kushoto) kuhusu eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda katika wilaya ya Sikonge wakati wa ziara yake mkoani Tabora. Wa nne kulia ni Mkuu wa wilaya ya Sikonge Peres Magiri, wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Martha Luleka na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Sikonge Joseph Kakunda.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Martha Luleka (wa kwanza kushoto). Wengine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri (wa pili kusho) na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Sikonge Joseph Kakunda
 (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

MKUU WA MKOA WA PWANI AWEKA MAWE YA MSINGI VIWANDA VYA NONDO,CHUMA NA GESI

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka wawekezaji wa viwanda kuhakikisha wanazingatia haki za wafanyakazi kwa kuwalipa maslahi yao kama inavyotakiwa bila la kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji na ubaguzi wowote kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu zote za nchi kwa lengo la kutimiza azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda.

Ndikilo ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya uwekaji wa mawe ya msingi katika kiwanda vitatu tofauti vya kuzalishia nondo,chuma pamoja na mitungi ya gesi vilivyopo Wilayani Kibaha,ambapo pia akusita kuwaasa watumishi na viongozi kuachana na vitendo vya urasimu kwa wawekezaji na badala yake watoe ushirikiano wa kutosha bila vikwazo vyovyote kwa lengo la kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi.

“Kwa sasa Mkoa wetu wa Pwani tunaendelea na kutekeleza agizo la Rais wetu Dk. John Pombe Maguli katika ujenzi wa viwanda mbali mbali, hivyo kitu kikubwa ninachowaomba wawekezaji wote wanaokuja kuhakikisha wanazingatia haki za wafanyakazi ili kuweza kutimiza malengo ambayo yamewekwa na serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,”alisema Ndikilo.

Aidha katika hatua nyingine alibainisha kuwa wawekezaji ni chanchu kubwa ya kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi kutokana na wengine wao kuweza kupata fursa mbali mbali za ajira pindi viwanda vinapoanzishwa hivyo ni jukumu la watendaji na viongozi kuwa bega kwa bega na wadau wa maendeleo ili kuweza kuongeza zaidi ujenzi wa viwanda vingine.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya lake group Ally Awadhi lengo lao kubwa ni kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika ujenzi wa viwanda pamoja na kuwainua wananchi kiuchumi hasa ambao wanaoishi katika kaya ambazo ni masikini kuwapatia fursa za ajira.

Pia aliongeza kwamba kutokana na kuwepo kwa uwekezaji wa viwanda hivyo kutasaidia kuwainua wananchi wa Wilayani Kibaha pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kutokana na kupata ajira ambazo zitasaidia kuwaongezea kipato sambamba na kuchangia katika ulipaji wa kodi amabazo zitafanya pato la Taifa kuongezeka.

Nao baadhi ya wafanyakazi katika viwanda hivyo walimpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kwa kuwa na sera ya ujenzi wa viwanda katika maeneo mbali mbali ambavyo wamedai vimewasaidia kupata fursa ya ajira, na kuondokana na wimbi la umasikini na kumwomba mwekezaji huyo kuwaongezea ujira kulingana na kazi wanazozifanya.

KUKAMILIKA kwa viwanda hivyo vitatu vya utengenezaji wa nondo,na chuma hususan cha kutengenezea mitungi ya gesi kutaweza kusaidia wananchi kwa kiasi kikubwa fursa za ajira pamoja na kupunguza changamoto ya ukataji wa miti ovyo kwa ajili ya kupata nishati ya mkaa ambayo imekuwa ni kero ya siku nyingi katika maeneo ya Mkoa wa Pwani
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kulia wakipongezana na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Lake Group Ally Awadhi maara baada ya kuweka mawe ya msingi katika viwanda vitatu tofauti vya kutengenezea nondo,chuma, pamoja na kiwanda cha kutengenezea mitundi ya gesi katika kata ya visiga Wilayani Kibaha.(PICHA NA VICTOR MASANGU.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kushoka akipata maelekezo na mmoja wa wataalamu wa kiwanda cha kutengenezea nondo na chuma, mara baada alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweka mawe ya msingi katika viwanda vitatu, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno.(PICHA NA VICTOR MASANGU.
  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa kulia akipeana mkono na Mkurugenzi mtendaji wa makampuni wa Lake Group mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uwekaji wa mawe ya msingi katika viwanda vitatu.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani wa kulia Mhandisi Evarist Ndikilo akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa kati kati,pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Lake group Ally Awadhi wakiopiga makofi kwa pamoja ikiwa ni ishara  furaja mara baada ya kukamilika kwa uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda cha kuzalishia Nondo.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa anafafanua jambo mara baada ya kumaliza zoezi la kuweka jiwe la msingi katika kiwanda   cha kutengenezea mitungi ya gesi ambacho kinatarajia kukamilika mwishoni mwa octoba  mwaka huu
Mkurugenzi mtendaji wa  kampuni ya Like group Ally Awadhi kushoto  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumptem Mshama wa akifuatiwwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya kumaliza kuweka mawe ya msingi katika viwanda vitatu vya kutengenezea Nondo, chuma pamoja na mitungi ya Gesi.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

HUDUMA ZA TIGO ZAVUTIA MKUTANO WA SADC JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Naibu Waziri Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Tigo alipotembelea banda la maonyesho wakati wa mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea jijini Dar es Salaam, Tanzania, ambapo Tigo ndio wadhamini rasmi wa Wi-Fi inayotumika katika mkutano huo.


CHAMA CHA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI CHAKABIDHI MASHINE YA MIONZI YA KUTIBU SARATANI NGOZI MKOANI SINGIDA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi nchini, Mussa Kabimba, akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya mashine maalum ya kutibu magonjwa ya saratani kwa mionzi. Hafla hiyo imefanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha walemavu wa ngozi nchini, Godson Mwoleli,(wa pili kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk.Angelina Lutambi (wa pili kulia), mashine maalumu kwa ajili ya matibabu ya saratani kwa njia ya mionzi.

Na Dotto Mwaibale
SERIKALI mkoani Singida, imeahidi kuendelea kupokea changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi na kuzipatia ufumbuzi ili kundi hilo nalo lijione kama jamii nyingine zisizo na ulemavu.

Ahadi hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk. Angelina Lutambi, wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya mashine maalumu ya kutibu kwa njia ya mionzi kwa walemavu wa ngozi.Mashine hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8.3 ni msaada  kutoka  chama cha watu wenye Ulemavu wa ngozi nchini.

Lutambi alisema serikali ya awamu ya tano imeboresha sekta ya afya kitendo kinachopelekea huduma mbalimbali, zipatikane wakati wo wote na  bila shida.

Akifafanua zaidi alisema kwa sasa vituo vya afya ikiwemo hospital mbalimbali nchini, vina dawa na vifaa tiba kwa kiwango cha kukidhi mahitaji.

“Huduma za maradhi ya saratani ambazo zilikuwa zikifuatwa Taasisi ya Saratani ya ngozi ya Ocean Road jijini Dar es Salaam sasa zitapatikana mkoani kwetu na hii mashine tunayoikabidhiwa leo,itatumika kutibu watu wenye ulemavu wa ngozi na wale wasio na ulemavu wa ngozi”,amesema Dk.Lutambi.

Amesisitiza kwamba  watu wenye ulemavu wa ngozi na wasio na ulemavu,serikali itaendelea kuhakikisha inatoa huduma za afya stahiki kwa Watanzania wote pasipo ubaguzi.

Lutambi ametumi fursa hiyo kukishukuru Chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi Taifa, kwa msaada huo wa mashine hiyo maalumu katika kutibu saratani za aina mbalimbali na kuwa usiwe wa mwisho, waendelee kusaidia mkoa huo ili kuhakikisha wakazi wanakuwa na afya njema na kuweza kujiletea maendeleo.


Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi Taifa,Mussa Kabimba,alisema wameamua kugawa mashine hizo mikoani kwa sababu ya vifo vingi vya watu wenye kansa ya ngozi. 

Alisema kazi iliyo mbele yao pamoja na kugawa mashine hizo ni kutoa elimu juu ya maradhi yatokanayo na magonjwa ya kansa ili watu wenye ulemavu wa ngozi waweze kutambua dalili zake mapema na jinsi ya kuyaepuka maradhi hayo. 

Katibu wa watu wenye mahitaji maalum mkoani Singida,Ramadhani Maulidi, ametumia nafasi hiyo kuishauri serikali iwaagize wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, manispaa na miji  wakati wa kuagiza madawa wahakikishe wanaagiza na mafuta maalumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi. 

Wakati huo huo mkazi wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Mariamu Mkumbo,ameziomba mamlaka mbalimbali zisaidie kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa watu wenye changamoto ya maradhi ya ngozi ili waweze kufanya shughuli za ujasiriamali zitakazowasaidia kuwa na uwezo wa kununua mafuta maalumu na dawa zao za kujipaka bila kuwa wategemezi kwa mtu.

NDIKILO AWAASA WAMILIKI WA VIWANDA KUCHANGAMKIA FURSA KWA NCHI ZA SADC PAMOJA NA KUTENGENEZA BIDHAA BORA

$
0
0



NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKUU wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo amewaasa ,wamiliki wa viwanda kutengeneza bidhaa ambazo zitapata soko kwenye nchi za jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika SADC ili kuinua pato la wananchi na nchi kwa ujumla.

Nchi za SADC zina wanachama 16 ambazo zina wananchi milioni 350 hivyo endapo vitafanikiwa kulipata soko hilo hakika watapata mafanikio makubwa kwa kuongeza kipato cha wananchi na nchi kwa ujumla.

 
Ndikilo aliyasema hayo mjini Kibaha wakati wa kuweka jiwe la msingi ya ujenzi wa viwanda vya Lake Steel and Allied Ltd ikiwa ni ziara yake ya kuweka mawe ya msingi kwenye viwanda 13 vipya.

Aliwapongeza kwa kuitikia wito wa serikali ya awamu ya tano chini ya Dk John Magufuli ya kuhimiza ujenzi wa viwanda ili kuifanya nchi kuwa na uchumi wa kati.

"Viwanda hivyo vinapaswa kutumia mkutano wa viongozi wa nchi hizo kwa kutangaza bidhaa zao kwani endapo watalipata soko hilo watakuwa wafanyabiashara kubwa"alibainisha.

Nae ofisa mtendaji mkuu wa Lake Group Ally Awadhi alisema kuwa lengo kuu la kuanzisha viwanda hivyo ni kuongeza ajira pia kuunga mkono serikali.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Pwani ,Ramadhan Maneno alisema ,ujenzi huo unasidia kupunguza changamoto za ajira kama sera ya chama inavyosema.

Maneno alisema, sera ya chama inahimiza uanzishwaji wa viwanda na kuongeza ajira hasa kwa vijana hivyo hiyo ni utekelezaji wa ilani.

Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumter Mshama , alisema kikubwa wao kama Wilaya walichokifanya ni kutenga maeneo ya viwanda na uwekezaji mwingine hivyo kuwaondolea usumbufu wawekezaji.
Viwanda vilivyowekewa mawe ya msingi kamapuni hiyo ni cha mabomba makubwa ya maji, mitungi ya gesi cha kwanza hapa nchini na kiwanda cha bidhaa za chuma.   

Nyongo amaliza mgogoro wa mpaka kuhusu madini

$
0
0
Machui Bausi akiwasilisha kero za wachimbaji wa eneo la kiegei kwa Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo kulia kwa mtoa kero.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akitolea majibu kero za wachimbaji wadogo wa madini ya vito kiegei wilayani Nachingwea. Mwenye Tshirt ya blue na Mtandio ni Katibu tawala wa Nachingwea Husna Sekibobo anae mwakilisha mkuu wa wilaya hiyo.
Sehemu ya Wachimbaji wadogo waliokusanyika kumsikiliza Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo hayupo pichani aliewasili machimboni hapo kusikiliza na kutatua kero zao. 
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Chiwamba kushoto, akifuatiwa na Katibu Tawala wa Liwale Mbwana Kambangwa na wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wa Nachingwea Husna Sekibobo mara baada ya kumaliza mkutano wa pamoja na wachimbaji wadogo


Na Issa Mtuwa “WM” Nachingwea Mtwara 

Mgogoro ulio dumu kwa muda mrefu kuhusu mpaka wa uchimbaji madini uliohusisha eneo (leseni) moja kwenye ardhi ya halmashauri za wilaya mbili ya Nachingwea na Liwale kila upande ukiwa na wachimbaji wadogo umetatuliwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo tarehe 15/08/2019 mara baada ya kufanya ziara katika eneo hilo na kufanya mkutano na wachimbaji wadogo wa pande zote mbili na viongozi wa kuu wa wilaya zote mbili. 

Mgogoro huo wa mpaka na leseni umedumu kwa muda mrefu ukiwa na vyanzo viwili vikuu vya mgogoro. Moja, mgogoro wa eneo ambalo wachimbaji wadogo wananchimba hivi sasa wamedai eneo hilo lilikuwa la Omar Said Kojogo ambae kwa mujibu wa wachimbaji wadogo walimlipa fidia ndugu Kojogi ili eneo hilo limilikishwe kwa jumuia ya wachimbajio wadogo lakini bado walikuwa hawajapatiwa leseni hiyo kama wamiliki wapya. 

“Mhe. Naibu Waziri tatizo la mgogoro wa leseni hapa bado haujatatuliwa kwa kuwa sisi wenyewe wanaaporo tulichangishana na kumpa Omar Said Kojogo Tsh. 2,852,000/= ili leseni hiyo iwe ya wanaaporo (Wachimbaji wadogo) lakini mpaka leo hatujapatiwa” alisema Machui Bausi. 

Chanzo cha pili cha mgogoro huo ni mgao wa mapato yanayopatikana katika eneo hilo. Kila halmashauri inataka ichukuwe mapato kitu ambacho kilikuwa kinaleta mvutano nani anastahili kwa kuwa leseni ya eneo hilo ipo katika halmashauri zote mbili. za Nachingwea na Liwale zote za mkoa wa Lindi. 

Aidha, changamoto nyingine ambayo wachimbaji wadogo wamemwambia Naibu Waziri ni tatizo la soko la kuuzia madini ambapo wamemuomba Naibu Waziri kuwasongezea soko la madini katika eneo hilo ili kuwaondolea ushawishi wa kutorosha na kwenda kutafuta soko kwingine na ili mapato ya serikali yasipotee. 

“Mhe. Naibu Waziri sisi hapa kiliochetu ni soko, hapa tulipo hata ukitaka kuuza madini lazima uende Ruangwa au Tunduru umbali uliopo ni mkubwa kufika huko. Na soko kubwa la Madini ya vito ni Tunduru, kwa hiyo ili mapato ya serikali yasipoteee tunaomba soko liwe hapa hapa sisi tuuze madini yetu na watu wa TRA wawepo ili tukiuza tuu serikali inachukuwa chake hapo hapo” alisema Ijumaa Iddi mwenyekiti wa wachimbaji wadogo katika eneo hilo. 

Katika kupatia majibu hoja zote zilizo wasilishwa, Naibu Waziri alianza kwa kusema. 

“Mimi na waziri wangu Biteko iwe mchana iwe usiku, tutafika mahali popote ili kuhakikisha serikali inapata mapato kupitia madini, hivyo uwepo wangu hapa ni kwa sababu hiyo na ili pesa hiyo ipatikane lazima migogoro na hizi kero lazima zimalizwe ili mchimbe, muuze na kisha mlipe mapato ya serikali” alisema Nyongo. 

Katika kujibu hoja, Naibu Waziri alianza kwa msimamisha Kaimu Afisa Madini Mkazi mkoa wa Lindi Mhandisi Iddi atoe ufafanuzi kuhusu leseni na umiliki wa eneo hilo. 

“Mhe. Naibu Waziri, kwanza kabisa niseme eneo hili lina leseni halali inayo milikiiwa na ndugu Omar Said Kojogo anae miliki kihalali kwa leseni Na. PML 36821 Southern Zone ya Tshs. 1,937,000. Na kwa mujibu wa sheria ya madini ya mwaka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017 hairuhusu kutoa leseni kwenye eneo moja ambalo teyari ilishatolewa na mahali hapa palishatolewa leseni kama nilivyosema, na kama itakuwa hivyo mlabda kwa kesi maalum, hata hivyo suala hili lilishashugulikiwa na muda si mrefu leseni yao itakuwa teyari” alisema Mhandisi Idd Msikozi. 

Kuhusu kilio cha masoko, Naibu waziri alisema kwanza anawashukuru wachimbaji hao kwa kitendo chao cha kulilia soko ili madini yao yakauzwe kwenye masoko rasmi. Amesema serikali imetoa agizo kila mkoa uwe na soko la madini ili serikali ipate fedha za kutosha kupitia madini ili fedha hizo zikatumike kwenye shuguli nyingine za maendeleo. 

Amesema mpango wa sasa wa wizara ni kuhakikisha kuwa kuna vituo vya kununulia madini kwenye maeneo ya wachimbaji ili wanaporo wasitembee mwendo mrefu kufuata soko. 

“Ndugu zangu wanaaporo, kiliochenu kuhusu soko kimenigusa sanaa, na sisi kama wizara ndio kitu ambacho tunakisisitiza kila mahali, kwa hiyo hapa hapa naagiza Afisa Madini Mkoa na Uongozi wa Wilaya kaeni chini kwa haraka mjadili ili kituo cha kununulia madini hapa kianzishwe mara moja na serikali ianze kukusanya mapato yake”. Aliongeza Nyongo. 

Baada ya kutolea majibu ya hoja za wachimbaji hao, Naibu waziri pia aliwaagiza wachimbaji kuanzisha mfuko wa mahafa na dharula ili uwezo kuwasaidia mara miongoni mwao anapopatwa na tatizo ahudumiwe kwa huduma ya awali huku akisubiri utaratibu binafsi wa kutatua tatizo lake. 

Kwa upande mwingine Nyongo ameuagiza uongozi wa Wilaya zote mbili ukae pamoja na kuweka utaratibu utakao wezesha kuwa na kituo cha kutolea huduma ya kwanza kwa maana pawe na “Nurse” kwenye eneo hilo kwa utaratibu watakao ukubaliana. Aidha, halmashauri hizo ziweke vyoo maeneo hayo kwa kuwa wachimbaji hao wanalipa fedha serikalini hivyo wanastahili huduma hiyo. 

Wakati huo huo Naibu Waziri amewapongeza viongozi wa Wilaya zote mbili kwa jitihada zao za kutatua mgogoro huo awali kabla hajafika hasa katika kukubaliana namna kukusanya mapato ya kila upande kwani mapato yote yanakwenda kwenye mfuko mmoja wa serikali. 

Kwa upande wao viongozi wa wilaya ya Nachingwea Katibu Tawala Husna Sekibobo na Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Chiwamba kwa pamoja walimshukuru Naibu Waziri kwa kufika katika eneo hilo na kujione hali halisi kutoa majibu ya moja kwa moja ya hoja zilizo wasilishwa na waliahidi maelekezo na maagizo yake watayatekelezwa. 

Ziara ya Naibu Waziri ilikuwa ya kukamilisha ratiba ya ziara ya Waziri wa Madini Doto Biteko aliesitisha ziara yake mkoani humo na kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya majukumu mengine.

TUPO TAYARI KUSHIRIKIANA NA AFRIKA KUSINI-MAJALIWA

$
0
0
 WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini katika kutimiza azma yake ya kukuza uchumi na kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025.

Amesema Tanzania inahitaji uungwaji mkono na Serikali ya Afrika Kusini hususan katika kipindi hiki ambacho imedhamiria kuimarisha shughuli za uzalishaji kupitia viwanda kwa lengo la kufikia uchumi wa kati..

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Agosti 16, 2019) wakati wa ziara ya Kiserikali ya Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro.

Ameyasema kwa kuwa changamoto zinazoikabili Tanzania katika nyanja mbalimbali zinafanana kwa kiasi fulani na zile za Afrika Kusini kwani historia za nchi hiyo na jiografia vinafana na Serikali ya Tanzania.

Akizungumzia kuhusu eneo la Mazimbu, Waziri Mkuu amesema kuwa lina uhusiano mkubwa na historia ya nchi hizo mbili kwa sababu huwezi kuulezea vizuri uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini pasi na kulitaja eneo hilo.

Waziri Mkuu amesema eneo la Mazimbu limebeba historia muhimu ya kumbukumbu ya vuguvugu la ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika pamoja na mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

“Mheshimiwa Rais, Tanzania ikishirikiana na nchi tano zilizokuwa katika kundi la mstari wa mbele (Angola, Tanzania, Zambia, Botswana na Msumbiji) ilijishughulisha sana katika ukombozi kusini mwa Afrika na katika kukomesha sera za ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini”. 
                                                       
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuwa sera za ubaguzi wa rangi zilikoma mwezi Februari 1994 na kufuatiwa na uchaguzi huru na wa haki uliopelekea kupatikana kwa Rais wa kwanza mzalendo wa nchi hiyo, Hayati Mzee Nelson Mandela mwezi Mei 1994.

“Tunapoongelea kukoma kwa sera za ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, siku zote tutawakumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwal. Julius Nyerere na Hayati Mzee Nelson Mandela kwa utumishi wao uliotukuka kwa kujenga misingi imara ya umoja katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini”.

Amesema misingi imara iliyojengwa na wazee wetu hao, imekuwa chachu ya ushirikiano kwenye majukwaa ya Kimataifa hususani katika kupambana na ubaguzi wa kiuchumi na unyanyasaji wa aina mbalimbali.

Waziri Mkuu amesema namna pekee ya kuwaenzi viongozi wetu hao ni kuendelea kujenga umoja na kushirikiana katika kuimarisha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa ajili ya maslahi ya wananchi.

Kwa upande wake, Rais Ramaphosa amesema anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa mchango mkubwa ulioutoa kwa nchi ya Afrika Kusini wakati wa harakati za kupigania uhuru wa nchi hiyo, hivyo wataendelea kuimarisha ushirikiano.

Rais huyo wa Afrika Kusini amesema Serikali yake ipo tayari kushirikiana na Serikali Tanzania katika kuboresha masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali na kukuza teknolojia.

Pia amesema watairisha chuo cha SUA kwa kuboresha miundombinu mbalimbali ili kulifanya eneo hilo kuwa la kisasa. “Tutaboresha na shule katika eneo hili na kuweka utaratibu wa walimu wake kutembeleana na wa Afrika Kusini kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.”

Rais Ramaphosa aliwasili katika uwanja wa ndege wa Morogoro saa 4.21 asubuhi na kupokelewa na Waziri Mkuu. Kisha alitembelea campus ya Solomon Mahlangu na kujionea maeneo ambayo wapigania uhuru wa Afrika Kusini walikuwa wakikutana na kupanga mipango mbalimbali.

Pia kiongozi huyo ambaye kwa mara ya kwanza amefika mkoani Morogoro leo alitembelea campus ya Mazimbu na kujionea sehemu ambazo waliishi wapigania uhuru wa nchi yake na kisha aliweka shada la maua kwenye makaburi ya wapigania uhuru. Ameondoka uwanja wa ndege wa Morogoro na kuelekea jijini Dar es Salaam saa 1.59 mchana.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,         
IJUMAA, AGOSTI 16, 2019.

RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS WA AFRIKA KUSINI RAMAPHOSA WASHIRIKI MKUTANO WA WAFANYABIASHA WA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa kikao cha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Afrika Kusini leo Agosti 15, 2019 jijini Dar es Salaam. Ambapo Mkutano huo umeudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye yupo nchini kwa ziara ya Siku mbili huku akisubiri kuhudhuria mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajia kufanyika Agosti 17 na 18, 2019.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (wa tatu kutoka kushoto) akipiga makofi. 
Wageni waliofika katika mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania na Afrika Kusini.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia katika wakati wa kikao cha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Afrika Kusini leo Agosti 15, 2019 jijini Dar es Salaam. Ambapo Mkutano huo umeudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye yupo nchini kwa ziara ya Siku mbili huku akisubiri kuhudhuria mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajia kufanyika Agosti 17 na 18, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akipeana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi mara baada ya kumaliza kuhutubia kikao cha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Afrika Kusini leo Agosti 15, 2019 jijini Dar es Salaam.
Wageni waliofika katika mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania na Afrika Kusini.

MBUNGE MGIMWA AKERWA NA UBOVU WA BARABARA ZA KATA YA MAPANDA

$
0
0
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mtwivila kilichopo kijiji cha Mapanda kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mtwivila kilichopo kijiji cha Mapanda kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa  kijiji cha Chogo kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Ihimbo kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
WANANCHI wa jimbo la Mufindi Kaskazini wanakabiliwa na changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo kutokana na wananchi kutofanya kazi kwa uhuru.


Akizungumza wakati wa ziara yake kwenye kata ya Mapanda Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwaamekiwa kuwa tatizo la ubovu wa miundombinu hiyo imekuwa kero na ameanza kuifanyia kazi ili kuzikarabati ziweze kupitika kirahisi.


“Nimebaini kuwepo kwa uchakavu wa barabara katika kata ya Mapanda ambazo zimekuwa zikififisha maendeleo ya jimbo langu hivyo natakiwa kufanya kila niwezalo kuhakikisha barabara hizi zinapitika” alisema Mgimwa


Mgimwa amesema kuwa amefaikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutengeza barabara zote korofi ili ziweze kupitika kwa urahisi.


“Nimefakisha kupata zaidi ya shilingi milioni mia nane kuhakikisha tunakarabati barabara hii ambayo imekuwa inatumiwa na watu wengi kimaendeleo katika jimbo hili” alisema Mgimwa


Mgimwaalisema kuwa kuna barabara inayotoka kuanzia Kibengu,Kipanga,Ihimbo,Uhafiwa,Kisusa,Ukami hadi njia panda ya Mapanda inayokadiliwa kuwa na urefu wa kilometa sitini na moja imetengewa fedha kidogo tofauti na matengenezo yanayotakiwa kufanyika katika barabara hiyo.


“Nitakuja na viongozi wa TARURA huku kuhakikisha wanajionea ubo vu wa barabara hizi ili wanavyotenga fedha wajue wanakarabati wapi na wanaacha wapi haiwezekani barabara hii ikatengewa kiasi cha shilingi milioni thelethini tu” alisema Mgimwa


Aidha Mgimwa amewataka TANROAD na TARURA kuzikarabati  barabara zote korofi kipindi cha kiangazi  ili zipitike kirahisi na sio kipindi cha masika ambapo mara nyingi hutokea kero kwa wananchi.


Wakitoa kilio chao kwa mbunge huyo wanachi wa vijiji hivyo walimwambia hakuna maendeleo yanayoendelea katika vijiji hivyo kutokana na ubovu wa barabara hizo.


Hakuna usafiri wa basi wala gari inayofika huku kutokana na ubovu wa barabara hizi hivyo tunakuomba uhakikishe unatusaidia kuzikarabati barabara hizo” walisema wananchi 

NMB wins Euromoney Awards 7th year in a row

$
0
0






· Innovation and technology contributed to the award


 NMB Bank PLC has for the 7th consecutive year scooped the Best Bank in Tanzania 2019 award by Euromoney Magazine outshining over 40 other banks operating in Tanzania. This is a top award issued by the leading global financial markets magazine based in London.

NMB Bank being one of the key players in financial inclusion in the country, has consistently strived to provide innovative financial solutions to Tanzania’s banked and unbanked. Supporting the nation’s financial inclusion agenda, NMB Bank has pioneered revolutionary products and services, maximizing on technology to enhance customer experience through the bank’s branches, NMB Wakala network and digital platforms such as NMB Mastercard, NMB Mobile, NMB KLiK and Internet Banking.

This award reflects the progress NMB Bank has made in delivering a banking experience that captures what customers need today and tomorrow, making it the best for financial inclusion.

NMB’s Interim Managing Director Jonkergouw said in a statement: “We are today the bank that works, rather than one which exists. Tough decisions around capital, businesses and people have been made. Throughout that process, we have continued to deliver strong financials and pay industry-leading dividends to shareholders.”

He added: “We are leveraging on the best of technology in digital banking, innovative products and our extensive branch network and Wakalas add real value to our customers’ lives.

Winning the Best Bank in Tanzania award is a clear indication that our efforts are recognized not only in Tanzania but across the region. We acknowledge the dedication of our staff, and thank our valued customers for being part of this digital journey.”

The Euromoney Award confirms the bank’s investment in digital transformation and technology has further strengthened its ability to deliver innovative solutions to the market.

Describing the selection criteria and reliability of the results, Euromoney’s editor explained: “We have received almost 1000 submissions from banks in our awards programme which covers 20 global awards, more than 50 regional awards, and best bank awards in close to 100 countries. This year our most successful banks have clearly defined what their core strengths are, and built their businesses around them."

This year’s Euromoney Awards for Excellence 2019, doubles Euromoney’s 50th anniversary as the most prestigious awards in the global banking industry, welcoming over 500 senior bankers around the world at the Tower of London recently where banks based in developing markets made a greater impact in the awards than ever before highlighted with NMB Bank being named the Best Bank in Tanzania.

Hospitali ya Mloganzila yazindua Baraza la Kwanza la Wafanyakazi

$
0
0
Charles Majinge (katikati) akimkabidhi mkataba wa Baraza la Wafanyakazi, Mwenyekiti wa baraza Prof. Lawrence Museru, kulia ni katibu wa baraza Bw. Nicholaus Mshana akishuhudia makabidhiano hayo. 
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge (wa pili kutoka kushoto) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa baraza la wafanyakazi la Hospitali ya Mloganzila, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Prof. Lawrence Museru, wa kwanza kulia ni Katibu Msaidizi wa baraza Bi. Neema Njau akifuatiwa na katibu wa baraza Bw. Nicholaus Mshana. 
Prof. Charles Majinge (aliyevaa tai, kwa walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Hospitali ya Muhimbili- Mloganzila mara baada ya uzinduzi wa baraza hilo. 


Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akizungumza katika uzinduzi wa Baraza la kwanza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila uliofanyika leo. 
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la MNH-Mloganzila wakimsikiliza Pro. Majinge wakati wa uzinduzi wa baraza hilo lenye wajumbe 115. 
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Mloganzila wakiimba wimbo maarufu wa mshikamano (solidarity forever) katika mkutano huo.


Na Neema Wilson Mwangomo

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Charles Majinge amelitaka Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila kusimamia utekelezaji wa dhamira ya kuhudumia wagonjwa kwa lengo la kuwaondolea wananchi kero mbalimbali zikiwemo rushwa, ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha na mali za Umma.
Prof. Majinge ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akizindua Baraza la Kwanza la Wafanyakazi la Muhimbili-Mloganzila.

Amesema baraza la wafanyakazi halina budi kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu wake kulingana na sheria na taratibu zilizowekwa, kudumisha utawala bora na kulinda nidhamu sehemu za kazi pamoja na kuondoa aina zote za uonevu au ubaguzi miongoni mwa watumishi.

Pia amewasihi kuhakikisha fedha za serikali zinatumika vizuri kwa mujibu wa sheria ya fedha ya mwaka 2001 na sheria ya ununuzi ya mwaka 2004 kwani utaratibu huu utapelekea matumizi mazuri ya fedha za serikali.
“Mnatakiwa kuhakikisha bajeti ya hospitali inatayarishwa kwa umakini mkubwa ikizingatia vipaumbele, hali halisi ya uwezo wa serikali na mahitaji ya hospitali ili kufikia malengo na kuimarisha huduma za kibingwa’’ amesema Prof. Majinge.

Pamoja na mambo mengine Prof. Majinge amewataka watumishi wa MNH-Mloganzila kutunza vitendea kazi wanavyovitumia katika kutimiza majukumu yao ili kuweka mali na miundombinu ya hospitali kuwa salama.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru amesema baraza la wafanyazi ni la kwanza kufanyika tangu kuanzishwa kwa MNH-Mloganzila hivyo amelitaka liwe na mwanzo mzuri.

Amefafanua kuwa Hospitali ya Mloganzila hivi sasa ina miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake hivyo jukumu lililopo mbele yetu ni kuhakikisha inakuwa na vifaa vinavyotakiwa pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi lengo ni kuhakikisha Mloganzila inakuwa sehemu ya Muhimbili pia isipoteze utambulisho wake.

CCM YARIDHISHWA NA MIRADI YA MAENDELEO NYASA

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho, Jana akikagua mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa inayojengwa katika Kijiji cha Nangombo Kata ya kilosa wilayani hapa ambayo imefikia Asilimia 95 ya ukamilishaji kulia ni Mganga mkuu wa Wilaya ya Nyasa DKT Aroin Hyera akitoa maelezo yanayohusu ujenzi huo.Picha na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa.

………………………………………….

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho, akiwa ameambatana na Kamati ya Siasa ya Mkoani hapa, ameridhishwa na Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo na ushirikishwaji wa jamii katika miradi iliyotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 katika Wilaya ya Nyasa.

Ameyasema hayo jana wakati akihitimisha Ziara ya kikazi siku mbili agosti 14-15, ya kutembelea na kukagua, miradi ya maendeleo katika Tarafa ya mpepo na Luhekei, Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma.

Bwana Mwisho alifafanua kuwa kwa Miradi nane(8)ambayo amekagua amefurahi kuona imetekelezwa vizuri na kwa kiwango cha hali ya juu, na Jamii imeshirikishwa na wanatambua miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao, na wanachangia nguvu zao licha yaSerikali kutoa Fedha ili kuunga Mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Aliitaja miradi aliyokagua kuwa nia Ujenzi wa Hosteri mbili shule ya Sekondari Kingerikiti,Ukamilishaji wa vyumba 3 vya madarasa shule ya msingi Kibaoni,iliyopo Kata ya Tingi ambayo iko hatua ya Ring bim, Ujenzi wa Vyumba nane vya madarasa,matundu sita ya vyoo,meza 240 na viti 240 na ujenzi wa bw Sekondari Mhandisi Stella Manyanya katika Kata ya Mpepo Wilayani hapa.

Aliongeza miradi minginwe aliyokagua nia Shamba la Miti ya Misindano (Pines Patula) iliyopandwa na Wakala wa huduma za Misitu Tanzania shamba ambalo lina ukubwa wa Hekta 20,905 zinazofaa kwa ajili ya upandaji miti na hekta 680 kati ya hizo zimetumika kwa kupandwa miti 555,500/= na upanuzi wa shamba ukiwa unaendelea,mradia ambao ulimfurahisha sana na kutoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma wapande miti ili kutunza mazingira na kuongeza kipato kwa wananchi kwa miaka ijayo.

Pia alikagua ujenzi wa hosteri na bwalo la Chakula shule ya Sekondari Nyasa katika Kata ya Chimate na Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa ambayo imefikia Asilimia tisini na tano(95) ya ukamilishaji, wa majengo saba yanayojengwa katia Kijiji Cha Nangombo Kata ya Kilosa Wilayania hapa na alitoa Pongezi Kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya Wananchi,wataalam na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba,

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Uongozi wa Wilaya ya Nyasa ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw.Jimson Mhagama kwa ushirikiano mliouonyesha katika Ujenzi wa Hospitali hii ya Wilaya ambayo imejengwa kwa Ustadi mkubwa na ushirikiano wa hhli ya juu kati ya Wananchi wataalam na Serikali.Naomba ushirikiano huu uendelee.

Miradi mingine aliyoikagua ni ujenzi wa Ofisi ya Mdhibiti wa Elimu Wilaya ya Nyasa na Ujenzi wa jengo la Tanesco lilopo katika kijiji cha kilosa na Kata ya KIlosa wilaya ni hapa.

Aidha alitoa wito kwa Viongozi wote wa Chama cha Mapinduzi(CCM) kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Kata Wilaya na Mkoa kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kushiriki shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo zinazotekelezwa katika Maeneo yao.

Imeandaliwa Na Netho c.Sichali ofisa habari,wilaya ya Nyasa,0767417597

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, atembelea Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro.

$
0
0
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiangalia moja ya kaburi la Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini, katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro. Agosti 16.2019.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakiangalia makaburi ya Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini, katika kambi ya Mazimbu mjini Morogoro. Agosti 16.201
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akipanda mti, wakati alipotembelea Kambi ya iliyotumika na Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini, iliyopo Mazimbu mjini Morogoro. Agosti 16.2019
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiweka shada la mauwa, katika mnara wa kumbukumbu ya Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini, wakati alipotembelea Kambi ya iliyotumika na Wapigania Uhuru hao, iliyopo Mazimbu mjini Morogoro. Agosti 16.2019.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, baada ya kutembelea Kambi ya Mazimbu, mkoani Morogoro, akiwa kwenye ziara ya Kiserikali nchini. Agosti 16.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).. Agosti 16.2019.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akizungumza na wananchi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro,alipotembelea Kampasi hiyo. Agosti 16.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro, kabla ya kumkaribishaRais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa kuzungumza. Agosti 16.2019.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiwa amesimama katika moja ya picha ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini, kwenye Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro. Agosti 16.2019.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akizungumza na mwenyeji wake Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akiwasili katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro. Agosti 16.2019.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiwa kwenye picha ya pamoja, kwenye ofisi ya Utawala, iliyotumika na Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini, katikaChuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro. Agosti 16.2019.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiangalia moja ya kaburi la Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini, katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro. Agosti 16.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, wakati alipowasili katika Mkoa wa Morogoro, akiwa kwenye ziara ya Kiserikali nchini. Agosti 16.2019. 

WAKULIMA ZAO LA TANGAWIZI MKOANI KIGOMA WAIOMBA SERIKALI KUONGEZA NGUVU KUBORESHA ZAO HILO

$
0
0
Moureen Tesha, Kasulu. 

Wakulima wa zao la tangawizi wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wameiyomba serikali kuongeza nguvu katika zao hilo kutokana na kuwa jipya katika mkoa huo. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika semina iliyoandaliwa na kampuni ya NOJEPACO CO LTD ya jijini Arusha, wakulima hao wamesema ipo haja ya ya serikali pamoja na mambo mengine kuhakikisha inawapa mikakati mbalimbali kwaajili ya kuboresha zao hilo. 

Mkulima wa tangawizi Oscar Gabriel, amesema kutokana na zao hilo kuwa jipya mkoani humo ipo hasa kwa serikali walifanya kuwa zao la kimkakati ikiwa ni pamoja na kusaidia uwepo wa masoko ya uhakika. 

"Kama serikali italifanya zao hilo kuwa la kimkakati kwa kuhakikisha soko la uhakikika linapatikana itasaidia wakulima wengi kulilima zao hilo kwa wingi katika mkoa wetu hali itakayosaidia kujikwamua kiuchumi," amesema Gabriel. 

Mkulima kutoka wilaya ya Kasulu Magreth Siame, amesema yeye ni mara yake ya kwanza kulima zao hilo lakini ameweza kuona faida na kwamba serikali iwasaidie mikopo hata kwa riba nafuu kwa vikundi vikundi ili waweze kumudu gharama za kulima zao hilo. 

"Wakulima waligundua zao la tangawizi lina faida ninauhakika watajitokeza wengi kulima lakini kitakachowaangusha ni gharama za kulima zao hilo kuwa kubwa, kama serikali italibeba hili kwa kutupatia mikopo kwa riba nafuu hakika umaskini utabaki kuwa historia katika wilaya yetu na mkoa kwa ujumla, "amesema Siame. 

Msimamizi wa kampuni ya NOJEPACO CO LTD ya mkoani Arusha, Suzana Kavishe amesema kampuni yao ipo kwaajili ya kutoa elimu kwa wakulima wa tangawizi na kuwahudumia kuanzia mwanzo wa kilimo mpaka wanapovua mazao yao. 

Amesema anawashauri wakulima wa tangawizi kulima aina ya Zingiber ya tangawizi ambapo watakuwa na soko la uhakika kutoka kwao na kuwainulia kipato cha familia zao. 

"Wao kama kampuni kazi yao ni kununua zao la tangawizi linalolimwa na wakulima hao pamoja na kuwapimia sampuli ya udogo kwa wakulima hao kwa gharama nafuu,"amesema Kavishe

Afisa wa Kilimo mkoani hapa Jerry Abeli, amesema serikali bado inaendelea kuhamasisha wakulima wadogo kuingia katika kilimo hicho kwani kwasasa kimekuwa mkombozi kwa wananchi wa maeneo mengi. 
Wakulima wa zao la tangawizi wakiwa katika semina ya jinsi ya kulima zao hilo katika wilaya ya kasulu mkoani Kigoma, iliyoandaliwa na kampuni ya NOJEPACO CO LTD ya jijini Arusha

Jafo Ataka Nchi za Afrika Mashariki Ziwe na Mkakati wa Pamoja kuendeleza Vipaji vya Wanamichezo

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akizungumza kwenye ufunguzi wa mashindano ya FEASSSA leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
Rais wa FEASSSA Justus Mugisha akizungumza kabla ya ufunguzi wa mashindano ya FEASSSA leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Tixon Nzunda akizungumza kabla ya kufunguliwa kwa mashindano hayo leo jijini Arusha
Picha mbalimbali zikionyesha matukio ya ufunguzi wa mashindano ya FEASSSA leo jijini Arusha

…………………..

Na Mathew Kwembe, Arusha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amelitaka Shirikisho la Michezo kwa shule za Sekondari za Afrika Mashariki (FEASSSA) kuwa na mipango ya pamoja ya kuendeleza vipaji vya watoto vinavyoibuliwa kupitia mashindano ya FEASSSA.

Akifungua mashindano hayo leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Mhe.Jafo amesema lazima viongozi wa michezo kutoka nchi wanachama za Afrika Mashariki kuhakikisha kuwa wabnakwenda kuvilea vipaji vya wanamichezo vitakavyopatikana kupitia mashindano hayo.

Amesema kuna tabia imejengeka kwamba watoto wenye vipaji wanaibuliwa kupitia michezo hiyo lakini vipaji hivyo vinapotea kwa kukosa matunzo na hivyo kupotea.

“Niwaombe nchi wanachama kila mmoja katika nchi anayotoka twende tukavilee vipaji mbalimbali vitakavyoibuliwa kupitia mashindano hayo,” amesema na kuongeza:

“Ninaamini tukifanya hivyo tutatenda haki sawa na changamoto kubwa ipo kwa wasichana ambapo taarifa zinaonyesha kuwa vijana wengi mahiri wasichana licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kimichezo lakini mdondoko umekuwa ni mkubwa.”

Mhe.Jafo amewataka waratibu wa nchi mbalimbali zinazoshiriki michezo hiyo kwenda kuwalea vijana wenye vipaji ili kuweza kuendeleza vipaji vya vijana hao kwa maendeleo ya michezo katika nchi zao.

Amesema jukumu la viongozi wa jumuiya ya Afrika Mashariki katika sekta ya michezo ni kuhimiza na kuwajengea mazingira rafiki vijana ili waweze kukuza vipaji vyao na kujiendeleza katika michezo, kutanua wigo wao wa ushindani ndani na nje ya nchi, kanda na bara la Afrika.

Aidha Waziri Jafo amewataka wanamichezo wanaoshiriki michezo hiyo ngazi ya kanda kudumisha nidhamu wakati wote wa mashindano hayo.

“Mtambue kuwa nidhamu ina mchango mkubwa katika mafanikionkatika michezo na maisha kwa ujumla. Katika kushindana mtambue kuwa kuna kushinda na kushindwa,” amesema.

Pia amewataka vijana hao kuitumia fursa hiyo ya kukutana na wenzao kutoka nchi nyingine za Afrika Mashariki kubadilishana uzoefu wa masomo pia kwa ajili ya kuinua taaluma zao.

Waziri Jafo amewataka viongozi kutoka nchi za Afrika Mashariki wanaoshiriki mashindano hayo ya FEASSSA kuitumia fursa hiyo ya kuwepo nchini kuona uwezekano wa kutembelea vivutio mbalimbali vinavyopatikana nchini hususani kutembelea mlima Kilimanjaro na mbuga za wanyama za Tarangire na Ngorongoro ambazo zinapatikana katika mkoa wa Arusha kunapofanyikia mashindano hayo mwaka huu.

Mapema Rais wa FEASSSA Justus Mugisha amesema nchi za Afrika Mashariki hazina budi kuweka misingi mizuri ya michezo shuleni ili ziweze kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Amesema hatua ya nchi za Afrika Mashariki kupeleka nchi nne katika mashindano ya AFCON yaliyomalizika hivi karibuni nchini Misri ni dalili njema kuwa nchi hizo zimejipanga kufanya vizuri katika mashindano yajayo ya kimataifa.

“Ni lazima tuwekeze katika michezo kwa vijana kama hawa wanaoshiriki mashindano ya FEASSSA kama kweli tunataka kupata mafanikio kwenye michezo ya kimataifa,” amesema.

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu bwana Tixon Nzunda jumla ya wanamichezo 3500 kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani na wenyeji Tanzania bara na Zanzibar watashiriki michuano hiyo huku nchi ya Malawi ikishiriki michuano hiyo kama mwalikwa.

Amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha michezo ya soka, riadha, netiboli, mpira wa mikono, mpira wa mikapu, vinyoya, raga, mpira wa magongo, mpira wa meza, na mpira wa kengele.

Bwana Nzunda ameongeza kuwa malengo ya mashindano hayo ni kukuza fani za michezo kwa wanafunzi kwa kuwashindanisha ili kubaini vipaji vya wanafunzi kutoka nchi za Afrika Mashariki na pia kudumisha na kuendeleza mshikamano kwa nchi wanachama miongoni mwa wanafunzi, walimu na viongozi wa shule kutoka Afrika Mashariki.

Mara baada ya ufunguzi rasmi wa mashindano hayo, kulifanyika mchezo wa kwanza wa soka wavulana baina ya timu ya soka ya Lindi ambao walikuwa washindi wa tatu wa UMISSETA mwaka 2019 ambayo ilicheza na mabingwa wa mashindano kama hayo wa nchini Kenya timu ya St.Antony ya Trans zoia ambapo matokeo yalionyesha mabingwa hao wa Kenya waliibugiza Lindi kwa magoli 4 kwa 0.

Michezo hiyo itaendelea kuchezwa kila siku hadi tarehe 24 agosti, 2019 ambapo fainali za michezo hiyo zitafanyika.

Ufunguzi wa mashindano hayo pia ulishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo na viongozi wa ngazi mbalimbali kutoka mkoa wa Arusha na nchi wanachama wanaoshiriki mashindano hayo.
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live




Latest Images